Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

MPANGO WA KONGO

  

MTUNZI: BAHATI MWAMBA



MAUAJI


Ilikuwa ni ndani ya majengo ya ubalozi wa Tanzania yalioko pembeni kidogo mwa mji wa mji mkuu wa Congo DRC katikakati ya mji mdogo wa Ivuba.


Katika moja ya meza zilizokuwa ndani ya vyumba vya juu kabisa ndani ya ubalozi huo kulikuwa kuna mtu amesimama kando ya meza hiyo huku kila mara akijaribu kukuna kichwa chake ambacho hakikuwa na unywele hata mmoja.


Mtu yule hakuwa mtulivu wa nafsi,akili na mwili.Bila shaka kwa sababu kadhaa alizozijua yeye na muda wote aliokuwa amesimama kando ya meza ile alikuwa akitazama dirishani,dirisha ambalo wakati huo lilikuwa lipo wazi na halikuwa limefungwa wala kushushwa pazia kubwa na zito ambalo wakati huo lilikuwa limekunjwa kwa namna fulani hivi kisha likashikizwa na kibanio maalumu ambacho kiliacha pazia lile likiwa limejikunja katikati na kujiachia chini.


Ingekuwa siku zingine bwana huyu angeliweza kumuita mfanya usafi na kumkanya juu ya kusahau kufunga dirisha na kushusha pazia,lakini leo hii hilo hakukumbuka kabisa na badala yake akawa amejielekeza kuwaza na kuwazua jambo fulani tata ambalo kamwe hakudhani linafanyika katika nchi ile ya Congo.


Macho yake yalitazama dirishani tena na hapo akashuhudia jengo lingine refu lililokuwa likitazamana na ofisi zake zile,jengo lile lilikuwa ni hoteli kubwa kabisa ndani ya jiji la Kinshasa na mji ule wa Ivuba.


Tofauti na siku zote ambazo huwa analitazama mara kadhaa huku akiwa na kikombe cha kahawa mkononi,lakini leo hii hakuwa na kikombe na hata yale mawazo yake ya kutaka siku moja yeye au mwanae ajenge jengo kama lile nchini Tanzania hayakuwa kabisa akilini mwake.


Akajikuna kichwa na kujiegemeza kwenye meza iliokuwa kando yake kisha akaketi huku sasa mwili wake ukianza kuhisi joto la ajabu ambalo hakujua ni la uoga ama la joto la ahsubuhi ile ya ajabu kwake.


Akiwa bado anatizama pale dirishani mara mlango wa ofisi yake ukafunguliwa bila mfunguaji kubisha hodi.


Akaingia mwanaume mkakamavu mwenye misuli imara na kusimama nyuma yake.


Balozi Ally Sapi akageuka kutoka kule alikokuwa anaangalia na kumgeukia mwanaume yule.


Walitazamana kwa muda kidogo kisha Balozi Sapi akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa mkupuo.


“Alikuwa sahihi yule bwana mdogo” alisema Balozi huku akimtizama usoni mwanaume yule aliekuwa amesimama mbele yake.


“ina maana ndicho kilichotokea kwako sivyo!”alisaili mwanaume yule.


“Haswaa na tena kinaeza kuniondoa duniani masaa machache yajayo!” alisema Balozi huku akimtizama yule mwanaume na kuuona mshituko wa wazi usoni pake.

Ikawa zamu ya yule mwanaume mkakamavu kujikuna kichwa na kushangaa huku nae kichwa kikijaa moto wa joto ambalo hakujua limetokea wapi ahsubuhi ile.


“aaah ina…” akataka kusema yule mwanume baada ya kuwa anahitaji maelezo zaidi kutoka kwa balozi Ally Sapi,lakini hakumaliza kauli yake tayari balozi Sapi alishaanza kusema.


“Nilipokea ugeni jana jioni wakati natoka hapa ofisini,na kabla sijafika nyumbani yakanipita magari sita kwa kasi na kwenda kusimama mbele kisha gari la mwisho likaanza kupunguza mwendo hali ilionifanya nipunguze na mimi pia na kisha nikaona ishara kutoka kwa dereva wa gari la mwisho kati ya yale magari sita akiniashiria nisimame nami nikatii kwa kusimama pembeni hasa kwa kuhisi inaeza kuwa ni heri tu. Kutoka katika magari yale wakashuka wanaume wanne wakaja karibu na gari langu na bila kusema kwa maneno wakanipa ishara nishuke ndani ya gari,nami nikatii,wakaniongoza hadi kwenye gari moja wapo na humo ndani ya gari sikuamini kabisa nilichokiona aisee” alimalizia kwa kusikitika balozi Sapi.


“kwa ikawa vile tulivyowaza na ulichokiona ni kile kile alichosema marehemu Bulembo!” alisema tena yule mwanaume na hapo ikawa ni zamu ya Balozi Sapi kutumbua macho kwa kutoamini alichokisikia.


“ina maana Bulembo amefariki,lini na wapi!” alihoji Balozi Sapi huku macho yake yakiwa bado yapo yanamtazama mwanaume yule bila kupepesa huku moyo wake ukiruka sarakasi kifuani kwake.

Mwanaume yule akajikuna kichwa na kurudi kumtazama Balozi Sapi huku akijaribu kukwepa kumbukumbu mbaya zilizoanza kumrudia kichwani.


“Nilifika kwake leo mapema kabisa, baada ya kuniandikia ujumbe wakunitaka nifike kwake,nikawahi kufika lakini ikawa kazi bure,nilikutana na maiti yake ikiwa imelala sakafuni na tundu kubwa la risasi shingoni lakini pia nilikuta nyumba yake yote imepekuliwa” alisema mtu yule huku kwa mbali machozi yakizilenga mboni za macho yake,akatumia mgongo wa kiganja chake kujifuta.


“sikijua kama inaeza kuwa namna hii na kwa uharaka mkubwa hivyo” alisema Balozi sapi.


“Hakuna namna lazima tutoe taarifa mapema ofisi kuu mheshimiwa” alisema yule mtu.


Balozi akainama kidogo chini ya meza na alipoinuka alikuwa na mkoba mweusi wa ngozi na bila kutoa kilichomo akamkabidhi yule mwanaume.


“kuuawa kwa Bulembo unamaanisha kuwa kuna msaliti kati yetu hapa ubalozini na pia ni ishara kwetu kuwa tayari tunawindwa tusiifikishe taarifa kunakotakiwa,lakini jitihada za Bulembo zimetuongezea uelewa wa hili jambo,hivyo peleka hivi vielelezo ofisi kuu na hakikisha wanahusika na uzuiaji wa hili jambo,msaliti acha aendelee kuwapo hapa ipo siku kiama kitakuwa juu yake…” Balozi Ally Sapi alisema huku akimkabidhi ule mkoba ambao ulikuwa na nyaraka muhimu sana zilizohusu kile walichokuwa wanakizungumzia pale wakati ule.


“kwa walivyokuteka walitaka uwe miongoni mwao sivyo!” alihoji yule bwana huku akipokea ule mkoba na kuutazama.


“Ndio na nilikataa licha ya kuahidiwa mazuri na bwana yule na kukataa kwangu kunamaanisha kifo kwangu hivi karibuni,hivyo basi hakikisha mpango huo unakoma mara moja,nakuamini Honda” alimalizia kusema Balozi Ally Sapi kisha akageuka na kumwacha Honda akigeuka ili atoke ndani ya ofisi zile za ubalozi wa Tanzania nchini Congo.


****


“kuliaa nyuzi sabiniii…hapo!”


“usijali Mimi ndie Kizibo,hata bila ramani yako tayari wamejaa kwenye jicho la mzungu” alijinadi Kizibo huku mkono wake wa kushoto ukiwa unachezea lenzi ndogo iliokuwa inefungwa juu ya bunduki ya kupiga masafa marefu na mkono wake wa kulia ulikuwa umekamata vyema eneo la kufyatulia risasi ya bunduki ile aina ya K2Lapua magnum rifle,bunduki safi ya kisasa ya kudungulia ukiwa umbali wowote ule. Kizibo hakuwa peke yake alikuwa na mtu mwingine eneo lile ambae yeye akikosa kazi huwa anashika kiona mbali na kisha humsaidia Kizibo kusoma masafa ya windo lao.


“Kojo hawa jamaa wanaongea sana,bila shaka wanajadili hii inshu Mzee” alisema Kizibo huku akijitahidi kufinya jicho lake ili kuhakiisha jicho moja linapata nguvu ya kutazama taswira iliojiweka ndani ya lenzi ya bunduki ile ya kudungulia.


Watu hawa walikuwa kwenye lile lile jengo lililokuwa likitazamana na dirisha la ofisi ya balozi Ally Sapi na wakati huu Kojo na Kizibo walikuwa kwenye moja ya vyumba vya jengo hilo la hoteli huku wakiwa wamekwisha kuweka mtego wao usawa wa lile dirisha ambamo kulikuwa kunafanyika mazungumzo kati ya Balozi Ally Sapi na Honda Makubi,mpelelezi na mfanyakazi ndani ya ofisi za ubalozi.


“Huu nao ni mwanya inabidi uzibwe Kizibo”alisema Kojo huku akishusha kiona mbali.


“Yule bwege anae toka na ule mkoba nenda uuchukue kisha utajua cha kumfanya,huyu kipara mimi bamzibua sasa hivi” alisema Kizibo huku akitema mate pembeni na kidole kikielekea kwenye kifyatulio cha bunduki yake alioipenda na kuihusudu sana.


***

Honda Makubi alifika nje baada ya kuwa ameshasaini kitabu cha mahudhurio na wakati huo huo alikuwa anapitisha mawazo ya kurudi nyumbani kwa marehemu Bulembo ama aendelee na taratibu za kupeleka zile nyaraka kuzihifadhi na kufanya utaratibu wa kuzituma ofisi kuu jijini Dar es laam na wao watajua cha kuzifanyia.


Akaingia ndani ya gari lake na kuliondoa kwenye maegesho maalumu kwa ajili ya wafanyakazi wa pale ubalozini,lakini ambacho hakujua japo alihisi ni kuwa watu wawili ndani ya ofisi zile walikuwa wakimtizama wakati akitoka eneo lile na mmoja kati yao akanyanyua simu na kupiga pahali kisha akarudi kuendelea na taratibu zake za kufanya usafi.


***

Baada ya kuhakikisha Honda ametoka ndani ya ofisi zake balozi Ally Sapi alichukua simu yake na kujaribu kumpigia Rais wa Tanzania,lakini ajabu simu yake ilikataa kutoa mawasiliano nje ya nchi ile ya Congo,akachukua tena simu nyingine maalumu ambayo hutumia kuwasiliana na mkurugenzi wa usalama wa Taifa nayo ikagoma.


Akiwa kashikwa na mashangao na hamaki ya kutoamini,Balozi akaanza kuzunguka ofisi yake kama asie amani uwepo wake mle ndani na hapo ndipo akalikumbuka tena dirisha lake na haraka akataka kuwahi kuishusha pazia.

Doh

Alikuwa amechelewa.

Risasi yenye nguvu ikatua katikati ya paji la uso wake na kusambaratisha kichwa chake kisha kumsukuma nyuma kwa nguvu na mwili wake usio na mhimili wa utimamu ukajibwaga chini kwa kishindo kisha kwa jitihada kidogo ukajitikisa kidogo na kutulia na ukawa mwisho wa Balozi Sapi.


Kule risasi ilikotokea,Kizibo akatema mate mengi chini.

“pyutyaaa”

Kisha akajiramba midomo yake na kuinyanyua bunduki yake na kisha akaanza kuitawanya huku akipiga mluzi hafifu wa ushindi.


*****


Honda Makubi aliegesha gari yake ndani ya geti la la nyumba ya marehemu Bulembo ,kisha akashuka taratibu na huku akiangaza huku na huko kwa umakini wa hali ya juu.


Kama alivyokuwa amepaacha ahsubuh na ndivyo alivyopakuta pakiwa katika utulivu wa kifo huku maiti ya mmliki wa nyumba ile akiwa ndani hana uhai japo wa kupigia chafya.

Honda akasimama kuupisha utulivu katika akili yake na muda huo mikono yake ilikuwa ikifanya jitihada za kujivika mipira maalumu ya viganja vya mikono.


Alipohakikisha amevaa sawia mipira ile,akapiga hatua ndefu na kuufikia mlango kisha akaufungua taratibu huku utulivu ukiwa ni ngao yake muhimu wakati ule.

Taratibu akachungulia ndani kwa tuo, na kutoka pale alipokuwa aliona mwili wa mpelelezi Bulembo ukiwa umelala vilevile alivyouacha na pembeni yake aliona mparanganyiko wa sofa ukiwa kama alivyoacha hapo ahsubuhi,akapiga hatua nyingine kubwa na kwa haraka zaidi kisha katika uharaka huohuo mikono yake ikaurudishia mlango na kuacha ukijibamiza kwa nguvu nyuma yake huku yeye akiwa hana habari nao tena.

Akatazama mazingira ya mle ndani,hakuona mabadiliko yoyote wakati ule. Akapiga hatua na kuufikia mwili wa hayati Bulembo,kisha akainama na kuanza kupekua mifuko ya suruali aliokuwa amevaa hayati Bulembo.

Katika dakika za mwanzo hakuona la maana katika jitihada zake za upekuzi katika mwili ule uliolala bila uhai.

Akasimama huku akili yake ikianza kujutia muda aliopoteza kurudi nyumbani kwa hayati Bulembo.

Hakuwa sahihi katika mawazo yake,hadi pale macho yake yalipo elekea miguuni mwa maiti aliokuwa akiipekuwa wakati ule na hapo tena akili yake ikaganda bila kufanya jitihada zozote za kutaka kujilaumu kama mwanzo.

Bila kufikiri zaidi,mwili ukafanya vitendo.

Haraka akainama na kupeleka mikono yake kwenye mguu wa kulia ambao ulikuwa umevikwa soksi huku ule wa kushoto ukiwa hauna soksi.

Akaivuta ile soksi na wakati ikimalizikia kuvuka akaona kikaratasi kidogo kikianguka kutoka ndani ya soksi ile.

Honda Makubi alitabasamu huku sasa akili yake ikijipongeza kwa kuwaza kurudi tena ndani kwa hayati Bulembo.

Akainama kuikota ile katasi na wakati ikiwa imeenea kiganjani kwake na mwili ukifanya jitihada za kunyanyuka baada ya kuwa umeinamishwa kuanzia tumboni kwenda juu,mwili wa Honda haukumaliza hilo tendo na mara hiyo kikafanyika kitendo cha haraka na wepesi wa hali ya juu kutoka kwa Honda japo matokeo yalikuwa ni kukosea hesabu za gafla.

Wakati akitaka kusimama akaona kivuli kikiwa karibu yake na mara hiyo akasikia msukumo mkubwa kutokea kiunoni kwake na haraka akajirusha mzima mzima kwenda mbele na bahati mbaya hakuwa ameiona meza iliokuwa hatua chache kutoka pale alipokuwa na alipotaka kujigeuza ili aone kilichomsukuma akajikuta akisambaratika chini baada ya kuipamia meza na kusambaratika nayo chini.

Hakuzubaa

Muda huo huo akajigeuza kwa namna ya ajabu kabisa kisha akatumia mkono mmoja kukita chini huku umbo lake refu likiwa wima katika nukta iliofuata na macho yake yakashuhudia kasi ya ajabu ya kiumbe mweusi na mrefu akimfuata kwa kasi ya upepo na kabla hajasimama imara akajikuta akipokea mateke mawili yaliopigwa kwa mtindo wa tandika reli nae hakuwa amajiandaa kwa hilo akaenda chini mazima kwa mara ya pili.

Hakuzubaa tena mana alishaona kasi na ujuzi wa adui yake,haraka akajizoa na kusimama wima huku akisikia maumivu yakimtambaa mwili mzima kuanzia kifuani,na hapo akajikuta akimsifu adui yake yule kwa kuwa na kasi na nguvu ya kumtetemesha namna ile.

Akajipanga.

Adui akausoma usimamaji wa Honda na akajua anapambana na mtu wa kiwango chake nae akafanya haraka ya kuokoa muda na hilo likawa kosa upande wake.

Adui akarusha ngumi kwa ustadi kumwelekea Honda,lakini Honda aliiona na kama utani akahepa na ngumi ikapiga hewa kisha kwa usitadi mkubwa akaachia konde lenye uzani uliokadiriwa na likampata adui ubavu wa kushoto na adui akabweka kama malaya kichochoroni.

Honda akaachia tabasamu la upande kisha akachumpa na kusimama nyuma ya adui aliekuwa anafanya jitihada za kupambana na maumivu ya mbavu zake,kisha akaachia teke moja kali lililojikita usawa wa maungio ya kiuno na uti wa mgongo na adui akabweka tena kwa mara ya pili huku Honda akiachia tabasamu lingine la ushindi na akihepa tena kujiweka mbali na adui aliekuwa anageuka kwa gadhabu.

Kisu.

Honda aliona kisu mkononi mwa adui na hapo akajipongeza kwa zile hesabu zake za kuwa mbali na adui.

Adui alitupa mikono harakaharaka kumchanganya Honda kisha akaachia teke kali lililopanguliwa kistadi na Honda kisha adui akatumia nafasi ile kumchapa konde kali la mbavu kama malipizi na huku akiachia ukelele wa furaha kwa lipizi lake.

Honda akayumba kwa kupoteza malengo kisha akafanya jitihada kusimama imara.

Hakufanikiwa.

Adui akatumia nafasi ile kumshindilia tena mateke mawili ya kifua na kumtupa kwa kishindo sambamba na kabati la vioo lililokuwa sebuleni pale na kusambaratika chini huku vioo vikimjeruhi hapa na pale.

Kutoka pale alipokuwa ameangukia,Honda alimshuhudia adui yake akinesa kwa aina ya ajabu kabisa na kumfikia pale alipokuwa huku kisu kikiwa kimeshikwa imara mkononi,Honda hakutaka kufa kizembe kwa nguvu alizobakia nazo akasimama kwa kasi kisha akajirusha huku mikono yake ikimkumbatia adui usawa wa kiuno na bega likijikita katikati ya tumbo na kumbwaga kwa nguvu chini ya zulia.

Ingekuwa ni mieleka basi hii ingekuwa ni Roman spear,ila hii sasa wakati huo ilikuwa ni Honda spear.

Walipoanguka chini Honda alizisikia kelele za adui yake wazi wazi masikioni mwake na na yeye akajinasua haraka kutoka pale chini akabaki akiwa amesimama huku akitweta kwa maumivu ya majeraha ya kukatwa na vioo vya kabati.


“Bwege sana wewe”

Jamaa alibweka pale chini huku akijizoa zoa kutoka chini na hapo Honda akapata kumtazama vizuri adui yake na akaona kovu baya usoni pake ambalo dhahiri lilimpa tabu sana yule jamaa kuliuguza bila shaka na lilielekea kumtoa jicho upande wa kushoto.

Kovu lile liliongezea mvuto mbaya kabisa katika sura nyeusi ya shababi yule.


“aah nusura univunje kiuno haini wewe” jamaa alizidi kulalama huku akifanya jitihada za kuupata mhimili mzuri kwa kusimama.


“unataka nini kwangu!” hatimae Honda aliuliza.

Na hapo akashuhudia yule bwege akikenua vibaya na hapo Honda akapata kuona kinywa kibaya kutoka kwa yule jamaa.

Kinywani hakuwa na meno mawili ya mbele na ulimi ulikuwa mweusi tofauti na ndimi za binadamu wa kawaida.

“nautaka mkoba mweusi komredi”

Jamaa alijibu swali la Honda.

Honda akatumbua macho kwa umakini kisha akauliza tena.

“mkoba upi?”


“ule uliopewa na Balozi”

Eh bana eh

Honda akizubaa kwa nukta kadhaa za kutoamini kilichosemwa na adui yake.

Kwa nini!.


Kwa sababu alipewa mkoba na Balozi Sapi ndani ya nusu saa iliopita na hakuwa amemuonesha yeyote ule mkoba muhimu wakati ule.

Honda akakumbuka aliuacha ndani ya gari huko nje.

Hata!

Akaruka juu kisha akaachia teke kali lilokuwa likimwendea yule jamaa,jamaa akalegea kidogo na kulikwepa lakini hakujua hila za Honda akajikuta anapokea konde zito katikati ya kifua,jamaa akabweka kama ngedere anaeiba mahindi.

Adui akaenda chini mazima.

Honda akamwendea huku akiunguruma kwa gadhabu lakini hakufika kwa adui yake ambae alijiinua kwa mtindo wa aina yake kisha akaruka kama kima na kuufikia mlango na kutokomea nje kwa kasi ya umeme.

Honda hakukubali Nae akapiga tambo kubwa na kuufikia mlango,haraka akatoka,lakini kasi yake haikumpa matunda aliotaka,isipokuwa kitu pekee alichoambulia ni kuona namna yule jamaa alivyokuwa akimalizikia nje ya geti na kuliacha likijipigiza kwa nguvu.

“Mkoba!!” Honda alijisemea huku haraka akikimbilia gari lake na kujilaumu kwa uzembe wa kutokutembea nao.

Akafungua mlango wa gari lake na kitu cha kwanza ni kuelekeza macho yake pale ulipokuwa mkoba ule ambao sasa alianza kuupa manani kwa kuwa kuna adui asie mjua akiuwinda.

Kwanini! Hakujua japo alihisi.

“kina nani hawa?” alijiuliza huku akianza kutoka ndani ya ile nyumba ya hayati Bulembo.

Akiwa tayari ametoka nje ya uzio wa nyumba ile,mara akasikia ving’ora vya magari ya polisi vikielekea kule alikotokea.

“shiit!!!” alimaka kwa gadhabu kwa kutoelewa ni nani aliewapigia polisi wa Congo katika uharaka wa namna ile.

“Mambo yanazidi kunoga aisee” alijisemea huku akiongeza mwendo wa gari lake kurudi kwa balozi Sapi kumpa taarifa ya alichokiona kule kwa Hayati Bulembo.

Hakujua yajayo…

***




akasikia ving’ora vya magari ya polisi vikielekea kule alikotokea.

“shiit!!!” alimaka kwa gadhabu kwa kutoelewa ni nani aliewapigia polisi wa Congo katika uharaka wa namna ile.

“Mambo yanazidi kunoga aisee” alijisemea huku akiongeza mwendo wa gari lake kurudi kwa balozi Sapi kumpa taarifa ya alichokiona kule kwa Hayati Bulembo.

Hakujua yajayo…

***

Kizibo alishuka ngazi taratibu na begi lake mgongoni huku akipiga mluzi wa wimbo usioeleweka na mara kwa mara akisitisha mluzi na kujisukutua pembe za meno yake kwa kutumia ulimi.

Ungemuona ungejua katoka kupata stafutahi ahsubuh ile ila sivyo,kwake hiyo ilikuwa ni furaha ya kukamilisha jambo fulani kwa uhakika.

Alizidi kupiga hatua zake kwa uhakika kabisa huku mluzi usioeleweka ukisindikiza hatua zake kutoka nje ya hoteli ile ya kifahari na yenye hadhi kubwa katika mji wa Ivuba ndani ya jiji la Kinshasa.

Kizibo alizidi kupiga hatua kuelekea upande kulipokuwa na maegesho ya magari katika upande wa kushoto wa lango la kuingilia ndani ya hoteli ile,lakini mara akasita kuendelea kwenda kule alikokusudia.

Akaitazama saa yake,nayo ikamhakikishia zilikuwa zimepita dakika arobaini na tano bila ya Kojo kurejea na ndie alikuwa na gari la kuwatoa pale na kuendelea na majukumu mengine,sasa gari haikuwepo na bila taarifa ya Kojo.

Hisia zake zikashindana kumpa hisia kamili ya kinachotokea huko aliko Kojo.

Fikira zake zikakoma baada ya simu iliokuwa kwenye mfuko wake wa koti mchinjo aliokuwa amevaa kuita akaitoa na kutabasamu alipoona mpigaji..

“Nambie shetani!!” akatulia kidogo na kusikiliza upande wa pili kisha akasonya na kukata simu huku akianza kubadili uelekeo na kuchukua ule utakao mtoa kabisa nje ya himaya ya hoteli ile.


Nje kabisa aliiona gari yao ikiwa imepaki pembeni kidogo ya barabara,haraka akapiga hatua na kuindea ile gari huku akiwa amehamanika vibaya.


“wewe umekuwaje tena Kojo” aliuliza mara tu alipoingia ndani ya gari ile.

“aisee yule jamaa ndie shetani sasa bwana!!” Kojo alijibu huku mkono wake wa kuume ukifanya jitihada za kujichua upande wa juu kidogo wa jicho lake.

Kizibo akabaki ametumbua macho usoni kwa swahiba wake yule huku akiacha midomo ikimuanguka kwa fadhaa.


“inamaana yule boya ndo kakufanya hivi?” aliuliza Kizibo kwa kutoamini.


“sasa wafikiri nani mwingine!yule jamaa ananguvu sijapata kuona” alijibu Kojo kwa masikitiko ya kukubali kushindwa mbele ya swahiba wake yule wa kufa na kuzikana.


“Dah kwa hiyo ukaumwaga bila…” Akasema kizibo lakini alikatishwa na swahiba ake.


“Aisee bora kujipanga upya jamaa kaniotea vibaya”


“Aisee!!” Kizibo alistaajabu kuona swahiba wake anakubali kushindwa mbele ya windo lao kwa mara ya kwanza tangu waanze kufanya kazi yao hiyo ya umamluki.

Na hata wakati akiendelea kushangaa uso wa Kojo uliozidi kuharibiwa kwa vipigo,na ni wakati huo simu ya mwito maalumu ipopigwa..

Walitazamana.


Kizibo aliipokea na pasipo kusema kitu akawa anasikiliza maelekezo kutoka upande wa pili na maelekezo yalipokoma,Kizibo akaachia tabasamu la upande mmoja huku ulimi wake ukisukutua pembe za meno yake,kisha akaachia mluzi usioeleweka masikioni mwa Kojo.


“sasa tajiri anasema turudi kupumzika matokeo amepata ya kazi yangu,Mkoba ule na kilichomo kasema tumwachie yeye ataona cha kufanya katika mkakati wa pili” alifafanua kwa kirefu Kizibo.


“Bora nami nijitibu kidogo mana yule jamaa angenivunja leo”

Wakaliondoa gari.

Lakini kama walijua wanaenda kupumzika walijidanganya.


***

Mawazo yalikuwa yanampita kichwani kwa kasi sana ,kwa kutoelewa ukweli wa mambo ulivyo,mara kwa mara alikuwa anatizama nyuma kuona kama alikuwa hafuatiliwi na alipojiridhisha aliendelea na safari yake.

Nusu saa badae alikuwa anashugulika na kuiweka sawa gari yake kwenye maegesho yalio katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Congo.

Honda alitizama nje kabla ya kushuka ndani ya gari na alichokiona kikamtia mashaka.

Akashuka taratibu huku mkoba mweusi ukiwa ameushika katika mkono wake wa kulia.

Alitembea taratibu kuelekea eneo la mapokezi,na hapo akaushuhudia mshituko na taharuki kwa baadhi ya wafanyakazi wa ubalozi ule.

Akamakinika zaidi hasa alipoona polisi wa Jamhuri ya Kongo wakiwa ni miongoni mwa wafanyakazi wale.

Akaangaza macho yake,kumtafuta mtu muhimu wakati ule na akamuona nae akiwa ni miongoni mwa watu waliopagawa kupindukia.

Walitazamana kisha zikafuata ishara na hapo mtu yule agaeuka na kuelekea upande kulikokuwa na ofisi zake,Honda akamfuata.

Alikuwa ni mkurugenzi wa usalama ndani ya ubalozi japo wachache walijua hivyo na wengi ya wafanyakazi walijua ni Ofisa uhamiaji pale Ubalozini.


“Kuna nini Mndewa!” aliuliza Honda punde tu baada ya kuingia ndani ya ofisi ile.


“Balozi Ally Sapi kauwawa na pia taarifa nyingine ni kuwa Bulembo nae kauwawa leo ahsubuh” alijibu kwa kirefu Mndewa.


“Doh!!.. Bulembo taarifa zake ninazo ila hii dah..” Honda alishindwa kumalizia na hapo akajikuta anaangusha chozi bila kutoa sauti.


“wamewezaje kumuua Balozi aisee!” Honda aliuliza kwa kutoamini kabisa tukio lile.


“kwa haraka haraka inaonekana amedunguliwa aisee” alijibu kwa huzuni Mndewa.

Kimya kikapita.

“Sasa umeshatoa taarifa makao makuu!” aliuliza Honda.

“ Huwezi amini,simu tangu ahsubuh hazitoki eneo hili,ila tumejaribu kutuma ujumbe wa tarakirishi na bado hatujajibiwa kabisa Honda”

Mkurugenzi Papi Mndewa alionesha masikitiko yake katika hilo.

“Hujuma!” Honda alijiwazia kisha bila kutoa na kumshirikisha mkubwa wake juu ya mashaka yake hayo, akamuomba waelekee huko ofisini kwa Balozi Sapi.

***

Dakika tatu baadae walikuwa ndani ya ofisi za Balozi Sapi na kulikuwa na askari kadhaa kutoka kituo kikuu cha polisi Kinshasa waliokuwa wakiendelea na utaratibu wao ili kuhakikisha wanakuwa na ushahidi mzuri katika harakati za kumsaka muuaji.

Mbali na askari hao,pia walikuwapo wafanyakazi kadhaa wa ubalozini.


Honda akatembea taratibu na kuufikia mwili wa hayati Ally Sapi uliokuwa umeshafunikwa shuka jeupe.

Aliufunua na kutazama na alishuhudia namna risasi ya mdunguaji ilivyofanya kazi yake ipasavyo.

Akatikisa kichwa kisha akaufunika ule mwili na kuendelea kuangalia kwa jicho la upelelezi ndani ya ofisi ile.

Macho yake yakagota kwenye dirisha.

Hapo akaona mpasuko wa kioo,na moja kwa moja akili yake ikamwambia mdunguaji alikuwa upande ule wa ile Hoteli.

Lakini kuna kitu kingine akaona hakiko sawa katika dirisha lile.

Mwanzo hakutilia maanani wakati walipokuwa wakizungumza na Balozi Sapi ahsubuh ila sasa alianza kuhisi jambo katika dirisha lile.


Dirisha lilikuwa wazi.

Yaezekana uwazi ule usingemshitua,ila kilichomshitua ni namna lilivyokuwa kimefungwa na hapo akili yake ikakumbuka kuliona dirisha likiwa wazi wakati akiwa anazungumza na Balozi Sapi.

Makusudi hii!

Alijiwazia hivyo wakati akijua kabisa Balozi Sapi hakuwa na kawaida ya kuliacha wazi hilo dirisha hata mara moja.

Akawageukia wafanyakazi wachache waliokuwa mle ndani,akawatazama mmoja mmoja bila kujua msaliti ni yupi.


“Nani hapa Honda Makubi?”

.sauti ya askari mmoja ikaunguruma kutokea mlangoni alikokuwa anaingilia yule askari ambapo baada ya kugeuka,Honda na wenzie walijua fika cheo cha askari yule ni Sajini kulingana na vazi alilokuwa amevaa kumtambulisha kwa cheo hicho.


“watu wote mle ndani walitazamana huku wote wakizisikia hatua zilizokuwa zikipigwa na Sajini Kebu Habyirimana.


“jamani okoeni muda tuna majukumu mengi ya kufanya huko!” alikoroma Sajini Kebu.


Sajini Kebu alizidi kuzipiga hatua zake taratibu hadi ulipokuwa mwili wa Balozi Ally Sapi,akainama na kuufunua kidogo kisha akaufunika na kunyanyuka.


“nani mwenye ji…” Sajini Kebu hakumaliza kauli yake,akakatishwa na sauti ya mtu mle ofisini.


“Ni mimi hapa,naitwa Honda Makubi!”


Sajini akageuka taratibu na kuelekeza kule usawa wa dirishani alikosikia sauti ya mtu aliejitambulisha kama Honda Makubi,macho yao yakagongana na kila mmoja aliyasoma mengi yalioongelewa na macho yale.


Wakati Sajini Kebu yeye akiona macho makini na yenye kutaka kujua utata wa kifo kile cha Balozi Sapi,..

Honda yeye alikuwa anatazama macho yaliojaa uhalifu na ujivuni wa matukio mengi ya umwagaji damu,alihisi yote lakini hakuwa na sauti ya kusema mapema kiasi kile kumtuhumu Sajini Kebu kuhusika na masakata yote yale ndani ya mitaa ya Ivuba Kinshasa Congo.


“Bwana kwa maelezo yaliopatikana inaonekana mtuhumiwa wa kwanza ni wewe,hivyo tutaenda na wewe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi!” alisema Sajini Kebu huku akipeperusha juu karatasi ya arresting order


Kaipata wapi muda mfupi hivi!!


Lilikuwa swali lilitambaa haraka kichwani mwa Mkurugenzi Papi na Honda Makubi kisha bila kutarajia na kama mawazo yao yalikua sawa wakajikuta wakitazamana na hapo wakapeana ishara ya kijasusi walioilewa wao wenyewe wakati ule.


“Sawa afande!!” alijibu Honda.

Kwa jibu lile ilikuwa ni zamu ya Sajini Kebu kushangaa.

Katika majibu rahisi aliotegemea kuyapata kutoka kwa Honda hili la kukubali bila kuhoji lilimshangaza sana,japo alijaribu kuuficha mshangao wake ila si kwa mtu makini kama Honda makubi na hilo alilitegemea.


“Nyakati kama hizi adui wa kwanza ni anaekukamata alietuma ukamatwe” alijiwazia Honda.


“Aah unampeleka kituo gani Sajini” alihoji Mkurugenzi Papi.


“Kituo kikuu hapo Ivuba” alijibu Sajini Kebu huku akianza kuondoka ndani ya ofisi ile na nyuma alifuatiwa na Honda Makubi.


Walitembea kwa dakika tatu nzima,kutoka zilipokuwa ofisi za Balozi Sapi hadi kutoka nje ya jengo lile la ubalozi.


Nje macho ya Honda yalikuwa yanatembea kwa hatua za uhakika na hapo yakatua kwenye gari aina Toyota defender ya kipolisi na ndani yake walikuwamo watu watano waliokuwa wamebeba silaha aina ya SMG na kila mmoja alikuwa amevaa fulana ya kuzuia risasi,mbali na hivyo kila mmoja alikuwa amevaa mipira mizito ya kufunika viganja vya mikono yake.

Yote haya aliyaona wakati wakizidi kupiga hatua kulifikia gari lile ambalo aliliona tangu akitoka ndani ya ubalozi.


Hatua kadhaa kabla hawajalifikia lile gari wawili Kati ya watu wale watano wakaruka chini katika namna ambayo ilimfurahisha Honda.

Ilimfurahisha kwa sababu aina ile isingeweza kuwa ya askari wa kawaida,aina ile ni ya makomando waliofuzu vizuri kabisa.

Kumekucha!!


Honda na Sajini Kebu walilifikia gari lile na hapo Sajini Kebu akaenda kukaa mbele upande wa pili wa dereva.


Honda hakuwa amefanya jitahada zozote kupanda katika karandinga lile na alikuwa na sababu zake za kufanya hivyo.

Haukupita Muda mrefu alichokitaka kikatimia na hii ni baada ya wale askari wawili waliokuwa wamesimama chini,mmoja wapo alimfuata kwa hatua za ajabu kabisa na alipomfikia akamshika suruali yake na kuinyanyua juu (huku kwetu tunaita Tanganyika jeki) na punde askari wa pili nae akamcharaza mtama safi kabisa kwa aina ya kidon,mapigano adhimu katika nyanja ya ujasusi na hapo Honda akajikuta anapaa juu bila kupenda na kabla hajaanza kushuka chini akadakwa na mikono imara ya askari mwingine aliekuwa ndani ya karandinga,kisha akamvutia juu kwa kasi na kumbwaga katikati ya miguu ya askari watatu waliokuwa wamebaki mle ndani ya karandinga ile na alipotaka kujizoa zoa kusimama akakutana na midomo miwili ya smg ikimtizama huku masikio yake yakinasa sauti ya mwendo wa karandinga lile na alipotizama kwa makini askari wote watano walikuwa ndani yake, hakujua wamepanda saa ngapi wale wawili kutoka kule chini walikomwadhibu.


Honda akatabasamu na hapo lengo la kutaka kujua uwezo wa askari wale lilikuwa limetimia,

“hakika hawa si askari polisi wa kawaida ni zaidi ya askari,wanauwezo na nguvu na uharaka wa mawasiliano” alijisemea Honda Makubi.


Safari yao ilikuwa imetawaliwa na ukimya wa kutisha,hakuna aliemsemesha mwenzie na muda wote macho ya askari wale hayakutoka kwa Honda,walikuwa makini na kila mjongeo alioufanya Honda.


Akili ya Honda iliendelea kufanya kazi kwa kasi na hasa hisia zake zilipomwambia hakuwa katika mikono salama,akautazama mkoba mweusi uliokuwa umetulia ubavuni mwake huku mikanda yake ikiwa imepita juu ya bega la kulia na kushuka hadi upande wa kushoto wa mbavu zake.


Akakumbuka alikuwa amepewa mkoba ule na Hayati Ally Sapi na hakuwa amemwambia kuna nini mana hata Sapi mwenyewe alikuwa amepewa na marehemu Bulembo.

Akiwa ndani ya fikira hizo akakumbuka kikaratasi alichotoa kwenye soksi za marehemu Bulembo kabla hajakurupuliwa na yule mtu mbaya wa sura na ulimi wa ajabu hajapata kuona.

Alitamani kukisoma kile kikaratasi,ila akajionya kutokufanya kosa lolote katika wakati kama ule ambao hajui wapi anapelekwa.



Alitamani kukisoma kile kikaratasi,ila akajionya kutokufanya kosa lolote katika wakati kama ule ambao hajui wapi anapelekwa.

*****


Gari ilizidi kuacha mji wa Ivuba na haikufuata barabara kuu ya Julius Nyerere kuelekea katikati ya Mji wa Kinshasa au barabara ya Nailogi kuelekea kituo kikuu cha polisi Ivuba,badala yake ikawa inaelekea katikati ya mji unaokaliwa na waasi wa ADF(Allied Democratic Forces) hiki ni kikosi cha waasi kinachoshambulia mara kwa mara nchi ya Congo japo hujipambanua kama kikosi kinachompinga Rais wa Uganda.


Karandinga lilizidi kuiacha Ivuba na Kinshasa na sasa uelekeo wake ulikuwa ni kaskazini mwa Congo katika Jimbo la Kivu.


Safari ilikuwa ni ya mwendo kasi sana na muda wote watu wale walikuwa kimya kabisa.


Wakiwa wameanza kutoka kwenye makazi ya watu mara gari ikasimama gafla na haraka Sajini Kebu akateremka kisha akaja nyuma ya karandinga lile,hakusema kitu akatoa ishara fulani na mmoja kati ya askari akashuka chini na kwenda kumsikiliza Sajini.


Honda alikuwa akiwatizama kwa makini sana na aliona wakiteta jambo huku wakimtizama kwa macho ya wizi wizi.

Macho yao na maongezi yao yakamtia shaka ila akajipa muda wa maamuzi kwa sababu hadi muda huo hakujua nini alitakiwa afanye na pia hakujua kwa nini mauaji yamewaandama katika ofisi yao,hivyo alihitaji kujua zaidi ila alikwamishwa na aina ya watu waliomzunguka.

Sajini Kebu aliendelea kuteta na yule askari aliemuita huku kila mara wakiendelea kumtazama Honda.

Baada ya mazungumzo yao kuisha ndani ya dakika tano,Sajini Kebu na yule askari wajongea kwenye lile karandinga na walipolifikia,tofauti na matarajio ya Honda kuwa Sajini arudi kuvunja kishoka kule mbele na safari iendelee,ilikuwa tofauti badala yake wote wawili wakaja hadi nyuma ya karandinga na kisha wakapeana ishara na wale waliokuwa ndani ya karandinga lile kisha wakateremka wote wanne waliokuwa wamesalia na hapo ndipo Honda akachezesha akili yake kuona lipi rahisi kulifanya kwa wakati huo na akapata wazo moja tu,kukisoma kikaratasi alichokichukua kwa marehemu Bulembo.

Akakisoma ila hakuelewa kilichoandikwa kwa uharaka ule,akakariri kilichoandikwa mana hakutaka kuamini kilikuwa kimeandikwa bahati mbaya,na kama ni bahati mbaya inamaana gani kufichwa kwenye unyayo wa miguu na kufunikwa na soksi?

Mana ipo!!

Akarudia tena kukisoma.


“142BOULEVARD DU JUIN

B. P. 1612

KINSHASA CONGO (81).”


Alipohakikisha kilichokuwa kimeandikwa kimemkaa kichwani,akakitafuna haraka sana kile kikaratasi na kukimeza.

Kitendo hiki kilifanyika ndani ya nusu dakika tu kiasi kwamba hata wale askari licha ya kuendelea kumtazama hawakufanikiwa kuona uharaka wa kitendo kile.


Wajanja walikutana na mjanja!!.

Dakika mbili badae askari watatu walipanda kwenye karandinga na bila kumsemesha wawili wakamfuata na kunyanyua juu kimabavu,nusura wambwage chini kisha kwa mbwembwe wakamsukuma nje ya karandinga nae akatua chini kwa mbwembwe zile zile bila kuumia na ilikuwa rahisi kwake mana walikuwa hawajafanya jitihada zozote kumfunga.

Kitendo chake cha kutoanguka kikawa kama kimewatia hasira,wale wawili waliokuwa wamebaki chini wakampokea kwa kipigo kizito bila kujali anakwepa au la.

Kipigo alichopewa Honda ndani ya dakika tano kilitosha kumuacha bila nguvu za kusimama na hapo ndipo akagundua alikuwa anapigwa na askari wote watano isipokuwa Sajini Kebu,ambae muda wote alikuwa kimya akishuhudia vijana wake wakimsulubu mfanyakazi yule wa ubalozi wa Tanzania nchini Congo.


Sajini Kebu alipiga hatua moja na kufika pale alipokuwa Honda akitweta kwa maumivu,akamwinamia na kumshika ukosi wa shati lake kisha akamvuta kwa nguvu na kufanya nyuso zao zitazamane kwa karibu zaidi na bila kusema kitu Sajini Kebu akamshushia kichwa kizito Honda na kumuacha akiwa na nundu kwenye paji la uso huku akijibwaga chini kama mzigo ulioozesha matunda.


Honda alipoanguka akafanya jitihada za kunyanyuka na hapo akaona Sajini Kebu anamfuata tena kwa gadhabu na bila kusema kitu akawahi kuushika mkoba uliokuwa ukininginia shingoni Honda.

Honda hakutaka kukubali kizembe,nae akajitutumua kumdhibiti Sajini Kebu asichukue ule mkoba.

Dhamira yake ya kuulinda ule mkoba ukagonga mwamba bada ya mmoja wa askari wale kumchapa teke la kifua na kumyanyua juu kisha kubwagwa chini kwa uzito wa teke lile na hapo askari mwingine akaudaka ule mkoba na kuutoa shingoni kwa Honda.

Honda hakuwa na la kufanya akabaki akitweta kwa maumivu huku akipanga namna ya kuwadhibiti watu wale ambao tayari walionekana si wema kabisa.


Baada ya Sajini Kebu na wenzie kuona wamemdhibiti Honda; akauchukua mkoba ule na kuanza kuukagua kwa umakini sana ...




Baada ya Sajini Kebu na wenzie kuona wamemdhibiti Honda; akauchukua mkoba ule na kuanza kuukagua kwa umakini sana.

Kitu cha kwanza kukutana nacho ni karatasi mbili nyeupe za ukubwa A4,sura ikambadilika Sajini Kebu, akafanya papara kuanza kupekuwa mkoba ule, na hapo akavuta hisia za wengine nao wakapoteza umakini wa kumlinda Honda, wakabaki wanashangaa zile karatasi nyeupe mbili zilizokutwa ndani ya mkoba walioagizwa kuukagua.

Kama Sajini Kebu alidhani mshangao huo ulikuwa kwake tu,alikuwa anajidanganya.

Mshangao mkubwa yaezekana kuliko wote waliokuwa eneo lile alikuwa ni Honda Makubi.

Licha ya wepesi wa wa mkoba ule, lakini hakudhani kutakuwa na karatasi mbili pekee tena moja ikiwa haijaandikwa kitu kabisa na nyingine ikiwa na namba tu tena namba zilikuwa nne tu huku mbili kati yazo zikiwa zimezungushiwa duara huku hizo mbili zingine zikiwa zimepigiwa msitari mfupi kwa chini kila moja.

Ina maana gani hii!!!!


Wakati Honda akiendelea kujiuliza; wakati huo Sajini Kebu nae alikuwa anapata mshangao mwingine zaidi.

Ndani ya mkoba alikuta kidole cha shahada cha binadamu, na kilionekana bado kina damu kabisa na ilionekana haina siku nyingi damu ile.

Aliogopa kukishika kidole kile na hata yeye hakujua kwa nini alijikuta anaogopa gafla namna ile.

“inamaana,… aha..” Sajini Kebu akili ilishindwa kupambanua na akajikuta anaishia kutabasamu tu huku akipitisha macho kushoto na kulia kuhakikisha wengine nao wanauona mshangao wake.

Sajini Kebu macho yake yakatua kwa Honda aliekuwa bado amekaa chini nae mshangao ukiwa juu yake. Sajini akamkazia macho Honda.


“Nini hii!?” aliuliza Sajini Kebu huku akiwa bado ameushikilia mkoba ule mweusi na kuulaza upande ili zipu ya katikati iliokuwa wazi imsaidie Honda kujua yaliomo ndani ya mkoba na kubwa zaidi wapate kujua Honda anataarifa na yaliomo?


“Na mimi kama wewe komredi!” alijibu Honda huku dhahiri mshangao ukiwa bado u machoni pake na masuali kadhaa yakiwa yanatiririka kichwani kwake.

“Kile kidole cha nani, na kwanini karatasi hazijaandikwa kitu” Maswali hayo yalipita bila kupata majibu.

Honda hakupata jibu la hayo maswali ila aliamini majibu yapo kwenye hizo karatasi,lakini sasa hiko kidole kimefuata nini tena humo kwenye mkoba!

“ina maana hata balozi alijua kuhusu hiko kidole? Mbona hakunambia?” Maswali kama mvua yalizidi kutiririka kichwani mwa Honda.


Sajini Kebu akiwa bado haamini alichokiona,mara hii akaamua kung’uta kabisa mkoba ule.

Hali ile ile!

Hakuna jipya lilopatikana zaidi ya karatasi zile mbili na kile kidole.


“sasa utatuonesha ilipo maiti ya hiki kidole Honda!” Sajini Kebu aliongea huku akiutupa ule mkoba mweusi chini na kupiga hatua ndogo ndogo zilizoonesha gadhabu ya hali ya juu kwa mtembeaji yule, ofisa wa jeshi la polisi Congo.

Hatua za Sajini Kebu zilihesabiwa vizuri na Honda akiwa pale chini, kisha akaacha masikio yaendelee kuusikia mshindo wa miguu ya Sajini Kebu na macho yakawatazama askari wengine watano na bunduki zao mikononi.

Alihitaji kufanya jambo.

Muda haukuwa rafiki wakati huo na alihitaji majibu kuhusu mauaji ya Bulembo na Balozi Sapi, hivyo kusubiri kipigo kutoka kwa watu wasio wema, ilikuwa ni kuzidi kujiweka mbali na ukweli.


Kebu alizidi kumsogelea Honda huku mkono wake ukiwa unatoa bastola iliokuwa ameisunda kiuononi kwake,hata wenzie hawakujua alitaka kuifanyia nini ikiwa walimhitaji Honda katika harakati za kuzima jambo wasilotaka lijulikane.


E bana eh!


Honda alisimama kwa mtindo wa ajabu haijapata shuhudiwa na askari wale na mkononi mwake alikuwa na kisu.

Alipokipata hawakujua!

Ila Honda alikichukua kwa mmoja ya askari wale wakati wakimshambulia kwa kipigo.

Wakati wakishangaa kasi ya usimamaji wa Honda, tayari Honda yeye alikuwa uso kwa uso na Sajini Kebu na bila kuchelewa akamnasa kofi kali la uso, wakati Sajini akifumba macho kusikilizia maumivu, tayari kasi ya Honda ilikuwa imemfikisha nyuma ya mwili wa Sajini.

Kebu bila kupenda akajikuta amejaa kwenye kabari matata ya Honda huku kwa mbali akizisikia pumzi za Honda nyuma yake.

Akawa mbuzi wa kafara!!

Askari wengine wakabaki kuzikoki silaha zao bila kuwa na maamuzi sahihi ya kufanya kumuokoa kibaraka mwenzao.


Honda nae akazidi kupiga hatua za kuwatoka, lakini anawatokaje wakati karatasi na kidole vimesambaratika chini?.


Pagumu!!


*****


NCHINI TANZANIA.


..JIJINI MWANZA….


“Hata!! Hii imekaaje tena sasa!!” alijiwazia wakati akiwa ameshika kiuononi na mkono mwingine akivua kofia iliokuwa imemziba uso wake, hakuwa anaamini anachokiona.Hii ilikuwa ni nyumba ya pili alioikusudia na hali aliikuta sawa na alikotoka.

Chumba alimokuwamo kulikuwa kumeparanganyika hovyo hovyo kuonesha kwamba kulifanyika varangati na upekuzi wa hovyo kabisa.


“na wao walikuwa wanatafuta nini sasa!” alijiuliza tena bila wa kumpa jibu kuonekana.


Hata!


Aliendelea kutalii kwa macho kile chumba ili walau apate pa kuanzia kujua maswahibu yaliomkuta mtu aliemkusudia.

Hakuona kitu zaidi ya maiti ya mwanaume iliokuwa ikimtizama kwa huruma ya kukutana na kiama.


“Hii ni kazi maalumu sasa nani kaaingilia gafla hivi mmh” alijiuliza tena bwana yule huku akitoa simu mfukoni mwake na kupiga pahali.


“Nambie Mtegaji !” ilisema sauti upande wa pili.


“Aisee hali ile ile kama kule nilikotoka” alisema Mtegaji na huku akisikilizia mguno wa mshangao upande wa pili.


“Sasa Mtegaji ; huoni wanakuchokonoa afu wanarudi pangoni?”ilisema sauti upande wa pili.


Kama kuna mtu alijua kucheza na akili za Mtegaji ni huyu aliekuwa anaongea nae na hapo alikuwa amegusa penyewe

Kajazwa kichwa ebo!!

Mzee Kinyonga alikuwa amempa ruhusa kijana wake wa kazi maalumu ya kuwasaka wanaotaka kutibua mipango yao waliopewa kuikamilisha.


“Mtega Nyoka, hao Nyoka wananitega mi Kinyonga, hebu wapekenyue komredi!” ilisema sauti ya Mzee Kinyonga na kukata simu.


“wao Nyoka mi mtegaji, ama zao ama zangu” alijiwazia


“Mimi ndie MTEGA NYOKA bana waga hawanishindi hawa Nyoka” alifunga mlango na kutokomea kama alivyokuja.


Mtega Nyoka!!

Ndio alikuwa ni Mtega Nyoka, Nyoka wanaomwinda Mzee Kinyonga!!


Ila kama alijua ni kazi rahisi kumlinda Kinyonga mbele ya nyoka wakaao pangoni, yaezekana alikosea kufikiri vema.




Mtega Nyoka!!

Ndio alikuwa ni Mtega Nyoka, Nyoka wanaomwinda Mzee Kinyonga!!


Ila kama alijua ni kazi rahisi kumlinda Kinyonga mbele ya nyoka wakaao pangoni, yaezekana alikosea kufikiri vema.

****

Katika mitaa ya Igoma, jirani na Ndama Hotel, msichana wa kadri ya miaka minne alikuwa amesimama kwenye kituo cha kungojea daladala.

Hakuna aliejua safari yake ilikuwa ni kuelekea Kishiri ama aliamua tu kupumzika pale huku akishuhudia magari ya upande wa pili yanayotoka Kishiri na Igoma yakielekea katikati ya mji, na pia akishuhudia magari ya upande wake yakishusha abiria zaidi kuliko kuwabeba.


Alivaa mawani ya jua,na hakuna aliejua kama anatazama kitu ama alikuwa anahamsini zake.


Kama angekuwa ameamkia sehemu safi na yenye hadhi, basi wakati huu angelikuwa ananukia uturi wa kisasa.

Lakini kama ungelimtizama kwa makini basi ungeligundua huyu binti hajapata lau hata nusu maji katika mwili wake kwa siku kadhaa.

Nae hakuonekana kujali uchafu wa mwili wake, pengine kwa kuwa alikuwa mweusi wa ngozi na uchafu haukuwa kigezo kwake tena.


Macho yake yakiwa yamefichwa nyuma ya mawani ila bado yalipepesa eneo lile alilokuwa amesimama na kuna kitu alikuwa anahakikisha upande wa pili wa barabara, kulikokuwa na kituo cha kuoshea magari na pikipiki.


Akatabasamu huku akitaka kuvuta hatua ili avuke barabara.


Akasita gafla huku tabasamu lake likififia na hofu ikauvaa mwili wake.

Haraka akatoa kofia aliokuwa ameishika kwenye mkono wake wa kulia na kupachika kichwani, kisha kama anaekimbia na nusu kutembea kutoka mbali na eneo lile.


Mtega nyoka nae alikuwa pale amekaa huku akiwa na mawazo lukuki, hasa baada ya kulala na kuamka bila kupiga hatua yoyote ile.


Akiwa ametulia tu, huku akiwaza wapi pa kuanzia ahsubuh ile, mara macho yake yakatua kwa mwanadada mrefu mweusi mwenye asili ya kitutsi akiwa amevaa miwani na kofia mkononi huku mgongoni akiwa na kibegi kidogo ambacho hakikuonekana kubeba nguo yoyote.


Kama ilivyo kwa wanaume wengi;nae Akaanz kumthaminisha binti yule huku akisahau mawazo yaliomfikisha pale.


Mbali ya tathimini yake, ila hakukawia kujua uchafu uliokuwa kwenye mavazi ya binti yule ambae hadi wakati huo hakuwa amefanya tashititi yoyote ile kumuangalia yeye ama yeyote aliekuwa nyuma yake.


Ilikuwa ni rahisi kwa mtu wa kawaida kuhisi binti yule anamatatizo ya akili ama kaibiwa siku chache nyuma, ama katoroka kwao na kafika mjini pasi na ramani ya kumfanya uzuri wake ubaki katika thamani yake. Lakini ilikuwa tofauti kidogo kwa Mtega nyoka ambae aligundua kitu kingine kabisa.

Kwa mtazamo wa haraka kulingana wajihi wa binti yule, aligundua yaezakuwa si mkazi wa jiji la Mwanza na Tanzania kiujumla.

“Mnyarwanda huyu binti” alijisemea Mtega nyoka huku akiamua kuacha kumtazama binti yule ambae aliamini tayari amekutana na wajanja wa mjini kulingana na hali aliokuwa nayo binti yule.


Mtega nyoka aliamua kuendelea kuwaza hili na lile na sasa alipata wazo moja tu,nalo ni kumtafuta msanifu wa majengo aliekuwa anafanya kazi binafsi.

Mbali ya kupata orodha kamili ya watu wanaofanya kazi na msanifu huyo; lakini pia angepata mwanga kidogo ni kwanini wafanyakazi wa msanifu huyo wa majengo walikuwa wanakufa vifo vya ajabu kiasi kile huku yeye akiwa nae akiwa amepewa kazi na serikali yake kuhakikisha wasaidizi wa msanifu mkuu wanafanywa ilivyotakiwa kufanywa ili kulinda itifaki.


Ni wakati akianza kujiinua kutoka alipokuwa amekaa, ndipo alipoona jambo lingine lililomsitua zaidi,yule binti alikuwa anaharakisha kuondoka pale kwa mwendo wa nusu kukimbia na nusu kutembea.

Ingelikuwa macho ya kawaida ungeona ni haraka tu za yule dada,lakini macho ya Mtega nyoka, yaligundua hofu na mashaka kwenye mwendo wa binti yule.


Kwa nini!! Hakujua.


Mawazo yake yakamtuma amfuate yule binti lakini akajikuta hana sababu ya kumfuata.

Akapuuza.


Yule binti alizidi kukata mitaa kuelekea Igoma katikati huku kila mara akigeuka na kuhakikisha usalama wake,alikokuwa akielekea hakupajua, japo aliamini aelekeako atapata mawazo mapya kuhusu maswahibu yanayompata na namna ya kukabiliana nayo japo aliamini kupona ni miujiza ya mwenyezi Mungu.

Roho mkononi!

Lakini kuna kitu kilichomchanganya akili zaidi ni kile alichokiona.


Aliemhitaji alimwona ni baada ya kumtafuta ndani ya mji wa Mwanza karibuni siku tatu. Lakini aliekuwa anamkimbia alimwona pale kwa mtu aliekuwa anamtafuta kwa udi na uvumba.


“alijuaje nitafika kwa Mwasu?” alijisemea binti yule.

“mh” akaguna na kusita kuendelea kupiga hatua zaidi.


“Mungu wangu!!” akasema kwa hamaki baada ya kuhisi jambo baya linaweza kumtokea Mwasu, au Mama Ujazo kama walivyopenda kumuita wateja wa chakula chake.

Binti yule akapiga hatua ndefu zaidi kurudi kule alikomwona Mwasu,huku dhahiri shahiri akionekana kupagawa kwa alilokuwa ameliwaza.


Dakika sita baadae alikuwa anatazamana na binti wa miaka kama kumi na sita hivi; aliekuwa anahudumia wateja kwenye mgahawa ule wa maturubai.


“kuna wali maharage;ugali dagaa..” alitaja vyakula vilivyokuwa vinapatikana pale mgahawani kwake.


“sihitaji chakula mdogo wangu” alijibu binti aliefika pale.

Ikawa mshangao kwa binti anaehudumia.

Lafudhi!!

Msukuma yule anaehudumia kwenye mgahawa wa Mama ujazo,alibaki anashangaa lafudhi ya mgeni wake yule,haikuwa lafudhi ya Kitanzania,lakini kubwa lafudhi ile inaufanano kwa mbali na lafudhi ya Mwasu.

Akashangaa!!

Licha ya kushangaa, ila hakutaka fikira zake zimuibulie maswali.

Akabaki kimya kumsikiliza msichana mwenzie alimzidi kimo cha urefu na weusi wa kung’aa.


“Namuulizia Mwasu!” alisema binti mweusi huku akimtizama Msukuma wa Bariadi.


Msukuma wa Bariadi akagundua kitu kingine tena.

Ustarabu!

Binti aliekuwa mbele yake, hakuwa na ustarabu wa Kitanzania,Mtanzania yeyote akitaka kuuliza lazima aanze na neno ‘Samahani’ila huyu huo ustarabu hakua nao kabisa.

“Sio Mtanzania huyu” alijiwazia Msukuma.


“mmh hilo jina silifahamu dada” Binti wa kisukuma akajibu huku bado akiwa amemkodolea macho binti mgeni.


Binti mgeni akalikumbuka jina maarufu aliloambiwa na Mwasu siku kadhaa nyuma, jina hilo lilimeza jina lake la kuzaliwa.


Mama ujazo!!


“mh nimekumbuka, anaitwa Mama ujazo” alisema binti mgeni huku akitabasamu ili kumtoa kwenye udadisi mwenyeji wake.


“aah sawa;katoka hapa punde tu na Kaka yake!”


“kaka yake!!?”


“ndio amesema ni kaka yake, na wameenda kwake”


Akili ya binti mgeni ikapiga kite cha hofu baada ya kuhisi huyo kaka alieondoka na Mwasu ni yule aliemkimbia dakika chache zilizopita.


Binti mgeni akasikia tumbo likiunguruma kwa woga,akaangaza kushoto na kulia kuona kama kuna choo maeneo yale,hakukiona.

Jasho la hofu likatanda mwilini mwake,kichwa kikamwasha mithili ya mtu mwenye mba sugu.


“my God! Mwasu hastahili kufa” akajiwazia haraka akataka kutoka mle mgahawani.

Akakumbuka cha muhimu.


“aah anaishi wapi kwani” aliuliza.


“anapoishi sipafahamu; ila ni huko Nyakato Meko” alijibu binti wa kisukuma.


“shiiit” akang’aka kwa fadhaa.

Binti mgeni akaanza kutoka kwa pupa akadakwa mkono.


“Hebu ngoja kwanza; kwani wewe ni nani yake?” aliuliza Msukuma.


“mdogo wake” alijibu Binti mgeni.


“unaitwa nani?”


Binti mgeni akafikiria kidogo kisha akajibu.


“Naitwa Remi”


“ooh, sasa nenda Buzuruga plaza,pale kuna ofisi za Kasuku contractors,hapo kuna mchumba wake anaitwa Malima,yeye anaeza kukufikisha kwake kirahisi,mana hapa harudi tena na mimi sina simu dada angu” alieleza kwa kirefu binti Msukuma.


Remi alishukuru kwa ukarimu wa aina ile kutoka kwa Msukuma. Akaaga na kuondoka kwa haraka ya ajabu huku akimwacha Msukuma akimwangalia bila kujiuliza haraka zile za nini.

Watanzania hatuna udadisi,amani imetujaa!!


***

Nusu saa badae,Remi alikuwa anashuka kwenye daladala huku tumbo la kukata lilomkumba gafla kule mgahawani kwa Mwasu,lilianza tena kukata huku jasho likianza kutoka tena.

Hali ile ilimkuta kwa sababu hakuwa na hakika na kumpata Mwasu.

Akatazama jengo lile lilivyopendeza huku watu wakiendelea na shughuli zao kama kawaida. Macho yake yalikuwa yanapepesa kila kona ili apate kuona kibao cha Kasuku Contractors.


Alikiona.


Akapiga hatua za tahadhari huku mapigo ya moyo yakiongezeka kama ya mkimbia marathon.

Alizidi kufuata ulekeo kama kibao kilivyoelekeza.


Alibaki akitazamana mlango wa mapokezi. Mapigo ya moyo yalizidi kwenda kasi ya zaidi.

Akapumua kwa nguvu kujipa ahueni kidogo.

Hatimae akausukuma mlango na kuingia ndani.

Akakaribishwa na mandhari nzuri za ofisi ile ya ujenzi na uhandisi wa majengo,lakini pia ilikuwa na watalaamu wa kusanifu majengo.

Ilimchukua dakika nzima kushangaa na kujaribu kuyazoea mazingira ya ofisi ile.


“Karibu dada!” ilisema sauti ya kike.

Remi alipiga hatua za woga kusogea pale alipokuwa dada aliemkaribisha,ambae hakuwa peke yake,kulikuwa na mtu mwingine mwenye jinsia ya kiume na kimtazamo tu nae alionekana kuwa ni mgeni ofisini pale.


Alieyekuwa pale mapokezi alikuwa ni Mtega nyoka.alifika pale kumuulizia Msanifu mkuu wa majengo wa kampuni ile inayomilikiwa na vijana wa kitanzania.

Akiwa ndo kwanza ameanza kusikilizwa mara akaingia mwanadada ambae yule yule ambae alimwona pale Igoma saa moja iliopita.

Akapigwa butwaa!


Remi hakujali uwepo wa mtu mwingine pale. Alikuwa anataka kuwahi kuonana na Mwasu.


“Nauliza ilipo ofisi ya Malima” aliuliza Remi.


Dada aliekuwa mapokezi akamtazama kisha akainama chini na alipoinuka alikuwa anadaftari na kalamu.


“Andika hapo majina yako na namba yako ya simu” akaeleza dada wa mapokezi.


“Sijui kuandika wala kusoma”


Ajabu hii.


Si dada wa mapokezi alieshangaa jibu la Remi; hata Mtega nyoka hakutaka kuamini kirahisi vile eti katika Dunia hii kuna mtu mwenye uzuri na sura ile hajui kusoma.

Hata!!


“Basi kama ndivyo hutaweza kusikilizwa” alisema dada wa mapokezi huku akionekana kukereka baada ya kuhisi amedharauliwa na mwanamke mwenzie.


“Ni muhimu,tafadhali nielekeze” alisema Remi.


Huku akibinua midomo na kuendelea kuwa bize na Tarakilishi iliokuwa mezani kwake akasema.


“Binafsi au kikazi?”


“Binafsi dada” Remi alijibu.


Muda wote huo Mtega nyoka alikuwa kimya kabisa.


“kwa hiyo Malima ndo huwa anakutana na wasiojua kusoma?” aliuliza dada wa mapokezi.


Tofauti na mawazo yao kwamba yule mgeni asiejua kusoma na kuandika ataendelea kubembeleza; haikuwa hivyo.

Remi akapiga hatua ndefu na kuanza kuondoka ofisini pale huku dhahiri akionekana kupagawa.


Dada wa mapokezi alimwita ila Remi hakugeuka wala kusimama aliendelea kuendea mlango.


“kwani huyo Malima yupo?” Hatimae Mtega nyoka akauliza,na kwa gadhabu dada wa mapokezi akajibu.


“Wameenda kuzika wahandisi wa kampuni waliokufa juzi”


Mtega nyoka hakustuka kwa vifo vya wahandisi hao mana alishuhudia miili yao ikiwa haina uhai usiku wa jana japo akiefanya vile hakumjua.


Mtega nyoka akaona kuna kitu kipo kati ya dada asiejua kusoma na huyo Malima ambae nae alikuwa na shida nae. Mtega nyoka akapiga hatua kumwahi yule dada kabla hajatoka kwenye viunga vya Buzuruga Plaza.


Remi hakuwa mjinga wa kutoka pale bila kujua au kuonana na Malima.


Kabla hajaingia pale ofisini ,pembeni yake aliona saluni ya kike kubwa na kwa tabia za wanaume na wanawake alijua kabisa mmoja ya wahudumu pale saluni atakuwa anajuana na Malima ama la anamawasiliano yake.

Akauendea ule mlango wa saluni.


***

Mtega nyoka alibaki amezubaa kwenye valanda pana iliotenganisha milango ya ofisi zilizokuwa pale.

Hakumuona aliemtaka.

.haraka akakimbia nje ya lango la kuingilia pale Plaza huko nako hakumuona.

Akili yake haikukubali yule dada ametoka ndani kwa haraka kiasi kile.

Akarudi tena kule ndani.

Wakati yeye anaingia akapishana na Remi akitoka huku akiweka kitu kwenye matiti yake.

Mtega nyoka akamwacha apite kisha awe nyuma yake.

Mtega nyoka hakujua sababu gani aliamua kumfuatilia yule dada, ila alijikuta tu anamfuatilia.


Remi aliendelea na safari yake huku akiwa na jambo moja tu,kutafuta simu na kuzipiga namba za Malima alizopewa na mmoja ya wahudumu wa saluni.

Kitu kimoja ambacho hakujua ni kuwa wakati wote wa harakati zake kulikuwa na mtu mmoja zaidi aliyekuwa nae bega kwa bega na sasa alikuwa amepokea amri ya kumchukua mzima ama mfu na kumpeleka kusiko julikana na kazi hiyo ilitakiwa kufanywa wakati Remi akitoka Buzuruga Plaza.


Remi hakujua hesabu anazopogiwa na watu wawili kwa wakati mmoja huku miongoni mwao akiwepo mwenye nia ya kujua sababu ya kumtafuta Malima na mwingine akiwa na sababu ya zaidi kuua.


Hatimae Remi akaanza kuambaa na kuifuata Barabara mara mbele yake akakutana na mtu ambae hakutarajia kumuona pale.

Mtekaji!!

Remi akataka kugeuka na kurudi alikotoka.

Alichelewa!


Mikono imara ikamdaka bega lake na kumvuta kwa nguvu,kisha kikafuatia kibao kikali kilichotua sawia mgongoni mwa Remi huku kikimtoa kelele ya uchungu.


Remi alipepesuka na kutaka kuanguka chini,lakini akajikuta akijaa mikononi mwa mtu mwingine aliekuwa nyuma yake.

Alinguka mikononi mwa Mtega nyoka!


Mtekaji akabaha baada ya kuona kasi iliotumika kumdaka Remi.


“ugomvi huu haukuhusu braza, nipe huyo binti niende nae zangu” alisema mtekaji.


Mtega nyoka alikuwa akitazamana na mtu mrefu mwembamba lakini alionekana kuwa imara sana.

Mbali na mwonekano huo, lakini pia Mtega nyoka aligundua lafudhi ya mtekaji na mtekwaji zinafanana lakini pia hata sura na mwonekano ni watu wa jamii moja.


Kuna nini! Hakujua na la muhimu zaidi ni kuomukoa kwanza binti kisha mengine yatajulikana badae.


Akamvutia nyuma na kuwa kinga yake.

Mchoro ukachorwa huku raia wakianza kujaa kushuhudia linalojiri.


****


KINSHASA CONGO


…kutoka pale alipokuwa Honda alibakiza hatua mbili tu afike kwenye ukingo wa daraja lililokuwa linapitisha maji kwa chini.

Na bado alikuwa amemkaba barabara Sajini Kebu.

Wale askari wengine walikuwa bado wanapiga hesabu za kumwokoa Sajini Kebu kwa kusuburi Honda afanye kosa lolote ambalo hadi wakati huo halikuwa limefanywa nae hivyo wakakosa la kufanya.


Lakini Honda mbali ya kuwa na hesabu za kutoroka bado alikuwa anawazia namna ya kuwatoroka ama kuzua varangati litakalo wafanya wasahau kuhusu mkoba na kile kidole pale chini.


Pale walipokuwa ilikuwa ni barabara isiopitisha magari kwa wingi.

Lakini kwa mbali masikio ya wote yalinasa sauti ya kuja kwa gari kubwa.


Honda alitabasamu huku watekaji wake wakiingiwa na mchecheto wa namna ya kumuokoa sajini Kebu kabla gari hakijafika.


Hesabu zilipigwa pande zote.


Dereva wa lori aliona tukio lililokuwa mbele yake. Kurudi nyuma akaona haiwezekani hivyo akaamua kuongeza mwendo ili avuke pale darajani kwa kasi huku woga ukiwa umemtamalaki na mkojo ukikaribia kugonga hodi kwenye kipamchulio.


Lori lilizidi kukaribia na Honda nae alizidi kujisogeza kwenye ukingo wa daraja huku akiwa bado amemtundika kabali matata Sajini Kebu.

Hatimae lori likafika na hapo ndipo lilitokea tukio ambalo yaezekana Sajini Kebu na wenzie hawatakuja kuliona likijirudia tena katika himaya za macho yao iwe akhera ama Duniani.




Kuna nini! Hakujua na la muhimu zaidi ni kuomukoa kwanza binti kisha mengine yatajulikana badae.


Akamvutia nyuma na kuwa kinga yake.

Mchoro ukachorwa huku raia wakianza kujaa kushuhudia linalojiri.


****


KINSHASA CONGO


…kutoka pale alipokuwa Honda alibakiza hatua mbili tu afike kwenye ukingo wa daraja lililokuwa linapitisha maji kwa chini.

Na bado alikuwa amemkaba barabara Sajini Kebu.

Wale askari wengine walikuwa bado wanapiga hesabu za kumwokoa Sajini Kebu kwa kusuburi Honda afanye kosa lolote ambalo hadi wakati huo halikuwa limefanywa nae hivyo wakakosa la kufanya.


Lakini Honda mbali ya kuwa na hesabu za kutoroka bado alikuwa anawazia namna ya kuwatoroka ama kuzua varangati litakalo wafanya wasahau kuhusu mkoba na kile kidole pale chini.


Pale walipokuwa ilikuwa ni barabara isiopitisha magari kwa wingi.

Lakini kwa mbali masikio ya wote yalinasa sauti ya kuja kwa gari kubwa.


Honda alitabasamu huku watekaji wake wakiingiwa na mchecheto wa namna ya kumuokoa sajini Kebu kabla gari hakijafika.


Hesabu zilipigwa pande zote.


Dereva wa lori aliona tukio lililokuwa mbele yake. Kurudi nyuma akaona haiwezekani hivyo akaamua kuongeza mwendo ili avuke pale darajani kwa kasi huku woga ukiwa umemtamalaki na mkojo ukikaribia kugonga hodi kwenye kipamchulio.


Lori lilizidi kukaribia na Honda nae alizidi kujisogeza kwenye ukingo wa daraja huku akiwa bado amemtundika kabali matata Sajini Kebu.

Hatimae lori likafika na hapo ndipo lilitokea tukio ambalo yaezekana Sajini Kebu na wenzie hawatakuja kuliona likijirudia tena katika himaya za macho yao iwe akhera ama Duniani.


***

Kilikuwa ni kitendo cha gafla na cha kutumia akili zisizo za kawaida kutumiwa binadamu mwenye nyama. Ila kwa Honda iliwezekana.

Japo si kwa kupenda ila ni kujitoa muhanga kuikoa uhai wake.


Lori lilikuwa mita tatu kutoka walipokuwa yeye na mateka wake Sajini Kebu,ni wakati huo Honda alipomsukuma kwa nguvu sajini Kebu kwenye kingo za daraja kisha yeye akajirusha kwa kasi uvunguni mwa lori lililokuwa kasi ya aina yake.

Kitendo kile kilionwa vizuri na askari waliokuwa wanataka kumteka tena,lakini pia kilionwa na Sajini kebu aliekuwa amejipigiza kwa nguvu kwenye kingo za chuma za daraja na kumtoa ukelele wa woga.

Lakini hakuna alietegemea Honda angeweza kujirusha kwenye uvungu kwa hesabu kali namna ile na kwa lengo gani.


Hawakujua!!


Lori lilipita kwa kasi na kumwacha chini Honda aliekuwa amelala kwa kujinyoosha bila kutikisika ili asidhuriwe na tairi kubwa za lori.

Hatimae Lori lilimwacha salama chini na lilipokwisha kupita akanyanyuka kwa kasi ya ajabu na kisu chake mkononi,kisha akawatazama adui zake waliokua bado wamezubaa.


Akaitumia nafasi hiyo kuwashambulia kwa kasi ya aina yake, huku miguu ikinesa kama mcheza dansi ya Apakacha.


Kisu chake alikirusha kwa kasi kikaenda kujikita begani kwa askari mmoja aliekuwa mbele yake, kisha haraka akawageukia waliokuwa kushoto kwake wanajiandaa kuachia risasi.

Mmoja akamchota mtama safi kisha bila kumjali akaruka juu na kumshindilia teke la kifua mwingine aliekuwa anajiandaa kumpiga na kuwaacha wakienda chini kama mizigo huku bunduki ikiangukia mikononi mwake na bila kusita akajiangusha chini na kukoswa risasi kadhaa na alipoachia za kwake zikaangukia kifuani kwa askari wawili na kuwatupa chini wakiwa hawana uhai.


Sajini kebu aliyaona yote ila hakuwa na la kufanya mana kasi ya Honda ilizidi hata kasi ya upepeso wa macho yake.

Na bila kupenda akajikuta akitazamana na domo la AK 47 iliokuwa mikononi mwa Honda tayari kumsambaratisha.

Kebu alipotizama vijana wake akawashuhudia wakijizoa zoa bila kuwa na uimara milini mwao.

Hawakuwa na la kufanya wote wakawa mateka wa Honda.


“Nani kawatuma?” aliuliza Honda.


Hakupata jibu.

Akaona kuwauliza majasusi kama wale kirahisi vile ni kujisumbua anamengi ya kufanya huko mtaani.

Alichoamua nikuwaamuru kujirusha ndani ya mto uliokuwa ukipitisha maji chini ya daraja walilokuwa juu yake.


Sajini Kebu na wenzie wakagoma.


Honda nae ili kuonesha msisitizo akaamua kumpiga mmoja wao risasi ya mguu na kitendo bila kupenda askari wote wanne waliokuwa hai wakajirusha ndani ya mto ambao haukuwa mrefu sana.


Baada ya kuhakikisha hawatakuwa na madhara tena kwake, haraka Honda akakimbia hadi ilipokuwa gari ilokuwa imewafikisha pale na kabla hajafanya lolote akachingulia ndani yake na kuona funguo ipo pahala pake.


Akatabasamu!!


Kisha akafika ulipokuwa mkoba na kuuchukua na kuyafuata makaratasi mawili yaliokuwa yamepeperuka huku na huko.

Akataka kuondoka, akasita.


Kidole!


Aliangaza macho yake huku na huko,haikumchukua muda akakiona.

Akainama kukiokota.

Akasita tena.

Kilikuwa ni kidole cha ajabu sana,kilikuwa kimepasuka pasuka kuota sugu.

Kwa haraka ungelikitizama ungehisi ni kidole cha sokwe.

Akainama kukiokota tena.


Hakufanikiwa!


Nyuma yake alikuwapo mtu na uwepo wake aliuhisi lakini kabla hajafanya lolote akajikuta akipokea teke kali lililomtupa chini kama mzigo na kabla hajasimama akashindiliwa tena teke jingine mgongoni.

Kwa uzito wa mateke yale akaona akilemaa basi ataumia zaidi na pia hakutaka kujichosha sana kwa mapigano wakati bado anasafari ndefu ya kufuatilia kifo cha Bulembo na Balozi Aly Sapi.

Akajinyanyua kwa mtindo safi ila kabla hajakaa sawa akajikuta tena akijaa kwenye anga za mvamizi.

Ila sasa alimuona.


Honda akatabasamu tena, huku akilini akijilaumu kwa kushindwa kumkumbuka dereva wa Land Rover ile ya kipolisi, sasa ndie alikuwa amesimama kukabiliana nae.


Mchoro ukachorwa, huku kila mmoja akijaribu kumsoma mwenzie namna anavyojongea.

Ulikuwa ni mviziano wa akili.


Honda akanesa kwa mtindo wa kidalipoo, kisha akasubiri kwa sekunde bila kufanya maamuzi na ni wakati huo alipoona matunda ya hila zake.


Mvamizi alimfuata Honda kwa kasi ya umeme huku akiunguruma kama bweha, lakini akakutana na hewa kisha akaambulia maumivu ya mbavu za kushoto.


Ngumi ya Honda ilileta matunda chanya.


Wakati mvamizi akijikunja kuugulia maumivu ni wakati huo ambao Honda alienda juu kisha akarudi kwa kutanguliza mguu mmoja mbele na alipotua tayari alikuwa juu ya shingo ya mvamizi na kumsambaratisha chini kwa kutanguliza uso.


Mvamizi alipigwa cub ya Seth Rollins! Hakuwa na uhai tena, na hata angelikuwa nao shingo na uso vingekosa mawasiliano kwa miaka kadhaa.


Honda hakutaka kupoteza muda zaidi akakiota tena kidole kisha akakitia ndani ya mkoba na kuliendea gari la polisi na kutokomea kurudi Kinshasa huku nyuma akiwaacha Sajini Kebu na wenzie wakifanya jihada za kutoka chini ya daraja.


****


Katika watu waliokiwa wamevurugwa kwa wakati huo ni Kizibo na mpambe wake Kojo.

Na hii ni baada ya kupewa taarifa ya kutoroka kwa Honda mikononi mwa Sajini Kebu, na sasa walipewa kazi ya kumsaka katikati ya mji wa Ivuba na Kinshasa kiujumla.


Mapumziko yalitumbukia nyongo mchana kweupe!


“Dah hata kabla sijatuliza maumivu ya kipigo cha yule bwege narudi….” Alilalama Kojo huku akipunguza mwendo wa gari walilokuwamo.


“Acha uoga komredi,umeanza lini kugwaya mkojolea pembeni eeh” alimaka Kizibo huku akimkata jicho la fedheha swahiba wake.


“Wewe hujui tu,yule jamaa anapiga hadi mitindo ya mieleka aisee” alisema Kojo huku akisimamisha gari karibu na supermarket ya Grace market.


“Nini!” aliuliza Kizibo baada ya kuona gari inasimama.


“sasa kusimamisha gari tu unagwaya ukimuona je!” alijibu Kojo kwa lugha ya dhihaka huku akitizama lango la kuingilia ndani ya supermarket ile na hapo ndipo Kizibo nae akaamua kuangalia huko.


“eeh huyu bwege kafika saa ngapi huku” alijisemea taratibu Kizibo huku akisukutua ncha za meno yake kwa kutumia ulimi.


Hata!


Kizibo hakukubali kuendelea kuteseka ndani ya nafsi yake, akashuka ndani ya gari huku akipapasa usawa wa kitovu cha tumbo lake, alipohakikisha bastola yake ipo pahali salama, akafunga mlango wa gari na kuvuka barabara kisha kwenda kule alikokusudia.


“Hii gari imefikaje hapa!” Kizibo alijesemea huku akiangaza huku na huko kuona kama atamuona mtu anaehisi kuifikisha pale ile gari Land Rover ya kipolisi ambayo dakika chache nyuma walitarifiwa ilikuwa na mtuhumiwa wao Honda.


Alah!


“Sasa hapa kafika saa ngapi na yuko wapi?” alizidi kujiuliza Kizibo huku akilizunguka gari lile la kipolisi kwa umakini wa hali ya juu.


Akiwa bado analizunguka ,mara akasikia ving’ora vya gari la polisi likielekea pale haraka akavuka barabara na kurudi ndani ya gari.


Akajikuta yuko peke yake.


“sasa huyu bwege nae..” hakumalizia kauli yake mara mlango wa dereva ukafunguliwa akaingia Kojo huku usoni akizidi kuvimba zaidi ya mwanzo.


Hii kali!!


“hee komredi, kwani ulienda chokonoa mzinga wa nyuki tena!?” aliuliza kwa kushangaa Kizibo.


“Bora hata Nyuki, aisee” alisema Kojo huku akijaribu kuwasha gari lao.


“Aah mzee hebu tulia kwanza, umevimba hivyo huko mbele utaona kweli” alisema Kizibo huku akipeleka mkono ulipo ufunguo ili kumzui Kojo asiwashe kisha akauliza


“Kwani vipi umegongwa na nini tena?”


“Nilikwambia yule jamaa sio aisee,yani unatoka tu na yeye anakuja hapa dirishani na manati ya mzungu, sikuwa na namna kiukweli!”


Midomo ikamwanguka Kizibo.


Akabaki amezubaa kama mgeni aliepigwa denda na mtoto mchanga.


“ina maa…” kabla kizibo hajamalizia; Kojo akadakia


“jamaa kaniteka aisee,”


“Halafu!,”


“Halafu nini wakati unaona usoni matokeo yake!” aling’aka Kojo.


“Ukaumwaga tena” Kizibo akasema huku sasa akibinua kiti alichokalia.


Alichoka!


****


Wakati analiacha pori walilokuwako, Honda aligundua walikuwa wametembea zaidi ya kilomita ishirini na pale walipokuwa, walikuwa ni karibu na mpaka wa kuingia mji mdogo wa Ben ulioko kilomita thelathini kutoka Kinshasa.


Aliamua kutembeza Land Rover kama kichaa alietoroka Milembe na ndani ya nusu saa tu alikuwa ameingia Kinshasa na wakati akiwa kwenye barabara ya RTe Matadi ndipo alipoamua kuegesha gari karibu Grace supermarket.


Mwanzo aliona ni muhimu yeye kupitia chakula cha kopo pale ambacho aliamini kitamfaa mbele ya safari.


Lakini wakati anatoka ili achukue usafiri mwingine na kulitelekeza gari lile pale, akili nyingine ikampa ushauri na akaamua kuufuata.


“ili nifikie majibu haraka, yanipasa kukutana na mtu wa kwanza kulisogelea lile gari” alijiwazia baada ya kuhisi taarifa zake tayari zimewafikia wabaya wake na ambao watakuwa wanalisaka gari na dereva wake.


Akaamua kukaa upande wa pili wa barabara kulikokuwa na harakati mbili tatu za kuwaingizia watu kipato.


Subira yake haikuchukua muda ikawa heri.

Macho yake yakaliona gari jeupe aina ya Toyota Camry ikipaki, kisha akaona watu wawili wakijadili kitu na mmoja akashuka kuliendea lile gari la Polisi.


Hakutaka kungoja sana.

Alimhitaji aliesalia ndani ya gari.

Akapiga hatua na kulifikia gari,akagonga mlango huku bastola ikiwa mkononi mwake na bila kutarajia dereva akashusha kioo.

Pengine hakuwa ameiona bastola.


Hamadi!!!


Akaiona sura mbaya yenye kovu kubwa upande wa kushoto,alikuwa ni yule mtu mwenye ulimi mbaya aliepambana nae ahsubuh nyumbani kwa Bulembo.


Aisee!


Hakuwa na namna zaidi alimuamuru ashuke ndani ya gari nae mtu mbaya akatii.


“Tujifanye marafiki, tuelekee kulee!” alisema Honda huku akimpa ishara ya macho kuelekea upande wa pili kulikokuwa na uchochoro ambao uliufuata ungekufikisha kwenye kituo cha kujazia mafuta cha Total.


Wakaongozana kama mtu na rafiki yake.

Kojo mbele; Honda nyuma.


“Nani anawatuma?” aliuliza Honda.


Kimya!!


Honda akaona muda si rafiki,akaikoki bastola yake na tayari walikuwa wameingia ndani ya kichochoro hicho.


Lakini kabla Honda hajatimiza azima yake mara wakatokea vijana wawili waliokuwa wakikimbizana huku wakipiga kelele.


Kojo akajua lazima Honda atakuwa kazubaa nyuma yake nae hakutaka kufanya kosa.


Akaruka sarakasi moja kavu kwa kwenda mbele huku nyuma akisikia mlio mdogo wa chafya,akajua kakoswa na risasi.

Nae akataka amuoneshe Honda ni mjuzi wa hizo kazi.

Akageuka haraka kama tiara na kuipangusa bastola mikononi mwa Honda kisha akamshindilia konde usawa wa juu kidogo mwa jicho la kushoto.


Honda akarudi nyuma hatua kadhaa huku akiyumba.

Punde akamuona Kojo anamfuata kama Ngiri katikati ya mbio na Simba.

Akacheza kidogo na kumkwepa kisha akaunasa mkono uliokuwa unakuja kumshambulia, akaruka kurudi nao nyuma kisha akaachia makonde mawili ya harakara usoni kwa Kojo huku bado akiwa ameushika mkono wa Kojo, kisha akarudi nao kwa kasi huku akiwa amepinda mkono wake wa kuume na kiwiko kikakajaa tena usoni kwa Kojo na kumuacha akiyumba huku na huko bila kupata muhimili sawia.


Honda hakutaka kuchelewa,akaruka kwa mtindo wa flying kick na kumtandika Kojo mateke mawili ya kifua na kumwacha akisambaratika chini kama gunia la Karanga.


Honda alisimama wima huku akirekebisha mkoba wake na hapo masikio yake yaliponasa sauti mbili tofauti .

Sauti ya kwanza ni ya mwanamke aliekuwa anapita kichochoro kile na sauti ya pili ilikuwa ni ya king’ora cha polisi.


Akabaki njia panda.


Ni hilo ndo lilikuwa kosa lake.


Akashangaa akipigwa mtama safi kabisa uliompeleka chini bila kupenda na alipotaka kunyanyuka hakuamini macho yake.


Alishuhudia Kojo akiumwaga kwa mbio za sungura jangwani.


Hakumfuata!!


Akatokomea kuwahi sehemu nyingine aliohisi itampa majibu.





Alishuhudia Kojo akiumwaga kwa mbio za sungura jangwani.


Hakumfuata!!


Akatokomea kuwahi sehemu nyingine aliohisi itampa majibu.


****


Akili yake ilimwambia bado nyumba ya marehemu Bulembo ina majibu ya sakata lote lile. Na sasa alihitaji tena kurudi kule kule nyumbani kwa Bulembo, japo alihisi kunaeza kuwa na ulinzi; ila akaona huko ndo ilipo njia ya kumtegulia kitendawili cha kazi ile ilioanza kuwa hatari kwake.


Honda aliendelea kuambaa na kingo za barabara ya Rte Matida, huku kila mara akitazama nyuma na kujihakikishia usalama zaidi.


Licha ya kuwa alikuwa amenunua chakula cha kopo, lakini bado alihitaji kupata chakula cha moto na hapo macho yake yalishauona mgahawa wa Tundu uliokuwa mkabala na kanisa katoliki lilokuwa na maandishi ya PAROISSE SAINT IGNACE.

Hakuyatilia manaani sana maandishi yale, akaangaza kushoto na kulia kisha akaingia ndani ya mgahawa akatafuta sehemu tulivu ambayo hakukuwa na watu akakaa na kungoja mhudumu.


Haikuchukua muda mrefu,akasikilizwa hitaji lake kisha akakaa na kungojea kiletwe alichaogiza.


Zilipita zaidi ya dakika tano bila kuona dalili ya mhudumu kuleta chakula.

Ilikuwa ni akili yake ilioanza kuleta hisia mbaya juu ya jambo asilolijua, na hakutaka kupuuzia hisia zake.


Kutoka pale alipokuwa, kulikuwa na tofauti ya meza sita hadi kufika sehemu ya mapokezi na ulipaji fedha. Hivyo basi ni kila lililokuwa linafanyika sehemu ile, wateja waliona, isipokuwa kule jikoni ndo haikuwezekana kuonwa na mteja.


Akainua macho na kutazama tena kule mapokezi na kweli hakuona harakati zozote za kutia shaka, ila mhudumu aliechukua oda yu wapi? Hilo ndilo alilojiuliza.

Akataka kuendelea na subira ila akahisi kuona jambo pale mapokezi!


Alah!! Njaa ingemponza.


Mapokezi kulikuwa kuna katwa simu na kuwekwa juu ya meza.

Hilo aliliona mwishoni kabisa wa utendekeji wake.

Yaezekana kukatwa simu isingekuwa jambo baya kwake ila jicho la mhudumu pale mapokezi lilieleza mengi kuihusu simu iliokatwa.


Honda akasimama bila kuonesha ishara ya kama anataka kuondoka ama kuita mhudumu mwingine.


Maajabu tena!


Ajabu mhudumu akatokea haraka baada ya kuona Honda amesimama, tena akiwa na sahani ya chakula alichoagizwa.


Honda akatabasamu kisha akaketi.


“Jifanye hujui adui ajifariji” aliwaza Honda kisha bila kuitisha maji ya kunawa akaanza kufakamia chakula.


Chini ya dakika mbili na nusu tayari wali na finyango mbili havikuwa juu ya sahani.


Jirani waliokuwa wanakula wakabaki wamezubaa.

Yaezekana hawakuwahi kuona ulaji wa kasi namna ile au la basi waliona Honda amekosa ustarabu wa kiutu uzima.


Binadamu unakulaje haraka hivyo!!


Hakujali macho ya watu ila alimakinika zaidi na macho ya mhudumu wa mapokezi.

Mhudumu alikuwa haamini anachokiona kwa kuwa aliamini Honda atatumia zaidi ya dakika kumi au kumi nato ila sasa anaona imetumika dakika mbili tu na sekunde kadhaa


Alipagawa hakika.


Honda alipiga hatua kikakamavu na kufika alipokuwa mhudumu yule, akaingiza pesa mfukoni na kulipa.

Ni wakati mhudumu akiinamana kutoa chenji ndipo Honda akathibitisha mashaka yake na wahudumu wa mapokezi.


Mezani aliona kipande kidogo cha gazeti kikiwa na picha yake huku maelezo katika kipande kile yalikuwa yameondolewa kwa kuchongwa ili isalie picha yenyewe.

Honda akajiwazia.


Lakini kabla hajaendelea na tafakuri; akakumbuka tena kuitazama picha ile.


Picha ile ilikuwa imepigwa wakati akiingia ofisini mwa balozi Ally Sapi na alipoitizama vizuri aliona imepigwa baina ya milango miwili ilioko karibu na mlango wa balozi Ally Sapi.


Nani kapiga na kwanini alipiga!


Hakupata jibu


Na hapo akaamua kuikodolea tena ili abashiri kona iliotumika kumpiga picha ile.


Kushoto kulikokuwa na ofisi ya mkurugenzi wa usalama Papi Mndewa; kona ilakataa na hapo akapata jibu ya kuwa picha ilipigwa kutoka mlango wa chumba cha mawasiliano pale ubalozini ambapo mlango wa kuingilia ulikuwa kulia mwa Ofisi ya Balozi Sapi.


Honda akaondoka ndani ya mgahawa ule kwa kasi ya kimbunga, wala hakwenda mbali alivuka barabara na kuelekea kwenye nyumba za kanisa huku akiwa na mawili kichwani.


La kwanza bado alikuwa anatafakari uhusika wa mtu wa ubalozi katika sakata lile, lakini pia alikumbuka namna alivyoambiwa mawasiliano yalikatwa wakati balozi akiuawa.


Hata!!


Lazima msaliti yuko pale pale na ndie anakwamisha harakati zake na za marehemu Bulembo katika sakata tata linalomhusisha mtu tata.


Lakini mbali na hivyo alikuwa na mtego wake kwa yule mhudumu mana kama mhudumu akisimama kutoa chenji asimkute, basi lazima atatoka nje kumtafuta na ndio mana alikuwa anaelekea kwenye nyumba za kanisa ili atizame vizuri harakati za kuingia na kutoka ndani ya mgahawa ule wa Tunde.


Haikuwa dakika nyingi alichokitarajia alikiona!!



Lakini mbali na hivyo alikuwa na mtego wake kwa yule mhudumu mana kama mhudumu akisimama kutoa chenji asimkute, basi lazima atatoka nje kumtafuta na ndio mana alikuwa anaelekea kwenye nyumba za kanisa ili atizame vizuri harakati za kuingia na kutoka ndani ya mgahawa ule wa Tunde.


Haikuwa dakika nyingi alichokitarajia alikiona!!


****


Mhudumu alipigwa na butwaa bada ya kuinuka na kumkosa mteja wake.


Akapagawa!!.


Alipagawa kwa sababu hakudhani, sekunde chache vile mtu ampotee kirahisi tu.

Akajaribu kungojea dakika moja au zaidi, lakini tofauti na matarajio yake hakumuona Honda.


Akaamua kutoka nje lau aone uelekeo aliopitia ili tarifa yake ikamilike kwa wakubwa wake.


Mhudumu yule alitoka hadi nje, akaangaza kushoto na kulia hakuona mtu wala kivuli chake.


Shiiit!!” mhudumu akamaka huku mikono ikiwa imeshika kiuno asijue afuate lipi.


Akiwa hajui lipi afanye mara gari ikasimama karibu na miguu yake na hakujiuliza mara mbili akasogea kwenye kioo cha upande wa dereva,akasikiliza kidogo kisha akarudi akandoka kurudi mgahawani.


Kutokea pale alipokuwa ametulia; Honda aliyaona yote yaliofanywa na mhudumu yule nje ya mlango wa mgahawa wa Tunde.


Hata wakati gari inakuja na kusimama na kisha kuzungumza na walioko ndani ya gari, yote Honda aliyaona na sasa alitaka kuona watu wale waliokuwa ndani ya gari wangelifanya nini, lakini pia hakujua wapo wangapi japo aliamini ni zaidi ya mtu mmoja.


Aliendelea kusubiri hadi aone hatima ya watu wale.


Baada ya dakika kadhaa milango ya nyuma ya ile gari ikafunguliwa na kutoka kila upande wakashuka wanaume wawili waliojazia kimazoezi hasa. Wanaume wale wakaangaza huku na huko kisha wakaingia ndani ya mgahawa ule wa Tunde.


Katika hesabu za Honda aliamini ndani ya gari kutakuwa bado na watu wawili,mmoja dereva na mwingine yupo upande wa pili wa dereva.


Kwa kasi aliambaa na kuta za nyumba kadhaa kisha bila kuonesha tashwititi yoyote akavuka barabara huku hesabu zake zikiwa ni namna ataweza kuifikia ile gari bila kutiliwa shaka.


Alipovuka barabara tu akainamisha uso chini kisha akaanza kutembea kama mlemavu mwenye mguu mmoja mfupi na mwingine mfupi huku mkoba ukiwa unaning’inia mgongoni.


Hila za Honda zikazaa matunda, hadi analifikia lile gari hakuna aliekuwa amemtilia shaka na kwa kasi ya hewa akafungua mlango wa nyuma na bila kujiuliza akakaa kwenye kiti huku akiwa amewaelekezea bastola wale watu wawili waliokuwa wamekaa viti vya mbele wakiwa na mzubao usio semekana huku dhahiri hofu ikiwa juu yao.


“ondoeni gari hapa!” alisema Honda huku akiwa makini ili asifanyiwe fitina.


Hakuna aliemjibu wala kutekeleza amri yake nae akajua jamaa wanapoteza muda ili wale mabaunsa watokee na wakitokea hatari ipo kwake tu.

Hilo kamwe hakutaka litokee.


Bastola yake iliokuwa na kiwambo cha kuzuia sauti ikatema jiwe la moto na kupenya katikati ya uti wa mgogo wa mtu aliekuwa upande wa kushoto wa dereva na wala mtu yule hakuomba hata maji akawa hana mawasiliano huku damu ikimwagika kama bomba bovu.


Dereva hakuwa na namna, akaiondoa gari bila kujua ni wapi anapaswa kuelekea.


“endesha hadi nitakapokupa maelekezo mengine.” Sauti kavu ya Honda ikaunguruma bila chembe ya mzaha.


****

Safari ya Honda ilikuwa imegubikwa na ukimya wa kutisha na baada ya kitambo kidogo Honda akamwelekeza pahali alipopswa kugesha gari.


Mateka aliegesha gari kando kidogo ya nyumba ya marehemu Bulembo na

Baada Yakuhakikisha mateka wake amezima gari, kwa kasi ya radi akampiga kwa kitako cha bastola chini kidogo ya kisogo na mateka wake akapoteza fahamu hivyo ndani ya gari akawa na watu wawili, mmoja hana fahamu na mwingine bila uhai.


Haraka akashuka na kulekea lango la kuingilia ndani ya nyumba ya Bulembo na alitegemea kukuta utepe wa polisi wa kuzuia aisehusika kuingia pale na ndivyo ilikuwa.


Licha ya kuwapo utepe, pia kuliwa kimya sana kuashiria hakuna askari anaelinda pale na kuhakikisha zaidi akaingia hadi ndani ya utepe na kujaribu kuita ila hakuitikiwa zaidi alisikia sauti yake tu ikitengeneza mwangwi kwenye eneo pweke.


Haraka akarudi kwenye gari na kumchukua mateka wake ambae bado alikuwa amepoteza fahamu, akaingia nae moja kwa moja ndani na huko akamfunga vizuri kwenye kiti kisha akarudi ndani ya gari na kuliondoa kurudi walikotokea ambapo kwa kitambo fulani akaingia njia za vichochoro kulitelekeza gari ile na maiti yake. Huku akichukua baadhi ya vitu alivyodhani vinaweza kumsaidia.


Alikodi usafiri binafsi na kurudishwa hadi karibu na nyumba ya Bulembo, akalipa pesa kisha akaelekea kwenye kichochoro fulani lengo likiwa ni kumchanganya dereva endapo akibanwa huko ili atoe taarifa zake.


Huko huko alikopitia akajikuta yupo ndani ya mitaa yenye nyumba anayoihitaji.


Alipokwisha kuingia ndani, moja kwa moja akaanza upekuzi wake huku akiwa amemweka mateka wake kama kiporo.


Licha ya kukuta ukaguzi wa hali ya juu lakini bado aliamini kuna kitu kitakuwa mle ndani chenye kuweza kumsaidia hasa katika mambo matatu makubwa.


La kwanza ni kujua mhusika wa mauaji ya Bulembo na balozi Aly Sapi, lakini kubwa zaidi ni kuhusu tetesi za kuwapo mtu ambae historia hailezi wazi kuhusu kifo chake, na sasa tarifa za mwanzo za marehemu Bulembo zinasema yupo hai na anampango wake mahususi juu ya nchi ya Tanzania.


Mpango gani;?


Ndilo lilihatajika kufumbuliwa na mpelelezi Honda.


Honda alikuwa ametumia zaidi ya dakika kumi na tano bila kupata hata dalili ya maelezo yenye kumsaidia.

Alijishika kiuno huku akitembeza macho kila kona ya chumba kilichotumiwa na Bulembo kulala huku kichwani akifikiria kuacha kufuatilia njia aliotumia Bulembo mana inazidi kumwacha njia panda na muda unazidi kwenda.

Alitamani sasa kuingia kivingine na kwa njia zake ili apate ukweli wa sakata lile.


Wakati akili ikitafakari maamuzi; macho yakanasa kitu ukutani juu kidogo ya mto na mto huo ulionekana ndio ulikuwa unatumiwa na marehemu Bulembo kwa kuwa ulikuwa unaonekana kuwa na mafuta ya nywele yaliotengeneza weusi kidogo kwa kulaliwa mara kwa mara.

Juu kidogo ya tendegu la kitanda aliona mikwaruzo, akasogea kwa hatua za aste aste na alipofikia karibu aliona maandishi ila yalikuwa ni maandishi yale yale alioyaona kwenye kikaratasi alichokitafuna wakati akiwa mikononi mwa Sajini Kebu.


Na yalikuwa yamepangiliwa vile vile kama yalivyokuwa kwenye karatasi alioitafuna.


“142BOULEVARD DU JUIN

B. P. 1612

KINSHASA CONGO (81)”


Aliyatazama tena maandishi yale, bado hakuwa amepata walau wazo la kujua Bulembo alitaka kumaanisha nini japo alijua hii ilikuwa ni anuani ya ubalozi wa Tanzania Lakini kilichomchangaya zaidi ni ile alama ya mabano kisha zikafuatia namba (81) ilimaanisha nini hii namba! Hakujua wala kufikiria mbali zaidi ya kuzidi kuchanganyikiwa na asijue afuate lipi katika anuani ile


***

Angalizo ; Mnaosoma na kupita kimya kimya hamtendi haki kabisa, kama haivutii sema, umependa sema pia huo ndio ujira wangu wala sihitaj pesa yako ili niendelee kuweka hapa mtaji Pekee ni koment yako ambapo itasaidia watu wengi kuisoma



Wakati akili ikitafakari maamuzi; macho yakanasa kitu ukutani juu kidogo ya mto na mto huo ulionekana ndio ulikuwa unatumiwa na marehemu Bulembo kwa kuwa ulikuwa unaonekana kuwa na mafuta ya nywele yaliotengeneza weusi kidogo kwa kulaliwa mara kwa mara.

Juu kidogo ya tendegu la kitanda aliona mikwaruzo, akasogea kwa hatua za aste aste na alipofikia karibu aliona maandishi ila yalikuwa ni maandishi yale yale alioyaona kwenye kikaratasi alichokitafuna wakati akiwa mikononi mwa Sajini Kebu.


Na yalikuwa yamepangiliwa vile vile kama yalivyokuwa kwenye karatasi alioitafuna.


“142BOULEVARD DU JUIN

B. P. 1612

KINSHASA CONGO (81)”


Aliyatazama tena maandishi yale, bado hakuwa amepata walau wazo la kujua Bulembo alitaka kumaanisha nini japo alijua hii ilikuwa ni anuani ya ubalozi wa Tanzania Lakini kilichomchangaya zaidi ni ile alama ya mabano kisha zikafuatia namba (81) ilimaanisha nini hii namba! Hakujua wala kufikiria mbali zaidi ya kuzidi kuchanganyikiwa na asijue afuate lipi katika anuani ile.


Honda alitoka pale kitandani, kisha akataka kutoka nje ya chumba kile lakini akasita.


Kuna sehemu alikuwa hajafikia mle ndani.


Godoro!!!


Hakuwa ameligusa kabisa lile godoro juu ya kitanda, akarudi na kulitoa shuka yake.

Macho yake yakaambulia patupu, akaamua kulitoa lote.


Aliona!


Macho yake yalikutana na karatasi nyeupe ikiwa imepachikwa kwenye kingo ya chaga,wala haikuonekana kuwekwa siku nyingi mana ilikuwa bado inamwonekano wa kuridhisha machoni.


“Ina maana alijua atakufa?” Alijiuliza Honda kisha akakichukua kikaratasi kile ambacho kilikuwa kimekatwa upande hivyo kupunguza ukubwa wake.


Akakifunua!


Kilikuwa kimeandikwa kwa mafumbo au kwa lugha ya kijasusi ‘code' lakini fumbo lilikuwa katika lugha rahisi ila ngumu kutafsirika.


Iliandikwa katika muundo wa mduara ila katika kila neno kulikuwa kuna mduara mwingine mdogo kumaanisha kila neno lilikuwa linajitegemea ila katika muunganiko mmoja.


Honda alirudia maneno yale.


“MTANZANIA X” kisha yakazungushiwa duara na ukafuata msitari ambapo ulikutana na mduara uliokuwa na neno lingine lililosomeka


“MAKANISA MATATU”


Kisha ukafuatia msitari mwingine ambapo nao ulienda kukutana na kiduara kilichokuwa na maneno


‘CLUB X'


Kisha ukafuatia mstari mwingine ulienda kuungana ni kiduara cha maneno ya kwanza.


Lakini kulikuwa na duara kubwa lililozunguka kiduara chenye muunganiko wa viduara vitatu na juu ya mduara ule kulikuwa na maneno makubwa yaliokuwa yameandikwa kwa kukolezwa.


“MPANGO WA CONGO”


Yote hayo aliyasoma kwa umakini wa hali ya juu huku akili yake ikijaribu kupambanua nini kilimanishwa kwenye mchoro ule.


hakika alipagawa!


Lakini alikumbuka pale ndani anamateka, haraka akatoka kule chumbani na kwenda chumba kingine alikokuwa amemfunga mateka wake.


Alipoingia akakuta mateka akiwa amesharejewa na fahamu.


Akamtazama kwanza!


Kisha akavuta kiti na kukaa mbele ya mateka wake.


“Mlifuata nini pale Tunde” aliuliza Honda.


“Tulikufuata wewe” alijibu mateka.


“Nani aliwatuma” Honda aliendelea kusaili.


“Mr X” alijibu mateka


Jibu la mateka lilimuinua kwenye kiti Honda,na hii ni kwa kuwa dakika chache tu katoka kuliona hilo jina X kwenye karatasi ilioachwa na Bulembo tena likiwa limesomeka mara mbili.


Mwanzo ilitanguliwa na Mtanzania kisha Club na sasa Mr.


Je X inatumika kote huko na X ndie mhusika mkuu? Sasa kama X ni mtu na ndie kiongozi, kwa nini awe mtanzania ikiwa mpango upo chini ya mtu aliewahi kusemekana kufa ila hakuwa mtanzania!?” alijiuliza Honda huku akimtizama mateka wake bila kusema lolote.


Pagumu!!!.


*****


.MWANZA TANZANIA.


Remi alibaki akiwa mgongoni mwa Mtega nyoka, mtu waliekutana ndani ya ofisi za Kasuku contractors.


Hakutaka kuamini kuwa mtu mgeni yule alieingilia ugonvi wake na mtekaji angeliweza kumdhibiti mtekaji ambae yeye alijua uwezo na ukatili wake kuliko mtu yoyote aliekuwa eneo lile.


Remi aliona ni kama mtetezi wake ameingilia jambo gumu asilojua uzito wake.


Akajisogeza nyuma zaidi huku akiomba watu wazidi kuongezeka eneo lile apate wepesi wa kuchomoka pale.


Mtekaji ni kama alikuwa anazihesabu karata za Remi kichwani pake.

Hivyo wakati Remi anapiga hatua moja nyuma, tayari mtekaji alikuwa anatarajia hilo na kwa kuwa mbele yake kulikuwa na mtu tata alietokea kutibua mpango wake, hakutaka akwamishwe nae na hatimae kumkosa Remi kwa mara nyingine.


Alimchukulia poa Mtega nyoka.


Kwa kasi ya aina yake, mtu yule mrefu na mwembamba akatisha kama anataka kushambulia,ila akagairi gafla na tayari hila zake zilikuwa zimezaa matunda kwa kumtikisa kidogo Mtega nyoka.


Mtu yule akampita kwa kasi ile ile Mtega nyoka; lengo likiwa ni kumfikia Remi kabla hajatokomea tena.


Ila hakufika mbali akajikuta akipaa na kudondokea tumbo na hii ni bada ya kupigwa mtama safi na Mtega nyoka.


Mtega nyoka hakutaka kumfuata pale chini akamngoja asimame.


Mtekaji akasimama kwa mbwembwe kisha akamgeukia Mtega nyoka kwa gadhabu na kwa kuokoa muda akaenda mzimamzima

Kwa kushambulia kwa mtindo wa haraka haraka, lakini mapigo yote; Honda aliyaona vyema na kuyapangua kisha akaachia konde safi lilitua kifuani mwa mtekaji na kumyumbisha kidogo lakini halikutoa madhara makubwa.


Watu walizidi kushangilia na wengine kupiga picha za video bila kujua kitu gani hasa kinaendelea zaidi ya kuona mapigano kama muvi za Jet Lee.


Makelele na simu za watu zilizidi kumchanganya mtekaji mana hakutaka kabisa hilo litokee ila kukua kwa techonolijia na eneo walipokuwa lilirahisisha asichokitaka kitokee.


Akanesa kidogo kisha akawa kama anapeleka teke la kulia na alipoona Mtega nyoka ameingia kwenye mtego wake akaachia konde zito lililotua sawia kwenye paji la uso la Mtega nyoka.


Mtega nyoka alijikuta akiona nyota nyota na alipojaribu kufumba macho alijikuta anaambulia kuona mashilingi mengi na alipofumbua macho akaona ni kama umati wa watu unaiba shilingi alizoona.


Akagwaya!


Mtekaji alitaka kutumia nafasi ile kummaliza Mtega nyoka, lakini kabla hajatimiza lengo lake mara ukasikika mlipuko wa risasi na kuzua taharuki kwa watu waliokua pale huku kila mmoja akijaribu kuokoa uhai wake.

Mtekaji alibabaika kidogo lakini punde akasikia mvumo wa pikipiki anayoijua haraka akapiga tambo kubwa huku akikwepa konde lililotupwa na Mtega nyoka na tambo la pili lilimfikisha juu ya pikipiki huku nyuma zikisikika tena risasi kadhaa.


Mtega nyoka alishuhudia pikipiki isio kuwa na namba za usajili ikitokomea kuelekea katikati ya mji.


Jicho la Mtega nyoka likabaki likiangaza alipo binti asie jua kusoma wala asimuone.


Akah!!


“yuko wapi tena?” alijiuliza huku akianza kupiga hatua huku macho yake yakiwa yanaangaza huku na huko miongoni mwa watu waliokuwa wanakimbia milio ya risasi.


“Tulia na nyoosha mikono juu!” ilisikika sauti ya kimamlaka ikamuamuru Mtega nyoka.


Mtega nyoka aligeuka taratibu huku aking’ata meno kwa gadhabu.


Alipotulia macho yake yakakutana na mitutu miwili ya bunduki kutoka kwa askari wawili ambao aliwatambua ni waliokuwa wanalinda benki ya NMB.


“Amani afande” alisema Mtega nyoka huku akiingiza mkono mfukoni na alipotoa alikuwa na kitambulisho rasimi cha kazi yake.


Kilichofuata ni saluti kutoka kwa askari wale. Mtega nyoka hakujali saluti zao aligeuka na kujichanganya kwenye umati wa watu ulioanza kujikusanya tena huku kwa mbali akisikia king’ora cha gari la polisi kilisikika kikija eneo lile hivyo akajua askari wale watakuwa waliomba usaidizi makao makuu kwa kudhani wao ni wezi wakiwa wanapanga kuiba benki.


Kilichofuata ni saluti kutoka kwa askari wale. Mtega nyoka hakujali saluti zao aligeuka na kujichanganya kwenye umati wa watu ulioanza kujikusanya tena huku kwa mbali akisikia king’ora cha gari la polisi kilisikika kikija eneo lile hivyo akajua askari wale watakuwa waliomba usaidizi makao makuu kwa kudhani wao ni wezi wakiwa wanapanga kuiba benki.


***

Dakika kumi badae Mtega nyoka alikuwa ndani ya nyumba ya kulala wageni ya D8,pembezoni kidogo mwa stendi ya mabasi ya Buzuruga.


Akilini mwake aliona mapicha ambayo hakujua yana mana gani.


Kwanza ni operesheni yake maalumu ya kuwatafuta wahandisi watatu waliohusika katika ujenzi wa jengo fulani, na kabla hajawafikia akakutana na maiti zao.


Nani alieua;? Hakumjua.


Pili ni wakati akijaribu kutafuta fununu za wahusika wa mauaji yale na kujua sababu za mauaji, mara anakutana na binti wa ajabu anaeandamwa na watu wa ajabu.


Lakini kilichomumiza zaidi ni kuwa wote wawili walijikuta ndani ya ofisi za Kasuku contractors huku wote wakimuulizia Malima.


“Kuna nini Kati ya Malima na yule dada?” alijiuliza huku akiwa anatizama uso wake kwenye kioo kikubwa kilichokuwa ndani ya chumba alichokuwamo.

Akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa nguvu, hapo ndipo alipohisi maumivu katikati ya paji la uso alipopigwa ngumi na mtekaji.


Akatabasamu!!.


Jamaa anangumi kavu” akajisemea huku akitoka kujitazama na kwenda kukaa kitandani.


Mara wazo likamjia.


Haraka akanyanyuka na kuvaa nguo na kisha akavaa raba safi nyeusi ilioendana na rangi ya fulana nyeusi aliokuwa amevaa, kisha akavaa kofia Kaki iloendana na suruali aliokuwa amevaa kisha akajitazama kwenye kioo.


Akajicheka mwenyewe!.


Hakuwa amevaa mpangilio sahihi wa rangi za mavazi yake.


“Nianzie wapi sasa!” alijiuliza mara bada ya kuongezeka wazo la pili tofauti na la awali..


Hatimae akanyakua simu yake na kutaka kupiga hatua ili atoke nje.


Simu ikaita.


Alipotizama mpigaji, sura yake ikajikunja kwa fadhaa huku akilini akijishauri namna ya kumjibu mpigaji.


Hatimae akapokea.


“Kimya sana mtegaji!’” iliunguruma sauti ya Mzee Kinyonga.


“Hali tete Mzee, ila nipo njia moja” alisema Mtega nyoka.


Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa.


“Hali imeshavuka Def Cond 0002” alisema Kinyonga.


Mtega nyoka akatumbua macho na asione alichokitumbulia.


Hii ilikuwa mpya kwake.


“ina maana ilishaanza Def Cond 0001 na sasa inavuka 0002?” aliuliza Mtega nyoka


“Lakini sio ile unayoijua wewe” alisema Mtega nyoka.


Hapo tena Mtega nyoka akakwama sauti kisha akamsikia Kinyonga akiendelea kuelezea…


“ Hii Def inaandaa Def cond 0008,na sio kama ni ya ndani; la hasha, hii ni ya kutokea nje ikihusisha watu wa ndani, hivyo basi kipimo changu kinasoma 0002 bado ni kimya kimya” alifafanua Mzee Kinyonga.


“ooh Sawa nimeelewa, kwa hiyo, kwa huo mkia umeonekana au kichwa ndo kimeonekana” aliuliza Mtega nyoka.


“aaah Mtega nyoka!!; kwani lini umeanza kuniuliza habari za kina nyoka mimi Kinyonga?” alilalama Mzee kinyonga.


Mtega nyoka, aliamua kukaa kimya mana alijua jukumu bado ni lake yeye kapewa tu fununu.


Na kikubwa aliwaza uzito wa kipimo alichodokezewa yani Def cond.

Def cond(defence control) ni kipimo cha migogoro ndani ya serikali huku kikianza na 1-8,sasa Mtega nyoka alikuwa ameambiwa hii Def cond sio anayoijua, hivyo basi katika uelewa wake alijua ya kuwa kuna mipango ya usaliti inafanyika kuiangusha serikali, mana def ilikadiriwa kuelekea def cond 0008 kumaanisha huko kunafukuta Vita kamili.

Lakini pia aliambiwa yakuwa kuna watu ndani na nje katika mipango hiyo na yeye ndo anapaswa kuwatafuta.


Akatabasamu hasa alipokumbuka vifo vya wahandisi, siku moja iliopita.


Fumbo!!


Hiyo ilimaanisha kuna fumbo lipo ndani ya kampuni ya Kasuku contractors lakini swali likabaki kwake.


Kwa nini Kasuku?


Na lilikuwa swali la msingi yeye kujiuliza kwa sababu Kasuku wanahusika na uchoraji na ujenzi wa majengo, lakini hata jengo lililojengwa nao lililomhusisha Mtega nyoka wao wajengaji hawakujua ni la nini lakini pia ramani ya jengo hawakuwa nayo yote.


Sasa ni vipi Kasuku wahusike na sakata gumu vile?


Mtego!!


Akajiwazia huku akipiga hatua kutoka ndani ya chumba alichokuwamo.


***


Safari yake ilimfikisha hadi soko dogo la machinjioni Mandu, kisha huko akaungana na wasafiri wengine kupanda daladala za kwenda kisasa kulikokuwa na mazishi ya mmoja wahandisi wa kampuni ya Kasuku.


Alichagua kwenda hapa, sababu wengine walisafirishwa mikoani kwao kwa ajili ya maziko.


Alifika mazishini na kushuhudia umati wa watu wengi sana ukiwa umejuimuika pamoja huku baadhi ya watu wakiwa wamejitenga huku na huko.


Msiba ulikuwa umepokea watu wa kila aina huku magari ya kifahari yakiwa yametapakaa kila sehemu hii ilimaanisha aliefariki alikuwa ni mtu wa watu lakini pia alikuwa ni mwenye kujiweza kifedha..


Roho ilimuuma mtega nyoka hasa aliposikia sauti za akina mama wakiomboleza.


“kwanini waluwawa watu hawa?” alijiuliza mtega nyoka bila kupata majibu.


“mtuhumiwa wa kwanza yupo kwetu au yupo ndani ya Kasuku” alizidi kuwaza mtega nyoka huku akipepesa macho huku na huko na hapo akaona vijana wa usalama kadhaa wakiwa katika majukumu yao ya kufuatilia kesi ile.


Akaachana nao na macho yake yakagota kwa kijana mmoja mtanashati akiwa amekaa na vijana wengine wawili wakijadili jambo huku mara kadhaa wakionekana kufurahia walichokuwa wanakijadili.


Lakini wakiwa katikati ya majadiliano mara akaja binti mmoja na kumuita yule kijana mtanashati alietizamwa na Mtega nyoka.


Yule kijana akaenda kumsikiliza yule binti, huku maongezi yao yakionekana kuwa ya utata upande mmoja kwani binti aliongea kwa kubabaika ama kuchanganywa na jambo huku kijana wa kiume akiwa makini kusikiliza.


Mtega nyoka akavuta hatua kujipitisha karibu yao, lakini kabla hajawafikia tayari walikuwa wamekwisha kuongozana kutoka eneo lile.


“una nini Malima!!” alijisemea Mtega nyoka huku akiangaza huku na huko ili aone kama kulikuwa kuna mtu mwingine aliekuwa anafuatilia nyendo za kijana yule.


Alimuona!




Mtega nyoka akavuta hatua kujipitisha karibu yao, lakini kabla hajawafikia tayari walikuwa wamekwisha kuongozana kutoka eneo lile.


“una nini Malima!!” alijisemea Mtega nyoka huku akiangaza huku na huko ili aone kama kulikuwa kuna mtu mwingine aliekuwa anafuatilia nyendo za kijana yule.


Alimuona!!


Macho ya Mtega nyoka, yalibahatika kuona muinuko wa kijana mwingine ambae kwa macho yake yaliozoea wahalifu, haraka akabaini yule hakuwa mwema kimtazamo.


Nae hakutaka kungoja akainuka na kufuata ulekeo alioona kijana mtanashati ambae alimtambua kama Malima akielekea na binti mwingine ambae hakumjua.


Macho ya Mtega nyoka yalikuwa sambamba kabisa na kijana mwingine aliekuwa akifuatilia hatua za Malima.

Kila kilichofanywa na kijana yule kilionwa vyema kabisa na Mtega nyoka.


Mazungumzo Kati Malima na binti, yalikuwa yanedumu kwa zaidi ya dakika nne kisha Malima akatoa ufunguo wa gari mfukoni mwake na kumuita kijana mwingine aliekuwa karibu na pale walipokuwa na alipofika akamkabidhi ufungo kisha akampa maelekezo kijana yule alieonekana kuwa ni dereva wa Malima.


Malima alipokwisha kutoa maelekezo, akaanza kurudi alikoacha wenzie wamekaa na dereva wake na yule binti wakapanda gari na kuondoka pale.


Yote yalitizamwa vyema na Mtega nyoka na pia hakuacha kutazama nyendo za kijana alieonekana kumfuata Malima.


Wakati Malima akiungana na wenzie na yule kijana akarudi kukaaa alipokuwa awali huku macho yake ya wizi yakiwa hayabanduki kwa Malima.


Muda si muda ukafika muda wa kuaga marehemu na ni muda huo ambao Mtega nyoka aliona unamfaa zaidi kumtumia yule kijana kuliko kumsubiri Malima.


Haraka akamsogelea na taratibu akamfikia yule kijana na kwa upole tu akamwambia;


“Tafadhali ndugu naomba msada wako”


“msada gani” aliuliza kijana kwa mashaka.


“aah ni pale kwenye gari yangu kuna kishida kidogo, yani dakika moja tu ndugu” alizidi kubembeleza na kusihi Mtega nyoka.


Kijana bila kujua hila alizowekewa akakubali huku akitoa tahadhari ya kuwa isizidi dakika moja.


Waliongozana kuelekea kwenye sehemu kulipokuwa kumepakiwa magari mengi zaidi, na Mtega nyoka ndie alitangulia ili kumpa kujiamini yule kijana.


Mtega nyoka alipohakikisha wamepotelea katikati ya magari akageuka gafla na bastola mkononi na kumstua kijana aliebaki ameganda kwa sekunde kadhaa bila kuamini anachokiona.


“Geuka bila ubishi la sivyo kunageuka msiba wa pili hapa” akaamuru Mtega nyoka na kijana akatii bila shuruti huku nae akipiga hesabu za kumvaa mtu yule asie mjua.


Kugeuka kwake likawa kosa!!

.

Kwa kasi ya aina yake, Mtega nyoka akaachia pigo kwa kutumia ubapa wa kiganja na kumpiga nyuma ya kisogo na kijana akaenda chini akiwa hana fahamu.

Mtega nyoka akatazama kushoto na kulia asione mtu aliemuona, haraka akaingiza mkono mfukoni na kutoka na waya mwembamba akaingiza kwenye kitasa cha mlango wa gari nao ukaachia bila kupenda haraka akajitosa ndani na alichofanya huko anajua yeye na punde gari likawaka na akashuka na kumuingiza yule kijana kisha akatokomea na gari la watu huku akiwa na mateka wake.


Akiwa njiani alituma ujumbe kwa Kinyonga ambao ulisomeka;


“Kitalu gani kina mwanya?”

Punde akapokea ujumbe kutoka kwa Mzee Kinyonga.


“Kitalu 1b G” akausoma na hapo alijua anapaswa kuelekea Gedeli kulikokuwa na nyumba ya usalama wa Taifa maalumu kwa kazi za dharura.


Aliamua kupitia mitaa ya Neshino kisha akaipata Gedeli na huko akanyoosha hadi alipokutana na kibao kilichoonesha mbele kuna nyumba inayotumika kufundishia watoto.


Akafika hadi kwenye nyumba hiyo kisha akapiga honi mbili na kusubiri.

Punde akatokea kijana aliekuwa na vitabu na chaki mkononi ikionesha ametoka kufundisha muda si mrefu.


Walitazamana kwa muda kisha Mtega nyoka akasema kwa lugha tata kueleweka.


“Nina guta hapa linahitaji kushushwa oili chafu tafadhali”


Kijana aliekuja akawa makini kidogo kisha akaangaza kushoto na kulia afu akasema;

“Sukutua tafadhali” akiwa na maana apewe utambulisho.


“Siku ya mwisho ndio kwanza” akasema kwa kujiamini Mtega nyoka.


Haraka kijana yule akampa ishara na ya yeye akatangulia kufuangua mlango ulikouwa umejengwa kienyeji tu ambapo ulitumika kuficha geti kubwa lillokuwa linaingia kwenye nyumba kubwa iliokuwa imepakana na lango la kuingilia kwenye darasa la watoto lililokuwa linafundishwa na yule kijana


Haraka haraka Mtega nyoka akaingiza gari na geti likafungwa kisha haraka haraka wakasaidiana kumtoa kijana ambae bado alikuwa hana fahamu na kumuingiza ndani.


Bada ya kuhakikisha Mtega nyoka amepata kila zana alioihitaji,kijana yule akaondoka na kurudi kuendelea na darasa la watoto ambao wakati huo walikuwa wameanza kupiga kelele.


Baada ya kupata kila alichokihitaji, Mtega nyoka akafungua kisanduku kidogo kilichokuwa na zana kadhaa za kutesea na dawa za hapa na pale kisha akachukua kichupa kidogo na kukizungusha juu kwenye mfuniko na kikatoka kitu kidogo mfano wa kidole cha mtoto na kilipotoka kiasi alichotaka akapiga hatua na kumfikia kijana ambae hadi wakati huo hakuwa amerejewa na fahamu.


Kile kichupa akakisogeza hadi karibu na pua za yule kijana na hazikupita sekunde kadhaa kijana akapiga chafya mfululizo kisha akatulia kujipa utulivu na alipotulia akakutana macho na Mtega nyoka ambae muda wote alikuwa kimya akimtizama.


“Hizi silaha ulikuwa nazo za nini?” lilikuwa swali la kwanza la mtega nyoka huku akimwonesha bastola na kisu kidogo cha kukunja.


Kijana akabaki kimya bila kujihangaisha kumjibu.


“Je unazimiliki kihalali au unazitumia kimagumashi?” akauliza tena Mtega nyoka.


Kijana akabaki kimya tu.


Hakujua akili ya mtu alie mbele yake ni ya aina gani.


Haikumchukua muda akatambua mtu aliembele yake ana akili gani.


Kwa kutumia kisu kile kidogo alichokichukua kwa yule kijana wakati alipomkagua akakishindilia kwa nguvu kwenye upaja wa mguu wa kushoto wa kijana yule na kufanya apige kelele ya maumivu huku akifurukuta kwenye kiti alichokuwa amefungwa bila mafanikio.


Na haikuishia hapo akamchana suruali na kufanya kijana abaki na pensi tu huku damu zikizidi kutiririka kama bomba la mvua.


Mtega nyoka alikisogeza kisanduku na kutoa kichupa kingine kilichokuwa na dawa ya unga na akaimiminia kwenye jeraha.


Dawa ile ilipokutana na damu ikaibadilisha kuifanya iwe kama ya njano na kutoa povu na ilipoingia kwenye jereha sawa sawa ikawa kama inachemka na kitendo hicho kilipelekea maumivu makali kwa yule kijana alijikunja huku akipiga ukunga kama mwanamke bikira akibikiriwa na mkuyenge inchi kumi na mbili.


“Haya sasa nambie unamiliki vipi hizi silaha” aliuliza tena Mtega nyoka.


“Mi sijui bana” alijibu kwa maumivu makali yule kijana.


“kwani sio zako?” alisaili tena Mtega nyoka.


“Nimepewa tu!” alijibu


“na nani”


Akaendelea kukugumia bila kujibu.


“Nani kakutuma na kwa kazi gani?” aliendelea kuuliza na hakupata majibu.


Kama kawaida yake, yeye huwa si muongeaji sana zaidi hufanya vitendo tu.


Akachukua praizi na kukishika kidole cha mwisho mguuni mwa yule kijana kisha akakibana na kukipasua katikati.


Mamumivu aliyayapata kijana yule hayaelezeki, alilia kwa uchungu bila kupata wa kumsaidia na bado aliziona harakati za Mtega nyoka aliekuwa anajiandaa kumwekea dawa ile ya unga ikabidi aombe kusamehewa.


“haya bwana mdogo sema na usijaribu kunidanganya kabisa huwa siongei wala kubembeleza” Alitahadharisha Mtega nyoka.


“Nilipewa na Amokachi!” akajibu kijana.


“Amokachi” akarudia kulitaja lile jina.


“kakutuma uifanyie nini”aliuliza tena Mtega nyoka..


“kujilinda wakati nikimfuatilia Malima”


“Alikwambia kwanini umfuatilie?”


“Hapana hajawahi nambia”


“Umefanya nae kazi muda gani?”


“Hii ni mara ya pili”


“Mara mbili;hivyo inaamana mmejuana muda si mrefu”


“ndio”


“Nani kawakutanisha?”


“Sukuna ndie alietukutanisha”


“kwa hiyo wewe upo chini ya Sukuna na unaripoti kwa Amokachi”


“ndio”


“Kati ya hao ni nani rahisi kumpata?”


“Wote sio rahisi”


“kwanini?”


“kwa sababu wanaishi kama Muhanga”


Mtega nyoka akaguna kisha akamtazama yule kijana aliekuwa amekaa kwenye kiti kwa kujipinda kwa sababu ya maumivu pajani na kidoleni.


“unazijua tabia za Muhanga kweli?”

Aliuliza kwa kustajabu kidogo.


“Muhanga ni mnyama asieogopa chochote katika maisha yake,huishi kwa kuvizia makazi ya wengine kisha hujitosa jumla jumla, Muhanga haogopi kabisa hatari yoyote,lakini sifa yake kuu ni kutokuonekana hovyo na anaweza kuishi Mwanza huku akiwa na choo Bariadi sasa ni juhudi zako kumtafuta” alifafanua kijana.


Mtega nyoka alimtizama tena bwana mdogo kisha akatikisa kichwa.


“Kwa hiyo maeneo yenu ya kukutana ni wapi?”


“tunapokea simu tu bro lakini mara chache sana huwa tunafika Club D!”


“iko wapi?”


“Hata mimi sijui kwa sababu huwa tunafika tukiwa tumezibwa macho na masikio, tunapokea oda kisha tunarudishwa hivyo hivyo”


Alipigwa na butwaa Mtega nyoka kisha akazunguka kidogo ndani ya chumba walichokuwamo na alipotulia aliuliza;


“kwa hiyo huwa mnatumwa kazi gani”


“Tumegawanywa na kila mtu na kazi yake na haturuhusiwi kuingiliana kikazi, mimi ni Tracer,lakini kuna Transporter, kuna Helper na kuna killer”


“kwanini mnafanya yote haya?”


“Huwa haturuhusiwi kuuliza, sisi tunafanya tu na pesa inaingia”


Mtega nyoka alimtizama kijana yule mdogo kisha akashawishika kuuliza jambo.


“kwanini wewe umenambia haya mana nikikutazama naona ulikuwa tayari kabisa kufa ila si kusema haya wala sitaki kuamini ni kwa sababu ya mateso yangu”


Kijana akatabasamu kisha akaongea kwa upole.


“kwa sababu nataka kutoka kufanya kazi hii, siipendi ila Sina namna imenilazimu”


Mtega nyoka akamtazama tena kijana yule na hapo akaona jambo lingine tena ambalo mwanzo hakulitilia maanani.


“wewe ni Mtanzania?”


“Hapana mi nilikuwa Mkimbizi tu vita ya Burundi, baba na mama walifia njiani wakati tukija Tanzania na mimi na mdogo wangu tulichukuliwa na kutenganishwa ambapo yeye alipelekwa kituo cha wakimbizi Kigoma na mimi ndo nikaishia kuwa mfanyakazi wa ndani wa Sukuna na badae nikafunzwa utracer yani mimi kazi yangu ni kufuatilia nyendo za mtu anaeshugulikiwa na kikundi cha sukuna na nikishapata habari na nyendo za kutosha basi kazi inaweza kuishia kwa killer au ikiwa na mlolongo basi Transporter na Helper huhusishwa.”


Alisema kijana yule ambae alijitambulisha kwa jina la Zanu.


Zanu akaona mduao alionao Mtega nyoka na akaamua kuomba jambo.


“Kaka bila shaka wewe ni usalama wa Taifa,na najua kanuni zenu huwa ni kutokujulikana na kwa njia yoyote na first rule ni kuto attract attention lakini pia key rule ni kutokutoa taarifa ama kuvujisha taarifa zenu, hivyo kaka mimi nimefunzwa kama nyie hizo sheria zote ila nimevunja na kukwambia hayo hivyo sitaki wala sifikirii itokee ule msemo wa wanausalama kwamba “trust will get you killed” hivyo sitegemei kuuwawa na mkono wako ila naomba unisaidie nisirudi tena mikononi mwa Amokachi na Sukuna niweke hata gerezani ila si kunifanya nikarudi mikononi

Mwao.”


Mtega nyoka akamtazama Zanu na moyoni mwake akajiridhisha na maelezo ya Zanu japo nae moyoni alijiwekea tahadhari ya trust will get you killed.


“sawa utaendelea kuwa hapa hadi nitakapokupa maelekezo mengine ila utaendelea kuwa mateka japo hautafungwa” alisema Mtega nyoka huku akianza kutoka ndani ya chumba cha mateso ndani ya nyumba ile ya usalama wa Taifa.


Alifika hadi sebuleni na kumkuta kijana wa usalama aliempokea.


“utamhudumia yule dogo na umtoe kule na mpeleke room C ila kuwa makini nae si wa kuchekea kwa sasa and remember one thing trust will get you killed” alimalizia maneno yake kisha akaanza kutoka nje ila kabla hajaufikia mlango wa kutokea kijana yule akamwambia;


“Nipo makini pia komredi na akizingua nitamkumbusna kitu hiki “time spent in enemy hands is the same as becoming the enemy himself”


Huo msemo maarufu katika tasnia ya kishushu ulimfanya Mtega nyoka atabasamu huku akkmalizia kuufunga mlango huku lengo likiwa ni kuipeleka gari alioipora msibani kituo cha polisi ili irudi kwa mwenyew kisha aanze rasimi msako wa kumtafuta Sukuna kisha Amokachi na sehemu pekee ya kuwapatia watu hao ni Club D.


Tatizo sasa hajui ilipo.


****


NB: Ni mchawi pekee ndie anaeweza kusoma na kuacha kulike ama kutoa komenti ama kushea na wengine wapate kusoma kazi hii. Basi leo soma kisha like, komenti ili usijifananishe na mchawi mwenye roho mbaya.


Alipofika nje hakutaka kutoka bila walau kupata maelezo kuhusu OCCID na alipokwisha kuyapata maelezo kuhusu makazi ya mtu huyo akaitisha usafiri wa bodaboda kuelekea kuitafuta Club D.


Tatizo hajui ilipo.


********


Remi baada ya kuona mnyukano wa wanaume wawili katikati ya milango ya Buzuruga Plaza; hakuwa na budi kufanya maamuzi alioona ni sahihi kwake.


Mwanzo alitamani kubaki ili aone hatima ya kijana waliekutana ndani ya ofisi za Kasuku Contractors na pia kugeuka kuwa msaada wake wakati akiwa amekabwa na mtekaji.


Wazo hilo alilipinga haraka hasa baada ya kushindwa kuwa na imani na kijana anaemtetea.


“kama ni mbinu yao ya kunitia mikononi!” alijiwazia na kisha haraka akawatazama akaona bado wamewekeana mchoro wa mapambano na pembeni aliona umati wa watu ukizidi kujongea huku kila mmoja akijaribu kuwa wa kwanza kuwa shuhuda wa mtanange ule wa kibabe.


Kisha akarudi tena kuwatazama mafahali wale na hapo akakutanisha macho yake na mtekaji na akaona jinsi macho ya mtekaji yalivyomakini nae.


Akangoja nafasi itokee.


Mungu alijibu maombi yake.


Ni wakati mtekaji alipojaribu kumnasa kwa kumpita hasimu wake na kuangushwa kwa mtama safi aliopigwa na hasimu wake.


Wakati mtekaji anamgeukia hasimu wake,ni wakati huo alipoona nafasi ya yeye kutokomea.


Akapenya katikati ya watu na kisha akakimbia kama mwizi aliekoswa na jiwe.


Mbio zake zilimfikisha njia panda ya mataa Buzuruga. Hapo akatulia huku akitizama huku na huko na alipohakikisha Hakuna anaemfuatilia; akaamua kuvuka na kuingia ndani ya kituo cha mabasi Buzuruga.


Alipokwisha kuingia tu tayari wahudumu na wapiga debe wa mabasi yaendayo Musoma na maeneo mengine walianza kumzonga huku wakinadi ubora wa mwendo na huduma za mabasi yao.


Hakuwajali!.


Akazidi kuwakwepa huku akionekana kupagawa kwa kuvutwa vutwa na baadhi ya wapiga debe wasio na staha.


Walipoona sio msafiri wakaamua kumuacha ajiendee zake.


Alipokwwisha kuachwa na wasumbufu hao ambao baadhi waliishia kumtusi,nae hakuwajali akaendelea na hamsini zake.


Miguu yake ilikoma akiwa katikati ya soko la Buzuruga.


Tumbo lilikosa ushirikiano lakini pia alihitaji kutuliza akili na kuamua jambo la kufanya wakati huo.


Alijongea katika mgahawa mmoja uliokuwa sokoni humo kisha kwa pesa kidogo aliokuwa nayo akaagiza chai ya moto na wali mweupe.


Alikula taratibu huku mawazo lukuki yakikizonga kichwa chake.


Licha ya akili yake kuuona ugumu wa kumpata Mwasu kwa siku hiyo,ila bado aliona mtu sahihi zaidi wa kumfikia ni Mwasu ili walau apate ushauri kutoka kwake na namna ataweza kuepuka masaibu yanayomzonga.


Lakini jambo moja lilimchanganya; ni vipi watu wale wamefika haraka Mwanza na pia wamewezaje kufuatilia nyendo zake kirahisi vile!?


Alijipa utulivu wa akili.


Jibu halikukawia japo hakujua kama ndilo litakuwa sahihi ama la.


Alidhani ya kwamba, watu wale wabaya walijua akifika Mwanza; Mtu wa kwanza kumtafuta atakuwa ni Mwasu na ndio mana alikuta wamemtangulia.


Alitoa kimkoba kidogo chenye ukubwa Sawa na pochi za akina dada ila hiki kilikuwa ni cha ngozi na pia kilikuwa na mikanda mirefu myembamba sana. Tofauti nyingine ni kuwa kimkoba hiki kingekuwa kinamilikiwa na wadada wa mjini basi ungekuta kimejaa vipodozi; kioo na taulo moja ya kike. Ila mkoba huu wenyewe ulikuwa na karatasi nne tu.


Karatasi hizi zilikuwa zinatokana na zao la miti hivyo hazikuwa nyeupe bali zilikuwa ni kaki.


Alitazama mazingira aliokuwapo na alipohakikisha hakuna anaejali anachokifanya,akazitoa zote.


Zilikuwa zimekunjwa kwa kuzungushwa kisha kwa juu zikabanwa na kamba nyembamba sana.


Alipokwisha kuziweka pembani karatasi zile akarudisha tena mkono kwenye mkoba ule na alipoutoa alikuwa na kadi ndogo ya kuhifadhi kumbukumbu.


Akakitazama kikadi kile kisha akayakumbuka maneno ya mtu aliempa vitu vile.


Kabla hajapewa alisisitiziwa sana kuhifadhi kadi ile kuliko karatasi, yani bora karatasi zipotee ila si kadi ile.


Lakini pia alikumbuka kuonywa ya kuwa kama anataka aendelee kuishi ni lazima awe na vitu vile huku akiambiwa kama atapokonywa basi ndipo uhai wake utakapoishia.


Akazishusha pumzi kwa mkupuo kisha akawaza kuifanyia kitu kadi ile ili awe na hakika nayo katika usalama wake na kadi ile.


Lakini wakati akikumbuka kurudia chakula mezani, wazo moja likapita kichwani mwake.


Polisi!!


Yesi aliwaza kwenda kuutua mzigo wa mateso ule kituo cha polisi. Japo aliamini anaweza kuzungushwa sana hadi kushugulikiwa,lakini aliamini ni lazima watalishugulikia kulingana na uzito wa suala lenyewe.


Akapitisha wazo la kwenda kituo cha polisi.


Alipogeukia chakula chake alikuta kimepoa na chai imegeuka kuwa maji ya baridi.


Akakimalizia kisha akalipa na kuinuka kisha akatafuta njia yenye watu wengi na kujichanganya akatoka nje ya kituo cha mabasi.

*****


Dakika ishirini badae alikuwa anatazamana na kituo cha polisi Nyakato Neshino.


Aliingia hadi mapokezi kisha akaomba kuonana na mkuu wa kituo kile.


Aliruhusiwa kumuona bila kuulizwa maswali mengi kama alivyotarajia.


“Unaitwa nani binti” aliuliza mkuu wa kituo.


“Remi” alijibu binti.


“Ndio Remi; unaishi wapi na utokea wapi” aliuliza tena mkuu wa kituo.


“Natokea Kigoma” alijibu binti.


Mkuu wa kituo akamtazama binti kwa makini sana kisha akatikisa kichwa kwa alichokiona kutoka kwa binti yule.


Mkuu wa kituo alihisi binti atakuwa na matatizo kiakili kwa sababu ya muonekano wake kuwa mchafu na anaonekana hajaoga siku kadhaa.


Hiyo huwa si kawaida ya wadada wenye urembo kama wa yule binti japo hakuwa akiuthamini urembo wake.


Mkuu wa kituo pia aliyajumlisha majibu ya binti yalivyo ya mkato kuzikamilisha hisia zake.


“Shida yako tafadhali” alisema mkuu wa kituo.


“nimepoteza wadogo zangu” alijibu binti.


“wamepoteje?”


“sijui walivyopotea ila wamepotea”


Mkuu wa kituo akaingiwa na gadhabu kwa sababu alijua kabisa binti yule hayuko sawa kiakili na pale anampotezea tu muda wake.


“Ok!!, unahisi ni nani aliefanya hivyo?” akauliza mkuu wa kituo huku akijaribu kuzizuia gadhabu zake.


“ninao ushahidi wa mwanzo huu hapa” alijibu binti huku akimpa Mkuu wa kituo karatasi nne ambazo zilionekana kabisa zimetolewa nakala kwa kirudufu muda si mrefu.


Mkuu wa kituo akazichukua karatasi zile na kuzifunua.


Akajikuta akicheka sana huku gadhabu zikimuisha na kuamini kweli binti alieyeko mbele yake ni mgonjwa wa akili.


“Dada nadhani unahitaji msaada wa haraka sana” alisema mkuu.


Remi akatabasamu kwa mara ya kwanza tangu aingie ndani ya jiji la Mwanza.


Lakini hakujua kauli ya Mkuu wa kituo haikumaanisha alivyodhani yeye.


Furaha na matarajio yake yakakoma gafla.


“sio msaada unaodhani wewe binti,msaada ninao kupa inabidi twende hospitalli ukapime akili yaezekana umekuja hapa ukiwa hujui”


E bana eeh!


Mshangao ukatamaradi usoni pa Remi huku akiona kabisa alivyodhaniwa na ukichaa tena mbele ya serikali.


Amah!!


“Afande kwanini…?” Alijikuta anakwama kuuliza.


“Remi huoni unaumwa wewe?,hivi unakujaje hapa ukiwa na karatasi zilizoandikwa kwa lugha ya kifaransa afu useme zinahusiana na upotevu wa wadogo zako?”


Jama!!


Akapagawa na hapo ndo akajua lugha iliotumika pale ni kifaransa mana tangu mwanzo alishindwa kusoma kilichopo kwa sababu hakuwa na uelewa wa lugha ile sasa hakujua ya kuwa hata hapo kituoni wapo wasiojua kifaransa kama yeye japo alishukuru walau tu kuambiwa ni kifaransa kimetumika kuziandika karatasi zile.


“anyway, nenda ofisi namba kumi ueleze shida yako vizuri kisha uwape hizi karatasi,sasa ikibainika unacheza ujinga utajuta kucheza na serikali” alisema kwa mkwara mkuu wa kituo huku akimpa Remi karatasi zake.


Remi alijua hajacheza vizuri karata yake ili aeleweke. Lakini nafsini mwake alijiambia yupo sahihi kuanza vile mana hajui ni nani yupo nyuma ya sakata lile na alijua kabisa hata serikalini wamo.


Remi hakutaka kufunguka lolote zaidi pale na ni baada ya kuhisi tangu mwanzo mazungumzo yake na mkuu yule yatakavyokuwa kwa sababu alionekana mjivuni sana bwana yule


Lakini pia hakutaka kuongea sana mana angejulikana si Mtanzania kwa lafudhi yake na hiyo ingemletea shida zaidi mana angekufa na ushahidi wake ndani ya gereza kwa kuwa mhamiaji haramu wala hakuna ambae angejua ni Mkimbizi alietoroka kwenye kambi ya wakimbizi huko Kigoma.


Ofisi namba kumi ndani ya jengo lile la kituo cha polisi ilikuwa inakaliwa na ofisa mkuu wa upelelezi katika kitengo cha makosa ya jinai na pia kilishugulika na ujasusi wa ndani.


OCCID alikuwa anatazamana na Remi na baada ya kumsikiliza maelezo yake ambayo yalikuwa sawa na aliyotoa kwa mkuu wa kituo,akazichukua karatasi zile kisha hakuzipitia akaziweka pembeni huku akimwahidi kulishugulikia swala lile kikamilifu.


Remi akaaga na kuondoka ndani ya ofisi zile na alipotoka nje alilakiwa na macho ya watu wawili tofauti.


Mmoja alikuwa ni Mtega nyoka na mwingine alikuwa ni askari wa usalama barabarani aliekuwa anaripoti kwa ajili ya kurudi nyumbani kupumzika.


Alimtizama kwa jicho lisilo la wema ila si yeyote aliejua isipokuwa ofisa yule wa usalama barabarani.


Tofauti na siku Zote ambazo ofisa yule huripoti kisha kuondoka,ila siku hiyo akabaki pale kituoni kwa dakika kadhaa, lengo ni kujua njia alizopita Remi na alifuata nini pale kituoni.


Hilo alifanikiwa mnoko yule.


*****


OCCID hakutaka kupuuzia lalamiko la Remi lakini pia hakutaka kuzipotezea karatasi zile hivyo haraka akamuita kijana mmoja kutoka kitengo cha upelelezi cha polisi (Intelligence Police) ambae anaijua lugha iliotumika pale ili ampe kazi hiyo ya kushugulikia kesi iliohusisha lugha ya kigeni.


Mwanzo hakujua kama lile ni suala kubwa sana na ndio mana alipomwita Intelligence Ofisa au maarufu ‘IO' hakuhitaji kutafsiriwa pale mana alijua itakuja kwenye ripoti atakayopewa badae.


Waswahili walisema; ‘mazoea mabaya' hilo lilidhihirika ndani ya ofisi zile za upelelezi mana hata IO alipopewa maelezo kidogo ya kesi ile na karatasi hakujihangaisha kusoma mbele ya mkubwa wake, akatoka na kwenda ofisini kwake kushugulikia baadhi ya viporo na kisha usiku akitulia aanze kupitia karatasi zile na ahsubuh aamkie kesi hiyo endapo ingekuwa na tija sana.


Hakujua yajayo!!


Hakujuwa kesho anaijua mungu pekee na hakuna binadamu aliewahi kuifikia kesho isipokuwa mauti pekee ndio hukufikisha katika ukomo wa kesho ila si mwanadamu aliehai mana kila siku ni kesho ijayo.


Hakujua! Hakujua! 




Hakujuwa kesho anaijua mungu pekee na hakuna binadamu aliewahi kuifikia kesho isipokuwa mauti pekee ndio hukufikisha katika ukomo wa kesho ila si mwanadamu aliehai mana kila siku ni kesho ijayo.


Hakujua! Hakujua!


******


2. FUMBO.


Askari wa usalama barabarani bwana Kambi kitime alihakikisha anajua ni nani hasa amewasiliana na Remi pale kituoni na ni kitu gani hasa kilichompeleka pale kituoni.


Upande wake wala haikuwa kazi hasa baada ya kuona kijana mmoja ‘IO' akiharakisha kuingia ofisi namba kumi.


Kwa uzoefu wake wa ushushu usio rasmi ambao hautambuliwi na ofisi za usalama,alijua kuna mwito maalumu wa kijana yule hasa baada ya kuhakikisha Remi ametoka ofisi namba kumi inayokaliwa na OCCID Shaban katwila.


Alimkariri ‘IO’ yule kisha akatoka ndani ya ofisi na kuaga kwa baadhi ya rafiki zake.


Alipohakikisha yupo mbali na viunga vya kituo cha polisi; akachukua simu yake kisha akalitafuta jina alilohifadhi kwa herufi kubwa.


‘Elchapo' alipohakikisha ndilo jina alilohitaji, akapiga.


Punde simu ikapokelewa upande wa pili.


“Sema kitime” iliunguruma sauti iliopokea.


“Kasuku alikuwa hapa kituoni dakika sita zilizoisha” alisema Afande Kambi Kitime.


Upande wa pili kwa mtu alietambulika kama Elchapo ulikaa kimya kwa sekunde kadhaa.


“Unahakika umemuona yule binti?” akauliza Elchapo.


“Aah!!, sasa nitashindwaje kumjua wakati picha ya Kasuku ninayo?” alihoji Afande Kitime huku akionesha dhahiri kuchukia.


“Aisee hii inaweza kutugharimu poti!” alisema Elchapo huku akisikika dhahiri kuwa juu ya uwezo wake wa kupumua.


“Umepata tetesi za alichokifuata?” Elchapo aliuliza kwa utulivu wa kutisha na hiyo ilimaanisha yupo kwenye kiwango cha mbali sana cha tafakuri.


“Aliingia ofisi namba kumi, na ameacha karatasi kadhaa na sijui kilichomo” alieleza Afande Kitime.


Elchapo akapumua kisha akasema; “Naomba unipe uwezo wa mtu aliekabidhiwa hiyo kesi”


“Solomoni Bukaba, ni intelligence ofisa na ni mjuzi si haba” alifafanua Kambi Kitime.


“Ok nadhani ataponzwa na hizo karatasi” alisema taratibu sana Elchapo.


Ukimya ulipita baina yao.


Sekunde kadhaa mbele Elchapo akavunja ukimya ule.


“Ahsante poti, kazi yako imeisha nenda benki saivi mzigo wako umeshasoma” akamaliza Elchapo kisha akakata simu.


Afande mnoko; Kambi kitime alifurahi kwa kazi yake nyepesi inayomuingizia mkwanja wa kutakata.


Malipo ya usaliti hakujua ni kifo na hilo hakujua afande huyu mnoko ambae rushwa ya barabarani kwa madereva aliona haiwezi kukidhi matakwa yake pengine aliona ni pesa ya kusafisha viatu tu kama alivyosema mheshimiwa mmoja nchini.


Hakujua usaliti wa damu hulipwa kwa damu.


*****


Solomini Bukaba ndie ofisa wa kitengo cha upelelezi ya makosa ya jinai na uhaini ndani ya Nchi na ndie aliepewa karatasi nne zilizotoka kwa Remi.


Kwa maelezo ya mwanzo aliopewa ni kuwa kesi hiyo inahusiana na upotevu wa watoto wawili na karatasi alizopewa ni ushahidi kwa mujibu wa Remi.


Solomoni Bukaba alikuwa na kiporo cha mkasa mwingine wa mauaji ya watu sita huko visiwa vya Mwabhurugu simiyu na yeye alipewa jukumu hilo kwa kuwa ilisadikika wauaji wamekimbilia jijini Mwanza.


Solomoni alikuwa anakamilisha ripoti ya uchunguzi wake kabla ya kuripoti kwa mkuu wake wa kazi hivyo kazi aliopewa na OCCID Shaban Katwila ilikuwa ni nyongeza ya mrundikano wa kazi kwake hivyo aliamua kuzisoma karatasi hizo akiwa nyumbani kwake usiku mnene.


Kiza kilipoingia tayari Solomoni alikuwa ameshakamilisha ripoti yake na akaihifadhi vizuri kwenye makablasha kisha akaihifadhi ndani ya droo ya moja ya makabati yaliokuwa ofisini kwake.


Alipomaliza akapiga mwayo mrefu kisha akajinyoosha ili kuondoa uchovu uliokuwa umeanza kumvaa.


Hakutaka kuendelea kukaa ndani ya ofisi zile, akatoka na kuchukua koti lake akavaa na kuliendea gari lake lililokuwa limepaki likiwa pweke baada ya magari mengine yaliokuwa pamoja nalo kuchukuliwa na wamikiki wake.


Aliweka kablasha lililokuwa limehifadhi nakala za karatasi za Remi kwenye kiti cha nyuma kisha akaingia ndani ya gari lake na kulitekenya.


Lilipostuka tayari alikuwa ameshaingiza gia na kuondoka kwenye viunga vya ofisi za kipolisi.


Mwendo wake haukuwa wa kasi, alikuwa anaendesha taratibu huku akisikiliza muziki safi kutoka kwa wazee wa kale Kilimanjaro Band wananjenje.


Ingelikuwa ni siku ambazo huwa yupo kwenye hekaheka za kukimbizana na wahalifu basi angekuwa makini sana na vioo vyake vya gari kuangalia mienendo ya gari zilizokuwa nyuma yake.


Labda kwa siku hiyo kwake ilikuwa kifo cha nyani miti yote huteleza au basi wimbi la kupoteza lilikuwa linamwandama.


Hakuweza kabisa kuiona gari ndogo nyeusi iliokuwa nyuma yake tangu atoke kituo cha Polisi Neshino.


Safari yake ilikoma mbele ya geti la kijani pembezoni kidogo ya soko la nguo Langolango.


Alishuka ndani ya gari kisha akaenda kufungua geti na kurudi kuingiza gari lake.


Moja kwa moja aliposhuka ndani ya gari lake, akaenda kuingia ndani kwake ambapo palikuwa pweke kwa sababu hakuwa na mke wala mtoto alieweza kuishi nae.


Makablasha yake akayabwaga kwenye sofa kisha akaenda bafuni kuoga.


Huko hakudumu sana akarejea sebuleni akiwa amevaa nguo nyepesi maalumu kwa kulalia.


Alianza kwa kuyaweka sawa baadhi ya makablasha yake ambayo hakuwa na kazi nayo kwa wakati huo.


Mikono yake ikalifikia kablasha lililohifadhi nakala alizopewa na mkuu wake.


Akalifunua na macho yake yakatua kwenye maandishi ya kwanza kabisa ambayo yalimshawishi aendelee kusoma.


Lakini kila alivyozidi kusoma alijikuta mwili wake unasisimuka kwa alichokisoma..


Hatimae akatua karatasi ya kwanza na kuendelea na ya pili hatimae ya tatu na ya nne ndio ilimtoa jasho.


Kwanini!!


Kwa sababu katikati ya maelezo ya ile karatasi kulikuwa kuna majina mawili yaliokuwa yamekolezwa kwa wino.


Mbali na majina yale kulikuwa pia kuna akaunti mbili za kibenki katika mabenki mawili tofauti.


Solomoni Bukaba akaingiwa na ganzi ya mwili hakika.


Kichwani mwake yaliibuka maswali mawili huku swali kubwa likiwa ni vipi ataindika ripoti yake kwa sababu kwa maelezo ya karatasi zile haikuwa rahisi kuandika tena upotevu wa watoto kama mkuu wake alivyotaka iwe.


Lakini pia alihitaji kumpata binti aliezileta karatasi zile ili amuulize maswali kadhaa.


Angelimpata wapi hilo hakujua na wakati huo mshale wa saa ulisoma ni saa tano na nusu za usiku.


Alihitaji kupiga simu kutoa taarifa ile na si kulala nayo mana hakutaka kabisa kuipuuzia.


Akatoka sebuleni na kuelekea chumbani kuchukua simu yake.


Akiwa chumbani huko huko akapiga simu.


Mwanzo alidhani hana salio mana simu iligoma kutoka. Bila papara akajaribu kuangalia salio.


Lilikuwepo!


“mmh” akaguna


Akarudia tena kupiga simu,hali ikawa ile ile.


Simu haikutoka.


“Alah!!” alagafirika.


Akaichomoa kitesi chake kisha akarudisha.


Bado hali ilikuwa ni ile ile simu yake haikutoka.


Pagumu!!!


Akahisi labda ni mtandao unasuumbua, akatazama juu ya meza ndogo iliokuwa chumbani mwake.


Akaiona simu ya mezani ikiwepo.

Akaiendea na kuzungusha mara kadhaa ila ilitoa mlio kuashiria hakuna simu inayoweza kupigwa ama kupokelewa na simu ile.


“Kum….ae” likamtoka tusi zito lenye uzani wa kilo kadhaa.


Akajishika kiuono huku akishindwa la kuamua.


Akavuta pumzi nyingi na kuzishusha nusu tu.


Akasita kuzimaliza akavuta tena.


Ewaah!!


Alinusa harufu ya kitu kuungua,akaangaza pale chumbani hakuona kinachoungua.


Haraka akapiga hatua ndefu na kutoka ndani ya chumba huku akibamiza mlango kwa nguvu.


Akapigwa na butwaa kwa alichokiona sebuleni.


Kulikuwa kuna mgeni aliezichoma moto karatasi zile nne huku akiwa amejikaribisha kwenye sofa.


Mgeni yule alikuwa ameziba uso wake wote na kubakiza macho tu.


Kifupi alivaa kininja.


Aligwaya.


Solomoni Bukaba alitazama tena mlango wake, ulikuwa umefungwa lakini pia alikumbuka alifunga mlango wa nje kihakika.


Kapitaje na wapi!!


Hakukuwa na wa kumjibu.


“Wewe ni nani na umeingiaje?” aliuliza Solomoni huku akijitahidi kuupoteza mtetemeko uliokuwa umeanza kuomba makazi mwilini mwake.


“Acha kuwa mjinga Solo; yani hujaona karatasi zilizoungua unauliza nimeingiaje au hazijakuuma karatasi hizo?” alimaliza kwa swali mgeni yule.


Maajabu!!


Solomoni alihisi kuota hivi, sauti ya mgeni wake ilikuwa ya mwanamke.


Lakini kulikuwa kuna kitu cha ziada kwa mwanamke yule na kitu hicho kilijaribu kumuingia Solomoni ila hakikuingia sawa sawa mana hofu na akili vilishindana kuziteka hisia za mwili.


Solomoni Bukaba akatupia tena macho yake pale zilipokuwa karatasi alizopewa na OCCID; zilikuwa zinamalizikia kuteketea.


Akagashabika!!


“Ulishazichoma kwanini usiondoke sasa” aliuliza kwa utaratibu Solomoni.


Mgeni akatokwa na cheko la kishambenga.


Hapo napo Solomoni akakazia tafakuri yake ili aone kama ubongo utamletea kumbukumbu ya sauti hiyo.


Ikagoma!!


“Unadhani nitaondoka kirahisi tu!” aliuliza mgeni yule wa ajabu huku akinyanyuka kwenye sofa.


“Kwanini isiwe kirahisi binti” Solomoni nae akauliza huku akimtizama kwa makini mgeni yule.


“Haya macho mbona..” akajisemea Solomoni ila hakumaliza kuyatafakari binti yule akakwepesha macho yake ili asitazamane na Solo.


“Hakuna aliewahi kuzitazama hizo karatasi akabaki hai” alijibu Mgeni.


“Una….” Solomoni hakumalizia kauli yake akajikuta akipokea teke safi la kifuani lililomsambaratisha chini kama gunia la Panya huko Nyasa.


Solomoni akashangaa alivyopigwa kitaalamu.


Kutoka pale alipokuwa kwa chini kulikuwa kuna bastola ambayo ni vigumu kujua huwa inawekwa mahali hapo karibu na sofa aliloangukia.


Akataka kuikwapua…!


Lauhaulah! !!” akashangaa kisu kikita karibu na mkono uliokuwa ukienda kuinyofoa mafichoni bastola yake.


“ Alijuaje naeka hapa mpuuzi huyu!” alijiwazia Solomoni huku akijizoazoa kutoka chini.


“Mwanaume mzima unakimbilia silaha mbele ya mwanamke, shame on you lazy boy!!” alichamba mwanamke yule.


Solomoni akajaa gadhabu.


Kosa hilo!!


Kwa kujitutumua akanesa juu ili amtandike teke mgeni, ila akaambulia patupu na kabla hajatua chini akajikuta akipokea teke la pumbu.


Solomoni akabweka kama mbwa koko aliegonganisha mabwana.


Maumivu yakamtambaa kila kona ya mwili wake.


Ili aisendelee kuotewa akajiegemeza kwenye kabati la vyombo lililokuwa lipo pale sebuleni huku mkono wake mmoja ukiwa umezikumbatia kende zake na macho yake yakiwa makini kwa binti mgeni ambae alikuwa amechora mchoro kwa mtindo wa fujtsu.


Patamu!


Dakika mbili zikapita za ukimya huku kila mmoja akijaribu kumsoma mwenzie mawazo yake.


Binti mgeni alionekana kujiamini sana kuliko maelezo.


Solomoni maumivu yakampungua nae akachora huku akimtizama binti kwa makini bila kufanya papara ya kushambulia.


Binti akacheza kidogo na kumpelekea makonde manne ya haraka haraka ambayo yalipanguliwa kihodari na solomoni.


Kisha bila kutarajia binti akajikuta akivutwa kwa kasi na kupigwa kiwiko cha uso kilichompeleka chini bila kupenda alipotaka kunyanyuka akajikuta akitandikwa teke la tumbo lililomrudisha chini kama mzoga wa kiboko majini.


Binti akawahiwa kwa kupigwa kabari matata wakati akijaribu kujiinua kupambana huku nafsini akijuta kumchukulia poa Solomoni.


Kabali ilizidi kumdumaza binti huku akikohoa na kutapatapa kama Mhaya aliepaliwa na Senene.


Solomoni akataka kupeleka mkono ili amvue kofia ya kuficha uso.


Hakutimiza matakwa yake akajikuta akipigwa mtama safi uliompeleka chini kwa mara nyingine huku akiona mpigaji akiwa nyuma yake.


Alimwachia binti na kusambaratika chini kama mzoga.


Akafanya haraka kujinyanyua baada ya kuona binti kapata usaidizi wa mtu ambae hakujua alikotokea.


Kabla hajasimama vizuri akajikuta kisu kikitua sawia tumboni mwake na kabla hajataka kukichomoa akapigwa mateke mawili ya kifuani na hata kabla hajaanguka akajikuta akijaa kwenye kabari matata ya mwanamke.


Akafurukuta lakini maumivu ya kisu na kuvuja damu kukampunguzia uwezo wa kujikomboa.


Taratibu akaanza kuhisi kizunguzungu na kuhisi akiachiwa na mkono wa chuma uliokuwa umemkaba.


Alihisi mabishano yakiendelea baina ya watu wale ila hakusikia kitu zaidi ya miluzi ilioanza kujenga urafiki na masikio yake.


***


Zilipita dakika kadhaa ndipo alipohisi kuna hali ya tofauti kutoka pale alipokuwa amelala.


Mwili hakuwa na nguvu lakini alisikia joto jingi huku akianza kupaliwa na alipofumbua macho akakutana na wingu la moshi mzito.


Nyumba ilikuwa inaungua!!.


Akajaribu kuinuka ila hakuwa na nguvu,akajaribu tena akashindwa.


Akakata tamaa na tayari alisikia mmomonyoko wa mabati kutokea huko vyumbani.


Kifo kilinusa pua za Solomoni Bukaba



Zilipita dakika kadhaa ndipo alipohisi kuna hali ya tofauti kutoka pale alipokuwa amelala.


Mwili hakuwa na nguvu lakini alisikia joto jingi huku akianza kupaliwa na alipofumbua macho akakutana na wingu la moshi mzito.


Nyumba ilikuwa inaungua!!.


Akajaribu kuinuka ila hakuwa na nguvu,akajaribu tena akashindwa.


Akakata tamaa na tayari alisikia mmomonyoko wa mabati kutokea huko vyumbani.


Kifo kilinusa pua za Solomoni Bukaba.


****


“Yule boya kakuotea leo aisee” alisema bwana mmoja mrefu aliekuwa anaendesha gari kwa kasi kutoka lango lango huku akipishana na magari na baadhi ya raia waliokuwa wameanza kujazana barabarani kushangaa moto mkubwa uliokumba baadhi ya nyumba zilizokuwa zimepakana na nyumba ya Solomoni Bukaba.


“Ndio mana kitengo kina Helper hasa killer akishindwa” alisema binti.


“Wapi sasa” aliuliza yule bwana.


“Club D nishushe pumzi” alijibu binti huku akiegemea kwenye kiti.


“mmh nadhani urudi nyumbani uoge” alishauri bwana dereva.


“ Haina shaka”


Gari ilichochewa moto.


****


..NCHINI CONGO..


Honda alihakikisha maelezo aliopewa na mateka wake yamemkaa sawia na hakutaka kuendelea kuhoji zaidi kwa wakati huo mana hakutaka kupoteza muda zaidi kwa kuwa alijua hapo ndipo ukomo wa ukweli kutoka kwa yule mateka na zaidi ya hapo ni kwa jasho na damu ndo ukweli atapata au kukosa kabisa.


Hakutaka kucheza bahati na sibu na muda.


Lazima amtafute X ambae kwa mujibu wa marehemu Bulembo ni Mtanzania na pia ni Club lakini kwa maelezo ya mateka; ndie aliewatuma wamkamate.


Akabaki na maswali kadhaa hivi.

Je X inahusu watu wangapi ama inahusu mtu mmoja?


Hakuwa na jibu.


Akajizoa zoa kutoka pale alipokuwa kisha akamsogelea mateka wake


“Kwanini mnamuita X?” aliuliza Honda Makubi.


Mateka akatoa cheko la kebehi kisha akajibu;

“Kwa sababu hafahamiki na hajulikani hata kwa sura!!”


“Duh!!” akaguna Honda kisha akaendelea kumsikiliza mateka wake.


“Kwa hiyo uliniona mjinga kukwambia tumetumwa na Mr X? au ulidhani ningemfahamu ninge….” Mateka hakumaliza kauli yake akajikuta anaelea hewani huku akishindwa kujitetea sababu ya kufungwa kamba ngumu kwenye kiti.


Mateka hakuwa na namna akasambaratika chini kama zigo la maharage mabichi.


Honda alijua kuna sababu za kuambiwa bila kukurukakara mwanzo na sababu aliipata na hakuwa tayari kuendelea kudhihakiwa hivyo akamtandika teke kali yule mateka lililomwacha akiwa hana msaada huko alikoangukia.


Honda akamwinua kisha akamshika kosi wa shati lake na kumvutia kwake wakawa wakitazamana kwa karibu.


“Nikirudi utanieleza aba,cha,da zote unazozijua Kimburu wewe” alichimba mkwara Honda kisha akamwachia na kukusanya vilivyo vyake na muhimu akavitia kwenye kwenye mkoba na kuuvaa kisha akatoka na kufunga milango yote vizuri na kuruka ukuta na kutokomea kuwahi pahali.


****


Kiza kilipoanza kuingia, Honda alikuwa nje ya ubalozi wa Tanzania nchini Congo.


Alikuwa amevaa kofia ya pama na suti matata iliomkaa vyema mwilini na kubadilisha mwonekano wake kwa kiasi kikubwa.


Wakati huu alivaa suti kwa sababu kwa waliomzoea kamwe hawakuwahi kumuona akiwa amevaa suti.


Mkononi alishika mkoba mweusi ambao alijua kabisa una uhumimu mkubwa licha ya kuhifadhi vitu asivyovifahamu maana yake.


Tayari wafanyakazi wengi walikuwa wameanza kurudi makwao.

Muda bado ulikuwa unaruhusu kwa watu wenye dharura kuingia na kutoka pale ubalozini kwa wakati huo.


Alijichanganya na watu hatimae alifanikiwa kuingia hadi mapokezi na bahati bado ilikuwa upande wake,mapokezi kulikuwa na watu kadhaa huku sehemu ya kupumzika kukiwa na watu wengine waliokuwa wakingoja huduma.


Akatumia nafasi ile kwa wafanyakazi kuwa bize akapita na kupanda juu kuelekea kwenye ofisi za Mkurugezni wa uhamiaji Papi Mndewa.


Alipofika karibu na mlango wa ofisi za Mkurugezi; Honda akasita kwenda zaidi akarudi nyuma kidogo akaangalia kushoto na kulia, hakuona mtu.


Kumbukumbu ya picha alioiona mezani kwa mhudumu wa mgahawa wa Tunde ikajijenga tena kichwani kwake.


Na hapo akajaribu kutazama tena ni wapi alipopigwa picha na mpigaji alipiga kwa kulenga kona akitokea upande gani!!


Hatimae macho yake yakatua kwenye kona iliotenganisha ofisi ya Balozi na chumba cha mawasiliano.


Konani pale kulikuwa kuna kamera ndogo mbili za usalama.


Macho yake akayahamishia tena kwenye kona iliotumika kutenganisha ofisi ya balozi na Mkurugenzi.


Tofauti na kona ya mwanzo yenye kamera mbili zilizofungwa pamoja, kona hii ilikuwa na kamera moja tu ambayo hata yeye alijua ilikuwepo na kona nyingine pia ilikuwa na kamera moja na ndivyo ilitakiwa iwe kila siku.


Alah!!!


Kamera ya pili ilitoka wapi na kwanini ilikuwa pale na ilikuwa na faida gani!!


Makubwa jama!!


Honda aliweka kituo kichwani kwake kumaanisha amefikia mwisho wa kufikiri wakati huo.


Wakati akitaka kufungua mlango wa mkurugenzi,mlango ukafunguliwa haraka akarudi nyuma.


Macho yao yakagongana.


Alikuwa ni mkurugenzi ambae alikuwa anataka kutoka kwenda kwake.


“Honda!!” aliita kwa kushangaa Mkurugenzi.


Honda akamwonyesha ishara warudi ofisini.


“Aisee nilijua nimeshakupoteza komredi” ndilo aliloweza kusema Mkurugenzi huku akimtizama Honda kama asieamini uwepo wake pale.


“Sio kunipoteza tu, hata uhai ningeupoteza na usingeniona kabisa” alisema Honda huku akikaa juu ya meza na kubaki wakitazamana kwa sekunde kadhaa.


“Nilijua wale jamaa watakuwa si watu wazuri japo kuwaingilia kiharaka vile kungeleta mkanganyiko wa kidiplomasia!!” alisema kwa masikitiko Mkurugenzi Papi Mndewa huku akitupa gazeti mezani pale alipokuwa amekaa Honda.


Honda alilitizama gazeti lile kisha akatabasamu.


“Kwani limeshatoka?” akauliza Honda bila kujishugulisha kulichukua mana ukurasa wa mbele ulikuwa umepambwa picha yake.


Picha ile haikumstua mana alishaiona tangu akiwa Tunde.


“Kwani linatoka lini hili gazeti mbona limesambaa sana!!” akauliza Honda.


“Nimeletewa na mtu wetu alieko huko linakopikwa na linatoka kesho.” Alijibu Papi.


“Kwani ilikuwaje!!” aliuliza Papi.


“Ni hadithi ndefu kidogo komredi ila kifupi tunazungukwa na watu wenye akili na ujuzi pia lakini ni lazima tupambane, na mchawi wetu wa kwanza anaanzia hapa hapa,unaionaje hiyo picha hapo?” alimalizia kwa swali Honda.


“ulipigwa wakati ukiingia hapa ofisni. Nimefikiria sana kuhusu mtu aliepiga picha hii na..!” Papi hakumalizia kauli yake alikatishwa na Honda.


“Picha haijapigwa na kamera ya mtu ila imepigwa kamera ilioko humu, lakini swali la kujiuliza, imewekwa lini na nani alieiweka?” akauliza Honda na kuacha swali lile likiambaa kichwani mwa Papi Mndewa.


Ukapita ukimya kidogo!


“Hii hatari sasa!!” alisema Papi huku dhahiri akionekana kuzama kwenye tafakuri!!


“Komredi mmefikia wapi na nyie!” alisema Honda.


“kiukweli tumeshindwa kujua kilichosababisha mawasiliano kukatika wakati balozi aliposhambuliwa. Tumejaribu kupitia kamera na miundo yote ya usalama ili kuona ni wapi hujuma ilianzia,lakini kote kulikuwa shwari aisee na nimeagiza baada ya kumsafirisha Balozi basi tuanze uchunguzi upya mana kuna ukakasi pahali” alimaliza kueleza Papi.


Honda akazishusha pumzi kwa mkupuo.


“Hali ni tete, lakini hili sakata litaisha, ikishindikana basi tutaomba makao makuu watuongezee nguvu” alisema Honda.


“Japo naamini hujashindwa lakini ikifikia huko tutakuwa hatuna namna!” alisema Papi.


“mmh wale vijana wa kitengo cha usalama wapo wangapi vile!!” alihoji Honda huku dhahiri akionekana kuwa na hisia za kumbukumbu.


“wapo watatu Komredi!!” alijibu Papi.


“Basi jicho lako lianzie hapo Komredi” Honda alimwambia Mkurugenzi wake!


Papi akatikisa kichwa bila kutoa sauti na hilo lilimaanisha tayari uchunguzi dhidi yao umeanza.


“Ok naomba unifikishe ofisini kwa Balozi kuna kitu nahitaji kutazama.” Alipokwisha kusema hivyo tayari miguu yao ilianza kufanya harakati za kuondoka ndani ya kile chumba.


Dakika moja badae wote walikuwa wanatazama tundu la risasi lilokuwa limejenga nyufa kadhaa kwenye kioo.


“Mdunguaji!!” alijisemea Honda huku taratibu akisogea lilipokuwa dirisha.


“ina maana hili pazia lingekuwa limerudishiwa basi mdunguaji angekosa shabaha” alisema tena taratibu Honda huku akishika tundu la risasi ilipopita.


Moja ya sifa kubwa ya kubwa ya Honda ni kutambua ukubwa wa vipenyo vya risasi na aina za silaha.


Hata hapo alijua.


“Hii ni Lapua Magnum bila Shaka” alisema Honda huku akimgeukia papi.


“Yes!! Kitengo kimethibitisha aina hiyo ya risasi na silaha ilikotoka.” Papi alijibu swali la kijana wake.


“Lakini kwa nilivyoona siku ile kabla sijakamatwa hili pazia lilikuwa limerudishiwa makusudi kabisa na nadhani wewe ungechunguza pia aliefanya usafi siku hiyo Mkuu au!” Honda alitoa mawazo yake kwa mtindo wa kuhoji.


“Hilo pia litafanyiwa kazi na sikuwa nimeliwaza kabisa komredi” alisema Papi huku akigonga tano kuashiria amekubali mawazo ya kijana wake ambae tangu wajuane walifanya kazi kwa ukaribu kiasi wakajikuta ni kama wanalingana wadhifa.


“Kile chumba pale ghorofani kinaweza kunifikisha kwa muuaji wa Balozi” alisema Honda huku akinyooshea kidole upande wa pili kulikokuwa na ghorofa kubwa na ndefu.


Ukimya ukapita.


Naendela na majukumu komredi ila usiponiona siku tatu pale ndani kwa Bulembo kuna kipanya nimekihifadhi pale kakichukue kinaweza kukufikisha nilipoishia” alisema Honda huku akianza kutoka pale ofisini.


Kitu kimoja ambacho watu hawa hawakujua ni kuwa kulikuwa na mtu mwingine aliewasikia walichokua wanazungumza.


Lakini kwao ni kama kiza hakuna walichojua.


****


Sajini Kebu alikuwa ametulia kimya huku akiwaza namna alivyonusurika kusombwa na maji yaliokuwa yanapita chini ya daraja alilitupiwamo na Honda.


Kimoyomoyo alihusudu uwezo wa akili wa mtanzania yule.


Sajini kebu akageuza macho yake kushoto kwake akakutana na jicho la Kojo ambae waliunganishwa pamoja baada ya vijana wa Kebu kuadhibiwa na Honda; hivyo sasa alikuwa ameungana na kundi la Kizibo na Kojo.


Aliona jinsi uso wa Kojo ulivyopasuka bila mpangilio.


“Umesema hii kazi ya yule bwege sio!!” aliuliza Sajini Kebu.


Swali lile lilionekana kumkera Kojo ila hakujibu akabaki kutazama pembeni.


“Bwana yule ananitesea rafiki yangu aisee” alidakia Kizibo aliekuwa amekaa kwenye kiti cha dereva.


“Hebu nipelekeni nikapumzike kwa mrembo wangu nikitoka huko risasi za kichwa zitammaliza Honda!!” alisema Sajini Kebu huku akiegemea kiti cha abiria alichokuwa amekalia.


Gari ikawashwa na kuondoka kuelekea viunga vya mji wa Gombe pembeni kidogo ya mji wa Kinshasa.


Ni kwa kuwa hawakujua lijalo halijawahi kujulikana kamwe.


**


Sajini kebu akageuza macho yake kushoto kwake akakutana na jicho la Kojo ambae waliunganishwa pamoja baada ya vijana wa Kebu kuadhibiwa na Honda; hivyo sasa alikuwa ameungana na kundi la Kizibo na Kojo.


Aliona jinsi uso wa Kojo ulivyopasuka bila mpangilio.


“Umesema hii kazi ya yule bwege sio!!” aliuliza Sajini Kebu.


Swali lile lilionekana kumkera Kojo ila hakujibu akabaki kutazama pembeni.


“Bwana yule ananitesea rafiki yangu aisee” alidakia Kizibo aliekuwa amekaa kwenye kiti cha dereva.


“Hebu nipelekeni nikapumzike kwa mrembo wangu nikitoka huko risasi za kichwa zitammaliza Honda!!” alisema Sajini Kebu huku akiegemea kiti cha abiria alichokuwa amekalia.


Gari ikawashwa na kuondoka kuelekea viunga vya mji wa Gombe pembeni kidogo ya mji wa Kinshasa.


Ni kwa kuwa hawakujua lijalo halijawahi kujulikana kamwe.


Na kama walidhani wanaenda kupumzika walikosea sana.


****


Simbi Musinza alikuwa ni mshindi wa mashindano ya ulimbwende katika mji wa Kishansa kisha akaenda kushiriki mashindano ya urembo yaliokutanisha warembo kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya nchini Congo.


Bahati mbaya kwake, hakufanikiwa kufanya vizuri sana hasa baada ya wandaaji kugundua Simbi alikuwa akitumia zaidi mwili wake kushawishi wandaaji wamchague.


Ukizungumizia warembo waliotikisa katika mashindano hayo basi huwezi kumsahau Simbi ila tabia yake ya kupenda rushwa kwa kutumia mwili wake ilisababisha aangukie pua.


Licha ya kushindwa katika mashindano hayo,lakini bado jina lake na uzuri wake uliendelea kutikisa kurasa za magazeti jijini Kinshasa.


Simbi alikuwa na maisha ya kupenda anasa, kila siku lazima avinjari viwanja kadhaa waliokuwa wanapapatika na uzuri wake na umaarufu wake.


Hakuna sehemu yoyote ya anasa ambayo Simbi hakufahamika.


Katika sehemu moja ya chumba cha watu maalumu(VIP) kulikuwa kuna watu wawili wamekaa huku wakisikiliza muziki uliokuwa utoka kwenye sipika zilizokuwa zimefungwa kila kona ya chumba kile.


Mwanaume mmoja wa kizungu alikuwa amekaa huku amenyoosha miguu yake na usawa wa tumbo lake kulikuwa kuna kichwa cha mwanamke kilichokuwa kimejaa nywele bandia za gharama kubwa.


Mwanamke yule alikuwa akiperuzi mtandaoni huku mara kwa mara akicheka peke yake na mara zingine alicheka huku akimtizama usoni mwanaume wake wa kizungu.


Alikuwa ni Simbi!!


Mzungu aliendelea kumpapasa Simbi kuanzia kifuani hadi kichwani.


Ni kama Simbi hakusikia mguso wowote kutoka kwa mtu wake huyo, yeye alikuwa bize tu na kuperuzi kwenye mtandao.


Kama si upofu wa mapenzi basi Mzungu yule angekasirika kwa kutokupewa muda na Simbi.


Ila hakujali!!


Simbi akiwa bado anaperuzi, mara akaona ujumbe kwenye simu yake.


“Uko wapi!!” ulisomeka hivyo huo ujumbe kutoka kwa mtu aliekuwa amehifadhi jina lake kwa SAJINI.


Akanyanyuka gafla kisha akamtazama mzungu ambae wala hakujali yeye aliendelea kuvuta shisha tu.


Simbi alibaki ameganda bila kufanya lolote huku akijua kabisa ni nadra sana kuona lile jina linamtafuta.


Na likimtafuta basi siku hiyo anajua lazima avuliwe chupi.


Kilichomfikirisha sio kuvuliwa chupi na mmiliki wa jina lile.


la hasha!


Yeye aliwaza dau la pesa ambalo angeachiwa ahsubuhi na bwana huyo.


Dau la bwana yule huwa ni kubwa kuliko analoachiwa na mzungu.


Akawaza jibu.


“Nipo njiani naenda home” alijibu kisha akamsogelea mzungu.


“Leo unatoa ngapi kwani!!” aliuliza kwa sauti kavu huku mkono akiwa ameshika kiunoni.


Mzungu alishangaa mabadiliko ya mwenzi wake huyo.


“Kama kawaida dola mia!!” alisema Mzungu.


“Ooh ok!!” alisema Simbi.


“Kwani vipi!!” Mzungu alionesha mashaka yake.


“Hapana mpenzi, ila nimeingia kwenye mzunguko wa hedhi sasa hivi!!”


Mzungu alinywea kama kapigwa denda na kichaa.


Wakati bado Simbi anangojea kauli nyingine kutoka kwa Mzungu; mara akasikia ujumbe mwingine ukiingia kwenye simu yake.


Akaufungua!!


Aisee!


Alitamani kuivunja simu wakati huohuo na asipatikane kabisa.


Akaurudia kuusoma ujumbe ule na kuhakikisha jina la mtumaji.

Halikubadilika lilikuwa ni lile lile na ujumbe ni ule ule na ulisomeka vile vile.


“Nipo nakuja kwako Chimamy” ulisomeka hivyo na mtumaji mtu aliekuwa amemhifadhi kwa jina la CHIBABY.


Simbi alihisi kubanwa na tumbo la kuhara,haraka akakimbilia chooni.

Huko wala alichotarajia kitoke hakikutoka, isipokuwa aliongeza joto mwilini kwa mbio zilizomfikisha huko maliwatoni.


Mapigo yake ya moyo yalitaka kuzidi kipimo cha kawaida cha udundaji wake.


Akatoka maliwatoni bila kufanya lolote huko na alipomtazama mzungu wake akamwona alivyosawajika na midomo kumuanguka kama rasi alienyolewa usingizini.


Hakumjali!!


Yeye alikuwa anawaza tu namna ya kutatua fumanizi huko kwake na ukizingatia wanaume wote aliwahitaji mana mmoja alikuwa anamhonga vizuri na mwingine ndie mwanaume aliempenda sana.

Nani alisema wapenda pesa hawana moyo wa kupenda!!


Simbi hakutaka kumpoteza kabisa chibaby wake, mwanaume wa kitanzania alietokea kumgusa kila kona ya mwili wake nae akagusika,mwanaume aliejua kumwacha hoi kila walipokutana,mwanaume aliejaliwa mwili mzuri wa kiume.


Hata!!


Wote aliwahitaji.

Mwanaume mwenye pesa na mwanaume wa moyo wake.


Lazima aue fumanizi hilo kivyovyote.


Haraka akakimbilia mkoba wake na kutoka nje ya chumba kile kilichokuwa kwenye jumba kubwa la anasa ndani ya mji wa Gombe.


****


Nje ya nyumba ya Simbi kulikuwa kuna gari moja jeupe limesimama huku ndani yake kukiwa na watu watatu.

Sajini Kebu;Kizibo na Kojo.


“Komredi mi naingia kupiga pumzi kidogo,nitakaa saa tatu!!”

Alisema Sajini Kebu huku akifanya jitihada za kushuka ndani ya gari.


“Kwa hiyo sisi tunabaki kuwa walinzi wako? Aliuliza Kizibo.


“Hapana! Kama kuna anaetaka kuingia nae akapumzike kidogo twenzetuni jama” Sajini aliwaelekeza wenzie.


Kizibo na Kojo walitazamana, kisha Kizibo akazima gari na kushuka huku akimwacha Kojo akijilaza kwenye viti kumaanisha yeye atapumzika ndani ya gari.


“Unalala tena kwenye gari yule bwege atakuotea tena aisee!!” alitahadharisha Kizibo na Kojo akanyoosha bastola juu kumaanisha akitokea tu anamlipua kwa risasi kadhaa.


Kizibo na Sajini Kebu wakatasamu huku wakiliendea geti.


Kitu ambacho hawakujua ni kuwa Simbi alikuwa ndani na mwanaume mwingine na mwanaume aliekuwa ndani nae hakujua kuna mwanaume mwingine nae anakuja hapo ndani.


Wao walikuwa hawajui ila Simbi alijua na alipanga kucheza nao wote usiku mmoja.


Tatizo hakuwahi kujua wanaume wanaonenda kukutana ndani ni wanaumeume wa aina gani!!


Patamu





Kizibo na Sajini Kebu wakatasamu huku wakiliendea geti.


Kitu ambacho hawakujua ni kuwa Simbi alikuwa ndani na mwanaume mwingine na mwanaume aliekuwa ndani nae hakujua kuna mwanaume mwingine nae anakuja hapo ndani.


Wao walikuwa hawajui ila Simbi alijua na alipanga kucheza nao wote usiku mmoja.


Tatizo hakuwahi kujua wanaume wanaonenda kukutana ndani ni wanaumeume wa aina gani!!


Patamu!!


Simbi alikuwa anaishi ndani ya nyumba kubwa yenye vyumba vinne huku vyumba hivyo vikitengenishwa na sebule pana iliojumuisha jiko na sehemu maalumu ya maakuli.


Honda ndie aliekuwa mwanaume wa kwanza kutangulia pale huku lengo lake likiwa ni kupumzika na kumuliza Simbi juu ya uwepo wa Club X ndani ya Kinshasa ama Gombe.


Alifikia hatua ya kumuliza kwa sababu, hakuna sehemu ya anasa na starehe ambayo Simbi hakuwahi kufika.


Honda alitoka bafuni na hakumkuta Simbi chumbani.


Hakujali!!


Akaendelea na hamsini zake kisha akajilaza huku akiutazama mkoba mweusi aliokuwa ameuweka kwenye sofa kubwa lililokuwa mle chumbani.


Mawazo yalipata kichwani mwake bila majibu.


Akanyanyuka na kuuendea mkoba ule.


“Ulitaka kusema nini Bulembo!!” alijiuliza huku akiushika mkoba ule.


Akaufungua na kuzitoa karatasi tatu ambazo hazikuwa zimeandikwa chochote kile.


Akazigeuza huku na huko lakini bado hakuona kitu katika karatasi zile.


Akilini mwake hakutaka kuamini kwamba karatasi zile zilikuwa mle bahati mbaya.


Akazirudisha kwenye mkoba, kisha akatoa kidole ambacho alishindwa kutambua kilikusudiwa nini kuwekwa mle ndani ya Mkoba.


Akakishika kwa tahadhari, huku akibinua huku na huko..


“Mtu gani anakidole cha hivi jama!!” akilijisemea huku akiendelea kuona namna kidole kile kilivyokuwa kimepasukapasuka.


“Kwa nini alikikikata,na…” hakumaliza alichokusudia kuwaza,akaona kitu kilichomsitabisha kidogo.


Ni baada ya kukibonyeza,kikawa kinatoa kimiminika mithili ya damu.


Akabonyeza tena na hali ikawa ile ile japo safari hii mbonyezo wake ulifikia kitu kingine ndani ya kidole kile.


Akajaribu kukibinua binua huku na huko tena.


Mara macho yakanasa kitu pale kulipokuwa kunatoa kimiminika mithili ya damu.


Kulikuwa kuna upenyo kama mchano wa wembe.


“ina maanisha nini hii” akajisemea huku akitazama huku na huko kuhakikisha kama bado yupo peke yake chumbani.


Bado alikuwa peke yake.


“Hapa si pahala sahihi” alijisemea huku akiweka tena karatasi na kidole kile ndani ya mkoba kisha akasafisha mikono kwa maji baada ya kuchafuka kwa kimiminika kilichokuwa ndani ya kidole kile cha ajabu.


Akajilaza tena huku akimsubiri Simbi ambae alikuwa amekawia huko sebuleni.


***


Wakati Honda akiwa anangoja,huku chumba kingine Simbi alikuwa anamalizia kutupia kanga mwilini mwake.


Ni baada ya kumpa mambo ya kikubwa Sajini Kebu ndani ya dakika tatu.


“Mbona sikuelewi Simbi”aliuliza Sajini.


“Sajini nimekwambia mama kaja kunitembelea yupo chumbani kwangu” alisema kwa madeko Simbi.


Sauti yake nyororo ikausisimua mwili wa Sajini;akakosa kauli kwa dakika kadhaa.


“Kwa hiyo mama yako anakukataza kulala mbali nae!?” aliuliza Sajini.


Simbi aliamua kutumia jinsia yake kama silaha ya kumlegeza Sajini.


Aliamua kulegeza sauti na kuongea kimadeko ili amweke sawa Sajini.


“No baby,nitakuja nakupa kama hivi afu narudi tena wala usijali” alisema kwa madeko huku akimpiga busu la sikioni kisha akaingiza ulimi wake wa moto sikioni mwa Sajini.


Sajini alihisi kapigwa na waya uliotengenezwa kwa barafu,mwili mzima ukaingiwa na mtetemeko wa ajabu.


Sajini akajikuta akicheka kibwege huku akimshudia Simbi akitikisa makalio yake kama abilia wa Mbagala akiwahi daladala.


Akatabasamu huku chini ya suruali kukifuruka bila mpango maalumu, mara kunese mara kulale ili mradi mtafaruku tu ndani ya kaptura aliokuwa amevaa.


***


Dakika sita baadae Simbi alikuwa akitoka bafuni huku akiwa na Kanga tupu mwilini, akatazama kitandani kuliko kuwa na mwanaume wa ndoto zake.


Nafsini mwake alijutia kwa kile anachokifanya yani kulala na wanaume wawili ndani ya nyumba moja huku wote wakiwa hawajuani.


Ila akapiga moyo konde huku akimwomba mungu asije kuumbuka.


Kitu ambacho hakujua ni kuwa tamaa ikiwa mbele mauti huwa nyuma kila mara.


“Chibaby kwani umechoka sana?!” Aliuliza Simbi baada ya kuona Honda amegeuka na kumtazama tu bila kufanya wala kuzungumza lolote.


Simbi alijua namna ya kucheza na hisia za Honda hivyo hakungoja jibu lake.


Akaitupa Kanga chini kisha akaienda kwenye meza ya kujipodoa ambayo haikuwa mbali na kitanda alicholalia Honda.


Akaugeuzia mgongo machoni mwa Chibaby wake kisha akainama huku akikata mauno taratibu kama wafanyavyo wanengua uchi kwenye Club za usiku.


Akaanza kujipaka mafuta huku kila mara akiyatikisa makalio yake yaliojaa kwa mpangilio thabiti.


Mtikisiko wa makalio yake ukamsisimua Honda ambae muda wote alikuwa amemkodolea macho Simbi kwa uchu wa ngono.


Akanyanyuka na kumvaa Simbi vile vile alivyokuwa ameinama na kilichoendelea hapo ni miguno na mtikisiko wa nyonga.


Hawakuishia hapo,wakahamia kitandani ambapo Simbi akawa juu ya Honda huku akitoa miguno kama Paka anaetekenywa na kiuno akikizungusha na kufanya makalio yake yapapatike kama kaumwa na siafu.


Walidumu katika mtifuano huo kwa zaidi ya saa tatu huku kila mmoja akionekana kufurahia tendo hilo adhimu.


Kilichoafuata ni kila mmoja kuangukia upande wake akiwa hoi.


Zilipita dakika zaidi ya araobaini ndipo Honda akanyanyuka kitandani kisha akatazama saa ukutani ambayo ilionesha ni saa saba unusu usiku.


Hakutaka kupoteza muda akiwa amelala na mwanamke wakati hajui kinaendelea nini huko nje.


Alienda kwa Simbi kupumzika na tayari alishapumzika na kupunguza uzito.


Alijihisi yupo sawa kuendelea na harakati zingine.


Akamtazama Simbi akaona bado amelala na hakutaka kumwamsha ili kuepuka usumbufu wa maswali.


Akavaa nguo haraka na kutaka kutoka.


Akakumbuka kilichompeleka pale ilikuwa ni zaidi ya kupumzika.


Alihitaji kujua ilipo Club X.


Taratibu akamwamsha Simbi.


Simbi aliamka huku akipiga mwayo kuondoa uchovu na usingizi.


“Chibaby mbona wavaa usiku huu?” aliuliza Simbi.


“Chimamy nimepigiwa simu sasa hivi kuna wadau wameingia usiku huu na lazima tuonane” alijibu Honda.


“Haiwezi kuwa ahsubuhi?”


“ Hapana; ahsubuhi wanaondoka na ndege ya alfajiri mpenzi”


“Mh haya bwana” alijibu kinyonge Simbi.


“Afu wamenambia wapo Club X na sipajui”


Simbi akaonesha msituko dhahiri bila kificho.


Honda aliuona msituko ule.


Kwanini asituke?

.

Ni swali ambalo alilijibu kwa hisia.


“yaezekana si sehemu salama!!” Honda aliwaza.


“Kwanini wamefikia Club X?” alihoji Simbi huku bado akionekana kuwa na msituko.


“Kwani vipi” Honda alitupa jiwe kizani, alihoji bila kufafanua alilenga nini.


“Kama huna kadi,pale huingii na ukiingia hutoki. Je una kadi?” alimaliza kwa kuhoji Simbi.


Honda alibabaika kidogo na mawazo yalipita kichwani kama mvua huku akitamani kuhoji maswali mengi kuhusu Club X.


Alijionya!!


Hakutaka kumuuliza maswali mengi ambayo yangemtia wasiwasi Simbi.


Alipanga kuhoji siku nyingine.


“Ipo wapi Club yenyewe?” aliuliza Honda.


Simbi akasimama.


“Honda mpenzi; kama huna kadi wambie rafikizo mkutane sehemu nyingine” alisema Simbi huku akionesha woga ambao Honda alishindwa kuutafsiri kwa haraka.


“Simbi chaurembo wangu,kwa sasa naomba unielekeze ilipo Club X tafadhali, mengine tutayongea nikirudi”


Simbi alibaki akimkodolea macho Honda kisha aazishusha pumzi zake kwa mkupuo.


“Ni Club ndani ya Club nyingine na ipo D…” Simbi hakumalizia kauli yake.


Mara mlangoni kukasikika kishindo na malumbano.


Honda akakaa chonjo huku Simbi akitamani ardhi ipasuke aingie mzima ili aepuke balaa linalokuja.


Haikuwezekana alichoomba.


Simbi akaanza kutetemeka.


****


Kizibo tangu waingie pale ndani alitokea kuuhusudu uzuri wa Simbi na hata wakati anapewa chumba akajipumzishe,yeye mawazo yake yalikuwa kwa Sajini jinsi anavyomfaidi mlimbwende yule..


Hata wakati Simbi anaingia na kuvua nguo kwa Sajini,yeye alinyata na kuchungulia kwenye tundu la funguo.


Alipoona haoni kitu akaamua kuweka sikio lake kwenye mlango huku hisia zake akiziweka sehemu moja tu.


Kilio cha mahaba alichokitoa Simbi kilimpagiwisha Kizibo huku akitamani avunje mlango na yeye aonje hicho kilio ila akajionya.


Hakutaka mgogoro wakati bado wanakazi.


Kilio cha Simbi hakikuzidi dakika tatu kikata.


Alilaani na kumdharau Sajini,mana alitegemea Simbi aendelee kulia hata zaidi ya dakika kumi.


Hata wakati wanaagana na Simbi kuahidi kurudi usiku,yeye alisikia na akaondoka mlangoni ili asikutwe.


Usiku ulikuwa mgumu kwa Kizibo. Kila alipofikiria umbo na kilio cha Simbi alitamani aende chumbani kwa Simbi walau amwekee hata kidole tu.


Aligalagala huku na huko kama mtoto aliebalehe huku akitizama filamu za kikubwa.


Ki kawaida alitakiwa awe kubwa jinga mana umri wake haukufanania kabisa na mawazo yake.


Akaanza kujichua huku akijifananisha yupo juu ya kifua kichanga cha mlimbwende Simbi.


Uvumilivu ukamshinda na yeye katika makuzi yake hakuwahi kutongoza.


Yeye alikuwa akitaka mwanamke basi njia pekee ni kumteka na kumbaka kisha kila mtu anapita njia yake.


Kizibo hakuwahi kupenda, yeye alichokipenda na kukihusudu ni bunduki yake iliotoa uhai wa watu kadri alivyoweza.


Mazoea mabaya.


Akaona njia pekee ni kubaka na aliamini Simbi na Mama yake kamwe wasingeweza kupiga kelele.


Alikuwa fundi wa kubaka.


***

Wakati Kizibo akiwaza kwenda kubaka,Sajini Kebu yeye alikuwa anaona anacheleweshwa.


Kila alipodhani Simbi angelitokea,haikuwa hivyo.


Muda ulizidi kusonga na alihitaji kuushika tena mwili wa Simbi.


Akaona ni uzuzu kuendelea kulala.

Akataka kwenda kumgongea Simbi.


Kamwe mwanamke hajawahi kuwa juu ya mwanaume. Ndicho alichokiamini Sajini.


Akanyanyuka.


Wakati anafungua mlango ni wakati huo Kizibo alikuwa tayari alikuwa ameshavuka sebule na kuelekea kilipo chumba cha Simbi.


Sajini alitoka taratibu akiwa hana habari ya Kizibo kuwa huko aendako.


Na si Kizibo tu aliekuwa huko ila ndani ya Chumba kulikuwa na kidume mwingine aliekuwa amefaidi utamu wa Simbi usiku ule na ndie adui yao alikuwa amewalaza kichovu.


Mi simo!!!


******



Akanyanyuka.


Wakati anafungua mlango ni wakati huo Kizibo alikuwa tayari alikuwa ameshavuka sebule na kuelekea kilipo chumba cha Simbi.


Sajini alitoka taratibu akiwa hana habari ya Kizibo kuwa huko aendako.


Na si Kizibo tu aliekuwa huko ila ndani ya Chumba kulikuwa na kidume mwingine aliekuwa amefaidi utamu wa Simbi usiku ule na ndie adui yao alikuwa amewalaza kichovu.


Kizibo alizidi kuukaribia mlango wa chumba cha Simbi.


Alipoufikia akasikilizia kwanza.

Akatazama kushoto na kulia hakuona mtu,akaingiza mkono mfukoni na kutaka kutoa funguo zake zisizoshindwa kitu.


Akasita!!


Alisita baada ya kusikia mabishano ya sauti mbili za kike na kiume.


Akavuta kumbukumbu ya sauti hiyo kama inaweza kufanania na sauti ya Sajini.


Haikuwa yenyewe!!


Akagwaya!


Haraka akaondoa dhamira yake ya ubakaji,akageuka ili aelekee chumbani kwa Sajini.

Hakugeuka hata hatua moja, akakutana na jicho kali la Sajini likimtizama, jicho lililokuwa limejaa husda na wivu.


Akagwaya!


Alibaki akiwa amezubaa asijue anataka kusema nini.


“Ulifuata nini huku komredi” alisema Sajini huku dhahiri akionekana kuwa na kovu la hasira na uchungu uliochanganyikana na wivu.


“hapana kiongozi ni…” hakumalizia kauli yake akakatishwa na Sajini.


“Hizo funguo je! Ulitaka kubaka mke wangu sio!!”


Kizibo midomo ikamuanguka na akashindwa ajitetee vipi.


Akakumbuka kuna sauti ya kiume chumbani kwa Simbi, akataka kumsanua Sajini Kebu.


“Kiongozi humu kuna…!” hakumalizia tena kauli yake akajikuta anachezea konde moja safi kutoka kwa Sajini ambae kipimo cha uvumilivu kilikuwa kimemwisha.


Konde alilopigwa Kizibo bila kutarajia likampeleka chini kama mzoga,akataka kunyanyuka akakutana tena na teke lililompelekea kujigonga kwenye mlango wa chumba cha Simbi na kumsambaratisha chini.


Kishindo kile ndicho kilichowasitua Simbi na Honda chumbani kwao.


Kizibo nae akashindwa kuvumilia akanyanyuka kama mbogo aliejeruhiwa na kumpelekea makonde mawili ya harakaharaka ambayo yote yalipanguliwa kisitadi na Sajini ambae nae akarudisha teke la mawashi lililopanguliwa na Kizibo kama mzaha.


Chumbani bado Honda alizidi kusikia vishindo vya watu wakipigana na kwa mdondoko tu,ilionesha wanaopigana ni wajuzi wa mambo.


Sasa kwanini wapigane na wapiganie ndani ya nyumba ya Simbi.


Akamgeukia Simba na kwa kumtazama tu tayari aliona kutetemeka kwa Simbi ni zaidi ya uoga ila ni uoga wa anachokijua.


Simbi nae akamtazama Honda na akakutana na macho yaliojaa viulizo.


Simbi akabaki kutikisa kichwa tu asijue ndio anakataa au anakubali au anasikitika.


“Najua unawajua,wasikilize tafadhali!!” alisema Honda huku tayari kichwani akijua cha kufanya kuepuka zogo.


Simbi hakuwa na namna kama ni maji sasa yalikuwa yanaelekea kuzidi unga.


Akaufuta mlango kinyonge kisha akaufungua.


Alichokishuhudia ni manundu usoni mwa wageni wake.


Hakusema kitu akabaki anawatazama wanaume wale waliotoshana nguvu.


Honda alikuwa anahitaji kuwajua waliokuwa wanatoana jasho huko nje ya chumba, hivyo akaanza kufuatilia kila hatua aliopiga Simbi na wakati alipokuwa akifuangua mlango wala hakujiuliza mara mbili kwa alichokiona.


Alimwona dhahiri shahiri Sajini Kebu na mwanaume mwingine ambae alikuwa amempa mgongo.


Hakutaka balaa usiku ule ikiwa hajui Sajini pale alipo ananguvu kiasi gani.


Hakujiuliza zaidi,macho yake yalielekea moja kwa moja lilipodirisha pana la vioo vya kisasa ambalo halikuwa na nondo ndani.


Akaliwahi na alipata nafasi nzuri ya kutimka baada ya Simbi kurudishia mlango nyuma yake.


Kizibo alitaka kujisafisha kwa kujitoa kwenye lawama za kutaka kumbaka Simbi; hivyo wakati ambao Sajini amezubaa akimtizama Simbi aliekuwa kwenye nguo za kulalia ndipo nae akatumia mwanya huo kuchoropoka na kuingia chumbani kwa Simbi.


Sajini Kebu akataka kumfuata ila Simbi akamwekea mkono kumzuia.


“Mnataka kupigania chumbani kwangu?” alihoji Simbi kwa sauti ya kitetemeshi ambacho Sajini hakujua kililetwa na nini.


“aah…” akababaika kujibu Sajini.


Mara akaja kwa kasi Kizibo.


“Wewe mwanamke ulikuwa unaongea na nani humu ndani?” aliuliza Kizibo baada ya kuingia ndani na kumkosa aliesikia sauti yake.


Simbi akagwaya na asijue cha kujibu.


“Acha dharau Kizibo,kwa hiyo umeamua kusingizia mengine.” Alihoji Sajini huku akipiga hatua kumfuata Kizibo.


Simbi aliingilia kati.


“umemkuta nani huko na ulimsikia nani huko!” aliuliza Simbi kwa ujasiri baada ya kugundua Kizibo hajamkuta Honda japo hakujua amejificha wapi. Hakutaka kulijua hilo wakati huo.


“Kuliku….” Akataka kusema kitu Kizibo ila Sajini akaingilia kati.


“Unasingizia mtu,mh mtu gani jamaa angu!”


Ikabaki kila Kizibo alipotaka kusema kusikia kwake sauti ya mwanaume pale ndani, hatia ya kunyatia vyumba vya watu ilimnyima kueleweka mbele ya Sajini ambae alikuwa amejenga chuki kwa Kizibo.


Malumbano yao yalikuja kukatishwa na sauti ya risasi huko nje na bila kungoja Kizibo na Sajini Kebu wakakimbilia vyumbani mwao kuchukua bastola walizokuwa wameziacha vyumbani walikokuwa kabla ya kitimtim hicho.


*****


Kojo alichoka kukaa ndani ya gari hivyo akashuka na kutembeatembea ili kunyoosha miguu iliokuwa imechoka kwa kukaa sana ndani ya gari huku kila mara akisonya kwa kuona muda unazidi kwenda huku waliokuwa ndani wakikawia kutoka.


Ni wakati akitaka tena kurudi ndani ya gari ndipo macho yake yakaona kivuli kikiwa juu ya ukuta na kisha kikachumpa na kuanguka chini.


Kwa msaada wa taa zilizokuwa zikiwaka kwenye nyumba za jirani; Kojo aliona mtu akinyanyuka na kujitikisa mikono yake.


Lakini kitu kimoja kilimsitua ni aina ya mtu aliemuona.


Kojo hajawahi kumsahau Honda,alimkariri kimo na mwendo lakini kilichomhakikishia kuwa aliemuona ni Honda ni mkoba uliokuwa ukining’inia mgongoni mwake.


Honda hajawahi kuuacha mkoba ule.


Kojo akajishauri kumfuata ila akajionya mana hakujua kule ndani ameacha balaa gani.


Akaanza kumvizia kwa kujikinga na gari kila alipohisi Honda anataka kugeuka.


Kitu ambacho Kojo hakujua ni kuwa Honda alikuwa ameliona lile gari tangu anaruka ukuta na kutua chini hivyo hata wakati anakawia kutokomea alikuwa anaipigia hesabu ya kuitumia ili awahi anakoenda.


Hivyo alishindwa kuamua lipi la kufanya,atumie miguu ama aibe lile gari.


Akaamua kulifuata.


Wakati Kojo akitaka kumalizia kujikinga na gari ndipo alipomuona Honda akigeuza na kulifuata gari lilipo.


Kojo akaingiwa na kiwewe,uwezo wa Honda aliujua japo hata yeye alijiamini ila alikubali amezidiwa mbinu na Honda hivyo akazidi kujionya ya kuwa akileta mbwembwe tu anakuwa tena chakula cha Honda. Hakutaka kuchekwa na Kizibo japo kwa alivyomjua Honda basi aliamini huko ndani kumeachwa balaa.


Kojo akainama kisha akakiweka vyema kivuli cha Honda na kuachia risasi ambayo ilimnyanyua juu na kumbwaga chini kama kiroba cha mirungi.


Kojo akatabasamu huku akitoka kule alipokuwa amejikinga kwenda kule alipoangukia Honda.


Alienda kumalizia kazi alioianzisha na alipanga kumshushia risasi zote zilizokuwa zimebaki kwenye bastola yake aina ya Revolver colt ya kipolisi.


Honda alinyemelewa na umauti…





Kojo akainama kisha akakiweka vyema kivuli cha Honda na kuachia risasi ambayo ilimnyanyua juu na kumbwaga chini kama kiroba cha mirungi.


Kojo akatabasamu huku akitoka kule alipokuwa amejikinga kwenda kule alipoangukia Honda.


Alienda kumalizia kazi alioianzisha na alipanga kumshushia risasi zote zilizokuwa zimebaki kwenye bastola yake aina ya Revolver colt ya kipolisi.


Honda alinyemelewa na umauti….


Kojo alizidi kumsogelea Honda huku akiwa na imani kabisa ya kuwa adui yake ameipata tamu yake.


Ni hadi alipofika karibu na alipokuwa Honda ndipo alipogundua hesabu zake zilikuwa batili.


Alishangaa Honda akinyanyuka chini kwa mtindo wa sukusi,kisha akamvaa mzima mzima na wakaenda chini wote huku Kojo akitoa kilio cha kuhamanika na uvamizi ule wa gafla.


Honda akadondoka juu ya mwili wa Kojo kisha akaachia makonde manne mfulululizo ambayo mawili yalimwingia Kojo na mawili yalipanguliwa.


Honda alijua mlio wa risasi utakuwa umewasitua mabaradhuli waliokuwa ndani.


Na alikuwa amejeruhiwa juu kidogo ya bega baada ya risasi ya Kojo kumpata eneo hilo.


Hivyo wakati yupo chini akavuta subira ili adui yake asishambulie tena na kumuumiza zaidi na hilo alifanikiwa kwani Kojo hakushambulia akamfuata na kilichomkuta atawasimulia wenzie.


Balaa gani hili Kojo.


Honda akamshindilia teke la tumbo kisha akatokomea kizani huku akilaani kukutana na wale jamaa kila alipoenda.


********


Kizibo na Sajini walitoka mkuku huku wakitazama huku na huko na kitu pekee walichokiona ni Kojo akinyanyuka chini kwa taabu kutoka chini.


Kojo alijilaani kwa kuwa na bahati mbaya ya kukutana na Honda na kilichomuuma zaidi ni kuona Kizibo na Sajini Kebu aliodhani wamepata balaa huko ndani na imekuwa tofauti wanakuja wakiwa wanakimbia kuonesha ni risasi aliopiga ndio imewakurupusha huko ndani.


Akaingiwa na fadhaa huku aibu ikimwelemea kwa kuona anapigika kila mara tofauti na walivyozoea katika kazi zao.


Wa kwanza kufika alipokuwa Kojo ni swahiba wake Kizibo.


“Balaa gani tena komredi!!” alihoji Kizibo huku akifanya jitihada za kumnyanyua kutoka chini.


Sajini Kube alibaki akiangaza huku na huko ili kuhakikisha usalama.


Kojo aliona aibu kusema kapigwa tena na Honda na aliogopa kuonekana mdebwedo mbele ya wenzake.

Akaamua kudanganya bila kujua madhara ya uongo ni makubwa kuliko ukweli wenye kupatiwa ufumbuzi.


“Kuna vibaka hapa wamenivia bana wakataka kunipora ndo nikajitetea aisee”


Jibu hilo likamtia mashaka Kizibo lakini hakutaka kuweka mashaka yake hadharani mana alijua atamkera rafiki yake ama la basi ungezuka ugomvi Kati yake na Sajini.


Nae akabaki na mashaka yake huku akiomba moyoni mjadala wa kufumwa akila chabo chumbani kwa Simbi usianze tena.


Walipanda ndani ya gari na kuondoka huku wakimwacha Simbi asiamini kama ametoka salama kwenye dhahama ile huku akimsifu Honda kwa kutokomea bila kuleta fujo.


Aliwasifu wanaume wa Kitanzania bila kujua limetokea kwa mikakati tu.


****


Honda alirejea nyumbani kwa marehemu Bulembo ambako aliamua kupafanya makazi yake ya muda.


Kama kawaida aliingia kwa njia za panya huku bado akiona utepe wa polisi ukiwa bado upo umezungushwa kwenye nyumba ile.


Alikuwa amejeruhiwa na damu bado ilikuwa ikimtoka hivyo alihitaji kuzuia.


Nyumba ya jasusi siku zote huwa haikosi vifaa vya huduma ya kwanza.


Nyumba ya swahiba wake aliijua,hivyo hakupata tabu kukifikia chumba kilichokuwa na vifaa hivyo.


Alifungua na kuingia ndani yake ambapo alikuta vifaa mbalimbali vya huduma alioihitaji.


Akatumia muda wa saa nzima kuhakikisha jeraha alilopata linapata tiba sahihi kisha akajichoma sindano ya kuondoa maumivu kwa muda wa saa kumi na mbili.


Bado alihitaji kujua ilipo Club X na alijua wa kumpa majibu ni mateka aliemwacha humo ama mwanadada Simbi.


Akatoka kwenye kile chumba na kuelekea kule alikomwacha mateka wake.


Alipoufikia mlango wa chumba alichokuwamo mateka, akashangaa kuona upo wazi wakati aliufunga wakati anatoka.


Akachukua tahadhari.


Akaufungua mlango kisha akasimama pembeni ili kuona kama kuna kitu au mtu atatoka au kushambulia.


Haikuwa hivyo.


Akaamua kuingia kwa mtindo wa aina yake ili kumpoteza yeyote ambae angekuwamo.


Alipofika ndani akajikuta akichunguliana na maiti ya mateka wake aliekuwa amechinjwa bila huruma.


Ni nani mwingine aliejua kuna mtu mle ndani tofauti na Mkurugenzi Papi Mndewa?


Hakupata jibu licha ya kujiuliza maswali mengi sana bila mpangilio.


Honda akiamiani anahujumiwa ila ilikuwa bado mapema kujua anaemhujumu.


Ndani ya nyumba ile hapakuwa mahali salama kwake kuendelea kupaishi,hivyo akaamua kuondoka na kutafuta makazi mengine tena.


Tangu alipomkamata mateka yule hakuwa amemmkagua wala kutaka kujua alibeba nini hivyo akaamua kumpekua harakaharaka.


Punde akakutana na kikaratasi kidogo kilichokuwa na maneno machache tu.


“HOTEL DEKUKU:8:0(88)”


Kikaratasi kile kilikuwa kimeandikwa kwa fumbo maalumu. Hivyo Honda alihitaji kufafanua fumbo lile.


Akatoka ndani ya chumba kile na kuanza kutoka huku akili ikicheza kujua hiyo Hotel Dekuku.


Kuhusu namba haikumsumbua mana 8:0 alijua ni badala ya saa mbili na pia 88 alijua ni chumba cha hotel hiyo ya Dekuku.


Akatoka hadi nje kabisa ya uzio wa nyumba ile ya Bulembo huku akili yake ikicheza kujua lilipo hilo jina la Dekuku ndani ya Kinshasa.


Tangu awe ndani ya Congo hakuwahi kusikia hilo jina la Dekuku.


Akili ikamzunguka,akakumbuka kitu.


Haraka akajipekua ndani ya mifuko yake na kutoka na simu yake aina ya simujanja.

Akafungua sehemu ya kuruhusu kutumia mawasiliano ya mawimbi.


Akaingia kwenye ramani iliokuwa ni moja ya kablasha liloko kwenye simujanja Ile kisha akaingiza neno Dekuku.


Bado haikumletea majibu alioyatarajia.


Akaamua kuacha kupoteza muda zaidi.


Akaendelea na safari huku akijaribu kuvuta kumbukumbu ni wapi amewahi kuliona jina lile.


Akakumbuka!!


Aliwahi kuona kitu kimeandikwa Dekuku na zilikuwa ni sahani za mgahawa ulioko kwenye jengo SAI PLAZA.


Jengo hilo ni lile lililopakana na ofisi za ubalozini ni lile jengo refu lenye hotel kadhaa na migahawa ya kutosha.


Akatabasamu kivivu baada ya kujipongeza kwa hisia zake tangu mwanzo kuhusu jengo lile.


Likabaki swali moja tu ambalo ni muda huo aliotakiwa kuwapo pale ni usiku ama ahsubuhi ama ni muda gani alietakiwa kuwapo awepo?.


Akajiahidi kujua huko huko cha msingi afike chumba namba 88 ndani ya gorofa ya SAI Investment.


Tayari mapambazuko yalikuwa yameanza kuchukua sura ya Dunia.


Kitu ambacho Honda hakujua ni kuwa ahsubuhi ile ilikuwa imaeamka na sura yake kwenye kila gazeti lililotoka siku hiyo tena akituhumiwa kumuua Balozi Ally Sapi na dau nono lilitangazwa kwa atakaesaidia kupatikana kwake.


Mida ya saa tatu na nusu hivi ilimkuta Honda akiingia ndani ya viunga vya SAI PLAZA.


Hakujali macho ya watu yaliokuwa yakimtizama,akafika hadi apokezi na hakwenda kwenye mgahawa wa Dekuku bali alienda kuulizia chumba cha karibu na namba 88 ambapo aliambiwa hakina mtu hivyo akalipia na kupewa kadi ya kufungulia kisha akaelekea huko juu.


Wakati akiwa kwenye chumba cha msaada kinachosafiri kuelekea gorofa ya tatu kuliko chumba hicho alichotaka kupanga,akajiwa na wazo.


“Vipi kama huu ni mtego” alijiwazia baada ya kujiuliza ni vipi kama karatasi ile iliwekwa baada ya kuuwawa yule mtu.


Akapanga kujipa tahadhari.


Alifika hadi kilipokuwa chumba namba 88 na hakujali tena kuhusu chumba alichokuwa amepanga.


Akakuta mlango ukiwa wazi. Akatazama kushoto na kulia hakuona mtu,taratibu na kwa tahadhari kubwa akausukuma mlango na kunyanta huku akiwa na tahadhari ya hali ya juu.


Macho yake yakawa makini upande wa dirishani alikoona kumewekwa bunduki kubwa ya kudungulia aina ya Lapua Magnum rifle.


Akajiuliza.


“Ni imeachwa makusudi au ni mtego?” akazidi kuingiza kiwiliwili ndani.


Mara akajikuta akidakwa na mikono imara iliomvutia kwa kasi ndani na kumbwaga chini ila nae kwa utalamu wake akawahi kusimama.


Ila kwa alichokikuta sicho alichokitegemea.


Wanaume watatu walikuwa wamesimama wakiwa wamenyoosha bastola kumwelekea na mmoja akaupiga mlango teke kwa nyuma ukajifunga.


Wote aliwajua!


Alikuwa ni Kizibo;Kojo na Sajini Kebu.


Kojo alitoa tabasamu baya usoni pake.


Alifurahi kumtia Honda mikononi mwake tena akiwa na usaidizi.


Huko nje nako raia wenye uchu na zawadi walikuwa wamewaarifu polisi uwepo wa Honda eneo lile.


Polisi nao wakawa njiani kumuwahi muuaji Honda.


Pagumu!!


****




Remi alipotoka kituo cha polisi alihitaji sana kuonana na Mwasu lakini pia alihitaji kupumzika walau saa kadhaa baada ya kuwa kwenye heka heka kwa siku kadhaa.


Akajipekua kwenye sidiria aliokuwa amevaa na kutoa kikaratasi kilichokuwa na namba za simu za Malima mtu aliesemekana kuwa na mahusiano na Mwasu.


Kwa msaada wa vijana waliokuwa wamesimama karibu yake,walifanikiwa kupata simu ambayo walimpa Remi.


Remi akampigia Malima.


****


Malima alikuwa ndani kwake akiwa ameshika kiuno huku akitikisa kichwa kushoto kwenda kulia na kulia kwenda kushoto.


Alichanganyikiwa!!


Alikuwa ametumia zaidi ya saa tatu akitafuta nyaraka fulani zilikokuwa kwenye mkoba wake wa kazini bila mafanikio.


Alipekuwa kila pahali bila kupata jawabu la wapi alipoziweka.

Mwanzo alidhani aliziacha ofisini lakini kumbukumbu zake zilimwambia hajawahi kuacha hizo nyaraka kila alipokwenda.


Na alikumbuka vyema kabisa ya kuwa hata wakati yupo msibani,nyaraka zile zilikuwa ndani ya gari hadi wakati aliporuhusu gari limpeleke Mwasu mgahawani kwake Igoma.


Kila alipofikiria ni nani hasa anaeza kuwa amezichukua kati ya dereva na Mwasu; hakupata jibu.


Hakuona kama Mwasu anaeza kuwa amezichukua nyaraka zile muhimu wakati ule ama dereva wake ambae amemwamini zaidi ya miaka mitatu.


Zipo wapi? Hakujua.


Alirudi tena kwenye mkoba na kutazama,alikuta nyaraka zingine zipo kama kawaida isipokuwa zile nyaraka tu.


Akaingiwa na wasiwasi.


Akatamani kumpigia mkubwa wake wa kazi ambae ndie aliempa kazi ya kuzimilisha nyaraka zile baada ya zile za mwanzo kuonekana zinahitaji marekebisho kadhaa.


Mbali ya yote ni kuwa mkubwa wake wa kusanifu majengo alikuwa amemwambia kazi ile ina pesa nyingi sana na pia ni sifa kwa kampuni yao kupata kazi ile ya serikali.


Alichanganyikiwa zaidi baada ya kugundua umuhimu wa kazi ile.


Wakati akiwa amekata tamaa ya kuzipata nyaraka zile ni wakati aliposikia simu yake ikiita kwa fujo.


Akasonya huku akienda kuipokea.


Alikutana na namba ngeni!!


Akapokea!!


"Habari!!" Ikasabahi sauti kavu ya kike.


Malima akasita kujibu huku akijaribu kubahatisha sauti itakuwa ya nani bila kupata majibu.


"Nzuri" akajibu Malima kwa sauti ya kukwaruza.


"Naongea na Malima!!" ikahoji sauti upande wa pili.


"Ndio,nawe nani?" akahoji Malima.


"Naitwa Remi!!" ikajibu sauti upande wa pili.


"Nikusaidie nini usiku huu" akauliza Malima.


"Naomba nielekeze au nipe namba za Mwasu tafadhali!!" akasema Remi.


"Mwasu!!" akashangaa Malima.


Ukapita ukimya wa nusu dakika.


"umepata vipi namba yangu!!" akauliza Malima baada ya kutilia mashaka mtu aliempigia.


"Samahani ndugu mi ni mdogo wake Mwasu; kupata namba nitakweleza siku nyingine ndugu!" akaeleza Remi.


Malima akakaa kimya kidogo kisha akauliza.


"Upo wapi!!?"


"Nipo hapa Soko la Mwendesha!!" akajibu Remi huku akimtizama kijana aliempa simu ambae alitikisa kichwa kuafiki ni sahihi alipotaja.


"Subiri kidogo!!" Malima akasema na kukata simu kisha akampigia Mwasu.


"Nambie mpenzi!!" ilisema sauti ya Mwasu baada ya kupokea simu.


"Samahani kwa kukusumbua usiku!!" alijitetea Malima.


"usiwe na shaka upo huru kunipigia muda wowote ule unaojisikia mpenzi." Mwasu alimtoa wasiwasi Malima.


"Ok! Nimepigiwa simu hapa na binti anaitwa Remi...!" hakumaliza alichotaka kusema akasikia mshituko alioupata Mwasu.


"Wewe unasema nani vile!!" aliuliza Mwasu huku akinyanyuka kitandani alipokuwa amejilaza huku kanga ikimdondoka na kubaki uchi.


Hakujali wala!!


"Remi!!" alijibu Malima na kuzisikia pumzi za Mwasu alizopandisha na kuzishusha kwa mkupuo.


"Kasema yuko wapi saivi!!" aliuliza Mwasu.


"Soko la Mwendesha" alijibu.


"Naomba umwambie anisubiri hapo hapo asitoke lakini pia mwambie namna ya kunipata!" alisema Mwasu huku akikita simu.


Malima akabaki akiitazama simu yake bila kufanya lolote.


Yalimchanganya mambo.


Akabinua mabega yake kuashiria hayamhusu.


Akampigia tena Remi.


Simu ikapokelewa.


"Kanambia umsubiri hapo hapo atakuja kukufuata ila akikawia shuka chini kutoka hapo ulipo ulizia kanisa la wokovu, na ukifika hapo ulizia kwa Bibi Tuku. Sawa!!" akaelekeza Malima.


"sawa" akajibu Remi na Malima akakata Simu.


Malima akakaa kwenye sofa huku akirudi kuwaza zilipo nyaraka za ofisi.


Hakupata usingizi.


*****


Ilikuwa saa, ikatimia hadi lisaa la pili bila kumuona Mwasu ama dalili ya kutokea Mwasu na kutoka pale alipokuwa tayari watu walianza kupungua baada ya usiku kuanza kuwa mkubwa.


Remi alitamani kuondoka pale alipokuwa ili aelekee huko kanisani kumtafuta Mwasu ila akajionya huenda kufanya hivyo kungempelekea Mwasu kumkosa.


Akavuta zaidi subira.


Kwake subira haikuwa heri,muda ulienda bila Mwasu kutokea.


Remi alikuwa amekaa kwenye kibalaza cha duka la kuuza filamu na mbele yake pia kulikuwa na duka lingine la kuuza filamu kifupi eneo lile lilizungukwa na maduka mengi ya kurudufu filamu na muziki.


Duka la tatu kutoka alipokuwa Remi kulikuwa na vijana wawili waliokuwa wamesimama kama hawafahamiani huku mara kwa mara wakimtizima kwa kuibia.


Remi hakutaka kuwatilia mashaka na aina ya utazamaji wao ila wasiwasi wake ulizidi pale ambapo mwenye duka alifunga na wale vijana wakabaki wakiwa wamesimama bila kuonesha jitihada zozote za kuondoka.


Remi aliishi kwa mashaka siku zote hivyo hakutaka kuendelea kukaa pale wakati roho yake haitaki.


Akanyanyuka huku akiwatizama vijana wale ambao nao walinyanyuka na kuanza kumfuata.


Remi aliongeza hatua za miguu yake,vijana nao wakaongeza hatua.


Remi akaingia katikati ya soko pweke lililogubikwa na kiza kizito.


Alipokelewa na kelele za mapaka shume yaliokuwa yanagombania mabaki ya chakula sokoni pale.


Akapiga hatua akiwa na lengo la kupotelea gizani ili kuwapoteza vijana wao ambao alijua dhamira yao.


Hakufika mbali akasikia sauti ikiamuru nyuma yake.


"Simama hivyohivyo!" ilikuwa sauti ya watu iliojaa mamlaka.


Remi akasimama na akageuka na akashuhudia vijana wale wakija mkukumkuku wakiwa wamewasha taa za simu zao.


Lakini hakumuona alieamrisha asimame.


Remi matatani tena!!


**


Vijana wale walimsogelea Remi.


"Tafadhali binti tulia usifanye ujanja wowote!!" alionya mmoja wa vijana wale huku akimsogelea Remi akiwa na bastola mkononi.


Remi akili yake ilifanya kazi harakaharaka bila kupata la kufanya kutoka mikononi mwa vijana wale walioonesha hawana mzaha endapo akiwabugudhi.


Remi akabaki akijiuliza alipo mtu wa tatu ambae alimkoromea na kumfanya asimame na hapo ndipo akafanya akili yake ivute subira kufanya lolote mana hakujua alieamrisha ni upande gani yupo na yupo kwa niaba ipi.


"Huwezi kutukimbia Remi yani wajisumbua tu" alisema kijana mwingine huku akifanya jitihada kuikwepa meza moja ya matunda iliokuwa imewatenganisha.


Remi akapiga hatua moja nyuma ili kujiweka mbali na watu wale lakini jamaa mmoja akamwonya ya kuwa asiendelee kusogea.


"Tulia hivyo hivyo,hatua nyingine nakupasua ubongo wako!!" alikoroma jamaa.


Remi akatulia!!


Jamaa mmoja akamkaribia zaidi huku akiweka simu sikioni kuashiria alihitaji kumpigia mtu wakati huo.


"Tupo nae...ndio..eeh!!" alisema jamaa huku Remi akishindwa kujua walichozungumza.


Punde yule jamaa akampa simu Remi.


Remi akaipokea na kuweka sikioni na kubaki kimya.


"Hatuna shida na wewe endapo ukiwapa hao vijana mzigo wetu na watakwacha uende zako" iliunguruma sauti iliojaa upole wa hali ya juu kana kwamba ni tabibu akisema na mgonjwa wake.


"Najua mtaniua nikiwapa ila.." alikatishwa Remi..


"Kukuua hata sasa vijana wangu wanaweza kukuua ila hatuna nia hiyo kabisa binti!!" ilisihi sauti ile ambayo Remi aliitambua vilivyo.


Remi alijuwa hawawezi kumwacha salama na usalama wake pekee ni kuendelea kuwa na alichonacho mana hata akiwapa bado alishuhudia mengi hivyo ni lazima azibwe mdomo.


Hata!!..


Remi alijakatilia nafsini mwake.


"Haiwezekani niueni tu!" alisema Remi.


Upande wa pili ulikaa kimya kwa muda bila kusema lolote.


"Una hakika unataka kufa Remi!!?" ilihoji sauti upande wa pili.


"Ndio!!" alijibu kimkato Remi.


"Wewe unakufa! Tabibu wako Santina je!?"


Eeh bana eeh!!


Remi alistuka manusura adondoshe simu.


Lilikuwa ni jambo jipya kwake hasa kutajiwa jina la tabibu Santina.


Ndipo alipoamini watu wale kweli wanamkono mrefu.


Akaamua kucheza pata potea!!


"Muueni nae, ila hautakuwa mwisho wa haya mambo" alisema Remi kwa sauti ya kitetemeshi.


Alicheka mtu wa upande wa pili,kisha akasema.


"Chaguo ni la..." sauti haikumalizia likatokea tukio la kustukiza ambapo mlinzi wa soko lile alitokea gafla na kuanza kuita kelele za mwizi huku akipiga filimbi na Remi hakutaka kuipoteza nafasi ile nae akairusha juu simu ile aliokuwa nayo.

Wakati jamaa mwingine akigeuka kumkabili mlinzi, jamaa aliekuwa karibu na Remi akatoa sauti ya hamaniko kwa kitendo kile alichokifanya Remi.


Akajitia mjuzi wa kutaka kuidaka simu yake mpya na ya garama, wakati yupo katikati ya jitihada zake hizo za kuokoa simu ndipo Remi akaachia kifuti kilichompata jamaa yule katikati ya kifua na kumbwaga chini yule jamaa ambae alibaki akitoa miguno kama kahaba aliedhulumiwa haki yake ya kifedhuli.


Jamaa mwingine akashindwa cha kufanya,iwapo amsaidie mwenzie ama amdhibiti mlinzi ambae bado alikuwa anapiga filimbi na kelele za mwizi.


Remi alimsoma vizuri bwana yule wakati anajinyanyua akiwa amepiga magoti.

Remi akamuwahi kwa teke safi lililoenda moja kwa moja kwenye shingo ya jamaa na kumrudisha chini asiamini kama ni Remi aliemtwanga teke lile.


Remi alijua yeye si mjuzi wa ngumi hivyo kuendelea kuwa pale ni kujiweka hatarini zaidi hivyo akaamua kuumwaga huku akijishangaa namna alivyoweza kumdhibiti yule jamaa.


Jamaa mwingine alipoona Remi ameumwaga akaamua nae kumaliza kelele za Mlinzi.

Ambapo alimtandika teke moja la kifua lililokata kelele zote na kumwacha mlinzi akibweka chini kama mbwa koko jalalani.


Akaenda kumnyanyua mwenzie aliekuwa amekaukwa na koo baada ya teke la Remi kumpata sawasawa.


Ikazuka tafrani ndani ya soko huku panya na paka shume wakishindwa kujua Dunia yao imeingiliwa na nini.


Remi alitokomea kwa kupita Mashi hotel kisha akatokezea shule ya Nyakato na kushika njia ya machinjioni.


Kama alidhani vijana wale walimwacha alikosea bado walikuwa nyuma yake haihai.


Kila kichochoro alichopita Remi na wao walipita huku wakiwa makini asiwapotee.


Remi akiwa anakaribia kufikia kiwanda cha pamba mara mbele yake likatokea gari lililowasha taa kali na kummlika usoni.


Akainama chini ili asiumie macho yake na bila kusema lolote kwa kitendo kile japo alijua si salama kwake na alipogeuka nyuma bado vijana wale walikuwa wanamnyemelea huku wakionekana kutokujali kabisa uwepo wa gari lile liliwamulika makusudi.


Remi matatani tena!!




Taa za gari lile ziliendelea kumulika na punde wakashuka watu watatu waliokuwa wamevaa mavazi ya Polisi!!


"Dadeki!!" alijisemea Remi.


Askari wale walipomfikia Remi wala hawakujihqngaisha kuuliza linalomkimbiza wao moja kwa moja wakamdaka!


"Nyie ndo wazururaji tunawatafuta twende...!!" alisema askari mmoja huku akianza kumsukuma bila utaratibu.


Remi akataka kujitete lakini askari mmoja akamkatisha huku akitishia kumtandika makofi.


Remi aliwatizama vijana wale ambao walizidi kusogea huku wakijifanya kama hawana habari na lile lililokuwa linaendelea kwa Remi.


Remi akanyoosha mkono ili aseme kuhusu vijana wale.


"Nitakutia mikwenzi sasa hivi nyau wewe!!" alikoroma askari mmoja huku sasa akimsukuma kwa jaziba.


Remi alipandishwa kwenye karandinga kisha safari ikaanza na ndani ya karandinga kulikuwa na vijana wengine watatu ambao nao inaonekana walikutwa na masaibu kama ya Remi.


Waliitwa wazururaji.


Vijana waliokuwa wakimkimbiza Remi wao walipitiliza na kushuhudia Remi akiwa ndani ya gari la Polisi.


Hilo lingewagarimu na hawakutaka Remi atue mikononi mwa jeshi la Polisi.

Mmoja wao akanyanyua simu yake na kumpigia mtu waliekuwa wamehifadhi jina lake ELCHAPO!!


walitoa taarifa kama ilivyo kisha wakaambiwa wao kazi yao imeishia pale hivyo waendelee na majukumu mengine.


Vijana wakatokemea wanakokujua.


Gari lile la Polisi likiwa na watuhumiwa wa uzururaji,liliendelea kuikata mitaa na kurudi barabara ya Musoma.

Wakiwa wamefika njia panda ya kiwanda cha maji cha AquarRock na Tanesco; ikatokea pikipiki kubwa ambayo hakuna alieitilia shaka na safari ikaendelea huku kukiwa hakuna askari alieitilia shaka pikipiki ile.


Ni hadi gari lilipofika karibu na kiwanda cha samaki cha Nile perch hatua kadhaa kabla ya kuifikia barabara kuu ya Musoma road.

Ni kitendo kilichofanyika kwa weledi wa hali ya juu kutoka kwa mtu aliekuwa juu ya pikipiki.


Kwanza aliongeza mwendo wa pikipiki kama anaehitaji kulipita gari lile,lakini haikuwa hivyo badala yake alipofika karibu na upande waliokuwa askari na watuhumiwa wao akatoa kitu kama kibomu kidogo ambacho aliking'ata na kukitupia nyuma ya gari ambapo kilianza kutoa moshi mzito na kupelekea waliokuwamo kuanza kukohoa mfululizo.

Baada ya yule jamaa kufanya vile aliongeza mwendo zaidi hadi usawa wa dereva ambapo nae alimtupia kibomu kile jambo lilklofanya dereva kukosa mwelekeo huku akiongeza mwendo badala ya kusimama kisha akaenda kuyapamia magari yaliokuwa yamepaki kwa ajili ya kushusha na kupakia samaki.


Kilichofuatia ni ajali mbaya sana.


Gari la Polisi lilinyanyuka juu kisha likajipigiza chini na kurudi tena juu kisha kuanguka na kubiringita mara mbili kisha likatulia huku moshi wa vile vibomu ukitanda angani ukiwa umechanganyikana na vumbi.


Watu walishika vichwa wengine vinywa vyao kwa kutokujua kama kuna aliesalimika kwenye ajali ile.


Jamaa aliekuwa kwenye pikipiki akageuza haraka kurudi ilipokuwa imedondokea gari ile na alipofika akapaki haraka na kuwa kama anataka kutoa msaada kwa watu waliokuwa nyuma ya karandinga ile.


Ila lengo lake halikuwa hilo,lengo lake lilikuwa ni Remi.


Akiwa mzima ama mfu ni lazima ampate!!



******


Mtega nyoka alikuwa ameshazunguka kila kona akijaribu kutazama wapi anaweza kuona ilipo Club D ila hadi inapata kuwa saa tano usiku bado hakuwa amefanikiwa kuiona..


Alichoka na alihitaji kupumzika!!


Alimwelekeza dereva wa bajaji ampeleke Meko darajani kulipokuwa na baa ya Tesha.



Alishuka na kuingia ndani ya baa ile iliokuwa imejaza watu wa kila aina,wengine walikuwa wanaserebuka na wengine walikuwa wamebambiana ili mradi tu kila mtu na furaha yake usiku ule.


Akachagua kiti kimoja kilichokuwa kipo wazi bila kukaliwa na mtu.


Mtega nyoka alipenda sana wanawake ila si wanawake wa kutongoza. Alipenda wahudumu wa baa ama makahaba kwa sababu wanawake wa kawaida huwa haamini usalama wake mana wengine hutumiwa kumfuatilia nyendo zake.


Makahaba ni nadra mana haingekuwa rahisi kujua ni lini na wapi angeingia kuchukua ili ajistareheshe.


Alihisi anakuwa salama zaidi akiishi bila kupenda.

.


Akiwa bado anapepesa macho ili kupata yule ambae angemfaa,mhudumu akamfikia na hakuwa na budi kuagiza kinywaji alichokipenda.


Kuna kitu aligundua!!

.

Tofauti na siku zote ambazo huwa kuna makahaba wengi ndani ya baa ile,ila siku hii hakuona kabisa wingi ule na kila aliekuwepo alikuwa yupo bize na mambo yake huku wengine wakiwa wamekaa watatu ama wawili wawili.


Hakushobokewa kabisa siku hiyo.


Alizidi kuukata tu huku wanawake wakitoka mafungu mafungu na kutokomea huko nje!!



Akaona si vibaya akiuliza.


Akamwita binti mmoja aliekuwa amekaa karibu na yeye!!


"Samahani tunaweza kuwa wote usiku huu?" alihoji Mtega nyoka.


"Unataka kuchetua ama unataka kulala?" alihoji binti yule huku macho yakiwa juu juu kama mkojoa stendi.


"Kulala!!" alijibu Mtega nyoka.


"Babu wee utanikosesha Dolali bure wewe!!" alisema kishambenga yule binti huku akichezesha vidole vyake kwa kuvigusanisha akiashiria pesa.


Mtega nyoka akashituka kidogo kisha akahoji.


"Nakukosesha vipi hizo Dolali wakati nami nakupa pesa utakayo?"


"Aah wee leo kuna midolali haiwezi kuwa kama hivyo visenti vyako labda nikuchetue dakika mbili hapo utoe vinyege vyako hivyo!!" alisema Yule dada huku akitikisa makalio yake kwa kuhamasisha kingono.



"Ooh sawa, vipi hizo Dolali mwazichukua wapi?" alihoji tena Mtega nyoka huku akiwa hajatilia mkazo swali lake.


"Aaah wa wapi wewe!!! Yani hujui huu mwisho wa mwezi Club Dekuku kunakuwa hivi yani..." alisema yule binti huku akimshangaa Mtega nyoka kwa kutokujua kinachoendelea huko Dekuku ambapo alionesha ishara ya kimbea yani kunakuwa moto.


"Dekuku!?" alishangaa Mtega nyoka huku akikaa vyema kwenye kiti chake.


"Ndio!; afu wanipotezea muda mi najiandaa bwana!" alisema yule binti huku akianza kuondoka.


Mtega nyoka akamdaka mkono yule binti ambae aligeuka kwa mshangao wa kitendo kile.


Mtega nyoka ili kumtoa wasiwasi akamwonyesha shilingi elfu kumi na binti akatabasamu kama chatu alieona windo.


"Aaah!! Kitu gani huko kinachowapeleka?!" alihoji Mtega nyoka huku akimpa ile pesa.


"Tunaenda kulala na vijana, ambao hutupa pesa nyingi sana kulingana na huduma utakayompa na vile ataridhika!" alisema yule binti.


"Huwa wanatoka wapi vijana hao"



"hakuna anaejua ila huwa tunafuatwa hapa na gari na kupelekwa huko kila mwisho wa mwezi!"



"unajua ilipo hiyo Dekuku?"


"Hapana huwa tunafungwa vitambaa tukishaingia ndani ya gari!!"


Mtega nyoka alizubaa kidogo huku neno Club D na Dekuku yakipita kichwani mwake kama upepo na asijue kama ni aina moja.


Akakumbuka maneno ya Zana bwana mdogo aliemteka kwenye msiba wakati akimfuatilia Malima.


Mtega nyoka alitoka nje ya Club ile kisha akatafuta sehemu nzuri na kutulia huku lengo likiwa ni kusubiri aone hilo gari.



Haikupita nusu saa gari aina ya kosta likapaki nje ya ile baa na dakika tatu baadae wakatoka mabinti kama saba hivi na kuingia ndani na haikupita dakika wakatoka kule baa wadada wengine kumi akiwemo yule aliekuwa anaongea na Mtega nyoka.


Punde ile gari ikaondoka!


Mtega nyoka haraka akadandia pikipiki na kumwelekeza dereva wake aifuatilie ile gari ambayo ilikuwa inaenda taratibu bila papara.


Ile gari ikawa inazunguka mitaa tofauti tofauti bila kuonesha ni wapi inapoenda.


"Big; mbona tunazunguka tu.." alihoji dereva wa pikipiki.


"Usiogope nitakulipa!!" alidakia Mtega nyoka.



"Sio kunilipa hapa mafuta yanaenda kukata broo!!" alisema dereva huku akiegesha pembeni.


Mtega nyoka akafyonza huku akishuhudia gari ile ikiongeza kasi na kupotea yani ni kama dereva alijua wanafuatiliwa na alitumia nafasi hiyo kutokomea.


Mtega nyoka alibaki akitoa matusi tu bila msaada na eneo walilokuwapo ni eneo pweke ambalo halikuwa na pilika za watu.


Wakageuza na kurudi ili kuokoa mafuta yaliokuwa yamesalia.


Mtega nyoka alilaani sana siku hiyo.


Akaenda kupumzika huku akingoja ahsubuh iliokuja na mambo mengi licha ya kuwa na muda kidogo!!


*****


Shusha utabiri wako tujue kinachofuata!!





Kitu pekee alichokifanya usiku ule,ni kuikariri namba ya gari ile iliokuja kuwachukua makahaba ndani ya baa.


Alipenda sana kuonana na Zana ili ampashe habari za Dekuku; lakini aliamini Zana hawezi kumpa habari mana hakuonekana kujua mengi licha ya kuwa ndie alietumiwa kufuatilia watu waliohitajika nyakati walizohitaji.


Mtega nyoka alirudi D8 sehemu aliokuwa amepanga tangu aingie jijini Mwanza.


Hakupenda alale bila kuwasiliana na Mzee Kinyonga. Alihitaji msaada wa Mzee yule ili aokoe muda katika sakata lile lililojificha.


"Komredi!!" alisema Kinyonga baada ya kupokea simu.


"Bado nipo gizani,nahitaji msaada wako." Alisema Mtega nyoka.



Mzee kinyonga alinyamza kidogo.



"Sina muda,mambo mengi..Nitafutie mmliki wa hii namba T117DHJ" aliuvunja ukimya Mtega nyoka.


"Sasa au badae!!" aliuliza Kinyonga.


"Muda wowote!!" alijibu Mtega nyoka na kukata simu kisha akajitupa kitandani na kuutafuta usingizi.


****


Ahsubuhi Mtega nyoka aliamshwa na muito wa simu. Haraka akakurupuka na kwenda kuipokea.


"Mmiliki wa T117 ni Kasuku Contractors!!" ikasema sauti ya Kinyonga kisha ikakata simu bila kusubiri ama kutoa maelezo zaidi.


Mtega nyoka akabaki anashangaa mambo yale yalivyo.


"Kwanini sasa waliwaua wafanyakazi wake?" alijiuliza Mtega nyoka baada ya kukuta wafanyakazi wawili wa Kasuku Contractors wameuwawa usiku mmoja na pia Malima ambae ndie msanifu mkuu wa majengo wa kampuni ile aliwekewa mtu wa kumfuatilia na sasa gari linalotumika kusafirisha makahaba anaambiwa linamilikiwa na kampuni ya Kasuku.


"Yakoje mambo haya!!" alijiuliza tena bila kupata jibu.


"Malima!!" hilo jina likapita haraka kichwani mwake.


"Aisee yule dogo yupo hatarini!!" alijisemea Mtega nyoka huku akikimbilia makiwatoni kujiswafi haraka ili pilikapilika zianze.


Dakika kumi baadae alikuwa anamalizia kuweka silaha zake mahali alipona panafaa,lengo likiwa ni kumweka Malima kwenye himaya yake ili ajue mbivu na mbichi za kampuni anayofanyia kazi.


Lakini hakujua ya kuwa muda unaweza kukuacha njia panda kama fisi na mialiko ya sherehe mbili kwa wakati mmoja.


..


Pahali fulani ndani ya jiji la Mwanza kulikuwa na kikao cha watu watatu huku wote wakiwa hawajakaa kwenye viti licha ya kuizunguka Meza moja ambayo juu yake kulikuwa kuna karatasi nne zenye mchoro wa jengo fulani.


Watu hawa walikuwa ni Amokachi;Sukuna na Elchapo.


Wote walikuwa ni warefu na wenye miili iliojaa kimazoezi. Na kila mmoja alikuwa na bastola kiuononi, sura zao hazikuwa na furaha kabisa.


"Kwa nini mliwachoma wale mabinti?" aliuliza Elchapo ambae alionekana ndie kiongozi wa kundi lile la watu watatu.


"Kulikuwa hakuna namna kwa taarifa tuliopata ilikuwa ni lazima kuwaua wale mabinti wote!!" alijibu Amokachi.


"Taarifa ilinifikia ikisema kuna mtu anafuatilia lile gari tangu ilipotoka Tesha baa,hivyo basi tukaweka mtego wa kumnasa ila tulipata taarifa mtu yule alirudia njiani na pia tuliarifiwa na mtu wetu pale baa ya kuwa kuna kahaba mmoja alionekana akiongea na mtu mule ndani" alisema Sukuna huku akijikuna kidevu chake.


"nadhani umeona umuhimu wa sisi kufanya vile!!" aliongeza Amokachi.


Elchapo akajikuna utosini kisha akawatazama kila mmoja kwa zamu yake.


"Inabidi lifanyike jambo moja ila itahitaji ushauri wenu kwanza" Elchapo alisema huku akizungusha macho yake kwa wote wawili na alipoona wanasubiri kumsikiliza akaendelea.


"Kuna vimeo lazima viondolewe,tunaanza na afisa usalama barabarani, yule anaweza kuwa kimeo kibaya sana endapo ukifanyika uchunguzi wa kina kuhusu kifo cha Solomoni Bukaba. Lakini pia inabidi na Kindo Seleman nae aondoke!"


Mshangao uliwapata wale jamaa wawili.


"imekaaje hii tena!" aliuliza Amokachi huku sasa mikono yake akiikumbata kifuani pake.


"Jamaa aliekuwa anafuatilia gari,huwezi jua kama alisoma namba za gari na kuzikariri inamana kama akiwa ni mpelelezi hiyo itamfikisha pale Kasuku Contractors na hiyo ni hatari sana kuliko sana!" alifafanua Elchapo ambae katika kundi lao alisifika kwa kuwa na mipango thabiti yenye mafanikio..


Amokachi na Sukuna walitikisa vichwa kukubaliana na wazo lile ila Sukuna akaguna kidogo tena..


"Mh!vipi sasa akiondoka si waona mchoro bado si sahihi huu!!" alisema huku akinyoosha kidole kwenye karatasi zilizokuwa mezani.


"Hapa wa kutupa majibu kamili ni Malima na hawezi kutupa majibu bila kuwa nae stoo,mana ndie alipewa kazi, sasa inaonekana inakuwa michoro miwili ambayo haijakamilika na hawawezi kumpa mchoro ukiwa nusu!" alisema tena Elchapo huku akiugeuzageuza ule mchoro uliokuwa kwenye karatasi nne mezani.


"Duh! Ila hii teka ua, teka ua itawaamsha hawa jamaa na mpango wa miaka kumi utakuwa kazi bure eti." alisema Sukuna huku dhahiri akionesha mashaka yake.


"Usiogope Mr X yupo,atatuliza hali ya hewa na tutamalizia tulipobakiza" alisema tena Elchapo huku akimpiga mgongoni Sukuna.


Waliendelea kuzungumza kuhusu mchoro wa jengo ulioko Mezani kwao.

Wakiwa wameshakubaliana na mambo kadhaa ndipo Amokachi alikumbushia jambo.


"Vipi kuhusu Kasuku!!"


"Nani; Remi ama!!" alihoji Elchapo ili kupata uhakika.



"Ndio" akajibu Amokachi


"Huyo nimeambiwa mipango ipo sawia na muda wowote anatia timu himayani" alijibu Sukuna.


Amokachi alifyonza.


"Pimbi yule atanikoma nikimuona machoni pangu walahi"


Hakuna aliemjibu wote wakakaa kimya kwa muda kisha Elchapo akasema.


" Nadhani tuanze na vimeo vyote,kisha tutamalizia na Malima na Remi!!"


Wote waliafiki kwa vichwa vyao huku kila mmoja akijua kitengo chake kinahusika na lipi.


****


Mtega nyoka alitoka nje ya nyumba ya wageni aliolala huku akiwa hajui yaliondelea.


Akaanza kutembea taratibu tu huku akipishana na watu kadhaa waliokuwa wakiwahi kwenye shuguli zao mbalimbali za kujiingizia kipato.


Macho yake yalivutiwa na kundi la watu lililokuwa likipigana vikumbo kwenye kibanda cha muuza magazeti hatua kadhaa kutoka alipokuwa.



Akataka kupotezea ili awahi anakoenda ila akajikuta tu anashawishika kusogea pale kibandani.


Macho yakanasa vichwa vya habari vya magazeti yaliokuwa yamebandikwa Kwenye wavu.


"MWANZA YANUKA DAMU; BASI LAWAKA MOTO USIKU; USIKU WA BALAA WAACHA SINTOFAHAMU MWANZA; GARI LA POLISI LAUA WATATU....." karibia magazeti yote yalizungumzia matukio yaliotokea Mwanza siku hiyo.


Mtega nyoka akavuta hatua na kumwendea muuza gazeti na akanunua moja na kukaa pembeni kusoma.


Hapo ndipo alipojikuta njia panda.


Ni baada ya kusoma tukio la kuungua kwa gari lenye namba za usajili T117DHJ kisha kuripotiwa kuuwa watu kumi wakiokuwamo.


"Wanapoteza ushahidi nyoka hawa!!" ni baada ya kukumbuka idadi ya makahaba walioondoka na lile gari kuwa walikuwa ni kumi tu na ndio waliopatwa na umauti.


"Dereva yu wapi?" alijiuliza Mtega nyoka huku akifunua ukurasa mwingine, na hapo aliganda kama sanamu bila kupepesa macho kwa zaidi ya dakika moja.


Alikuwa anatazama picha ya binti aliekuwa amechafuka mavazi yake na hakuwa mwingine ni yule yule binti aliekutana nae ndani ya Ofisi za Kasuku Contractors kisha kituo cha polisi na sasa anamuona akiwa amepata ajali na akiwa na polisi.


Aliposoma zaidi akagundua majeruhi wote walikimbizwa hospital kwa matibabu zaidi.


Lakini pia kulikuwa kuna taarifa ya kuungua kwa nyumba ya afisa wa jeshi la polisi Langolango.


Alivutiwa na kumwona Remi ili ajue kipi kinamsibu.


Akapanga kwenda kituo walicholazwa majeruhi wa ajali ile.

.

Lakini akakumbuka jina la Malima.


Wote muhimu, amfuate nani sasa.


Akabaki njia panda.



*****




Zahanati ya Rorya ndio iliowapokea majeruhi wa ajali iliotokea karibu na kiwanda cha samaki cha Nile perch.


Walikufa watu watatu akiwemo ofisa mmoja wa Polisi aliekuwa ndie dereva wa gari ile.


Miongoni mwa majeruhi wale alikuwamo Remi ambae alipata majeraha kichwani na baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili.


Kitu pekee alichokumbuka kukihifadhi ni mkoba wake mdogo ambao alitembea nao kila sehemu.


Alitamani kutoka kwenye kitanda hasa baada ya kukumbuka jinsi alivyonusurika kuangukia mikononi mwa Mwendesha pikipiki.


Na ilikuwa ni kukosea hesabu labda upande wa wabaya wa Remi mana ajali ilitokea hatua mia kutoka kilipo kituo kidogo cha polisi cha Mwatex.


Na kwa kuwa gari lililopata ajali lilikuwa ni la Polisi; haikuchukua lau dakika mbili kabla askari Polisi hawajajaa pale hivyo kufanya mwendesha pikipiki akose lengo lake na kutimka.


Remi mwili haikurusu kabisa kuinuka na kuendelea na shuguli zake.


Akaamua kutulia tu..


Upande mwingine Mtega nyoka bado alikuwa hajapata la kuamua kabisa.


Aliona anahitaji kumpata Malima lakini pia aliona ni vyema akimpata Remi. Wote walikuwa muhimu kwake kwa wakati huo na aliwahitaji.


Akanyanyuka na kuligawa gazeti kwa mtu mwingine kisha akaita pikipiki alihitaji kwenda Kasuku Contractors haraka iwezekanavyo.

.


Haikupita hata dakika kumi akawa amefika zilipo ofisi za Kasuku Contractors.


Alimlipa dereva wa Pikipiki na kuelekea ulipo mlango wa utawala..


Alifika kwa binti aliekuwa amekaa mapokezi..

Hakukaa sana ni baada ya kuelekezwa nyumbani kwa mkurugenzi wa kampuni bwana Kindo Selemani na msanifu mkuu bwana Malima ambao wote hakuwakuta ofisini.


Akachomoka kuwahi ilipokuwa zahanati ya Rorya.


Nusu saa tu ilitosha kumfikisha mbele ya zahanati ile ya Rorya.


Ila alichokuwa amekifuata hakukikuta!!


Eba eeh!!


***


Mwasu alizipata taarifa za Remi kupelekwa kwenye zahanati ya Rorya. Vile alipata taarifa haijulikani ama ni kwa kusoma gazeti ama kwa mtu tofauti!


Alijua yeye!!


Baada ya kukamilisha taratibu za kulipia malipo ya huduma aliopokea Remi; Mwasu akapewa nafasi ya kwenda kuonana na mgonjwa wake ambae alijitambulisha kwenye uongozi wa zahanati kama ni Dada yake.!!


Tabasamu lilijijenga usoni mwa Remi baada ya kuomuona Mwasu na Mwasu nae alijawa na tabasamu lisilosemekana baada ya kumuona Remi.


Ilikuwa ni furaha baina yao!!.


"Nimekutafuta sana Dada yangu!!" alisema Remi baada ya kujaribu kuinuka na kuweza kukaa japo kwa shida kidogo.


"Usijali mdogo wangu,tumekwisha kuonana!!" alisema Mwasu huku akienda kumkumbatia Remi.



Walikumbatiana zaidi ya dakika tatu huku kila mmoja akiwa na hisia zake juu ya mwenzake kisha wakatengana.


Remi alijifuta machozi na kumshuhudia Mwasu nae akifanya vivyo hivyo.


Ilikuwa ni furaha iliochanganyikana na huzuni.


"Pole sana mdogo wangu!!" alisema Mwasu huku akikaa karibu na kitanda cha Remi.


Lakini kwa dakika chache tu Remi alizokaa na Mwasu alitambua mabadiliko makubwa kwenye mwili wa Mwasu.


Hakuwa Mwasu yule waliotengana miaka kadhaa kwenye kambi ya wakimbizi. Mwasu ambae alikuwa legelege na nyama uzembe nyingi.


Huyu alikuwa ni Mwasu alietengeneza mwili wake na kuwa wa kuvutia sana huku nyama zote zikiwa zimekaa pahala sahihi.


Mazoezi yalimjenga.


Remi hakujua ni mazoezi ya kawaida ama ni zaidi ya mazoezi ya kawaida.


Lakini pia Remi aliisikia mikoni imara ya Mwasu wakati wakikumbatiana.


Kwanini!? Hakutaka kujua hilo.


"Ahsante Dada" Hatimae alisema Remi.


"Jana nilipata taarifa zako,ila nilipofika pale nilipoambiwa upo sikukuta, nilihangaika hadi niliposoma gazeti ahsubuhi hii ya kuwa upo hapa na Majeruhi wengine kwenye ile ajali" alisema Remi huku bado akimtizama Remi.


Remi alitizama pembeni,kumbukumbu mbaya ya kilichotokea usiku ule ilimrudia, akajikuta chozi la uchungu linamtoka.


"Usijali mdogo Wangu,pumzika kwanza kisha utanisimulia tu!!" alisema Mwasu huku akimfuta machozi kwa upande wa Kanga aliokuwa amevaa.



Mwasu alitoka kidogo na baada ya dakika kadhaa alirejea.


"Mdogo wangu inabidi hapa tuondoke ukatibiwe sehemu nyingine! Huduma za hapa ni chini ya kiwango" alisema Mwasu.


Remi alishukuru kwa ukarimu wa ndugu yake huyo.


Kwa msaada wa matabibu wawili waliomsaidia kutembea kwa kumshika huku na huku,walifanikiwa kumuingiza ndani ya gari iliokuwa imesimama nje ya uzio wa Zahanati ile.


Wakati gari ile inaondoka pale ni wakati huohuo ambao pikipiki iliombeba Mtega nyoka iliingia ndani ya zahanati ile.


"Dakika chache zilizopita kuna mtu kasema ni Dada yake, amemchukua kwenda kwenye matibabu zaidi" alieleza Tabibu mmoja..


"Kasema ni hospitali gani wataelekea?" aliuliza Mtega nyoka.


"Hapana!!" alijibu Tabibu.


"naombeni kuona taarifa zake huyo aliemchukua mgonjwa!" aliongea kimamlaka Mtega nyoka.



Tabibu alibabaika kidogo! Ila baada ya kukutana na jicho kavu la Mtega nyoka; alitoa kitabu cha wageni.


Mtega Nyoka alisoma vyema namba za simu na mtaa alioishi Dada wa Remi;Mwasu.

.

Akaondoka kurudi Kasuku Contractors.


****


"Ni nani anahusika na usajili wa magari ya kampuni!" alihoji Mtega nyoka punde tu alipofika kwenye meza ya mapokezi.



"Kila kitu hufanywa na mkurugenzi!" alijibu binti aliekuwa mapokezi.



Ndilo jibu alilohitaji Mtega nyoka.


Akapitiliza hadi ofisi iliokuwa imeandikwa "MKURUGENZI" huku nyuma hakuzijali kelele zilizopigwa na dada wa mapokezi aliehitaji aombwe ruhusa y kuelekea huko ofisi za utawala.


Baada ya kugonga mlango na kuruhusiwa kuingia; Mtega nyoka akasukuma mlango na kuingia ndani.



Alikutana na sura ya Mzee wa makamo na kibao kilichokuwa mbele yake kilichokuwa na jina la Kindo Selemani.


"Kilichonileta kwako ni jambo dogo ila linaweza kuchukua muda kidogo kama..." alisema Mtega nyoka ambae alikatishwa na sauti ya majivuno ya Kindo.


"Sema shida yako moja kwa moja kijana tusipotezeane muda"


"Naomba kujua idadi ya gari zinazomilikiwa na kampuni yako tafadhali" alisema Mtega nyoka.



Kindo alishituka baada ya kusikia swali hilo.

Mshituko ambao Mtega nyoka aliuona dhahiri shahiri.


"Wewe ni nani! Polisi?" aliuliza kwa jaziba Kindo.



"Ni polisi ndio na ninayo ruhusa ya kukuhoji kuhusu umiliki wa magari ya kampuni" alisema Mtega nyoka huku akisimama kutoka alipokuwa.


"Unatakiwa kuongea na mwanasheria wa kampuni na si mimi!" alisema Kindo huku akianza kupeleka mkono ilipokuwa simu ya mezani.


Mtega nyoka aliwahi kumzuia.


"Nisingependa tusumbuane kwa jambo dogo hili ndugu!" alisema kwa upole Mtega nyoka.


Kindo akagwaya!


"Tatizo hujui unaongea na nani bwana mdogo nita..." hakumaliza kauli yake akajikuta akipokea bonge la Mkofi, uliomfanya aone shilingishilingi na kufumba macho na alipofungua hakuziona.


"Nisingependa tufike huko unakotaka ndugu" aliongea tena Mtega nyoka.


Kindo alibaki akitetemeka tu.


"Unajua unalofanya litakugarimu kijana" alisema Kindo huku sauti ikimkwama.


"Haya naomba kujua unamiliki magari mangapi" alihoji tena Mtega nyoka.


Kindo akainama kwenye droo na kutoa karatasi moja iliokuwa imenakishiwa na karatasi nyingine kwa juu yake.


Mtega nyoka aliichukua na kuisoma.

Alikutana na orodha ndefu ya magari ya kampuni ile na wanaoyatumia.


Hakuona gari namba T117DHJ.


Sijaona gari lilioungua moto huko Kitangili. Au halimilikiwi na kampuni yako." alihoji Mtega nyoka huku akimtizama usoni Kindo ambae alianza kutokwa jasho jepesi licha ya kuwa na kiyoyozi ndani ya ofisi ile.


"Afu kuna nini huko Dekuku!" alihoji tena Mtega nyoka.


Ilikuwa ni kabla ya jibu likatokea tukio moja matata lililohitaji akili na uwezo kulikwepa.


Mlango ulisukumwa kwa nguvu huku ukifuatiwa na mvumo wa kitu kilichokua kimemlenga katikati ya uti wa mgongo Mtega nyoka ambae bila kujiuliza alijipinda na kuangukia ubavu na kuacha kitu kile kiende kujikita kwenye kifua cha Kindo ambae alitoa mguno wa uchungu.


Kutoka alipoangukia; Mtega nyoka aliona mtu akiingia kwa kasi na bastola mkononi huku akiwa ameziba uso wake kama ninja.


Mtega nyoka nae kwa utalamu akawahi kuinuka pale chini na kutaka kumvaa mvamizi.


Mvamizi nae akaona kitendo kile haraka akarudi nyuma na kumpisha Mtega nyoka kisha akaachia risasi moja ilioenda kutua kwenye paji la uso la Kindo na kisha haraka akamgeukia Mtega nyoka.


Alichelewa!

.

Mvamizi alijikuta akipaa juu na kusukumwa kwa nguvu hadi ukutani na alipotaka kuanguka alijikuta akipokea mateke mengine mawili ya harakaharaka yaliomtia kiwewe.


Akataka kuinuka ajipange zaidi ila hakupewa nafasi na Mtega nyoka; akajikuta akipokea mateke mengine mawili chini ya magoti na kujikuta akitepweta kama aliepigwa na denda na kichaa.


Mvamizi alihusudu uwezo wa Mtega nyoka kwa vile alivyojua kucheza na nafasi alioipata.


Akagwaya!!


Mtega nyoka alijikuta amesimama peke yake baada ya kuona mwenzie aliepambana nae akienda chini bila upinzani zaidi.


Aliona damu ikimwagika.


"*****, what the fuc...!!" alisema mtega nyoka baada ya kuona adui aliechukua uhai wa Kindo nae uhai wake umechukuliwa.


Akabaki amesimama peke yake katikati ya chumba kilichokuwa na maiti mbili.


Haraka haraka akamkagua mvamizi,mfukoni alikuta kadi iliomshangaza kidogo!!


"inakuwaje hii!!"



Hakukuwa na wa kumjibu.



****




Kitambulisho kile alikigeuza huku na huko bila kupata maana ya kile alichokiona.

Kitambulisho kilikuwa kina picha ya Makanisa yaliojengwa pamoja huku milango ikiwa inajitegemea na kila mlango ulikuwa na msalaba juu yake!


"Ina maana gani hii!!" Mtega nyoka alijiuliza bila kupata majibu sahihi.


Haraka akatoka ndani ya ofisi ile na kuelekea mapokezi kisha akatimka kutoka ndani ya Kasuku Contractors.


Haraka akadandia pikipiki iliokuwa inashusha abiria ndani ya buzuruga plaza.


Lengo lilikuwa ni kuwahi ilipo Kanisa ya wokovu kama ananuani ya Mwasu ilivyoonesha.

.


Alipanga kumuwahi Remi.


*****


Mwasu na Remi walifika salama ndani ya makazi ya Remi. Hii ilikuwa ni tofauti na maelezo aliyopewa ya kuwa anaenda kutibiwa kwenye kituo kikubwa cha matibabu.


"Usijali mdogo wangu,nitakupeleka hospitali kisha tutarudi tena hapa na utakuwa ukitibiwa hapa hapa." Mwasu alimtoa wasiwasi Remi.


Remi hakuwa na usemi alibaki mtazamaji.


Ndani ya nyumba ya Mwasu kulikuwa kuna mtu mwingine na walipoonana na Remi wote hawakutambuana.


Alikuwa ni Malima.


Malima alifika nyumbani kwa Mwasu ili atafute nyaraka alizopoteza kwa kuhisi huenda aliwahi kuziacha pale.


Na sasa ilikuwa imepita saa nzima huku akiwa amepekua kila pahali bila kuona alichokihitaji.


Malima hakumtabua Remi kabisa licha ya kuongea usiku wa siku iliopita.


Malima alishangaa kidogo kisha akahoji.


"Kabla hata sijajua mnaendeleaje,nadhani huyu mgeni hakustahili kuwapo hapa, alitakiwa awe anapewa matibabu sasa hivi"


Mwasu hakumjibu badala yake alikuwa anafanya jitihada za kumkaliza Remi kwenye sofa.


"Hauna pesa ya matibabu nikupe?" aliendelea kuhoji Malima.


"Pesa ninayo ila nina sababu zangu za kumleta hapa kwanza." alijibu Mwasu.


"Sababu gani kwa mtu alieumia kiasi hiki?" alimaka Malima.


"Unataka kuijua?!" alihoji Mwasu huku akimtizama Malima usoni bila kupepesa macho yake.


"Sina shida ya kuijua Mwasu; zaidi ya afya ya huyu binti kuzingatiwa, akifia hapa je!!" alisema Malima huku akitanabaisha wasiwasi wake.


Mwasu akitikisa kichwa tu huku akielelea chumbani kwake ambako alikuta kumevurugwa vya kutosha.


Mwasu alitabasamu!!


Alijua nini Malima alitafuta.


Dakika tatu badae Mwasu aliungana na Remi sebuleni huku wakimwomba Malima awapishe kidogo.


Hakuuliza akatoka kwenda kibalazani.


"Ni nini kimekukuta Remi!!" alisema Mwasu huku akikaa kwenye sofa lililokuwa kando ya sofa alilokalia Remi.


Remi alikaa kimya kidogo kisha akasema;


"Tangu tulipoachana pale kambini, kulitokea sintofahamu kadhaa hivi ambazo inasemekana zilianza kuwapo hata wakati upo..." alinyamaza Remi baada ya kujikuta roho yake inakuwa nzito kuendelea kuzungumza.


Hata yeye mwenyewe hakujua ni kwanini.


"Aah nitakweleza siku nyingine Dada!!" alisema Remi huku akishika kichwa kuashiria hajisikii vizuri.


"Ooh pole sana!!" alisema Mwasu huku akinyanyuka na kwenda kumshika kichwa Remi kwa kutumia mgongo wa kiganja chake.


***


Malima aliendelea kuwaza ni vipi atamwambia mkurugenzi wake kuhusu upotevu wa nyaraka za jengo muhimu sana.


Alijikuna kichwa akiwa haelewi ni lipi afanye.


Malima kila alipofikiria bado akili yake ilimpa kumbukumbu ya mwisho ni Mwasu alieondoka na gari huku kukiwa na nyaraka.


"Ziko wapi!!" Malima alijigonga kichwa huku akishindwa kabisa kuchanganua mambo yalivyo kuhusu nyaraka zile.


Kama ni akili kugoma,basi za Malima ziliamua kusimama kabisa kutatua kitendawili kile.


Alihofu!!


Alihofia kazi yake kupotea.


****


Mwasu bado walikuwa wamekaa wanazungumza mambo mbalimbali ya huko nyuma na jinsi walivyotokea kushibana pindi walipokuwa pamoja.


"Dada hakuna aliekushitukia kwamba wewe ni mgeni hapa jijini?" alihoji Remi.


"unajua mdogo wangu, Tanzania sio kama nchi zingine. Ni ngumu sana mgeni kuulizwa ukazi wake, hivyo nilipofika hapa wala hakuna aliehangaika kujua ubini wangu,hivyo nami sasa ni Mtanzania." alijibu Mwasu.


"Mh!! vipi sasa ukishitukiwa?" alihoji tena Remi.


Mwasu aliachia cheko dogo huku akijifuta midomo kwa kiganja cha mkono wa kulia.


"Ni ngumu sana mdogo wangu,nimeshakuwa Mtanzania kabisa sasa,najua lugha yao na ninajua tamaduni zao,hivyo si rahisi kabisa" alijibu Mwasu.


Remi aliguna tu.


"kwanini hujiulizi kuhusu wewe Remi!!" alihoji Mwasu.


"Basi tu imenibidi na ni bora nikamatwe!" alijibu bila shaka yoyote Remi.


Mwasu akatafakari kwa kauli ile kisha akahoji tena.


"Kwanini ulikuja huku?"


Remi alibabaika kidogo kujibu huku akijiuliza kama ni sahihi kwake kumwambia yaliomsibu dada yake huyo wa hiyari.


"Mmh nadhani kwa sasa ningepona kwanza halafu tutazungumza kwa kina kabisa hili suala." alisema Remi.


Mwasu akapandisha mabega kisha akatazama saa yake na kutaka kunyanyuka ila Remi akauliza swali.


"Hivi Amokachi nae nilisikia kalowea huku,mliwahi onana?"


Lilikuwa swali la mtego ambao Mwasu hakujua autegue vipi. Akababaika kidogo kisha akageuka na kumjibu.



"Nadhani hana hata mawasiliano yangu,hivyo ni ngumu kuonana. Mwanza kubwa hii!!"


Remi akatikisa kichwa kukubali bila kuongeza neno.


"aah hujala bado,ngoja niandae chakula ule na shemeji yako!!" alisema Mwasu huku akielekea upande wa jiko lililokuwa ndani ya nyumba ile.


Remi alibaki na maswali kadhaa baada ya kubaki peke yake.


Siku anaingia Mwanza na kuelekea Igoma alikoambiwa ni ofisini kwa Mwasu; macho yake mwenyewe yalimuona Amokachi na Mwasu wakiteta jambo na ndio sababu yeye akatimua mbio ili asiingie mikononi mwa Amokachi anaemtafuta kwa udi na Uvumba.


Sasa alishangaa Mwasu kumwambia hawajawahi kuonana.


Utata!!


Jambo lingine ni vile alivyoona maisha safi ya Mwasu ambayo ni tofauti na kazi anayofanya ya umama ntilie hadi watu wakamwita Mama Ujazo.


Hapo akamfikilia Malima ambae anaeza kuwa ndie mtu aliempangia Mwasu.


Hapo napo akabaki njia panda.


Remi akabaki na fumbo.


***


Nje bado mawazo yalimzonga Malima akabaki amejiinamia tu bila kufanya lolote huku mara kwa mara akichorachora chini bila kujua alichokichora.


Mara akaona kiatu kikubwa(Buti) kikisimama miguuni pake.


Malima akanyanyua uso wake ili aone mmiliki wa buti ile ya jeshi.


Alishuhudia mwanaume mwembamba mrefu aliejenga kimazoezi akiwa amesimama akimtizama yeye.


Kwa utazamaji ule; Malima akagwaya.


"Simama!!" Malima aliamriwa kwa sauti kavu.


Akatii!!


"Haya geuka rudi ndani!!" aliamrisha tena yule mtu.


"Kiongozi tungetambuana kwa..." Malima alitaka kujitetea akaishia njiani baada ya kuona bastola ikimwangalia.


Malima alishikwa na tumbo la kuhara gafla huku akishindwa hata kupiga kelele.


Akajikuta akinyanyua mikono juu kusalimu amri huku akigeuka na kuelekea ndani.


Kule ndani Remi alipitisha wazo moja tu.


Alihitaji kutoroka pale!!


Akajaribu kusimama bado hakuwa na utimamu sawia.


Akajaribu tena.


Mara hii akaweza kusimama na akaanza kupiga hatua ili afike mlangoni.


Wala hakumalizia hatua zote mbili akajikuta akiingiwa na ubaridi wa gafla baada ya kuona Malima akiingia huku akiwa amenyoosha mikono na nyuma yake kukiwa na mtu alieshika bastola.


"Amokachi!!?" alijikuta akitamka bila kupenda..


"Ulidhani unaweza kukimbia kuliko mimi Remi!!?" alihoji amokachi huku akimalizikia kuingia ndani.


Muda huohuo Remi alimshuhudia Mwasu akitokea kule jikoni akiwa hana wasiwasi na kile alichokiona pale sebuleni.


"Kazi nzuri Mwasu; Pimbi wote wamenaswa" alisema Amokachi huku akitabasamu.


Mwasu nae alitabasamu huku akienda haraka na kuuchukua mkoba aliokuwa nao Remi na kuufungua.


Hola!!


Haukuwa na kitu ndani yake! Ulikuwa tupu.


"Viko wapi ulivyochukua?" alikoroma Mwasu huku akiukunguta mkoba ule bila mafanikio zaidi ilidondoka pedi moja tu.


Amokachi na Mwasu walibaki wamepigwa na butwaa.


"Hii ndio sababu ya kumleta mgonjwa hapa!?" alihoji Malima huku akitetemeka.


Mwasu alicheka kidogo.


"Ningeshangaa kama usingeikumbuka hii sababu!!" alijibu Mwasu.


"Niacheni mana nadhani sihusiki!!" alijitetea Malima.


Amokachi alicheka kwa kebehi.


"Yani ungejua wala usingejisumbua kujitetea kunguni wewe!!" alisema Amokachi.


Malima akapigwa na butwaa. Anaingiaje kwenye mkasa asiojua?


Jibu halikukawia!!


"Ramani sahihi iko wapi?" alihoji tena Amokachi.


Malima alitoa macho kwa mshangao kama changudoa aliedondosha simu yenye namba muhimu.


"Hata mimi naitafuta,tena wewe unai..." Malima alikatishwa na mluzi uliopigwa na Mwasu.


Punde wakaingia vijana wengine wawili ambao waliwaziba midomo kwa vitambaa fulani na punde Remi na Malima walijikuta hawana fahamu.


Walibebwa kama mizoga.


Majibu wangeenda kuyatoa huko huko wanakopelekwa.



*****





****


Solomoni Bukaba alibaki akiwa hana la kufanya licha ya kuzidi kuzibana pumzi ili asiendelee kuvuta hewa nzito ya moshi.


Alijikakamua licha ya mwili wake kutokuwa na nguvu za kutosha kufanya vile ila ilikuwa ni lazima ajiokoe la sivyo maisha yake yangelifika tamati siku hiyo.


Akarudi kulala tena baada ya kugongwa na ubao uliotoka juu ya paa la nyumba.


Kuna sehemu alihitaji kuifikia na ilikuwa mita mbili tu kutoka alipo.


Alijivuta tena licha ya kuwa na udhaifu uliokithiri.

Akajivuta hadi alipopafikia alipopahitaji.


Akalala na kutulia eneo lile na taratibu akaanza kuzama kwenda chini na upande wa zulia aliokuwa amelalia juu yake.


Alizama kabisa hadi alipoikuta chemba ya maji machafu iliokuwa inatiririsha maji yake bondeni mabatini.


Akatulia bila kufanya jitihada zozote kujiokoa ndani ya maji yale yaliokuwa yanatiririka kwa kasi ya ajabu.


Solomoni alijua ni wapi maji yale yangemfikisha.


Akabana pumzi ili zimsaidie kufika salama huku moyoni akishukuru idara yake kumweka kwenye nyumba kama ile.


Haikuchua dakika tano mdomo wa bomba la maji machafu ulimtupa binadamu kwenye mto uliokuwa unatiririsha maji kuelekea ziwa Victoria(Zamani Nyanza).


Alipondondoka hakutaka kusombwa na maji hadi ziwani ila alifanya jitihada kidogo kujinasua kutoka kwenye mkondo wa maji na kujitupa pembeni kidogo.


Alijua watesi wake walitaka afie ndani ya nyumba yake ila mungu alikuwa upande wake.


Alisimama kwa tabu kidogo huku jeraha la risasi likimuuma na kichwa pia kilimuuma kwa kutokwa na damu nyingi.


Alijiinua na kujikokota akatoka bondeni huku akili yake ikimuwaza mwanamke wa kinyarwanda akietokea kumpenda sana.


Sundi!!


Aliwaza sehemu pekee yenye usalama kwake ni nyumbani kwa mpenzi wake Sundi.


Makazi yake hayakuwa mbali sana na kwake.


Sundi aliishi karibu na kiwanda cha kusaga mifupa.


***


Sundi hakuwa amepata usingizi,kuna kitu kiliisumbua roho yake usiku ule na kila alipojaribu kulala alijikuta akijiwa na ndoto za ajabu ajabu.


Sundi alikuwa na taaluma ya utabibu hivyo ndani kwake hakukosekana dawa na baadhi ya vifaa kwa ajili ya kazi yake hiyo endapo kungelitokea dharura yoyote.


Alinyanyuka kutoka kitandani alipokuwa amejilaza na kuelekea kwenye chumba alichokifanya kama ni stoo ya vifaa tiba vyake.


Huko akachukua dawa za usingizi na kumeza kisha akatulia kwenye kiti kilichokuwamo mle.


Bado mawazo yalimwandama.


"Yeye hakutarajia! Hata mimi sikutarajia ni bahati mbaya tu" alijisemea huku akijifunga kanga yake vizuri kuzungushia kifuani.


Akapiga hatua kadhaa na kuelekea chumbani kwake.


Hakika Sundi hakuwa sawa kabisa.


Kwanini!!


Hakuna aliejua!!


Akiwa anakaribia kusombwa na usingizi wa dawa,kengele ya mlangoni ikalia.


Akashituka kisha akatazama ukutani.


Ilisomeka saa ni saa tisa na nusu alfajiri.


Nani tena!! Alijiuliza bila kupata jibu.


Kengele ikalia tena.


Akasita kunyanyuka mana alikuwa na miadi na mtu saa kumi na moja ila si saa tisa usiku.


Alijiwazia kama kuna mpenzi wake yeyote aliewahi kumgongea usiku mkubwa kama huo.


Hakupata kuwapo!!


Akanyanyuka akavaa suruali harakaharaka bila hata kuvaa chupi kisha akaokota fulana nyeusi iliokuwa imedondoka chini akaivaa.


Akajitizama baada ya kuivaa fulana ile.


Ilimjia sura ya mahabuba wake Solomoni Bukaba.


Akatabasamu!!


Akavaa raba zake harakaharaka na kuelekea mlangoni ambapo alifungua na kuelekea geti la nje ambalo ndiko kengele ilitokea.


Alifungua!


Kwanza aliruka nyuma kwa uwoga huku akitoa kilio cha woga kwa kile alichokiona.


Alikutana na sura ya Solomoni iliochakaa na kuchafuka huku akiwa na majeraha hapa na pale mwilini mwake.


Solomoni Bukaba alibaki akiwa amezubaa mlangoni huku akishindwa kuelewa mshituko ule uliompata Sundi ni kwa kumuona alivyo ama kuna lingine.


Hakuwa na nguvu za kuwaza zaidi!


"Nipe msaada tafadhali" alisema Solomoni huku akijiegemeza kwenye geti lililoshindwa kuhimili uzito wake na kurudi nae ndani kisha likambwaga chini baada ya kukosa mhimili katika mwili wake na geti kuteleza.


Sundi alibaki akiwa amesimama huku amejishika mdomo kwa mshangao.


Kuna mawazo fulani yalikuwa yanakinzana kichwani kwake na hakujua afuate lipi kwa wakati huo.


Nguvu ya mapenzi ikamwelemea!!


Akamvaa Solomoni pale chini kisha akamnyanyua na kumkokota hadi kwenye chumba maalumu kilichokuwa kinatumika kama stoo ya vifaa tiba vyake.


Huko harakaharaka akamlaza kwenye kitanda na kumvua nguo zote ambazo zilikuwa zinanuka sana kisha akawasha taa maalumu na kuanza kumsafisha mwili kwa dawa maalumu kisha akaanza jitihada za kumtoa risasi na alipomaliza alimsafisha sehemu aliokuwa amechomwa kisu na kupashona.


Pale ndani alikuwa na akiba ya chupa tatu za damu salama.


Akachukua moja na kumtundikia Solomoni ambae hadi wakati huo alikuwa yu hoi sana na kichwa kilimgonga sana.


Licha ya udhaifu wa mwili ila kichwani bado swali lilibaki moja kuhusu Sundi.


Ni kweli yeye ni tabibu wa hospital kubwa tu jijini Mwanza ila haimaanishi ndio awe na hospital yake ndogo hapo nyumbani. Lakini pia alijiuliza kuhusu chumba walichokuwamo ambacho hakuwahi kuingia licha ya kuwa na mahusiano kwa muda murefu sana na Sundi.


Sawa vifaa tiba kwa tabibu ni muhimu kwa dharura ila sio kuwa hadi na damu ya akiba.


Huwa anamtibu nani sasa!?


Majambazi yanamtumia!!?


Hakukuwa na wa kumjibu maswali yake.


Solomoni alipitiwa na usingizi baada ya kuchomwa sindano ya usingizi na tabibu wake Sundi.


Sundi alibaki akimtizama Somolomon huku akitikisa kichwa.


Akachukua simu akatafuta jina fulani akataka kulipiga ila wazo lingine lilikataa!!.


Alijikuta chozi la huruma linamdondoka.


Alitamani kufanya vitu viwili kwa wakati mmoja.


Sundi akajikuta njia panda.


Akatazama saa yake kwenye simu ilionesha ni saa kumi na moja na dakika ishirini zilisalia dakika chache tu kabla hajaonana na mtu mwingine pale ndani.


Kizungumkuti!!



****



Sundi alikaa karibu na Solomoni ambae alikuwa ametopea kwenye usingizi mzito.


Sundi alikuwa bado anaitazama simu yake huku akiwa hana maamuzi sahihi ya nini anatakiwa kufanya wakati ule.


Kuna jambo lilikuwa linamsumbua moyoni mwake hasa alipomtizama Solomoni na majeraha yake mwilini.


Sundi akiwa bado ametopea kwenye lindi la mawazo,kengele ya mlangoni ikalia.


Sundi akavuta pumzi ndefu na kuzishusha kwa mkupuo kisha akasimama na kuzishusha pazia kuzunguka kitanda alichokuwa amelalia Solomoni.


Sundi akaenda kufungua mlango huku akihakikisha hakuna ambae angeweza kujua kama kuna mtu kalala kwenye kitanda kile.


Baada ya dakika kadhaa Sundi akarejea ndani ya chumba kile kile akiwa na mtu mmoja mrefu mwembamba aliejengeka vyema kimazoezi na kuelekea kuficha wembamba wake!!


"Tena kimetokea mbona jeraha!!" alihoji Sundi bada ya mtu aliekuwa akimtegemea kuingia akiwa na jeraha kubwa karibu na mguu!!


"aah ni harakati tu si wajua!!" alijibu yule mtu.


Ulipita ukimya wa dakika kadhaa huku Sundi akishika hiki na kile kuhakikisha anapata vifaa tiba sahihi kwa kumtibu yule bwana jeraha lake.


"inabidi ujikaze sitatumia ganzi!!" alisema Sundi huku akiinama ili kulitazama vyema jeraha.


"Ohoo kwa hiyo ndo kunikomoa au!!" alihoji yule bwana.


"Nope!!" alijibu Sundi huku akimwaga dawa ya kutoa wadudu nyemelezi kwenye vidonda..


Bwana yule akagumia kwa uchungu.


Dakika thelathini badae; Sundi alikuwa anamalizia kufunga bandeji kwenye jeraha la bwana yule.



Muda wote kulikuwa kimya kabisa.



"Kwa hapa hali ilivyo tunahitaji msaada wako wa hali na mali Sundi!!" alisema yule bwana.


Sundi akatazama kule kulipokuwa na mapazia meupe!


Alimwonesha ishara mtu yule ya kuwa watoke wakaongelee sebuleni.


Bwana yule wala hakuwa mbishi,alimwamini Sundi.


Walitoka na kuelekea sebuleni.


"Kuna nini tena!!" akihoji Sundi baada ya wote wawili kukaa kwenye sofa za kutazamana.


"X anaumwa sana na anahitaji matibabu zaidi ili kuokoa uhai wake." alisema yule bwana.

.


Sundi akaguna.


"sasa msaada wangu ni nini ikiwa sura tu ni ngumu kumuona?" alihoji Sundi.


"Kwa ilipofika ni ngumu tena kukwepa kuonekana ni lazima aonekane ili asaidiwe" alisema yule bwana.


"Sawa!! Lakini tatizo ni nini?" alihoji tena Sundi..


"Anakansa ya ngozi,inaonekana upasuaji wa ngozi aliofanya mara ya mwisho ndio umemharibu kiasi kile" alifafanua yule bwana.


Sundi aliguna tena.


"Sasa mpango utakuwaje kama yupo koma huyo bwana!" alihoji tena Sundi..



"Mpango ni mrefu!! Na umechukua watu warefu pia hivyo upo pale pale na ni lazima ufanikiwe japo bado tunakwamishwa na jambo moja tu!!" alisema yule bwana.



"Jambo gani tena!!" alihoji Sundi huku akikaa vyema sofani.


"Ramani haijapatikana bado na ili mambo yaende sawa ni lazima ramani ipatikane ili tuwe sawa siku husika!!" alisema yule bwana.



"ooh ok sawa,sasa mimi msaada wangu zaidi ni upi?" Sundi alihoji.


"ni kumpa huduma ya haraka zaidi ili tupange utaratibu wa kumsafirisha kwa matibabu zaidi" alijibu yule bwana.

.

"Sawa" alijibu Sundi.


"Vipi jana mlimaliza ule mwanya?" alihoji yule bwana.


Sundi akibabaika kidogo kisha akajibu.


"Yah! Kwani hujasoma hata gazeti?"


"Mambo mengi muda kidogo" alijibu yule bwana.


Sundi akanyanyuka kisha akaelekea chumbani kwake na baada ya dakika kumi alitoka akiwa amevaa vyema suruali nyeusi na fulana nyeusi na raba nyeusi.


Alipendeza kumtazama!!


Alipokwisha kufika sebuleni akamuomba yule mtu waongozane kutoka nje!!


Walitoka pamoja huku nyuma waliacha nyumba ikiwa na mtu ambae alimjua Sundi pekee.


***


Yawezekana Sundi hakuona vyema aina ya dawa ya usingizi aliomchoma Solomoni.


Alikuwa na hakika asilimia mia ya kuwa alimchoma Solomoni dawa ya kulala zaidi ya saa tatu.


Sivyo!


Alikuwa amechukua kichupa chenye dawa ya kumlaza usingizi mgonjwa dakika arobaini na tano tu!


Ilikuwa ni bahati mbaya iliomgarimu yeye na wenzie wote.


Lakini Pia ilikuwa bahati mbaya ile imebebwa na nguvu ya mapenzi ndani yake.


Solomoni alikuwa ameamka bado wakiwa wako ndani ya chumba kile cha kitabibu na maongezi aliyasikia.


Hata wakati wanatoka kwenda kuongelea sebuleni, bado yeye alinyata hadi mlangoni na kutega sikio lake vyema na kuyasikia maongezi ya Sundi na mtu yule.


Japo maongezi yao yalitawaliwa na mafumbo mengi ila yalimwachia alama ya kiulizo kichwani mwake.


X!

Ninani mtu huyo? Mgonjwa! Kwanini haendi hospitali anatibiwa kienyeji uchochoroni?


Yalikuwa ni maswali bila majibu.


Lakini Sundi ni nani hasa!!


Solomoni alianza kuingiwa na wasiwasi na mienendo ya Sundi.


Akapanga kufanya jambo.


Wakati Sundi na yule bwana wanaondoka kuelekea huko kusiko julikana,huku nyuma Solomoni hakujali maumivu alionayo.


Haraka akafungua mlango na kutoka hadi sebuleni,akaangaza huku na huko akaona nguo zikiwa zimetundikwa kwenye enga.


Zilikuww ni za kike! Akaziendea ila akasita baada ya kuona vile zimewekwa kimitego afu akaona ajabu nguo kuwekwa sebuleni.


Hakuzichukua!!.

.

Akaelekea chumbani kwa Sundi huko akaingia kwenye kapu la nguo chafu na kuchagua hijabu jeusi akalitinga kisha akajitazama kwenye kioo.


"*****! Leo naeza tongozwa huko!" kisha akacheka peke yake na kuondoka kuharakisha kuwahi Sundi na mtu wake wasije wakampotea!!



Bahati ilikuwa upande wake kwani wakati anaruka uzio na kudondoka nje na hijabu lake ni wakati huo aliliona gari likitoka mitaa ile.


Hakuwa na usafiri ila alijua barabarani atakuta usafiri hivyo haraka sana akawahi kukata uchochoro ambao alijua utawahi kumfikisha barabarani kabla ya gari ile haijafika.


Ndivyo ilivyokuwa.


Akasimamisha pikipiki na kumwomba dereva asubiri kidogo.


Dakika chache badae ile gari ikapita kwa mwendo wa kawaida tu.


Solomoni akaagiza dereva wa pikipiki aipite gari ile awe mbele yake.


Dereva akatii bila kushitukia sauti nzito ya kike ya abiria wake!


Ulikuwa ni mwendo wa dakika arobaini na tano hadi Solomoni alipoona lile gari likisimama yalipokuwa makanisa manne.


Eneo hili la makanisa manne ni eneo maarufu sana kulingana na aina ya makanisa yaliopo.


Lakini eneo hilo lilipewa umaarufu zaidi na kanisa la Efather!

Huku makinisa mengine matatu yaliojengwa kama jengo moja yakiwa hayajulikani ni dhehebu gani licha ya watu kusali kila jumapili kwenye mlango wa kanisa moja huku milango miwili ikiwa haijawahi kutumika kabisa kuingiza waumini.


Siku hiyo hakukuwa na ibada ila kulikuwa kuna magari mengi kidogo yaliongia na kutoka, mengine yakishusha na mengine yakipakia.


Kama ungeliona basi ungejua pale kuna kikao cha viongozi wa makanisa mana wakishuka watu waliovaa mavazi kama ya makasisi na wengine kama mapadiri wengine kama watawa wa kike na kiume.


Kilichokuwa kikiendelea huko hakuna aliejua!!


Sundi alishuka kwenye gari na mtu yule aliemfuata!.


Wakaongozana kuingia huko ndani.


Solomoni kutoka alipokuwa alijifanya kuendelea na shuguli zake kwa kumfuata muuza genge na kununu ndizi kisha akaondoka eneo lile. Huku akitizama kwa makini mambo yaliokuwa yakiendelea pale.


Solomoni alielekea karibu na kanisa la Efather ambalo wakati huo lilikuwa limefungwa!


Alienda sehemu kulikokuwa na makazi ya watu akatulia na kuangalia kilichokuwa kikiendelea kule.


Wakati akiwa bado anashangaa hili na lile akaona kuna mtu mwingine nae akiingia pale huku mbele yake kukiwa na gari jeupe kama la kubebea wagonjwa.


Gari lile halikusimama mbele kama mengine ila lilielekea upande wa pili kulikokuwa na geti na kuingia huko.


Yule mtu aliekuwa nyuma ya gari lile la wagonjwa hakuigia na gari lile badala yake alipitiliza na kwenda usawa wa geti la kuingilia nyumbani kwa mchungaji wa kanisa la Efather.


Macho ya solomoni yaliona yote yale.


Solomoni alimtilia shaka bwana yule alieelekea nyumbani kwa mchungaji.


Alitabasamu!!


Kumbukumbu zilimwambia aliwahi kumuona mtu yule akitoka ofisini kwa OCD siku alipopewa karatasi za ajabu ambazo nusura zimtoe roho.


Alimwona mtega nyoka!!





***


Mtega nyoka hakuwa mbali na nyumba ya Mwasu ila alishindwa kuingia baada ya kuona tukio fulani akiwa hatua chache kutoka ilipokuwa nyumba ile.


Alikuwa na mwenyeji wake aliemwongoza pale.


Mwenyeji alimwonesha tu wakiwa mbali nyumba ya Mwasu.


Ni wakati akipiga hatua fupifupi ndipo alipoona watu wawili kibalazani.


Mmoja alikuwa amesimama na mwingine amekaa.


Aliekuwa amesimama alikuwa na wajihi sawa na mtu aliepambana nae Buzuruga Plaza siku kadhaa nyuma.


Mtu aliekuwa amesimama alimwona alivyochomoa bastola yake kutoka kiunoni kwa kasi ya ajabu na kumwelekeza jambo mtu aliekuwa amekaa.


Mtu aliekuwa amekaa wakati anasimama ndipo mtega nyoka alipomuona vyema.


Alikuwa ni Malima.


"Kumekucha!!" alijisemea Mtega nyoka..


Alijibanza nyuma ya nyumba iliokuwa jirani.



Haukupita muda mrefu aliona wakitokea vijana wengine wawili na kuingia ndani.


Zilipita dakika tatu ndipo alipoona watu watano wakitoka ndani huku wawili wakiwa ni Malima na Remi.

Na wengine ni mtu mrefu waliepambana Buzuruga Plaza na vijana wengine wawili.


Nyuma yao alitokea Binti mmoja mrembo sana ambae aliishia mlangoni tu na kuwasindikiza kwa macho.


Watu wale ambao walitembea ki kawaida tu bila kuonesha kama kuna mateka kati yao,walipita nyuma ya nyumba walimokuwamo na kutokea kwenye uwanja wa kanisa la Wokovu.


Huko walikuta gari ikiwa imenawangojea!


Wakapanda na kuelekea barabara kubwa kwa kupitia Nyakato shule ya msingi kisha wakakamata barabara kubwa na kuwa kama wanaelekea buzuruga.


Walipofika kona ya Nyakato sokoni,walikunja na kuelekea Meko,walipita karibu na baa ya ShaTemba na kuelekea njia ya vumbi ya Meko majanini.


Nyuma yao alikuwapo Mtega nyoka safari hii akiwa na pikipiki alioendesha mwenyewe huku abiria akiwa ni mwenye pikipiki.


Kwa msaada wa mwenye pikipiki, alimwelekeza kama wenye gari wamepitia njia ya Meko majanini basi wataenda kutokea njia ya Meko shule ya msingi hivyo wao waelekee shuleni na wangoje hapo.


Baada ya dakika kadhaa ilipita gari ya wagonjwa ikitokea Meko majanini.


Mtega nyoka aliona mtu aliekuwa amekaa kushoto mwa dereva.


Alijua wamebadilisha gari!


Akaifuata gari ile ya wagonjwa.


Safari yao ilikuwa ya uangalifu sana ili wasije wakashitukiwa.


Gari ile ilienda kuishia makanisa matatu na ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Mtega nyoka kufika eneo lile.


Hapo ndipo Mtega nyoka alipoona majengo sawa na yale yalioko kwenye kadi alioichukua mifukoni mwa mvamizi aliemuua bwana Kindo Seleman; Mkurugenzi wa Kasuku Contractors.


"Sasa kama ni kanisa ile kadi ya nini?" alijisemea Mtega nyoka huku akielekea kwenye makazi ya mchungaji wa kanisa la Efather.


Bado Mtega nyoka nae alikuwa anashangaa harakati zilizokuwa pale.



Akili yake ilishindwa kabisa kupata walau lililokuwa likiendelea pale.


Kama ni kikao basi ilitakiwa watu waingie na kutulia! Ila watu walikuwa wanaingia na kutoka.


Lakini pia yalikuwa ni mavazi yao.


Mavazi waliovaa ilitakiwa yavaliwe na waumini wa madhehebu ya Roman Catholic ama KKKT na si vinginevyo!!


Kwa mtazamo kanisa lile lilikuwa sawa na kanisa la kakobe ama Mzee wa upako ama wachungaji wenye sifa za utajiri kuliko uwezo wa waumini wao.


Sasa tangu lini makanisa ya aina hiyo yakawa na watawa?


Ajabu hii.



Ilikuwa ni wakati akitoka huko kwa mchungaji ndipo alipomuona mwanamke alievaa hijabu jeusi na kufunika uso wake wote na kubakiza macho tu.


Mwendo!!.


Aliutazama mwendo wa mwanamke yule.


Hata!!


Mwanamke gani huyu anatemebea kama kakanyaga moto!!


Aliachana nae akapanda pikipiki iliomleta pale na kutokomea.


Mwanamke wa hijabu nae akapanda pikipiki iliomfikisha pale na kuondoka.


Huku malipo ya dereva akimwandikia kwenye karatasi na kumuomba dereva afike kituo cha polisi atapewa pesa yake yote endapo akimwonyesha karatasi ile OCCID.


Dereva wa pikipiki akakubali japo roho ilimdunda.


Polisi hakuzoeleki!!



*****


Solomoni Bukaba alirudi ndani kwa Sundi na kuvua yale mavazi kisha akaenda kuyarudisha kama alivyoyakuta na kurudi kule chumbani alikokuwa amelala.


Akalala kama alivyoachwa.


****


Mtega nyoka alikuwa ameona Malima alivyotekwa pamoja na Remi.


Hivyo akapanga kurudi hadi nyumbani kwa Mwasu ili ambane Mwasu.


Hakuchukua zaidi ya saa mbili akawa yupo mlangoni kwa Mwasu.


Akagonga na kutulia.


Punde mlango ukafunguliwa akachomoza binti mrembo mwenye asili ya watu wa Rwanda ama Burundi.



"Nikusaidie nini!" Alisema Mwasu huku akimtizama Mtega nyoka usoni kwa makini.



Mtega nyoka alitabasamu.



"Nikaribishe ndani tuzungumze kidogo," alisema Mtega nyoka.


"Nakuingizaje ndani sikufahamu? Alisema Mwasu.


Mtega nyoka alikaa kimya kisha akatazama kushoto na kulia,alipoona kupo shwari Hakuna mtu akafanya kitendo cha haraka na kasi ya ajabu.


Akamsukuma Mwasu ndani kwa kasi kisha akatulia na kufunga mlango kwa nyuma.


Mwasu alijinyanyua chini huku akishangaa kasi alionayo bwana yule ambae alikuwa amesimama akimwangalia tu.


"unataka nini kwangu?" aliuliza Mwasu huku akijifuta kitu asichokiona mwilini mwake.


"naomba kufahamu alipo Malima" alisema Mtega nyoka.


Mwasu alishangaa!


"Malima?; mbona simjui!" alisema Mwasu.


Mtega nyoka akacheka kisha akatazama juu ukutani.



"Huyo uliebandika picha yake hapo ukutani ndie ninae mtaka" alisema Mtega nyoka huku akisonta kwa kidole picha kubwa iliokua imebandikwa ukutani.


Mwasu akagwaya huku akijutia uongo wake alioutoa bila kufikiria.


Mwasu alijua yupo matatani hivyo lazima afanye jihada za kujinasua kisha aombe usaidizi kama atashindwa kumdhibiti Mtega nyoka.


"Mi sujui alipo!" alisema Mwasu huku akimtizama usoni Mtega nyoka.


"Na Remi je!" aliuliza tena Mtega nyoka.


Mwasu alikodoa macho huku akishindwa kuelewa dhamira ya mgeni wake huyo.


"Hebu sema shinda yako bwana mana naona sikwelewi; Malima; Remi tuelewe lipi sasa" alikoroma Mwasu.


"Ukinijibu wote kwa pamoja itakuwa vizuri sana" alisema Mtega nyoka.


"watafute mwenyewe utajua walipo" alisema Mwasu.


Mtega nyoka alitulia kimya akimtizama Mwasu.


"Vipi kuna nini pale Makanisa matatu?" lilikuwa swali la mtego ambalo Mwasu hakulitarajia.



Akaingiwa na ubaridi wa gafla.


"Sasa mbona wafahamu mengi, kwanini waniuliza?"



"Kwa sababu na..." Mtega nyoka hakumaliza kauli yake alijiukuta akirudi nyuma kwa kasi na kujipigiza kwenye mlango na kusambaratika chini.



Mwasu alikuwa amemfanyia shambulizi la kushitukiza.


Mtega nyoka aliharakisha kunyanyuka ila alijikuta akienda chini tena baada ya kupigwa teke ubavuni.


Mwasu hakutaka kucheza na mtu kama yule.


Akapaa juu na kurudi na pigo la kifo.


Mtega nyoka aliliona akakwepa kisha akaachia konde zito lililompata Mwasu tumboni.


Mwasu akaenda chini huku akitoa kilio kama cha mwanamke anaebakwa.


Mwasu akasimama ila akajikuta anaingia kwenye wakati mgumu kujiokoa na makaonde mfululizo kutoka kwa Mtega nyoka.


Yapo aliopangua na mengine yalijaa mwilini mwake.



Mwasu akaona akifanya uzembe atakuwa mateka ili aseme anachokijua.


Hakutaka hilo litokee.


Akajifanya kama anaenda chini ila hakufika badala yake alifyatuka kichwa kikali kilichotua tumboni kwa Mtega nyoka na kumpeleka chini. Kisha yeye akasimama haraka na kujirusha mzimamzima na kwenda kulikumba dirisha la vioo lililokuwa sebuleni pale na kusambaratika nalo nje kisha bila kujiuliza akasimama na kutimua mbio za mbwa mwizi.


Mtega nyoka nae aliharakisha kutoka kwa kupitia pale pale dirishani baada ya kuwa wazi kwa kuvunjwa.


Alipotua nje hakuona hata unyayo wa Mwasu.


Alikwama tena.




*****


Sundi alirejea nyumbani kwake jua likiwa linaelekea kuwa la utosi.


Alifanya haraka haraka na kuelekea jikoni kupika chakula.


Alipokwisha kupika alihitaji kwenda kufungua na kusafisha majeraha ya Salomoni.


Alivaa mavazi maalumu na kuvaa kitambaa maalumu chenye kamba zilizoenda kushika masikio huku kikiwa kimeziba mdomo na pua.


Sundi alifunua mapazia yaliokuwa yamekizunguka kitanda alicholalia Solomoni Bukaba.



Alikuta Solomoni akiwa ameshazinduka kutoka usingizini.


"Wajisikiaje mpenzi!" aliuliza Sundi huku akimtizama Solomoni usoni.


Macho yao yalipogongana yaliongea Lugha ya upendo wa hali ya juu.


Walipendana kiukweli.


"Naendelea vyema hivi sasa mpenzi wangu" alijibu Solomoni kwa uchovu.



"mmh pole,ngoja nikusafishe ili uendelee kupumzika" alisema Sundi huku akimwanamia Solomoni.


Macho yao yaligongana tena.


Solomoni aliona kitu.

Kitu hicho ndicho alichokiona siku anavamiwa ndani kwake.


Macho!!


Uangaliaji ule ulifanana sawasawa na ule alioangaliwa na mwanamke aliekuwa amevaa kininja.


Macho yalikuwa ni yale yale.


Alikumbuka sawia.

.


Akajikaza bila kuuliza hilo jambo.


Sundi aliendelea kumshugulikia Solomoni.


Alimaliza kumsafisha majeraha kisha akavua mavazi aliokuwa amevaa na kuyatundika mle chumbani kisha akamuomba Solomoni aende sebuleni kwa ajili ya chakula.


Solomoni aliamka kivivu na kwenda sebuleni.


Dakika kadhaa badae walikuwa wanakula chakula kitamu alichopika Sundi huku kila mara Sundi akimsaidia Solomoni kumlisha.


Walikuwa wakitaniana hapa na pale ili mradi kila mtu anaonesha kumjali mwenzie.


Walipomaliza kula walielekea bafuni ambako Sundi alimwogesha Solomoni huku wakitaniana hapa na pale huko bafuni.


Walimaliza kuogeshana wakaelekea chumbani na kujilaza kitandani.


"Mpenzi sijakuuliza kilichokupata jana mana niliona ulikuwa hujiwezi kabisa" alisema Sundi.


"Kwani hujasoma magazeti leo!? Nyumba yangu iliungua moto ila kabla nilivamiwa na watu walionishambulia namna hii kama unavyoona" alijibu Solomoni huku akimtizama Sundi usoni.


Sundi alitazama pembeni.


"hao watu walisema wanataka nini kwako?" aliuliza Sundi.


"Hawakusema wanachotaka" alijibu Solomoni alijibu huku akiwa bado anamtazama usoni.



Sundi alikaa kimya kidogo kisha akamchumu midomoni na kumpa ulimi Solomoni ambae nae aliupokea na wakagandana huku mikono yao ikitalii kwenye miili yao.


"Mmh unaumwa Solo wangu, tuishie hapa" alisema Sundi huku akijinasua Mikononi mwa Solomoni.


Kabla Solomoni hajasema lolote kengele ikalia.


Wakaangaliana.


Kengele ikaendelea kulia kwa fujo.


Sundi akatupa kanga aliokuwa amevaa,harakaharaka akavaa suruali aliokota chini na shati pana jeupe hakujali kuvaa hata chupi akaenda kufungua mlango.


Alipigwa na butwaa!!


"Mbona nyinyi leo mnamabalaa hivi" alisema na mtu aliekuwa getini.


"Mambo yanazidi kuwa mabaya tu" alijibu mtu aliekuwa getini.


"Duh afu niliwambiaje kuingia hapa kabla hatujawasiliana?" alihoji Sundi huku akifungua geti.


Alimfungulia Mwasu.


Mwasu alikuwa anamajeraha mwili mzima ya kuchanika chanika hasa usoni.


Haraka akapelekwa kwenye chumba kilichokuwa na vifaa tiba na kuanza kuhudumiwa.


Huduma ilichukua si zaidi ya saa mbili tayari majeraha yalikuwa yamesafishwa na kushonwa vizuri.



Hakuwa na majeraha makubwa sana hivyo akawa yupo timamu kimwili.


Walitoka kukaa sebuleni.


Walimkuta Solomoni akiwa ametulia akitazama runinga.


Mwasu akamtazama Sundi.


Sundi akatoa ishara ya kuwa asijali.


Wakaenda kukaa wote sebuleni huku Mwasu akipeana salamu na Solomoni.



Kitu ambacho Sundi alikijua na Mwasu hakujua kama Sundi anajua ni kuwa katika mipango yao endapo akitokea mtu hatarishi wa kushugulikiwa basi picha yake husambazwa kwa wote na akishakufa pia taarifa hufika kwa wote.


Hivyo Mwasu alishangaa sana kumkuta Solomoni nyumbani kwa Sundi.


Alimchukulia Sundi kama ni msaliti kati yao.


Akapanda kufanya jambo.



Waliendelea kuangalia runinga huku wakisemezana hili na lile.


Mwasu akaomba kutoka nje kidogo akapunge upepo kwa madai amechoka kukaa na majeraha yalimuuma.


Alikubaliwa huku Sundi akijua ni nini Mwasu anaenda kufanya huko nje.


Hakutaka alilowaza litokee.


Mwasu alipofika nje tu akatoa simu yake harakaharaka akatafuta namba za Elchapo ili apige.


Ni wakati simu yake inaita ndipo akajikuta yupo chini bila kupenda.


Sundi alikuwa amempiga teke la mgongoni.


Ngumi zikapangwa na watu walianza kupigana vita ya hatari.


Solomoni Bukaba akisikia vishindo huko nje,mwanzo alipotezea lakini vishindo viliongezeka.


Nae akatoka.



Alijikuta akishuhudia mpambano safi wa wanawake wanaojua vizuri mchezo wa ngumi.


Sundi alikuwa anacheka ili kumgadhabisha Mwasu.


Kicheko chake kilielea vyema kwenye ngome za masikio ya Solomoni.


Alikumbuka kicheko kile.


Ni cha yule yule mwanamke aliemvamia usiku wa balaa kwake.


Ebana eeh!


"Sundi ni nani na anashirikiana na nani!?" alijiuliza Solomoni.


Ni hadi pale alipoona Mwasu akichomoa kisu kutoka maungoni mwake na kwa ustadi wa hali ya juu akakirusha kumwendea Sundi. Na Sundi nae kwa wepesi wa ajabu akajikunja na kisu kikampita sentimita chache tu.


Solomoni hakujua kama Sundi wake laini laini anaweza kuzichapa kiasi kile.


Ilikuwa ni ajabu ila ndivyo ilikuwa.


Sundi alienda juu kama nyani na aliporudi akaachia teke safi lililoishia shingoni kwa Mwasu na kumsambaratisha chini kama mzigo.


Sundi aliona kumwachia Mwasu ni kujizika zaidi yeye hivyo akachomoa bastola ambayo Solomoni hakujua ilitokea wapi mana Sundi alivaa wakati yeye akiwepo na hakuiona.


Hatari hii.


Kisha akashuhudia Sundi akiachia risasi sita bila huruma ambazo zote zilijaa kifuani kwa Mwasu na kumwacha akiwa hana uhai.


"Why!!" aliuliza Solomoni baada ya kuona Sundi amegeuka na kumnyooshea bastola yeye.


Sundi alitamani apasue kichwa cha Solomoni ila nguvu ya mapendo ilizidi utimamu wa akili.


Akajikuta akishusha silaha chini.


"Tuondoke hapa hakutufai" alisema Sandi huku akiishindilia risasi simu ya Mwasu iliokuwa chini.


Iliwabidi kuondoka eneo lile.





***


Usiku ndio muda ambao Mtega nyoka alipanga kufika tena kule makanisa matatu na kwa ushushu wake aliokuwa ameufanya mchana mzima alikuwa amefanikiwa kujua eneo lile huwa lina ulinzi wa kawaida tu nyakati za usiku.


Hivyo usiku ulipofika aliondoka kuelekea huko makanisa matatu.


Alishuka kwenye pikipiki iliomfikisha pale. Akajichanya kwenye vichochoro viwili vitatu lengo likiwa ni kuendelea kusoma ulinzi ulivyowekwa eneo lile.


Lakini pia alijiuliza endapo kulikuwa kuna umuhimu wa kuwa na ulinzi kwenye kanisa lile na nyumba zake.


Hakuona umuhimu huo.


Ilikuwa yapata saa tano usiku,mitaa ile ilikuwa imeishiwa pilikapilika na hivyo kukabaki kimya kabisa.


Mara akiwa ametulia pahali aliweza kuona tena mwanamke mwenye hijabu akikatiza maeneo yale akiwa na haraka zake.


Bado aliutazama mwendo wa mwanamke yule jinsi ulivyokuwa unautata.


Kwa kawaida mwanamke huwa hanyanyui nyayo za miguu yake.

Huburuza.


Ila mwanamke yule alikuwa ananyanyua nyayo zake juu kabisa kama dume.


Akapotelea kwenye kigiza.


Mtega nyoka akaachana nae.


Akarudisha macho yake pale kwenye malango matatu ya kanisa.


Lango la katikati lilikuwa linafunguliwa na wakatoka watu watatu waliokuwa wamevalia suti safi nyeusi.


Watu wale waliangaza huku na huko kisha mmoja akarudi ndani na wawili wakabaki wanaangalia tu.


Kama ungewatazama haraka basi ungejua ni walinzi wa Rais ama Makamu wake.


Baada ya dakika tatu tu likatoka gari la wagonjwa upande wa pili wa lango la kushoto ambako kulikuwa kuna nyumba za watumishi.


Gari ile ilifika hadi karibu na lango lile la katikati ikapaki.


Na ilikinga lango hivyo Mtega nyoka kutoka alipo alishindwa kujua inapakia nini eneo lile.


Baadae kidogo gari ile ikatoka na kuanza safari ya kuelekea mjini.


Na nyuma yake kulifuatia magari mengine kama sita hivi yote yalifanana isipokuwa yalitofautishwa na namba tu za usajili.


Mtega nyoka akataka kutoka pale alipokuwa na kuanza kuyafuatilia ila hakuona usafiri eneo lile na mara nyingi hakupendelea usafiri wa gari zaidi ya pikipiki.



Akaendelea kuvuta subira.


Haikupita nusu saa likaja gari lingine nalo likapaki pale pale na kushusha watu wengine kama sita walikuwa ni wa kiume wote na wakaingia ndani ya Lango lile la katikati.


Mtega nyoka ni kama wazo fulani likamjia.


Akataka kwenda na yeye pale pale langoni ashuhudie kinachoendelea.


Ila akapanga kudandia ukuta na kutokea nyumba za watumishi ambazo kwa haraka alitambua zina milango ya kuingilia ndani ya makanisa yale.


Hivyo akahepa kutoka alipokuwa na kuzunguka mtaa wa nyuma ambao ulikuwa umetulia isipokuwa mbwa waoga walikuwa wanabweka huku na huko.


Akadunda mara ya kwanza na mara ya pili akafanikiwa kuwa juu ya kichochoro fulani cha ukuta na kwa kukitumia akafanikiwa kudaka kingo ya ukuta wa nyumba aliotaka kuingia.


Akafanikiwa kutua kwenye kichaka cha maua na kutulia.


Alimaliza dakika mbili akiwa kimya ili kujua kama kuna aina yoyote ya kiumbe eneo lile.


Hakusikia!!


Akataka kutoka, akasita.


Alisikia sauti ya watu wakiteta


Lakini walionekana wamelewa.


Ajabu hii!!.

.

Watumishi wanalewa!!


Sauti za watu wale zilizidi kukaribia alipokuwa na dhahiri shahiri watu wale walikuwa wamelewa si mchezo.


Waliongea lugha walioelewana wao kwa wao tu.


Waliongea kilevi!!


Hakuna alichojua watu wale walikuja kufanya nje ila akasikia wakiondoka na kuelekea ndani.


Nae haraka akachoropoka na kuingia ndani ya kibalaza walichpoitia watu wale.



Hakuona mtu.


Kwa tahadhari kubwa akaingia ndani ya nyumba ile.


Akapokelewa na sebule tupu.


Nini hiki!!


Akafanya utalii kwenye vyumba alivyoona ni rahisi kukagulika.


Hakuona kitu.


Akaelekea upande kulikokuwa na jiko.


Hakukua na chombo hata kimoja kilichokuwa ndani ya jiko ile.


Ila kuna kitu kilimvutia kwenye ukuta wa jiko lile.


Kulikuwa na kitu kama ufa hivi.


Akaugusa.


Ajabu ukafunguka mithili ya vyumba vinavyotembea ndani ya majengo marefu.


Akapokelewa na hewa safi ya kiyoyozi na taa za rangi.


Akaingia na nyuma ule mlango ukajifunga.


Alijikuta yupo kwenye njia ambayo hakujua ingemfikisha wapi.


Akaifuata!


Akajikuta anaishia kwenye lango lingine ambalo lilikuwa na watu wawili wamesimama na kuliweka kati.


Watu wale walikuwa wamevaa suti kama za wale watu aliowaona wakipokea gari la wagonjwa.


Watu wale wakaziba njia baada ya kumuona na mmoja akanyoosha mkono.


Mtega nyoka hakuelewa ile ilimaanisha nini.


Akapotezea kama anajipapasa mifukoni.



Aligusa kadi!!


Haraka akili yake ikakumbuka kadi aliochukua kwa mvamizi wa Kasuku Contractors.


Akaitoa!!


Alieipokea akaikagua huku na huku aliporidhika akamrudishia kadi ile na kumpisha njiani.


Kanisa gani hili!


Alijiwazia.


Alipoukaribia mlango ule nao ukajifungua kama wa mwanzo na hapo ndipo alipojikuta roho yake ikikosa amani kwa alichokiona.


Langoni alikutana na maandishi makubwa yaliokuwa yamepambwa kwa nakshi nyingi za kuvutia.


WELCOME TO HEAVEN CLUB D


Ndio maneno aliyoyasoma Mtega nyoka.


Miaka buku hii hakuna ambae angeijua!!


Alijiwazia.


Akashuka ngazi zilizokuwa zinaelekea chini na hiyo ilimaanisha anaelekea chini ya majengo yale.



Club D kweli ilikuwa ni kama peponi.


Kulipendezeshwa kuanzia kuta zake hadi sehemu ya kukanyaga na kila hatua aliopiga alipishana na wanaume waliobambiana na wadada walioko uchi huku mziki laini ukitoka kwenye sipika zilizokuwa zimefungwa kitalamu bila kuonekana.


Alizidi kuingia ndani ya Club na hapo alikutana na watu wengine ambao walikuwa wamekaa wanakunywa tu.


Wote walionekana ni watu wa shari nyusoni mwao.



Alifika hadi sehemu kulikokuwa na kaunta ambapo wahudumu wa kike waliokuwa uchi kabisa.


Na kitu alichogundua ni kuwa kila mwanamke aliekuwa mle hakuwa na nguo na hakukutaa kila alieenda kumbambia.


Ufusika ulifanyika hadharani.


Alipewa kinywaji na kukaa viti virefu huku akijizuia kushangaashangaa.


Akiwa bado ametulia akafuatwa na dada mmoja aliekuwa uchi na kumbusu nae akakubali kisha akavutwa mkono na yule dada na taratibu akashuka na kumfuata binti yule ambae alimwonesha ishara ya kidole cha kati ya kuwa huko wanaenda kuburudika kwa ngono.


Waliingia mlango mwingine ambao sasa uliwafikisha kwenye ufuska kamili.


Huko kulikuwa na watu wengi kuliko alikotoka na ngono ilifanyika wazi wazi kwenye jukwaa lililokuwa na warembo waliokuwa wanacheza uchi huku wanaume wakipanda na kufanya nao ngono kidogo na watu wanashangilia kweli kwa kitendo kile.


Macho ya mtega nyoka yalinasa mlango mwingine mbele kidogo ya jukwaa. Mlango ule kulikuwa kuna watu wawili na kila baada ya dakika tatu kuna mtu anaingia na kutoka na mkoba mweusi.


Mtega nyoka alibambiwa na mwanadada aliempeleka kule nae akabambia likawa kosa.


Alisikia tu kucha ikimkwaruza na haikupita hata dakika moja akaanza kuona nyota za rangi nyinginyingi.


Mtega nyoka akawa matatani


******



MWISHO





0 comments:

Post a Comment

Blog