Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

URITHI WA GAIDI

   

MTUNZI: BAHATI MWAMBA



1:HISABATI



Jua lilikuwa linaelekea magharibi na kuelekea kuzamia kabisa ili kutowesha nuru ilioanza kufifia kabisa na kuliacha anga likiwa jeusi na kiza juu yake.


Ilipata saa kumi na mbili kasoro dakika kadhaa!!


Ilikuwa ni furaha kwa watu kadhaa kuukaribisha usiku huku wengi wakiwa njiani kurejea makwao kujumuika na familia zao baada ya kutoka kuhangaika kutwa nzima. Wengine pia walifurahi kwa kuwa muda huu wa usiku kwao ndio ulikuwa muda sahihi kuingia mtaani na kutafuta riziki yao hasa wezi na vibaka lakini pia makahaba.

Furaha ya giza ilikuwa ni njema zaidi kwa watu wenye baa na kumbi za miziki mana kwao giza ndio riziki yao ya halali bila wizi kwa mtu.



Jioni hii haikuwa njema sana kwa mwanadada mrembo aliepata kuwa na miaka thelathini na mbili hadi na nne hivi. Alikuwa ni mdada mwenye familia ya mume na mtoto mmoja aliepata kuwa na miaka kama mitano hadi sita hivi. Lakini pia alikuwa na mume na maisha yao hayakuwa na tabu yoyote. Familia ilijaa upendo na amani lakini pia kipato kwao hakikuwa na utata.


Milo mitatu kamili ilikuwa ni kawaida kwao.


Hakika ilipendeza!!


Lakini hayo yote sasa yalikuwa yametoweka kwa miaka miwili.

Hakuwa na furaha kama ile aliokuwa nayo mwanzo wakati anaingia kwenye mahusiano na mume wake.


Kwanini!


Kwa sababu alikuwa anaishi yeye peke yake na mwanae zaidi ya miaka miwili na miezi kadhaa huku mume wake akiwa ameondoka kwenda kwenye kazi maalumu Nchi za mbali.


Kazi gani, Hakuzijua na hakupaswa kujua.


Ilikuwa ni ahadi ya kurejea kwa miezi sita tu ila sasa ilikuwa ni miaka miwili bila mume wake kurejea na kila aliemuliza hakuwa na jibu la kumpa akaridhika.


Amekufa?


Hata!!


Haiwezi kuwa rahisi hivyo.


Alijakatalia.



Jioni hii ilimkuta mwanadada huyu mwenye urefu na uzuri wa asili akiwa ndani ya gari akitoka Mwenge kurejea nyumbani kwake Kinondoni akitokea ofisini kwake. Ofisi alioianzisha miaka kadhaa nyuma ikiwa inajishugulisha na utafiti wa mambo ya kale.


Yeye alisomea fani hiyo katika chuo kikuu cha Dar es laam.


Alikuwa ni Archeologist.


Mawazo mengi yalikizonga kichwa chake hasa suala la mume wake kutokuwa na mawasiliano nae zaidi ya miaka miwili na ushee.


Je upendo umeisha! Au huko alikoenda kakutana na mabinti wazuri kumliko basi akaamua kulowea kabisa huko?


Haiwezi kuwa!!


Alijikatalia tena.


Mawazo yake yalizidi kumuumiza kichwa chake na kupelekea jasho jepesi limtoke licha ya gari lake kujitahidi kumpa kiyoyozi bila upendeleo.


Foleni nayo ilizidi kumchosha.


Licha ya kuchoka na foleni lakini kwake aliona ni heri zaidi kuliko kurejea nyumbani na kukutana na nyumba tupu isio kuwa na uchangamfu wowote mana ilikuwa ni yake peke yake kwa sababu mume hakuwepo na mwanae wa kiume alikuwa anasoma shule za kulala huko huko hivyo kwake alikuwa ni yeye kama yeye tu.


Karaha ilioje!!.


Alisonya huku fukuto la jaziba na wivu vikimsonga hasa alipofikiria namna mume wake huko aliko anavyowabambia wanawake wa kizungu au kiafrika huku lugha yao ikiwa ni kizungu ama kihindi ama kiarabu ambazo zote mume wake alizimudu vyema kabisa.


Akasonya tena.


***


Ilikuwa ni majira ya saa mbili usiku ndipo alipoingia nyumbani kwake Kinondoni B.O.B ni baada ya kuwa amepita kwa Bonita saloon kuweka Sawa nywele zake ambazo hakuwa amezijali kwa siku kadhaa hivi.


Alipita kuzifunga tu na kuelekea nyumbani kwake.


Alishuka ndani ya gari na kufungua geti kisha akarudi na kuingiza gari ndani ya uzio wa nyumba yake ya kifahali ambayo sasa aliiona kama jehanamu ya nafsi yake.


Ilikuwa ni bora kukaa nje kuliko kurudi nyumbani kwenye nyumba pweke namna ile.


Akachukua makabrasha yake ya kiofisi na kupiga hatua kadhaa kuingia ndani kwake.


Akawasha taa na kujitupa kwenye sofa huku macho yake yakitua ukutani na kujenga kibanda.


Alibaki akiikodolea picha ya mume wake iliokuwa imetundikwa ukutani pale. Mume wake alikuwa ndani ya vazi la kiofisi huku mabegani mwake akiwa amejaa beji tatu zilizotambulisha cheo chake.


Mume wake alikuwa ni ofisa mkubwa wa jeshi la polisi.


Yeye hakuwa anakodolea vyeo vile bali alikuwa anatazama tabasamu adhimu la mume wake pale kwenye picha. Tabasamu ambalo ni nadra kuliona kwenye uso wa mumewe.

Alitazama kidevu cha mumewe kilichokuwa kimejaa ndevu zilizochongwa kwa mtindo wa Timberland.


Hakika alimkumbuka mumewe.


Pembeni ya picha ile pia kulikuwa kuna picha ya mwanae ambae nae kama baba yake alikuwa na tabasamu safi la kitoto huku akiwa ameegemea kwenye mikono imara ya baba yake.


Mwanadada alifumba macho kwa hisia kali. Kisha akanyanyuka na kuelekea maliwatoni, huko alitumia dakika kadhaa kujiswafi na kurejea sebuleni ambapo napo hakukaa sana akaelekea jikoni ambako hakufanya lililompeleka akabaki akiwa amejishika kiuno tu na kulikodolea jiko lake kama mtumishi aliesusiwa upishi.


Uvivu!!


Uvivu wa kupika chakula chake mwenyewe ndio uliomsumbua.


Hakuona umuhimu wa kupika akaamua kufungua jokofu. Humo ndani akakuta chakula cha kopo akakichukua na kukipasha kisha akarudi sebuleni na kukaa kukila huku akishushia na mvinyo mwekundu.


Dakika kadhaa badae uchovu na msongo wa mawazo vikampelekea aelekee chumbani kwake kulala huku akisahau kufunga milango.


Akalala fofofo!.


Ilikuwa yapata usiku wa saa saba kwenda saa nane hivi, mwanamke yule alipata kuhisi kitu ndani ya nyumba yake. Mwanzo alitaka kupuuzia kile alichokihisi akiwa katikati ya usingizi mnene,lakini hisia za kutambua zilizidi kumsumbua.


Akafumbua macho kisha akatulia na kusikilizia kile kilichofanya aamke.

Masikio yake yalinasa mchakacho wa miguu ya kiumbe hai ndani ya nyumba yake.

Haraka nae akaingiza mkono chini ya mto na kuibuka na bastola na kwa kuwa alikuwa amelala na nguo,hivyo hakupata tabu kuinuka na kunyata kuelekea sebuleni.


Hakusikia kitu tena.


Akafumba macho na kutuliza hisia zake.


Bado hakusikia kitu.


Akanyata hadi mlangoni kisha akachungulia sebuleni.


Ajabu!!


Alibutwaika kwa sekunde kadhaa hivi hasa baada ya kugundua aliacha taa zikiwaka kote mle ndani na sasa zinawaka chumbani pekee huku sebuleni kukiwa giza.


Akagwaya!


Mwili ukamsisimka na hofu ikamjaa!.


Mwanamke akatetereka.


Kutoka pale alipokuwa aliendelea kusubiri zaidi ili kumhadaa aliezima taa sebuleni lakini akajishitukia baada ya kukumbuka kuwa pale chumbani kulikuwa kuna mwanga na sebuleni kiza hivyo yeyote ambae angelikuwa amelikaa sebuleni basi alikuwa akimuona yeye ama kivuli chake.


Hata!!


Haraka na kwa wepesi akanesa kwa kutumia ncha za vidole vya miguu na kufikia kiongoza taa na kuzima taa ya chumbani. Wakati akirudi mlangoni, alisikia mlango wa sebuleni ukibamizwa kwa nguvu kumaanisha kuna mtu katoka muda huo.

Kwa wepesi uliokusudiwa, mwanadada yule nae akapiga hatua ndefu na kufika sebuleni kisha kwa kasi ile ile akaufikia mlango wa sebuleni na kuufungua.


Hola!!


Hakuona mtu wala kivuli cha mtu na geti lilikuwa vilevile limefungwa kumanisha hakuna mtu aliepita muda mfupi uliopita.

Mwanadada yule akaona ajaribu kuzunguka nyumba nzima pengine atafanikiwa kuona mtu aliekuwa sebuleni ila alizunguka bila kuona lau dalili ya mtu.

Alibaki akiwa anatazama mlango wa kuingilia ndani na geti kubwa la kuingilia pale ndani.


Akamakinika na kitu na kumbukumbu zilimrejea vyema.


Akasonya kwa gadhabu!!


Hakuwa amemkumbuka askari anaelinda usiku nyumbani kwa kiongozi wake na pia alikumbuka wakati anaingia hakumuona wala kuhisi uwepo wake.


Hatari kabisa!


“Yani najiwaza hadi nasahau mlinzi” alijisemea huku akipiga hatua kwa makini kuelekea kwenye kibanda cha mlinzi.


“Afande! Afande!” aliita mara mbili na aliitikiwa na sauti yake mwenyewe iliokuwa inajirudia kutokana na utulivu wa kifo uliokuwa nyumbani pale. Akazidi kuukaribia mlango wa kibanda cha mlinzi na alipokifikia akatulia na kusikiliza endapo kungekuwa na harakati zozote ndani ya kibanda.


Kimya!!


Hakuna alichokisikia zaidi ya pumzi zake mwenyewe.

Akausukuma taratibu mlango wa kibanda kile kisha akaingia kwa fujo kidogo.


Hakuna alichokikuta!!


Hakukuwa na mlinzi wala dalili za kuwapo mlinzi ndani ya eneo lile na hiyo ilimaaisha kuwa mlinzi hakuwa amefika pale siku hiyo.


Kwanini!!


Hilo hakujua na wala hakutaka kuamini kama limewekwa makusudi ama vipi.


Lakini alibaki na swali moja kichwani ya kuwa inawezekana vipi nyumba ya ofisa mkubwa jeshini tena special operation asahaulike kuletewa mlinzi.


Hata!! Ni ngumu hilo kufanyika. Lakini sasa mlinzi yuko wapi ikiwa haonekani pale ndani?


Mwanadada alipagawa.


Haraka alirudi ndani na moja kwa moja alielekea mezani kulikokuwa na rununu yake ya mkononi na kulitafuta jina la mtu aliemhitaji na kupiga.


“Ndio nakusikiliza!!” iliunguruma sauti ya mtu aliepokea simu upande wa pili ambae alionekana kutoka usingizini.


“Afande leo mlinzi aliandikishwa kufika hapa kwangu?” aliuliza mwanadada.


Ukimya ukapita kidogo.


“Kuna mambo yamebadilika kidogo na mimi sipo ofisini tangu juzi hivyo sijui kama kuna mtu aliekuwa amepangiwa hapo kwenu!!” alijibu mtu yule baada ya kukaa kimya kwa sekunde kadhaa.


Mwanadada akavuta pumzi za kushindwa kuelewa kinachoendelea.


“Kwani kuna tatizo?” alihoji mtu yule baada ya kusikia ukimya ukiwa umetawala kwenye simu.


“Kesho nitakutafuta tuzungumze Afande!” alisema mwanadada.


“Ni ngumu kesho kunipata mana nasafiri kwenda Ufaransa kwenye kikao cha wakuu wa idara za usalama wa jumuia ya madola nikimuwakilisha Mkuu wa jeshi la polisi nchini” alifafanua yule mtu.


“lakini nahisi kuna tatizo, kwanini mlinzi hajafika hapa nyumbani leo!?” aliuliza yule mwanadada .


Mtu wa upande wa pili akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akasema.


“siwezi jua pengine nikupe namba za mtu anaeshugulikia hayo kwa sasa na ambae amekaimu nafasi yangu hadi nikirejea” alisema yule bwana huku akianza kuzitaja namba hizo na alipomaliza alikata simu bila kungoja maelezo zaidi.


Suala lile likamchanganya kidogo mwanadada yule na kumuacha na maswali mengi bila majibu. Ilikuwa ni tabia mpya kuoneshwa na mtu yule tangu amfahamu na pia alikuwa ni rafiki wa karibu wa familia yake licha ya mtu yule kuwa ni kiongozi wa mumewe kikazi.


Akaguna tu na kuendelea kujishugulisha kuipiga namba aliopewa dakika chache zilizopita.


Simu ilianza kuita kwa fujo na punde ikapokelewa.


“Remi Haji; nakusikiliza”


Ebanaee! Maajabu.


Remi alitamani kukata simu dakika hiyo na kutafakari upya alilosikia. Mtu yule aliekaimu alikuwa anamjua jina lake kwa ufasaha kabisa!


Alimjuaje sasa na kwanini amjue ikiwa yeye si mfanyakazi wa idara yoyote ya jeshi la polisi?


Hakika ni maswali yaliomuacha kinywa wazi na alijikuta akikosa la kusema kwa dakika moja nzima.


“Heloo Remi!!” mtu yule aliita kwa madaha jina la Remi baada ya kuona ukimya umetawala.


“aah nimepewa namba na Kamishina wa jeshi la polisi Zenge wa Zenge.” Aliongea kwa kirefu Remi.


“elekea kwenye suala lililokufanya upige simu tafadhali ninahitaji kupumzika!” mtu yule aliekaimu nafasi ya Zenge wa Zenge alisema kwa utulivu wa majivuno.


“Hapa kwangu hadi sasa sijaona mlinzi akifika wala kuripoti nilitaka kujua nini tatizo tafadhali” aliuliza Remi.


“Kabla ya kunipigia mimi usiku huu ulipaswa kuwapigia maafisa wanaoshugulika na malindo ya wakuu wao, mimi ni mtu mkubwa sana kuulizwa malindo usiku wa manani namna hii” aling’aka bwana yule.


“Nina sababu afande za kukutafuta wewe na…” alikatishwa kusema Remi.


“Hiyo sababu ilikuwa zamani ila sio sasa. Kwa sasa utaratibu unafuatwa kuanzia ngazi za chini binti” alisema yule bwana kwa ujivuni.


Remi alibaki akiwa amezubaa kwa fadhaa na simu sikioni.


Hakupata kuona mambo haya hapo kabla.


“Naomba kesho ufike ofisini kwangu nina ujumbe” alisema bwana yule na kukata simu.


Remi alibaki akiwa hana hamu na majibu ya ujivuni ya kamishina yule wa jeshi la polisi nchini.


Akaitoa simu sikioni na kulitafuta tena jina la Zenge wa Zenge ili apige lakini alikutana na jibu lililozidi kumuacha wazi kichwani.


Hakuwa akipatikana!


Haijawahi kutokea akazima simu tangu wafahamiane miaka kadhaa nyuma wakati akiwa katika misukosuko ya Ukimbizi ndani ya nchi ya Tanzania kisa ambacho kiliandikwa vyema na mwandishi wa riwaya Bwana Bahati Mwamba.


Sasa baada ya muda wote huo eti Kamishina anazima simu.


Kuna namna si bure.


****


Remi Haji Makame; usingizi ulimpaa na hapo akakumbuka kitu baada ya kushindwa kumtafakari vvyema Zenge wa Zenge.


Ujumbe!!


Alikumbuka mchana aliona ujumbe kutoka kwa mwandishi ambae pia aligeuka kuwa rafiki wa familia hasa baada ya kuwa anaandika mikasa mingi inayomhusu mume wake. Aliupokea ujumbe wa Davis Minja ila hakushugulika nao wakati ule.


Aliufungua!


“Siku ya sita sasa kuna gari silielewi nyuma yangu mumeo sikumpata!” ujumbe ulisomeka hivyo.


Sasa hii tena inakuwaje! Alijiuliza Remi na uso wake ulielekea juu ya ukutani na kuitazama saa.

Mishale iliendelea kuwa mashariki kumaanisha ni usiku wa maanani.

Alizima taa na kuacha usiku upite akiwa amekaa sebuleni kuongojea kuona kama mtu aliemtembelea usiku ule atarejea ili amjibu kwa nini alimtembelea kinyamela na alifuata nini.


Lakini kitu kimoja hakujua ni kuwa hesabu zake zilikuwa nyuma ya hesabu za mtu aliemvizia usiku na kumwacha bila kumduhuru.


Mtu yule hakurejea tena hadi mapambazuko.


Na yakawa ni mapambazuko ya Kihisabati; hesabu za akili.


****


Ahsubuhi ilimkuta Remi akiwa amelala kwenye sofa na bastola yake mkononi. Milio ya ndege waliokuwa juu ya miti ndio waliomsitua kutoka kwenye tope la usingizi wa mang’amung’amu.


Alijisonya bila sababu na kuelekea chumbani kwake ambapo moja kwa moja alielekea maliwatoni na kutumia dakika kumi na ushee kujiswafi kisha akarejea chumbani kwake ambapo hakumaliza muda murefu akawa tayari amekwisha kujiweka sawa na kuvaa suruali ya buluu mpauko na T-shirt nyeusi kisha akachukua mkoba wake wenye nyaraka za kiofisi na kuweka bastola yake kisha akaelekea sebuleni ambako alichukua funguo za gari na kutoka nje ambako alichukua gari lake jeusi aina ya Toyota Nadia na kisha akajifungulia geti na kutoka nje na alipokwisha kutoka akarudi tena kwa miguu na kulifunga kisha akaondoka kwa mwendo wa wastani tu.


Hakufika mbali kwa kupitia vioo vya gari ama side mirror akaona jambo.


Kutoka kwenye kona moja ya nyumba yake aliona mtu alievaa kofia akichepuka na kuivuka barabara kwa kasi na kupotelea kwenye nyumba za watu mtaani pale.


Akili yake ilimwambia mtu yule hakupita eneo lile kwa bahati mbaya au labda ni mkazi wa eneo lile.

Hakika akili yake ilikataa kukubaliana na hilo.


Alikuwa pale anafanya nini na kwanini akimbie kwa kujificha namna ile? Au ndie aliemtembelea usiku na…

Alibaki kutikisa kichwa tu bila kujua kama kuna kusudi baya juu yake ama ni akili yake tu.


Kamwe hakujua mana ya matukio yote yale yalioanza kumwandama siku kadhaa nyuma.


Aliendesha gari lake huku kila mara akitizama nyuma kuona kama kuna jambo lolote lisilo la kawaida.


Hakuona!!


Safari yake ilimfikisha hadi makao makuu ya jeshi la polisi na alipokwisha kufika akapaki gari lake eneo maalumu kisha akaomba kuonana Naibu kamishina. Alioneshwa zilipo ofisi zake.


Hatua zake zilimfikisha hadi kwenye korido pana iliokuwa na ofisi nyingi kushoto na kulia. Akasoma namba za ofisi zile na vitengo vyake hadi pale macho yake yaliponasa jina la ofisi alioihitaji. Ilikuwa ni ofisi ya kitengo maalumu yani special operesheni.

Akagonga mlangoni na kukaribishwa kuingia.


Alikaribishwa na uturi ghali ulionyanyasa pua zake kwa harufu kali. Lakini macho yake hayakuhadaika na na harufu za pua bali yalimakinika kumtazama mtu aliekuwa amekaa kwenye kiti nyuma ya meza na kibao kikiwa mbele yake kilichonasibisha jina lake.


Bwana yule aliitwa P. Kagoshima ambae ndie alikuwa Naibu kamishina wa jeshi la polisi kazi maalumu aliekaimu nafasi ya Kamishina Zenge wa Zenge. Bwana yule hakuonekana kuwa na umri wa kutisha ila umri wake aliukadiria kuwa kati ya miaka arobaini na nne hadi hamsini kasoro. Alikuwa ni mrefu wa wastani ila hakufikia urefu wa Mumewe ama Kamishina Zenge wa Zenge. Sura yake ilionesha ni mtu mjivuni sana lakini mbali na hayo Remi aliona kitu ndani ya macho ya yule bwana. Remi aliona tamaa ya kifisi imejaa kwenye mboni za macho ya Kagoshima ila hakujua ni tamaa ya nini, Pesa ama kitu kingine zaidi ila ilitosha tu kujua yule bwana ni mwenye ujivuni na tamaa.


“Naitwa Remi” alijitambulisha Remi.


“Ooh karibu bibie!” alisema Naibu kamishina Kagoshima huku akiachia tabasamu la upande na kuegemea kiti kilichopokea mwili wake wa kikakamavu.


“Nimeitikia wito Afande!!” alisema Remi huku akitizama saa yake ili kuhakikisha yupo ndani ya muda na sikuchelewa pale ofisini.


“OK! Bila shaka mumeo ni ofisa wa jeshi la polisi!” alihoji Kagoshima huku akijishugulisha kupekua makablasha kadhaa yaliokuwa mezani kwake.


Remi hakumjibu.


Kagoshima aliendelea..


“Na ndie Haji Makame!”


“Afande nadhani yote hayo unayajua na unapaswa kujikita kwenye mada tafadhali” alisema Remi kwa kukereka kidogo.


N. Kamishina alitabasamu kivivu huku akichukua kipande cha gazeti na kukitupia karibu na mikono ya Remi ambae alikuwa amekaa na kuweka mikono yake juu ya meza.


Remi alikichukua kipande kile ambacho kilikuwa ni cha ukurasa wa mbele wa gazeti la Daily News la Marekani. Remi alishuhudia picha mbili kubwa na picha moja ndogo. Picha ndogo ilikuwa ni ya mtu mgeni machoni pake na picha moja kubwa nayo hakuifahamu kabisa lakini picha nyingine ilikuwa ni picha ya mumewe Haji Makame licha ya kuwa na mabadiliko makubwa katika uso wake,lakini kamwe hakuwahi kumsahau mwanaume wa maisha yake.


Akasoma kichwa cha habari cha kipande kile cha gazeti ambacho kilikuwa kimeandikwa kingereza.


Mwili ukamwingia ubaridi kwa alichokielewa. Alimtizama Kagoshima; na alikutana na uso makini ukimtizama kisha akarejesha macho yake kwenye kipande kile.


Tafsiri Kiswahili.


“Tanzania yazidi kuzalisha magaidi, Wawili wasakwa na marekani na mmoja atoweka Guantanamo”


Yalikuwa ni maelezo machache lakini yenye kuchoma akili za watu.


“Sijaelewa Afande!” alisema Remi huku dhahiri akionekana kupagawa.

Naibu Kamishina P. Kagoshima alisogeza kiti huku akiguna kusafisha koo lake na mkono wake wa kushoto akikichukua kipande kile cha gazeti kutoka mikononi mwa Remi.


“Huyu anaitwa Ahmed Twalibu” alisema huku akinyooshea picha ndogo ya jamaa mweusi alieonekana kukomaa sura yake licha ya uso wake kuonesha umaridadi wake vyema.


“Na huyu anaitwa Aahmed Boka Ghailani” alionyeshea picha kubwa ya mwanaume ambae nae hakutofautiana sana na yule aliekuwa kwenye picha ndogo licha ya kuwa walionekana kuwa ni wanaume wawili tofauti.


“Na huyu ni Haji Makame” alisema tena huku akielekeza kidole kwenye picha ya mwanaume aliekuwa amenyoa upara na kuchonga ndevu zake kwa mtindo wa Timberland. Licha ya kunyoa ambayo si tabia alioizoea Remi; lakini ndevu zilimhakikishia yule ni mumewe kipenzi Haji Makame.


Gaidi!!


Ameanza lini ugaidi hadi kutafutwa na serikali ya Marekani!? Na kwanini ahusishwe na Ahmed Twalibu ambae siku za nyuma aliaminika ameuwawa kwenye shambulizi lililotekelezwa na Wataleban walishambulia chopa aliokuwamo?


Na vipi alipona na kuhusishwa tena na ugaidi sambamba na mumewe!?


Ebanae!!


Yalikuwa ni maswali bila majibu na hesabu ziligoma kuunganisha kachumbari ile kichwani mwa Remi ambae siku zote alijua mumewe ni mstari wa mbele kupigania masilahi ya taifa kwa kupambana na ugaidi ama uvunjaji wa sheria wa aina yoyote!


Hata haiwezekani.

Remi alijakatalia kata kata.


“eeh! Hapa kuna watu wawili wanafanana majina kwa kutamkwa ila herufi tofauti yani Ahmed na Aahmed .” Alisema tena Kagoshima huku akitoa picha nyingine kubwa kidogo ambayo nayo aliitupia kwenye meza na kuchukuliwa na Remi.


Picha ile ilifanana sawa sawa na picha ndogo ya mtu alieitwa Ahmed Twalibu aliesemekana kutoroka Guantanamo na sasa anatafutwa na serikali ya Marekani.


Remi alimtizama Kagoshima kwa macho ya kuuliza.


“Ok. Huyo bwana anaedaiwa kuitwa Ahmed Reality ambae unaona picha yake hapo,tumefuatilia na kugundua sio Ahmed Reality ila ni amewahi kuwa askari wa jeshi la polisi kitengo maalumu kama mumeo anaitwa Honda Makubi. Swali tunalojiuliza ni kwanini Marekani iseme ilikuwa nae gerezani kwake na ametoroka wakati miaka miwili nyuma alikuwa anahudumu hapa nchini? Lakini pia Ahmed wa kweli anaweza kuwa miongoni mwa hawa watatu yani huyu Aahmed Ghailani; Haji Makame ama Honda Makubi na hapa anaetafutwa sana ni Ahmed Twalibu ambae nasadiki ndie huyu Aahmed” alisema Naibu kamishina Kagoshima.


Remi alibaki akimtizama akiwa hajui ni kwanini anahusishwa katika jambo lile tena kwa kuelezwa kwa marefu na mapana na kiongozi mkubwa wa jeshi la polisi nchini.


“Kwanini unanambia yote haya na mimi nahusikaje na hili sakata!” alivunja ukimya Remi.


Kagoshima aliegemea kiti chake kisha akamtazama Remi kwa tuo huku akiwa amefumbata mikono yake pamoja.


“una hakika huhusiki?” aliuliza Kagoshima.


Jama!!


Remi alibutwaika kwa kauli ile ya ofisa yule wa jeshi la polisi.


“Nahusika vipi na mambo haya ambayo ni kama hadithi za kufikirika?” alihoji Remi.


“Inaonesha mumeo anashirikiana na magaidi muda mrefu kidogo na wewe yaezekana unajua hiko kitu na ndio mana unahusika katika sakata hili mwanamke!” alisema Kagoshima huku akilambalamba midomo yake kama wafanyavyo wasanii njaa wahojiwapo na vituo vya runinga.


“Huko ni kumkosea mume wangu kabisa na kamwe hajawahi kuwa gaidi. Yani mazuri yote alioyafanya leo mnamwita gaidi?” alisema Remi huku akivuruga nywele zake kichwani kwa mikono yake.

Alihisi kichwa kinawasha kwa taarifa zile.


“Kwanza nataka nikwambie mumeo hajawahi kuwa ofisa wa jeshi la polisi na hata katika rekodi zetu hayumo,hivyo inamaanisha hajawahi kuwa ofisa kabisa na hatumtambui Haji Makame na cheo chake na tunamhesabu kama mhujumu nchi tu aliejichomeka jeshini kutimiza matakwa yake ya kigaidi” Jibu la moto kwa Remi Makame.


“Hajawahi!? Inamaana, dah..” alishindwa kuelewa aseme nini katika dakika ile Remi. Alibaki akiwa ameachama mdomo akiwa hajui ama alie ama acheke ama tabasamu, mana hakuona kama kuna utani katika uso wa Kagoshima ambae ni ofisa mkubwa tu wa jeshi la polisi.


Sasa alielewa ni kwanini hakukuta mlinzi usiku wa jana nyumbani kwake.


“Mengine inabidi utuachie kama serikali tuyashugulikie ila kwa sasa taarifa hii inaweza kukuweka pabaya ama pazuri mrembo” alisema Kagoshima huku akikenua meno kama ngiri maji.


Haaa!!

Urembo tena unaingiaje katika sakata hili!


Remi alisimama kisha akauliza.


“kwanini inaweza niweka pabaya ama pazuri?”


“ukimficha mumeo na washirika wake itakuweka pabaya ila ukitoa taarifa utakuwa pazuri” alisema Kagoshima huku akitoa kadi mfukoni mwake na kumpa Remi.


“Ukiwa na shida utanipigia nami nitakusaidia muda wowote” alisema huku akiona Remi anaitazama ile kadi.


“sina hakika kama itafikia hatua ya kukuomba msaada” alisema Remi huku akiisunda kadi ile mkobani mwake.


“unahakika hutauhitaji msaada wangu?” alihoji Naibu Kamishina huku akitabasamu. Remi alimtizama bila kumjibu na kuondoka ofisini mule huku kichwa kikimuwaka moto kwa taarifa zile.


Hakika alichanganyikiwa.


Dakika kadhaa badae alikuwa ndani ya gari lake na lengo lilikuwa ni kuelekea Mwenge zilipo ofisi zake za utafiti wa mambo ya kale.


Tatizo hakujua huko nako ni moto mwingine utakao acha akili yake ikiwaka. Ila hakujua na angejua hakika angejirudia kwake tu akalale.


***



Tatizo hakujua huko nako ni moto mwingine utakao acha akili yake ikiwaka. Ila hakujua na angejua hakika angejirudia kwake tu akalale.


***


Wakati Remi akiingia kwenye lango la ofisi yake alikutana na hekaheka ambazo hakujua chanzo ni nini. Ofisi zake zilikuwa ni kwenye nyumba ya kawaida tu ambayo ilijengwa maalumu kwa kazi za kiofisi na pembeni yake kulikuwa kuna gorofa kubwa lenye ofisi nyingine pia. Kampuni yake iliitwa REMI ARCH COMPANY LIMITED. Ilishugulika na utafiti wa mambo ya kale fani ambayo aliipenda sana.

Hekaheka zile zilianzia nje ambako kulikuwa kuna askari wa jeshi la polisi wenye silaha za moto ambao walipumuona wala hawakujali,waliendelea kuweka usalama eneo lile lakini pia alipoingia ndani alikuta wafanyakazi wake wote walikuwa wamekusanywa na kuwekwa pamoja huku kukiwa na maafisa kadhaa wa jeshi la polisi na wale wa ukusanyaji mapato yani TRA.

Alishindwa kuelewa kuna nini pale ofisini kwake licha ya kuona heka heka zile. Wafanyakazi wake nao walipomuona wakaelekeza macho yao kwake huku kila jicho likisadifu yalio myoyoni mwao.


Remi alielekea moja kwa moja kwa askari mmoja aliekuwa na cheo cha sajini na alionekana ndie kiongozi wa kundi na heka heka zile.


“Afande shida nini hapa!?” aliuliza kwa kihoro Remi.


Afande yule alimtizama kuanzia juu hadi chini kisha nae akauliza bila kutoa jibu.


“wewe ndie mkurugenzi hapa?”


“Ndio. Nieleze shida tafadhali!!” alisema Remi.


“Tusogee pembeni kidogo” alisema Sajini yule huku akimshika mkono Remi na kusogea nae pembeni.


“Kuna mambo mawili yanaendelea hapa. Mosi; inasemekana hujalipa kodi yako ofisi ya mapato kwa miaka kadhaa ila hilo silo lililotuweka hapa sisi maofisa wa polisi. Lilituweka hapa ni kuwa tulipigiwa simu ahsubuhi kabisa kwamba kumetokea mvurugano hapa ofisini kwako na kupelekea mwandishi wa riwaya Tanzania bwana Davis Minja kuchukuliwa na watu wasio fahamika na kuua mlinzi wako” alieleza Sajini aliejitambulisha kwa jina la Vengu.


E bana ee!!


Remi alihisi moyo unataka kuchomoka kwa kasi ya mdundo wa mapigo yake. Alitamani aangue kilio ili akinyamaza mauzauza yale yakatike ila haikuwezekana.


Nini sababu ya yote haya?


Mume gaidi na sasa anaambiwa mtu katekwa ofisini na mauaji kutendeka ofisini kwake na bado anadaiwa kodi na mawakala wa ukusanyaji na ofisi tayari zinapigwa kufuli.


Aah mkosi gani huu tena kwa Remi.


Hakika ni kipindi kigumu kuelezeka. Remi chozi lilimtoka.


“aah inapaswa tukuhoji kidogo dada kisha tukuache umalizane na maofisa wa TRA.” Alisema sajini Vengu.


Remi alipandisha pumzi na kuzishusha kwa mkupuo mara mbili kisha akayarudisha macho yake kwa Sajini.


“Eeh!! Unamahusiano gani na Davis Minja?” aliuliza Sajini.


“Ni rafiki wa familia”


“kwa muda gani”


“Muda mrefu”


“aliwahi kukwambia chochote kuhusu upande wa adui yake?”


“Hapana!!”


“unahisi kwanini ametekwa ofisini kwako?”



“siwezi kujua!”


“unahisi kwanini alikuwa hapa ahsubuhi sana badala ya kuja kwako!”


“sijui!”


“sawa sisi kwa sasa hatuna maswali mengi. Badae tutakuhitaji kituoni Mwinjuma uje kutoa maelezo zaidi lakini kwa sasa tutaendelea na utaratibu wa kipolisi kuukagua mwili wa mlinzi wako” alisema sajini huku akiondoka na kumuacha Remi akiwa amesimama bila kujua ni kipi cha kufanya.


Mambo yanayotokea yanachanganya.


Akiwa bado amesimama pale mara mtu mwingine aliekuwa amevaa suti akamfuata. Bila salamu akasema.


“Ofisi yako inakashifa ya kutokulipa kodi serikalini hivyo tutaziondoa kufuli na kukuacha uendelee na shuguli zako ukisafisha madeni yako”


Remi alimtizama bwana yule ambae hakuonekana kujali kutazamwa kule.


“wiki jana ndio nimetoka kufanya malipo ya makadirio ya kodi sasa inakuwaje nadaiwa?”


“kwa hiyo unataka kusema hapa sisi tumekosea kufika? Unadhani wewe ni mjanja kuliko serikali?” alibwata bwana kitambi yule alieonekana kuwa na mwili wa rushwa.



“Nyaraka zote ninazo sasa sijui nyie mna ofisi ngapi ambazo mnafanyia malipo hadi mshindwe kujua nimekuwa mlipaji tangu nisajili kampuni hii” Remi nae alimaka.


“Mwanamke angalia usije kujibia kituo cha polisi. Wewe ni sawa na mhujumu uchumi hivyo huna haki ya kuhoji lolote kwa sasa zaidi ya kuclear madeni yako na sisi tufungue ofisi zako” bwana kitambi alizungumza kwa majigambo makubwa.


“Nyaraka zipo aisee usinitishe na hili litakugarimu bazazi wewe” Remi nae alifoka,hakutaka kupelekeshwa kama tiara wakati ana uhakika kabisa amekuwa akilipa serikalini tangu aliposajili ofisi yake kuwa kampuni kwa ajili ya utafiti wa kujitegemea wa mambo ya kale.


Bwana kitambi alicheka kwa dhihaka kisha taratibu akasema kama vile asietaka wengine wasikie anachozungumza na Remi.


“Itakugarimu hiyo jeuri yako mwanamke na huna pa kukimbilia safari hii”


Ebana eeh


Huyu bwana anazungumza nini. Safari hii safari nyingine ilikuwa wapi!


Jama yakoje mambo haya?

Alijiuliza Remi huku ile sauti ya bwana kitambi ikijirudia kichwani mwake.


“Sauti hii nimepata kuisikia wapi?” alojiuliza mara nyingi bila kupata jibu na alipokuja kurudisha macho yake pale alipokuwa bwana kitambi hakumuona zaidi aliona wafanyakazi wake wakitoka pale walipokuwa na kuanza kumfuata. Askari polisi na maafisa wa mapato nao walikuwa wameanza kuondoka pale ofisini.


Hakika zilikuwa ni hesabu ambazo kamwe Remi hakujua njia ya kuzikokotoa.


Hisabati ilifanya kazi na hakika aliona anaenda kupata zero yenye masikio makubwa.


*****


Jambo la kwanza aliloona kwake linafaa ni kurudi nyumbani kwake kuzitafuta nyaraka za malipo ya kodi ili aelekee zilipo ofisi za mapato na kujua undani wa suala lile kwa marefu na mapana.

Alifungua geti na kuingiza gari kisha haraka akaelekea ndani ambapo moja kwa moja alielekea kwenye kabati maalumu la kuhifadhia nyaraka muhimu za kiofisi.


Kwa pupa aliokuwa nayo hakujihangaisha hata kudadisi nyumba yake,alipitiliza moja kwa moja kwenye chumba maalumu cha kuhifadhia nyaraka muhimu.


Alipofungua mlango wa chumba kile alishangaa kwa alichokiona.


Vitabu vilikuwa vimesambaratika hovyo, nyaraka zilizokuwa kwenye karatasi zilikuwa zimechanguka hovyo na kabati lilikuwa wazi.


Upekuzi ulifanyika!!


Ni nani sasa anaeweza kuingia ndani na kupekua kiasi hiki!


Alijiuliza bila kupata jibu.


Haraka akarejea sebuleni,na ndipo aliposhuhudia mtafaruku wa ajabu ambao alishindwa kuelewa wakati anaingia ni nini kilisababisha hakuona mambo yale. Kila sehemu ilikuwa imeguswa hovyohovyo na kupelekea baadhi ya mapambo kusambaratika hovyo mule ndani; sofa zilikuwa zimendolewa sehemu yake na kusogezwa pembeni na hata zulia zito lililokuwa chini nalo lilikuwa limebinuliwa. Alipotizama ukutani aliona picha zikiwa zimegeuzwa hovyo kabisa na moja ya picha zake ilikuwa inaamandishi madogo yaliomfanya amakinike. Akasogea taratibu na kwenda kuyasoma.


“it’s showtime!!” aliyarudia mara mbili maandishi yale na taratibu akaona kuna mchezo wa matukio yale na ule ni ujumbe maalumu kwake na hakika alikubali ile ilikuwa ni showtime kwake, lakini swali lilibaki linakizunguka kichwa chake.


Baada ya showtime ni nini kitafuata ama tukio gani? Na nini lengo hasa. Je ni ugaidi wa mumewe ama ni kisasi cha watu juu yake? Watu gani?.


Yalikuwa ni maswali mengi kwa mtu tofauti na Remi ila kwa Remi lilikuwa ni swali moja lenye jibu moja na vipengele vyake.

Remi nae aliandika kwa vidole vyake lile neno showtime kisha akaingiza mkono mfukoni na kuchukua kalamu ndogo ambayo huiweka kwa dharura na kuandika chini ya maandishi yale neno “mathematics; Hisabati” aliandka kwa kingereza kisha kiswahili. Alikuwa na maana ya kwamba wao watacheza mchezo wa kufurahisha na kukarahisha ila yeye atapiga hesabu kujua mbinu za mchezo wao. Remi hakuwa na akili za mtu wa kawaida; Remi aliamua kutulia na kufikiri zaidi, alijionya kuhamaki mana kungemtoa sadaka kwa wacheza mchezo wa utangulizi Showtime.


Akaiacha ile picha pale sebuleni na kurejea kwenye chumba kile cha kuhifadhia nyaraka.


Vilevile alivyokuta kumepekuliwa,nae akaamua kupekua kutafuta nyaraka za kampuni yake.


Kila alichogusa hakikuwa anachokihitaji.


Jama!!


Ziko wapi nyaraka hizo?


Alitafuta kila pahali bila kupata kile alichokitaka. Nyaraka hazikuwepo na hakuziona kabisa. Kumbukumbu zake zilimwambia aliweka mule kabatini na si sehemu nyingine. Hakuona hata risiti za malipo.

Haraka akatoka mle chumbani na kuelekea kwenye chumba chake cha kulala nako alikuta mkono wa mtu umepita na kufungua droo za kitanda na meza ya kujipambia. Remi alishika kiuno na alikubali kweli ilikuwa ni mchezo wa utangulizi. Waliamua kumkwamisha kwa kuchukua nyaraka za kampuni yake.


Lakini kwa nini?


Hakujua sababu ya yale yote ni nini na wala akili yake haikutaka kuyaunganisha na tuhuma za mumewe ambae kwa sasa lau alijua yu mzima na anatafutwa kwa tuhuma za ugaidi.


Ugaidi?


Hapana mume wangu hawezi kuwa gaidi. Alijikatalia.


Ooh shit!! Akamaka huku akitoka chumbani na kurudi sebuleni. Alikuwa amekumbuka matukio yaliotokea ofisini kwake.


Kwanza mauaji pili kutekwa kwa Davis Minja.


Kwanini ofisini kwangu na kwanini Davis alienda ofisini na si kunipigia simu ama kunijia hapa nyumbani?


Hakukuwa na wa kumjibu maswali yake na hesabu zake ziligoma kuyaunganisha matukio ili apate njia ya utatuzi, alibaki mshuhudiaji wa mchezo ule wa utangulizi huku akiwa hajui onyesho kamili litakuwaje.


Remi alitatizika.


****


Hakutaka kuendelea kukaa pale alitoka na kuingia kwenye gari yake na kuelekea zilipo ofisi za ukusanyaji mapato posta na jua lilikaribia saa nane alasiri.


Saa nane na dakika arobaini na tano; saa tisa kasoro dakika kumi na tano ilimkuta akiwa makao makuu ya kitengo cha ukusanyaji mapato na tayari mtu wa Tehama alikuwa anashugulikia swala lake kwenye vibarizi kadhaa vilivyokuwa mle ofisini.


“Dada tunasikitika taarifa zako hazionekani kabisa na inaonekana mara ya mwisho kulipia ni wakati unachukua leseni ya uendeshaji wa kampuni yako” alisema yule bwana huku macho yake yakiwa kwenye kibarizi(kompyuta).


Ajabu hii!!


“Lakini siku chache tu ndio nimetoka kufanya malipo na makadirio mapya!” alijitetea Remi.


“Hapana dada; takwimu zetu hazionyeshi jina la kampuni yako katika orodha ya walipaji ila lipo kwenye orodha ya watu wanaodaiwa na mamlaka ya mapato nchini” alifafanua yule bwana ambae kitambulisho chake kilimtambulisha kwa ubini wa Pius Kangwa.


Remi alivuta pumzi ndefu na kuzishusha kwa mkupuo.


“Unahisi kimefanyika nini hadi takwimu za kampuni yangu hazionekani?” hatimae Remi aliuliza.


“Ni ngumu kuelewa ila sina hakika kama ni mchezo umefanyika ili kukuhujumu, hatuna wafanyakazi wa aina hiyo katika ofisi zetu zote nchi nzima dada” alifafanua Pius.


“ Lakini nina uhakika na ninachokisema” alisema Remi.


“Kama unahakika,unazo risiti za malipo ya Bank na mhuri wa uthibitisho?” aliuliza Pius kangwa.


Lilikuwa swali muhimu na wakati muhimu ila hesabu za Remi hazikuwa na jibu la swali lile. Hesabu ziligoma.


“Hapana. Kwa sasa sina” alijibu kwa kubabaika Remi.


“Hauna kabisa Dada; na kama unazo njoo nazo kesho tafadhali” alisema kijana yule.


“kwani Bank nilikolipia hakujaunganishwa na mfumo wenu ili kutambua moja kwa moja walipaji?” alihoji Remi.


“Ukiona hapa hakuna takwimu za kumbukumbu,basi jua hata huko bank hakuna. Dada jaribu kuwa na muda wa kuwa unaleta mwenyewe usiwe unatuma watu” alishauri Pius.


“Nope!! Huwa naleta mwenyewe na nilifanya miamala mwenyewe” Remi alijibu.


“Basi utakuwa unaugua Schizophrenia dada angu, wahi hospital”

Alisema yule jamaa.


“Whaat! Umesema nini vile!” alimaka Remi na kumfanya Pius aruke juu ya kiti na kumkodolea macho Remi.


“Samahani dada,sikumanisha hivyo ulivyodhania ila nimekushauri tu mana ukiugua ugonjwa huu wa schizophrenia unakuwa unapoteza kumbukumbu” alifafanua kwa tabu Pius.


Remi alibaki akimtizama bwana mdogo yule huku akijiuliza maswali mawili kichwani bila kusema lolote.


Katamka bahati mbaya ama makusudi? Alijiuliza kimya kimya. Ugonjwa huo ndio uliomtesa kwenye mkasa ulioandikwa na Davis Minja; na sasa anatajiwa aina ya ugonjwa ule ule na kijana wa mamlaka ya ukusanyaji mapato nchini.


Kichwa kiliwaka moto na bila kusema lolote akachukua mkoba wake na kuutundika begani na kuanza kushuka chini akitokea ndani ya ofisi ile ya kusikiliza shida za wateja ndani ya mamlaka ile.


Wakati anamalizia ngazi ili atoke ndani ya ofisi zile, macho yake yalimuona Kitambi nae akikaribia pale.


Wote wakasimama.


“kama ulikuja kulipa ni heri ila kama ulikuja kuhakikisha madai yetu umekosea sana” alisema yule bwana kitambi waliekutana kwa mara ya kwanza ofisini kwake Mwenge.


Remi hakujibu tuhuma zile ila akili yake ilicheza kidalipo kuikumbuka sauti ile aliwahi kuisikiliza wapi kabla ya siku ile.


Kumbukumbu haikumpa ushirikiano licha ya kuhisi kabisa sauti ile si ngeni kwake.


Hakujishugulisha zaidi akamkwepa na kutaka kuendelea na safari.


“It’s showtime baby!!” Kitambi alitamka kwa madaha kama jingo ya radio free Africa mwanza.

Remi aliganda kama sanamu huku akizisikia hatua nzito za bwana Kitambi zikielekea juu alikotokea yeye.


Ebana eeh hili lilikuwa sawa na somo la hisabati gumu kulielewa na linahitaji utulivu na usikivu kulifaulu.


****







“It’s showtime baby!!” Kitambi alitamka kwa madaha kama jingo ya radio free Africa mwanza.

Remi aliganda kama sanamu huku akizisikia hatua nzito za bwana Kitambi zikielekea juu alikotokea yeye.


Ebana eeh hili lilikuwa sawa na somo la hisabati gumu kulielewa na linahitaji utulivu na usikivu kulifaulu.


****


MOGADISHU – SOMALIA.


Pembezoni kidogo mwa pwani ya mji wa Mogadishu ndani ya Somalia kulikuwa kuna tukio linaendelea kwa umakini wa hali ya juu bila kuwa na bughudha ama kelele yoyote. Kulikuwa kuna makundi mawili yaliokuwa yanafanya jambo katika barabara ya Old Mogadishu pembeni kidogo mwa fukwe ya Second Lido. Kutoka pahali fulani ndani ya hoteli ya Lugo kulikuwa kuna watu waliokuwa wamevaa kanzu za bei mbaya na vibandiko vya bei mbaya vile vile. Miongoni mwa watu wale kuna wawili waliokuwa wanakazi maalumu ambayo mmoja alikuwa na kiona mbali na kazi yake ilikuwa ni kuona mjongeo wa kile kilichowaweka pale. Lakini pia kulikuwa na mtu mwingine ambae alikuwa na mzigo mkubwa mgongoni ambao ulikuwa na mawimbi maalumu ya kupokelea simu za upepo kutoka kwa watu maalumu waliokuwa wamepandikwa kwenye barabara ile ya old Mogadishu.


Nyuma ya vijana wale kulikuwa kuna walinzi zaidi ya kumi ambao walihakikisha ulinzi eneo lile huku wakionekana kujali zaidi usalama wa watu wawili waliokuwa wamekaa kwenye viti ndani ya chumba kile cha gorofa tatu katika hotel ya Lugo.


Watu wale wawili walionekana kufuatilia kwa makini kila taarifa waliopewa na vijana wao kutokea nje ya eneo lile na kunaswa na mawimbi maalumu yaliokuwa katika mtambo uliokuwa umekaa sawia mwa kijana shababi aliekuwa mle ndani.


“Kabla ya dakika kumi ndege ataangusha YAI kiotani” ilisikika sauti kupitia simu ya upepo mle ndani na hapo mmoja ya watu waliokuwa wamekaa ambae alionekana ni kijana zaidi kuliko mwingine alinyanyuka na kuelekea dirishani kisha akanyoosha mkono na kijana aliekuwa na kiona mbali alimpatia nae akakipachika usoni mwake.


“Wapo ndege watatu, hatujui YAI lipo kwa ndege gani” Alisema yule jamaa kijana aliesimama dirishani na kiona mbali.


Hakuna aliemjibu nae hakujali akaendelea..


“Wamarekani ni wajanja sana,sina hakika kama watatupa YAI kamili”


Kauli ile ilimyanyua bwana aliekuwa amekaa peke yake nae akasogea karibu na dirisha na huku nyuma walinzi nao walisogea eneo lile kuhakikisha usalama zaidi.


“Unahisi wanaweza kutufanyia janja yao?” aliuliza yule mzee.


“Nahisi! Japo sina hakika” alisema yule kijana huku akishusha kiona mbali na kukirudisha mikononi mwa kijana aliekuwa nacho mwanzo.


“Kwani kuna anae mfahamu huyo Ahmed?” aliuliza yule kijana.


“Hapana! Na aliekuwa anamfahamu aliuwawa kwenye mashambulizi yaliotekelezwa na wamarekani mwaka 2006. Hivyo tunacheza pata potea japo ni muhimu sana kwetu huyu jamaa.” Alijibu Mzee wa kisomali.


“Mimi nakumbuka tu nilichokiona kwake wakati anaonana na Baba ila nimemsahau wajihi wake” alisema Kijana na jambo lile likafanya wote mle ndani wamakinike hasa yule Mzee.


“Nadhani ukiwakumbusha vijana ulichokiona itakuwa vyema zaidi ili tusipokee yai viza” alisema Mzee huku akijikuna kidevu chake kilichokuwa na ndevu ndefu wastani kama walivyo mashekhe wengi.


“Bwana alikuwa na kovu baya sijapata ona,Kovu lilianzia kifuani upande wa kushoto kuelekea upande wa mbavu za kulia likiwa limechora michirizi mingi huku lilipoanzia ni kama alijeruhiwa na mnyama mkali; Simba ama Chui” alisema kwa hisia kijana huku akijaribu kurekebisha kanzu yake ili imkae vyema.


Mara ileile taarifa ikatolewa kwa mapandikizi yalioko nje nayo yakaifanyia kazi.

*


Kundi lingine ndilo hasa lilikuwa linalengwa na kundi la kwanza lililoko Lugo Hotel. Kundi hili lenyewe lilijitenga katika viunga viwili. Kiunga cha kwanza kilikuwa upande wa mashariki mwa old Mogadishu na kilikuwa na watu wawili na Kiunga cha pili kilikuwa ndani ya magari matatu yaliokuwa na nembo za kikosi maalumu cha kulinda amani Mogadishu cha AMISOM(Africa Union Mission).

Ndani ya gari lililokuwa mbele kulikuwa kuna askari saba waliokuwa tayari kwa lolote na gari la nyuma pia lilikuwa na askari saba ila gari la katikati lilikuwa na askari komando watatu tu na mtu mwingine mmoja aliekuwa amefungwa minyororo mikono na miguu huku sura yake ikiwa imechakaa na mwili wake ukiwa umedhoofu sana.


Gari ya mbele ilionesha ishara kuwa wanapaswa kusimama eneo husika.


Magari yote yakasimama.


Kwenye gari la katikati, Komando mmoja alitoa kinasa sauti alichokuwa amekipachika sikioni mwake na kukipachika sikioni kwa yule mtu aliekuwa amefungwa kwa minyororo.


“Wanaweza kukujaribu kwa kila namna ili wathibitishe kama kweli wewe ndie Ahmed Twalibu sahihi,usije kutetereka na jukumu lako ni moja tu kuhakikisha tunajua maficho ya FLAMINGO kisha tutakupa utaratibu mwingine” ilisikika sauti kutoka kwa mtu aliekuwa kiunga cha kwanza mashariki mwa eneo lile.


“Nitawasiliana vipi na nyinyi kusubiri maelekezo?” aliuliza mtu aliekuwa amefungwa kwa minyororo.


“Siku mkipokea mzigo wa silaha hakikisha unatafuta risasi moja ambayo ni blanco hiyo itakuwa na ujumbe wako. Lakini kumbuka mwili wako ni mawasiliano na sisi Honda” ilisema sauti kutoka kiunga cha kwanza.


“Goda up kamanda!” ilisema sauti nyingine tofauti na ya awali iliokuwa upande wa kiunga cha kwanza.


“Goda up komredi” alijibu Honda p.a.k Ahmed Twalibu.


Kutokea nje ya gari walilokuwamo kukagongwa mara kadhaa na ikawa ni ishara kwao kushuka ndani ya gari huku Honda au Ahmed wa bandia akiwa amezingirwa na makomando watatu wa kikosi cha AMISOM. Na kutoka eneo lile lote ilikuwa limezingirwa na makomando kumi na saba kiujumla huku madereva wa magari yale wakiwa nao wametulia vyema kwenye gari zao tayari kwa lolote.


Ukimya ulikuwa wa kutisha kwenye barabara ile na makomando nao walikuwa kimya wakiwa makini na hatua zao wenyewe na mbele ya magari yao kulikuwa kuna gari dogo lililokuwa wazi na juu ya gari lile kulikuwa kuna kijana mdogo mwenye kupata umri wa miaka kumi hadi kumi na tano na alikuwa amebeba silaha ya kivita mikononi mwake bila wasiwasi wowote na ile ndio ilikuwa ishara ya kuwa pale ni eneo husika.


Wote wakiwa kimya,mara ukasikika mkoromo kutoka kwenye mifuko ya mmoja wa makomando waliokuwa wamemzunguka Ahmed Twalibu.


Komando yule alitoa simu ya upepo iliotoa mkoromo kuashiria kuna simu nyingine inayoingia.


“Mwacheni asogee mbele peke yake na nyinyi mrudi nyuma” iliunguruma sauti kutokea kwenye simu ile kwa lugha mbovu ya kingereza kwa lafudhi ya kihabeshi.


“Ni jicho kwa jicho komredi,tunaomba tuone upande wenu” Alisema komando wa kikosi kilichompeleka pale gaidi Ahmed.


Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa.


“Anzeni nyie kisha tutawapeni wa kwenu” ilisema sauti kutoka upande wa pili.


Komando yule aliwaangalia wenzie ambao nao waliishia kutazama tu bila kusema kitu.


Akili zao zilikuwa zinapiga hesabu kali kukubaliana na jambo lile.


“Ok!!” alijibu kifupi komando yule na hapo komando wengine waligeuka na kutazamana kwa maamuzi yale ya kiongozi wao.


Dakika iliofuata walimpisha Ahmed asogee mbele kama ilivyotakiwa akiwa amefungwa vile vile minyororo mikononi na miguuni.


Honda; p.a.k Ahmed Twalibu alipiga hatua kivivu huku nae akiangaza macho yake kushoto na kulia taratibu bila papara.

Hatimae alifika kati kati ya gari lililokuwa wazi na juu kukiwa na mtoto aliebeba silaha na wale makomando ambao muda wote walikuwa kimya bila hata kupepesa macho yao.


Kutoka kwenye chumba ndani ya hotel ya Lugo; kijana yule aliekuwa na asili ya Saudia,alishusha chini kiona mbali na kuwageukia wenzie waliokuwa na asili ya kisomali.


“Anaweza kuwa ndie,mruhusuni tutamjua akiwa chini yetu” alisema huku akikabidhi tena kiona mbali kile kwa mtu aliekuwa nacho awali.


“Basi itifaki izingatiwe” alisema mzee wa kisomali huku akikuna msitachi wake.


Vijana walijua nini wanapaswa kufanya.


*


Kijana aliekuwa kwenye gari na mtutu wa bunduki,alisikia mlio wa mluzi mara mbili na hivyo alijua ni kipi cha kufanya wakati huo.


Haraka kutoka pale alipokuwa, akashuka kibabe utadhani ni mtu mzima. Akapiga hatua bila wasiwasi wowote na kumfikia Honda p.a.k Ahmed Twalibu.


Hakujishugulisha na pingu alizokuwa amefungwa Ahmed bali alibaki akimtizama usoni bila kupepesa. Honda aliona macho ya yule mtoto yalivyojaa ukatili ingali ni mdogo. Alikakamaa mithili ya wabeba mizigo bandarini.


Hakika ilihuzunisha.


Ila mtoto yule hakuonekana kujali.


Akachomoa kisu na kuiweka pembeni bunduki yake kisha akamfuata Ahmed.


Mtoto yule bila uoga alianza kurarua nguo za Honda p.a.k Ahmed Twalib gaidi aliesakamwa na makundi mbalimbali wakitaka ajiunge nao na sasa Ahmed yupo Somalia mbele ya kikundi cha kiharamia na kigaidi huku yakiwa ni makabidhiano maalumu na serikali ya Marekani.


Mtoto yule alieonekana ni fundi wa kutokea kutumia kisu,hakumaliza dakika moja tayari nguo za Ahmed zilikuwa hazitamaniki na yule mtoto akabaki akilikodolea kovu baya kifuani mwa Ahmed. Yule mtoto alishindwa kuelewa kovu limesababishwa na nini na ni binadamu gani anaweza kuhimili kuishi na kovu kubwa kiasi kile maishani mwake.


Hakika bwana mdogo aligwaya.


Bwana mdogo yule akabeba mtutu wake na kugeuka, lakini kama alisita hivi na kugeuka tena kulitazama kovu lile.


Kuna kitu kilipita akilini mwake.


Kovu gani hili? Mbona kama ni bandia? Aah!!” alijakatalia haiwezi kuwa maigizo katika mwili wa mtu.


Bwana mdogo aligeuka na kumpa ishara Ahmed amfuate. Ahmed akaanza kujivuta kivivu kumfuata huku makomando waliomfikisha pale wakiwa kimya na umakini wa hali ya juu.


Bwana mdogo yule alipiga mbinja kadhaa kisha akajipiga kifuan mara kadhaa. Ilikuwa ni ishara ya kukamilisha kazi yake na sasa wakubwa wake waendelee na utaratibu wao.


Wakati Ahmed anapakizwa kwenye gari na bwana mdogo yule, Makomando walishuhudia watu wengine watatu wakitokea kwenye jengo moja bovu lililokuwa pembezoni mwa barabara. Watu walionekana wakiwa wamedhoofu kupita maelezo na walizeeka kweli.


Walikuwa ni mateka wa kijeshi tangu miaka ya tisini baada ya vita kati ya kikundi cha kigaidi cha AIAI(Al-Itihaad Al-Islamiya).


Komando kiongozi aliona wahusika wa mabadilishano yale, akatoa ishara kwa makomando wale wa AMISOM nao wakaanza kuelekea kuwapokea watu wale walioonekana kudhoofu miili yao.


Lakini gafla ikasikika risasi moja hewani na makomando wote wakakoki silaha zao tayari kwa lolote.


Alikuwa ni bwana mdogo aliepiga risasi juu.


Akashuka kwenye gari na kumwacha Ahmed akiwa na dereva akawafuata wale makomando ambao walikuwa wamesimama bila kujua wafanye nini.


Akawafikia!!


“Oya!! atakaepiga hatua kusogea hapo alipo nitamvua chupi hadharani, nguruwe weupe nyie” alifoka bwana mdogo bila kuogopa macho ya kikazi ya makomando wale ambao mitutu yao ilikuwa sawia kifuani mwa bwana mdogo yule.


Walipigwa mkwara wakatulia.


Bwana mdogo akageuka kibabe na kuwafuata wazee waliokuwa wanakikokota kuwaendea wale makomando.


“Na nyie vibwenzi nitawatoa roho sasa hivi, mtaondokaje bila mi Mzee wenu kutoka hapa.” Bwana mdogo akaachia mkwara mbuzi wazee wale waliokuwa makimando miaka hiyo kabla ya dhahama iliowakumba na kujikuta wakiwa mateka miaka mingi.


Bwana mdogo alianza kuondoka kwa madaha huku akipiga mluzi wa wimbo asioujua,na kabla hajafika kwenye gari akawageukia wale wazee.


“Mnadhani na huo uzee mnaenda kufanya nini. Nendeni mshikishwe tunguli na Wamarekani vibwengo ninyi”


Alah!!!


Mtoto anatema mkwara kwa wakubwa.


Makomando wote walibaki wakiwa wameganda kama sanamu. Mtoto aliwashangaza kwa kujiamini kwake.


Na kweli walitulia hadi bwana mdogo alipoondoka pale ndipo na wao walipowahi kuwapokea wazee wale na kuwaingiza ndani ya magari yao na kuondoka eneo lile la Old Mogadishu.


Wao hesabu zao zilienda sawa siku hiyo na hesabu za kikundi kile ambacho hakikuwa na jina kubwa la ugaidi miaka ya karibuni, nacho kilijua kipo safi katika hisabati yao.


**


Bwana mdogo yule hakwenda mbali na mateka wake Ahmed. Walizunguka kona ya kwanza na ya pili wakaingia kwenye jumba lililoonekana kama ni karakana ya kutengenezea magari.


Humo ndani kulikuwa kuna magari mengi mabovu na mazima yalioonekana kupitia shuruba nyingi sana. Mbali na hayo pia kulikuwa kuna watu wengine wanne.

Kati ya watu hao wawili walikuwa na mitutu ya kivita huku mikanda ya risasi ikiwa imezunguka mabegani mwao, na wawili walikuwa ni wasichana wazuri wa kihabeshi wenye umri si zaidi ya miaka kumi na saba ambao walikuwa wamefungwa mikono kwa nyuma na vitambaa vyeusi machoni pao. Walionekana kupitia mateso mengi mana walidhoofu na miili yao kugandana na makovu mabichi.


Hakika ilitia huzuni.


Honda p.a.k Ahmed alitazama kwa huzuni wasichana wale.


Watekaji hawakujali.


Bwana mdogo yule alibaki akiwa anamtazama Honda kwa dakika kadhaa,kisha akaanza kumzunguka kwa madaha kama anaekagua kitu hivi kisha aliporidhika na tambo zake alisimama mbele ya Honda na kwa gafla akamtandika ngumi kali ya tumbo na kumfanya Honda ainame kwa maumivu makali yaliosambaa tumboni kwake.


Ngumi ya bwana mdogo ilikuwa ni ngumi ya mtu mzima hakika..


“Naitwa Sozi mfalme wa wajane hapa Somalia”alijigamba bwana mdogo huku akirekebisha mtutu wake begani na kuutia mikononi kisha akapiga mluzi na hapo akaja jamaa mwingine aliekuwa na zana za ufundi na alipofika bila kuelekezwa alianza kushugulika na vifyatuo vya minyororo iliokuwa mwilini mwa Honda.


Dakika nne baadae Honda alikuwa huru lakini hakuruhusiwa kupiga hatua hata moja.


“Ahmed; nataka ufanye kazi moja tu hapa” alisema Sozi bwana mdogo mtata au alivyopenda kuitwa mfalme wa wajane. Haijulikani wajane gani aliomaanisha huyu bwana mdogo.


Aliita wale vijana waliokuwa na wale mateka nao wakaanza kuwaburuza mabinti bila huruma na kuwafikisha pale walipokuwa Sozi na Honda au kama walivyomjua kwa jina la Ahmed.


“Hawa ni wahabeshi wa huko Ethiopia; mabwana zao walituchafua ndani ya nchi yetu sasa waliwaacha hapa na kifo kimefika na wewe ndo utawauwa” alisema Sozi huku akiikoki silaha yake na kitendo bila kutegemea akaachia risasi ilioenda kutua kichwani mwa binti mmoja na kumsambaratisha ubongo wake bila huruma.


Hakika Sozi alikuwa katili zaidi ya umri wake.


Akamgeukia Honda.


“wewe ni gaidi Ahmed; hivyo huoni huruma kwa hawa mende,piga risasi tu huyu aliebaki ili tujue kweli sifa unazopewaga ni za kweli.” Alisema Sozi huku akimpa mtutu wa kivita Honda waliemjua kwa jina la Ahmed.


Mmoja wa wasomali wale alimvua kitambaa yule binti. Binti alimlitizama Honda kwa huruma sana.


Honda alibaki akiwa hana la kufanya.


Ukitaka kumuua nyani usimtizame usoni.


Mfalme wa wajane alibaki akimtizama Ahmed na maamuzi yake.


Honda alikuwa katikati ya hisabati za Wasomali.


Hakujua aepuke vipi mtego wa hesabu ile, huruma ilikuwa kubwa karibu ibebe ujasiri wake.


Ataua?


***





Mfalme wa wajane alibaki akimtizama Ahmed na maamuzi yake.


Honda alikuwa katikati ya hisabati za Wasomali.


Hakujua aepuke vipi mtego wa hesabu ile, huruma ilikuwa kubwa karibu ibebe ujasiri wake.


*


Honda alibaki akiwa anazungusha akili namna ya kuepuka kumuua yule binti ambae alikuwa anamtazama Honda kwa huzuni na machozi yalikuwa yanambumbujika kwa kasi.


Honda alikoki mtutu tayari kwa kumuangamiza yule binti.

Aliusogeza mtutu usoni kwa yule binti na kidole kilikuwa tayari kipo kwenye kifyatulio na tayari alianza kuvuta kilimi cha mtutu.


Azana ikalia kutoka kwenye msikiti uliokuwa jirani na maeneo yale.


Honda alitumia nafasi ile vilivyo.

Akatupa chini mtutu na kuinama pembeni na kuanza kuswali swala ya adhuhuri.


Sozi na wenzie walibaki wakimtizama bila kutia neno na kisha alianza mmoja na kufuatia wa pili hatimae wote walijiunga na Honda kuswali.


Honda alitumia hesabu za akili kuliko walivyodhania.

Kimsingi kikundi cha AIAI; kilikuwa ni kikundi chenye mlengo wa dola ya kiislamu na lengo kuu la kukita mizizi yake katika pwani ya Somalia ni kuhakikisha wanaunda nchi ya kiislamu katika ukanda huo, hivyo ilikuwa ni karata safi alioamua kuitumia katikati ya malaika watoa roho na ukuu wa Mungu ulidhihirika.


Baada ya dakika kadhaa, wote walisimama wakiwa wamemaliza kuswali.


Sozi alikuwa bado anataka kukamilisha swala lake na alitaka Honda atekeleze.


“Ahmed shika hii” alisema Sozi huku akiokota chini silaha yake na kumpa Honda.


“Mungu hawezi kujibu maombi yetu tuliofanya sasa bwana mdogo,hivyo mtunze nitamuua katikati ya adhuhuri na jioni.” Alisema Honda p.a.k Ahmed ambae hakujishugulisha kuichukua silaha ile,badala yake alikuwa anahangaika kuunganisha nguo yake iliotatuliwa na kisu cha Sozi Mfalme wa wajane.


Sozi aliona ni dharau haraka akatoa kisu chake kwa lengo la kumshambulia Honda; ila hakujua mtu aliepembeni yake alikuwa ni mtu wa aina gani.

Kwa wepesi wa kawaida tu alikikwepa kisu kile na kumtandika Sozi ngumi moja ya shingo na kumpeleka chini bila kupenda. Washirika wa Sozi waliokuwa pale nao hawakutaka kuona Sozi akiadhirika nao wakaingilia ila kwa ustadi licha ya kudhoofu mwili aliwachapa kama mzaha vile na kujikuta wakiwa hawana la kufanya zaidi ya kumwangalia Honda ambae hakuwajali wakati huo wao walipokuwa wakiugulia maumivu.


Sozi alibaki akimwangalia Honda akiwa hana la kumfanya. Mara akawa kama aliekurupushwa kutoka usingizini akainyakuwa silaha yake iliokuwa pale chini na kumcharaza risasi binti ambae muda wote alikuwa akilia kwa hofu kwa yale yaliokuwa yanaendelea pale.


Binti aliaga dunia.


Honda alibaki akimtizama bwana mdogo Sozi aliekuwa amesimama na mtutu wake akiwa hana wasiwasi wowote.


**


Kutoka ndani ya Lugo hotel, kila kitu kilichokuwa kinaendelea kwenye karakana ile kati ya Sozi na Ahmed;kilionwa vyema kabisa na watu waliokuwa mle ndani.


“Licha ya kudhoofu ila bado anaweza kupambana, huyu kweli ni Ahmed Twalibu” alisema kijana mweupe huku akitabasamu, tabasamu ambalo hakuna aliejua linamaana gani.


“Kabla hatujaonana nae na kumdai tunachokitaka kwake, inabidi atumike kufanya jambo letu kesho kutwa na kabla ya keshokutwa hiyo kesho aingie kwenye majukumu mengine yaliopo. Hapo ndo tutajua tulienae ni Ahmed wa kweli au ni mtu tu tumeuziwa” alisema mzee wa kisomali aliekuwa mle ndani.


Wengine walikaa kimya kuhakikisha kila kitu kinachopangwa hakiharibiki.


**

Kutoka jengo lingine tena kulikuwa kuna watu wengine wawili ambao walikuwa wamekaa na vifaa kadhaa vya mawasiliano na walionekana kuwa bize kukata nyaya kadhaa za mawasiliano yale.


Hawa ndio waliokuwa kwenye kiunga cha kwanza ambao mwanzo waliwasiliana na Honda wakati akiwa ndani ya gari la AMISOM.


“Zedi; jamaa ameingia kwa hawa jamaa ila sina hakika kama atatoboa kutoka, tangu mwanzo naona ni mtu mwenye huruma sana” alisema jamaa mwingine aliekuwa amekaa kwenye kiti huku akiwa bize na kuchezea tarakilishi aliokuwa ameiweka kwenye meza.


“Haji; Huyu jamaa hatujawahi kufanya nae kazi, ila anaonekana yuko makini sana katika mambo yake Lakini pia hii tenda ya CIA itakuwa inafuta mashaka yetu kwake.” Alisema Zedi.


“ok!” alijibu kifupi Haji Makame.


“Afu keshokutwa anakuja Rais wa Kenya hapa Somalia; na kama ujuavyo hapa kuna hiki kikundi cha Al-Islamiya na kikundi cha Al-shabab na wote ni maadui wakubwa wa Kenya huoni kutakuwa kuna shida hivi” Alisema Zedi Wimba.


“Yawezekana kikosi chake cha skauti kimempa taarifa sahihi kuhusu usalama wake, tutege masikio tu” alisema Haji Makame.


Zedi alinyanyua mabega juu bila kutanabaisha liloko moyoni mwake.


“Serikali utatulaumu sana tusipomlinda Honda huko aliko” alikumbusha Haji.


“Sahihi, ila tutajitahidi turudi salama kwenye mpango huu na FLAMINGO apatikane” alisema Zedi.


“Hivi inaweza kuwa kweli Mohamed Farrah Aidid yupo hai kweli?” alihoji Haji.


“Majibu atakuja nayo Honda ila pia naamini yupo hai kwa sababu ya mateka wale wa ile vita kuwa hai hadi sasa” alijibu Zedi.


“Inawezekana pia” alijibu kifupi Haji na kuendelea kuchezea tarakilishi yake.


**


Sozi alimwongoza Honda kuingia ndani ya gari jingine ambalo kimwonekano halikustahili kuwa barabarani kisha Safari ikaanza kuelekea pembezoni kidogo mwa mji wa Mogadishu kwenye kitongoji kilichoitwa Atwa.


Baada ya mwendo wa saa moja na dakika kadhaa ,hatimae waliingia kwenye kitongoji cha Atwa.

Kwa harakaharaka Honda alitupia macho nje ya gari na kuona makazi ya watu yalivyosadifu umasikini wa hali ya juu na baadhi ya watu waliokuwa wamekaa nje ya nyumba zao walionekana kukata tamaa kabisa ya maisha,nguo chakavu na miili iliokondeana ilitangaza shida yao hadharani. Baadhi ya maeneo mengine yalikuwa yamebaki magofu ambayo kimsingi yalionekana kubomolewa na bomu ama kitu cha mlipuko mkubwa sana.


Safari iliendelea kimya kimya huku Honda akizidi kuona uharibifu mkubwa uliofanyika na hayo ni matokeo ya vita ya wenyewe kwa wenyewe.


Wakiwa wanaingia kwenye kijiji fulani kilichochangamka; Honda alipata kuona tukio la kutisha sana.

Watu zaidi ya kumi walikuwa wamepangwa mstari huku wakiwa wamefungwa mikono na miguu na nyuma yao kulikuwa kuna vijana watatu waliokuwa wameshika mapanga na kisha wakaanza kuwacharanga watu wale bila huruma kabisa.


Hakika ilitisha.


“Kwanini wanafanya vile?” aliuliza Honda kwa mara ya kwanza.


“Watakuwa wamekataa kuchangia chakula na pesa na hiyo ni haki yao” alijibu Sozi huku akionekana kufurahia lile tukio na jibu alilompa Honda ama Ahmed Twalibu.


“Napenda sana kuua, ila kuua kwa upanga ni uoga” alisema Honda kwa lengo la kuteka hisia za Sozi alieonekana kupenda sana kuua kuliko hata kula.


“kwani wewe unauaje?” aliuliza Sozi huku akiwa makini sana kusikia jibu la Honda.


Honda aliguna kidogo.


“Nitakwambia siku nyingine. Kwani mkuu wenu ndie naenda kumuona au?” alijibu Honda kisha akatupia na swali.


“Aisee,hakuna kosa kubwa kama hilo,kuulizia mkuu alipo ama anaishije na yoyote anaekuja na swaga za kuumuliza huwa haishi aisee usirudie” alisema Sozi huku akionekana kukereka sana.


“ooh sawa” alijibu Honda na kukaa kimya.


*

Waliingia katikati ya kijiji cha Atwa. Huko karibia kila sehemu ilikuwa inatoa uvundo kwa mizoga iliokuwa imezagaa hovyo bila wakazi wa maeneo hayo kujali harufu hiyo, wao walionekana kuzoea mazingira ya eneo lile.


Safari yao ilienda kuishia katikatia ya jumba kubwa la kifahari lililokuwa kama limebeba hadhi dhaifu ya kijiji kile kilichokuwa kimezungukwa na umasikini wa hali ya juu na ilikuwa ni ajabu kukuta jumba zuri katikati ya mizoga ya watu.


Jumba lile lilikuwa linalindwa na vijana wadogowadogo wengi waliokuwa wamebeba silaha za moto zenye zaidi ya kilo tano.


Honda aliamliwa kushuka ndani ya gari kisha akaongozwa kuingizwa ndani ya jumba lile la kifahari ambalo lilikuwa lina wasichana wadogo wadogo waliokuwa wamevaa nusu uchi licha ya kuonekana kama ni wafanyakazi wa pale.


Sozi alienekana kuwa ni mwenyeji wa eneo lile alianza kuwachekea mabinti wale ambao walionekana kuchukia kuwapo mazingira yale.

Gafla Sozi alifanya kitendo cha ajabu kidogo.


Alimdaka binti mmoja kwa ustadi mkubwa na kumkandamiza ukutani kisha akaanza kumchojoa vinguo alivyokuwa amevaa na kuanza kumwingilia bila huruma.

Binti yule alionekana kutofurahia kabisa kitendo kile ila hakuwa na namna alitega tu na mkuyenge ukapita kunako tonkito.


Dakika tano baadae, Sozi alikuwa anachekelea tendo lile alilolifanya hadharani mbele ya macho ya mabinti wengine na Honda.


Baada ya unyama ule; Sozi alimuongoza kuingia katika chumba fulani ndani ya jengo lile, huko aliachwa peke yake aoge na kufanya usafi wa mwili wake vile anavyotaka.


Baada ya dakika kadhaa Honda alikuwa amemaliza kujiswafi na kuvaa nguo alizozikuta mle ndani kisha akatoka na kumkuta Sozi.


Sozi alimchukua tena na kuelekea chumba kingine na huko Honda hakuamini alichokiona.


Kulikuwa ni kama machinjioni jinsi kulivyokuwa kumejaa damu nyingi na vichwa kadhaa vya watu, lakini pia kulikuwa kuna mtu mmoja aliekuwa amefungwa kwenye kiti na pembeni yake kulikuwa kuna mtu aliekuwa ameshika kamera na kuilekeza kwa yule mtu aliekuwa amefungwa. Lakini pia kulikuwa kuna watu wengine wawili ambao walikuwa wamesimama na visu mikononi mwao na mmoja Kati yao alikuwa amevaa mavazi ya kijeshi na sura ya mtu yule ilikuwa ya kuogofya lakini licha ya sura hiyo lakini alikuwa anakichwa kidogo kilichokuwa kimechongoka mithili ya kichwa cha samaki Kamongo.


Sozi alionekana kumheshimu sana mtu yule mwenye kichwa kama Kamongo na alipofika alimpa maelezo kadhaa kisha akarudi kusimama karibu na Honda.


Mtu yule mwenye kichwa cha Kamongo akapiga hatua kumfuata Honda na alipomfikia akamwambia..


“Somalia ina vikundi vingi sana vinavyotaka kutawala ila sisi tunataka tusimike dola la kiislamu hapa Somalia na ukanda huu wa Africa ila hatutaweza bila kuwa na nguvu na nguvu tunaitangaza kwa kuwaua hawa wengie ili tusalie sisi” Kamongo alisema.

Honda alimtizama kwa dakika moja nzima kisha akamwambia.


“Kwa hiyo mkiua unatangazwa kama muislamu umeua au gaidi umeua?”


Kamongo alibabaika kujibu swali lile akabaki kumtazama tu.


“Kama mmenikomboa kwa wamarekani ili nije kufanya mauaji ya kidini, sitaweza kabisa na labda mniue tu, ila kama tunaua wanaofadhiliwa na Marekani na washirika wake waache kutuchonganisha waafrika, hakika nitakuwa mstari wa mbele kabisa kufanya ninachokijua” alisema Honda ama Ahmed Twalibu.


Kukapita ukimya kidogo.


“Kama mkuu wenu yupo mwambieni tubadilishe mlengo wetu na tusichafue dini ya Kiislamu kuonekana dini ya ugaidi, tupambanie haki ndani ya Somali bila kuweka udini katika masilahi yetu, tofauti na hapo sitaungana nanyi japo najua ndicho mlichonikombolea” alisisitiza Honda.


“Ok! Hayo hayatusaidii sasa ila kikubwa upo hapa kufanya kazi kadhaa na kikubwa ni kutangaza ujio wa Al-Itihaad Al-Islamiya; tulipotea miaka mingi sasa tumerejea na tunajiengua kutoka kwa Al-shabaab kwa kuua mmoja wa mpiganaji wake. Somalia ni yetu sasa” Kamongo alisema huku akimkabidhi jambia Honda na mtu alieshika kamera nae alianza kurekodi.


“Chinja huyo jamaa mana wao na Al-Qaida wanajua ni msaliti kwao hivyo waoneshe wewe sio msaliti na wamekukosea kukupa tuhuma hizo” alizidi kusema Kamongo.


Kamera iliendelea kurekodi na Honda akashika jambia huku rohoni akitetemeka. Hajawahi kuchinja mtu.


Dah!!

Honda kwenye majaribu tena.


Atachinja?


***




Kamera iliendelea kurekodi na Honda akashika jambia huku rohoni akitetemeka. Hajawahi kuchinja mtu.


Dah!!

Honda kwenye majaribu tena.


Atachinja?


Honda alimsogelea yule mtu ambae alionekana yuko hoi kwa mateso aliopitia.


Kamera iliendelea kurekodi tukio lile.


Honda alishika vyema lile jambia kwa mkono wa kushoto, kisha akalipeleka shingoni kwa mtu yule na kwa kasi ya mkono wake wa kulia akapiga piga moja tata sana kwenye mfupa unaounga mifupa ya bega na shingo na ukasikikia mlio mmoja hatari kama kuvunjika kwa kijiti kikavu cha mti wa mninga.


Akatupa jambia pembeni na mtu yule akalegea na kujibwaga chini.


Hakuwa amechinja.


“Yeehaaa!” Sozi alishangilia kitendo kile cha pigo la kifo la Honda; kwake ilikuwa ni burudani tosha kwa mtu kuuwawa. Sozi alipenda kuua kuliko jambo lolote katika Dunia hii.

Kamera ilizimwa na Kamongo alimfuata Honda kwa gadhabu.


“Paka wewe! Kama isingekuwa amri ya mtawala ningekunyofoa kende keremanzi wewe.” Alifoka Kamongo baada ya kuona kitendo alichokifanya Honda sicho alichokitarajia.

Wote walitoka ndani ya chumba kile na kuelekea sebuleni mwa jumba lile kisha wakamuamuru Honda akae kwenye kiti kimojawapo mle ndani.


Kamongo aliekuwa amefinya sura kama kalambishwa kinyesi akamrukia Honda na kumkaba ukosi wa shati alilokuwa amevaa.


“We nguruwe, upo hapa leo tu ila unajifanya mkaidi eti, ndo umefanya nini pale” alifoka Kamongo huku akilamba midomo yake miembamba iliochongoka kama anakunywa supu ya moto.


Honda hakujibu!!..


“Huko tuendako nahisi tutaishia kuuana mimi na wewe bwege wewe” alikoroma tena Kamongo huku wengine wote wakiwa kimya bila kusema neno.


“Nimekombolewa nanyi ili nifokewe na wewe au kuonana na viongozi wenu waseme shida yao kwangu?” alisema kiutaratibu sana Honda.


Kamongo alitoa cheko la dharau kiasi.


“Boss ni invisible, haonekani, majukumu yako ni kutekeleza unaloambiwa na mimi ili kufidia garama zetu za kukukomboa bada ya hapo utafanya kilichokuleta hapa Ahmed” alisema Kamongo huku akitoa kipande kidogo cha karatasi kutoka mfukoni kwake na kukikunjua mezani..


Sozi na wenzie wakasogea karibu na meza ilipowekwa karatasi.


“Mipango yetu ni kuisafisha Somalia kisha tutawale jumla,na ili kufanikisha hili kuna mambo mawili inabidi yafanyike.” Kamongo akasema huku akiwatizama wenzie waliokuwa kimya wakati wote.


“Ni kukifarakanisha kikosi cha Al-Shabaab kisha tunamuua kisiki katika ukanda huu Rais wa Kenya” Alisema Kamongo huku akiitandaza karatasi kwenye meza.


“Hapa ni kijiji cha Sadaan na hapa leo usiku ama kesho kuna mzigo wa silaha unaingia kutoka kwa wafaransa na wanauleta kwa Al shabaab” alisema Kamongo huku akionesha kidole kwenye karatasi iliokuwa inaonesha ramani ya kijiji cha Sadaan kusini mashariki mwa Mogadishu na nusu kilomita kutoka pwani ya bahari.


Wote walitazama vyema ramani ile.


Tukifanikiwa kuzichukua silaha hizi kabla hawajajipanga itabidi tumuue kiongozi wao ili kudhoofisha nguvu yao” alisema tena Kamongo.


Akamtazama Honda.


“Osama alikuamini sana Ahmed na aliamini sana uwezo wako wa kupanga matukio na kuyatekeleza na ndio sababu upo hapa Ahmed.” Kamongo alisema na kumtupia jicho Honda ambae alikuwa kimya wakati wote.


“nadhani nafaa zaidi kusema na kiongozi wenu” alisema Honda.


Sozi akapiga ngumi nzito mezani na kuwafanya watu wote waangalie alipopiga.


“Chawa wewe! Nilishakwambia kumsema kiongozi ni sawa na kubeti ushuzi wa tembo kuwa unanuka kwa tani ngapi za harufu” alikoroma Sozi huku akiwa ameinamisha uso wake karibu kabisa na uso wa Honda ambae wakati huo wala hakuhangaika kufanya lolote.


“Ok! Tuachane na hayo, kikubwa tushirikiane kwa sasa kufanikisha hili jambo na dunia ijitayarishe kusafisha jina letu. Sisi sio magaidi” alisema Kamongo huku akivuta kiti na kukaa karibu na Honda.


**


Walitumia zaidi ya nusu saa kujadili namna ya kuingia katika kijiji cha Sadaan na kuzipora silaha za wafaransa wanazowauzia wapiganaji wa kikundi cha Al-shabaab.


Baada ya majadiliano yao, walielekea chumba maalumu kwa ajili ya chakula kisha wakaelekea sehemu nyingine kulikokuwa na chumba cha mateka.


Huko Honda alipata kuona wazungu wawili wakiwa miongoni mwa watu waliotekwa na kupewa mateso sana.


“Wale nguruwe mwitu walitumwa kufanya ushushu kuhusu kuibuka kwa kikundi chetu kilichopotea mwaka 2006. Bahati haikuwa kwao wapo hapa leo na kifo ndo kengele yao” alisema Kamongo huku akichukua kisu kutoka kwenye ala yake na kumsogelea mzungu mmoja na bila huruma alididimiza kisu shingoni mwa mzungu yule na kufanya damu ziruke kama mbuzi aliechingwa bahati mbaya huku akitoa mkoromo wa ajabu.


Hakika ilitisha hali ile mle chumbani.


Lakini Sozi alifurahia kwa kupiga mluzi mrefu huku akijilamba midomo yake kwa furaha ya kuona mauaji yale.


“Sasa kabla hatujaenda masikani, inabidi tupite kule Kole tukusanye chakula na madada poa kazi mbele yetu ni kubwa” Alisema Kamongo huku akimalizia kufuta damu zilizokuwa zimejaa kwenye kisu kwa kutumia nguo za yule mzungu mwingine aliebaki hai ambae wakati huo alikuwa anaomboleza kama aliefiwa na mke.


**


Nusu saa badae walikuwa kijiji cha Kole; huko walikutana na kundi lingine la wapiganaji ambao walionekana kumheshimu sana Kamongo.


Walipeana maagizo kadhaa na kuingia kusumbua wanakijiji ambao wakati huo wengi walikuwa wamejikunyata pembezoni mwa nyumba zao huku wakiwa hawajui hatima ya maisha yao.


Hekaheka zilianza, risasi zililirindima bila sababu maalumu lengo ni kuwavuruga wanakijiji wale ambao walikuwa wapo kinyonge katika himaya zao.


Mauaji yalifanyika mbele ya macho ya Honda huku mabinti wadogo wakibakwa hadharani na wapiganaji wale wa kikundi cha Al-Islamiya.


Sozi aliongoza vyema mauaji ya watu waliokuwa wanagoma kutoa chochote walichokuwanacho ama wale ambao hawakutaka kuona mabinti zao wakidhalilishwa hadharani.


Honda kuna kitu alihitaji kukifanya na katika heka heka zile akamdaka binti mmoja kama na kuelekea nae kwenye moja ya mabafu ya kienyeji.

Binti alipiga kelele za woga na hamaniko lakini Honda hakujali alizidi kutokomea nae kuelekea bafuni.


Alipokwisha kuingia nae kwa wepesi alimpiga yule binti kwa ubapa wa kiganja chake na kumpoteza fahamu.

Honda alianza kuchojoa nguo alizokuwa amevaa na kubaki mtupu kisha akamrarua yule binti nguo zake na kumwacha mtupu.

Lakini hakujihangaisha kumwingilia isipokuwa kwenye uume wake kulikuwa kuna kitu kama kata nyeusi ya raba ilikuwa imezunguka kuja usawa wa korodani,aliitoa kata ile iliokuwa imebana vyema shina la uume wake na alipoivua akaaangaza huku na huko bado alisikia makelele ya wanakijiji wakijaribu kuokoa nafsi zao.

Aliibinya pete ile mara mbili kisha akatulia.

Punde pete ile ikawaka mara mbili, hiyo ilimaanisha ujumbe umepokelewa akarudi kuivaa kama mwanzo kisha akaanza kuvaa nguo zake harakaharaka na kuanza kutoka ndani ya bafu ile.


Akasita!


Alisita baada ya kuona Sozi amesimama mlangoni mwa bafu lile akimtizama.


“Sijasikia ukifanya lolote komredi!” aliuliza kwa dhihaka bwana mdogo Sozi ambae alikuwa na kisu kilichotapakaa damu.


Honda aligwaya.


****


2: HUJUMA

JIJINI-DAR-


Akili ya Remi ilikuwa bado inazunguka kwa matukio alioyashuhudia tangu mwanzo mwa mkasa ule ambao hakujua ni nini hasa lengo lake.

Alimkumbuka bwana Kitambi.


“Hivi bwana yule anajiamini nini na ni nani hasa katika hii showtime?” alijiuliza Remi bila kuwa na wa kumpa majibu.


Sajini Vengu!!


Alimuwaza Sajini Vengu na akaona kuna haja ya kuelekea kituo cha Mwinjuma mwananyamala kuonana nae.


Kuna kitu alitaka kuweka sawa kuhusu jambo lile na alitaka kujua alipofikia Sajini kuhusu kutekwa kwa mwandishi Davis Minja na kuuwawa kwa mlinzi wa kampuni yake.


Bwana kitambi!


Nilipata kumuona wapi kabla ya leo? Alijihoji bila kupata majibu ya kutuliza ubongo wake.


**


Saa kumi jioni ilimkuta akiwa anaingia kwenye uwanja wa ccm mwinjuma kisha akashuka na kuelekea kilipo kituo kidogo kile.


Alikaribishwa kisha akasema shida yake.


Akaitwa Sajini Vengu ambae alikuwa chumba cha mahabusu na kazi nyingine.


“Sikutarajia kukuona hapa wakati huu japo nilitaka kukutafuta jioni hii” Alianza kwa kusema Sajini Vengu punde tu baada ya kumuona Remi.


“Nadhani tunapaswa kuzungumza kidogo!” Alisema Remi.


Wakaingia kwenye chumba kilichokuwa ni ofisi za kituo kile kidogo.


“Nakusikiliza Remi” alianzisha Mazungumzo Sajini.


“Nilitaka kujua tu umefikia wapi kuhusu kesi ile” Alisema Remi.


“Bado hakuna mwanga zaidi ya wewe kuonekana ni mhusika bado ambae kila sehemu upo” alianza kueleza Sajini.


“Kwanini?” alihoji Remi.


“Inaonekana mwandishi Davis Minja aliwasiliana na wewe jana na ujumbe wake ulikuwa ni wa kukupa taarifa kuhusu gari jeupe” Alisema Sajini.


Akaendelea..


“Katika ujumbe wake alisema anamtafuta jamaa hapatikani,sasa nikuulize jamaa gani alikuwa anatafutwa na Davis na kwanini akwambie wewe,na hilo gari lilitaka nini na kwa nini atekwe ofisini kwako?”


Yalikuwa ni maswali mfulululizo na yote yalikuwa yanaleta mana katika kadhia ile.


Remi akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kwa mkupuo.


“Kwa hakika sijui alimlenga nani ila nahisi mume wangu mana ndie rafiki yake” alijibu Remi.


Umakini uliongezeka usoni mwa Sajini.


“Taarifa zinasema mumeo hajaonekana zaidi ya miaka miwili, sasa yeye alikuwaje akamtafuta na anajua kabisa mumeo hayupo?” aAlisema Sajini Vengu.


“Sijui kama hawakuwa na mawasiliano kati yao katika miaka hiyo miwili na…” Remi hakumalizia kauli yake Sajini akamkatisha.


“Remi; mumeo tumeambiwa ni gaidi na haonekani sasa iweje Davis aseme hapatikani, hivyo unajua mumeo alipo sio?” Alihoji Sajini Vengu.


“Sijasema aliulizia mume wangu, bali nimesema pengine ndie alimaanisha afande” alisema Remi.


“Watch yo step madame!!” Alitahadharisha Sajini.


Remi akagwaya!!


Baada ya mazungumzo ya dakika kadhaa, Remi aliaga na kuondoka huku akimwacha Sajini akiwa amepata jambo jipya kuhusu mume wa Remi.


Remi alipanda gari lake na lengo lake alitaka arudi tena kule ofisini kwake, alitaka kufanya jambo ambalo alijua anaweza kubahatisha kulipata!


“Walioyafanya pale ofisini sina hakika kama kweli hawajaacha kosa moja, Hakuna mkamilifu” alisema Remi huku akiipita hospital ya mwananyamala, alikuwa anaelekea Mwenge zilipo ofisi zake. Hakutaka kuendelea kuhujumiwa, alitaka kukokotoa hesabu katikati ya hujuma na mitego.


Kitu kimoja hakujua madhara ya kile alichotaka kwenda kukifanya na kama angejua basi bora angeacha tu aendelee kushuhudia showtime alioahidiwa na bwana kitambi…


Hakika hakujua madhara yake kwa alichokusudia.


**.




Umakini uliongezeka usoni mwa Sajini.


“Taarifa zinasema mumeo hajaonekana zaidi ya miaka miwili, sasa yeye alikuwaje akamtafuta na anajua kabisa mumeo hayupo?” aAlisema Sajini Vengu.


“Sijui kama hawakuwa na mawasiliano kati yao katika miaka hiyo miwili na…” Remi hakumalizia kauli yake Sajini akamkatisha.


“Remi; mumeo tumeambiwa ni gaidi na haonekani sasa iweje Davis aseme hapatikani, hivyo unajua mumeo alipo sio?” Alihoji Sajini Vengu.


“Sijasema aliulizia mume wangu, bali nimesema pengine ndie alimaanisha afande” alisema Remi.


“Watch yo step madame!!” Alitahadharisha Sajini.


Remi akagwaya!!


Baada ya mazungumzo ya dakika kadhaa, Remi aliaga na kuondoka huku akimwacha Sajini akiwa amepata jambo jipya kuhusu mume wa Remi.


Remi alipanda gari lake na lengo lake alitaka arudi tena kule ofisini kwake, alitaka kufanya jambo ambalo alijua anaweza kubahatisha kulipata!


“Walioyafanya pale ofisini sina hakika kama kweli hawajaacha kosa moja, Hakuna mkamilifu” alisema Remi huku akiipita hospital ya mwananyamala, alikuwa anaelekea Mwenge zilipo ofisi zake. Hakutaka kuendelea kuhujumiwa, alitaka kukokotoa hesabu katikati ya hujuma na mitego.


Kitu kimoja hakujua madhara ya kile alichotaka kwenda kukifanya na kama angejua basi bora angeacha tu aendelee kushuhudia showtime alioahidiwa na bwana kitambi…


Hakika hakujua madhara yake kwa alichokusudia.


***


Jua lilikuwa linaelekea kuiachia dunia kiza; lilielekea magharibi.


Remi aliegesha gari lake pembeni kidogo mwa ofisi zake za utafiti wa mambo ya kale.

Eneo la ofisi zake lilikuwa lipo kimya na utepe wa njano ulikuwa umewekwa kwenye geti la kuingilia ndani ya ofisi zile.


Alitazama kushoto na kulia, kisha akaita kama kubahatisha tu ili ajue kama kuna askari atakuwa eneo lile.


Kukawa kimya!!


Akapiga hatua za mnato huku akiwa makini sana ili asije kuvuta jicho la mtu yeyote ambae alikuwa mitaa ile kufuatilia yeyote ambae angelifika pale nyakati zile.


Hakuona wala kuhisi jambo hilo eneo lile.

Akachukua funguo zake na kutia kwenye kitasa cha geti na likafunguka.


Akaingia!!


Akaelekea lilipokuwa gari la mwandishi Davis Minja lililokuwa limetelekezwa kabla haijafika kwenye maegesho.


Taa zilikuwa zimezimwa na eneo lote lilikuwa giza na kumezwa ukimya wa kifo.


Remi alitoa kurunzi ndogo kwenye mkoba aliokuwa ameubeba na kuanza kulitazama gari lile ambalo lilionekana kubondeka sehemu moja chini kidogo ya mlango wa kutokea dereva.

Remi aliinama na kugusa eneo lile na alichogundua ni kuwa mmbondeko ule ni wa chuma kilichobamiza pale kwa nguvu.

Zilifanyika harakati za la lazima kumchukua mwandishi yule.

Alisimama na kwa taratibu kabisa alianza kulizunguka gari lile ambalo hadi wakati huo lilionekana kupitia dhoruba kadhaa wakati likiwa njiani.


Remi hakuona cha maana zaidi katika lile gari,akaachana nalo.


Akaelekea mlango wa kuingilia ofisini kwake, akafungua na kuingia ndani taratibu huku akiangaza huku na huko.


Macho yake yakanasa mvurugano wa makablasha.


Kulipekuliwa!!


Saa ngapi na kwanini, hakujua!!


Akazidi kuona namna upekuzi ulivyofanyika kwa fujo.


Walitaka nini hawa!


Alijiuliza bila kupata jibu.


Alizidi kuingia ndani ya vyumba kadhaa vilivyotumika kama ofisi.

Hali ilikuwa ni ile ile.


Kulipekuliwa.


Hatimae alielekea kulipokuwa na ofisi yake,kuna kitu alitaka kukifanya huko.


Alipotaka kuingiza ufunguo, alishangaa kukuta kupo wazi.


Nani kafungua ilihali aliacha kukiwa kumefungwa na hakuna mwingine ndani ya ofisi zile mwenye funguo za ofisi yake?


Alisita kuingia.


Aliendelea kusikilizia nje ya chumba kile cha ofisi yake bila kusikia lolote kutokea ndani.


Akasukuma mlango na kuingia.


Macho yake kwa kusaidiwa na mwanga wa taa ya kurunzi yake ndogo, yalielekea kulipokuwa na meza yake.


Napo aliona mtawanyiko wa karatasi kadhaa za utafiti ziliokuwa zimetupwa huku na huko bila mpangilio.


Alipita hadi kwenye kiti kilichokuwa nyuma ya meza na huko alitaka kuona kile kilichompelekea aende tena kwenye ofisi zile.


Akainama kwenye droo moja wapo ya meza, na kuifungua.


Akaona kifaa maalumu cha kuhifadhia matukio yanayochukuliwa na kamera zilizofungwa kwa siri maeneo mbalimbali katika ofisi ile.


Kwa namna zilivyokuwa zimefungwa ni wachache sana waliojua kuna kamera za siri eneo lile.


Akafungua sehemu ya kuhifadhia santuri ya mtambo ule.


Hamna kitu!!


Santuri ilikuwa imechukuliwa na alipojaribu kutafuta, hakuna alichoambulia zaidi ya kuona kunyofolewa kwa waya kadhaa ili kukata mawasiliano ya kamera na ule mtambo wa kuhifadhi data za kamera.


Remi aliinuka na kushika kiuno lakini mbele yake aligundua hakuwa peke yake tena ndani ya ofisi yake.


Mbele yake alisimama mtu aliekuwa amejiziba sura yake na kuvaa nguo nyeusi chini hadi juu na viganja vya mikono yake alikuwa amevificha kwa mipira maalumu mieusi.


Remi aligwaya!!


Hakutarajia kuona mtu yule katika mazingira yale.


Alitokea wapi, hakukuwa na wa kumjibu.


“Wewe ni nani na utafuta nini humu?” aliuliza kwa kitetemeshi Remi huku akili yake ikizunguka mara nyingi zaidi kujua atafanya nini kwa mtu yule ambae hakuonekana kuwa mwema kabisa.


“Nikuulize wewe, unafanya nini usiku huu wakati umefunga” yule mtu aliuliza huku akionekana kuwa makini sana na nyendo za Remi.


“Unatafuta hii?” aliuliza mtu yule huku akimwonesha Remi santuri.


Haswaa!!


Ndicho alichokuwa anakitafuta sasa anakiona mikononi mwa mtu ambae ni mvamizi wa ofisi zake na pia mtu yule alikuwa ni mwanamke mwenzie.


Remi alipandwa na gadhabu akaruka kutoka kule alikokuwa na kutua karibu na yule mwanamke mvamizi.


Akanyoosha mkono ili ampore lakini lilikuwa ni kosa, alijikuta akichezea ngumi safi katikati ya kifua na kumnyima pumzi kwa dakika mbili.

Lilikuwa ni pigo mujarabu lililopigwa makusudi na mtu anaejua kupigana.


Remi alipata tena pumzi zake, akataka kujiinua ila akajikuta anarudishwa tena chini kwa pigo safi lililoishia shingoni mwake na kumfanya ahisi anahitaji kunywa maji mengi ili kujiokoa na dhaham ya kukaukwa na koo.


“Uko wapi ukurasa wa Bombay?” aliuliza yule mwanamke huku akimwinamia Remi pale chini alipokuwa.

.

E bwana!!


Remi alitoa macho kama aliebanwa na haja kubwa ya kuhara katikati ya umati wa kariakoo.


“Ukurasa wa Bombay;ndio nini tena?” alihoji kwa tabu Remi.


Yule mwanamke alicheka kwa dharau.


“Unajifanya hujui ninachomaanisha siyo! Sasa leo utasema mwenyewe na sitaki niendelee kupata kazi ya kukufuata burebure kila mara” alitamba yule mwanamke.


Ndipo Remi alipopata jibu ni kwanini aliingiliwa nyumbani kwake usiku na kwanini alimuona mtu akiishia kichochoroni wakati wa alipokuwa akitoka nyumbani kwake.


“wewe ndo ulikuwa kwangu usiku?” alihoji Remi huku akipiga hesabu za kutoingia tena mikononi mwa bazazi yule wa kike.


“unalala kibwege mno kama ulietoka kupigwa bao nne na mumeo!” alikejeli yule mwanamke.


“Nakuuliza tena uko wapi ukurasa wa Bombay?” alihoji yule mwanamke.


“Sijui unachosema bwana!” alikoroma Remi huku akionekana kuchanganyikiwa kwa swala lile jipya.


Yule mwanamke akamfuata taratibu bila kusema neno.


Lakini gafla Remi aliinuka chini kwa kasi akiwa ameshika bastola mkononi mwake kumtupia risasi mbili yule mvamizi.


Patupu!


Yule mwanamke alikuwa ni mwepesi kama unyoya, akachumpa na kuangukia upande mwingine huku risasi zikimkosa sentimita chache kutoka alipokuwa.

Remi nae hakutaka kuzubaa akaendelea kutupa risasi kumwelekea yule mwanamke ambae alikuwa anaruka kutoka sehemu moja kwenda nyingine.


Mwanamke mvamizi akaona mambo yasiwe mengi akaamua kuumwaga na kutokomea na santuri.

Remi alimfuata nyuma kwa kasi lakini kasi yake haikuwa sawa na ile aliotumia mvamizi.

Hadi anafika nje hakuwa amemuona yule mwanamke wala kivuli chake.


Bastola ilimuokoa mikononi mwa mwanamke yule baradhuli mana kwa mapigano asingeweza hakuwa mjuzi wa upande huo.


Remi nae hakutaka kukawia pale, alitoka haraka na kuelekea getini, lakini akakumbuka kitu, haraka akarejea ilipokuwa gari ya mwandishi Davis Minja.


Akaanza kulikagua tena kwa umakini wenye haraka ya wasiwasi.


Aliona alichokitaka!!


Kwa kawaida aina ya magari ambayo yalitengenezwa na kampuni ya Toyota toleo la miaka ya karibuni, magari yote ya Harrie yalikuwa na kamera moja kwa nyuma na ndio aliotaka kuona kama ipo.


Alielekea kwenye milango ya mbele upande wa kushoto na kwa dhoruba moja la kitako cha bastola alifanikiwa kuvunja kioo na kuingiza mkono na kufyatua kabali ya mlango kisha akaingia na kufungua hapa na pale kwenye upande wa kushoto wa usukani na punde akatoka na kikanda kidogo kilichoenea kwenye kiganja na kuondoka nacho haraka.


Afunga geti kama alivyolikuta na kuelekea ilipokuwa gari yake..


Akazama ndani na kuwasha, mara sauti kavu ya kiume ikaunguruma nyuma yake.


“Tulia hivyo hivyo mwanamke” ilifoka sauti ya kavu na Remi alisikia mguso wa chuma kisogoni kwake.


Mkojo ukagusa nyeti zake tayari kwa kutoka,na tumbo likamuunguruma kwa woga.


**





Alielekea kwenye milango ya mbele upande wa kushoto na kwa dhoruba moja la kitako cha bastola alifanikiwa kuvunja kioo na kuingiza mkono na kufyatua kabali ya mlango kisha akaingia na kufungua hapa na pale kwenye upande wa kushoto wa usukani na punde akatoka na kikanda kidogo kilichoenea kwenye kiganja na kuondoka nacho haraka.


Afunga geti kama alivyolikuta na kuelekea ilipokuwa gari yake..


Akazama ndani na kuwasha, mara sauti kavu ya kiume ikaunguruma nyuma yake.


“Tulia hivyo hivyo mwanamke” ilifoka sauti ya kavu na Remi alisikia mguso wa chuma kisogoni kwake.


Mkojo ukagusa nyeti zake tayari kwa kutoka,na tumbo likamuunguruma kwa woga.


“Ulifuata nini huku usiku huu?” sauti iliokuwa nyuma yake ilisaili.


Remi kwa haraka haraka aliitambua sauti ile ni ya Sajini Vengu.


Akashusha pumzi na kuitowesha hofu.


“Kuna kitu cha muhimu sana nilikuja kukichukua ambacho najua hakuna aliekumbuka kukichukua kati yenu” Alijibu Remi.


Sajini akapiga kimya kidogo.


“kwa hiyo unadhani tutakuwa hatukufanya uchunguzi vizuri?” Alisaili Sajini.


“Mnaweza kuwa mmefanya vizuri,ila ni ngumu kukifikia hiki ambacho nilikuja kukichukua” Alijibu Remi.


Sajini Vengu aliguna huku akitoa bastola kuchwani kwa Remi.


“Kitu gani hicho” aliuliza Sajini.


Mkanda wa kuhifadhi matukio yanayorekodiwa na kamera za siri za hapa ofisini”


Sajini alikaa sawa baada ya kusikia habari hiyo.


“Uko wapi sasa huo mkanda na unahisi utakuwa umerekodi vyema tukio lililotokea hapa?” Alisaili kwa kimuhemuhe Sajini.


Remi alitikisa kichwa kwa masikitiko kisha akasema…


“Wakati naingia, sikujua ndani kuna mtu nae alikuwa na lengo kama langu hivyo amenipiga na kuondoka na rekodi hiyo”


“Ooh shiit! Sasa ndo nini?” alihoji bila kujua Sajini.


“Yawezekana mi na wewe hatujajua nguvu inayotumika na hawa waliofanya hiki kitendo mana wanawahi kila sehemu tunayoifikia” alisema Remi na hapo Sajini akamtupia jicho la kiulizo katikati ya kiza kilichowatenganisha.


“Lakini nikuukize sasa; kwa nini unaingilia jeshi la polisi katika kazi zake?” alihoji Sajini.


“Kwa sababu mi ni mtuhumiwa wa hili tukio, lakini pia mume wangu ambae sijui aliko nae anahusishwa katika haya, hivyo nina kila sababu ya kujitahidi kulisaidia jeshi ili niepukane na hii dhahama” alijitetea Remi.


“Lakini hii ni hatari kwako, kufanya haya unayoyafanya na inaweza kukugarimu hadi uhai” Sajini alitahadharisha.


Remi alipiga kimya.


“ok una lolote la kunambia?” alivunja ukimya Sajini.


Remi akawasha taa za mle garini na kumgeukia Sajini.


“Hii inaweza kukupa mwanga katika kesi hii na mimi mkanitoa rasimi katika sakata hili ambalo hakika sijui linapotaka kunipeleka” Remi alisema huku akimpa Sajini kanda ndogo iliokuwa mkononi mwake.


Sajini aliichukua na kuitazama, na alitambua ni rekodi ya mienendo ya gari aliopewa.


Sajini akashika kitasa cha mlango wa gari na kutoka.

Alipokwisha kukanyaga chini, akaenda hadi upande wa dereva na kumtazama Remi.


“Ni heri zaidi ungekaa mbali na sakata hili na uache jeshi lifanye kazi yake bila kuingiliwa na wewe ambae unaweza kuharibu upelelezi.


Alisema Sajini na kugeuka kupotelea vichochoroni alikokuwa ametokea wakati akimfuatilia Remi.


Remi nae akaitia moto gari yake na kurejea nyumbani kwake kinondoni.


***


Wakati inatimia mida ya saa nne ahsubuhi kwa saa za Africa mashariki; kuna mambo mawili yalitokea kwa makusudi au ni bahati mbaya tu ilikuwa imesababisha yale yote.


Mosi; wakati kunapambazuka, tayari Sajini Vengu alikuwa ameshapata rekodi zilizorekodiwa na kuhifadhiwa ndani ya kifaa alichokuwa amepewa na Remi usiku uliopita.

Lakini kuna kitu kilimchanganya zaidi Sajini.

Rekodi ilionesha vizuri gari lililokuwa nyuma ya gari la mwandishi Davis Minja na pia liliendelea kurekodi hadi wakati linasimama na watu waliokuwa kwenye gari la nyuma walishuka.


“Military fatigue!” alijuliza Sajini huku akijitahidi kuzikuza sura za watu wale bila mafanikio.


“Sasa polisi anahusika vipi tena na utekaji?” alijiuliza Sajini bila kupata wa kumjibu.

Akaguna na kuzinakili pembeni namba za gari lililokuwa linafuatilia mwandishi Davis Minja.


Sajini akachukua simu na kupiga pahali kisha akahitaji kujua mmiliki wa gari ile.


Na hilo ndilo lililomkuta saa nne hiyo ahsubuhi akiwa na taharuki ya kutoelewa mambo yalivyo.


Eti gari lililotumiwa na watekaji linamilikiwa na Haji Makame.


Ebana ee!


Ajabu hii!!


Inakuwaje tena gari linalomilikiwa na Haji Makame lihusike na utekaji?


Mambo yalimchanganya Sajini na alishindwa kupambanua vyema kabisa.


Akili yake ilimwambia bado Remi anaweza kuwa anahusika, lakini kama anahusika kwanini utekaji na mauaji afanyie ofisini kwake?


Hata!!


Haiwezi kuwa rahisi hivyo,kuna tatizo sehemu na kilichomchanganya zaidi ni yale mavazi ya jeshi la polisi waliokuwa wamevaa watekaji.


Alihitaji kupata jibu litakalo mpunguzia msongo wa mawazo kuhusu matukio yale yaliokuwa yanazidi kuchukua sura mpya.


Alichukua simu na kumpigia Remi..


**

Upande mwingine pia ndani ya saa nne ile kulikuwa kuna jambo la pili lenye kumchanganya pia.


Remi hakuwa ametaka kutoka nje kwa siku hiyo,alikuwa amekaa kwenye meza akipangilia hesabu zake namna anavyoweza kutatua jambo lile bila papara na pia alikuwa anagojea simu ya Sajini kuhusu alichokiona kwenye rekodi aliompa.

Mawazo yake yakiwa bado yapo kwenye lindi la ukungu,aliamua kuchukua simu janja yake na kuperuzi hapa na pale.

Wakati anawasha data tu, akapokea ujumbe kwa njia ya whatsapp na ulitoka kwa mmoja wa wafanyakazi wake.


Aliufungua na kukutana na link mbili alizokuwa ametumiwa.


Akafungua!!


Link ya kwanza ilimpeleka kwenye tovuti ya mamlaka ya ukusanyaji kodi na mapato nchini. Ambapo alikutana na majina ya wadaiwa sugu wa kodi nchini yaliokuwa yametolewa na mamlaka hiyo.


Jina lake na kampuni yake lilikuwa miongoni mwa majina ya mwanzo kabisa katika orodha.


Hilo halikumstua sana japo lilikuwa geni kufanywa na mamlaka ile.


Link ya pili ndio iliokuwa na wahaka mkubwa katika fikira za Remi.


Aliifungua na kumpeleka kwenye tovuti ya mtandao wa matukio na habari muhimu wa Jamii forums.


Kichwa cha habari cha habari ile kilisomeka hivi:


“Mkimbizi anaeishi kinyemela nchini;aibuka kuwa mdaiwa sugu wa kodi katika kampuni yake inayofanya kazi kinyemela nchini.”

Remi aliufungua uzi ule na kuusoma.

Ndani alikutana na habari ndefu iliohusu wasifu wake na kampuni yake ambayo wasajili wa makampuni walikaririwa wakisema hawajui chochote kuhusu hiyo kampuni, lakini pia licha ya kuwapo kinyemela inahitajika kulipa kodi kwa muda wote ilipokuwapo na mbaya zaidi watu wa uhamiaji nao walikiririwa wakisema wanamtafuta mmiliki wa kampuni hiyo athibitishe uraia wake.

Baada ya hapo yalifuatia maoni mengi ya wanachama wa mtandao ule ambao kila mmoja alisema lake.


Remi alijikuta akilowa jasho mwili mzima huku moyo ukiongeza kasi ya udundaji wake.


Kweli alikuwa ameingia kwenye hujuma na wale watu waliendelea kumpa show waliomuahidi.


Remi alishindwa kujua ni kwanini kapokonywa uraia wake na kutangazwa kama mkimbizi, lakini pia ni kuhusu umiliki wa kampuni yake ambayo alikuwa ameisajili kikamilifu na kodi alilipa bila kukwepa.


Dah!!


Remi alichanganyikiwa hakika.


Ilianza ya mume wake kuitwa gaidi na sasa yeye ni mkimbizi halali sio tena mkimbizi aliejificha kwa kivuli cha kupewa uraia baada ya kufanya makubwa katika mkasa ulioandikwa kama Mpango wa Congo.


Alibaki akijuliza kama nchi hii ilistahili kumlipa ubaya wa aina hii hata baada ya kufanya mengi mazuri ili kuikomboa na watu dhalimu na majahili.


Remi alikuwa amehujumiwa hakika.


Lakini kama alijipanga kukukabiliana na hujuma zile, alikuwa anakosea na hakujua ndo kwanza hujuma zilianza.


Kwa kuwa usilojua ni sawa na usiku wa kiza kinene.


Remi hakujua yajayo hakika!!




Ilianza ya mume wake kuitwa gaidi na sasa yeye ni mkimbizi halali sio tena mkimbizi aliejificha kwa kivuli cha kupewa uraia baada ya kufanya makubwa katika mkasa ulioandikwa kama Mpango wa Congo.


Alibaki akijuliza kama nchi hii ilistahili kumlipa ubaya wa aina hii hata baada ya kufanya mengi mazuri ili kuikomboa na watu dhalimu na majahili.


Remi alikuwa amehujumiwa hakika.


Lakini kama alijipanga kukukabiliana na hujuma zile, alikuwa anakosea na hakujua ndo kwanza hujuma zilianza.


Kwa kuwa usilojua ni sawa na usiku wa kiza kinene.


Remi hakujua yajayo hakika!!


**


Akiwa bado hajui afanye nini na kichwa kinamzunguka kwa taarifa zile; Simu yake ilitetema.


Akaangalia namba ya mpigaji.


Sajini!!


Ilisomeka hivyo.

Akaipokea huku akiwa bado hajapata sauti walau ya kusema heloo!!


“Uko wapi hivi sasa?” Aliuliza Sajini baada ya kubaini simu yake imepokelewa.


“Nipo nyumbani!” alijibu Remi.


“Ok! Hii namba ya gari(akitaja namba) unaifahamu?” aliuliza Sajini Vengu.


Remi alishusha pumzi nyingi kwa mkupuo kisha akakaa sawa kwenye sofa, alihisi kuna habari nyingine mbaya zaidi.


Na ndivyo ilivyokuwa..


“Ndio, naifahamu. Ni namba za gari la mume wangu Haji” alisema Remi huku akingoja Sajini upande wa pili ajibu.


Sajini nae alipumua kwa nguvu na kusema.


“ile kanda ulionipa, nimeifanyia kazi na kufanikiwa, lakini gari lilofanya utekaji ni lenye namba hizo nilizokutaji”


“unasemaa!!” Remi alimaka kwa mshangao.


Na haraka akakimbilia dirisha lililokuwa upande wa pili kutoka alipokuwa na kusukuma kidogo kioo na kutazama nje kulikokuwa kunapakiwa magari ya mume wake na lake pia.


Magari yote matatu yalikuwepo na mawili kati ya matatu yalikuwa yamefunikwa kwa turubai jeusi kwa juu.


“Are you there?” alihoji kimombo Sajini Vengu huku akijistukia kama yupo sahihi ama la.


“aah hii inakuwaje afande!!” alihoji tena Remi.


“Nikuulize wewe, hii imekaaje” Alimrudishia mpira Remi.


Remi alikuna kichwa kwa kuchanganyikiwa.


“Afande; gari lenye hizo namba lipo hapa kwangu na hakuna ambae amewahi kulitumia tangu mume wangu aondoke nchini” alijibu Remi.


“una hakika gari hilo silo lililofanya haya?” alisaili Sajini.


“Hakika silo, mana hili gari lipo hapa limepaki kwa muda murefu sana bila kutamika”


Sajini aliguna kisha akasema.


“Usitoke hapo nyumbani nakuja kulikagua hilo gari na pia tuzungumze kitu fulani hivi kinachoweza kutupa mwanga japo inategemeana na ushirikiano wako” Alisema Sajini na kukata.


Wakati Sajini anakata simu, kuna upande mwingine nao ulikuwa unaweka chini simu na kutafarakari yale alioyasikia kutoka kwa Remi na Sajini Vengu.


“Vengu anataka kumshirikisha nini huyu mwanamke?” alijihoji yule bwana ambae wakati huo alikuwa amesimama akiangalia dirishani huku mikono akiwa ameifumbata kwa nyuma.


“Bado mapema sana kuruhusu makosa” alijisemea tena, huku mara hii akiingiza mkono mfukoni na kutoka na simu ngingine ndogo ambayo kwa kuitazama tu haiukuendana na hadhi yake.


Yule bwana kwa kutumia simu hiyo akapiga mahali..


**


Remi ndani kwake hakukulika, aliona ni kama anaenda kutumbukia kwenye shimo refu lisilo na mwisho wa kina chake, huku mara kwa mara akihisi atavamiwa na maaskari muda wowote na kumkamata.


Hakika aligwaya!!


**


Akiwa bado yupo njia panda huku akimsubiri Sajini Vengu; Remi akapata wazo na kuelekea chumbani kwake ambako alichukua kompyuta mpakato yake na kuiwasha kisha akaingia upande wa kuandika email na kuutuma kwa akaunti ya mumewe.


Aliamini kama ni mzima basi ipo siku ataufungua na kusoma na atajua kilicholendelea wakati yeye akiwa hayupo.


Akarejea sebuleni na ni wakati huo aliposikia mlango ukigongwa kwa kengele maalumu ilioko nje ya geti.


Alienda kufungua na alimkuta Sajini Vengu akiwa na usafiri wa pikipiki! Akaingia ndani ya ua kisha moja kwa moja walielekea kulipokuwa na maegesho ya magari ya nyumba ile.


“Kama unavyoona, gari hili hapa na lina hizo namba ulizozitaja,lakini tizama lilivyo,je waona limeingia barabarani hivi punde?” alisema Remi huku akifunua turubai lililokuwa limezifunika gari mbili za kampuni moja ila matoleo tofauti.


Sajini aliyatizama magari yale kwa makini na kweli aliona zile namba alizoziona kwenye picha iliorekodiwa na kamera maalumu kwenye gari alilokuwamo mwandishi Davis Minja.


Gari halikuonekana kuwa na dalili yoyote ya kutumika siku za hivi karibuni.


Sajini aliinama hadi kwenye uvungu wa gari ili kusikia kama gari linapumua kuashiria limetumika karibuni, ila alikutana na ukimya ambao ulimhakikishia hakukuwa na matumizi ya injini ya gari lile.


“Sasa mambo yanazidi kuwa makubwa Remi; na hadi sasa hakuna mwelekeo tuliopiga licha ya kujitahidi sana. Kwa akili za kawaida inamaana inatakiwa nikuweke chini ya ulinzi ili usaidie jeshi katika utata huu, lakini kwa askari makini huwezi kufanya hivyo ila utatakiwa kujua sababu zaidi ya kumweka huyo mtu chini ya ulinzi.” Alisema Sajini huku akijipangusa mchanga kwenye viganja vya mikono yake.


“Remi;unaweza kunambia mumeo alikuaga anaenda wapi na kwanini hajarudi?” Aliuliza Sajini.


Siwezi kujua kwa nini hajarudi ila wakati anaondoka alinambia anaenda Pakistani kwenye kozi maalumu” alijibu Remi.


“mh!! Sasa kwanini hajarejea na huku ofisi zinakana kuwa na mtu wa aina hiyo? Unahisi nini hapo?” alihoji Sajini huku akiwa makini sana kusikia jibu la Remi.


“Siwezi jua sababu ni nini, ila mambo ni mengi muda hauruhusu kujadili hayo ambayo yameanzia ndani ya uongozi, kwa sasa nadhani tunapaswa kujadili hili linalonihusu moja kwa moja afande!” Alisema Remi.


“Bado mumeo anahusika sana tu na inawezekana yote haya lengo ni yeye na ndivyo wanakutumia wewe ili atoke aliko aje!” Alisema Sajini.


Wazo lile lilionekana kumuingia Remi; lakini ikabaki swali moja kichwani mwake, ni nani yupo nyuma ya haya na ni nani aliemteka Davis au nae anahusikaje katika haya!


“Anyway,kuna mambo ambayo wewe hupaswi kuyajua ila kuna mkono mrefu katika hili na nimeanza kuingiwa na hofu hata mimi” alisema Sajini huku akiegemea kwenye gari na kuifumbata mikono yake kifuani pake.


“Kila ninakopita hawa jamaa wamefanya usafi wa kutokuhusishwa na tukio hili” alisema Sajini.


Remi aliguna tu!!


“Hakuna mtu yeyote unaehisi anahusika katika sakata hili au kutuongoza katika mkasa huu?” alihoji Sajini.


Remi alitatizika na alitaka kumtaja bwana kitambi ila alijikuta anasita tu kufanya hivyo na akaishia kutikisa kichwa kuashiria hajui lolote hadi wakati huo.


Sajini akatoka kwenye gari na kuanza kujongea,, lakini hakufanikisha dhamira yake hiyo ya kujongea bila kumpa taarifa Remi ya kile alichotaka kufanya, kama ni kuondoka ama kufanya kitu gani.


Sajini alijikuta akipaa juu na kudondokea kwenye gari alilokuwa ameegemea huku upande wake wa kushoto usawa wa moyo ukiwa na tundu kubwa la risasi na damu ilikuwa inamwagika kama bomba la maji lililotoboka.

Sajini koo lilimkauka na alishindwa hata kutamka kitu chochote alibaki akiwa amemkodolea macho Remi ambae alikuwa ameshikwa na mshangao mkubwa kwa kile kilichokuwa kinatokea mbele yake!!


Hakujua risasi ilikotokea na muuaji alikuwa amepiga kutokea wapi. Kwanini alimuua sajini wakati ambao yuko kwa Remi.


Hakika ulikuwa ni mtihani mwingine tena kwa Remi na hakujua atajinasua vipi katika hujuma ile.

Hesabu zake bado hazikuzaa matunda katika awamu ya pili ya showtime.


Alipiga hatua za aste aste na kufika pale alipoangukia Sajini Vengu; akainama na kuweka vidole vyake kwenye shingo ya Sajini ili kujua kama bado anapumua ili ampeleke hospital lau awahi kuokoa maisha yake, ila alikuta tayari mishipa imeanza kupoa na haidundi tena.


Ni wakati akinyanyuka ndipo alipohisi mwanga mkali wa kamera ukimmlika usoni. Haraka akageuka na kutizama kule alipohisi umetokea na kweli upande wa geti dogo alisimama mwanamke aliekuwa amevaa mavazi meusi juu hadi chini na kufunika uso wake na kubakiza macho tu.


Mwanamke yule begani mwake alikuwa amening’iniza silaha kubwa ya kudungulia na mkononi mwake akishika kamera kubwa sawa na za waandishi wa habari.


Remi alikuwa anatazamana na mwanamke waliepambana usiku ofisini kwake!!


Mwanamke yule akanyoosha vidole viwili kumwelekea Remi kisha akavipunga hewani mara mbili ishara ya mpigo wa bastola na kisha akavikunja vidole vyote na kubakiza kidole gumba kisha akakiinamishia chini ishara ya kuzika.


Remi aligwaya!!


Mwanamke yule akatoweka na Remi alishindwa hata kumfuata na punde tu kikasikika king’ora cha gari la polisi kikivuma kuelekea mitaa ile.


Moyo wa Remi ukapiga kite nguvu.

Macho yake akayageuza ulipo mwili wa Sajini.

Alijua ni nini kinafuata!


Remi matatani jama!!




Remi alikuwa anatazamana na mwanamke waliepambana usiku ofisini kwake!!


Mwanamke yule akanyoosha vidole viwili kumwelekea Remi kisha akavipunga hewani mara mbili ishara ya mpigo wa bastola na kisha akavikunja vidole vyote na kubakiza kidole gumba kisha akakiinamishia chini ishara ya kuzika.


Remi aligwaya!!


Mwanamke yule akatoweka na Remi alishindwa hata kumfuata na punde tu kikasikika king’ora cha gari la polisi kikivuma kuelekea mitaa ile.


Moyo wa Remi ukapiga kite nguvu.

Macho yake akayageuza ulipo mwili wa Sajini.

Alijua ni nini kinafuata!


Remi hakutaka kuingia kwenye mikono ya dola kirahisi vile huku akiacha mengi yakiwa yana makandokando.


Haraka akaruka na kuingia ndani kwake na kama kichaa akaanza kupekua hovyo vitu vyake vya muhimu na alipopata alivyohitaji akavitia kwenye mkoba na kwa kutumia mlango wa stoo aliweza kutoka nje na kuacha askari polisi wakiingia ndani kwake kwa fujo na wasimuone bali walishuhudia mwili wa Sajini Vengu ukiwa umesambaratika chini bila uhai.


Askari polisi walifika na kuendelea na taratibu zao, ikiwemo kuchukua alama za vidole na kutathimini tukio kwa mazingira walioyakuta, kisha wakatafuta vitu kadhaa walivyodhani vinaweza kuwafikisha kwenye ushahidi wa kumtia hatiani mtu aliehusika na mauaji ya askari mwenzao.

Kikosi kizima cha maaskari kilikuwa kinaongozwa na Sajenti Kobelo wa kituo kikuu cha wilaya ya Kinondoni.


Sajenti Kobelo ndie aliepokea simu kwa mtu aliejitambulisha kuwa ni raia mwema na alimtaarifu kuna mauaji ya mtu kwenye nyumba ile ambayo wao wamo hadi wakati huo.


Sajenti Kobelo aliingia ndani mwa nyumba ile na kuanza kukagua kwa weledi wa hali ya juu sana bila kupuuzia kila alichokiona. Hatimae macho yake yaligota kwenye picha moja ya askari mmoja ambae alikuwa amechafuka vyeo kwenye mabega yake na moja kwa moja alijua kabisa nyumba ile ilikuwa inamilikiwa na afande yule.

Macho yake pia yalikutana na picha ya mwanamke mzuri mweusi ambae alikuwa na uzuri wa asili na ngozi ya kuvutia na pembeni ya mwanamke yule alikuwa amesimama bwana mmoja mrefu na sura lenye tabasamu na alipotizama vizuri aliona sura ya bwana yule ndio ililiokuwa kwenye picha ya yule askari mwenye vyeo vya kutisha.


Sajenti aliifuata picha ile na kuichukua kisha akaitazama kwa umakini sana na hapo alijiridhisha ya kuwa watu wale walikuwa ni mke na mume.

Akaitupa pembeni picha ile na ndipo alipoona maandishi kadhaa nyuma ya picha ile baada ya kuwa imeanguka kwa kujigeuza mbele nyuma.


“Showtime!!” maneno yalikuwa yameandikwa hivyo na chini ya maneno yale pia aliona maneno mengine yakiwa yameandikwa kwa herufi kubwa ila mwandiko ulionekana kuwa ni tofauti na ule aliouona katika maandishi ya mwanzo.


“MATHEMATICS”

Yalisomeka vile yale maandishi na kitu kimoja kilipita kichwani mwake; kwa nini iwe miandiko miwili kwenye picha moja na kwanini inaonekana kuwa kama ni majibizano fulani baina ya waandishi wale?


Hakukuwa na kumfafanulia,akasonya na kuendelea na ukaguzi wake.


Nyumba ile ni ya askari na kwanini askari mwingine auwawe kwenye nyumba hiyo hiyo!! Na kwanini hakuonekani kuwa na mmiliki wakati huo!


Sajenti Kobelo alichukua kitabu chake kidogo na kuandika andika mambo kadhaa kisha akarudisha mfukoni kitabu kile na kuanza kutazama upya sebule aliokuwamo!!


Kitu alichogundua ni kuwa kulikuwa kuna mtu mle ndani muda mfupi uliopita, na pia nyumba ile aliona imepekuliwa na mikono miwili zaidi na mkono mmoja alihisi ni mkono wa mtu mwenye haraka na mwingine ni mkono wenye kukagua kiweledi sana ni kama unaotafuta kitu cha muhimu sana.


Sajenti yule akaandika tena kwenye kitabu chake ambacho alikitoa tena mfukoni baada ya kuwa amekihifadhi.


Sajenti akatoka hadi nje na kukuta harakati kadhaa zikiwa zinaendelea na akarudi hadi kwenye maiti alioikuta pale.


Alieuwawa alikuwa ni ofisa aliemfahamu vizuri tu kwa kuwa waliwahi kuwa wote kituo kimoja kabla ya kusambaratika na kila mtu kupangiwa kazi kituo kingine.


Alimfahamu Sajini Vengu.


Akamfunua shuka jeupe alilokuwa amefunikwa na akatazama tundu lililoingiza risasi mwilini mwa Sajini Vengu.


Alilitizama tundu lile kwa dakika moja nzima kisha akatoa kitabu chake na kuandika kitu alichohisi kuona kwenye jeraha lile lililopelekea kifo cha Sajini.


Aliona risasi iliopenya pale ni kubwa na yenye nguvu na ndio maana iliacha tundu kubwa lakini haikutokea nyuma ya mgongo!


Kwa nini!


Kwa sababu silaha zote ndogo ili ziwe na nguvu ya kuacha tundu kubwa ni lazima bastola iwe karibu kabisa na eneo ilipopenya risasi na kisha huenda kufumua nyama za nyuma na kutokea nje hivyo kuacha jeraha kubwa nyuma kuliko mbele ilikoingilia.

Lakini risasi ile ambayo inaonekana ilipenya na kukwama baada ya kuwa imetoka umbali wa mita kadhaa na hivyo kupoteza nguvu baada ya kuwa imeingia kwenye nyama.


Alipata jibu kwa hesabu zake ndogo ya kuwa mpigaji hakuwa karibu na marehemu ila alikuwa mbali na mwili wa marehemu wakati akishambulia.

Pia risasi iliopenya haiwezi kuwa ya bastola hata kidogo.


Akanyanyuka na kitabu chake kisha akafunika mwili ule na kuwageukia askari waliokuwa nyuma yake.


Lakini tofauti na alivyotegemea kukuta askari wake pekee, alikutana pia na sura moja ngeni iliokuwa imejaa kwenye vazi safi la jeshi la polisi huku cheo chake kikijitanabaisha kuwa ni Inspekta na mkononi alikuwa na kablasha na pia kalamu nyeusi na usoni alikuwa amepachika miwani ya macho huku akiwa tabasamu la ajabu usoni, yani hakueleweka alikuwa atanataka kucheka ama kulia ama kupiga chafya!!


Inspekta yule hakuongea, alitoa simu mfukoni na kumpa Sajenti Kobelo.


Sajenti nae bila kuuliza akaipokea na kuiweka sikioni kisha kilichofuata ni kukunja sura huku akiitikia “ndio” na alipomaliza akamrejeshea Inspekta simu yake.


“Yah!! Ndo hivyo unapaswa kuniachia mimi kesi hii kuanzia sasa na wewe na watu wako mnapaswa kuondoka hapa haraka iwezekanavyo Sajenti.” Aliunguruma yule bwana.


“Sawa afande!!” alijibu Sajenti Kobelo na kuwapa ishara askari aliokuja nao, nao walianza kumfuata ili waondoke!!


“Aah; naitwa Inspekta Kibe Kengeleo kutoka makao makuu na wengi hupenda kuniita Kenge badala ya Kengeleo” Alijitambulisha Inspekta Kenge.


Sajenti alitoa tabasamu la pembeni na kuendelea na safari yake na askari wake.


**


Wakiwa kwenye gari wanarejea kituoni; Sajenti alitoa karatasi ndogo katikati ya kitabu chake kidogo na kuipitia.

Karatasi ile alikuwa ameichukua mfukoni mwa suruali aliokuwa amevaa marehemu Sajini Vengu.


Kitu kimoja alichobaini ni kuwa Sajini alikuwa amendika namba za gari lililokuwa karibu na pale alipokuwa amepigiwa risasi lakini pia alikutana na maneno yalioandikwa kama kiulizo.


“Askari wanahusika vipi na utekaji?” ilisomeka hivyo katika karatasi ile.


Askari; utekaji!!


Aliyarudia maswali yale na hapo ikaja akili ya kuwa Sajini alikufa akiwa yupo kwenye kesi aliyokuwa anafuatilia.

Lakini kwa nini namba za gari lililokuwa pale ndizo zilizoko kwenye karatasi aliokuwa nayo marehemu na inaonekana ziliandikwa kabla ya umauti haujamkuta.


Hata! Haiwezekani!!


Sajenti alijikuta anatamani kuendelea kufuatilia kesi ile licha ya kuwa alipokea amri ya mkuu wake ya kuwa asifuatilie kesi ile na kumwachia Inspekta Kibe Kengeleo au Kenge kama alivyopenda kuitwa.


“Kenge!!” alirudia kulitaja hilo jina Sajenti Kobelo.


Sajenti alijiapiza ya kuwa hatoweza kuacha kesi ile bali ataifuatilia kimya kimya na hapo alikumbuka kitu.


Yawezekana kuna kablasha ambazo alikuwa anahifadhi mwenendo wa kesi yake nahitaji kuupata!



Alijiwazia Sajenti kisha akamwabia dereva ampeleke kituo cha Mwinjuma alikokuwa anafanyia kazi Sajini Vengu.


Gari ilielekea huko!!


***


Remi baada ya kukimbia nyumbani kwake, alielekea kwenye nyumba nyingine iliokuwa inamilikiwa na mumewe mitaa ya Moroco. Na alikuwa amekaa ndani na kufunga milango yote huku akilia kwa uchungu.


Simu zote alikuwa amezima na hakuna simu ilioingia ama kutoka na alifanya vile ili kukwepa yeyote ambae angelikuwa anamfuatilia kwa njia ya mtandao.

Alifuta machozi yaliokuwa yanamminika kama maji kisha akanyuka na kwenda kuuchukua mkoba wake ambao ulikuwa na vitu vingi alivyochukua wakati akitoka nyumbani kwake!


Akavimwaga chini vile vitu vyote, na alichokitaka alikiona.


Mkasi!!


Alihitaji kupunguza nywele zake ambazo alihisi ni mzigo mwingine usiokuwa wa lazima.


Alijikuta akimaliza zaidi ya saa zima kuzikata nywele kwa sababu kila mara alikuwa anakaa na kulifikilia swala lake lile na pia jinsi alivyomuona Sajini Vengu akivuta pumzi zake za mwisho!


Kwani ilikuwa lazima afe? Remi alijiuliza taratibu huku akivuta nywele na kuzikata.

.

Alikufa kwa sababu aligundua jambo au kwa kuwa wanahitaji kuniweka kubaya zaidi?


Remi bado hakupata jibu sahihi!!


Alimaliza kuzikata na kuziacha vile alivyotaka ziwe na kisha akataka kuurudisha kwenye mkoba na hapo macho yake yakaangukia kwenye kadi ndogo ambayo alipewa na Naibu Kamishina P Kagoshima.


Ilikuwa ni miongoni mwa vitu vilivyokuwa vimesambaa pale chini.


Akaikota na kuchukua simu ndogo ambayo hakuwa akiitumia sana.


Akaingiza namba zilizokuwa kwenye kadi ile na kupiga.


Simu iliita na kupokelewa punde.


“Ni mimi Remi!!” alisema Remi punde tu baada ya simu yake kupokelewa.



Kagoshima aliguna!


“Uko wapi wewe!!” Alihoji Naibu Kamishina.


“Nipo kwenye matatizo makubwa tafadhali naomba msaada wako”

Alisema Remi.


N. Kamishina Kagoshima alicheka sana kisha akasema…


“Wewe si ulisema hutakuja kuhitaji msaada wangu?” alihoji Kagoshima.


Remi hakujibu kitu.


“Nimesikia taarifa zako na kwa hili inabidi ujisalimishe jeshi la polisi ili kuepuka mambo mengi ambayo hayana mana” Alisema Kagoshima.


“Ni ngumu sana kwa mimi kujisalimisha kituoni, sijui adui yangu hivyo siwezi” Alijitutumua Remi.


“Serikali haishindwi kukutia nguvuni ili ujibu tuhuma zako Remi. Anyway unataka msaada gani kutoka kwangu.” Alihoji Kagoshima.


“Nahitaji kuonana na wewe!”


“Sasa nitaonana vipi na mtuhumiwa wa matukio makubwa!”

Alisema Kagoshima.


Remi aliguna tu.


“Sawa!! Naomba tuonane Panda hotel chumba namba 10,ila itabidi wote tusaidiane” alisema Kagoshima.


“Nikusaidie nini upande wangu” Alihoji Remi huku fikira fulani zikipita kichwani mwake.


“Ni mapema sana kusema ila lazima ujue ili nikusaidie lazima ujitoe” alisisitiza Kagoshima.


Toba!!


Remi alishika midomo yake huku akisikia utulivu wa hali ya juu kutoka upande wa pili.

“Sawa!!” alijibu Remi na kukata simu.


Naibu Kamishina P Kagoshima alitabasamu tabasamu fulani la ushindi.


“Namkula na kumfunga!! Mtoto safi huyu” Alisema Kagoshima akiwa peke yake ofisini kwake.


Je Remi atakubali kuliwa ili asaidiwe? Na vipi picha alizopigwa zina kazi gani? Sajenti Kobelo je atatimiza adhima yake? Na vipi kuhusu Kenge?


Ungana nami jioni!!





ma.


Remi aliguna tu.


“Sawa!! Naomba tuonane Panda hotel chumba namba 10,ila itabidi wote tusaidiane” alisema Kagoshima.


“Nikusaidie nini upande wangu” Alihoji Remi huku fikira fulani zikipita kichwani mwake.


“Ni mapema sana kusema ila lazima ujue ili nikusaidie lazima ujitoe” alisisitiza Kagoshima.


Toba!!


Remi alishika midomo yake huku akisikia utulivu wa hali ya juu kutoka upande wa pili.

“Sawa!!” alijibu Remi na kukata simu.


Naibu Kamishina P Kagoshima alitabasamu tabasamu fulani la ushindi.


“Namkula na kumfunga!! Mtoto safi huyu” Alisema Kagoshima akiwa peke yake ofisini kwake.


**


Mida ya saa mbili na nusu usiku ilimkuta Remi akiwa Pamba hotel na tayari alikuwa amekwishaingia ndani ya chumba namba kumi na alikuwa anatazamana na sura yenye ujivuni mwingi.


“Unakunywa wine?” alihoji Kagoshima.


“Hapana!” alijibu kwa mkato Remi.


Kagoshima alivuta funda moja la wine kisha akafinya midomo yake huku macho yake yakimtizama Remi.


“Ni kwamba hujawahi kunywa kabisa au ni leo tu” Alihoji tena Kagoshima.


“Sijawahi kunywa” Remi alijibu.


“Ooh sawa!! Na inakuwaje mrembo kama wewe unakosa kunywa lau hata tone la kileo?” Alihoji Kagoshima huku akigida tena funda la wine nzuri alioipenda.


Remi hakusema kitu.


“Mumeo Haji Makame hakika alifaidi sana kuwa na mwanamke mzuri kama wewe” Alisema tena Kagoshima.


“Afande nadhani tungelizungumza zaidi kilichotuleta hapa moja kwa moja” Alisema Remi huku akijitahidi kuzuia jaziba zilizoanza kumzonga kwa aina ya maongezi yale.


Kagoshima alitabasamu kifedhuli.


“Hata maongezi ya aina hii pia ndio yamenifanya nikubali kuonana na wewe japo wewe ni mtuhumiwa wangu” Alisema Kagoshima huku akitikisatikisa miguu yake aliokuwa ameibebanisha.


“Nadhani ulipaswa unisikilize shida yangu kisha utumie cheo chako kusimama katika haki na si uelekeo unaotaka tuelekee afande” Alisema tena Remi.


Kagoshima alicheka kwa sauti kisha akasema…

“Kwanza nikiwa mitaa hii huwa siruhusu kuitwa afande, na pia mwanadamu ni mwanadamu tu haijalishi ni yapi anakutana nayo ila hisia zinabaki kuwa pale pale” Alisema Kagoshima huku akiwa sasa ameifumbata mikono yake pamoja na kuikunja usawa wa kinywa chake.


“Kabla sijakwambia shida yangu naomba unambie unalenga nini” Alihoji Remi.


“Hakuna nacholenga zaidi ya mahusiano na wewe kisha nitajua namna ya kukusaidia” Alijibu Naibu Kamishina Kagoshima.


Remi alihisi mwili ukipitiwa na upepo baridi mithili ya pumzi za panya kwenye kidole cha mguu.


“Ila si wajua mi ni mke wa mtu?” Alihoji Remi.


“He is no more,hayupo tena na ni kama amekutelekeza tu huku akiwa amehamia na kuwa gaidi” Alisema kwa kebehi Kagoshima.


Remi alikunja ndita na kushusha pumzi ili kujaribu kuzuia gadhabu zilizoanza kumpanda.


“Lakini utawezaje kuwa na mahusiano na mkimbizi ambae habari zake zimetapakaa kote nchini ama ni vipi utakuwa na mtuhumiwa wa utekaji na mauaji?” Lilikuwa ni swali muhimu sana ambalo Remi aliuliza.


Kagoshima akacheka kisha akasema

“Lakini usasahu mi ni nani katika nchi hii”


“Sawa! Lakini usisahau ya kuwa cheo ni dhamana na nyakati hazidumu pia ila hatia ama tuhuma zinaishi milele na zaweza ibuliwa wakati wowote” Alisema Remi.


Kagoshima aliingiwa vyema na maneno yale nae akaamua kuhamisha mada.


“Anyway naomba unambie kilichofanya ukahitaji tukutane hapa”


“Nimegairi, kwa sababu ili unisaidie utanidai ngono” Remi alitamka wazi wazi mbele ya Kagoshima.


“Hapana,yote ni mapenzi yangu tu nilionayo kwako tangu siku ya kwanza niliokuona hivyo kuhusu tuhuma ni nje ya haya” Alijitetea Kagoshima.


Remi akasimama kwa lengo la kutoka ndani ya chumba kile, lakini kwa wepesi wa hali ya juu alijikuta akidakw mkono na mikono imara ya Kagoshima.


Vipi mrembo mbona unaenda tukiwa hatujamalizana” Alihoji Kagoshima.


“Kwani wataka tumalizaneje?” Alihoji huku akitetemeka.


“Aah kwani mi nimekwambiaje?”


“Lakini wajua utahukumiwa kwa kutaka kulala na mtuhumiwa?” Alihoji Remi.


Kagoshima akatoa macho kwa gadhabu na kumnasa kibao kikali Remi.


“Mimi sijawahi kataliwa wewe..iweje wewe unipe kebehi?” Alihoji kwa gadhabu Kagoshima.


Remi alijishika shavu lake lililokuwa linachonyota kwa ukali wa banzi alilopigwa.


“sasa naita maafande wakukamate”


Remi alinyoosha mikono na kumwambia..


“funga pingu, na unipeleke kituoni, matatizo yangu sio fursa kwa mafisi”


Kagoshima akaishia kumtazama Remi na asimmalize kwa ujasiri aliomuonesha.


Remi hakuwa mwanamke wa kutishika kwa vitisho vidogo; Remi tangu anakuwa hadi anafika hapo alipo ameshuhudia mengi kuliko hilo alilotaka kufanyiwa na Kagoshima.


Remi hakuteteleka kamwe. Remi alijali utu wake na kumvulia nguo Kagoshima ilikuwa ni kama kuutupa utu wake na kumdhalili mumewe.


Hata!! Hilo asingeweza kulifanya kamwe, huku akiwa hajui kama kukubali kudhalilishwa inaweza kuwa bado ni hasara, akachezewa na bado akaingizwa kwenye hatia!!.


Remi akaona bado afande amepigwa na butwaa,akavua mkoba wake na kuutupia kwenye sofa kisha akaanza kuvua T-shirt aliokuwa amevaa akaitupa pembeni na kubaki na braa kisha akaanza kufungua zipu ya suruali yake.


Dah!!


Kagoshima akabaki akiwa amebutwaika bila kujua lengo la Remi.


Kagoshima akamdaka mikono Remi wakati akianza kuishusha suruali yake.


“Sasa nini mana yake?” Alihoji Kagoshima.


“Nimekwambia wapigie wanikamate umeshindwa, sasa nataka nikuvulie nguo unifanye unavyotaka ili roho yako iridhike,shida yako si mwili wangu?” Alizungumza kwa jaziba Remi huku akifanya jitihada za kujinasua mikononi mwa Kagoshima.


“Ni kweli nakuhitaji ila unanishangaza kidogo kwa…”


“sio nakushangaza ila wewe ndie wanishangaza, hakuna haki inayopatikana kwa kuhongana mwili ndani ya Pamba hotel” alifoka Remi.


Kagoshima aligwaya na aliona amekosea mbinu, ikabidi awe mpole.


“Tafadhali naomba uvae nguo zako na uende” Alisema Kagoshima huku akirudi kukaa kwenye sofa lililokuwa mle ndani na kubaki akimtizama Remi akishugulika kuvaa nguo zake.


Remi alipokwisha kuvaa akadaka mkoba wake na kutoka nje.


Alipofika tu nje ya chumba akapumua kwa ahueni huku akitikisa kichwa kwa kushindwa kuamini kama kweli amejinasua mikononi mwa baradhuli yule anaetaka kutumia matatizo yake kujistarehesha.


“Kagoshima mtu mwenye tamaa nyingi sana” Alijisemea Remi huku akitokomea mbali na hotel ile.


Kagoshima nae alibaki akiwa amenuna na asiamini kilichomkuta kutoka kwa mwananke yule.


Akatoa tusi zito na kujitupa kitandani huku akimalizia kutuma ujumbe kwa kimada wake aende kumsindikizia usiku wake ulioharibiwa na Remi.


Usiku ukapita na ikaja ahsubuhi yenye mauzauza yake.


***

Ahsubuhi ilimkuta Sajenti Kobelo akiwa na gazeti mkononi mwake huku akiwa kwenye foleni akielekea mwananyamala.


Kurasa ya mbele ya gazeti lile ilikuwa imepambwa na picha kubwa ya Remi akiwa ameinama kutazama maiti iliokuwa chini huku kichwa cha habari kikisomeka “Balaa la mkimbizi laondoa uhai wa polisi” huku maneno ya pembeni yaliosindika picha zile yakisema “ni yule aliekwepa kulipa kodi na kuishi nchini kinyemela, aua askari aliefuatilia kesi yake…”


Sajenti akalikunjua kwa ndani na kuanza kusoma yaliondikwa kuhusu sakata lile.


Alipomaliza akarudi kutazama tena picha ile.


“Mbona hajaonekana kuwa na bastola au silaha yoyote? Lakini kama sie ni nani muuaji na aliepiga picha ni nani na alijuaje kuna mauaji tena ndani ya jumba lenye uzio?”


Akiwa anajiuliza hayo akapigiwa honi na gari lililokuwa nyuma yake kuashiria atembeze gari foleni inasogea!!


Kichwani mwake maswali yalikuwa ni mengi kuliko majibu.


Ahsubuhi ile radio mbali mbali zilikuwa zinatangaza vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali huku ikionekana habari kubwa ni ya mauaji ya ofisa wa jeshi la polisi.


Remi pia ambae hakuwa na usiku mzuri pia alikuwa ameamka na habari zake zilizoonekana kutikisa ahsubuhi ile.


Remi aliishiwa nguvu na kubaki akiwa anachuruzikwa na machozi sambamba na kamasi.


Remi alijuta kuijua Tanzania; na bado hakujua kiini cha yale yote na nini hatima ya mchezo ule na kwanini alilengwa yeye.


Hakika alitatizika!.




Akiwa anajiuliza hayo akapigiwa honi na gari lililokuwa nyuma yake kuashiria atembeze gari foleni inasogea!!


Kichwani mwake maswali yalikuwa ni mengi kuliko majibu.


Ahsubuhi ile radio mbali mbali zilikuwa zinatangaza vichwa vya habari vya magazeti mbali mbali huku ikionekana habari kubwa ni ya mauaji ya ofisa wa jeshi la polisi.


Remi pia ambae hakuwa na usiku mzuri pia alikuwa ameamka na habari zake zilizoonekana kutikisa ahsubuhi ile.


Remi aliishiwa nguvu na kubaki akiwa anachuruzikwa na machozi sambamba na kamasi.


Remi alijuta kuijua Tanzania; na bado hakujua kiini cha yale yote na nini hatima ya mchezo ule na kwanini alilengwa yeye.


Hakika alitatizika!.


***


MOGADISHU


“Sijasikia ukifanya lolote Komredi” Aliuliza Sozi ambae alikuwa ameshikilia kisu kilichokuwa kimetapakaa damu.


Honda alibaki akimtizama bila kusema neno, kisha akaendelea na safari yake na Sozi akaingia ndani ya bafu alilokuwako Honda.


Alipiga mluzi mkubwa baada ya kuona binti yupo chini na nguo zake zimeraruliwa hivyo.


Alijua Honda p.a.k Ahmed atakuwa amemaliza kazi.


Sozi akatoka nje haraka na kukuta Honda amerejea kwenye gari akiwatizama wengine walichokuwa wanakifanya kwa raia wasiokuwa na hatia.


Sehemu nyingine ndani ya mji wa Mogadishu kulisikika mlio wa bip mara tatu mfululizo na hapo Haji aliekuwa anavaa suruali akaruka na kuiendea rununu iliotoa mlio ule na pia Zedi aliekuwa amejilaza kitandani nae akakurupuka na kumfuata Haji ambae wakati huo alikuwa ameshika rununu maalumu kwa ajili ya kuwasiliana na Honda ambae alikuwa kwenye kikundi cha Al-Islamiya kama double Agent.


“Hawa jamaa hawana muda wa kumpuzika aisee” Alisema Haji huku akibonyeza hapa na pale juu ya rununu ile ya kijanja.


“Inamaana wamempa kazi sio!” Alihoji Zedi.


“Bila shaka” Alijibu Haji.


Mlio ule ulikuwa ni taarifa maalumu kwao ya kuwa Honda atakuwa na ujumbe kwao mahali fulani hivyo ilibidi kwa kutumia kifaa maalumu wamfuatilie kujua ni wapi watakutana nae.


Haji ambae alikuwa ni mtaalamu wa tehama aliweka mambo sawa na kisha walianza kujiandaa kwa ajili ya kutoka na kufuatilia mienendo yake.


Wakati walipomaliza kujiandaa ni wakati huo ambao waliona kifaa kile kikitoka kijiji cha Saadan na kuelekea kusini mwa Mogadishu kwenye pwani ya bahari ya Hindi ambako kulitumika kushusha mizigo mbalimbali na meli kubwa zilikuwa zinatia nanga huko.


Honda alikuwa mtulivu ndani ya gari huku akiwa amepewa smg iliokuwa imejaa risasi.

Kamongo nae alikuwa amekaa pembeni yake huku akitupia macho huku na huko kuhakikisha safari yao inakuwa salama kabisa.


Nyuma ya magari yote kulikuwa kuna magari zaidi ya sita na yote yalikuwa yamejaa wapiganaji wa Al-Islamiya.


Njia nzima ilitawaliwa na ukimya huku kila mara Honda akiona watu wanakimbia kila walipoona msafara ule.


Hatimae magari yalisimama pembezoni kabisa mwa bandari kisha wapiganaji wote wakasambaratika kila mmoja kuchukua usawa wake na ndani ya gari alibaki Honda na Kamongo.


“Wewe teremka na utakaa pale kwenye kontena na ukiona msafara wa magari mawili unaelekea ndani ya lango la bandari piga mluzi mrefu mara moja kisha shuka na unisubiri” Kamongo alimwambia Honda huku akimpiga juu ya bega na Honda akashuka bila kuuliza zaidi.


Honda alitizama eneo lile jinsi lililovyokaa na upande wa mbele yake aliona jumba kubwa lenye muonekano wa majumba ya kale.


Alitamani kufanya kitu ndani ya jumba lile ila hakuona upenyo wa kufanya hivyo.


Akajipa muda!!


Alienda kukaa juu kabisa ya kontena moja lililoonekana kutotumika muda mrefu kidogo na ni kama lilisahaulika na mamlaka za bandari.


Akatulia tuli na mtutu wake.


Haikuwa hadi nusu saa alipona gari mbili zenye nembo na bendera ya Somalia zikiwa zimeongozana zikiingia upande wa mashariki mwa bandari ambako kulitumika kupakua mizigo iliokuwa inaletwa na meli kubwa.


Honda alipiga mluzi kama alivyoelekezwa na Kamongo kisha akashuka na kumsubiri.


Punde kamongo akatokea akiwa na kisu pekee huku mtutu wake akiwa ameuacha ndani ya gari, akaongoza kuelekea kwenye usawa wa lango linalotumiwa na makuli kuingia na kutoka katika bandari ile.


Honda nae akafuata!!


Safari yao ilikuwa ni kuelekea kwenye meli moja iliokuwa imetia nanga pembezoni kidogo mwa bandari na ilikuwa ipo tayari kwa kupakuliwa mzigo.


Waliingia hadi ndani ya meli ile na kushuka chini kisha wakapita korido mbili na kushuka tena na hatimae walijikuta wakiwa wametokea kwenye ukumbi mkubwa tu na ndani yake kulikuwa kuna watu watatu.


Wawili kati yao walikuwa ni wenye asili ya ufaransa yani wazungu na mmoja alikuwa ni mwenye asili ya kisomali na umri ulianza kumtupa mkono.


Honda alimtambua mtu yule na hapo akaguna kimoyomoyo!!


Mtu yule alikuwa na wadhifa mkubwa serikalini.


Isa; huyu ni nani?” Aliuliza mzee yule huku akiwa ametupa macho kwa Honda.


Honda nae akajua jina la kamongo ni Isa.


“Anaitwa Ahmed; tumemkomboa kwa wa Marekani.” Alijibu Isa.


Yule mzee alibaki akiwa anamkodolea macho Honda; p.a.k Ahmed.


“Back to bussnes” Alisema yule mzee na kumgeukia mzungu mmoja na kumpa ishara ya kugonganisha vidole kwa pamoja.


Mzungu mmoja aliondoka pale ndani na kuelekea kwenye vyumba vingine vilivyokuwa kushoto mwa ukumbi ule.


Hakukaa sana akarejea akiwa na begi kubwa akiburuta chini.

Alipofika akaliweka juu ya meza na kufungua!


Ilikuwa ni shehena kubwa ya risasi na silaha tatu kubwa za kivita na bastola mbili za kisasa.


“Hawa watu ni hatari sana” alijisemea Honda.


“Mzigo upo ndani hii ni sampo” Alisema yule mzee.


Kamongo alizishika zile risasi na kuzitekenyetekenya, kisha akachukua bunduki moja na kuikoki mara kadhaa na aliporidhika akachukua kiwambo cha kuzuia sauti na kuweka risasi kisha akalenga na kupiga chini risasi zote alizoweka.


Akachelelea Kamongo au Isa kwa jina lake kamili.


Alipenda nguvu ya silaha ile.


Alimgeukia Honda na kumpa ishara na Honda akachukua bastola moja na kuitia risasi saba kisha akaivesha kiwambo cha kuzuia sauti na kupiga chini pia.


Zilitoka risasi sita na ile ya saba haikutoka na ndio risasi aliyotarajia hasa baada ya kuiona ikiwa na kimo na kipenyo tofauti na risasi zingine.

Alijua ni ujumbe kutoka CIA kama walivyokuwa wamemwambia ya kuwa atakutana na ujumbe siku kukiwa na ununuzi wa silaha.


Kila mtu alimtizama Honda baada ya risasi ya saba kugoma kutoka.


Honda nae aliwatizama na hatimae macho yake yakagongana na ya mzungu mmoja.


Mzungu yule akapepesa macho kwa namna ya ajabu kabisa.


Honda alishindwa kuelewa ishara ile ilimaanisha nini japo alijua ina ujumbe fulani.


Honda akafungua kibeti cha risasi na kuichomoa risasi ile kisha akaitazama tena huku akijua macho yote yapo kwake!!


“Ipo vizuri ila imechanganywa humu kimakosa” Alisema Honda.


Wale wazungu walitabasamu na Honda akaichukua risasi ile na kuitupia kwenye mfuko wa shati lake.


“Tunamalizana vipi sasa!!” Aliuliza yule mzee.


“Msikiti wa Masjid nuur; Imamu Shafi’i” Alijibu Isa.


Yule mzee akampa karatasi Isa kisha akaongea kwa lugha ya kihabeshi ambayo bila shaka si Honda ama wale wazungu walielewa na hakuna aliejua ni kwanini aliamua kuongea kilugha sehemu kama ile.

Na laiti wangejua, hakika kila mtu angelitafuta jeneza lake!.



***


Wale wazungu walitabasamu na Honda akaichukua risasi ile na kuitupia kwenye mfuko wa shati lake.


“Tunamalizana vipi sasa!!” Aliuliza yule mzee.


“Msikiti wa Masjid nuur; Imamu Shafi’i” Alijibu Isa.


Yule mzee akampa karatasi Isa kisha akaongea kwa lugha ya kihabeshi ambayo bila shaka si Honda ama wale wazungu walielewa na hakuna aliejua ni kwanini aliamua kuongea kilugha sehemu kama ile.

Na laiti wangejua, hakika kila mtu angelitafuta jeneza lake!.


***


Isa alimuita pembeni Honda baada ya kuwa amemsindikiza nje yule mzee.


Kulitokea mabishano kidogo kisha Honda akelekea kule ambako kulitolewa sihala za majaribio.


Huko alienda kukutana na shehena kubwa ya sihala nzuri na za kisasa huku kukiwa na mabomu ya kurusha kwa mkono na RPG za kutosha.


“Watu hawa wanajiandaa kufanya nini?” alijiuliza Honda huku mikono yake ikitalii kwenye vitako vya silaha zile.

Lakini tena alikumbuka mbinyo wa macho wa mzungu yule.


“Alitaka kunambia nini yule jamaa?” alijiuliza tena huku akitoka ndani ya chumba kile na kurejea ukumbini ambako bado wale wazungu wawili na Isa ama Kamongo kama ambvyo Honda alipenda kumuita.


“Kila kitu naona kipo sawa,ita vijana!!” Alisema Honda.


Isa hakumjibu, akageuka na kuchukua bastola moja iliokuwa imewekwa risasi nyingi na hazikuwa zimetumika.


Mzungu mmoja akaingiwa na mashaka!


“Nadhani tunemaliza na tuondoke sasa” yule mzungu aliepepesa kope zake wakati Honda anakagua silaha alizungumza.


Isa alicheka kwa dharau.


“Nani alisema ukioniona unapaswa kuishi?” alisema Isa huku akivuta kilimi cha kuondoa usalama.


Mara mzungu mmoja ambae alijua ni nini kitafuatia aliruka juu na kutua juu ya meza kisha kwa wepesi wa hali ya juu akapiga teke bastola iliokuwa mkononi mwa Isa na kusambaratika chini.


Isa hakutegemea kile kitendo na alipotaka kurudi nyuma alijikuta amechelewa akajikuta akienda chini mzimamzima baada ya kupigwa teke la sukuma katikati ya kifua.

Isa akataka kunyanyuka akajikuta akijaa mikononi mwa mzungu yule ambae alikuwa amegeuka mbogo ndani ya ukumbi ule.


Honda alibaki akiwatizama na huku kwa makini akifuatilia nyendo za mzungu aliekuwa amesimama huku akipeleka mkono wake nyuma ya kiuno.


Isa alipigwa kichwa cha paji la uso na kubaki akiona nyota nyota.


Mzungu yule akataka kutoa kisu na kupoteza umakini kwa Isa.

Isa nae hakutaka kupoteza hiyo bahati, kwa wepesi wa hali ya juu akamsukuma kwa nguvu yule mzungu kisha akaruka juu na kuachia teke safi lililoenda kutua kichwani kwa mzungu na kabla hajatulia akarusha tena teke zito lilitua mbavuni mwa mzungu na kumsambaratisha chini mzungu yule na ni wakati huo ambapo yalifanyika matukio mawili kwa wakati mmoja.


Isa alimuona vyema mzungu ambae alikuwa anajaribu kucheka na hisia za Honda kwa kuvuta silaha yake nyuma ya kiuno, hivyo haraka akachomoa kisu mbavuni mwake na kukirusha kistadi hadi kilipoenda kutua shingoni mwa mtu yule na ni wakati huo ambao mwili wake uliagana na nyonga kisha kupaa juu na kushuka huku akiwa amekunja goti moja na alipotua; alitua kwenye shingo ya mzungu aliekuwa anapambana nae na kuvunja shingo yake.

Isa akaruka na kutua pembeni huku akigonganisha viganja vyake kuashiria kazi imeisha.


Wazungu wote walienda chini kama mizigo.


Kazi kwisha!!


“nguruwe anamsumbuaje bwana wake!!” Alijitapa Isa; mtu mwenye kichwa kidogo na uso mwembamba huku akiwa na midomo kama samaki,alionesha umaridadi wake katika sanaa ya mapigano.


“U mjuvi sana wa kazi hizi komredi” Alisifia Honda.


“Ndio mana nilipewa kitengo na mrithi wangu ni Sozi.” Alizidi kujitapa Isa huku akichomoa kisu chake shingoni kwa mzungu ambae alikuwa anapigania pumzi zake za mwisho.


Isa alitoa simu ya upepo na kuwasiliana na vijana walioko nje kisha akamgeukia Honda.

“Mzee yule aliagiza tuwauwe hawa wazungu walioleta hizi silaha mana alihisi si wauzaji wa kawaida” Alifafanua ni kwa sababu gani aliwaua.


“Inapendeza!!” alijibu kiufupi tu bwana Honda.


Dakika sita baadae tayari silaha zilianza kusombwa kutoka ndani ya meli kuelekea nje ambako kulikuwa kuna ulinzi wa kutosha kuhakikisha usalama upo wa kutosha.


Honda nae alitaka kutumia mwanya ule kuelekea kule kwenye lile gofu aliloliona.


Taratibu akatoka akiwa ameongozana na vijana waliokuwa wanasomba silaha.


Hakuna alimtilia shaka!


Akatoka nje ya meli na huko alikutana na Sozi ambae alikuwa bize kabisa kuhakikisha usalama unakuwa wa asilimia zote.


Akaambaa na giza kama anaeenda kujisaidia kisha akapotea na kuelekea liliko gofu alilioona.


Safari yake ilikuwa ya umakini wa hali ya juu huku akihakisha hakuna anaemfuatilia.


Alijua anafanya jambo la hatari lakini hakujali kitu mana aliamua kujitoa muhanga kufanya operesheni ya hatari na watu hatari.


Alizidi kutokomea na hatimae akaingia kwenye jumba lile lililokuwa lina upweke wa kutisha.


Nyasi zilianza kutengeneza makazi ndani yake.

Akatoa kalamu ndogo iliokuwa maalumu kwa kumulika nyakati za usiku na kuanza kumulika ukutani.

Ulionekana kuwa ni ukuta wa rangi ilioanza kuchakaa.


Alisakanyasakanya jiwe ama kijiti na hatimae alipata kijiti ambacho kilimfaa sana.


Akaandika kitu ukutani kisha akatoweka ndani ya gofu lile na kuanza safari ya kurudi kule alikotoka.


Lakini alihisi kitu nyuma yake na kwa uzoefu wake alijua kabisa nyuma yake kuna mtu na ndivyo ilivyokuwa nae ilibidi atumie mbinu za kimedani kumtambua mtu yule.


Mara nyingi walifundishwa mbinu za kujificha kwa adui (camouflage).


**

Sozi alimaliza zoezi la kusimamia usalama na akampa taarifa Isa ambae alitoka na wakapanda wote ndani ya magari, ila Honda hakuonekana.


Wakajipa muda kidogo.


Dakika sita zilikatika bila Honda kutokea.


Isa akatoa amri ya kuanza msako wa kumtafuta Honda.


Vijana walizunguka kwa dakika tatu tu kila eneo bila kumuona Honda.


Isa alichanganyikiwa na hesabu zake zilimwaminisha ya kuwa Ahmed atakuwa ameamua kuwatoroka na kuendelea na maisha yake!


Akajua adhabu ambayo angelikutana nayo ni kubwa na ni kifo kwa uzembe alioufanya.


Vijana wakajipanga kungojea amri kutoka kwa Isa na muda ulizidi kwenda na eneo lile walihitajika kutoka kwa kuwa vikosi vya serikali vingepita pale kuweka doria.


“Mnadhani nini sasa!!” Honda aliwastua wote bila kufafanua kauli yake.


Wakamgeukia kwa pamoja.


Honda hakuwa peke yake,alikuwa amebeba mtu kwenye bega la kushoto na mkono wa kulia alishika mtutu wa bunduki.


Akajongea taratibu na kupita kati yao kisha akambwaga chini yule mtu ambae alikuwa amevaa koti refu jeusi na alikuwa na bastola kiunoni mwake, lakini pia shingoni kulikuwa kuna mkanda wa kamera ndogo yenye uwezo mkubwa wa kuchukua picha gizani.


Sozi akaiwahi kamera ile na kuanza kupitia picha zile zilizokuwa mle.


“Huyu bwege alitupiga picha tangu tuko kule kijijini” Alisema Sozi huku akimkabidhi Isa ile kamera.


Wote walizika hisia mbaya walizoanza kujenga kwa Honda na sasa walianza kumuona ni mtu mwenye akili nyingi sana.


“Umefanya kazi kubwa sana kujua uwepo wa huyu nyoka” Alisema Isa huku akimwinamia yule mtu ambae alionekana kupitia dhoruba nyingi kutoka kwenye mkono wa komando na gaidi aliekubuhu Ahmed Gailan p.a.k Honda.


“Huyu ni kutoka AL shabaab; nadhani wanajua uwepo wetu sasa” Alisema Isa kisha akatoa ishara fulani na vijana waliuchukua ule mwili na kuanza kuucharanga mapanga kisha kuutenganisha kiungo kimoja baada ya kingine.


Zoezi lilipokamilika msafara ukaondoka.


*****


Zedi na Haji walikuwa makini kabisa kufuatilia mwenendo wa ile alama nyekundu iliokuwa kwenye kifaa chao.


Nao walikuwa mitaa ile ya bandari, hata wakati alama ile inaelekea upande wa lile gofu, wao hawakuwa mbali na gofu lile na baada ya kuhisi kuwa ujumbe umeachwa alama ile ilizima na ilimanisha kazi imeishia pale.


Wakabaki na kazi moja tu kuhakikisha wanajua ilipozimia.

Haikuwachukua muda mrefu walijua ilizimikia kwenye jengo la mambo ya kale liliteketea kwa moto miaka kadhaa nyuma.


Waliingia hadi kwenye hilo gofu na kuanza kuangaza huku na huko kwa kutumia kurunzi ndogo kwa sababu hawakutaka kuvuta hisia za mtu ambae angelikuwa anakatisha mitaa ile.


“Kaa nyuma yangu na unitazame” Zedi alimwambia Haji Makame.


Zedi aliendelea kupitia kila sehemu na hatimae akaona mkwaruzo wa soli ngumu chini.


Nae akaenda hadi pale na alipotizama chini aliona aina ya mkwaruzo ule ni kama ulikusudiwa.


Akasimama huku akipiga hesabu za namna alivyokuwa amesimama mkwaruzaji.


“Aliposimama hapa, alitizama huku” Alisema Zedi huku macho yake yakielekea kule alikohisi msimamaji alisimama na kutazama.


Aliona!!


Macho yake yaliona mikwaruzo hafifu ukutani, akasogea na kuimulika kwa karibu zaidi.


“KEKERA” aliyanakili maneno yale kisha akaendelea kuchunguza ukutani pale na hatimae aliona tena maandishi mengine.


“Nü..Mdjust..flshai>”

Akayanakili tena maneno yale kisha akamstua Haji na wakapotea kwenye eneo lile na kurudi kwenye makazi yao ambayo yalikuwa katikati ya mji wa Mogadishu.


Saa moja badae iliwakuta wakiwa wametulia kwenye nyumba za viongozi wa serikali wakiwa ni kama walinzi wa viongozi wa ngazi za juu walioishi eneo lile ni hii ni baada ya kuhama kwenye hotel waliokuwa wakiishi tangu wafike Mogadishu. Makazi yao yalikuwa karibu na ubalozi wa Uturuki na hawakuwa mbali na Lido beach.


Waliweka mezani maneno walioyakuta kule kwenye gofu na yaliandikwa kwa code za kificho ili ambae atakutana nao na hahusiki basi asiweze kutambua kinachondelea.

Walianza na neno KEKERA.


Ndio ni kekera ila ila alimaanisha nini katika ujumbe huu” Alisema Haji huku akili yake ikizunguka kuhakikisha wanavunja code ile na kujua maana halisi ya ujumbe uliokusudiwa.


Zedi alikuna kichwa,hakujua ni nini sababu ila alijisikia tu kukuna kichwa.


Na kilichowachanganya ni kuwa ujumbe ulikuja kwa haraka sana tofauti na matarajio yao na hivyo kufanya kujua ya kuwa ujumbe ule ni wa muhimu sana.


Tatizo ni wa kuvunja fumbo.


Nywele ziliwasimama na ni lazima wafumbue ili wajue yaliomo.


Kazi ilikuwa ngumu hakika na muda ulizidi kusonga.


****





Akasimama huku akipiga hesabu za namna alivyokuwa amesimama mkwaruzaji.


“Aliposimama hapa, alitizama huku” Alisema Zedi huku macho yake yakielekea kule alikohisi msimamaji alisimama na kutazama.


Aliona!!


Macho yake yaliona mikwaruzo hafifu ukutani, akasogea na kuimulika kwa karibu zaidi.


“KEKERA” aliyanakili maneno yale kisha akaendelea kuchunguza ukutani pale na hatimae aliona tena maandishi mengine.


“Nü..Mdjust..flshai>”

Akayanakili tena maneno yale kisha akamstua Haji na wakapotea kwenye eneo lile na kurudi kwenye makazi yao ambayo yalikuwa katikati ya mji wa Mogadishu.


Saa moja badae iliwakuta wakiwa wametulia kwenye nyumba za viongozi wa serikali wakiwa ni kama walinzi wa viongozi wa ngazi za juu walioishi eneo lile ni hii ni baada ya kuhama kwenye hotel waliokuwa wakiishi tangu wafike Mogadishu. Makazi yao yalikuwa karibu na ubalozi wa Uturuki na hawakuwa mbali na Lido beach.


Waliweka mezani maneno walioyakuta kule kwenye gofu na yaliandikwa kwa code za kificho ili ambae atakutana nao na hahusiki basi asiweze kutambua kinachondelea.

Walianza na neno KEKERA.


Ndio ni kekera ila ila alimaanisha nini katika ujumbe huu” Alisema Haji huku akili yake ikizunguka kuhakikisha wanavunja code ile na kujua maana halisi ya ujumbe uliokusudiwa.


Zedi alikuna kichwa,hakujua ni nini sababu ila alijisikia tu kukuna kichwa.


Na kilichowachanganya ni kuwa ujumbe ulikuja kwa haraka sana tofauti na matarajio yao na hivyo kufanya kujua ya kuwa ujumbe ule ni wa muhimu sana.


Tatizo ni wa kuvunja fumbo.


Nywele ziliwasimama na ni lazima wafumbue ili wajue yaliomo.


Kazi ilikuwa ngumu hakika na muda ulizidi kusonga.


Ilipita zaidi ya nusu saa,hakuna mtu Kati yao aliekuwa ametongoa lau maana ya maneno yale.


Tunafanya nini sasa!? Zedi alimuuliza Haji.


Hebu tujaribu kudadavua hili neno la pili.


“Nü..Mdjust..flshai>”


Waliyapitia tena maneno yale kisha kwa pamoja walianza kukubaliana kitu kimojakimoja kilichoonekana kuwaletea maana.


Walianza na neno “físhai”


Walianza kulipindua pindua ili kuleta maana katika lugha inayoeleweka.


Hatimae jibu waIilipata.


“Bila shaka ukiliweka liwe jina la mtu intapendeza sana!!” Alisema Haji.


“Ok jaribu kulisuka liwe jina” Alisema Zedi huku sasa akiwa anatazama mikono ya Haji iliokuwa bize kuandika.


“Ona hii” Haji alimwonesha Zedi karatasi.


“Shafi’i” Zedi alilitamka lile jina.


“Yesi ni Shafi’I” alisisitiza Haji.


“Aisee!! Inaleta mana hii” alisema Zedi huku akitabasamu.


“Na kama ni jina basi hilo ni la kiislam na kama ndivyo,basi alitaka tujue kitu kuhusu huyu jamaa” Alisema Zedi.


“Na nionavyo huyu atakuwa ni Imamu na kama ni Imamu basi haya maandishia yaliosalia ni jina la Msikiti.

“Nü..Mdjust..


“Yes,hebu igeuze hiyo u iwe a kisha tukiivunja tuseme hilo ..Mdjust. alimaanisha Masjid na hii “Nü..” inamaanisha nuur kwa sababu hapo juu ya u kuna doti mbili ikimaanisha hizo ni u mbili hivyo basi tunaweza kuusoma kama “Masjid nuur” Alisema Haji.


Zedi alitabasamu kiushindi.


“Kwa hiyo anamaanisha tumtafute Imamu Shafi’I kwenye msikiti wa Masjid nuur” Alisema Zedi.


“Lakini tunamtafuta kwa uzuri ama ubaya” Alihoji Haji.


“Haiwezi kuwa uzuri mana hapa Somali tupo sisi tu katika hii suicide mission na hakuna mwingine, hivyo huyo ni mbaya” Zedi alitanabaisha hisia zake.


Walikubaliana katika hilo.


Wakarudi tena kwa neno “KEKERA”


“kwani kesho ni siku gani?” Aliuliza Haji


“Alhamis” Alijibu Zed.


“Rais wa Kenya anahutubia si ndio” alihoji tena Haji na Zedi akaitikia.


“Basi tuliweke hili neno kama Kesho kenya Rais” Alifafanua Haji.


Zedi akaruka juu na kupiga mluzi wa nguvu kisha akaachia bonge la mtusi kuashiria kuwa anakubaliana na wa mawazo ya Haji.


“Sasa nimeelewa alichomaanisha bwana, yani mbali na kumtafuta Imamu Shafi’I; inatakiwa pia tujue kesho kuna tukio lingine kwenye hotuba ya Rais wa Kenya hapa Somalia” Alisema Zedi.


“sasa ana maana gani” Alihoji Haji huku akijikuna kichwa.


“He need to rescue the president” Alisema Zedi.


“Yah hilo linaweza kuwa ndilo wazo lake, lakini sasa hajasema litatokea tukio gani nyakati hizo” Alionesha mashaka Haji.


“Hawa ni magaidi na magaidi siku zote huwa wana njia mbili za kutekeleza mashambulio yao. Kwanza ni kwa kutumia collar bomb, hapa ni kujitoa muhanga na njia ya pili ni kwa kutumia wadunguaji” Alisema Zedi.


“Sasa hapa watatumia njia gani?” Aliuliza Haji.


“Ndo kazi yetu kujua ila nadhani wanaweza kutumia mdunguaji kwa sababu kujitoa muhanga mazingira yatakuwa hayawaruhusu.

Haji aliguna huku akikaa karibu na kompyuta lengo alitaka kujua ni wapi hasa mkutano wa Rais wa Kenya utafanyikia.


Aliwasha data na kuanza kuperuzi habari zinazohusu ziara hiyo.


“Watakuwa katikati ya mji kwenye ukumbi wa hoteli ya Lamada.” Alisema Haji huku akiendelea kuchezesha vidole vyake.


“Pale ni rahisi sana shambulio kufanyika kwa sababu ya majengo yaliozunguka hotel ile” Alisema Zedi.


“Hapa tukimtafuta mdunguaji tutachelewa, ila inabidi tuweke taharuki dakika chache baada ya hotuba kuanza” Alishauri Haji.


“Hatuwezi jua nafasi gani wanatumia ili kutekeleza tukio lao,hivyo inabidi tujue tunavuruga vipi mkutano huo kabla haujaanza” Alisema Zedi.


“So!” Alihoji Zedi.


“Tupange fake bomb, lile litazua taharuki na viongozi wataondolewa kabla ya kufanyika tukio”



“ooh sawa kamanda” Alisema Haji huku akiinuka na kuchukua chupa ya soda iliokuwa mezani kisha akachukua shati lake na kuiviringisha juu yake na alipomaliza alichukua kinyundo kidogo ambacho hutembea nacho kwenye begi akaanza kuiponda.


Dakika kumi baadae ule unga alikuwa anaujaza kwenye chupa nyingine na kisha alichukua njiti za kiberiti nazo pia alizisaga na kumchanganya ndani ya chupa iliokuwa na unga wa chupa iliosagwa kisha akachukua wine nyekundu iliokuwa kwenye jokofu na kuimimina mle na alichukua pia kiasi kidogo cha soda ya pepsi na kuweka kisha alianza kutikisa kwa nguvu na ilipoleta fukuto akafunika na kizibo kwa juu kisha akagongelea ili kuziba vizuri.


“ewaa,sasa huo mlio wake, bomu la nyukilia likasome kibada dadeki” Haji alijigamba.


“Hongera komredi mana naona unakamilisha taharuki” zedi alisema huku akicheka na kukaa kitandani.


“Zedi; hatuna muda wa kupoteza, ngoja tumsake huyu Imamu na msikiti wake” Alisema Haji huku akirudi tena kwenye kompyuta na kuendelea kutafuta jina la Masjid nuur.


Ukapita ukimya kidogo.


“Huu msikiti upo karibu na Casapoplare road na kilomita moja nyuma pia kuna shule ya msingi ya Imamu Shafi’I” Alisema Haji huku vidole vyake vikifanya kazi ya kusonta kwenye kioo cha kompyuta ambapo kulikuwa kuna ramani ya eneo lile.


“Jamaa inaonekana yupo vizuri mfukoni” Alisema Zedi.


“Tutajua mbivu na mbichi akijaa kwenye kumi na nane zetu” Alisema Haji.


Waliendelea kusoma ramani ile ili wajue mazingira ya kumtafuta Imamu Shafi’I.


Usiku nao ulizidi kuwa mkubwa!.


***


Honda na kundi la wapiganaji walipokewa katika misitu ya Ganigani kulikokuwa na kambi yao kubwa. Misitu ile ilikuwa juu ya vilima vya Ganigani na asilimia kubwa mji wa Mogadishu ulionekana vyema kuanzia pale.


Eneo lile lilikuwa ni la kimkakati kwao kwa sababu ya za kiusalama.


Mahema mengi na vidungu vilitamalaki eneo kubwa sana la kambi ile.


Wapiganaji wengi walikuwa ni watoto chini ya miaka kumi na saba lakini kwa mazoezi makali waliokuwa wanapitia walionekana kuwa ni wakubwa kuliko umri wao.


Sozi alimvuta mkono Honda na kuelekea nae kwenye hema moja lililokuwa pembeni kidogo ya kimlima.


“Hii ndo nyumba yako, maisha yetu unayajua hivyo vumilia, siku za furaha zinakaribia” Alisema Sozi.


Honda alitabasamu.


“Kwani kule Saadan kulikuwa ni kwa nani na kwanini kambi isiwe kule?” Alihoji Honda


“Hata mimi sijui ile nyumba ni ya nani, na sijawahi kuona mmiliki wake,lakini pia haiwezi kuishi mjini na hakuna usalama kabisa kule” Alisema Sozi na kisha akagongesha mikono na Honda na kuondoka kwenye hema lile.


Honda alibaki peke yake,alizunguka kila pahali kukagua na alipohakikisha kila kitu kiko sawa akaelekea kwenye godoro la sufi lililokuwa limewekwa juu ya kichanja.


Akajaribu kulala, alikutana na vumbi kubwa sana likitimka.


Akaguna.


Akalitoa godoro lile na kulipigapiga ili kupunguza vumbi.


Isa nae akaingia!!


“Inabidi uzoee na ndio maisha yetu yalivyo” Alisema Isa.


Honda hakujibu!


“Sasa hapa kuna jukumu kubwa la kufanya kesho na jukumu lenyewe ni kumwondoa mtu anaetusumbua hapa Somali ikiwa na yeye ana nchi yake, Kesho atakuwa hotel Lamada na vijana watu wameshafanya ukaguzi wa kutosha na hali ya ulinzi ni kubwa sana hivyo tumeona bora tutumie wadunguaji ambao watakaa jengo hili na hili” Alisema Isa huku akimwonesha Honda ramani aliokuwa ameshikilia mkononi.


“Vipi una uhakika una wadunguaji makini?” Alihoji Honda.


“Ninao vijana sita ni hodari sana kwa kazi hiyo” Isa alijibu.


“Good!!” Aliitikia Honda.


Isa aliondoka kwenye hema lile ili kumwacha Honda apumzike mana usiku ulikolea na mvua ilianza kunyesha.


Honda alipobaki peke yake, alitoa ile risasi alioikuta kwenye furushi la risasi zingine.

Akaifungua kichungi chake na ndani alikutana na kidude kidogo mithili ya kadi ya simu ila kilikuwa kinavibonyezeo kama viwili hivi na pia kulikuwa kuna kikaratasi chembamba kilichokuwa na maneno machache ya kiingereza.


“Press when you meet flamingo” Alijua ni kwanini alipewa kidubwasha kile kwa njia ile.


Alitafuna kikaratasi kile kisha akachukua kikasha cha risasi na kukifunga na kurudisha mfukoni huku kidubwasha kile akikipachika ndani ya nywele zake ndefu alizokuwa amezikata mtindo wa afro.


Kitu ambacho hakujua ni kuwa wakati analazimisha kikae sawia kwenye nywele alikibonyeza bahati mbaya na kilianza kusoma mawimbi.


Sozi alikuwa amelala na Isa pia alikuwa amelala.

Ila kuna mtu hema fulani hakuwa amelala na ni mwiko kwake kulala.

Mtu huyu alikuwa ni mtaalamu wa mawasiliano na kazi yake alihakikisha ananasa mawimbi ya radio yoyote ambayo ingelikuwa inasogelea kambi yao kwa sababu makomando ili wavamie ni lazima wawe na vifaa vya mawasiliano na pia alikuwa ndie anaeunganisha mawasiliano yote ya kambi nzima na watu waliokuwa nje ya kambi ambao ni viongozi wao.


Kifaa kimoja kilianza kukoroma kuashiria kuna muunganiko wa mawimbi rasimi na yasio rasimi.

Bwana yule akakifuatilia kifaa kile nacho kiliendelea kukoroma na kila alipojaribu kufuatilia mwelekeo wa mawimbi alipata ugumu kwa sababu ya mvua kubwa ya radi na miungurumo iliathiri utendaji wa kifaa kile.


Aligwaya!!


Ilimaanisha kufeli kwake ni kuangamiza kambi nzima.


Akavaa nguo za kuzuia mvua, akachukua kurunzi na kisu kisha akanyofoa kifaa kile na kutoka nje huku taratibu akiendelea kufuatilia mawimbi yale.


Honda alikuwa amelala chali huku mawazo lukuki yakipita kichwani kwake na utulivu wa mwili kwake ilikuwa ni afueni ili achanganue mambo.


Baada ya dakika nyingi za kuwaza hili na lile, taratibu usingizi ukaanza kujenga kibanda kichwani pake.


Mara muungurumo mkubwa wa radi ukarindima.


Usingizi ulikata.


Lakini akili yake ilimwambia kuna kitu cha ziada amekisikia wakati wa ngurumo ile.


Akatega sikio vyema.


Wakati wa mtiririko wa mvua “tatatatata……!” kuna sauti nyingine aliisikia katikati ya mtiririko ule.


Akatega tena!!


“tatatata.. ti..tatatata..ti..”


Ile ti,ilimwashia kengele ya tahadhari.


“hakuna mlinzi anaeweza kutembea katikati ya mvua kubwa hii” Alijisemea!!


Ndipo alipoamka na pia akahisi kitu kikiwaka na kuzima kichwani kwake.


Akakitoa kifaa kile na kukibonyeza kikaacha kumweka.


“tatatata…ti….tatatata..ti..”

Bado aliendelea kusikia sauti ile na sasa ilizidi kukaribia kwenye hema lake.


Roho ikamdunda!!





“hakuna mlinzi anaeweza kutembea katikati ya mvua kubwa hii” Alijisemea!!


Ndipo alipoamka na pia akahisi kitu kikiwaka na kuzima kichwani kwake.


Akakitoa kifaa kile na kukibonyeza kikaacha kumweka.


“tatatata…ti….tatatata..ti..”

Bado aliendelea kusikia sauti ile na sasa ilizidi kukaribia kwenye hema lake.


Roho ikamdunda!!


Kule nje yule bwana aliendelea kuhangaika kutafuta mwelekeo wa mawimbi na bado alijua mawimbi yale yalitokea kwenye moja ya mahema aliokuwa amesimama kati yake.


Akawa anapiga hatua moja mbele na hatua moja nyuma,yani bila kutoka pale alipokua lengo likiwa ni kujua mweleko sahihi wa mawimbi mageni.


Hatimae alijua ni upande gani mawimbi yale yalikuwa.


Honda nae kule ndani alikuwa amesimama karibu kabisa na mlango na kwa kusaidiwa na mwanga wa radi, aliweza kuona mtu akiwa hatua chache kutoka mlangoni kwake na alikuwa anahangaika huku na huko.


Honda akili ikamjia na haraka akawasha kidubwasha kile na kukirudisha ndani ya kikasha cha risasi kisha akaruka hatua kubwa na kuangukia kitandani na kulala.


“Aisee hawa watu wana mitambo yenye nguvu sana” Alijiwazia huku akimalizia kujifunika shuka.


Dakika moja badae, yule bwana aliingia mule ndani na bila kujali kama alikuta mtu au la, yeye aliendelea kukagua hapa na pale.

Hatimae kile kifaa kilianza kutoa mlio mkubwa mfululizo na Honda akaamka na kukutana na kisu kikiwa shingoni mwake.


“ulikuja kutupepeleza sio? Alihoji yule bwana huku akitumia mkono mwingine kuwasiliana kwa simu ya upepo.


Hazikupita dakika tatu wapiganaji zaidi ya sita wenye mitutu waliingia mle ndani na kumweka kati Honda.


Isa nae akaingia.


Yule bwana akampa maelekezo kwa lugha ya kienyeji na kisha akamwonesha kifaa kile chenye muundo wa risasi alichokikuta kwenye viatu vya Honda.


“Hii si ni ile ya kule melini?” Alihoji Isa huku akimtizama Honda.


“Ndo yenyewe! Kwani kuna nini mbona navamiwa usiku huu? Alihoji Honda.


“Aah ni usalama tu unazingatiwa ila usijali” Alisema Isa huku akiwapa ishara wapiganaji wake nao wakashusha silaha zao.


“Wale wazungu walikuwa ni mamluki na tulikuwa sahihi kuwapoteza, walituwekea mtego wa kujua tulipo aisee” Alisema Isa huku akimwangalia Honda ambae wakati huo alikuwa anafanya jitihada za kunyanyuka kitandani.


Isa aliongea na vijana wake kuwaelesha na kisha wakasambaratika mle hemani na kukiharibu kifaa kile.


Honda alipumua kwa afueni na kurudi kujilaza na hakulapua lau tone la usingizi hadi ilipotimu ahsubuhi.


***

Ahsubuhi ilikuwa na mengi ya kufanya kwa pande zaidi ya tatu.


Honda na wapiganaji wa AIAI waliamka wakiwa na lengo moja la kufanya mauaji katikati ya Mogadishu huku wadunguaji wakifanya zoezi kwa ajili ya kukamilisha kazi yao mida ya jioni ya siku hiyo.


Upande mwingine ulikuwa ni ule wa Zedi Wimba na Haji Makame ambao wao lengo lao lilikuwa ni kuvuruga mipango ya wauaji na kumuokoa Rais bila uwepo wao kujulikana popote.


Kundi lingine lilikuwa ni kundi la ulinzi na usalama wa viongozi wote watakao hudhuria mkutano huo na bila kujua lolote linalopangwa, wao waliendelea na taratibu zao kama kawaida kuhakikisha usalama upo kwa asilimia zote.


Hatimae wakati uliwadia!!


Maeneo yote yalikuwa na ulinzi wa kutosha kuhakikisha eneo la Lamada na viunga vyake lipo salama.


Misafara ya viongozi mbalimbali ilianza kuwasili kwenye hotel Lamada.


Aliingia Rais wa Somalia kisha akafuatia Rais wa Kenya na wajumbe wake.


Katika majengo matatu yaliokuwa yanatazamana na hotel ile, kulikuwa kuna makundi mawili yenye malengo tofauti.


Kundi la kwanza lilikuwa lile la wadunguaji ambao kila mmoja alikuwa amekaa sehemu yake kuhakikisha mlengwa wao hawamkosi na walitaka kufanikisha azima yao hiyo wakati rais huyo atakapokuwa akitoka ndani ya hotel.


Kundi lingine lilikuwa ni lile ambalo lilikuwa na watu wawili tu na wao walikuwa kwenye chumba cha hotel nyingine wakiwa na chupa yao iliokuwa na unga wa chupa nyingine na vitu vingine kadhaa ambavyo vingehakikisha sauti iliokusudiwa inatoka.


Walikaa wakihakikisha kabisa kila tukio linaloendelea kule chini linatazamwa na wao mubashara bila kukosa hata nukta.


Muda wa kuanza kikao ulianza na watu mbalimbali walikuwa wapo na radio zao wakisikiliza.


Waliongea viongozi kadhaa na hatimae wakati rais wa Kenya anataka kuzungumza; Zedi na Haji walikonyezana.


Na hatua iliofuata ilikuwa ni kufungua dirisha kisha wakapachika chupa ya bia kwenye mdomo wa bunduki aina ya gobole kisha wakafyatua kuelekea kule ilipokuwa Lamada hotel na kilichofuata ni sauti kubwa ilioambatana na moshi mzito.


Ilikuwa ni taharuki iliozuka,walinzi wa viongozi hawakujua kimetokea nini na harakati zao zilikuwa ni kuhakikisha hakuna madhara yanayotokea kwa viongozi hao.


Wadunguaji nao walibaki wakiwa wamebutwaika wasijue kilichotokea.


Isa ambae alikuwa karibu ya eneo la tukio na Honda; walishuhudia mtafaruku usiosemekana.

“Shukeni wote, na msiache alama” Isa alitahadharisha vijana wake kisha akaondoa gari na wakarejea porini huku wakiwa wameshindwa kuekeleza mpango wao.


Zedi na Haji nao walikuwa wako mbali na eneo lile huku wakiwa wanashingilia ushindi wao kwa kuvuruga mpango ule ambao hawakuwa na hakika kama walikuwa sahihi,ila walijua wamefanya kile walichopaswa kufanya.


Na kazi ikabaki ni kumtafuta Imamu Shafi’I wa msikiti wa Masjid nuur.



***


- TANZANIA-


Ahsubuhi ile ilikuwa ni ahsubuhi mbaya kabisa kwa Remi.


Alilia peke yake na kulikuwa hakuna wa kumsaidia wala kumuonea huruma.


Alilia na Mungu wake.


Nchi nzima kulitapakaa taarifa zake na picha zake, mitandao ya kijamii ilikuwa ndio taarifa kuu.


Alikuwa amesahau kuzima simu yake na mara ikaita.


Namba zilikuwa ni za Kagoshima.


“Nadhani kuna haja ya wewe kujisalimisha kituoni”

Alisema Kagoshima.


“Muda ukifika nitafanya hivyo ila sio sasa” Alijibu kinyonge Remi.


“Ila tambua serikali ina mkono mrefu itakufikia tu” Alisema Kagoshima.


“Haina shida” Alijibu Remi na kukata simu.


Alishusha pumzi na kuzishusha, alihitaji kuhama pale mana si pahali salama tena kwake.


Walikuwa na nyumba nyingine mwananyamala kisiwani.


Wakati anatoka kwenye ile nyumba alihisi hayuko peke yake,licha ya kujifunika kanga juu hadi chini.

Licha ya kuhisi huko lakini kamwe hakuona mtu mwenyewe yupo umbali gani nae mana watu walikuwa ni wengi nyuma yake.


Alichukua bodaboda na kwenda kushukia komakoma na kuanza kutupa tena miguu yake kwa hatua za mashaka tele.


Hakufika hata mbali, alihisi kitu kidogo kikipenya kwenye shingo yake na kilichofuata hakujua licha ya kuhisi akiangukia mikononi mwa mtu.


Remi mbio zake ziliishia ukingoni.




- TANZANIA-


Ahsubuhi ile ilikuwa ni ahsubuhi mbaya kabisa kwa Remi.


Alilia peke yake na kulikuwa hakuna wa kumsaidia wala kumuonea huruma.


Alilia na Mungu wake.


Nchi nzima kulitapakaa taarifa zake na picha zake, mitandao ya kijamii ilikuwa ndio taarifa kuu.


Alikuwa amesahau kuzima simu yake na mara ikaita.


Namba zilikuwa ni za Kagoshima.


“Nadhani kuna haja ya wewe kujisalimisha kituoni”

Alisema Kagoshima.


“Muda ukifika nitafanya hivyo ila sio sasa” Alijibu kinyonge Remi.


“Ila tambua serikali ina mkono mrefu itakufikia tu” Alisema Kagoshima.


“Haina shida” Alijibu Remi na kukata simu.


Alishusha pumzi na kuzishusha, alihitaji kuhama pale mana si pahali salama tena kwake.


Walikuwa na nyumba nyingine mwananyamala kisiwani.


Wakati anatoka kwenye ile nyumba alihisi hayuko peke yake,licha ya kujifunika kanga juu hadi chini.

Licha ya kuhisi huko lakini kamwe hakuona mtu mwenyewe yupo umbali gani nae mana watu walikuwa ni wengi nyuma yake.


Alichukua bodaboda na kwenda kushukia komakoma na kuanza kutupa tena miguu yake kwa hatua za mashaka tele.


Hakufika hata mbali, alihisi kitu kidogo kikipenya kwenye shingo yake na kilichofuata hakujua licha ya kuhisi akiangukia mikononi mwa mtu.


Remi mbio zake ziliishia ukingoni.


***


Sajenti Kobelo; aliegesha gari kwenye uwanja wa ccm mwinjuma kisha akatembea kwa miguu kuelekea kilipokuwa kituo cha polisi.


Baada ya kufanya taratibu zote za kujitambulisha na kueleza nia yake pale kituoni, hatimae alielekezwa ilipokuwa ofisi ya marehemu Vengu ambayo ilikuwa inakaimiwa na mtu mwingine wakati huo.


Aliingia na kumkuta mtu yule ambae alikuwa na cheo sawa na chake.


Itifaki ilizingatiwa kisha akasema kilichompeleka pale.


Alipewa faili ambalo alikuwa akilitumia Sajini Vengu.


Alianza kuyakagua kwa umakini wa hali ya juu sana.


Alikutana na maelezo yaliokuwa yameandikwa na Remi. Pia alisoma namna tukio la kutekwa kwa mwandishi lilivyomhusanisha na ofisi za uchunguzi wa mambo kale na pia ni kwanini mtuhumiwa alitakiwa kuwa Remi.


Alitoa kitabu chake kidogi a kuanza kuandika yale alioona ni muhimu kwake na pia alikutana na namba za simu za Remi.


Alizinakili pia kisha akawa ametoka na picha mbili tofauti.


Remi anahusika na pia Remi hahusiki.


Kwanini?


Kwa sababu Remi aliwasiliana na Davis Minja na kumwelekeza jambo hivyo anahusika kwa asilimia kadhaa kujua alipo mwandishi yule.


Lakini pia Remi anaweza kuwa hahusiki kwa sababu asingeweza kufanya tukio akiwa ofisini kwake.

Hoja ya mwisho ilikuwa na mashiko kidogo.


Lakini kuna kitu kingine kilimpa maswali…

Kwa nini Davis afuatiliwe na kisha atekwe kwenye ofisi za Remi?


Remi Haji Makame!!

Aliliandika jina lile kwenye kitabu chake kisha akaaga na kuondoka.


Lakini kabla hajatoka mle ofisini akamgeukia ofisa aliemkuta mle ndani.


“Kama kuna mtu atakuja kujitambulisha kwako kwa jina la Kenge; basi mwambie lolote ila sio hizo kablasha nilizokagua” Alisema sajenti Kobelo.


Ofisa yule alikubali.


Sajenti alitoka na kuelekea alikokuwa amepaki gari lake, akapanda na kuondoka lengo likiwa ni kuelekea nyumbani kwa Sajini Vengu ambae msiba ulikuwa umewekwa kwao kimara na yeye alikuwa anaishi mwananyamala kwa Bibi titi.


Njiani yalipita maswali kadhaa kichwani kwake.


Alihitaji kumjua kwanza Remi.

Haji Makame ni jina la watu wa Pemba na kiasili ni waislam na Remi ni jina ambalo halijasidifu imani yoyote ila si jina lenye asili ya huko Pemba; sasa vije tena Remi iungane na Makame?


Hata!!


Kuna walakini katika jina hilo.


Lakini kulikuwa kuna haja gani ya kumuua Sajini Vengu?


Kuna jambo si bure.


Alipiga ngeta baada ya mwili wake kumsisimka.


Moja ya vitu alivyokuwa amejaliwa Sajenti kobelo; ni hisia.

Kila anapokuwa katikati ya jambo zito, mwili wake huamsha msisimko usiokifani na hapo hujiandaa kukabiliana na hatari.


Kwa maelekezo ya ananuani alioikuta ndani ya kituo cha mwinjuma ni kuwa Vengu aliishi nyumba namba kumi na tano.


Njia haikuruhusu gari kupita, alitafuta sehemu alioona inafaa akapaki gari kisha akaanza kutafuta namba ya nyumba hiyo.


Hakukawia kuiona!


Kulikuwa kuna geti jekundu na nyumba ilionekana kuwa pweke.


Akasukuma geti na kuingia ndani kisha akageuka na kulitazama lile geti.


Inamaana hakuwa amelifunga hili geti?


Hakukuwa na wa kumjibu.


Akapiga hatua zake ndogo ndogo huku akijaribu kutazama mazingira ya nje ya nyumba ile ambayo haikuwa kubwa licha ya kuwa na geti.


Kulia kwake kulikuwa kuna kibanda ambacho kwa ndani kulikuwa kuna pikipiki kubwa ya Baja.


Akarudisha macho kutazama mlangoni mwa nyumba.


Mmmh!!


Aliguna baada ya kuhisi kuchunguliwa na mtu kutokea ndani upande ambao alihisi kuna chumba kulingana na dirisha lilivyokuwa limekaa.


Alihisi kabisa kuna mtu alikuwa amesogeza pazia na kumtazama.


Ni nan na anafanya nini?


Akaongeza tahadhari!!


Akasukuma mlango.


Nao ulikuwa wazi.


Ala!!


Akaingia kwa tahadhari kubwa huku akiwa makini kuliko makini yenyewe.


Mezani alikuta kuna kompyuta mpakato iliokuwa imefungwa nusu yani kama vile mfungaji alikuwa na haraka sana.


Akaikunja kompyuta ile kisha akaiacha pale mezani na kuanza kupiga hatua kuelekea kwenye chumba alichohisi kuona mtu akimtizama.


Alipokaribia mlangoni tu akajikuta akirushwa sebuleni kwa teke zito lilitua sawia kifuani mwake na kwenda kumsambaratisha chini kama mzigo.


Akakataka kusimama ila alijikuta akijaa kwenye mikono ya mvamizi na kupigwa double hit kifuani kwa lengo la kumvunja mifupa ya kifua ila akawahi kujua hila hiyo hivyo kwa tabu akajitahidi kurudi nyuma kwa mtindo wa aina yake na kujikuta akipamia kabati ambalo alisambaratika nalo chini.


Bado mvamizi hakumwacha, akamzoa chini kwa mikono miwili kisha akamtwisha kichwa katikati ya paji la uso na Kobelo akabweka kama mbwa dume aliepokonywa mwanamke wake.


Maumivu yakamsambaa mwili mzima.


Kobelo akaona akizubaa nae ataitwa maiti.


Kwa nguvu zilizosalia akajiachia na kufyatuka kichwa kikali kilichoenda kutua kifuani mwa mvamizi na kisha kumrusha nyuma kwa kasi na kumbwaga chini akasambaratika kama gunia la nyanya mbichi huku akilia kama mbwa jike aliezidiwa na mkuyenge.


Sajenti kobelo aligundua kitu wakati akijipanga kumkabili adui.

Alihisi kichwa chake kimekutana na nyama laini hivi lakini kilio kilichotoka kilikuwa cha kike.


Ebana e!


Mvamizi alisimama,alikuwa ni mwanamke.


Kila mmoja alijipanga kumkabili mwenzie.


Mvamizi akanesa kidogo na kuachia ngumi za harakaharaka lakini zote zilienda kupiga hewa na alijikuta akipokea makonde mawili ya nguvu mbavuni mwake.


Akabweka kama bwege.


Akajaribu tena kurusha mateke, lakini yalipanguliwa kistadi na sajenti kisha akamwachia konde zito kwenye mbavu za kulia.


Mvamizi alimanusura atapike dagaa aliokula.


Alipojaribu kuhema akashindwa na alipotaka kusimama pia alishindwa.


“Mwanamke waacha kuoelewa unakuja kupambana na waume zako pumbavu wewe” Alisema Sajenti Kobelo huku akiwa anamtazama mvamizi akijaribu kujiinua bila mafanikio.


Mara likatokea tukio ambalo Kobelo hakulitarajia.


Mvamizi kwa kasi ya ajabu alitoa kitu mifukoni kwake na kupiga chini na kuzuka moshi mzito ambao ulimchanganya Kobelo na alichosikia ni sauti ya mgongano wa mtu na mlango na alioojaribu kufuata nyuma hakuna alichoambulia zaidi ya sauti za mgongano wa milango ya geti.


“ooh shit” alimaka Sajenti huku akirudi ndani na kuikwapua kompyuta kisha akatoka haraka eneo lile.


Kitu ambacho hakujua ni kuwa kompyuta ile ilienda kuzua utata.


Utata ambao ulizidi kuwa utata!!


***


Nb: hakuna kitu kinachokatisha tamaa Kama kuona uposti zaidi ya vipande sita kwa siku tatu afu unakutana na komenti nne tu na pale unapokuwa na majukumu mengine usipoposit siku mbili kuna watu wanatokea na kukuvurumishia majina ya kila aina mara unalinga mara hivi mara vile,wakati ukipost huwaoni.


Ni wambie kitu!!


Hakuna kitu ambacho mwandishi anapenda na kupata moyo kuendelea na kazi yake kama kuona anapata sapoti na ushauri wa watu kuhusu kazi anayoipost kwa sababu unapoandika huwa upo peke yako na unapopost unabaki kuwa peke yako dah lazima ukate tamaa au hata ule mzuka wa kutupia kila siku unaweza kuisha na usijali.





Mvamizi kwa kasi ya ajabu alitoa kitu mifukoni kwake na kupiga chini na kuzuka moshi mzito ambao ulimchanganya Kobelo na alichosikia ni sauti ya mgongano wa mtu na mlango na alioojaribu kufuata nyuma hakuna alichoambulia zaidi ya sauti za mgongano wa milango ya geti.


“ooh shit” alimaka Sajenti huku akirudi ndani na kuikwapua kompyuta kisha akatoka haraka eneo lile.


Kitu ambacho hakujua ni kuwa kompyuta ile ilienda kuzua utata.


Utata ambao ulizidi kuwa utata!!


***


Sajenti Kobelo alizidi kuona ugumu wa kazi ile hasa baada ya kupambana na mwanamke aliekuwa amejiziba uso wake kuanzia juu hadi chini.


“Alifuata nini nyumbani pale?” Alijiuliza bila kupata majibu na alizidi kuendesha gari kurejea nyumbani kwake.


“Kuna tatizo pahali kuhusu inshu hii” Alijisemea tena huku macho yake akiyatupa kwenye kompyuta mpakato iliokuwa kwenye kiti cha kushoto kwake.


Safari yake ilimfikisha nyumbani kwake na alishuka moja kwa moja alielekea ndani na kupitiliza hadi kwenye chumba kidogo kilichokuwa kimesheheni vifaa vingi vya mawasiliano.

Alikaa kwenye kiti kisha akachukua waya uliokuwa umeungwa kwenye umeme na kuchomeka kwenye kompyuta alioingia nayo mule ndani.


Akaiwasha na kuanza kupekuwa mafaili yaliokuwa yamehifadhiwa mule na hakuna la maana alilolipata.


Alipokuwa mbioni kukata tamaa akaona kwa chini kuna faili limeandikwa “REMI”


Akalifungua!!


Akakutana na maneno “inawezekana vipi?” kisha yakafuatia maneno mengine kwa chini “kwanini askari?” Alizidi kushuka na maneno mengine kadhaa ambayo yalikuwa na viulizo vingi.


Hatimae alifika kwenye ujumbe wa picha na kuufungua.


Video ile ilionesha gari likiwa linakimbia kwa kasi sana na ilivyoonesha picha zilizpigwa kutoka kwenye gari lililokuwa mbele na ilionekana ni mfukuzano uliokuwa baina ya gari zile.

Kuna kitu kilimshangaza kwenye gari ile iliokuwa nyuma ya gari la mbele.


Namba za gari!!


Namba alizoziona ni zile zile namba zilizokuwa kwenye gari aliloliona kule alikofia Sajini Vengu.


Aliguna!!


Kisha akachukua kalamu na kutaka kuandika ila akakumbuka karatasi alioichukua mfukoni mwa marehemu, akaitoa.


Alikutana na maneno yale yale ya viulizo na kisha kufuatiwa na namba za gari zilezile alizokuwa akizitazama kwenye picha mjongeo.


Video ilifika wakati ambao kuna tukio liliendelea ila kwa kuwa kamera ilikuwa inachukua kwa nyuma tu, hakuweza kuona ila alisikia purukushani kisha ikafuatiwa na mlipuko wa risasi na miguno na kisha akaona tena watu waliovalia sare za jeshi la polisi na kilichofuatia hapo ni video kuzima.


“ina maana polisi walihusika katika utekaji huu? Sasa kwa nini walitumia gari lenye namba sawa na za lile lililokuwa kwa Remi?”


Akaguna tena!!


Lakini kwanini Remi na Remi ni nani hasa?


Akajiuliza huku akihamia kwenye kompyuta kubwa iliokuwa mezani na kuiwasha kisha akawasha data na kuanza kuperuzi kuhusu Remi.


Alichokutana nacho ndicho kilichomshangaza.


Kweli Remi alikuwa ni mkimbizi ila alishatunukiwa uraia kwa ushujaa wake katika mkasa wa Congo sasa vije tena aitwe mkimbizi? Na vipi wale waliomtunuku nishani ya ushujaa wapo wapi wakati huu.


Aliguna tena na kisha akachukua kitabu chake na kurejea yale aliokuwa ameyaandika wakati alipokuwa anautazama mwili wa marehemu Vengu.


“Huyu binti hakuuwa bwana!!” Alijikatalia peke yake.


Hili tundu sio la mpigo wa bunduki ndogo” Alijisemea tena huku akiwa anazidi kupitia hiki na kile kuhakikisha anapata picha kamili ya tukio lilivyokuwa.


Bado nafsi yake ilimwambia Remi hawezi kuwa mhusika.


Akakumbuka kitu


Alikumbuka kachumbari ya jina la Remi.


Remi Haji Makame!


Akalitaja tena lile jina na kuliandika kwenye kompyuta na kufuta lile la Remi na kubaki Haji Makame.


Ex soldier? Alijiuliza baada ya kuona tovuti moja ikimtaja kama ni mwanajeshi zamani, lakini pia alitajwa kama aliwahi kuwa askari polisi wa cheo cha juu na hivi sasa hatambuliki baada ya kuwa anajihusisha na ugaidi na sasa anatafutwa na serikali ya marekani.


Mmh!! Inawezekana vipi hii! Alijiuliza tena.


Mambo yalizidi kumchanganya.


Haji tayari alikuwa ameshafutwa katika utumishi na alinasibishwa kama mtu hatari.


Hapo akawa amepata jibu ya kuwa Haji alikuwa ni mume wa Remi na walioana miaka kadhaa nyuma.



Alihitaji kumpata Remi.


Alichukua namba za simu zilizokuwa zimeandikwa kwenye vitabu vya Vengu na kuzipiga ila hazikuwa zikipatikana.


Alishusha pumzi nyingi na kuzishusha, hakujua aanzie wapi kudadavua jambo lile.


Wanataka nini kwa huyu mwanamke?


Alikumbuka kitu, akatoka na kuelekea kwenye gari lake na kuchukua gazeti lililokuwa limeandika habari za mauaji ya Vengu.


Alikuwa anatafuta mwandishi wa habari ile ila kama kawaida katika habari kama hizo huwa kunakuwa na neno “Na mwandishi wetu”


Alifyonza!!


Akapiga tena namba iliompigia kumpa taarifa ya mauaji ya Vengu; nayo haikupatikana.


Alirudi tena kwenye sifuri.


Akaigemea kiti na kushika kichwa huku akitizama kompyuta yake.


Hakupata jibu!!


Akainuka na kurejea tena kwenye kitabu chake, akarudia kusoma baadhi ya mambo alionukuu kutoka kwenye kablasha la Vengu kule kituoni.


Akasoma tena muda uliokisiwa kutumika katika utekaji na mauaji ofisini kwa Remi.


Akafikiria kwa zaidi ya dakika sita bila kupata cha kumuongoza katika sakata lile.


Mara akawaza jambo ambalo hakuwa na hakika nalo, akachukua simu yake na kutafuta namba fulani kisha akapiga.


“nambie kipanga!!” Sauti ya kike ilipokea kwa uchangamfu.


“Acha zako Habiba” Alisema kwa masihala Kobelo.


“Aah kipanga; vipi leo tena mmepigana na shoga angu?” Alihoji huku akicheka.


Yalikuwa ni masihala ya Habiba na Kobelo.


“aah umekariri tu, sikia leo naomba unisaidie jambo fulani hivi” Kobelo alisema.


Habiba aliguna kisha akasema

“Shida gani tena naweza kukusaidia mimi?” Alihoji Habiba kwa mshangao kidogo.


“Hivi inawezekana kupata mawasiliano ya mtu akiwa hayuko kwenye eneo alillopo wakati huo” Alisema Kobelo.


“Sijakwelewa kipanga”


“Ok yani namaanisha unaweza kujua mawasiliano ya simu katika eneo fulani hata kama akiwa ametoka kwenye hilo eneo?” Alifafanua Kobelo.


“eeh mbona rahisi tu” Alijibu Habiba.


“Sasa subiri kidogo nitakutaarifu kwa ujumbe mfupi sasa hivi unisaidie hiyo kazi”


“Sawa”


Kobelo akakata simu na kuanza kutafuta anuani ya ofisi za Remi na alipozipata akazituma kwa Habiba huku akiambatanisha na ujumbe mfupi wa maneno.


“Nitafutie mawasiliano yaliokuwa karibu na eneo hilo au ndani ya eneo hilo mida ya alfajiri”


Kama alijua kupokea jibu lile na kulifanyia kazi ni kazi nyepesi, alikosea sana Sajenti Kobelo.


**+





Remi alikuja kuzinduka akiwa amelala sakafuni na alikuwa na maumivu nyuma ya kisogo chake, maumivu ambayo hakujua yalisababishwa na nini.


Alitulia na kurejesha kumbukumbu zake na ndipo alipokumbuka vizuri kitu cha mwisho kumkumba ilikuwa ni maumivu kama ya kuchomwa sindano nyuma kidogo ya kisogo chake na pia alihisi anadondokea mikononi mwa mtu.


Alinyanyuka chini alipokuwa amelala na kujaribu kuangaza ila hakuona mwanga zaidi ya kidirisha kidogo kilichokuwa juu kabisa ukutani.


Pua zake zilinusa harufu nzito iliokuwa mle chumbani.


Akajaribu kupapasa ukutani labda ataona sehemu ya kuwashia taa, ila hakuona.


Hakujua alipoteza fahamu kwa muda gani hadi wakati huo alipojikuta akiwa amelala sehemu ngeni kabisa.


Akakaa chini na kuegemea ukuta, kisha akatulia na kuacha kichwa kiwaze yanayomsibu.


Wala hakufikiria sana, mlango ukafunguliwa na wakaingia wanaume wawili waliokuwa na kamba mikononi mwao na walipomfikia bila kumuuliza wakamfunga mikono na miguu kisha wakambeba mzegamzega na kwenda nae sehemu nyingine bila kusema kitu.


Kwa makadirio walikuwa wamekata kona za korido kama nne hivi na kwa kudhania alihisi yupo kwenye nyumba ya horofa.


Wakaingia kwenye chumba kilichokuwa na taa kali na wakambwaga chini bila huruma kisha wakatoka na kumwacha akijizoazoa kunyanyuka.


Akanyanyuka!!


Hakuwa peke yake mule ndani.


Kulikuwa kuna mtu amekaa kwenye kiti huku akiwa ameshika kisu kikali akikichezea kwenye vidole vyake.


Mtu yule alikuwa na asili ya watu wa India.


Alikuwa anatabasamu kana kwamba alifurahia uwepo wa Remi pale ndani.


"Kaa kwenye kiti tafadhali" yule mtu alisema.


"Naitwa Sultani" Akijitambulisha bila kusuburi Remi akae kwenye kiti.


Remi alikaa!


"Nambie wataka nini kwangu" Alihoji Remi.


"kwani unajua u wapi hapa?" Alisema Sultani.


"Ni mtoto tu ndo anaweza asijue alipo ila sio mimi. Kwanini mmeniteka?" Alihoji Remi.


Sultani alicheka.



"Ni kweli umetekwa, ila unaweza kuwa huru ukionesha ushirikiano" Alisema Sultani.


"wewe usivyojua alipo hata mimi sijui" Alijibu Remi.


"Remi;tatizo huwa unajiona shujaa sana wewe ila ushujaa ukizidi hugeuka kuwa upumbavu" Alisema Sultani huku akipitisha kisu kwenye mdomo wake.


Remi hakujibu!!


"Sikia,kutwambia alipo mumeo ni safi sana mana si wewe ama mumeo watakaoendelea kuteseka na haya masahibu" Alisema Sultani huku akiwa analamba kisu kwa ulimi wake.


"Nimekwabia vile usivyojua alipo, hata mimi sijui alipo aisee" Remi alizidi kushikilia msimamo wake.

.

Sultani alicheka kinafiki.


"Ok tuachane na mumeo, vipi kuhusu ukurasa wa Bombay?" Alisema Sultani.


Remi alitumbua macho, lilikuwa jambo geni kwake kulisikia.


"Ndo nini hicho?" aliuliza Remi.


"Hizi ni karatasi nne zenye maneno ya kiarabu, na zilipotea miaka kadhaa nyuma na inasadakika zipo hapa nchini" Alisema Sultani.


"Hebu usinichanganye tafadhali, mara mume wangu mara karatasi, sasa mimi nahusika na lipi hapo eti" Alisema Remi huku akionekana dhahiri akiwa amepagawa kwa maneno hayo.


"Yote unahusika nayo, kwa sababu mumeo alionana na Ahmed; Gaidi ambae ndie aliepotea na vitu hivyo" Sultani alisema huku sasa macho yake yakiwa yameanza kubadilika kama mtu aliekula pilipili.


Remi aligwaya!


"Ninyi watu mwanifurahisha sana aisee, yani kila siku maigizo na sijui kabisa uhusika wangu katika hizi show" Alisema Remi.


"Sio tena muda wa showtime bali ni muda wa event kabisa na bado uhusika wako upo" Alisema Sultani na hapo Remi akabutwaika baada ya kusikia showtime.


Hapo alijua kabisa bado yuko mikononi mwa watu wale wale wanaompa tabu kila siku.


"Kwa sasa hatutakuumiza, ila wakati mwingine hatutakuwa na swalia mtume juu ya jambo hili, lakini pia kwa usalama wako, endapo ukiona karatasi yoyote usioielewa basi toa taarifa" Alisema Sultani



"Nitoe taarifa kwa nani" Alihoji Remi.


"Mwanamke mjanja kama wewe nani akwambie pa kutoa taarifa? Ukiziona sisi tutajua umeziona na tutazifuata" Alisema Sultani huku akinyanyuka.


Aya!!


Yakoje mambo haya, mara nitoe taarifa mara watajua, duh! Sasa kwa nini hawakuniacha hadi wajue nimeziona ndo watokee? Alijihoji Remi na alipokuja kutazama alipokuwa sultani hakumuona tena.


"Kapita wapi bwege huyu?" Alijihoji Remi huku akigeuka huku na huko pasi kumuona Sultani.


Akiwa bado na taharuki, mara akaanza kuhisi baridi sana ndani ya chumba kile huku kila dakika ikiongezeka.


Mara ukaanza kutoka na mvuke wenye harufu nzuri sana na Remi alipovuta akaanza kupoteza fahamu taratibu.


**


Saa sita baadae Remi alizinduka kutoka kwenye koma ya kifo na usingizi

.


Akashangaa kuona akiwa amelala kwenye sofa, akaamka haraka na kutulia.

Dakika moja mbele akarudiwa na ufahamu wake na ndipo alipotupia macho kwenye ukuta.


Lahaula!!


Alikuwa yupo ndani kwake na alikuwa akimtizama mumewe kwenye picha.


Alipagawa!!


Alijua kabisa pale sio sehemu sahihi kwake na alihitaji kuondoka pale haraka iwezekanavyo.


Kitu ambacho hakujua ni kuwa ile ilikuwa imepangwa iwe vile.


Alipotaka kufungua mlango ili atoke, alikutana na domo la bastola huku polisi kama sita wakifungua mlango na kuingia ndani harakaharaka na yeye kubaki akiwa kama kapigwa sindano ya ganzi.


Mbele yake alikuwa amesimama ofisa mwenye cheo cha Inspekta na alikuwa na tabasamu lisiloeleweka kama ni chafya alitaka kupiga ama alikuwa anataka kucheka ama kulia.


Usoni alipachika miwani ya macho na kufanya aonekane kama Mr Bean.


"Niite Inspekta Kibe Kengeleo; au wengi hupenda kuniita Kenge na upo chini ya ulinzi kwa tuhuma za mauaji na kuwakimbia polisi, lakini pia unatuhumiwa kutaka kuhujumu uchumi wa nchi na pia kuishi nchini kinyume cha sheria" Kenge alimsomea makosa yake mtuhumiwa wake ambae alikuwa ameganda kama sanamu la posta akiwa hajui ni vipi yametokea hayo yanayomtokea.


Kilichofuata ni kupigwa pingu kisha wakatoka nae na kumpandisha kwenye karandinga na kutimua nae kuelekea kituo cha polisi kwa taratibu zaidi.


Remi alikuwa mikononi mwa polisi.


***


Habiba alimtumia ujumbe mfupi Kobelo akiwa ameambatanisha na namba mbili za simu ambazo pia kila namba aliweka jina la mmiliki wake.


Namba ya kwanza ilioonekana kuwa eneo hilo, mmiliki wake alikuwa ni Davis Minja. Huyu alimtambua kama mwandishi alietekwa.


Na namba ya pili ilikuwa na jina la mmiliki ambae ni Seki Zayd.


Kobelo akatuma tena ujumbe kwa Habiba ya kuwa alihitaji kujua ilipo namba hiyo wakati huo.


Habiba alijibu ujumbe ule kwa kusema namba ile inaonekana ipo posta kwenye jengo la mamlaka ya mapato.


Sajenti Kobelo aliharakisha kutoka na kuelekea nje kulikokuwa na gari lake kisha akaingia na kutia moto kuelekea posta huko.


Kwa kutumia uzoefu wake wa kuishi ndani ya jiji la Dar; alikatisha njia zisizo rasimi na hatimae aliingia posta akiwa ametumia saa moja na nusu tu.


Aliegesha kwenye maegesho ya wafanyakazi wa ofisi zile na kumtumia ujumbe Habiba ambae nae alijibu kwa kumwelekeza kuwa mtu yule bado alikuwa maeneo yale.


Kobelo aliendelea kungojea hadi nyakati za jioni ambapo ofisi zilikuwa zinafungwa.



Akapokea ujumbe wa Habiba ya kuwa mtu yule alikuwa anatoka na amekaribia alipo.


Kweli Kobelo aliona bwana mmoja mrefu wastani akiwa ameshika vitabu akifungua mlango wa gari jeupe.


Kobelo alijaribu kumpigia.


Bwana yule alipokea na Kobelo akakata.


Alipata hakika ya mtu wake anaemfuatilia.


Akaunga msafara kumfuata bwana yule ambae alikuwa na kitambi cha kuzugia umasikini.



Safari yao ilikuwa ni ya mdogomdogo kwa sababu ya foleni, lakini hatimae walifika walikokuwa wanaenda.


Mtu yule aliegesha gari kando ya barabara na kushuka kuelekea kilipo chuo huria Kinondoni.


Kobelo nae alishuka na kuelekea huko.


Bwana yule hakuingia chuoni ila alizunguka na kuwa kama anafuata ofisi za kuchapa na kurudufu karatasi zilizokuwa kule na hatimae safari yake iliishia kwenye gari moja la kifahari.


Bwana yule hakuingia, bali kioo kilishushwa na bwana yule akapokea bahasha fulani na kuanza kurejea kwenye gari lake.


Kobelo nae alifuata.


Alipanda kwenye gari na kutokomea kuelekea njia ya kawe.


Kobelo nae alikuwa nyuma.


Bwana yule aliingia kwenye nyumba moja nzuri iliokuwa na geti zuri la kisasa.


Kobelo hakuwa na namna, alipaki mbele kidogo kisha akangojea giza liingie ili akwee ukuta.



**


Giza lilitamalaki na ni wakati huo ambao Kobelo nae alikuwa amevaa kofia yake pana na kuvaa gloves mikononi huku akiwa ameshika kisu kidogo mkononi mwake.



Akatumia ukuta wa nyumba ya pili kupata msaada wa kuingia ndani ya nyumba ile.


Na hatimae alidondoka kistadi pembeni kidogo ya kichaka cha maua.


Na alipotaka kusimama, alisikia silaha kubwa ikikokiwa nyuma yake.


"Tulia Kanga wewe"


Sauti ya jitu ilikoroma.






Kobelo alibaki akiwa haamini kinachomtokea.


Akagwaya!


Aligwaya sababu hakujua mtu alienyuma yake alitumia kasi ya aina gani hadi kumfikia wakati yeye alijiridhisha kabisa na usalama wa eneo lile.


"nyoosha mikono juu" Aliamriwa na sauti kavu nyuma yake!


Alinyoosha.


Mtu yule pengine hakujua hila za Kobelo kunyayua mikono juu.


Mtu yule akaanza kumpapasa Kobelo ili kumpokonya silaha yoyote aliokuwa nayo.


Kobelo alijua kabisa mtu yule mkono alioshika silaha utakuwa hauna umakini wowote wa kufanya shambulizi na pia mwili wake hautakuwa na mhimili pindi tu akiwa ameinama kuendelea na ukaguzi.


Kweli hesabu zikatiki.


Mtu yule aliinama ili akague miguuni mwa mateka wake.


Likawa kosa.


Alishangaa akipaishwa juu na kisigino safi kilichompata kwenye kidevu na kumfanya ainuke juu na kuiacha silaha yake ikisambaa chini huku yeye akiishia kushika kinywa chake kilichogongana na meno.


Kabla hajakaa sawa, alishangaa akipigwa mateke mawili kwa mpigo yaliojaa vyema kifuani kwake na kumfanya atoe mguno mithili ya malaya aliebambiwa na njemba mbili.


Mtekaji akagwaya ila akajipanga na kumsubiri Kobelo.


Kobelo nae alihitaji kumaliza mchezo mapema.


Akafanya papara bila hesabu.


Kosa!!


Kobelo alijiachia kwa mapigo safi, ila alikutana na hewa kisha akapigwa ngumi safi iliojaa pembeni kidogo ya moyo.


Alihisi anataka kutapika na kutema nyongo kwa wakati mmoja.

Akajigeuza ili amkabili adui yake ambae wakati huo alikuwa amenesa kumzunguka.


Napo akakutana na teke lilikosa uzito wa kutosha na kumyumbisha kidogo.

Mtekaji akaona ushindi u karibu.

Nae akatia mbwembwe kwa kuchezesha miguu kama mcheza dansi za asili ya mdundiko.


Kobelo alimsoma.


Mvamizi akaachia teke safi kwa kutanua msamba hewani, ila Kobelo alitanua msamba wa chini na kuachia ngumi maridadi ilioenda kuzipasua korodani za mtekaji na kumwacha mtekaji akiruka juu kama mtoto alieng'atwa na siafu kalioni huku mikono akiwa ameifumbata kumziba mkojolea uke ambae alikuwa hana mawasiliano tena na korodani zake.


Mtekaji alilia kama kabwela aliedhulumiwa kiwanja katikati ya stendi ya mabasi.


Kobelo hakutaka kuchelewesha akamdaka shingo mithili ya Simba na windo lake kisha akatumia nguvu kidogo kuivunja na kumwacha mtekaji akijibwaga chini kama teja aliekosa unga.


Hakuwa na uhai.


Kobelo alitumia vidole vya miguu yake kutembea kuelekea kwenye nyumba ile ambayo ilikuwa kimya.


Uani aliona gari alilokuwa analifuatilia tangu posta.


Akasukuma mlango na kuingia ndani kwa tahadhari kubwa.


Ila aligundua mle ndani hakukuwa na mtu.


Aliamua kukagua hapa na pale ili kuona lolote linaloweza kumsaidia, aliambualia patupu.


Alikata tamaa na ile nyumba ambayo aligundua ilikuwa na mlango wa dharura na ambao alihisi ulitumika kumtoa bwana kitambi ndani ya ile nyumba.


Akapiga hatua ili atoke.


Simu ikaita!!


Ilikuwa ni simu ya mezani.


Akaifuata na kupokea!


"Ukimalizana nae njoo Temba hotel kuna maagizo yako" Iliongea sauti ya upande wa pili kisha kukatwa simu.


Ndio ni Temba hotel; chumba gani sasa.

Alijiuliza bila kupata majibu.


Akatoka na kumwendea mtakaji wake ambae wakati huo alikuwa mbali na dunia hii.


Alimkagua na kuchukua simu yake ndogo mana kubwa ilikuwa na pini na asingeweza kuifungua.


Akakagua jumbe fupi zilizoingia na hazikufutwa.


Bahati ilikuwa kwake!


Alikutana na ujumbe uliomtaka afike Temba hotel chumba namba tisa na aliposoma tarehe ya ujumbe ule ilikuwa ni siku tano nyuma.


Akaijaribu bahati yake.


Akaelekea huko Temba Hotel.


***


Kabla ya saa tano na nusu usiku; Sajenti Kobelo alikuwa anaegesha gari karibu na Temba hotel. Alishuka na kumlipa mmlinzi ili amwangalizie usalama wa gari lake.


Alipiga hatua za uhakika na kuelekea mapokezi kama wageni wengine.


Alipofika mapokezi alikadibishwa kwa tabasamu mwanana na mwanamke wa makamo aliekuwa mapokezi pale.


"Nahitaji kuelekea chumba namba 9" alisema Kobelo.


Yule dada alistuka kiasi ambacho kilimpa mashaka Kobelo.


"una wenyeji na hicho chumba au umekosea kutaja?" Aliuliza mhudumu.


Kobelo alitabasamu.



"Kuna jamaa angu amehitaji tuonane hapo" Alisema Kobelo.

.

Mhudumu aliguna.



"Kwani hicho chumba kina kitu gani labda" Kobelo alidadisi.


Mhudumu alijichekesha na kujibu...


" Hamna kitu, ila hakina wapangaji zaidi ya mwaka mzima sasa na ndio mana nimeshangaa unapokiulizia"



Eeh!!



Kobelo alibaki akiwa anamtazama yule mhudumu ambae alikuwa anaendelea na shuguli zake baada ya wageni wengine kuwasili kwenye kaunta aliopo.


Kobelo alisubiri hadi wakati ambao mhudumu yule alipoinama kuchukua funguo ndipo na yeye alipochepuka haraka na kuishia kwenye korido iliokuwa na ngazi kuelekea vyumba vya juu.


Alipanda ngazi kwa haraka kidogo na alifika kwenye varanda iliotenganisha vyumba upande wake wa kushoto na kulia.


Alipishana na watu wawili watatu ambao walikuwa wanatokea vyumbani mwao.


Alitupia macho kwenye namba za vyumba bila kuona hicho chumba.


Hadi anamaliza varanda ile,hakuwa ameona chumba hicho.

Mwisho wa varanda ile kulikuwa kuna korido pweke na alipoifuata alikutana na kibao kilichokuwa kimeandikwa maelekezo ya kuonesha ili ufike vyumba vya juu panda ngazi na pia ukiendelea kuifuata korido ile unaelekea kwenye vyumba vya ofisi za meneja wa hotel.


Hata yeye hakujua kwa nini aliamua kutokupanda juu na kujikuta akielekea kule kuliko na ofisi za utawala.


Maajabu!!


Kabla hajafikia ofisi ya utawala alikutana na chumba kilichokuwa kimeandikwa namba 9.


Akatazama kushoto na kulia na kuona hakuna aliekuwa anamuona.


Akajaribu kusukuma.

Kikafunguka.


Akajitosa ndani kwa umakini wa hali ya juu.


Ajabu nyingine!!


Chumba kile kilikuwa kidogo tofauti na matarajio yake na mbele yake kulikuwa kuna mlango uliokuwa na kibao kilichosomeka

"Only members"


Aliguna!!


Mwili ukamsisimka na hamu ya kuelekea huko ikamvaa.


Akausukuma mlango ule.


Akajikuta anazama kwenye korido tulivu iliokuwa inataa za rangi rangi na chini kulikuwa kuna zulia la bei mbaya.


Akaifuata korido ile na kitambo kifupi alikuta mlango mwingine kushoto mwa korido na kuufungua.


E bana ee!!


Alikutana na Dunia nyingine kule na hakuwa amedhania kama katika hotel ile kuna Club kubwa namna ile na watu wanafanya anasa mbele za watu bila kujali.


Alipoingia hakuna mtu ambae alionekana kumjali na alichogundua kwa haraka ni kuwa watu waliokuwa mle ndani wengi walikuwa ni wenye asili ya uarabuni.


Na ngozi nyeusi walikuwa ni wadada ambao wengi walikuwa watupu wakichezea nyeti zao na kushangiliwa na waarabu wale.


Kila mtu alionekana kujali zaidi raha zake kuliko kitu kingine.


Kwa hesabu za haraka haraka Kobelo alihisi waarabu wale hawakuwa pungufu ama zaidi ya thelathini.


Nae akatafuta meza moja na kukaa!


Macho yake yalitembea kila kona ya ukumbi ule na hatimae aliona kile alichokuwa anahisi na kukitafuta.


Alimuona kitambi.


Na aliona kitambi akiongea na njemba moja huku wakimtupia jicho la wizi.


Hatimae wote walinyanyuka na kuelekea upande mwingine wa ukumbi ule na kuingia kwenye mlango uliokuwa umeandikwa "Toilet"


Kobelo nae alifuata!.



Tofauti na alivyodhani kuwa kule ni sehemu ya vyoo; alikutana na korido ambapo alijua ni ya kutokea ndani ya ukumbi ule.


Alipofuata zaidi alikuta inamfikisha kwenye vyumba vya juu kabisa.


Akazidi kuwa makini, mara mbele yake alikutana na njemba iliokuwa inapiga soga na Kitambi..


"Anga hizi zina wenyewe na hupaswai kukatiza" Alifoka yule jamaa na bila kusubiri jibu la Kobelo; akamvamia..


Wakapiga mweleka chini na kila mmoja alipiga ukelele wa uwezo wake.


Bila kupoteza muda walisimama wote kwa pamoja kwa kuruka sarakasi safi.


Wakategana!.


Mchezo wa kuviziana ukafika ukomo.


Kobelo akazuga kutisha.


Njemba ikatishika!!.


Kobelo akaenda juu na kukanyaga ukuta kisha akarudi kwa kasi na kuachia ngumi nzito iliotua sawia kwenye taya ya njemba na kumwacha akilia kama mwanamke alieshikwa makalio bahati mbaya.


Kobelo hakutaka kumpa nafasi.

Akaruka tena na kumpiga double kick zilizomsambaratisha chini jamaa yule aliekuwa na mwili mkubwa nguvu kisoda.


Jamaa akataka kuamka akajikuta akijaa kwenye kabali matata ya Kobelo.


"Sema nyie ni kina nani" Aliuliza Kobelo.


Ikawa kimya!


Na alisikia mpinzani wake akianza kulegea.


Akamwachia!!


Njemba ikaenda chini bila pingamizi.



Akawahi kuitazama na alipigwa na butwaa.


Njemba ilijing'ata ulimi.


"Duh hawa jamaa ni hatari" Alisema Kobelo na aliposimama alikuta hayuko peke yake kwenye korido.


Watu wengi walijaa huku wengine wakiwa na vyupi tu na walikuwa wanatazama sinema ile kutokea kwenye milango ya vyumba vyao.


Mara yakaanza makelele baada ya kuhisi Kobelo ameua mpinzani wake.


Kobelo hakutaka makuu akatokomea.


***


Kobelo alifika chini yalipo mapokezi, lengo lake ni kutaka kuzungumza na mhudumu yule aliempokea, alihisi kuna mengi anayajua.


Alipotokeza tu, alikutana na umati wa watu wakishangaa kule mapokezi huku wengine wakipiga picha na wengine wenye roho nyepesi walikuwa wanalia.


Nae akaenda kutazama!


Shiit nimewahiwa tena!


Alijisemea peke yake baada ya kuona mwanamke yule mzuri akiwa amelala sakafuni na tundu kubwa kichwani.


Alipigwa risasi.


Kobelo alitoka huku roho yake ikimuuma sana na pasi na shaka alijua yeye ndie chanzo cha kuuliwa mwanamke yule.


Akapanda gari yake huku akiwa hana hata nusu ya lolote aliloangua kwenye mkasa ule.


Usiku nao ulikuwa unaelekea kuukaribisha mwanga wa ahsubuhi.


Na alihitaji kupata lepe la usingizi huku ahsubuh akiwa na lengo moja tu.


Kitu ambacho hakujua ni kuwa lengo lake lilizidi kuzua balaa na utata mkubwa.





***


Inspekta Kenge alikuwa katikati ya barabara huku akipiga mluzi usioeleweka masikioni mwake..


Mara akapigiwa honi na gari lililokuwa nyuma yake.


"unaendesha kama unaingia kwako bwana!!" Alilalama konda wa gari lililopiga honi na kumpita Inspekta.


Inspekta Kenge akajinunisha ndani ya gari, kisha akaongeza mwendo na kuanza kulifuata gari lile lililokuwa linapiga ruti za Mbagala hadi kawe.


Mbele kulikuwa kuna foleni!


Gari lilisimama na Kenge nae akasimamisha gari lake kisha akashuka kwa gadhabu na kumfuata dereva,akamshusha na kuanza kumsomea lisala.


"Hivi hujui kuona magari mengine ni ya serikali na waliomo ndio serikali yenyewe,au hujui sheria zinatukataza kukimbiza magari kwenye misongamano ya watu vyombo vingine vya usafiri"


Dereva akataka kujitetea; Kenge akamzuia.


"yani serikali inaongea na wewe unaongea, bado konda wako amenitukana, inamaana hukuona kuwa alieko kwenye gari ni Inspekta?"


Ebanaee!.


Dereva akagwaya!


Mara gari zikaruhusiwa kusogea na zilizposogea gari la Inspekta na lile la abiria havikusogea!


Bado waliendelea kulumbana,honi zilipigwa kwa fujo na magari yaliokuwa nyuma yao.


Inspekta mtata alirudi ndani ya gari lake baada ya kutupiwa chini kiasi cha pesa ya kununulia dawa ya kusafishia viatu vyake.


Inspekta Kenge alikuwa amevurugwa na mambo mengi siku hiyo ikiwemo suala la Remi kuhusika katika mauaji ya ofisa wa jeshi la polisi.


Kilichomchanganya zaidi ni kuona tangu aanze kazi yake amekuwa akipigiwa simu na kupewa maelekezo namna ya kufanya kazi yake.


Tangu lini nikaelekezwa mimi.


Kenge alipiga ngumi kwenye usukani na kusababisha mlio mkali wa honi huku yeye mwenyewe akiruka kwa msituko.


Alikumbuka namna alivyopokea simu na kupewa maelekezo ya kuandika kuhusu mkasa ule na aliahidiwa pesa ya kutakata endapo Remi angekubali kusaini maelezo yale.


Alijikuta anakunja sura kama kaonja kamasi za mtoto.


Alijikuta anamchukia Remi.


Kwa nini!


Kwa sababu Remi alikataa kusaini karatasi zile.


"Siwezi kusaini karatasi ulizoandika wewe na kamwe sitakaa nifanye hivyo, kama mtaniacha nifie humu sawa" Alikumbuka maneno ya Remi.


Remi kutokusaini inamaanisha yeye hatopata mpunga aliohadiwa na mtu anaempigiaga simu.


Alifyonza!


"Kile kipigo nilichompa nikirudi atatia adabu na kusaini mwenyewe" Alijisemea tena.


Kenge alihitaji kufanya jambo moja ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kuaminika kwa wakubwa wake.


Alihitaji kuwa karibu na ukweli zaidi kuliko uongo anaopangiwa kuufanya.


Mawazo yake yalimwambia anahitaji kukutana na mhariri wa gazeti la Chaupeku; gazeti la udaku ambalo kwa ufukunyuku wake alifanikiwa kujua ndilo lililosambaza picha na taarifa kwenye magazeti mengine.


Alihitaji kukutana na mhariri ili ajue yeye alizipataje hizo picha na ni nani alimtumia.


Kwake aliona ni silaha kubwa kujua pande mbili za mchezo ule.


Hatimae alifika kwenye ofisi zile na kushuka kwa madaha huku akirekebisha miwani yake usoni.


Wakati Kenge anafika ni wakati ambao mhariri alikuwa kwenye mazungumzo na Sajenti Kobelo na bado walikuwa katika ubishani.


Kenge aliingia.


Akamkuta Sajenti ambae hakuonekana kujali uwepo wake pale.


"Sajenti nashindwa kuelewa kwa nini hunipigii saluti" Alihoji Inspekta huku akivuta kiti na kukaa.


"Sijavaa military fatigue" Sajenti alijibu kwa mkato.


Kenge akatabasamu kimajivuno.


"Nadhani unapaswa kunipisha, ni wakati wangu bwana mdogo" Alisema Kenge.


Sajenti akasimama na kuanza kuelekea mlangoni.


"Afu hii haipo mikononi mwako na ni kosa kisheria" Alisema Kenge huku akikaa..



Sajenti hakujibu akatoka.


Ndani ya ofisi walibaki mhariri mkuu na Inspekta Kenge.


Kenge alijawa na wivu baada ya kumkuta Sajenti akiwa ndani ya ofisi zile na ile aliitafsiri kama dharau na pia inaweza kumuondolea sifa kwa wakubwa wake endapo Sajenti atafanikiwa kujua ukweli kabla yake.


Akajikuta anataka kuhakikisha kama kweli Sajenti alikuwa pale ni kuhusu sakata lile.


Akauliza swali la kijinga tu.


"Huyu bwana mdogo alikuwa hapa kwa sababu gani eti"


"kazi yangu hainiruhusu kusema shida za wageni wetu kwa watu wengine" Alijibu mhariri ambae alikuwa ni kijana wa makamo tu na haiba ya upole.



Kenge alitabasamu!


"Naitwa Inspekta Kibe Kengeleo au wengi huniita Kenge nina maswali machache ndugu mhariri" Alijitambulisha Kenge..


Mhariri ambae kibao juu ya meza kilimtambulisha kama J Malao alitabasamu bila kutanabaisha dhamira yake ya kutabasamu.


"Jana habari kubwa ilikuwa ni mauaji, na gazeti lako lilikuwa la kwanza kupata picha na habari,naomba kufahamu ilitoka wapi habari ile ama mwandishi gani alieipata na wapi alikoitoa"


J Malao aligabasamu tena.


"Ni kinyume kabisa na maadili ya kazi yangu, na ndio mana unaona habari imeandikwa na mwandishi wetu" Alijibu J Malao.


Kenge aligafirika!


Mara simu ya J ikaita,akaipokea na kisha akasikiliza kidogo na kukata.


"Bwana afande, nadhani tunahitaji kutoka kidogo hadi nyumbani kwangu" Alisema J Malao huku akiinuka kwenye kiti.


Kenge bila kufikiri akasimama na kichwani akihisi huko waendako kuna taarifa anazozihitaji.


Kama alidhani kuna taarifa zinapatikana bure alikosea sana.


Kwa kuwa J Malao hakuwa na usafiri, basi iliwalazimu watumie gari la Inspekta Kenge.



Kenge hakutaka kujishugulisha na kujua alipoelekea Sajenti Kobelo baada ya kumkuta ofisini kwa mhariri.


Makazi ya J Malao yalikuwa ni mbezi mwisho.


Baada ya foleni ya hapa na pale hatimae gari la Kenge liliingia kwenye makazi ya J Malao na kwenda kupaki pembeni kidogo ya mlango wa kuingilia ndani kwa J.


Walishuka huku wakisema mawili matatu bila kugusia lililowapeleka pale.


Waliingia ndani na J alimkaribisha Kenge.


Nyumba haikuwa na samani za bei kubwa wala haikuonekana kuwa na hadhi kubwa licha ya kupangiliwa vyema muoenekano wake wa ndani.


"Chochote ambacho ungependa kutumia tafadhali" Alisema J.


Kenge alitikisa kichwa kukataa kisha akasema.


" Nadhani ni wakati sasa wa kupeana habari kuhusu swali langu"


J alitabasamu, na hilo lilimfanya Kenge ajue ni moja ya tabia za J Malao mhariri yule wa gazeti la Chaupeku.


"Sina hakika kama maelezo yangu yanaweza kukutosheleza afande" Alisema J


Kenge alikunja sura na kufanya azidi kuonekana kituko kwa sura yake isiokuwa na mpangilio maalumu wa muonekano.


J alielewa!


"Namaanisha maelezo sina bali nina kitu ambacho nahisi kinaweza kukusaidia kufika unakokutaka" Alisema J.


"Ok unaweza kunionesha tafadhali, nipo nyuma ya muda" Alisema Kenge.


"Nisubiri kwa dakika mbili tafadhali" Alisema J huku akinyanyuka na kuelekea chumbani kwake.


Kenge alingojea sebuleni.


Ilikuwa ni dakika mbili; zikaongezeka na kuwa dakika kumi na hatime nusu saa; J hakutokea.


Kenge aliona kama ni dharau anafanyiwa.


Akaanza kuita!


Aliita midomo mitatu bila kupokea majibu na kwa kuwa alikuwa na asili ya kuwehuka kwa muda, basi hakutaka kudadisi, akanyanyuka na kumfuata huko huko chumbani.


Akasukuma mlango.


Dimbwi la damu!!


Kenge akaruka juu kwa woga na badala ya kuruka kurudi alikotoka; yeye aliruka kuvuka mwili wa J Malao na kusogea kitandani.


Eeh!!


Alibwata kwa mshangao!


Mlango ulifungwa na alipotupia macho alikutana na pande la mtu likiwa na bastola mkononi yenye kiwambo cha kuzuia sauti.


E bwana eeh!


Kenge alidata; chini kunamaiti na mlangoni kasimama mtu mwenye bastola na sio mtu tu bali ni jitu lenye sura isio na masihara hata chembe.






Kenge alibaki akimtizama yule bwana ambae alikuwa anachezesha shingo yake ambayo ilikuwa inatoa mlio kama mvunjiko wa kijiti kikavu.


Kenge alitazama vyema bastola ya jitu lile ikiwa imeenea vyema kwenye mikono yake. Kenge akapiga hesabu ni jinsi gani ataweza kuvuka maiti iliomiguuni mwake na kumfanyia shambulizi bwana yule ambae hakujua wepesi wake.


Kenge akajionya!


Akatabasamu kinyonge, hakuwa na namna.

Alitegemea jitu lile lipokee tabasamu lake kirafiki ila ndio kwanza alikutana na macho makali yaliokuwa mbali na mzaha.


"Fanya kile unachoelekezwa, tofauti na hapo unajitakia matatizo tu" Lilionya jitu lile.


Kenge akatikisa kichwa kukubaliana nae na hapo hakutaka kukaa mule, akavuka maiti ya J na kutaka kulipita jitu lile.


Kosa!


Kenge alijikuta akirudishwa nyuma kwa nguvu baada ya kupigwa kofi usoni lililoubganisha midomo na uso kiujumla.


Kenge alitoa mguno kama mbwa koko.


Kenge akagadhibika!


Kenge hajawahi kupenda dharau na akichukia huwa haoni ukubwa wa mtu ama uwezo wa mtu; Kenge aliona Katdharauliwa na jitu lile.


Akaachia ngumi nzito alioamini inaujazo wa kulitetemesha jitu lile lililokuwa limejaa kimazoezi.


Ngumi yake iliishia shingoni mwake na tofauti na matarajio yake, aliona jitu lile likichezesha tu shingo yake na kuweka bastola pembeni.


Ebanaee!!


Kenge alinywea gafla huku akijitahidi kujichekesha ili kutengeneza urafiki bandia.


Cheko lake halikusaidia!


Kenge alishikwa ukosi wa shati yake kisha akabebwa na kunyanyuliw juu kama karatasi na kutupwa kitandani ambapo alidunda mara moja na kuangukia chini.


Kenge alilia kama mbweha!


Kenge akataka kujizoa chini, ila hakufanikiwa alishikwa shati lake usawa wa mgongo kisha akanyanyuliwa tena na kutupwa kwenye kabati la nguo na kwenda nalo chini huku akisikia mvunjiko wa vioo vya kabati lile nae akitoa mguno kama mtoto anaeugulia maumivu ya bakora.


Jitu liliunguruma kwa gadhabu huku likimtizama anavyojinyanyua chini bila mafanikio.


Kenge alijitahidi kunyayuka na hatimae alifanikiwa na kukaa kitako.


Alilishuhudia jitu lile likienda kuokota bastola yake chini na kisha likamnyooshea huku uso ukiwa mbali na masihara.


Kenge aligwaya!


Jitu lile likaondoa kitunza usalama huku likianza kukenua meno kifurahia kifuatacho. Kenge hakuwa na namna zaidi ya kungojea hukumu, nguvu zake hazikuwa kitu mbele ya baunsa yule.


Mara likatokea tukio ambalo Kenge haelewi hadi leo hii lilitokeaje ila alikuja kushangaa jitu lile likijibwaga chini na kuacha bastola yake ikisambaratika chini huku ikitoa milio ya risasi bila mpangilio.

Na ndani hawakuwa wawili tena bali walikuwa ni watatu na watatu alivyoingia ndio ilimshangaza Kenge.


Alikuwa ni Sajenti Kobelo ambae alikuwa nje ya chumba kile akifuatilia kwa makini sauti za humo ndani.

Sajenti alikuwa nyuma ya msafara wa J Malao na Inspekta Kenge; na pia alifanikiwa kusogea hadi karibu na mlango na yote yaliotokea mle ndani aliyanasa vyema kabisa na sasa alikuwa ameingilia mpango wa jitu ambalo lilitaka kutoa uhai wa Inspekta kama lilivyotoa uhai wa mhariri J Malao.


Jitu lilishangaa kikumbo lilichopigwa na mtu mwenye mwili mdogo kuliko wake.


Hata!


Halijawahi kuangushwa na mwili mdogo, likajinyayua na kusimama kisha likaunguruma kwa gadhabu na kwenda kumvaa Kobelo.


Likaambulia patupu! Kobelo alikuwa mwepesi kubaini hila zake, akaepa na kusimama pembeni kisha akaruka mtindo safi wa kuambatanisha miguu yake na kulisukumia dhoruba ile lile baunsa ambapo alilipiga mbavuni.


Baunsa likaenda chini tena ila safari hii lilimwangukia Kenge na kuwa juu yake.

Kenge akaguna kwa maumivu na uzito wa baunsa lile ambalo wakati huo lilikuwa linajitikisa ili kujiinua.


Kenge akaona linamwelemea, akatumia mbinu ya kitoto kabisa, akalitekenya.

Baunsa likasimama kwa gadhabu ya kutekenywa likaachia kwenzi mujarabu ilioenda kutua utosini mwa Kenge na kumzubaisha kwa sekunde kadhaa.


Baunsa halikuwa na shida na Kenge; likajiinua tena kwa jaziba na kumwendea kwa pupa Kobelo.


Kobelo alielewa anapambana na jitu lenye nguvu, yeye alitumia akili tu ili awe bingwa wa pambano lile.


Akaruka hadi juu ya kitanda kisha akafanya kunesa kidogo na kwenda juu kisha akakunja goti na kushuka kulikabili baunsa lile.


Mbinu ilitiki.


Goti likatua kichwani mwa baunsa na kumsambaratisha chini kama kiroba cha mavi ya kuku, likabweka kama taahira.


Bahati mbaya bado ilikuwa kwa Kenge.


Baunsa alidondoka karibu na alipokuwa Kenge ambae alikuwa bado amezubaa na kwenzi ya baunsa.


Baunsa hakutaka kupigwa peke yake nae akamchapa kibao Kenge wote wakiwa chini; Kenge akarejewa na fahamu ila akakabiliana na maumivu ya shavu lake, akaachama ili upepo umwingie kinywani kumpunguzia maumivu.


Baunsa akaachana na Kenge akamvaa tena Kobelo; safari hii Kobelo hakupiga hesabu zake vyema akajikuta akijaa mikononi mwa baunsa kisha akapigwa kichwa matata pajini mwa uso wake na kuona nyota za rangi ya nyeusi.

Baunsa halikumwachia, likamnyanyua na kumtupia ukutani na kumwacha Kobelo akigugumia kwa maumivu ya dhoruba ile.


Baunsa akamfuata pale chini.


Kosa!


Kobelo kwa utalamu wa hali ya juu akaserereka kutoka alipo na kumvaa baunsa miguu mwake kisha akajiweka pembeni na kumwacha baunsa akienda chini kwa kupiga magoti na Kobelo akawa kama anainuka chini na kuacha mkono mmoja chini kisha akaachia mateke mawili kwa mpigo wa tofauti ya sekunde moja kila teke moja lilipotua shingoni mwa baunsa. Baunsa hakuwa na namna alienda tena chini kama zigo la karanga mbichi.


Bahati mbaya kwa Kenge; Baunsa akamwangukia kwenye mguu uliokuwa umejeruhiwa na vioo vya kabati..


Kenge akapiga ukunga kama bikira.


Hakuna aliemjali na Baunsa akataka kuinuka ila alichelewa alijikuta akijaa kwenye kabali ya miguu ya Kobelo ambae alimpiga kabali ya kumrukia huku amekunja miguu na alipotua alitua na shingo ya Baunsa na akapiga soti ya kubinuka, miguu ilibinuka na shingo la ulisikika mlio mmoja tu wa kuvunjika kwa kitu kikavu.


Baunsa alitikisika mara moja na kutulia.


Habari yake iliisha.


Kobelo akamfuata Kenge ambae alikuwa bado ameshika mguu kwa maumivu.


"Pole afande!!" Alisema Kobelo.


"Lakini sikukuita uje kunisaidia ujue" Alijitutumua Kenge kwa maumivu.


"Hata mimi najua, vipi umeumia" Aliuliza Kobelo.


"aah! Afande haumiagi ujue, afu ungechelewa kidogo ningemtoa nyongo huyu baunsa uchwara" Kenge alijitapa.


Kobelo alitabasamu tu na kutazama pembeni ambapo aliona mwili wa J ukiwa umelelala katikati ya dimbwi la damu.


Akaachana na Kenge ambae alikuwa anajitutumua kibwege.

Akaugeuza na kufanya kitendo cha haraka sana ambacho Kenge hakuona.


Alikwapua simu janja mfukoni mwa J na kuifutika mfukoni mwake na kuendelea kuipekuwa maiti taratibu.


"Wewe bwana mdogo acha kazi isiokuhusu, niache nimpekue mwenyewe, kesi hii ipo kwangu na sijui unaingilia kwa masilahi ya nani" Kenge alifoka.


Kobelo alijiinua taratibu bila kusema neno na kuanza kuondoka mle ndani.


"wee! tulia hapo hapo unamwachaje mkubwa wako akiwa kama hivi, ndivyo ulivyofunzwa chuoni?" Alifoka Kenge.


Kobelo alicheka tena na kumgeukia Kenge.


"Afande si useme unaogopa hilo jabali lililolala hapo? Usijali halitaamka fanya taritibu askari wengine waje hapa afande" Alisema Kobelo huku akilinyooshea kidole baunsa liliokuwa limelala bila uhai.


"Mh nani aogope, mimi au" Kenge Aliuliza kibwege tu.


Kobelo alitabasamu na kufungua mlango wa chumba na kutoka huku akiamini kabisa Kenge atadanganya watu ya kuwa yeye ndie alieliuwa lile baunsa.


Akapepea kuendelea na hamsini zake na huku nyuma Kenge akapiga simu kituoni kuomba msaada wa maaskari zaidi katika eneo lile.




***

Akiwa njiani; Sajenti Kobelo aliamua kupita kwenye vibanda vya kutengeneza simu, na alipofika aliomba wamtolee mfumo wa kudai neno la siri kwenye kioo kabla hujaendelea kufanya mengine kwenye simu.


Alilipa na kuahidiwa dakika chache kila kitu kitakuwa sawa.


Haikupita hata dakika ishirini, tayari fundi alimkabidhi simu janja aliopora mfukoni mwa marehemu J Malao.


Akaondoka huku akiwa na lengo la kuelekea kituoni kwake kuripoti mchana ule kama zamu yake ilivyohitaji kwa siku hiyo.


Njiani mawazo lukuki yalikuwa yanampitia hasa alipokumbuka kauli ya baunsa kwenda kwa Kenge.

Aliirejea "Fanya yanayokuhusu"


Aliguna!


Inamaana Kenge kuna kitu anajua kuhusu sakata hili sasa vije tena aonekane kushupalia suala hili, na kama baunsa aliamua kumuonya tu ili ujumbe umfikie kwa nini sasa alitaka kumlipua?


Yalikuwa ni maswali bila majibu na kulikuwa hakuna wa kumjibu zaidi ya yeye mwenyewe kulitafuta jibu.


Kenge kuna kitu anajua bwana" Kobelo alijisemea peke yake.


Kobelo aliingia kwenye maegesho ya utawala na kupaki gari lake kisha akashuka na kuelekea kituoni.



"Sajenti; kuna ujumbe wako hapa" Aliseme WP Mengi ambae alikuwa anatoa huduma mapokezi.


Kobelo alisogea karibu yake.


"Unahitajika kwa OCD tafadhali" Alisema WP Mengi.



"Nashukuru" Alisema Kobelo na kupiga hatua kuelekea mlango wa ofisi za mkuu wa kituo kile kidogo.


Alisukuma mlango na kuingia ndani baada ya kuruhusiwa kuingia.

Ndani alikuatana na Mzee wa makamo ambae umri wake ulikuwa bado unaruhusu kuendelea kufanya kazi kwa miaka kadhaa badae.



"Sajenti; unaweza kunambia ni kitu gani kimekuweka bize siku mbili hizi" alisema OCD huku akiwa amefumbata mikono pamoja na kuegemea juu ya meza iliokuwa karibu yake.



"Afande nipo tu nashuguli zangu za kila siku hasa baada ya kutoka kazini" Kobelo alijibu.

.

Mzee alitabasamu.


"Umri unanienda ila bado sijafikia kudanganywa namna hiyo bwana mdogo" OCD alisema huku macho yake yakiwa usoni mwa Kobelo.


Kobelo alitizama pembeni kwa aibu ya kugundulika.


"Umefikia wapi na kesi unayofuatilia?" OCD alihoji.


Kobelo alishituka licha ya kutoonesha mshituko wake hadharani.


"Najua umejipa kesi ambayo hutakiwi kuifuatilia na ipo mikononi mwa askari mwingine, huko ni kukosa nidhamu na pia ni viashiria vya rushwa kwa sababu hadi sasa umesababisha mauaji ya mhariri J Malao" Alieleza mzee.


Ohoo!!


Ilikuwa ni ngumu kumeza; Kobelo alitumbua macho mithili ya jogoo aliekosa kitoweo. Amesababisha vipi mauaji wakati hajui hata namna alivyokufa huyo mtu na ni nani mhusika kati ya Kenge na yule baunsa.


Ebenaee!


Kobelo aligwaya kwa muda na alijua msala umemwangukia jumla jumla.


"Ni kweli ila sijahusika na mauaji yake afande" Alijitetea Kobelo.


"Hata kama hujahusika na vipi unahusika katika kesi isiokuhusu? Au hujui huko ni kuharibu upelelezi? Na kwanini waenda kinyume na maadili ya kazi yako?" OCD aling'aka.


Kobelo alipiga kimya.


OCD alibinua droo na kutoa bahasha na kumkabidhi Kobelo.


"Unasimamishwa kazi kwa muda usiojulikana hadi uchunguzi juu yako utakapokamilika na wakati wote huu usijaribu kufanya jambo lolote la kijinga, hatutakuwa na huruma na wewe tena zaidi tutakusekweka ndani" Aliunguruma Mzee huku akiwa amemtolea jicho Kobelo.


Kobelo alinywea gafla na kushindwa kuamini, hakupata kauli japo ya kujitetea na hatimae alibeba barua ile na kusaluti kisha akatoka nje akiwa mnyonge kupitiliza.


Kobelo alitupwa nje ya kazi kwa muda usiojulikana.



***


Upande mwingine alikuwepo Kenge akiwa amefungwa bandeji karibu uso mzima na kubakiza sehemu ndogo tu ya uso wake.


Licha ya kupachikwa bandeji hizo ila bado alionekana uso umemvimba na pia majeraha mengine yalikuwa yamejitokeza kwenye mikono yake..


Vioo vya kabati vilimuumiza sana ila uso uliumizwa na kofi alilopigwa na baunsa.


Licha ya kuwa na bandeji usoni bado miwani yake haikumtoka usoni ila wakati huu aliivaa juu ya bandeji na kufunika macho kwa juu juu tu.


Alikuwa ameshika kalamu na karatasi, ambazo alikuwa anazisoma kwa kuzinyayua juu mana kutazama mezani asingeweza kwa kuwa bandeji ilifungwa kuanzia shingoni.


Alizungusha shingo yake na kumtazama afande mwenye cheo cha koplo aliekuwa amesimama peke kando yake ndani ya ofisi ile.



"Nenda uniletee yule mwanamke" Aliagiza kibabe.


Koplo alitoka kutekeleza amri na dakika chache badae alirudi akiwa ameongozana na Remi ambae kimuonekano alionekana kudhoofu sana.




Kenge alipomuona alinyanyuka kwa hasira ila alirudi gafla kwenye kiti huku akigugumia kwa maumivu, alijisahau ya kuwa mbavu zake na mguu mmoja navyo vilikuwa vimefungwa kwa bandeji kuzungushia pande zote baada ya kuonekana mbavu zilipata athari kidogo wakati wa makabiliano.


Ingelikuwa ni mtu mwingine basi wakati ule angekuwa nyumbani ama hospitali kama alivyoshauriwa na matabibu, ila sio Kenge ambae bado alisisitiziwa kupewa pesa endapo angefanikiwa kumsainisha karatasi zenye maelezo ya kukiri kuua na kuhusika kwa sakata lile msichana Remi.


Angelala vipi wakati ameahidiwa donge nono!



Hata!!


Lazima Remi asaini.


Kwa hasira alimsukumia karatasi na kumuamuru asaini.


Remi akazichukua na kuzisoma kisha akacheka.


"Hata kama ningekuwa nimeua kweli, bado nisingekubali kusaini maelezo ya mtu mwingine; Polisi ni sehemu ya kupata haki vije tena ionekane mwataka kukandamiza haki ya mtu asiehusika."

Remi akanyamaza kidogo na kuendelea.


"Sikia nikwambie wewe askari mabandeji, nifungeni mtakavyo ila sisaini, nipigeni muwezavyo ila sisaini." Akanyamaza tena na kumtazama Kenge.


"Afu aliekufanya hivyo, angeongeza kidogo hakika hata nguo ningemvulia, mbona kakupiga kidogo afande" Alimalizia kwa tabasamu.


Kenge huwa hapendi dharau, ila afanye nini sasa wakati anamaumivu kila sehemu, kuinuka tu ni tabu vipi kurusha mkono.


Kenge alijikuta akivimba tu bila kumfanya lolote mtuhumiwa wake.


"Afu ulisema unaitwa Kenge; wewe kweli ni askari Kenge; yani unashindwa kutafuta ukweli unakuja na maelezo feki na kwanini nipo humu muda wote bila kupewa karatasi niandike mwenyewe? Askari Kenge" Remi aliongea kwa uchungu na maneno yake yakazidi kumuumiza Inspekta Kenge..


Kenge chozi likamtoka.


Kwanini?.



Kwa sababu alilia hana uwezo wa kumwadabisha Remi na alishaonywa na wakubwa zake kuhusu kuruhusu mtu mwingine kumwadhibu mtuhumiwa aliemikononi mwake hadi viongozi wajiridhishe na uhitaji huo, lakini pia alilia kuona Remi katia ngumu kusaini ili yeye apate pesa na kukabidhi kesi mahakamani.


Ilitia uchungu hakika.


"Wewe mwanamke nikipona utalipa maneno yako yote ya leo fisi wewe" Alijitutumua Kenge..


"Ukiona askari anaependa kutukana watuhumiwa, basi huyo kichwa chake kinawalakini. Mimi ni mtuhumiwa tu wala sio muuaji na nipo kwenye mikono salama hivi sasa, sasa kwanini mnataka nionekane nipo jehanamu" Remi alisema kwa uchungu.


"Najua uonaongea hayo kwa kuwa waniona nipo hivi afu..." Kenge hakumalizia kauli yake, akaingia mtu mwingine ndani ya ofisi zile.


Kenge alishituka kuona mtu mwenye cheo kikubwa na anaefanya kazi makao makuu akiingia mle ofisini kwake.


Kenge akapaparika kutoka saluti ila kajikuta hawezi na kuishia kupiga mweleka huku akitoa mguno wa maumivu.


Ofisa alieingia akatabasamu kwa tukio lile kisha kwa madaha alikaa kwenye kiti alichokuwa amekalia Kenge.


"Inspekta Kibe nadhani unahitaji kupumzika lau siku mbili hivi, nitaongea na mkubwa wako akuache upumzike na hongera kwa kuipenda kazi yako" Ofisa alisema.


Kenge akajichekesha huku akifanya juhudi za kusimama na kisha kutoka mle ndani baada ya kupewa ishara atoke.


Alikuwa ni Naibu Kamishina P. Kagoshima.


"Najua hupendi kuwa humu Remi; ila hakuna namna ni lazima uwepo humu kwa usalama wako" Alisema Kagoshima.


Remi hakumjibu.


"Nimekuja hapa kukusalimia na pia kuweka mambo fulani sawa" Kagoshima alisema tena.


Remi kimywa.


"Uwezo wa kujisaidia unao, ila hutaki tu Remi"


"Vipi unataka nijisaidie kwa kukiri kuuwa? Au najisaidia vipi sasa ikiwa nipo selo?" Remi alisema..


Kagoshima alitabasamu.


"Remi sio kukiri, ila ombi langu tu linaweza kukutoa humu" Kagoshima alisema.


"Lionee haya vazi tukufu ulilovaa, mbona walidhalilisha namna hiyo? Unawezaje Ofisa mkubwa kutega kwa kutumia matatizo yangu?" Alijitutumua Remi.


Kagoshima alikunja uso.


"U jeuri sana, ila jeuri yako si lolote, kumbuka upo mikononi mwa dola na unatuhumiwa kuua, mumeo anatuhumiwa ugaidi, vipi kuhusu mwanao Pius?" Kagoshima alitupa karata makini sana.


Remi alistuka kukumbushwa mwanae ambae alikuwa shule wakati huo na hajui maendeleo yake. Ni vipi kama ataendelea kushikiliwa na mwanae afunge shule nani atampokea ama nani atampa pesa aende kwa ndugu zake Zanzibar alikozaliwa baba yake?


Ebana eeh!!


Ubaridi ulimtambaa mwili mzima. Alimtizama Kagoshima kwa huruma na Kagoshima akainua mabega juu bila kusema neno.


Ilimaanisha maamuzi yapo kwa Remi mwenyewe,abaki selo mwanae ahangaike ama akubali kuwa mpango wa kando kwa Kagoshima ili ajue namna ya kumweka sawa mwanae.


Utata!!..


***


---MOGADISHU---



ilikuwa ni siku ya pili tangu Haji aanze kufuatilia nyendo za Imamu Shafi'I. Na kutoka msikiti wa Masjid nuur; kuna kitu Haji alibaini.


Kila inapokuwa alfajiri huwa kuna gari mbili zinafika kwa wakati mmoja na gari moja humshusha Imamu na gari la pili humshusha mtu alievaa mavazi ya kike na kujitanda juu hadi chini.


Mwanzo alidhani anaweza kuwa ni mke wa Imamu ila siku ya pili alihisi kitu kikubwa zaidi.

Mtu yule hakuwa akielekea mlango wa kuingilia upande wa wanawake ila aliingia mlango wanaposwali wanaume na kutokea hapo hapo wakati wa kutoka.



Haji nae ni muumini wa dhehebu la suni; akaingia siku ya pili yake.


Ajabu hakumuona yule mwanamke na pia hakuona kama kuna pahali unaweza kupita na kuelekea upande wa pili ambako wanaswali wanawake ni kama kulikuwa kuna ukuta ambao haukuruhusu pande zile kukutana endapo mtu angetaka kuingia huko baada ya ibada.


Lakini pia hakuona tena mtu alievaa nguo zile za kike.


Aah!


Sasa aliemuona anaingia yupo upande gani na kama hajavaa mavazi hayo amekaa wapi!


Haji aliendelea na utaratibu alfajiri ile huku macho yake akiyazungusha kama kinyonga na kutazama watu wote ambao aliamua wawe mbele yake.


Hakuona kabisa alipo mtu yule.


Ila alihisi mtu yule anafanya sala nyuma ya mimbari kulikokuwa kuna radio iliokuwa inatumika kurusha matangazo ya ibada ile ya ahsubuhi.


Akapanga tena kwenda kukaa pale anapokuwaga kila siku na kutazama yanayoendelea kule msikitini.


Siku hiyo aliwahi kutoka kabla ya wengine na kwenda mbali kidogo na eneo lile kisha akachukua kiona mbali na kukaa vyema kusubiri kuona kama mtu yule atatoka tena..


Karibu watu wote walikuwa wameshaondoka msikitini baada ya swala ya ahsubuhi ndipo alipoona tena Imamu anatoka akiwa ameongozana na mwanamke yule na kisha wakazungumza kidogo na kila mmoja kupanda kwenye gari lake na kuondoka.


Haji Makame aliguna.


Sasa kama ni mwanamke kwa nini asisali kunakomhusu? Na kwanini mule ndani hakuonekana wakati wa ibada?



Kuna nini?.



Hakukuwa na wa kumjibu Haji.


Haji alijikuta anaanza kumhusisha Imamu na Shafi'I na kile wanachokitafuta Mogadishu na hapo ndipo alipojikuta anaanza kumchukia Imamu yule.


Kwanini!


Kwa sababu wanatumia vibaya mwamvuli wa dini kufanya mambo yao ya hovyo. Wakati wengine wakipigana kusambaza uislamu Dunia nzima, wao wanautumia kufanya hujuma kwa masilahi yao.


Haji alijiapiza kula nae sahani moja, hawezi kuchafua dini yake ya haki kwa mabaya wanayoyafanya.


Alitoka alipokuwa amejibanza, akapanda gari na kurudi wanakoishi ili kujadili kile alichokiona msikitini kwa Imamu Shafi'I.


***


Majira ya saa nne tayari Haji alikuwa mezani na Komando Zedi wakijadili kazi yao.


"Hapa kwenye mtandao naona wasifu wake ni kuwa ni mwanazuoni wa shahada mbili za uzamivu na pia amehitimu katika chuo cha dini ya kiislamu huko Saudia. Na tofauti na hapo wamemtaja tu kama mwanzilishi wa shule na...." Haji hakumalizia kauli yake; Zedi akadakia.


"Hapo shuleni napo kuna kitu nimeona hizi siku mbili"


Haji alikaa kitako tayari kwa kusikiliza .


"Kuna wanafunzi wengi huletwa na magari kila siku na kufuatwa, ila kuna mwanafunzi mmoja huletwa na gari la kifahari na mbali ya ufahari huo ila pia huletwa akiwa ameongozana na walinzi watatu wakiwa na silaha na hukaa pale hadi wakati wa kuondoka huondoka nae" Alisema Zedi.


Haji alipiga kimya.


"Kuna namna hapa, kwanini ulinzi? Na vipi ulifanikiwa kujua anakoishi?" Alihoji Haji.


"Yah! Nilifuatilia hadi gari lao lilipoingia kwenye mtaa wa Ibiru kando ya ubalozi wa China na kuingia kwenye nyumba kubwa na ya kisasa na bada ya hapo sijapata kuona mtu akitoka wala kuingia ndani ya jumba lile" Alisema Zedi.


Haji alitikisa kichwa.


"Honda yupo sahihi na taarifa zake" Alisema Haji huku akiparaza kwenye kompyuta.


"Inabidi tumtumie Imamu Shafi'I kumfikia Mohamed Farrah Aidid." Alisema Zedi.


"Tunamfikiaje sasa, mana wanaoekana wapo makini sana watu hawa" Aliuliza Haji.


"Wapo makini ila hawakosi kuwa na kosa litakalotufikisha kwao" Alisema Zedi huku akionekana kuzama mawazoni kutafuta ufumbuzi.


"Nadhani nirudi tena kujua zile gari zinazokuja ahsubuhi msikitini zinaelekea wapi na baada ya hapo tutajua cha kufanya kamanda" Alisema Haji.


Zedi alitikisa kichwa kukubaliana nae.


"Kwani mchana haziambatani pamoja?" Alihoji Zedi..


"Hapana,Mchana huonekana Imamu peke yake, labda tujaribu jioni" Alisema Haji huku akijilaza kitandani.


**


Jioni ilifika na Haji kama kawaida alikuwa ni miongoni mwa waumini wa msikiti wa Masjid nuur.


Alikuwa amevaa kanzu yake safi na balagashia safi.


Aliingia akiwa amechelewa dakika chache tu tangu wengine walipoanza ibada.


Kama kawaida alijiweka nyuma ya wengine na kuanza kusujudu kisha akawa anazungusha macho yake kila pande kwa umakini sana na kuna kitu alikiona nyuma ya mgongo wa Imamu Shafi'I ambae alikuwa anaongoza ibada.


Aliona pazia likitikisika na kuna mtu alichungulia kupitia tundu ilikopita waya ya maiki.


Aliona mawazo yake yalikuwa sahihi kuwaza kuwa kuna mtu huwa anakaa nyuma ya mimbari wakati wa Ibada.


Kwanini?


Hakika hakujua sababu za mtu yule kufanya vile.


Ibada iliisha ilifuata hotuba nayo iliisha na waumini waaanza kutoka na kila mmoja kuelekea zake.


Haji alirejea kwenye gari yake na kuanza safari kisha hakufika mbali alisimamisha na kuelekea dukani na kununua vocha kisha akajichelewesha pale kwa kujifanya anakwangua na kuweka.


Punde magari mawili yalipita kwa mwendo wa wastani tu.


Lilikuwa ni gari la Imamu na lile la mwanamke mvaa hijabu.


Akaacha tofauti ya dakika tatu na kuingia ndani ya gari lake na kisha kuendelea na safari yake.


Haikumchukua muda murefu akawa nyuma ya magari yale mawili huku akiacha magari matatu yawe mbele yake ili kutokuwastua walioko gari la mbele ambazo anazifuata.


Waliifuata barabara ya corso Somalia kisha wakakunja na kuelekea kwenye makutano ya mnara wa askari, na hapo ndipo magari yaliokuwa mbele ya gari la Haji yalitawanyika kila gari kuchukua uelekeo wake na wao wakazidi kuelekea ulipo mtaa wa Ibaru.


Mwendo ulikuwa wa taratibu na hapo ndipo Haji alijistukia akaamua kuyapita magari yale na kunyoosha hadi barabara ya kwenda ubalozi wa China kisha akasimama.


Hazikuzidi dakika saba magari yale nayo yakatokea na kuelekea kwenye nyumba za jirani na ubalozi.


Haji nae akajipitisha pale na kuona gari la Imamu likiingia huku lile lingine likiwa limesimama tu bila kuonesha dalili za kuingia.


Gari lile liliokuwa linaendeshwa na mwanamke yule alievaa hijabu likaondoka.


Haji akalifuata.



Safari ilikuwa ndefu kidogo na halikuonekana kufika karibuni.


Na gafla gari lile likakunja kwa kasi na kuelekea mtaa watu masikini, mtaa mpweke wa Kanisaab.


Haji alijua ule ni mtego tu na ili kuukwepa akaendelea kwenda taratibu na alipoufikia mtaa ule aliona majengo yakiwa na muonekano wa ajabu na kulionekana kuishi watu wa hali duni sana.


Kila alipokuwa akisonga, mwili wake ulianza kukataa kumpa ushirikiano.


Akasimamisha gari na kutulia kidogo.


Mara akaona watu waliovaa hovyohovyo wakijitokeza barabarani.


Alipowatizama kwa makini aliona bunduki mikononi mwao na alipotupia macho kwenye majengo marefu aliona watu wakijitokeza na mawe mikononi mwao.


Alijua kaingia cha kike.


Akataka kugeuza mara gari yake ikapatwa na dhoruba ya kunyanyuliwa kidogo na kubwagwa chini.

Ilikuwa imekoswa na bomu la RPG

.


Bahati ikawa kwake, akafanikiwa kuigeuza gari ila mawe yakaanza kushuswa kama mvua na risasi zikaanza kumwandama akakoleza moto wa gari ila mbele yake pia kulikuwa kuna kundi kubwa la watu wenye silaha.


Jasho likamtoka Haji.




***


Haji Makame aliona akizubaa umauti utamkuta, hivyo kwa kujitoa aliamua kuendesha gari katikati ya umati wa watu wale ambao walikuwa tayari kuiwinda roho yake kwa udi na uvumba.


Risasi zilidi kurindima kwa fujo.


Hakujali!


Aliongeza kasi ya gari lake ambalo bado lilikuwa linapatwa na risasi huku akikoswa na mabomu ya hapa na pale.


Hakuna anaependa kifo jama!!


Baada ya wale watu kuwa wameziba njia, walishangaa ujasiri wa mtu wao kuendelea kuendesha bila kuogopa milio ya risasi.


Ilikuwa ni patashika kwenye mitaa ile.


Watu wale waliona wakiendelea kukaa barabarani si ajabu watagongwa na lile gari ambalo licha ya kudhurika pakubwa bado liliweza kuendelea na Safari na sasa ilikuwa inawalenga wao.


Walijikuta wanahama barabara bila kupenda.


Na Haji alipita kwa kasi ya kimbunga huku bado mawe na risasi vikizidi kumuandama.


Bahati ilikuwa kwa Haji na hatimae alifanikiwa kutoka kwenye mitaa ile, ila nyuma alisikia magari yakija kwa kasi.


Hakutaka wajue anakoelekea.

Haraka alishuka ndani ya gari na kutoa bastola yake kisha akalenga upande wa hifadhi ya mafuta na kuachia risasi kisha hakasubiri,akatimua mbio na kuacha gari lake likiteketea kwa moto.


Alitokomea vichochoroni na kurejea kwenye makazi yao.


**


"Pole sana kamanda" Alisema Zedi huku akijitahidi kumsafisha majeraha alioyapata.



"Dah! yule mwanamke ni hatari sana aisee,yani mitaa yote ile wamejaa vibaraka wake" Alisema Haji.


"Na hapo ndipo inabidi tupitie kuufikia ukweli" Alisema zedi huku akiinuka na kuelekea kwenye droo kutoa dawa zaidi.


"Ok tumeshajua tatizo yule mtoto na Imamu wanaishia nyumba moja kifuatacho sasa!" Alisema Haji.


"Nadhani kuna haja ya kuingia ndani ya nyumba ile" Alisema Zedi.


"Inawezekana vipi kuingia wakati inaonekana inalindwa sana" Haji alionesha mashaka yake.


"Itabidi tumpe ugonjwa yule binti" Alisema Zedi kifupi huku akifungua kibegi chake na kutoka na kichupa kidogo na kukitikisa.



"Hiyo nini Komredi," Aliuliza Haji.



"Hiki ni kirusi Maria na tulikitengeneza Pakistani kwa kazi kama hii" Alisema Zedi huku akitoa huyu kichupa kingine chenye ukubwa kama ule ule wa kichupa cha kwanza.



"Hii ni tiba yake" Alisema Zedi.


"kinafanyaje kazi sasa" Aliuliza Haji.


"Hii kitu akiambukizwa, anakuwa na tatizo la kustukastuka kila mara na mwilini hukosa nguvu" Alisema Zedi.


Haji aliguna.


"Usiwe na shaka, hakuna daktari atakaeweza kuponyesha hii kitu zaidi ya hii dawa" Alisema Zedi.



"Ok!! Mpango ukoje sasa" Aliuliza Haji.


"Inabidi tutege barabarani na kisha, tutengeneze ajali bandia ili kuwavuta wale walinzi na baada ya hapo tutajua cha kufanya mana inatakiwa ivutwe hewa yake ili iweze kufanya kazi" Alisema Zedi.


Haji alitikisa kichwa kwa kukubaliana na mpango huo.


Mara ujumbe wa kengele ya tahadhari ulilia kutokea kwenye kompyuta iliounganishwa na Honda kwa mawasiliano ya dharura.


Haji aliruka kwa kasi na kuifikia huku akimsikia Zedi akiguna kwa fadhaa.



"He's in trouble" Alisema Haji huku akiwa ameshindwa kuelewa afanye nini ili kuondoa hali iliomkumba gafla.


Zedi alibaki akizunguka asijue la kufanya.


"Imekuwa haraka sana aisee" Alilalama Zedi.


Haji aliishia kushusha pumzi tu.


****


Honda alikuwa amebebwa kwenye gari akiwa chini ya ulinzi mkali wa wapiganaji wa AIAI.


Kwa mtazamo tu alijua kutakuwa kuna tatizo limejitokeza.


Akaamua kuwa na subira huku mawazo lukuki yakipita kichwani mwake.


Woga nao haukuwa mbali.


Safari yao ilikuwa ni ya kimya kimya hadi waliporejea tena kwenye lile jumba kubwa lililokuwa Sadan.


Aliamriwa kushushwa na kuingizwa ndani ya nyumba ile kisha wakamfungia kwenye chumba chenye giza.


Honda alishindwa kuelewa ni kitu gani kilikuwa kinaendelea.


Akiwa bado anawaza hili na lile mara mlango ulifunguliwa na alirejeshwa tena sebuleni na mara hii alikutana na wapiganaji wengine tofauti na waliokuwa wamemleta pale.


Hawa walikuwa ni wapiganaji ambao kwa mtazamo tu alijua inaweza kuwa ni makomando waliofuzu hatua zote kwa jinsi walivyokuwa wanaonekana.


Walikuwa sita jumla yao.


Bila maelezo walimuomba aongozane nao kuelekea nje ambako walipanda gari lingine na kuelekea katikati ya mji.

.


Walipofika Old Mogadishu walisimamisha gari na kumfunga kitambaa usoni na kisha safari ikaendelea hadi walipoingia ndani ya geti la nyumba ambayo hakufahamu ukubwa wake.



Mawazoni mwake alijua labda walistukia nyendo zake wakati anaenda kutoa taarifa ya kuhusu njama za mauaji ya Rais wa Kenya ambayo yalivurugwa dakika za mwisho.


Alijua hawezi kupona kwa kuwa msaliti huwa haponi Zaidi ya kuchinjwa.


Mwili ulimzizima.


Alihofia kwa kuwa suala lile tayari ilikuwa limeshaleta mzozo baina yao, na tayari kikosi chao cha upepelezi kilikuwa kimeshaingia mjini kujua kilitokea nini hadi jaribio lao lilishindwa dakika za mwishoni.


Honda aligwaya ila alijipa ujasiri bandia.


Aliketishwa kwenye kiti kisha akavuliwa kitambaa usoni na hakuwa peke yake pale alipokalishwa.


Mbele yake kulikuwa kuna kijana mmoja mwenye asili ya watu wa Saudia na mzee ambae alikuwa na asili ya kisomali.



Mzee yule alimtambua.


Na ndie alikuwa lengo la operesheni yao.


Huyu ndie alikuwa FLAMINGO kwa lugha yao ya kazi ile.


Alikuwa ni Mohamed Farrah Aidid kiongozi wa kikundi cha Al-Islamiya.


Alitetemeka ndani ya mwili wake bila kuonekana nje.


Wapiganaji waliomleta waliopewa ishara fulani na ndani ya dakika moja alishangaa akiwa amepigwa pingu mikononi na miguuni kwa kasi ya ajabu.


Wapiganaji wale walikuwa si mchezo.



Kijana yule wa kisaudia alitoa picha mbili.


Moja akamuonesha Honda.



Honda alitamani kuona akiota na akiamka aambiwe ni masihara tu yale.


Ila haikuwezekana.


Alikuwa amepewa picha ya Haji Makame.


Picha ile iliambatanishwa na kipande cha gazeti, kilichokuwa na picha tatu, picha yake akitambuliwa kama Ahmed Twalib na picha nyingine ikiwa ni ya Zedi akitambulishwa kama ni Aahmed Boka Ghailan na nyingine ikiwa ni ya Haji ambae haikuwa na maelezo mengi zaidi ya kumhusisha na kutoroka kwa Ahmed gerezani.



"Ahmed; mtu huyu yupo hapa Mogadishu na kama walivyondika wamarekani ndivyo yupo hapa kukutafuta" Alisema Mohamed Farrah.


Honda alitikisa kichwa kukataa.


"Huyu jamaa simfahamu kabisa" Alijitetea Honda.


Mohamed alicheka kisha akampa ishara tena yule kijana wa kisaudia na kijana yule akatoa picha nyingine mbili na kumpa Honda.


Honda alizidi kuchanganyikiwa zaidi.


Picha moja ilikuwa ni ya kwake akiwa na mavazi ya kijeshi na picha nyingine ilikuwa ni ya Haji akiwa na mavazi ya kipolisi huku cheo chake kikijionesha mabegani.



"Hizi ni taarifa kutoka kwenu Tanzania; na mara ya mwisho ulikuwa kazini mwaka juzi ila sisi Ahmed tunaemtafuta alitoweka tangu mwaka 1998 baada ya shambulio la ubalozi wa marekani jijini Nairobi." Alisema tena Mohamed Farrah.


Ebana ee!


Kitumbua kimeingia mchanga mapema.



"Ila umekuwa ukitumika kutuhujumu, na hata mauaji ya Osama inasadikika ulitengenezwa tena na ulifanikiwa kumhujumu Osama hadi mauti yake" Aliendelea Kuongea Mohamed Farrah Aidid.



Kitu kimoja alichogundua Honda ni kuwa watu wale licha ya kuzipata taarifa zake ila hawakuwa wakimjua Ahmed halisi na hilo likampa afueni kidogo japo hakujua hatima yake.

.


Honda alikana kuzijua picha zile na akasingizia ya kuwa labda zimechongeshwa tu ila si yeye.


Watu wote waliangua kicheko cha dhihaka mule ndani.


"Ok! Mengine tutaongea badae, ila kwa sasa tunahitaji jambo moja tu" Mohamed Farrah alisema na kuweka kituo na kumtazama Honda.



Mlinzi mmoja akaweka kitabu kikubwa chenye ukubwa kama msahafu kwenye meza karibu na Honda.


Honda akaoneshwa ishara ya kukifunua, nae akafunua.


Alikutana na maandishi ya kiarabu.


Lugha ile aliilewa!..


Kwa haraka alijua kile ni kitabu cha wosia kilichokuwa na mambo mengi ikiwemo Fatwa'a nyingi kuhusu maonyo Osama kwa wamarekani na namna ya kupambana na wabaguzi wa nchi za kiarabu.


Kifunikwa kitabu na kuondolewa.


"Kitabu hiki kimeondolewa kurasa sita za katikati na ndizo kurasa muhimu katika kitabu hiki, na inasemekana ulihusika katika kuzinyofoa kurasa zile" Alisema Mohamed Farrah.


Ebana eeh lilikuwa ni jambo jipya kwa Honda.


Hakujua kabisa kitabu kile na kurasa hizo zinazoongelewa.


Akabaki njia panda na mateso yalinukia.





Haji na Zedi hawakulala, mana hawakujua ni kitu gani kitamkuta mwenzao huko aliko.


Wakati wao wakimuwazia vile, tayari Honda alikuwa ameiingizwa kwenye chumba cha mateso huku akiwa amevuliwa nguo zote.


Yule kijana wa Kisaudia aliona ile pete ikiwa kwenye uume wa Honda na alipoishika akashindwa kuelewa ni kitu gani kile.


Pete ile ilikuwa imetengenezwa maalumu kwa ajili ya kushikwa na Honda peke yake na kama ikishikwa na mtu tofauti basi sehemu ilipounganishwa hutoa taarifa ya hatari.


Kijana yule akaitazama kwa makini ila akaona ni pete za kawaida tu ambazo huvaliwa na watu wenye mikuyenge mikubwa mikubwa.


Hakuitilia shaka zaidi na akaitupa chini.


Likaletwa dumu la mafuta ya taa na kumwagwa mwilini mwa Honda kisha wakamuuliza zilipo zile karatasi za kile kitabu.


Akashindwa kusema.


Na kitu alichogundua ni kuwa zile karatasi zilikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa wale watu kuliko hata uhusika wake katika kuwapepeleza.



Alikaa kimya.


Mafuta yalipomwagwa mwilini yakasalia kidogo kwenye dumu na yakamiminwa chini na kusambaa kisha jamaa mmoja alikaa pembeni na kiberiti.


Leo tutakuchoma moto Ahmed." Alisema yule kijana.



***


Mapambazuko yaliwakuta Haji na Zedi wakiwa wameshajadiliana vya kutosha kuhusu namna ya kufanya ili waweze kusambaza kirusi Maria.


Walijiandaa na kutoka nje ya makazi yao na kuelekea kutega njia ambayo waliamini gari lililombeba binti yule litakuwa linapita.


Kabla ya saa mbili kamili, gari moja la bei mbaya liliwapita njiani, na wao walilifuata kwa nyuma na walipofika makutano ya mnara wa kijeshi, wakafanya hila za kutaka kulipita gari lile likiwa katika mzunguko wa mwanajeshi asiefahamika.


Wakaparazana na kukosa mwelekeo na kwenda kuingia kwenye bustani ya mnara ule.


Walinzi wawili walishuka kwa gadhabu na kuliendea gari la Zed huku wakitukana.


Zedi alishuka!


Kwa makusudi aliongea lugha tofauti na kiingereza huku wale jamaa nao wakiongea lugha tofautitofauti, mara kingereza,mara kisomali ili mradi wapunguze jaziba zao.


Lengo la kuongea Kiswahili ni kutaka mlinzi wa tatu nae ashuke.


Na kweli alishuka, na Haji nae akashuka.


Haji alikifungua kichupa kile na kukiziba mdomo kwa kidole chake kisha akakifumbata mkononi.


Ajabu ni kuwa mlinzi wa tatu alieshuka alikuwa anaongea kiswahili safi kabisa.


Jamaa yule anaezungumza kiswahili aliwatuliza wenzie kisha akaanza kuongea na Zedi na hata Haji alipofika waliendelea kuongea kiswahili.


Walinzi wale ilitakiwa wawahi kutoka pale ili mwanafunzi awahi shule.


Hivyo ilikuwa ni kujitahidi kusawazisha suala lile.


Zedi aligundua wanataka kuondoka, hivyo akaanzishaa tena mgogoro kwa kuonesha yeye ndie amekosewa na wale jamaa.


Zogo likazuka upya!


Haji alikaa makini kwa ule upande ambao aliamini yupo mwanafunzi.


Mwanafuzi nae aliona anacheleweshwa, akashusha vioo vya upande wake.


Kosa!.


Macho makali ya Haji yalikuwa sambamba na na kwa wepesi wa hali ya juu akajifanya nae amaeingiwa na jaziba kwa kurusha mikono hovyo na pale ndipo alipokirusha kichupa kile chenye kirusi Maria.


Mtoto yule alikiona kichupa kile na bila kujua akakichukua na kukinusa kisha akakitupa nje na kuwaita walinzi wake.


Walifanikiwa!



Baada ya kufanikiwa walituliza mashetani yao nao walipanda gari na kuondoka huku wakiwa wametumia dakika saba tu na walijua ndani ya dakika kumi askari wa Mogadishu wangeliwakuta pale.



Waliondoka wakijipongeza huku Haji akitema kidonge alichokuwa amebugia ili kuzuia a athari za kirusi kile wakati alipokuwa amekifungua.



Walirejea kwenye makazi yao na kuanza kupanga mikakati ya namna watakavyoweza kuingilia tiba ya binti yule.


Haji alikaa kwenye kompyuta na kuanza kupika taarifa na wasifu wa mganga bingwa wa magonjwa ya kuambukiza ambae alikuwa anafanya kazi kwenye hospital kubwa pale Mogadishu kama mganga mkuu.


Na hapo walipata mtu mwenye sifa sawa na zile walizozihitaji.


Na waliangukia kwa Dr Azam.


Zedi alichukua vifaa vyake na kukaa kwenye kioo huku Haji akiwa anaendelea kupika taarifa za Dr Azam.


Alibadili maeneo muhimu na hasa mawasiliano,aliweka anuani ya barua pepe na namba za simu za kwao,kisha akaifunga kompyuta na kumgeukia Zedi.



"Aisee! wewe mtu ni hatari yani hutofautiani na sura ya huyu jamaa kabisa."Alisema Haji huku akichukua kamera yake kumpiga picha Zedi ambae alikuwa amefanikiwa kujichongea sura sawa na ya Dr Azam.


"Hii ni raha ya ukomando,kila kitu MI see rahisi kukifanya" Alijigamba Zedi.


"Ila hatuwezi kufanya hii kazi vizuri bila Azam mwenyewe kutoweka mjini" Alisema Haji.



"Upo sahihi, hebu tumtafute mjini na tutoweke nae" Zedi aliafiki.


***


Jioni ya siku ile Zedi na Haji walikuwa na kazi moja tu, nayo ni kuhakikisha wanajua alipo Dr Azam.


Walifanikiwa kujua anapoishi na kwa uzoefu wao wa kuteka watu ambao hawana madhara, walifanikiwa kumchukua na kuondoka nae hadi kwenye makazi yao.



Wakati wao wakimteka Azam; Imamu Shafi'I alikuwa anapokea taarifa kutoka kwa tabibu wake ya kuwa mwanae amepata maambukizi ya ugonjwa wa ajabu hajapata kuona na hajui kama aliwahi kusoma popote kuhusu ugonjwa ule.


Ugonjwa ule ulisababishwa na kirusi ambacho kina shambulia seli nyeupe kwa kasi kubwa sana na kupelekea mwili kukosa nguvu na mgonjwa kuwa anastukastuka kila mara.


Imamu alipagawa!


Kwa haraka alituma sampo ya damu ya binti yake kila kulipokuwa na tabibu wanaefahamiana.


Na hadi giza linaingia alikuwa amepata majibu yenye kufanana na kila tabibu alishindwa kujua ni wapi atapa dawa za kuzuia kirusi kile kisifanye kazi.


Na pia wapo waliomtahadharisha ya kuwa siku chache zijazo binti yule anaweza kukosa uhai.


Hali ilizidi kuwa mbaya kupindukia.


Imamu Shafi'I aliita watu wake wa karibu usiku ule na kuwataka ushauri.


Wengi walishauri walivyoweza ila mmoja alishauri aitwe Dr Azam; mganga mkuu wa hospital ya old Mogadishu.


Haraka haraka haraka wasaidizi wake waliingia mtandaoni kutafuta sifa za Dr yule.


Walijiridhisha na taarifa zake,kisha wakampigia simu.


Walikubaliana kuonana ahsubuhi katika mnara wa kanisa katoliki.


***


Zedi na Haji walipongezana baada ya kuona ujumbe wa barua pepe kisha ukafuata ujumbe wa simu.


Makubaliano yalifanyika na wakajipanga kufanya walichokubaliana.



**


Ahsubuhi kama kawaida Dr Azam wa bandia alitumia gari la Dr Azam wa kweli na kuelekea nalo kule kwenye mnara wa kanisa katoliki kama walivyokubaliana.


Ungelimtazama Zedi; basi ungeamini ndie Dr Azam halisi.


Alipofika pale, alipigiwa honi na gari moja lililokuwa limepaki pembeni ya duka moja la vifaa vya baiskeli.


Akaenda na gari lake ila alishuka kijana mmoja na kumwomba ashuke aache pale gari lake na apande kwenye gari lao.


Dr Azam wa bandia alitii.


Alichukua kibegi chake chenye vifaa tiba na kupanda ile gari.


Safari ilianza.





Dr Azam wa bandia alipofika ndani ya gari na gari likaondolewa na kisha ikaanza safari ya kumzungusha Dr yule.


Dr Azam wa bandia aliwaza ya kuwa zile ni mbinu tu zinazotumika ili asijue wanakoelekea.


Dereva alizungusha gari zaidi ya dakika arobaini na tano na hakuonesha dalili ya kusimamisha gari.


Dr Azam aliamua kuwapunguzia safari,akajilaza na kukoroma.


Dereva na wasaidizi wake bila kujua hila ya Dr; wao walijua kweli Dr kalala hivyo walizunguka kidogo na hatimae waliingia nyumbani kwa Imamu Shafi'I.


Dr aliamshwa na vijana waliompokea.


Akapiga miayo ya uchovu kisha akajivuta na kurekebisha miwani yake na kushuka.


Kama mwewe angani, akazungusha macho yake kwa haraka sana na kufanikiwa kuona walinzi sita wenye bunduki wakiranda huku na huko.


Dr Azam wa bandia aliona mmoja wa walinzi akiwa na mbwa.


Akashanga!


Muislam safi kamwe huwezi ona mbwa akiranda nyumbani kwake hata kwa bahati mbaya hasa nyumba yenye uzio kama ile.


Hapo Dr Azam wa bandia alikubaliana na mawazo ya Haji kuwa Imamu na watu wake walikuwa wanatumia uislamu kama mwamvuli wa kufanya mabaya yao.


Dr alitukana kimoyomoyo.


Alikaribishwa ndani na Imamu Shafi'I na baada ya utambulisho alipelekwa kwenye chumba maalumu alichokuwa amelazwa binti yake.


Dr alijitia kusikitika kwa hali aliomkuta nayo binti yule.


Kila nusu dakika binti alikuwa anastukastuka na mwili ulianza kumpauka huku midomo ikiwa imekauka.



"Naombeni mlete maji ya kunywa" Aliagiza Dr Azam.


Walinzi wakaangaliana kisha Imamu akasema "Tulizuiwa kumpa maji jana Dr"


Dr Azam akamgeukia na kumkata jicho kali.


"Mimi ndie Dr na naomba mlete maji, mnazidi kumdhoofisha kwa kutokumpa maji,msiogope tafadhali" Alisema Dr Azam huku akiwa bize kuweka sawa vifaa tiba vyake.


Maji yaliletwa na Dr akamywesha yule binti.


Binti akapata kauli kwa mara ya kwanza tangu usiku uliopita.


Imamu alitabasamu kwa kitendo kile.


"Mgemuua huyu mtoto aisee" Alilalama Dr Azam.


Dr Azam alichukua damu kidogo na kuihifadhi kwenye kifaa maalumu kisha akaweka kwenye mkoba wake na kisha akaendelea kumkagua hapa na pale binti yule.



"Naiomba hewa tafadhali" Dr alisema huku akiinuka kuwatazama walinzi waliokuwa mle ndani.


Imamu aliwapa ishara nao wakatoka.


Alibaki Imamu Shafi'I ndani ya chumba kile.


Dr Azam alikuwa na sababu za kumbakiza Imamu mule ndani.


"Hii inaweza kuwa imesababishwa na nini Dr" Alihoji Imamu huku akikaa kwenye kiti kilichokuwa pembeni ya kitanda.


"Kwa haraka naona ni ugonjwa wa mlipuko kutoka kwa wanyama au basi alikula chakula chenye kuukataa mwili wake" Alijibu Dr.


"Chakula kinapimwa kabla ya kuliwa Dr; labda mnyama na sijui ni mnyama gani" Alisema Imamu Shafi'I.



"Huwezi jua katika mazingira yake ya kujidai" Alijibu Dr Azam.


Imamu alikunja uso kisha akasema

"Inabidi nimbadilishie walinzi, wamekuwa wazembe sana siku hizi".


Dr hakujibu.


Mara simu iliita na Imamu akampiga jicho Dr kwa wizi na kuipokea.


Kama imamu alidhani Dr hajamuona alikosea sana.


Macho ya Zedi Wimba p.a.k Dr Azam yalimnasa vyema kabisa na hilo ndilo lililomfanya awatoe walinzi mle ndani na kumbakiza Imamu peke yake.



Kabla ya kuongea Imamu alimuuliza Dr Azam


"Hivi kwenu ni wapi, waonekana si msomali eti"


"Kwetu ni South Africa" Alijibu Dr


Imamu aliongea kwa kipakistani(punjaban).


Kama alijua komando aliepembeni yake ni zwazwa basi alikosea sana.


Pakistani walikaa zaidi ya mwaka mmoja kabla ya kuanza kazi ile, hivyo moja ya lugha waliofundishwa ni hiyo Punja inayozungumzwa sana na watu wa mashariki mwa Pakistani.


Dr alielewa kilichozungumzwa, ila akaendelea na huduma yake ya msingi kwa yule mtoto wa kike.


Imamu alimaliza kuongea na simu kisha akaendelea kumtazama Dr Azam.


Dr Azam nae hakutaka kuendelea kuweka muda mrefu pale ndani hivyo,akachukua vidonge viwili na kumpa yule mtoto.


"Inabidi nikafanyie utafiti hii damu kisha nitakuja na majibu kuhusu aina ya dawa inayoweza kutumika kumtibu ila hizo dawa nilizompa zitamsaidia hadi keshokutwa nitakaporejea" Alisema Dr Azam.


Imamu alionekana kuwa na shaka.


Kwa nini?


Kwa sababu alihitaji mwanae apone haraka na pia alikuwa na sababu yake kubwa zaidi ambayo hakutaka kabisa Dr Azam afike pale siku hiyo.


Siku hiyo ambayo Dr aliahidi kurejea na majibu ni siku ambayo alitarajia kupokea ugeni nyeti sana na kwa kawaida akipokea wageni wa aina hiyo kamwe mgeni mwingine huwa had huruhusiwi kuingia ndani ya jumba lile.



Jitahidi iwe hata kesho Dr" Alisihi Imamu Shafi'i.


Dr alizidi kusisitiza huku akiweka sababu zake zenye mashiko kabisa.


Mwisho Imamu kwa kujali afya ya mwanae aliamua kukubali ombi la Dr.


Dr Azam alitolewa nje na kusindikizwa hadi ndani ya gari lililomleta kisha wakaanza tena kumzungusha kwenye vichochoro vya Mogadishu.


Saa moja badae walimfikisha kwenye lile duka la vifaa vya baiskeli na kumwacha apande kwenye gari lake.


Dr alielekea kwenye kituo chake cha kazi huku akiamini kabisa kuna watu maalumu waliwekwa kumfuatilia.

.

Dr alitabasamu baada ya kuwa amemtega Imamu kuhusu kwenda kwake siku ya tatu yake na alifanya vile baada ya kumsikia akiongea kuhusu kupokea wageni muhimu.


Dr Azam wa bandia alitaka kuwaona wageni wale.


Hakika hesabu zao zilikuwa sahihi kwa wakati huo.



***


Honda alikuwa hatamanila kwa kipigo alichopata na mwili wake ulikuwa umebabuka baada ya kuwashwa na moto.


Bahati nzuri ni kuwa moto hakumfikia kichwani na pia hakumpa madhara makubwa kwenye ngozi yake.


Ila vidonda vilipatikana.

Alikuwa amelipuliwa kwa dakika moja tu.


Alikuwa amefungwa na kuachwa aning'nie kwenye kamba huku chini kukiwa kumewekwa chupa zilizopondwa pondwa na hivyo kumfanya muda mwingi akunje miguu na kila alipoishusha aliishia kuchomwa na chupa.



Mwili vidonda na miguu ni vidonda vya kukatwa na chupa huku damu ikiwa inamwagika.



Pembeni yake alisimama jamaa ambae alikuwa ameshika bakora ya mpira.


Hakika alipitia mateso.


Yule kijana wa kisaudia alikuwa amesimama huku akingoja apewe majibu ya zilipo hizo karatasi ambazo zilikuwa zimepewa jina la Ukurasa wa Bombay.


Honda hakuwa na jibu la kuwapa.


****


Siku ya tatu iliwadia na Dr Azam alienda pale pale alipoambiwa angojee.


Alifika na kulikuta gari lile lile lililokuwa limemfuata siku iliopita.


Utaratibu ukawa ule ule na akapandishwa kwenye gari na kuzungushwa.


Nae hakubadilika alilala baada ya dakika thelathini kisha aliamshwa walipowasili kwenye jumba la Imamu.


Kama kawaida, macho yake makali yakanasa sura za walinzi sita aliowakuta siku ile pamoja na mbwa na pia aligundua kuna walinzi wengine zaidi waliokuwa wapo pale ndani.


Siku hii Dr Azam alikaguliwa na vifaa vya kisasa ili kama anasilaha aweze kuisalimisha.


"Dr; samahani kwa kinachotokea ila lazima usalama uzingatiwe" Imamu alimuomba radhi Dr Azam kisha akamwongoza wakaelekea kwenye chumba cha tiba.



"Dawa zako zimemsaidia sana mwanangu, anacheza hivi sasa na ameanza kurejewa na nguvu zake" Alisema Imamu Shafi'I.


Dr alitabasamu tu.


Kitu kingine alichogundua Dr Azam; ni kuwa nyumba ile hakukuwa na mwanamke hata mmoja tofauti na yule mtoto wa kike wa Imamu Shafi'I.


Dr Azam alitoa kichupa chenye tiba na kumchoma mtoto kisha akachukua dawa nyingine tena na kumchoma mtoto na hazikupita dakika sita mtoto alipitiwa na usingizi.



"Itabidi nisubiri hadi azinduke ndipo niondoke, hii ni kwa usalama wa afya yake" Alisema Dr Azam.


Imamu akang'aka!


Hakutaka Dr aendelee kupoteza muda pale.


****


Nb;bado hujachelewa ofa! Riwaya hii itakufanya usome nyingine zaidi kwa kuilipia Tsh 1000/= yani elfu moja utapata riwaya mbili, zile ambazo hujawahi kusoma kutoka kwangu.



"Nadhani hatuna haja ya kubishana bwana Shafi'I; Mimi naenda zangu ila tatizo likitokea tafadhali usinishirikishe mana nitakuwa bize na kuwahudumia wagonjwa wengine." Dr Azam alitahadharisha huku akiandaa mizigo yake kwa ajili ya kuondoka.


Imamu akaona asipotumia busara basi atamkosa Dr na pia atamkosa mwanae.


"Usichukulie hasira bwana mdogo,ni mambo fulani tu yananipelekesha,usijali kaa humu usitoke hadi nitakapokuambia" Alisema Imamu huku akianza kutoka ndani ya chumba kile.


Dr Azam alirusha ngumi kwa majivuno ya kufanikiwa hila zake.


Haikuwa muda murefu sana tangu alipokaa ndani ya chumba kile mara alisikia harakati huko sebuleni na alijaribu kutazama kwa makini kama kutakuwa kuna kamera zilizofungwa mule ila hakuziona.


Alipojaribu kuangalia kama ataweza kuona nje, mara kwa juu aliona uwazi wa venti na aliona panamfaa kutizama.


Akasukuma kitanda akicholalia mgonjwa kisha akakipanda na kutazama nje kupitia vitundu vile.


Alifanikiwa kuona magari mawili ya kifahari yakiwa yamepaki huku kukiwa kuna walinzi wengi wenye silaha za kutisha.


Na katika gari mojawapo alishuka mzee mmoja aliekuwa amevaa kofia ya pama huku akichechemea kwa mbali na aliposhuka kulionekana kuongezeka ulinzi wa hali ya juu sana.


Dr Azam wa bandia aliamua kushuka na kurejesha kitanda.


Na punde mtoto aliamka.


Alimpa huduma zinazostahili kisha akakaa kwenye kiti na walibaki wanatazamana tu.



Dakika chache badae Imamu aliingia na kufurahi na mwanae, huku akijitahidi kumtania hapa na pale



"Dr unahisi mwanangu anaweza kupona sasa" Alisema Imamu..


"Yah! Kwa hapo alipofikia nadhani anastahili kupona kwa sababu nimepata dawa ya ugonjwa wake na baada ya wiki moja atakuwa sawa kiafya." Alisema Dr



"Sijui nitakulipa nini Dr ila naomba nikupe hii" Alisema Imamu huku akitoa hundi ya dola elfu hamsini na kumpa Dr; kisha akamwambia..


"Nitakuwa nakuhitaji kila mara ili unisaidie mambo fulani kuhusu afya ya watu wangu wa karibu,umenifurahisha sana kwa hili ulilofanya" Alisema Imamu.


"Sawa na ahsante sana" Alijibu Dr Azam huku akikusanya vitu vyake na waliongozana kutoka nje.


.

Utaratibu ulikuwa ni ule ule kama ni kawaida kurudishwa kwa kuzungushwa mitaani na kisha kuachwa kwenye duka la vifaa vya baiskeli.


Dr Azam alichukua gari lake na kuondoka kuelekea kazini kwake.



****


Usiku ulikuwa ni wakati wa kujadili kile walichokiona kwa siku nzima.


"Kwa mtazamo wangu naona huyu mzee atakuwa ndie Flamingo mwenyewe" Alisema Haji huku akiigeuza picha waliokuwa wamechora baada ya maelezo ya Zedi Wimba ambae alikuwa anatumia jina la Dr Azam.


"Kama ndie basi tutakuwa na kazi ya kufanya kuanzia kesho" Alisema Haji.


"Basi kesho ukiamka tu elekea pale mana inaonekana ni kikao cha siku na kadhaa hivi" Alishauri Zedi.



"Sawa" Alikubali Haji.


Makubaliano yao yalizua jambo jingine ambalo halikuwa kwenye mipango na hapo ndipo mchezo ulipokolea na Zedi kurudi kwenye hekaheka ndani ya mji wa Mogadishu.


Aliigeuza hekaheka ile kuwa ni operesheni Mogadishu.


Ahsubuhi ilimkuta Haji akiwa ameshafika karibu na jumba la Imamu Shafi'I na alikuwa makini ili nyendo zake zisistukiwe.


Kitu kimoja ambacho hakujua ni kuwa siku ile ilikuwa ni tofauti na siku zingine zote ambazo amekuwa akizitumia kupiga jicho la mwewe.


Ugeni uliokuwa pale kwa Imamu siku ile ulikuwa ni zaidi ya ugeni wa Rais wa Marekani katika moja ya nchi za bara la Africa.


Ulinzi ulikuwa ndani na nje katika hali ya kutisha, hivyo hata wakati yeye anaingia pale tayari macho zaidi ya kumi yalikuwa sambamba nae.


Jua lilipoanza kuwa kubwa ndipo Haji alipoona msafara wa gari kama nne hivi zikitoka langoni mwa nyumba ya Imamu Shafi'I.


Zilimpita nae alifuatia kwa nyuma. Gari zile zilikuwa ni za kisasa na kasi sana ila Haji alikuwa na gari ambayo haikuwa na ubora sawa na gari zile.


Msafara ule ulikuwa ni wakasi sana kiasi ambacho gari la Haji halikufua dafu kuunga msafara ule na hatimae zilimpotea machoni.


Alijisonya kwa kushindwa kufuatilia msafara ule na ule ulikuwa ni mwanzo wa kushindwa harakati zao.


Hakika ilisikitisha.


Wakati akiwa bado anazubaa barabarani mara ikatokea gari kwa nyuma na kugonga gari yake kisha ikamsereresha kwa kasi na kila alipojaribu kukwepa alijikuta anashindwa na kubaki akiwa ameshikilia usukani bila kufanya lolote na kisha kwenda kujingonga kwa nguvu kwenye gari lililokuwa mbele yake hivyo kujikuta akiwa amepata ajali mbaya sana iliomsababisha kujingonga kwenye vioo mara kadhaa na kumpasua juu kidogo ya paji lake la uso.


Akiwa bado anahangaika kujinasua ndani ya gari, wakatokea watu wawili wenye silaha na kuuvuta mlango kwa nguvu kisha kumtoa kwa mzegamzega na kumtupia ndani ya gari lao.


Alidondokea kwenye miguu ya watu wengine na alipotaka kuinuka alijikuta akipigwa kisogoni na kitako cha bunduki na taratibu uso wake ukapoteza nuru na kutanda kiza.


Akatulia tuli.


***



Masaa sita badae alikuja kustuka na kujikuta akiwa amefungwa uchi wa mnyama huku shining'inia na miguu yake ikiwa imewekwa kwenye beseni la umeme lenye kupooza maji mithili ya jokofu.


Alihisi miguu imeanza kupooza na ilikuwa inakuja kukamata mwili mzima.


Alipojaribu kutupa macho pembeni, aliona mtu akiwa ametundikwa kama yeye na alikuwa anangozi kama kuku anaeokwa na miguuni kulitandazwa chupa zilizotapakaa damu, damu ambayo alijua imetoka miguuni mwa mtu yule.


Kamba iliomfunga ilikuwa inazunguka kutoka upande mmoja kwenda mwingine na ndipo ilipozunguka na kumgeuzia uso upande alipo Haji.


Haji alitoa macho kama kinyonga.


Alikuwa anatazama uso wa Honda ambae alikuwa amechoka kwa kipigo na pia alikuwa ameiva mwili mzima kwa moto uliompata.


Hakika alitisha kutazama


*****

Haji alijaribu kugunaguna kama ishara ya kuwasiliana na Honda ila Honda akachezesha bega lake kwa tabu na kufanya vile Haji alijua Honda hataki wawasiliane kwa njia yoyote katikati ya chumba cha mateso.



Haji alitulia huku akiwaza namna ya kujinasua katikati ya mateso na kumwokoa Honda ambae alikuwa hoi na ngozi yake ilikuwa inazidi kuharibika.


Kama wangechelewa zaidi basi angeweza kupoteza maisha..

.


Alilia kikomando, alilia bila kutoa machozi na sauti, alilia tumboni kama kobe.


Wakati wao wakiwa chumba cha giza; Zedi yeye alikuwa anahangaika kujua alipo Haji ambae mawasiliano yalikuwa yamepotea tangu jua la saa nne.


Alijaribu kufuatilia njia zote bila kupata hata habari ya kuonekana gari lake.


Wakati alipokaribia kukata tamaa alipata habari kupitia simu maalumu, habari ilitoka makao makuu iliompasha habari za kutekwa kwa Haji na kupelekwa sehemu isiofahamika.

.

Mwili ulizizima; jasho likamtoka; akili ikamzunguka kwa kasi.


****


-----DAR ES LAAM----


Remi alibaki akimtizama Naibu kamishina Kagoshima.


.

Aliwaza kuhusu utu wake na aliwaza kuhusu mtoto wake na aliwaza kuhusu mumuwe.


Akaamua jambo kwa kuliweka kuwa mpango 'a' na akajipanga katika mpango 'ba' ambao aliamini atafanikiwa licha ya kujua inaweza kuwa na madhara upande wake.


"Sawa nimekubali" Alijibu Remi huku akimtizama usoni.


Kagoshima alitabasamu na kumwonesha dole gumba la kulia,kisha akaaga na kuondoka.


Hazikupita dakika arobaini; Remi alifuatwa kwenye selo aliokuwamo na kutolewa hadi kaunta kisha akapewa vitu vyake vyote hadi bastola yake na kuruhusiwa kuondoka.


Alikaribishwa na Dunia, akapumua na kumuomba Mungu amsamehe kwa kosa la kukubali kutumika kimwili ili aokoe mwanae ambae hakujua kinapangwa nini juu yake.



*4: UKWELI*


Sajenti Kobelo baada ya kupewa barua ya kusimamishwa kazi, aliiweka kushoto mwa gari lake bila kusoma kisha akaelekea kwa Habiba ambae alikuwa anafanya kazi katika mtandao wa simu nchini.


Huko alienda na simu akiochukua mfukoni mwa J Malao.


Na baada ya kuifikisha waliingia kuichunguza mawasiliano yake na hapo bado tena namba ya Seki Zayd I ilionekana na ndio iliotuma ujumbe kwa njia ya mtandao kwenda kwa mhariri wa gazeti la Chaupeku.


Namba ya Seki nayo ikachunguzwa na kuona ilipokea ujumbe ule kutoka kwenye namba ya simu ya mtu ambae alisajiliwa kwa jina la Nadia na simu ile ilionekana kuwa ipo kimara.


Kobelo hakutaka kuacha kuifuatilia, akapita kituo cha mafuta na kujaza mafuta kisha akaelekea kimara.


Kwa foleni za hapa na pale hatimae alifika Kimara kisha akampigia simu Habiba.


Akaelekezwa nyumba ambayo simu ile ipo. Ilikuwa ni nyumba ya kawaida tu na ilikuwa na wapangaji kadhaa.


Akaongoza kwenye chumba ambacho alihisi kutakuwa kunapatikana namba ile.


Akagonga na kuingia ndani na kukutana na sura ya binti mrembo akiwa amekaa kwenye sofa moja lililokuwa mule ndani.


Binti yule baada ya kumuona alistuka na kutulia.



Kwanini astuke au ananifahamu? Aljiuliza Kobelo.


Binti alikuwa amejifunga kanga tu na alionekan kutoka kuoga muda huo.


Zilipita dakika kadhaa bila yeyote kuzungumza.


Kobelo alikuwa na sababu zake kufanya vile.


Kwa mtu ambae hakufahamu ukiingia kwake atakukaribisha kisha hatokawia kukutaka utambulisho.


Ndivyo alivyotaka iwe ila haikuwa ndani ya chumba kile.


Ukimya ulitawala na yule binti alikuwa anatizama kwa tahadhari ya hali ya juu.


Kobelo akajiweka kwa hadhari.


Tahadhari yake alikuwa sahihi.


Kwa wepesi wa hali ya juu, yule binti akavua kanga yake na kuirusha kumwendea Kobelo pale alipokuwa amesimama.


Kobelo hakuzubaa nae akahepa na kudondokea kwingine ila alikuwa amechelewa, alijikuta akitandikwa teke zito tumboni na kujihisi anataka kutapika na kabla hajakaa sawa akatandikwa tena ngumi nzito ya taya na kujisikia kama amevunjwa hivi,kizungunzungu kikakamvaa ila hakutaka azembee katika pambano lile na mtoto wa kike kama yule.


Akaruka kidogo na kuegemea ukuta kisha akatulia na kuacha wenge lipite ili akili imkae sawa.


Akatulia.


Ndipo aliona binti akiwa amevaa bikini peke yake na kuacha mwili wote bila kujali.


Chuchu zilisimama na tumbo lilikuwa safi bila michirizi, kitovu kiliita na hipsi hazikudanganya uzuri wa kiumbe kile cha kike.


Ila kwa mapigo yale ni dhahiri hakuwa mwanamke wa kawaida na ndipo Kobelo alipomtazama machoni na kugundua binti yule ndie walipambana nyumbani kwa Sajini Vengu.


Kobelo akatisha kidogo kisha akawa kama anataka kukimbilia mlangoni, binti aliona hawezi kuachwa akataka kupiga hatua, lakini Kobelo alikanyaga ukuta na kujipindua kiubavu na kumpa pigo mujarabu kwenye mbavu na kumsukuma hadi chini ambako alienda kujibwaga kama zigo la nyanya na sokoni.


Binti akajaribu kuinuka akashindwa,akajaribu tena akashindwa.


Mara damu zikamtoka mdomoni ,binti alitoa machozi kama mtoto huku kushindwa kuamini ndo anapotea kirahisi vile.


Heri fadhaa kuliko fedheha; Binti akajitutumua na kusimama kisha akafanya tukio ambalo Kobelo hakujua limefanyikaje na alichokuja kushuhudia ni kuona binti akitua chini huku akiwa hana uhai.


Ajabu hii!!


Kobelo alishuhudia ufundi wa hali ya juu wa kujitoa uhai.


Haraka haraka akaanza kupekua pale ndani, na kwa chini ya sofa alilokuwa amekalia yule binti kulikuwa kuna vipande vya bunduki ya kudungulia masafa marefu aina ya Lapua Magnum.


"Hii ndo ilifanya tukio kule nyumbani kwa Remi" Alijisemea Kobelo.



Akapiga picha silaha ile kisha akaelekea chumbani, huko alikutana na simu ikiita na jina alikuwa ameandikwa Zayd; Kobelo aliona ile ni turufu kwake, akaipokea.


"Njoo nyumbani" kisha simu ikakatwa..



Nyumbani kwa Zayd anakufahamu.


Kobelo akachukua simu yake na kuzitafuta namba za mtu aliekuwa amehifadhi jina kwa "Chief" alipiga.


"Hili suala linaelekea ukingoni Chief"


"Umegundua lolote hadi sasa?" Aliuliza Chief.


"Nipe msaada wa vijana makini wafike hapa kimara baruti kuna mambo waweke sawa kisha nitakuambia nilichokiona hadi sasa" Alisema Kobelo.


Kobelo alikuwa anaongea na mkuu wa kikosi cha operesheni maalumu Kamishina Zenge wa Zenge.


Kamishina Zenge wa Zenge alikuwa amemwambia Remi ya kuwa anasafiri kwenda marekani, kwanini hadi sasa bado yupo Tanzania? Hilo hakuna aliejua kabisa zaidi yake na kijana wake Kobelo.


Kobelo alitoka na kuelekea nyumbani kwa Zaydi na ambako alikuwa amedhibitiwa siku kadhaa nyuma na mtu ambae aliamini ni mlinzi wa pale.


Mara hii alijipanga vyema wakati wa kuingia pale.


Alidandia ukutani na kutazama kwa makini ndani ya ua wa nyumba ya Seki kisha kwa wepesi akatua chini na kusimama haraka na kujitupa upande mwingine..



Alitulia kama dakika moja hivi kisha akasimama na kuliendea dirisha moja na kwa wepesi wa kutisha akalifungua na kujitoma ndani kwa sarakasi matata na kabla hajatulia akabebeshwa konde zito lililompepesua hadi ukutani, nae kwa ujuzi wake akajigeuza na kusimama.


Alikutana na bwana kitambi akiwa anamwendea kwa kasi huku akiwa ameshika kisu.


***


MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog