Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

SISTAHILI KUSAMEHEWA

   


MTUNZI : JUMA HIZA





Naitwa Tullah Ambrose nimezaliwa miaka ishirini iliyopita, naishi na wazazi wangu katika mkoa wa Daresalaam, Tabata Bima, hapo ndipo nilipozaliwa na kukulia japo katika upande wa kielimu nimesoma kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha sita ‘bording.’ (Bweni.)

Kwa upande wa maisha yangu ya kielimu yalihamia na kuwa ya bweni tangu nilipokuwa mdogo, kusoma katika shule ya jinsia moja (Wasichana watupu.) hakika iliniwiavigumu sana mpaka kuzoea maisha hayo.

Lengo langu si kukusimulia maisha yangu ya shule au maisha ya wazazi wangu ambao walikuwa na uwezo na jinsi walivyokuwa wananichunga lah! isipokuwa nipo hapa kukusimulia simulizi iliyotoea miaka saba baada ya kumaliza elimu yangu ya sekondari.

****

Nakumbuka ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kujiingiza katika ulimwengu wa mahusiano, ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuuruhusu moyo wangu upende, nilijikuta nikishindwa kujizuia na kuamua kumkabidhi moyo wangu wa mapenzi Gilbert mwanaume ambaye niliamini aliumbwa kwa ajili ya maisha yangu, kwa ajili ya hisia zangu.

Nilimpenda sana Gilbert kwa moyo wangu wa dhati japo naweza kusema hakuwa ni mwanaume wa kwanza kunitamkia nena nakupenda lakini uvumilivu wake pamoja na kujitoa kwake kuliweza kunishawishi mpaka nikajikuta namkubalia ombi lake. Nakumbuka aliwahi kuniambia kuwa anafanya kazi katika kampuni moja iliyokuwa ikijihusisha na uuzaji wa magari.

Niliingia rasmi katika ulimwengu wa mapenzi huku nikiwa sijui hili wa lile kuhusiana na mapenzi. Gilbert ndiye aliyekuwa mwanaume wangu wa kwanza kunitoa usichana wangu.

Kila siku alikuwa akinionyesha mapenzi ya kweli, mapenzi ambayo kwa kweli sikuwahi kuyapata mahali popote pale. Gilbert ndiye aliyekuwa mwanaume wa kwanza kunifundisha kila kitu kuhusiana na mapenzi.

Nakumbuka kipindi kile nilikuwa likizo nikisubiri kujiunga na elimu yangu ya chuo kikuu. Nilionekana kuwa mwingi wa furaha kila wakati maisha niliyaona kuwa mazuri sana. Kitendo cha kumpata Gilbert hakika kulikwenda kufungua ukurasa mpya wa maisha yangu.

Hakukuwa na mwanaume ambaye alikuwa akiishughulisha akili yangu zaidi yake, kila kitu nilichokuwa nikikiwaza nilikiwaza pamoja na kumuhisisha yeye. Alitokea kuiteka akili yangu ambayo haikuwa ikifikiria chochote zaidi ya mapenzi yake aliyokuwa ananipa kila siku.

“Nakupenda sana Tullah.”

“Nakupenda pia honey.”

Nakumbuka maneno haya hayakuwahi kukauka katika vinywa vyetu, kila tulipokuwa tukikutana ilikuwa ni lazima tuambiane maneno haya, naweza kusema ilikuwa ni kama desturi yetu.

Baada ya miezi kadhaa kupita hatimaye matokeo ya kidato cha sita yaliweza kutoka, sikutaka kuamini kile ambacho nilichokuwa nakisikia na kukiona kwa wakati ule. Nilikuwa miongoni mwa wanafunzi ambao walifanya vizuri katika mtihani huo ambao waliweza kutangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali.

Baadae tuliweza kupangiwa vyuo na ilikuwa kama bahati vile hatimaye niliweza kupangiwa nikasome chuo kikuu cha Daresalaam.

“Umepata bahati ya kusoma mpaka chuo kikuu nakuomba ukasome mwanangu, usifate mengine kule,” aliniambia Mama usiku mmoja huku akionekana kuwa na hofu na mimi, wakati huo tulikuwa mezani tukipata dina.

“Mama nakuahidi siwezi kujisahau,” nilimjibu kwa kumuondoa hofu.

“Tutafurahi kama ukizidi kufanya vizuri hata huko uendapo,” alisema Baba.

“Sawa Baba ila nawaahidi kuwa nitazidi kufanya vizuri kila siku,” niliwaambia kisha huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu. Niliwaaga na kwenda chumbani kwangu huku nikionekana kuwa mwenye furaha sana.

Nilipoingia chumbani kwangu hakukuwa na kazi nyingine zaidi ya kuwasiliana na Gilbert mwanaume niliyekuwa nikimpenda kuliko kitu chochote kile katika hii dunia. Nilipoichukua simu yangu niliingia upande wa ‘Gallery’ kisha nikaingia upande wa picha halafu nikaanza kuitazama picha ya Gilbert ambayo ilionekana kunivutia sana kwa kila kitu.

Baada ya kuitazama kwa muda mara simu yangu ikawa inaita, nilipoitazama alikuwa ni Gilbert ambaye nilimsave kwa jina la “My Everything.” (Kila kitu.)

“Hallo Baby,” nilisema kwa sauti laini mara baada ya kupokea.

“Hallo mpenzi,” alinijibu kisha akanyamaza kiasi cha kuvuta pumzi halafu akaendelea kuzungumza.

“Hongera mpenzi wangu kwa kufanya vizuri katika mitihani yako.”

“Asante mpenzi wangu yani nina furaha isiyo na kifani.”

“Najua baby ila nikuambie kitu.”

“Ndiyo niambie.”

“Usisahau kumshukuru Mungu kwa kila kitu kilichotokea kwani yeye ndiye aliyepanga yote haya kutokea.”

“Ni kweli mpenzi hata hivyo namshukuru sana tu.”

“Nakupenda sana.”

“Nakupenda pia hubby.”

Huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu.

****

Hatimaye niliyaanza maisha ya chuo rasmi, maisha ambayo niliyaona kuwa ya tofauti sana kutofautisha na maisha ambayo niliwahi kuishi kipindi nilipokuwa sekondari.

Maisha ya chuo tuliishi kwa kuchanganyika wavulana na wasichana, macho yangu yalipata wasaa wa kutazama baadhi ya wavulana watanashati ambao walionekana kunivutia kwa kiasi fulani. Nilianza kuingiwa na tamaa na kujikuta nikianza kuwapenda wavulana wa chuo ambao baadae walikuja kunipa funzo ambalo kwa kweli kila nikikumbuka machozi hayanikauki mashavuni mwangu.



Taratibu nilijikuta nikianza kumsahamu Gilbert, mwanaume ambaye alikuwa akinipenda sana. Nilihisi kumuona kutonifaa katika maisha yangu licha ya alikuwa na kazi nzuri, maisha ya kujiweza lakini moyo wangu ulianza kuyaona mapungufu makubwa sana kwake. Kwanza alikuwa mweusi halafu mimi nilikuwa mweupe, pili hakuwa na mvuto kivile, nilimuona kuwa wakawaida sana. Kipindi kile naanza chuo huku nikiwa nasomea masomo ya sheria kwa mara yangu ya kwanza kabisa nilijikuta nikitumbukia katika dimbwi la mahusiano na mvulana mmoja ambaye alikuwa na asili ya kiarabu, huyu alijulikana kwa jina la Haroon, alikuwa akimalizia mwaka wa mwisho pale chuoni, alikuwa akisomea Sheria, alikuwa akiishi Hostel.

Nilitokea kumpenda sana Haroon kutokana na mvuto wake aliyokuwa nao, kila siku wasichana hawakuisha kujigongagonga kwake lakini wote aliweza kuwakataa, hakika kumpata maishani nilijiona kuwa mshindi sana. Kila mahali nilipokuwepo alikuwepo, tulipendana sana na hatimaye hata ile siri tuliyoiita siri mwanzo iliweza kuvunjika. Kila mtu alikuwa akifahamu juu ya uhusiano wetu.

“Tullah,” aliniita Diana rafiki yangu mkubwa sana ambaye tulikuwa tumeanza naye chuo. Alikuwa akifahamu mambo mengi sana kuhusu mimi, nilikuwanikimwambia kwasababu nilikuwa nikimuamini sana, hata uhusiano wangu na Gilbert alikuwa akiufahamu. Wakati huo tulikuwa kantini tukila chakula cha mchana.

“Abee,” nilimuitikia huku nikimtazama.

“Naona sasa hivi mambo yamekolea.”

“Mambo yapi tena.”

“Umedata na mtoto wa kiarabu.”

“Hahahaha! Embu acha utani wako.”

“Niache nini sasa kwani uongo.”

“Yeah! Ni kweli nampenda sana tena sana tu.”

“Mmh! ina maana Gilbert ndo basi tena.”

“Gilbert wa nini sasa.”

“Wa nini tena?”

“Sasa hivi nipo na Haroon.”

“Hivi unajua umebadilika sana.”

“Nimebadilika nimekuwa mwekundu au?”

“We haya.”

“Bhana embu kwanza tuachane na hayo,” nilimwambia kisha huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mazungumzo yetu.

Sikutaka mtu yeyote yule aingilie mapenzi yangu na Haroon, nilikuwa nikimpenda sana.

Baada ya kupita siku kadhaa tangu uhusiano wetu ulipoanza, Haroon alianza kunitaka kufanya naye mapenzi. Kwa kuwa nilikuwa nikimpenda na sikuwa tayari kuachana naye niliamua kumkubalia.

Nilianza kufanya naye mapenzi, nilikuwa nikimfuata Hostel kisha tukawa tunafanya mapenzi kila siku tulipokuwa tunajisikia kufanya.

Mchezo wetu haukukoma uliendelea kila siku na kadri siku zilivyokuwa zikisonga mbele ndivyo ambayo nilizidi kumpenda sana Haroon mpaka nikawa naanza kumsahau Gilbert mwanaume ambaye alikuwa wa kwanza kunitoa usichana wangu.

“Haroon,” nilimuita siku moja tulipokuwa tumemaliza kufanya mapenzi.

“Niambie malkia wangu,” aliniambia huku akinibusu katika paji la uso wangu.

“Nakupenda sana.”

“Nakupenda zaidi yako.”

“Natamani ungekuwa mwanaume wangu wa kwanza kunitoa usichana wangu.”

“Kwanini?”

“Kwasababu nakupenda sana, kwa mapenzi unayonipa sitaki kukupoteza.”

“Usijali nimeshakuwa wako.”

“Nakupenda mpenzi.”

“Nakupenda pia.”

Tuliendelea na mapenzi yetu huku kichwa changu kikianza kumsahau kabisa Gilbert, nilianza kumsahau kutokana na ahadi alizokuwa akiniahidi Haroon, nakumbuka aliwahi kuniahidi kuwa kipindi atakapomaliza chuo na kupata kazi atanioa na kunifanya kuwa mke wake halali wa ndoa. Kwa kweli mara baada ya kuyasikia hayo moyo wangu ulijikuta ukimpenda sana, nilimuamini kupitiliza hata lilipokuja suala la kutaka kufanya mapenzi na mimi kinyume na maumbile niliweza kumkubalia kwasababu niliamini yeye ndiye aliyekuwa mwanaume wa maisha yangu, mwanaume wa ndoto zangu, mwanaume ambaye siku moja angeweza kunibadilisha jina na kunifanya niitwe mama fulani ambaye ningeweza kuwa na heshima katika jamii inayonizunguka. Mapenzi ya Haroon yalinifanya nianze kumchukia sana Gilbert,nilijikuta nikianza kuingia na chuki kali dhidi ya Gilbert. Kila nilipokuwa nikiiona simu yake aliyokuwa akinipigia niliiona kuwa kama usumbufu, niliamua kuikata. Sikutaka kuongea naye wala kuonana naye. Hakika mapenzi ya Haroon yalitokea kunibadilisha sana. Wakati alipokuwa akijaribu kunipigia simu na kuwa nikiikata, aliamua kunitumia ujumbe mfupi.

“Mbona umebadilika mpenzi.”

“Nimekuwaje kwani.”

“Naona sasa hivi hautaki kuwasiliana na mimi kabisa.”

“Nipo bize sana.”

“Haya mpenzi wangu nakupenda sana.”

“Asante.”

“Mbona unanijibu hivyo?”

“Nakujibuje?”

“Sijazoea kuona ukinijibu hivyo.”

“Unataka nikujibuje?”

“Basi mpenzi.”

“Poa.”

Nilijikuta nikimchukia sana Gilbert bila makosa yoyote, ni ukweli kwamba alikuwa akinipenda sana lakini mapenzi yake sikuyajali hata kidogo, niliyaona kuwa kama mzigo ambao ulikuwa ukinichosha katika maisha yangu.

Sikuwahi kumtambulisha nyumbani kwetu hivyo niliona mapenzi yetu kutokuwa na nguvu. Nilijiamini kwakumwambia kila aina ya neno baya, sikujali hata pale nilipoamua kumtukana nilimtukana kwani sikutaka tena kuwa naye, kwa kifupi nilimchoka, mapenzi ya Haroon yaliniteka vilivyo.

Siku moja nilipokuwa darasani niliamua kumtumia ujumbe mfupi Gilbert, ujumbe ambao ulilenga kuachana, nakumbuka nilimuandikia hivi;

“Naomba huu ndiyo uwe mwisho wetu. Asante kwa upendo wako, asante kwa mapenzi yako, Kwa sasa nimempata mwanaume mwingine ambaye ananipenda na mimi nampenda sana hivyo naomba ukae mbali na mimi,” nilimuandikia ujumbe huu kisha nikaamua kumtumia. Niliamini ulikuwa ni ujumbe ambao ulienda kumuumiza sana katika moyo wake lakini sikujali lolote lile kwa wakati ule.




Akili yangu sikutaka iendelee kumfikiria tena Gilbert. Niliamua kumtoa katika mawazo yangu na sasa nilikuwa nikiutumia muda wangu mwingi katika kumfikiria Haroon mwanaume ambaye niliamini alikuwa akinipenda ssana kuliko mwanamke yoyote pale chuoni.

Gilbert alianza kuniomba msahama kwa kitendo kile cha kumtumia ule ujumbe mfupi uliyokuwa na lengo na kuachana. Hakujua ni kosa gani alilokuwa amelifanya mpaka nikaamua kumtumia ujumbe ule, aliamua kuniomba msahama kwa kosa ambalo hata hakulifahamu, alijihisi tu kunikosea jambo ambalo si kweli bali nilitokea kumchukia tu bila sababu ya msingi.

“Naomba unisamehe mpenzi wangu,” aliniambia siku moja nilipokuwa nimepokea simu yake, alikuwa akizungumza kwa sauti iliyonidhidiris

hia kuwa alikuwa akilia kwa wakati ule.

“Nikusamehe nini?” nilimwambia huku nikiubetua mdomo wangu, nilikuwa nikimchukia sana.

“Naomba unisamehe turudiane mpenzi wangu, sitaki tuachane bado nakupenda sana,” alizidi kuniambia kwa sauti ya kulalamika.

“Sitaki naomba tuachane kwani mwanamke niko peke yangu jamani si uende kwa wengine ukawalilie?” nilimwambia kwa kumuuliza swali ambalo lilizidi kumuumiza sana, sikuyajali maumivu yake kabisa, sikutaka kukijali kilio chake wala yale malalamiko aliyokuwa akinilalamikia juu ya kunipenda sana. Nilifahamu fika kuwa Gilbert alikuwa akinipenda sana ten asana tu na ndiyo fimbo niliyokuwa nikiitumia katika kumuadhibu bila ya hatia yoyote. Niliendelea kuzitesa hisia zake bila ya kumuonea huruma yoyote.

“Tullah nikwambie kitu?”

“Niambie.”

“Siunajua kuwa nakupenda sana.”

“Sijui mimi.”

“Baby usiseme hivyo unazitesa hisia zangu.”

“Nazitesaje?”

“Unaniumiza sana kwanini unanifanyia hivyo au nimefanya makosa kukupenda, kukupa moyo wangu wa mapenzi?”

“Nilikutuma unipende?”

“Usiseme hivyo basi.”

“Embu niache huko kawapende wengine sasa hivi niko na mwanaume mwingine.”

“Unasemeje?”

“Kampende hata Mama yako au ndugu zako lakini sio mimi,” nilimwambia kisha nikakata simu.

Sikutaka kuendelea kuwa na mawasiliano na Gilbert. Kitu nilichoamua kukifanya ni kuifuta namba yake. Niliamua kufanya hivyo kwasababu sikutaka tena kuendelea kuwa na mahusiano naye, mahusiano ambayo nilitokea kuyachukia sana, niliyachukia mpaka kuna kipindi nilikuwa najuta kukutana naye katika maisha yangu.

Gilbert hakuchoka kunisumbua kwa ajili ya kuniomba msamaha. Aliendelea kunitumia jumbe mbalimbali zenye lengo la kuniomba msamaha na mapenzi yetu kurudi kama zamani.

Kila ujumbe aliokuwa akinitumia nilikuwa nikiusoma na kuufuta, sikutaka kumjibu lolote kwani kwakufanya hivyo ningeweza kufanya mawasiliano yetu yasifike kikomo.

Baada ya kuona anazidi kunitumia jumbe nyingi bila kuchoka niliamua kumtumia na ujumbe ambao kwa kweli naamini ulienda kumuumiza sana. Nakumbuka alikuwa amenitumia ujumbe mfupi uliosomeka “Unaniacha Tullah.” Nilipousoma nilicheka kisha nikaamua kumjibu.

“Nani mwenzangu?” nilimtumia ujumbe huu kwa kumuuliza kuwa alikuwa ni nani? kwa kweli nilikuwa nikiuandika ujumbe huu huku nafsi yangu ikinisuta, kuna muda nilikuwa nikijistukia lakini sikutaka kujali lolote, niliamua kumtumia na ni hapo ambapo alinijibu jibu ambalo naweza kusema lilikuwa ni jibu lililoukaribisha ukimya kati yetu mpaka leo ninapokusimulia haya. Alinitumia ujumbe uliosomeka;

“Tullah najua unanichukia sana, unanichukia na sijui sababu ni nini? Nimejaribu kukuuliza kila aina ya maswali lakini unanijibu unavyojisikia. Sijui kwanini umebadilika mpenzi wangu unanifanyia visa lakini mimi bado nakupenda, nimejitoa sana kwako, nimejitahidi kufanya kila kitu kukuonyesha ni jinsi gani ninavyokupenda lakini leo unaniambia umenichoka. Sawa nimekubali kuachana na wewe lakini naomba unitunzie kila kitu nilichowahi kukupa kama zawadi kwako. Hii ndiyo meseji yangu ya mwisho kwako sitakusumbua tena endelea na maisha yako salama salimini lakini ipo siku utanikumbuka.” alinitumia ujumbe huu niliyousoma kisha nikaupuuzia, niliyaona kuwa kama ujumbe uliyobeba maneno ya mkosaji.

****

Niliendelea kuwa na mahusiano na Haroon mpaka pale alipomaliza mwaka wake wa mwisho pale chuoni, kipindi hicho na mimi nilikuwa naingia mwaka wa pili pale chuoni. Alikuwa akinipenda sana na mimi nilikuwa nikimpenda sana. Mapenzi yake yaliniteka sana mpaka kuna kipindi nilikuwa sifanyi vizuri katika masomo yangu jambo ambalo liliwashangaza sana wazazi wangu ambao niliwahi kuwaahidi kuwa sitowaangusha katika masomo yangu.

Baada ya kupita siku kadhaa tangu Haroon amalize chuo, siku moja aliweza kuniambia nimfuate Magomeni majira ya mchana. Niliamua kumkubalia bila kipingamizi chochote nikachukua usafiri wa bajaji na kuanza kuelekea eneo alilokuwa ameniambia nimfuate.

Nilipofika nilimkuta akinisubiria kituoni, aliponiona aliweza kufurahi sana, tukakumbatiana kwa furaha huku tukisindikizana kwa mabusu moto moto halafu tukaanza kuondoka huku mimi nikiwa kama mgeni ninaye mfuata popote pale alipokuwa akienda.

Safari yetu iliishia katika chumba kimoja ambapo tuliweza kuingia. Nilionekana kuwa na furaha wakati wote hasa baada ya kuwa na Haroon mwanaume ambaye nilikuwa nikimpenda sana.

Baada ya kuinga katika chumba kile ambacho kilionekana kuwa na kitanda tu, Haroon alianza kunishikashika kwa kunipapasa mwilini mwangu kiasi kwamba nikajikuta najiwa na hisia za kufanya mapenzi. Niliamua kufanya mapenzi na Haroon huku ule mchezo wake wa kuniingilia kinyume na maumbile akiendelea nao. Tulifanya mapenzi mpaka pale niliposhangaa kuona wanaume wanne wakiingia katika chumba kile. Walikuwa ni wanaume ambao walionekana kuwa katika mavazi sare, mikononi mwao walikuwa wamebeba kamera pamoja na vifaa mbalimbali vya kurekodia picha. Nilipowaona nilianza kuogopa sana huku nikimkumbatia Haroon ambaye kwa wakati huo alionekana kutokuwa na wasiwasi wowote ule.

“Baby,” nilimuita Haroon huku nikiogopa.

Haroon hakunijibu lolote lile bali nilimuona akiwapa ishara wale wanaume ambao walianza kuandaa vifaa vyao tayari kwa kurekodi.

Kilichoendelea hapo ni Haroon kuanza kufanya mapenzi na mimi huku akiniingilia sehemu zote na wale wanaume kurekodi kila kitu. Hakukuwa na maumivu makali ambayo niliwahi kuyapata kama yale niliyoyapata siku hiyo. Wale wanaume walinipiga picha nyingi za uchi na kwa kweli sikuweza kupiga kelele kwani waliniambia endapo ningeweza kufanya hivyo wangeniua. Najuta mimi, najuta ni bora ningekumbuka kupiga kelele ili waniue kama walivyoniambia. Kukaa kwangu kimya kuliweza kuwarahisishia kazi yao ya kurekodi.

Baada ya kupita siku mbili tangu tukio lile lilipoweza kutokea nilianza kuyaona magazeti mbalimbali yakianza kuchapisha habari kuhusiana na tukio lile nililofanyiwa na Haroon. Ilikuwa ni skendo chafu ambayo ilinikuta katika kipindi ambacho nilikuwa nakaribia kufanya mitihani pale chuoni hatimaye bodi ya chuo iliweza kunifukuza hata Wazazi wangu pia baada ya kuzipata habari hizi nao waliweza kunifukuza nyumbani.

(Haroon aliweza kuhama nchi baada ya kuuza video na picha zangu za utupu kwa waandishi wa habari na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mapenzi yetu.)

Niliyaanza maisha ya kutangatanga mitaani rasmi, maisha ya kujiuza kufanyiwa kila aina ya mabaya. Kuna kipindi nilitamani kurudiana na Gilbert mwanaume ambaye alikuwa akinipenda kwa dhati lakini nilipokumbuka yale niliyowahi kumfanyia kwa kweli nilishindwa kumfuata.

Sikujua ni wapi alipo na hata kama ningeweza kujua asingeweza kunisamehe. SISTAHILI KUSAMEHEWA kwa yale yote niliyoyafanya katika maisha yangu, nimeamua kukisubiri kifo changu wenda ndiyo utakuwa mwisho wa kuyavumilia mateso haya ninayoyapitia katika hii dunia isiyokuwa na huruma.


MWISHO.




0 comments:

Post a Comment

Blog