Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

KABILA LA WALA WATU WALIVYOWATAFUNA WANANGU

   


MTUNZI : ALLY KATALAMBULA




“We ni nani?”

“Naitwa Jamila Mustapha”

“Unapiga simu kutoka wapi shida yako ni nini?”

“Nipo Temeke...bila shaka wewe ni Hussein Mwanda, mwandishi maarufu wa habari za kichunguzi?”

“Ndio”

“Basi nisikilize kwa makini”

“Eeh!”

“Nje ya nyumba yako, karibu na geti kuna pipa la kuhifadhia takataka, chini ya pipa hilo kuna flash-harddisk naomba uchukue flash hiyo na uipachike katika kompyuta na kuifungua halafu fanyia kazi maelekezo yaliyomo humo”

“We ni nani, na nini mantiki ya kunieleza hayo usiku huu wote”

“Nikwambie mara ngapi kuwa naitwa Jamila Mustapha”

“Ok fine, kwanini unanieleza yote hayo?”

“Kwasababu nimeuwa watu saba miongoni mwao yumo mume wangu, natarajia kujiua muda mfupi baada ya kukata simu hii, sina muda wa kujibu maswali yako yote unachotakiwa ni kufanya kama nilivyokueleza”

Yalikuwa ni mazungumzo baina ya Hussein mwandishi maarufu wa riwaya akizungumza na mtu aliyejitambulisha kwa jina la Jamila.

Ilikuwa yapata saa saba usiku, Hussein alikuwa amekamata simu kiganjani huku akikodolea macho kwenye kioo cha simu akiitizama namba ya mpigaji ambaye kwa wakati huo tayari alikuwa amekwisha kata simu.

Maneno ya mwanamke aliyetoka kuwasiliana naye kwa simu usiku huo yalikuwa kigonga kichwa chake, haikua ni mara ya kwanza kupigiwa simu na wasomaji wake mbalimbali kutoka kila kona ya nchi akipokea pongezi na sifa mbalimbali lakini simu ya siku hiyo ilikuwa tofauti.

“Nje ya nyumba yako, karibu na geti kuna pipa la kuhifadhia takataka, chini ya pipa hilo kuna flash-harddisk naomba uchukue flash hiyo na uifungue kisha ufanyie kazi maelekezo yaliyomo humo......nimeuwa watu saba miongoni mwao yumo mume wangu, natarajia kujiua muda mfupi ujao” sauti na maneno ya yule mwanamke yalijirudia akilini mwake.

Hussein Mwanda aliketi kitandani huku akijiuliza kama alitakiwa kufuata maelekezo ya mwanamke aliyempigia simu ama laa! Aliikumbuka tena sauti ya mwanamke yule, kengele ya hatari ikagonga kichwani mwake.

Alichukua simu yake tena na kupiga namba flani kisha akaweka simu sikioni, muda mfupi simu upande wa pili ikapokelewa.

“Kiongozi samahani kwa usumbufu” alisema Hussein, baada ya simu yake kupokelewa na mtu wa upande wa pili.

“Nimepigiwa simu na msomaji usiku huu, kanieleza vitu vya ajabu sana” Hussein alianza kusimulia mkasa wote dhidi ya simu ya msomaji aliyejitambulisha kwa jina la Jamila

“Kwa hiyo umekwisha kwenda kuitizama hiyo flash-harddisk?” mtu wa upande wa pili alimuliza

“Hapana”

“Kwanini?”

“Naogopa kiongozi, mtu mwenyewe anaonekana siyo mwema,kama nikienda nikakutana na bomu?”

“Hauwezi kuwa ni mtego halafu akakupeleka kwenye mtego kipumbavu kama hivyo”

“Kwahiyo?”

“Nenda kaangalie hiyo Flash-Harddisk kisha angalia hicho kilicho ndani yake ni kitu gani halafu kesho asubuhi njoo ofisini na maelezo” mtu wa upande wa pili alisema.

Baada ya kukata simu Hussein akajizoa pale kitandani na kutoka nje, alitoka akiwa na hadhali kubwa, akatembea katika giza hadi getini, ukingoni mwa geti kweli kulikuwa na pipa la kuhifadhia takataka.

Akalisogelea lile pia na kulinyanyua, alihisi ubaridi ukipita kwenye maungo yake baada ya kuona kitu alicho ambiwa. Flash ndogo ilikuwa imepachikwa kwenye kifuko cha nailoni ili isiharibike, aliichukua na kurudi ndani haraka.

Akiwa ni mwenye shauku baada ya kufika ndani akaiwasha kompyuta yake na kuipachika ile flash-harddisk sekunde chache kifaa kile kikafunguka, ndani yake kulikuwa na dokomenti.

Akaifungua.

Baada ya kufungua dokomenti ile, akakutana na maandishi yenye kurasa zipatazo mia mbili, usiku ule ule akaanza kusoma kurasa moja hadi nyingine kila alivyokuwa akimaliza kurasa wa kwanza akajikuta anavutiwa kusoma ukurasa unaofuatia

Ilikuwa ni simulizi ya kusisimua, simulizi ya maisha ya kweli ambayo alipitia mtu katika maisha, simulizi ile iliandikwa hivi:

*******

Jina langu naitwa Jamila Mustapha.

Tangu nikiwa mdogo nilifundishwa kuwa ndugu zangu wa pekee katika dunia walikuwa ni watoto wenzangu ambao nilikuwa nikiishi nao katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Sanganigwa huko Mkoani Kigoma.

Nilifunzwa kuwa na adabu na heshima kwa mtu yoyote bila kujali kama ni mdogo ama mkubwa. Katikatika maisha yangu yote ya utotoni nililelewa katika misingi hiyo

Nikiwa naishi katika kituo hicho tangu utoto wangu hadi nilipopata akili, sikuwahi kumjua mzazi ama ndugu yoyote yule, ndugu zangu wa pekee walikuwa ni watoto wenzangu ndani ya kituo hicho.

Nilishi nikiwa mtoto hadi nakuwa mkubwa na kupata akili, nikiwa na miaka kumi na saba tayari nilikuwa ni binti mwanamwali ambaye nilivutia macho ya kila mwanaume aliyenitizama

Pamoja na hayo lakini nilikuwa ni mtu mwenye matarajio makubwa sana katika maisha, nilikuwa na ndoto ya kuwa msichana msomi, nikiwa na kiu ya kuwa mwalimu, baada ya hapo kuwa na mume mzuri ambaye nitazaa naye watoto wawili tu, mmoja wa kiume mwingine wa kike.

Pamoja na malezi yenye upendo niliyoyapata kutoka kwenye kituo cha watoto yatima sikuwa na sababu ya kutokuwa na matarajio kama haya.

Hata hivyo mambo yote hayo yalikuja kutoweka taratibu na kubaki kuwa ni ndoto ya alinacha, hii ilikuwa ni baada ya kujiingiza katika mahusiano ya kimapenzi na mvulana mmoja ambaye nilimpenda sana. Ambaye alinipa ujauzito na kunitelekeza.

Nakumbuka mwanzo kabisa kujiingiza katika ulimwengu wa mahaba ilikuwa ni kipindi ambacho nipo kidato cha tatu, nilikuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na mvulana mmoja aliyeitwa Sheby alikuwa ni dereva tax.

Nikiwa binti mrembo mwanamwari ambaye sijapata elimu ya uzazi na ujinsia ambaye kwa wakati huo nilikuwa nimezama kwenye penzi tamu la dereva tax, bila kutegemea nilijikuta nikishika mimba.

Ni walezi wangu wa kituo cha kulelewa watoto yatima ndio waliokuwa wa kwanza kubaini kwamba nina ujauzito, kwa mujibu wa sheria na taratibu ilibidi niondolewe kituoni kwa mantiki kwamba nimeshakuwa mtu mzima




Ni walezi wangu wa kituo cha kulelewa watoto yatima ndio waliokuwa wa kwanza kubaini kwamba nina ujauzito, kwa mujibu wa sheria na taratibu ilibidi niondoke kituoni kwa mantiki kwamba nimeshakuwa mtu mzima.

Ulikuwa ni wakati mgumu kwenye maisha yangu, sikuwa na ndugu yoyote katika dunia, kituo cha kulele watoto yatima nilichokulia tangu nikiwa mdogo ndio palikuwa nyumbani kwetu, kufukuzwa pale kituoni ulikuwa ni mtihani mzito maishani.

Mategemeo yangu pekee niliyahamishia kwa Sheby, nilitembea kutokea pale kituoni mkononi nikiwa na begi langu la nguo hadi nyumbani kwa Sheby, hata hivyo kile nilichokitarajia kilikuwa tofauti.

Sheby alinigeuka kama hanijui. Yeye pia Alinifukuza.

Kuanzia siku hiyo nikawa ni mtu wa kutangatanga mtaani, mimi na tumbo langu makazi yangu yakawa ni kwenye vibaraza vya maduka nikijumuika na ombaomba wa mjini ambao wengi wao walikuwa ni wazee vikongwe na walemavu.

Kila giza liingiapo roho yangu itaabani kwa mfadhaiko, zilikuwa ni nyakati zilizo nipa simanzi moyoni, mbu pamoja baridi viliniadhibu kila siku, niliishi maisha hayo bila kujua nini hatma yake.

Kila siku asubuhi nilitembea katika migahawa ya mama ntilie na kufanya kazi ndogondogo, jioni ilipowasili nililipwa ujira wangu mdogo ambao niliutumia kwa kula na kununulia mahitaji yangu machache sana nikisubiri maduka yafungwe ili niweze kuweka ubavu wangu katika vibalaza

Hayo ndio yalikuwa maisha yangu kwa kipindi chote hadi siku nilishikwa na uchungu wa kujifungua mtoto. Kwa msaada wa samaria wema nilikimbizwa katika hosptali ya maweni nikiwa kwenye hali mbaya sana.

Namshukuru Mungu nilijifungua salama mtoto mzuri wa kiume, katika kipindi chote ambacho nipo Wodini moyo wangu ulikuwa katika hofu kubwa namna ya kumlea mwanangu, sikuona mwanga wa maisha yangu, kila nilivyomtizama mtoto wangu roho yangu ilipatwa na uchungu usio kawaida.

Niliona maisha ya malaika huyo namna yatakavyokuwa mabaya, pamoja na ukweli kwamba maisha ya kila mja hupangwa na Mungu lakini bado akili yangu haikuwa tayari kukubali falsafa hiyo.

Kwa mara ya kwanza mawazo ya kumtelekeza mtoto wangu yalipoivaa akili yangu, nikaamini kuwa kitendo cha kumwacha mtoto pale wodini ni jambo zuri kwa kuwa anaweza kupata bahati ya kuchukuliwa na mtu ambaye anauwezo mzuri wa kiamaisha na kumlea kuliko kwenda naye mtaani na kuishi maisha kama ya kunguru.

Jioni moja baada ya kumnyonyesha na kuhakikisha kalala usingizi nilijitoa kwenye kitanda na kuanza matayarisho ya kuondoka, sikutaka kuchukua chochote ili manesi wasije kuhisi baada ya kumnyonyesha na kulala nikatoka kama kwenda chooni.

Sikurudi tena, niliondoka kabisa nje ya hosptali ya maweni na kutimkia mtaani, wakati natemba nikiwa mbali na hospitali ile moyo wangu ulikuwa katika maumivu makali sana, taswira ya mwanangu akiwa amelala kitandani peke yake iliendelea kujitengeneza kwenye akili yangu, machozi yalinibubujika.

Nilitembea hadi stesheni dhamira yangu ilikuwa ni kutoweka kabisa Kigoma ingawa sikujua ni wapi nilitakiwa kukimbilia, nilifahamu kitendo nilichokifanya kingezua gumzo kubwa mjini hivyo kwa kuhofia kukamatwa niliona ni kheri nitimkie mbali kusiko julikana

Bahati nzuri siku hiyo kulikuwa na treni iliyokuwa inaelekea Jijini Dar, nilingia ndani ya treni kwenye mabehewa ya daraja la tatu nikatulia huko.

Muda mfupi badaye treni ilipiga honi na safari ikaanza, niliendelea kujikunyata huku uso ukiwa umenichonyota vibaya mno.

Masaa matatu badaye nilikuwa nimepitiwa na usingizi, nilikuja kustushwa na sauti ya mkagua tiketi, alikuwa amesimama mbele yangu pembeni akiwa na askari polisi kama wawili.

“Leta tiketi yako.” Sauti ya ukali ilinisemesha, nikastuka hata hivyo nikajenga utulivu wa ghafla na nikajifanya kuitafauta katika mifuko ya nguo huku nikiwa na wasiwasi moyoni.

“Nimepoteza tiketi.”

“Umepoteza?...umepoteza vipi?” yule jamaa aliniuliza kwa ukali.

“Hata sijui, nafikiri nitakuwa nimedondosha”

“Unaelekea wapi?”

“Tabora...agh!. Naenda Dar es salama.” Nilibabaika.

“Inaonesha hata huelewi unakokwenda, sasa itabidi ulipe nauli nyingine”

“Kusema ukweli sina kabisa pesa” nilisema kwa sauti ya huruma huku nikiwatizama wale jamaa kwa zamu.

Baada ya jibu hilo kilichofuata ni kukamatwa na wale askari polisi na kupelekwa hadi kwenye behewa la nyuma kabisa ambalo lilikuwa ni maalum kwa kuhifadhia watuhumiwa.

Ndani ya lile behewa sikuwa peke yangu kulikuwa na utitiri wa watuhumiwa tulichanganywa wanaume na wanawake.

Tukawa tunaulizwa maswali mmoja mmoja anayeshindwa kujieleza vizuri anatenganishwa na wenzake, ikafika zamu..




Tukawa tunaulizwa maswali mmoja mmoja anayeshindwa kujieleza vizuri anatenganishwa na wenzake, ikafika zamu yangu, hofu ikasambaa kifuani mwangu, askari polisi akanisogelea na kunikazia macho.

“Jina laako?”

“Latifa Mustapha”

“Unaakotoka ni wapi na unasafiri kwenda wapi?”

“Nataoka Kigoma naenda Dar,”

“Unakwenda kufanya nini Dar es Salama?”

“Kuwasalimia ndugu zangu”

“Ndugu zako wanaishi Dar sehemu gani.” Nilitambua lilikuwa ni swali la mtego, lakini haikuwa tabu kwangu, licha yaa kwamba nilikuwa sijawahi kufika kwenye Jiji hilo lakini nilikuwa nikiyasikia baadhi ya maeneo maarufu yanayapatikana kwenye mji wa Dar es Salam. Nikamjibu bila wasiwasi.

“Wanaishi Kariakoo wengine Kinondoni na baaadhi wanaishi Mbagala”

“Bakia hapa” alisema yule askari na kuhamia kwa mtu mwingine.

Kidogo presha ilishuka, hata hivyo bado sikuwa tayari kuendelea kuwa mikononi mwa polisi, niliamini kabisa hadi kufika siku inayofuatia tukio la kutupa mtoto lingekuwa ni habari kubwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Magazeti, nikaamini kuendelea kuwa mikononi mwa polisi ni kuzidi kuwa karibu na mdomo wa mamba wenye meno makali.

Tuliaandikishwa majina watuhumiwa wote tuliosafiri kinyemela ndani ya treni kisha askari akaanza kutupa maelekezo mengine.

“Watu wote mliokuwa mkisafiri ndani ya treni Kinyamela mtafikishwaa kwenye maeneo yenu mliyokuwa mkielekea mkiwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi, baada ya kufika tutawakabidhi katika vituo vya polisi vya maeneo husika. Mtaendelea kuwa chini ya ulinzi wa polisi hadi hapo mtakapo lipa ralway nauli yake.

Zilikuwa ni taarifa mbaya mno kwa upande wangu,niliamini jambo hilo linanisigeza karibu na mikono ya dola ambao muda si mrefu wataanza kunisaka kila mahali,kamwe sikuwa tayari kukamatwa kwa makosa ya kumtupa mtoto. Pamoja na kulitambua hilo Lakini sikuwa na la kufanya tayari ndio hali halisi ilivyokuwa kuwa, sikuwa na namna ya kuubadili ukweli. Nilikuwa chini ya mikono ya jeshi la polisi.

Tulikaa ndani ya behewa lile dogo kwa masaa mengi mno, usiku ukaingia hatimaye kukakucha, na wakati wotehuo sikuweza kununua hata kipande cha muhogo,nilikuwa sina hata senti mfukoni, nilishinda na njaaa nikalala nayo tena! hadi tunafika Dodoma nilikuwa hoi bin taabani kwa njaa.

“Shika hii”

Sauti ya mvulana mmoja ilinistua nyuma yangu, nilipogeuka na kutupa macho nilimwona kaka mmoja mweusi akinipa mfuko wa rambo ndani yake kukiwa na chips kavu, nilipokea chakula kile nikamshukuru yule mkaka huku nikimwona kama malaika wa ukombozi ailiyeibuka ghafla jangwani nikiwa katika hatuaa ya mwisho kukata roho kwa kiu, kilichofuata ilikuwa ni kushambulia chakula kile hadi tumbo langu likajaa, akanipa maji ya ya chupa ya baridi nikapata ahueni.

“Unaonekana una mawazo mengi sana dada yangu.” Alisema yule mkaka huku akinitizama namna ninavyo kishambulia kwa pupa kile chakula.

“Hapana kaka yangu niko sawa”

“Naitwa Charles Okole ni mwenyeji wa Kigoma, bila shaka jina lako ni Latifa Mustapha?”

“Umejuaje jina langu?”

“Nilisikia wakati ukiitambulisha kwa afande”

“Yeah naitwa Latifa Mustapha”

“Kesi yako mwisho wake ni Dar kama mimi?” yule mvulana aleniuliza akimaanisha kwamba kesi ya kupanda treni bila nauli hatma yake kwa upande wangu itakwenda kumalizika Dar es salama

“Ndio” nilimjibu.

Mazungumzo kati yangu na yule mkaka aliyejitambulisha kwa jina la Charles yalianzia hapo na kuendelea kwa muda mrefu sana, tulizungumza mambo mengi na yule mkaka tukiwa ndani ya treni chini ya ulinzi wa askari polisi.

Kwa muda mfupi niliotumia kufahamiana na yule mtu tulijikuta tukielewana mno, ilikuwa ni mithili ya marafiki wa muda mrefu ambao hawakuwahi kuonana kwa miaka mingi na sasa wamekutana.

Ilikuwa nia kiasi cha masaaa zaidi ya 48 kupita tukiwa ndani ya treni tukiendelea na safari ya kuelekea Dar es Salama, walikuja askari polisi ndani ya behewa tulimohifadhiwa watuhumiwa, safari hii palikuwa na askari wawili wa kike, mkononi mwa wale polisi walikuwa wamekamata Gazeti la Uwazi.

Macho yangu yalipotua katika Gazeti nilihisi tumbo lote likipata joto, picha yangu kubwa ilikuwa imepamaba ukurasa wa mbele wa Gazeti hilo huku kukiwa na maandishi yaliyokolezwa kwa wino mweusi yakisomeka: “MREMBO ATUPA KICHANGA NA KUTOKOMEA KUSIKO JULIKANA.”

Niliogopa mno baada ya kuona maneno hayo katika Gazeti, niliamini mambo yamekwisha haribika, ingawa treni ilikuwa kwenye mwendo mkali nilitamani nijilushe nje kupitia dirishani na kupotelea mbali kuliko kuingia mikononi mwa polisi.

“Ndio huyu afande.” Mara sauti ya askari wa kike ilisema kwa wahaka baaada ya kunitupia jicho na kunilinganisha na picha ya kwenye gazeti.

“Nimekwisha!” nilisema kwa sauti ya kunong’ona uso wangu ukiwa chini.

“We simama” amri nyingine ilitoka.

“Wewe ndio huyu wa kwenye gazeti?” askari mmoja mtu wa makamo alisema huku akiniangalia mimi kwa na kunifananisha na picha ya kwenye Gazeti.

Badala ya kujibu nilijikuta nikitokwa na machozi, wale polisi kwa kuona hivyo hawakutaka mjadala tena na mimi walichofanya ni kunifunga pingu na na kutakiwa kushushwa kituo kinachofuata na kurejeshwa tena Kigoma kujibu mashtaka ya kutelekeza kichanga hospitalini.

Nilishushwa katika kijiji cha Goweko mkoani Tabora, nikapelekwa kwenye kituo kidogo cha polisi cha Goweko ambako nako nilisafirishwa tena hadi Kigoma mjini nikiwa nakabiliwa na kesi ya kujibu ya kutupa mtoto mchanga.



Badala ya kujibu nilijikuta nikitokwa na machozi, wale polisi kwa kuona hivyo hawakutaka mjadala tena na mimi walichofanya ni kunifunga pingu na na kutakiwa kushushwa kituo kinachofuata na kurejeshwa tena Kigoma kujibu mashtaka ya kutelekeza kichanga hospitalini.

Nilishushwa katika kijiji cha Goweko mkoani Tabora, nikapelekwa kwenye kituo kidogo cha polisi cha Goweko ambako nako nilisafirishwa tena hadi Kigoma mjini nikiwa nakabiliwa na kesi ya kujibu ya kutupa mtoto mchanga.

Baada ya kufikishwa Kigoma Mjini, nilipelekwa moja kwa moja hadi kituo kikubwa cha Polisi na kuwekwa selo, katika kipindi chote ambacho nilikuwa selo, nilikuwa nikikejeliwa na kutukanwa na askari polisi hasa wa kike, kwa kitendo nilichokifanya cha kumtelekeza mtoto wangu Hospitalini.

Nililala selo kwa siku tatu, bila kupelekwa mahakamani wala kutoa maelezo yoyote, katika kipindi chote nilichokuwa mule ndani, nilitamani kujua hali ya ‘katoto kangu’ inaendeleaje, lakini niliogopa kuuliza nikihofia kutukanwa.

Nakumbuka Siku ya nne, majira ya saa tatu asubuhi, mlango wa selo ulifunguliwa, nikatakiwa kutoka.

Niliongozwa hadi kwenye ofisi moja ndogo ndani ya kituo kile, nilipopata kuingia ndani ya ofisi ile niliwakuta watu watatu masister wa kanisa Katoriki pamoja na OCD.

Katika wale Masister mmoja alikuwa amembeba mwanangu huku akimpa maziwa ya chupa kwa mapenzi makubwa.

Askari aliyenileta alipiga saluti mbele ya mkubwa wake aliyekuwa ameketi nyuma ya meza kubwa, kisha akatoka nje, nikabaki na wale watu.

“Latifa Mustapha.” Yule Kamanda aliniita huku akinitizama machoni.

“Abee.”

“Kwanini humtaki mwanao?”

Lilikuwa ni swali ambalo ningeweza tu kusema, namtaka ila ugumu wa maisha ndio umenifanya nimkimbie, Lakini nilipofikiria sababu ya ugumu wa maisha, eti ndio iwe chanzo cha kumtupa mwanangu, niliona ni sababu ya kipuuzi mbele ya binadamu yoyote mwenye akili timamu.

Nikakaa kimya.

“We Latifa.” Afande aliita tena.

“Kwanini humtaki mwanao?”

“Sina uwezo wa kumelea.” Hatimaye nilisema kwa fadhaa huku machozi yakinitoka. Nilijisikia vibaya sana kwa kile kilichokuwa kikiendelea.

Nafsi yangu ilikiri kuwa jambo nilikuwa nimefanya lilikuwa ni jambo baya ambalo sikustahili kufanya, pamoja na changamoto za maisha bado sikutakiwa kumtupa mwanangu.

Hivyo, yale maswali ya yule afande yalikuwa yakinichoma moyoni vibaya mno.

“Mpeni mtoto wake.” Kamanda alisema kwa upole huku akionekana kuwa mtulivu.

“Sikiliza we binti.” Kamanda alisema tena safari hii kwa sauti ya ukali kiodogo.

“Hutochukuliwa hatua zozote za kisheria kutokana na hekima za watumishi wa Mungu, unachotakiwa kufanya ni kumlea mwanao kwa mapenzi yote huku ukiwa unaripoti kituo cha polisi asubuhi na jioni kila siku...Tumeelewana?”

“Ndio”

“Lakini tutahitaji kujua ni wapi unaishi ili tujrlidhishe na usalama wa huyu Malaika.” Sister mmoja alishadadia.

“Unaishi wapi?” Afande alidakia.

“Huko mjini, kwenye vibaraza.”

“Uwe unaishi kwenye vibaraza ama shimoni tunachohitaji ni wewe kuzingatia maelekezo...sawa?”

“Sawa Afande.”

Niliachiwa huru nikaondoka na mwanangu, sikuwa na pa kwenda zaidi ya kutangatanga mtaani.

Nilijiapiza kutofanya ujinga wa kumtupa tena mtoto wangu kwa sababu zozote zile, nilikuwa tayari kuhangaika naye kwa hali yoyote.

Nilitembea hadi sehemu moja inaitwa Nazareth Makaburini, wenyeji wa mkoa wa Kigoma wanapafahamu sana eneo lile, kando ya makaburi huwa kuna Viwanda vya Sido ambavyo vinajishughulisha na utengenezaji wa sabuni za Magadi.

Kule kulikuwa na mama ntilie wengi ambao walikuwa wakifanya kazi ya kuwauzia wafanyakazi chakula, dhumuni la kwenda kule ilikuwa ni kuona kama nitapata kibarua chochote cha kutoka kwa wale mama ntilie.

“Utafanyaje kazi huku una mtoto?” mwanamke mmoja mtu mzima aliniuliza baada ya kumwomba kazi.

“Huyu akishiba hana tatizo nitamlaza pale kivuli huku nikifanya kazi utakayonipa.”

“Kweli?”

“Ndio mama”

Nilimtandikia mwanangu vizuri kwenye kivuli cha mti na kuhakikisha kalala, kisha nikaenda kuanza kazi kwa yule mama ntilie.

Hayo ndiyo yakawa maisha yangu kwa muda mrefu, kila siku niliamka alfajiri nikawa naenda kuripoti polisi, kisha natembea tena hadi Sido na kufanya kazi kwa yule mama, na ifikapo jioni niliripoti tena polisi, kabla ya kwenda kwenye makazi yangu ambapo ilikuwa ni kwenye vibalaza.

Siku moja kama ilivyo kawaida, niliamka alfajiri na kwenda kituoni, lakini nikiwa natembea kwa mguu nikabaini kwamba naweza nikachelewa kwenda kazini, ikabidi niende kituo cha basi ili nipande daladala.

Muda si mrefu likaja basi aina ya kosta likiwa limejaa, nikajitoma ndani basi lile nikiwa na mwanangu.

“Mlete mwanao nikusaidie.” Dada mmoja aliyekuwa ameketi katika siti ya mbele ilinisemesha.

Kwakuwa basi lilikuwa limejaa nikaona ni jambo jema kukubali ule msaada, nikampa mwanangu.

Mwendo wa dakika kumi nikawa nimefika kituo cha Maweni ambacho ndipo nilikuwa nikitelemkia.

Nilipotupa macho kwa yule mtu niliyempa mtoto sikumwona, Wakati huo konda akawa anatutaka abiria tunaoteremka Maweni tushuke upesi.

“Yule dada niliye mpa mtoto alikaa siti hiyo hapo yuko wapi?” nilimuuliza mtu mmoja aliyekuwa ameketi na yule mtu.

“Aagh..mbona ameteremka muda mrefu akiwa na yule mtoto”

“Mungu wangu nimeibiwa mtoto!.” Nilimaka.

Hofu na mashaka vilitanda kifuani mwangu, niliendelea kulia huku nikibwabwaja hovyo:

“Nimeibiwa mtoto...mtoto wangu kaibwa...jamani mwanangu!” nilisema nikiwa nimechanganyikiwa.

“Chukua bodaboda uwahi pale Mwembe Togwa aliposhukia yule binti ambaye alikuwa na mwanao, unaweza kufanikiwa kumkamata, kabla hajafika mbali.” Mwanamke mmoja alinishauri.

Niliona ni ushauri mzuri, upesi nilikodi bodaboda na kukimbizwa hadi kituo cha Mwembe Togwa, hata hivyo hakuna nilichofanikiwa, sikumtia machoni yule mwanamke.

Rasmi, nikawa nimempoteza mwanangu, nakumbuka nililia kama mtoto, uchungu niliokuwa nao kifuani hakuwa na maelezo.

Tangu nilipopata akili katika dunia, nilijikuta nikiwa yatima, yatima ninayelelewa kwenye kituo cha watoto, mbali na wazazi, sikuwahi kumjua kaka, dada, mjomba wala shangazi, mtoto wangu ambaye sasa nilimwona kama ndugu yangu kwenye huu ulimwengu, naye nilimpoteza kizembe.

Hakika niliumia mno, nililia na kulia lakini hakuna kilicho badilika. Mwanangu alikuwa kaibwa na mtu nisiye mfahamu.




Wazo la kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi nikaliondoa kabisa kichwani mwangu, niliamini kabisa polisi hawawezi kuniamini kwa mashtaka nitakayokuwa nimeyafungua, hilo lilitokana na lile tukio nililolitenda la kumtelekeza mtoto.


Nikaendela kubaini tena, kama nisipokwenda kutoa taarifa kituo cha polisi, maana yake ni kwamba, hata yale masharti niliyopewa na jeshi la polisi kuwa natakiwa niwe naripoti asubuhi na jioni kituoni nayo niyavunje.


Swali kuu likawa nikiacha kwenda kuripoti kituoni kama nilivyo amriwa, je nitaachwa niendelee kuwa huru pasina kupewa kashikashi na polisi? Jibu ni kwamba nitakamatwa na polisi.

“Sasa nifanye nini” nilijiuliza mwenyewe kiwazimu.


“Lazma nikimbie...nitoroke...mbali na hapa” nikajijibu tena mwenyewe.

Wazo la kukimbia kwa mara nyingine likatawala kichwani mwangu, nikaangalia akiba yangu nikaona nina kama Shilingi elfu sitini, nikaamini pesa hiyo inaweza kunisadia kujiweka mbali kabisa na mji wa Kigoma, na sehemu ambayo niliona ni Mbali na Kigoma ni Jijini Dar.


Nikaelekea stendi.

Nilikata tikieti ya Dar kwenye ofisi za mbasi ya Saratoga, nikawa tayari kwa safari ya Dar kwa siku inayofuatia.




Safari ya Dar ilichukua siku mbili, siku ya pili saa kumi na moja jioni ndio tukaanza kuingia Jijini Dar, hiyo ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuingia kwenye jiji hili.

Sikuwa na ndugu, wala yoyote nimjuye kwenye mji huo, nakumbuka niliteremka stendi ya mabasi ya Ubongo njaa ikiwa inaniuma huku nikiwa sina mwelekeo.


Nilitoka nje ya stendi ile nikawa nalandalanda mtaani, saa mbili usiku bado nilikuwa sijajua nini nifanye kwenye mji huo mgeni.


“Latifa Mustapha!” Nilisikia sauti ikiniita nyuma yangu.

Nilipogeuka nikamwona mvulana mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni machoni mwangu.


“We ni nani?” hatimaye nilimuuliza.

“Charles Okole, siku moja tuliwahi kukutana ndani ya treni, tulikamtwa pamoja na polisi na kufungiwa kwenye behewa.”


“Woooh!..ni wewe!” nilimaka, baada ya kumkumbuka, alikuwa ni mvulana aliyewahi kunisaidia kipindi cha nyuma, kipindi ambacho nilikuwa nikikimbia mji wa Kigoma na kupanda treni kinyamela kabla ya kukamwatwa na polisi. “Ni mimi Latifa, vipi hali? Wajionaje, mbona upo hapa namna hii?” Charles alinitupia maswali ya mfululizo.


Ukweli niliona hiyo ni fursa ya kupata msaada, nilimweleza kila kitu bila kumficha, tangu nilivyo mtupa mwanangu na kukamatwa ndani ya treni, nikarejeshwa Kigoma na kutakiwa kuwa naripoti kila siku kituo cha polisi.


Sikusita kumweleza hadi siku nilipo ibiwa mwanangu na mtu ndani ya daladala.

“Aisee pole sana.” Alisema.

“Nimekwisha poa Charles”

“Kwahiyo umeingia leo hapa Dar?” “Ndiyo”

“Na huna pa kuishi”

“Sina” “Basi twende kwangu” Alisema Charles.


Ingawa nilihitaji msaada, lakini nilisita kuipokea rai hiyo, sikutaka kabisa kujidanganya, kwamba nikienda nyumbani kwa mvulana huyo hatoweza kunigeuza mke wake.


“Mbona unaogopa? Twende kwangu?”

“Sasa tuta..tutaa..ishi..aje..vip..yanii?” niliongea kwa mashaka huku kigugumizi cha kukubali ama kukataa kikinizonga. “Unataka msaada hutaki msaada?.” “Nataka msaada”

“Basi nifuate” alisema Charles



“Unataka msaada hutaki msaada?.” “Nataka msaada”

“Basi nifuate” alisema Charles.

Sikuwa na chaguo jingine zaidi ya kumfuata. Nyumbani kwa Charles Okole palikuwa ni sehemu moja panaitwa Sinza Vatikani.


Nilishangaa kukuta mvulana yule akiishi katika nyumba ya kisasa, ambayo haikufanana na mwonekano wake.

“Hii nyumba ni yako?” “Ndiyo..kwani vipi?” “Kwani wewe unafanya kazi gani?” badala ya kujibu mimi pia nikamtupia swali.


“Mimi ni wakala wa Kabila moja lililopo huko Kongo, linalojihusisha na ulaji wa watu na chakula” Charles alisema kwa sauti ya kujimini.


Pamoja na ushirikiano wa majibu ya maswali yangu, lakini hakuna nilicho kielewa kwenye majibu yale.


“Ulaji wa watu na chakula ndio nini? Niliuliza uso wangu ukiwa na mwingi mshangao. “Achana na maswali ambayo hayatakusaidia chochote maishani, karibu nyumbani na jisikie huru” Charles aliniambia.


Kauli hiyo ilifuta kabisa udadisi uliokuwa umeanza kujitengeneza kichwani mwangu.


Mvulana yule alinipa chumba miongoni mwa vile vilivyokuwa mule ndani nikaweka begi langu, maisha ndani ya mji ule nikayaanza rasmi.

Maisha yangu na mvulana yule yalikuwa ni kama kaka na dada, kile nilichokuwa nikikiwaza awali juu yake ilikuwa tofauti kabisa.


Alikuwa akitoka asubuhi na kwenda kwenye mihangaiko yake, huku nyuma nilibaki nyumbani peke yangu, nikishughurika na kila kitu cha pale, kama kuweka nyumba katika hali ya usafi, kupika na kadhalika.


Maisha yaliendelea huku kumbukumbu za mwanangu zikiendelea kuisugua nafsi yangu kila kukicha, kuna wakati nilikuwa nikilala kitu kama jinamizi lilikuwa likinijia katika ndoto, nilikuwa nikimsikia mwanangu akilia kwa sauti ya juu ndani ya nyumba ile.


Wakati mwingine nikiwa nafanya kazi za nyumbani nilikuwa naona kama vile natakiwa kufanya kazi upesi kabla mwanangu hajamka kwenye usingizi aliolala.

Kwakeli jinamizi la mwanangu lilinipa tabu.


Pamoja na changamoto, hizo hata hivyo maisha kwenye nyumba ya Charles yalikuwa ni maisha mazuri, yalikuwa ni maisha ambayo mwanamke yoyote angetamani kuishi huku Charles akiwa ni mumewe.





Mwanamke yoyote angeweza kutamani jambo hilo, lakini kwangu ilikuwa tofauti. Sikuwahi kutamani maisha ya ndoa, nafikiri ni sahihi kusema, sikuwahi kutamani maisha ya uhusiano wa kimapenzi dhidi ya mwanaume yoyote yule.


Sheby, mwanaume niliyempenda na kuwa na matarajio makubwa, ambaye badaye alinigeuka, alikuwa ameharibu kabisa akili yangu, saikorojia yangu haikuwa sawa kabisa kwenye mambo ya mapenzi.


Nasema haya yote kutokana na tukio moja lililotokea siku moja pale nyumbani.

Ilikuwa ni siku moja, baada ya chakula cha usiku, Charles aliniomba kuzungumza na mimi.


Kwa sauti ya heshima na upole, uso wake ukionesha kumaanisha kile alichokuwa akizungumza aliniambia:


“Nimekuwa nikijiuliza mara mbili na zaidi kama natakiwa kukueleza haya niyawazayo, ama laa! Lakini sauti kutoka ndani ya moyo wangu imendelea kuniaminisha kwamba niko sahihi kusema,” alisema Charles, akapiga kimya kidogo, kisha akaniita.


“Latifa”

“Abee” “Nahitaji kukuoa…kufaunga ndoa na wewe, uwe wangu leo hadi milele,” Charles aliniambia.

Nilijisikia vibaya kuelezwa jambo lile na mvulana yule.


Hali hiyo ilitokana na ukweli kwamba, sikuwa tayari kwa ombi lake tendo la kumkatalia mtu aliyenifanyia ikhisani mjini, lilinivuruga nafsini.


Hata hivyo, sikutaka kabisa kuwa mtumwa wa mapenzi dhidi ya mwanaume ambaye sijampenda wala kuwa na hisia naye. “Sitaki ndoa Charles.” nilimjibu kwa kifupi huku nikitizama kando.

“Kwanini?...kivipi? Hutaki jmbo la kheri Latifa?”


“Sina sababu, sijisikii tu”

“Kwanini hujisikii?” “Basi tu, sina sababu”

“Kweli Latifa?”

“Kabisa”

“Pamoja na mema yote niliyokutendea?”

“Hatujawahi kukubaliana malipo yake yawe mapenzi”


“Lakini mie nataka ndoa, siyo mapenzi!”

“Sijakupenda Charles, wala sijawahi kuvutiwa kimapenzi na wewe.” Hatimaye nilimpasulia waziwazi huku nikimtizama machoni bila woga.


Baada ya jibu hilo wote tukawa kimya, mimi nikimtizama mvulana huyo kwa macho makavu, yeye akiniangalia kwa kutoamini jibu nililompa.


“Hunipendi Latifa!.” Aliuliza kwa suati ya kutoamini huku akinitizama usoni, nilitikisa kichwa kumkubalia kwamba simpendi.

“Sawa mama.” Alisema kwa masikitiko na kuondoka.




Mie pia nilingia chumbani mwangu na kujitupa kitandani huku nikilaani kwa kuharibiwa kwa siku yangu.


Nilijisikia vibaya sana kutongozwa na Charles kisha kumkatalia, nafsi yangu ilikiri waziwazi kwamba mvulana yule aliibuka kama malaika wa ukombozi jangwani na kunipa maji.


Hata hivyo nafsi yangu ikaendelea kukiri kwamba, nilikuwa sahihi kumkatalia mtu yule kwa sababu moja muhimu. Nilikuwa simpendi kimapenzi.


Miasha yaliendelea, Charles akiendelea kunibembeleza nimkubalie. Kuna wakati nafsi yangu ilikuwa ikinigeuka na ikinisuta waziwazi kwa kitendo cha kumkataa mtu yule.


Siku zilikwenda hatimye siku moja nikafanya uamuzi mgumu, nilikubali kuolewa na mvulana yule nisiyemjua vizuri historia yake ya maisha.


Nakumbuka siku chache badaye, nilifunga ndoa na mtu yule, ilikuwa ni ndoa ndogo tu ya mkeka iliyojumuisha marafiki wachache.

Baada ya ndoa, nikayaanza maisha mapya nikiwa mke wa Charles Abdallah Okole.


Tofauti na nilivyo tegemea, mvulana yule alinipenda zaidi ya vile ninavyoweza kusimulia, kwa mara ya kwanza nilijiona ni binadamu mwenye furaha maishani, penzi la mvulana yule liliniondolea unyonge.

Sikuuona uyatima wangu, sikuona upweke tena, sasa nilikuwa ni mtu katika watu. Hata hivyo faraja ile ilikuwa ni ya muda.


Furaha ilianza kuyeyuka baada ya kubaini jambo moja baya mno.

Jambo hilo lilinifanya niwe ni kiumbe mwenye mashaka na wasiwasi wakati wote.


Na ndani ya kipindi hichohicho mume wangu naye akawa kiumbe mbaya na wa ajabu asiye na mfano.


Nilijikuta najuta!.

Kwa miaka mitatu niliyobahatika kuishi na mwanaume yule, ukweli ni kwamba nilikuwa sishiki Mimba, nilisota kila kona kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, lakini wapi.


Wataalamu mbalimbali walitufanyia uchunguzi mimi na mume wangu, hata hivyo karibu madaktari wote walibaini tatizo la kutoshika mimba lilikuwa kwangu, ndoa ikageuka ndoano, lile pendo alilokuwanalo Charles likaaanza kupotea.


Mume wangu akawa ni mtu wa wanawake, kiburi na jeuri vikashika hatamu, niliumia kila nilivyona ndoa yangu inavyoangamia, eti kwa sababu tu sipati mtoto, Nyakati hizo kumbukumbu za mwanangu aliyeibwa kwenye daladala zikawa zinanitesa kichwani.




Mume wangu akawa ni mtu wa wanawake, kiburi na jeuri vikashika hatamu, niliumia kila nilivyona ndoa yangu inavyoangamia, eti kwa sababu tu sipati mtoto, Nyakati hizo kumbukumbu za mwanangu aliyeibiwa kwenye daladala zikawa zinanitesa kichwani.


Niliumizwa sana na hali hiyo, nilijiona ni kiumbe nisiye na bahati hapa ulimwenguni, furaha kwenye maisha yangu ulikuwa ni kitu kimoja adimu.


Siku moja, mume wangu alikawia kurudi nyumbani, saa saba usiku alirejea akiwa kalewa vibaya sana, hakuwa peke yake, alikuwa kaongozana na mwanamke.


Kwakuwatizama halakahalaka nilibaini walikuwa ni wapenzi, bila haya wala hofu waliingia ndani na kuanza kula chakula nilichopika mimi huku wakiendelea na mazungumzo ya kilevi. “We Latifa, hebu kuja hapa.” Charles aliniita kwa sauti ya amri. “Nimekuletea mke mwenzio, mtaishi naye hapa, sawa?”


Alisema kihayawani. “Kwanini umekuwa hivyo mume wangu!. Unafikia hatua ya kuniletea malaya ndani…kweli?”. Nakumbuka baada ya kuzungumza kauli hiyo, kilichofutia ilikuwa ni kipigo cha nguvu, nilipigwa na watu wale wawili bila huruma, walinipiga kiasi cha kupoteza kabisa fahamu zangu.


Masaa kadhaa baadaye nilirejewa na fahamu na kujikuta nipo hospitali Mwananyamla huku mume wangu akiwa kando ya kitanda. “Pole mke wangu.” Alisema kwa sauti tulivu huki akinitizama kwa upole.


Nilihisi labda bado niko ndotoni, nasema hivyo kwa sababu sikutegemea huruma yoyote kutoka kwa mwanaume yule ambaye alishageuka Nyang’au. “Pole mke mama…pole sana mke wangu” “Unasema!” “Nisamehe sana niliteleza”

Kabla sijamjibu lolote mara alingia dokta aliyekuwa amekamata faili na makablasha mengine.


“Pole sana binti lakini hongera pia” alisema Dokta huku akitoa tabasamu pana. “Hongera ya nini?” “Kwani mumeo bado hajakueleza?” Dokta aliuliza huku akitutizama kwa zamu. Mume wangu alitikisa kichwa kumkatalia kuwa hajanieleza chochote.


“Ooh! ulivyoletwa hapa kwa tatizo la ajali ya gari uliyopata, hata hivyo, baada ya kukufanyia uchunguzi tukabaini jambo jingine…..unaujazito wa miezi miwili, zaidi ni kwamba, tatizo ulilopata halijaathiri mimba yako”


Maneno ya daktari siyo tu yalinistua bali yalinifanya nipate nguvu ya kunyanyuka kitandani.



MWISHO



0 comments:

Post a Comment

Blog