Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

BAHARIA

   

MTUNZI: BAHATI MWAMBA


--Gazeti Mwananchi—


Ndege ya shirika la ndege la Tanzania imepotea dakika ishirini tangu ilipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa JNIA. Ndege hiyo ndogo ilibeba watalaamu wa tafiti za magonjwa ya binadamu wapatao watatu. Taarifa zaidi zinasema ndege hiyo ilikuwa ikielekea jijini mwanza katika uzinduzi wa tiba ya magonjwa ya akili na ukichaa kwa binadamu na wanyama, tiba ambayo ilikuwa imegunduliwa na watalamu hao.

Hadi gazeti hili linaingia mitamboni hakuna taarifa zaidi zinazohusu ndege hiyo na wagunduzi hao wa tiba ya magonjwa ya akili...


Siku mbilli mbele..


---Gazeti la Uhuru—


Mabaki ya ndege ya ATCL yamepatikana katika pori la akiba la Inara Njombe. Taarifa zaidi zinasema hakuna mabaki ya miili ya rubani ama matabibu waliokuwamo katika ndege hiyo. Uchunguzi zaidi bado unafanyika kubaini chanzo cha ajali hiyo na utafutaji wa abiria ambao walikuwa ni matabibu bado unaendelea ili kuthibitisha ni wazima au wamepoteza maisha. Tutazidi kukupa taarifa kupitia mitandao yetu ya kijamii kuhusu kile kinachoendelea…



----1------



Miezi nane badae


Unaweza kuwa ni ushamba ndio ulikuwa unamsumbua au la basi ni vile maji hayazoeleki. Ila kwa binti huyu ilikuwa ni ushamba na uoga tu zaidi ndivyo vilivyokuwa vikimsumbua mana kila mara alikuwa anawaza ukubwa wa bahari na vipi kama chombo walichomo kikizama? Mawazo yake yalimjengea woga katika nafsi yake na kila mara alikuwa anatajiwazia namna ambavyo atakuwa anahangaika kuinusuru roho yake wakati chombo hicho alichomo kikienda mrama.

Alichukua chupa ya pombe kali na kumiminia kwenye glasi na kufakamia funda kadhaa lengo likiwa ni kuichangmsha akili yake ili iende sawa na tukio lililokuwa likiendelea mle ndani ya meli kubwa wastani ila ya kifahari sana.

Ndani ya meli ile ya kampuni ya Serengeti Marine kulikuwa kuna tukio maalumu lililokuwa linaendelea kwenye moja ya kumbi za kisasa zilizoko mle kwa matukio maalumu.


Watu wawili walikuwa wanafunga ndoa, ndoa ambayo iliandikwa karibu na kila kituo cha radio; gazeti na runinga. Ilikuwa ni ndoa ya kifahari sana kuwahi kutokea ndani ya nchi ya Tanzania.


Vigegele vilikuwa ni kama vimemzindua binti yule ambae alikuwa amekaa mwishoni kabisa mwa ukumbi ule huku akili yake ikiwa imegawanyika mara mbili, huku akiwaza maji na huku akiwaza sherehe iliokuwa inaendelea.


Aliwatizama maharusi wale ambao walikuwa wanafuraha ya ajabu nyusoni mwao.


Akatabasamu huku na yeye akiungana na wanawake wengine kupiga vigelegele.


Harusi ile ilikuwa ni ya rafiki yake kipenzi alietwa Nyamizi.


Kiukweli katika maisha yake hakuwahi kudhani kama angefikia hatua ya kupanda meli na hakuwahi lau kufikiria kuipanda hata bahati mbaya tu,ila kwa upendo aliokuwa nao kwa rafiki yake wa karibu Nyamizi ulimfanya avunje kiapo chake cha kutokuja kuutumia usafiri huo wa majini.


Nyamizi alikuwa anaolewa na mchumba wake mfanyabiashara kijana kabisa alietwa Boneka na sherehe za ndoa yao waliamua kuzifanyia ndani ya meli ya ya Mv Upendo kutoka katika kampuni za Serengeti Marine.


Angewezaje kusimamia msimamo wake wakati rafiki yake kipenzi anafurahia ndoa yake, na angeonekanaje mbele ya watu waliojua vizuri mahusiano yake na Nyamizi!


Alihudhuria harusi ile ya aina yake na kila aliengia mle ndani alikuwa ni mtu alieheshimiwa na familia za pande mbili zote yani familia ya upande wa Boneka na familia ya upande wa Nyamizi.


Vedi alikuwa amecheza muziki na kuchoka na ndipo alipoenda kupumzika kwenye viti vilivyokuwa mle ukumbini huku watu wengine wakila na kunywa kwa furaha. Maharusi walikuwa wamekaa pahali maalumu palipokuwa pameandaliwa kwa ajili yao na kila aliehitaji kuwapa chochote alifika na kupiga nao picha na kufurahi pamoja.


Vedi pamoja na watu kadhaa walikuwa wameshafanya yote na baadhi walibaki ni kula na kunywa na wengine walielekea kujipumzisha kwenye vyumba vilivyokuwa vimeandaliwa kwa ajili yao ndani ya meli ile.


Meli ile ilikuwa imetengenezwa kwa oda maalumu ili kuvutia wateja wanaopenda kujipumzisha wakati wa safari, hivyo haikuwa na shida kwa walioikodi siku hiyo kutumia vyumba hivyo kujipumzisha na wale waliohitaji kukesha waliendelea kuserebuka wakila na kunywa.


Vedi hakuwa muumini mzuri wa kukesha ama kuserebuka usiku, hivyo pombe kidogo aliokunywa alijikuta ikimchanganya na alihitaji kujipumzisha.

Alimfuata mhudumu mmoja wa meli aliekuwapo maalumu kwa ajili ya kuelekeza watu mambo kadhaa kuhusu huduma walizohitaji. Aliomba kuelekezwa sehemu ya kulala mana alichoka kwa mserebuko aliokwisha serebuka.

Mhudumu yule alimpeleka upande wa chini wa meli ambako kulikuwa kumebaki na chumba kimoja tu baada ya vingine kuwa vimeshajaa na ni kama bahati kukipata hicho alichopata.


Alipokwisha kupewa chumba, alijitupa Kwenye kitanda kidogo kilichokuwa mle ambacho kilitosha kulala mtu mmoja tu, hakuhangaika hata kuvua viatu na usingizi ukampitia.


Ilikuwa karibu saa zima tangu alale, alisikia sauti kama za mabishano kutoka ndani ya vyumba vilivyokuwa kule chini.


Hakutilia mana sana kwa sababu kulikuwa kuna hekaheka nyingi kila pande ndani ya meli ile.


Aliendelea kuuchapa usingizi huku kichwa kikimuwia uzito wa kilo kadhaa kutokana na kugida pombe.


Mzozo uliendelea na sasa waliokuwa wanazozana walikuwa karibu na chumba chake. Vedi alistuka toka usinguzini tena, ila hakusikia kilichokuwa kikiongelewa vyema kulingana na kuwa na wenge la usingizi mzito.


Mkojo!.


Mkojo haunaga adabu siku zote, alibanwa na alijisikia kujisaidia ila kwa kuwa hakuwa mzoefu katika upandaji wa meli, hakuwa amejua upande vilipo vyoo na ukichanganya woga wa kupanda meli basi hakuwa amehangaika kabisa kujua vilipo vyoo.


Akanyanyuka kufungua kile chumba na kutoka nje ambako kulikuwa kuna korido pana na ilikuwa imetenganisha vyumba kadhaa ambavyo vingi vilikuwa vimeandikwa kuonesha vinatumika na mabaharia na vingine viliandikwa kwa kiitaliano na hakuelewa vilimaanisha nini.


Alizidi kuyumba kufuata korido ile upande mwingine tofauti na ule ambao waliingilia na baharia aliempeleka kwenye vyumba vile. Aliendelea kusonga taratibu huku kila mara akiyumba na kubeua.

Korido ile ilimfikisha hadi upande ambao kulikuwa kuna ngazi zilizokuwa zikishuka chini zaidi kwenye meli ile.


Wala hakujiuliza bali alizidi kwenda huku akisoma vyumba kadhaa vilivyokuwa na maandishi.


Kwa mbali alianza kusikia migongano ya vyuma na hewa nzito upande huo alikokuwa anaelekea.


Alikuwa amefika upande wa injini ya meli ile.


Akaamua kugeuza baada ya kuhisi hali ya hewa haiwezi kuwa rafiki nae tena.


Hakupiga hata hatua tatu akaona korido nyingine akaamua kuifuata korido hiyo ambayo ilimfikisha kwenye chumba kilichokuwa wazi na makororo mengi yalioonekana kuwa ya ufundi na dumu kadhaa za mafuta.


Kibofu kilikuwa kimejaa mkojo na ni lazima akojoe la sivyo angeadhirika.

Akaona chumba kile kinamfaa kumaliza shida zake harakaharaka ili arudi kuendelea kuukata usingizi wake kwa raha zake.


Tofauti na alivyodhani kwamba chumba kile ni kidogo,chumba kile kilikuwa kina upana wa kutosha tu na baada ya kuingia alibaini kwa mbele yake kulikuwa kuna taa zinawaka.


Hakujali!


Alianza kupapatua nguo zake za ndani na kuchuchumaaa huku akiwa amejibanza nyuma ya mapipa.

Alipokamilisha hitaji lake akasimama ili atoke kwenye kile chumba, ndipo aliposikia nyayo za miguu ya mtu ikiingia kwenye chumba kile kwa mwendo wa taratibu huku akijiongelesha peke yake.


Vedi akataka kutoka ili aendelee na hamsini zake akiamini ni miongoni mwa watu tu waliokuwa kwenye sherehe ndani ya zile meli.


Ila alijikuta anasita kutoka alipokuwa na kutulia kimya kabisa.

Mtu yule alimpita taratibu na kuelekea mbele kulikokuwa kuna waka taa.


Vedi alinyanyua kichwa chake taratibu na kumtizama mtu yule ambae alikuwa amevaa kofia kubwa ya pama kichwani mwake na koti zito mwilini mwake na alivaa suruali ya jinzi mpauko na mikono alikuwa ameiweka mfukoni.


Vedi alitoka pale alipokuwa akanyata na kujikinga nyuma ya pipa moja lililokuwa karibu na njia alioingilia na hapo aliweza kuona vyema upande ule kulikokuwa na mwanga wa taa.

Mtu yule safari yake iliishia kwenye kontena dogo na akalifungua kisha akaingia ndani yake.

Vedi alistajabu kidogo, tangu aingie mle ndani hajapata kuona mtu alievaa mavazi kama yale isipokuwa kila mtu alikuwa amevaa mavazi mazuri ya kuvutia na hata wahudumu na mabaharia kadhaa waliokuwa mle ndani walikuwa wamevaa mavazi maalumu kwa ajili ya sherehe ile ili watambulike kirahisi na wageni waliokuwa mle.

Sasa vipi tena mtu kuwe na mtu mwingine ambae hana mavazi maalumu na amevaa kiajabu ajabu namna ile?

Na ndani ya kile kikontena kafuata nini mtu yule.


Vedi hakuwa na wakumjibu na alitaka kutoka kuendelea na mambo mengine ila akajikuta anashindwa kufanya hivyo,hajui ni nini kilimsababisha kutaka kuendelea kubaki eneo lile.


Zilipita dakika zaidi ya tano bila kuonesha dalili ya kutoka kwa mtu yule na ndipo Vedi akataka kuondoka mana hakuona kama ni busara kuendelea kukaa pale.

Wakati anataka kunyanyuka ili aondoke,masikio yake yalinasa sauti ya muanguko wa kitu kama chuma kutokea kwenye kile kikontena,akarudi tena kujibanza pale alipokuwa awali na kutulia.

Haikupita dakika; mtu yule alieingia ndani ya kile kikontena akatoka huku akivaa kofia yake kichwani kwa mkono wa kulia.


Ajabu nyingine!


Mtu yule alikuwa amevaa miwani katika usiku ule.


Eeh makubwa!


Alijisemea Vedi huku sasa akiona mtu yule akimpita pale kwa mwendo wa haraka tofauti na mwanzo alivyoingia.


Mtu yule akatokomea akabisa na pale ndani alibaki Vedi peke yake.


Ni kiherehere chake tu kilichomsababisha aelekee kule kwenye kile kikontena,nae akaingia ndani yake.


Alikutana na giza zito na harufu kali ya kitu ambacho hakujua kama ni uozo ama ni vumbi lenye mchanganyiko wa vimiminika kadhaa.


Vedi akawasha simu Janja yake iliokuwa inamwanga wa kutosha tu kumulika mule ndani.


Tofauti na matarajio yake ya kuwa pengine mle ndani ni pachafu sana, la hasha kulikuwa ni kusafi licha ya kuwa kuna mpangilio wa meza za chuma mbili zilizokuwa zimewekwa kwa mtindo wa kulaliana, yani moja ilikuwa imesimamishwa kama kawaida na nyingine ilikuwa imesimamishwa kitako juu ya ile nyingine huku mgongo wake ukiwa umetazamana na Vedi na miguu ikiwa imetizama upande wa pili wa ile kontena.


Pale kwenye meza iliokuwa imeagamiwa na nyingine kulikuwa kuna kitabu kidogo cha kumbukumbu(Diary).


Hakukijali!!


Akapiga hatua zake taratibu na kuelekea kule ambako kulikuwa kuna miguu ya meza iliosimamishwa juu ya meza nyingine.


Alianza kwa kuona viatu vyeusi na suruali ilionza kutatuka,kisha akaona koti jeupe likiwa limefikia usawa wa magoti ya suruali aliiona.


Vedi akaanza kuingiwa na wasiwasi na alizidi kujongea na mara macho yake yakanasa taswaira ya ajabu kwenye miguu ya meza. Vedi aliruka juu na kupiga ukelele wa woga huku akirudi nyuma kwa hamaniko ya kile alichokiona.


Maiti ya mtu!!


Aliona mtu akiwa amesimama huku uhai ukiwa mbali na yeye,mtu yule alionekana kufa siku kadhaa nyuma na tayari ngozi yake ilianza kunatana na mifupa huku nyama na misuli ikiwa imeanza kuyeyuka mithili ya sponji.

Mtu yule alikuwa ameachama kuonesha alikufa kwa mateso na macho yake yalionekana kutumbuka kwa woga wa kifo kilichomkuta. Mikono ya yule mtu ilikuwa imetandazwa kwenye vyuma vilivyokuwa vinaunganisha miguu ya ile meza na miguu yake ilionekana kufungwa pamoja na kamba ambayo ilianza kuoza.


Ilikuwa picha ya kutisha machoni mwa Vedi;pombe yote ikamuisha na roho yake ikachafukwa.


Aliuwawa lini na kwanini; Vedi hakujua ila kitu pekee alichobaini ni kuwa mtu yule alikuwa amevaa mavazi maalumu ya wapishi wa meli, hasa koti lilikuwa limefanana sawa na makoti wanayovaa wapishi.


Mtu yule alikuwa baharia bila shaka kulingana na mavazi aliokuwa amevaa.


Vedi alishindwa kuelewa kwa nini jambo lile limetokea na kwanini auwawe afu aachwe mle mle ndani ya meli bila kutupwa kwenye maji au kuzikwa kabisa. Alishindwa kujua ni nini kusudi la kuihifadhiwa pale yule jamaa.


Au hawajui kama kuna mtu kafia kwenye karakana hii ya ufundi?


Hapana!!


Yule mtu aliemuona akiingia mle anaonekana anajua kinachoendelea ndani ya kikontena.


Aisee!!


Vedi alikurupuka kutoka alipokuwa na kutaka kukimbia kutoka nje ila wakati anafika kwenye meza iliobeba meza nyingine yenye maiti ya mtu, aliona tena kile kitabu kidogo cha kumbukumbu, akakiokota na kukitia kwenye mfuko wa koti la suti yake kisha akarudi tena kuitazama ile maiti na akaona kitambulisho kilichokuwa kinang’inia shingoni mwake, akaamua kukipiga picha na hapo akanasa sura nzuri ya kijana iliokuwa kwenye picha ndogo ilioambatanishwa kwenye kitambulisho kile. Ila hakuona jina kwenye kitambulisho kile na alipokuza picha aliopiga aliona likiwa kimekwanguliwa.


Kwa nini?

Hakujua sababu ya kukwanguliwa kwa jina kwenye kitambulisho kile.


Mikono ilikuwa ikimtetemeka na roho ilikuwa ikimdunda, hajawahi kuona mtu akiwa amekufa katika mateso namna ile.


Kwa nini wamekuuwa baharia!!?


Hakujibiwa na maiti ile.


Vedi aliamua kuondoka ndani ya kikontena kile, akapiga hatua chache na kabla hajatokeza kwenye mlango akasita kutoka.


Nje ya kikontena kile kulikuwa kuna mtu akiongea na mwenzie kwenye simu..

Kwa wizi wizi akarefusha shingo na kufanikiwa kuchungulia nje ya kikontena kile.


La haula!!


Alikuwa ni yule bwana aliemuona akiingia na kutoka ndani ya kikontena kile kidogo ambacho sasa yeye ndo alikuwamo.


Vedi alitamani kufanya miujiza ya kina Shumireta ya kupotea ila haikuwezekana, na alitamani apige kelele ila kwa alivyoona meli ile ilivyo hakuna ambae ambae angemsikia zaidi ya yule bwana ambae alikuwa nje ya kontena na alionekana sio mwema kabisa na wakati huu alikuwa amevua kofia na kufanya upara wake uonekane na kichwa chake kikubwa kilichojaa kisogoni.

Haieleweki sababu gani ilimfanya yule bwana avae miwani usiku.

Vedi alibaki akitetemeka.


Mara simu yake ikatetema kuashiria inaita.


Vedi akaruka juu na kuitupa chini na kuiacha ikisambaratika hovyo.


Aliiogopa mtetemo wa simu yake mwenyewe.


Yule bwana kule nje alisikia msambaratiko wa kitu kwenye kikontena kile na akageuka kutazama.


Ebanaee


Vedi mkojo uligonga hodi langoni kwa kalichumbage wake na jasho la kucha lilimtoka.



SEHEMU YA PILI



Yule bwana kule nje alisikia msambaratiko wa kitu kwenye kikontena kile na akageuka kutazama.


Ebanaee


Vedi mkojo uligonga hodi langoni kwa kalichumbage wake na jasho la kucha lilimtoka.


Bwana yule

hakuonekana kujali.


Pengine aliamini ni panya tu wanagombania mzoga au ni vyuma vilivyoko mle.


Aliendelea kuongea na simu bila wasiwasi wowote kisha alipomaliza akairudisha kwenye mfuko na kuanza kutoka tena kurudi nje ya chumba kile chenye zana za ufundi wa meli na pipa kadhaa za mafuta.


Vedi alishusha pumzi kwa nyingi na kumshukuru muumba wake.

Haraka haraka akajinyanyua pale alipokuwa ameangukia baada ya kusituliwa na mtetemo wa simu yake.

Akaanza kupapasa chini na alifanikiwa kupata mfuniko na betri na kisha kwa papara akaviunganisha na kuchukua mfuniko wa urembo(kava) na kulipachika juu kisha haraharaka akachomoka kama mshale hata vile viatu vyenye visigino virefu havikumpa shida kabisa kuzikata pepo.

Akatoa kabisa kule chini na kuanza kupanda juu kwa kasi huku akizehesabu ngazi kama mchezo na hatimae alifika kwenye korido ile ambayo kulikuwa kuna chumba alichokuwa amelala.

Akaingia harakaharaka na kufikia kitandani ambako kulikuwa kuna mkoba wake akaukwapua na kutaka kutoka, akakumbuka kitu…


Kwenye mgongo wa mfuniko wa simu na kava alikuwa amepachika kadi ya harusi iliokuwa na jina lake kamili.


Shiit!! Alimaka kwa gadhabu.


Haikuwepo!!


Aliitafuta huku na huko bila mafanikio alipekua kwenye mkoba bila kuipata na bado akili ilimwambia aliiweka kwenye mgongo wa simu yake na atakuwa ameiacha kule kwenye kile kikontena!!.


Mungu wangu!!


Alishika kichwa kwa huzuni mana asingeweza tena kurudi kule kukitafuta kikadi kile cha harusi ile.


Kitu kimoja alichohofia ni kuwa endapo polisi wangefika kuchunguza kule chini na kukikuta kadi ile basi yeye angekuwa mhusika wa kwanza kutafutwa.


Aligwaya zaidi baada ya kutokujua yule bwana aliemuona yupo upande upi hasa,kati ya usalama na watu waliohusika na mauaji yale.

Kama ni usalama na akirudi tena kule akute kile kikaratasi basi atamharibia.


Ila dah!!


Yule bwana hakufanania kuwa mtu wa usalama kwa mwonekano wake tu alionekana ni mtu wa shari shari na kichwa chake kizito kama mamumunya.

Vedi hakutaka kuendelea kuumiza akili yake kuhusu hilo jitu na kile kikaratasi, akafungua mlango na kutoka.


Ebanaee!!


Alikutana na yule bwana tena akitoka kwenye chumba cha jirani na kile alichokuwamo huku akiwa na kisu mkononi.


Vedi aliruka nyuma na kujingonga kwenye mlango huku akiachia ukelele wa woga na macho yake yakiwa kwenye kile kisu alichokuwa ameshika bwana yule huku nae akiwa ameganda kwa kushindwa kuelewa binti yule alihamanika nini baada ya kumuona.


Bwana yule akahamisha macho yake na kutazama mkono wake uliokuwa umeshika kisu,akatabasamu kifedhuli baada ya akili yake kuhisi pengine yule binti aliogopa kile kisu na namna alivyokishika.

Bwana yule akakivutia kwa juu na kisu kile kilipotelea kwenye mkono wa koti alilokuwa amevaa.


“No problem, relax and enjoy the night” alisema yule bwana huku akitabasamu kumuondoa Vedi kwenye hofu.


Vedi alianza kujisogeza huku mgongo ukiwa unajiburuza kwenye kuta za korido ile na macho yakiwa kwa yule bwana ambae nae alianza kuondoka kuelekea kule chini.

Vedi alipohakikisha yule bwana amepotelea kwenye kona nae akachomoka kwa kasi na kuelekea juu ukumbini, hakutaka tena kulala wala kuwaza kulala huku akiwa ameona jambo gumu kutazamika.


Alifika ukumbini,hakuna alichoona kipo cha kupendeza, hata watu alioona wanacheza aliona kama wanapoteza muda, waliokuwa wamekaa wanapiga soga za hapa na pale aliona kama ni watu wanaodhihaki maisha yake.


Kuna kitu kimoja kilimjia Vedi; alitamani sana kuweka bayana lile jambo na watu wakajua kinachoendelea ndani ya meli ile, lakini alijikuta akijawa na hofu kusema jambo lile na kama akisema ni nani wa kumwamini?


Aliona mtu pekee wa kumuamini ni Bi harusi Nyamizi; rafiki yake wavaa nikuvae.

Akataka kusimama kutoka alipo ili aende sehemu alipowaacha maharusi,ila hakuwaona. Aliangaza huku na huko mle ukumbini ila hakuwaona na hapo alihisi inaweza kuwa wameenda kujipumzisha baada ya hekaheka za kutwa na usiku ule.


Akataka kupiga simu, ila hakuona kama ni busara kumsumbua mtu na mkewe ambao walikuwa wamejipumzisha wakati huo.


Saa iliokuwa kwenye simu yake ilimwambia ni saa kumi kamili alfajiri.


Aliona muda haiuendi kabisa na kwa mujibu wa ratiba, wakati huo ndio wakati ambao meli ilitakiwa ifike kwenye fukwe za Pemba na kisha igeuze kurudi jijini Dar es laam na kila mtu arejee nyumbani kwake huku maharusi wakielekea jijini Nairobi kwa ajili ya fungate.


Kwake yeye aliona muda huo ni mwingi sana hadi kufika hiyo ahsubuhi ambayo ilipaswa meli itue nanga jijini Dar.


***

Shamra shamra zilikuwa zinaendelea na hata wale ambao walikuwa wamelala,sasa waliamka na kurudi tena ukumbini na wale ambao wamezoea kuukata ulabu, waliamkia supu iliokuwa imeandiliwa kwa ajili ya kukata pombe na wale wazee wa kubuma sana walikunywa supu kisha wakaendelea kugida pombe.


Ukumbi ni kama ulianza upya tena utadhani ndio sherehe zinaanza, kumbe ndio zilikuwa zinamalizikia.


Vedi alikuwa amekaa mwishoni kabisa mwa ukumbi na ambako hakukuwa na mwanga wa kutosha, alikuwa amekaa huku taswira ya maiti ikimrudia akilini mwake kila mara na ni kama aliona ikimlilia.


“Sasa unaninilia nikufanyeje!?” alijisemea peke yake akiwa amejikunyata kama kuku anaeumwa mdondo.


Wakati akiwa bado anatafakari hili na lile kuhusu kile alichokiona, mara akahisi karibu yake kuna mtu kapita, akanyanyua uso wake.


La haula!!


Alikuwa akitizama mgongo wa yule bwana ambae alionekana kama anaetafuta kitu au mtu katikati ya watu waliokuwa wakicheza na kunywa huku wengine wakiwa wamekaa kwenye viti na vilaji vyao kwenye meza.


Mtu yule alikuwa anapiga hatua taratibu huku akizungusha kichwa chake taratibu kama bundi awindae.

Hakujali msonagamano wa watu wengi waliokuwa mle ambao kimavazi ni yeye tu alienokena amevaa mavazi yasio rasimi na hayakuendana na hadhi za sherehe ile inayoelekea kufika ukomo.


Hilo hakujali bwana yule.


Kichwa chake kiliendelea kuzunguka taratibu huku akionekana kumakinika na kila mwanamke aliemuona mle ndani.


Hatimae yule bwana alipiga hatua na kuzidi kuelekea upande ambao kulikuwa kuna mpiga muziki na wachukua video kadhaa.

Akajichanganya nao, kisha akageuka na kuwa na nafasi nzuri zaidi ya kumtazama kila mtu kutokea kona ile maalumu kwa wapiga picha na muziki.

Bwana yule aliendelea kuzungusha kichwa chake alichokivika kofia huku macho akiwa ameyaziba na miwani nyeusi.


Macho ya yule bwana yaligota kwenye kona moja ambayo haikuwa na mwanga wa kutosha zaidi ya ule wa taa za rangi zilizokuwa zimefungwa upande ule.


Vedi alibaki akitetemeka baada ya kuona macho ya mtu yule yakiwa yameganda kutazama pale alipokuwa.


Hakika hakujua yule bwana alikuwa anamuwazia nini kama akiwa amemuona pale alipokuwa.


Na yakabaki maswali kadhaa kichwani mwa Vedi.


Kwa nini mtu yule kaingia mle ukumbini wakati huu? Na kwanini amtazame kiasi kile, vipi amejua kuwa aliingia kule kwenye kontena?


Mungu wangu; ananiwazia nini huyu?”alijiuliza Vedi bila kupata jibu.


“au amejua niliingia kule? Na amejuaje sasa” aliendelea kujiuliza bila kupata majibu.


Kadi!


Aliikumbuka ile kadi alioidondosha kule chini.


“ooh my God!!” alijishika kichwa Vedi baada ya kukumbuka kadi ile.


Lakini tena akajiuliza, kama ameikuta ile kadi, amejuaje kuwa ni mimi mmliki wake?


Aah shiit!! Alizidi kuchanganyikiwa Vedi.


Mtu yule alibaki akiangalia pale alipokuwa Vedi kwa zaidi ya dakika tano, kisha akamgusa mpiga picha mmoja na kumwelekeza jambo na bada ya hapo mpiga picha yule alielekeza kamera yake kule alikokuwa Vedi na kisha akapiga picha kadhaa hivi bila Vedi kutilia maanani maongezi ya mpiga picha na yule baradhuli.


Vedi hakujua kama anapigwa picha na kamera ile ambayo haikuwa na mwanga.


Vedi nae alikuwa bado anamuwaza mtu yule ambae wakati huo alikuwa ameshatoweka kwenye ukumbi ule.

.

“Mtu huyu ni nani lakini?” alijiuliza Vedi.


Mana hakuonekana kuwa ni baharia au Nahodha; hakuonekana kuwa hata tabibu wa dharura ndani ya meli ile.


Ni nani hasa ndani ya meli ile na yule mtu aliekufa kwanini hatupwi au kuzikwa?


Ebana e!


Maswali mengi kuliko majibu.


Vedi alitatizika na raha ya harusi ile kwake ikawa ni karaha huku akilaumu ni kwanini alifakamia pombe ambazo ziliishia kumletea mkojo uliompelekea kuona yale alioyaona.


**

Zilipita kama dakika kumi tu tangu mtu yule atoke ndani ya ukumbi ule, ndipo kikazuka kizazaa kilicholeta taharuki isiosemekana mwishoni mwa sherehe zile.


Ilikuwa ni wakati ambao mshehereshaji alipotangaza ya kuwa huko nje ya meli kuna binti aliejitupa ndani ya maji na sababu ya kufanya hivyo haikufahamika.


Watu wote walitoka na kuelekea nje ya ukumbi na kutazama kule ambako ilisemekana amejirusha, mabaharia kadhaa walikuwa wameshajitosa majini ili kuangalia uwezekano wa kumuona huyo aliejitupa majini.


Licha ya jitihada nyingi kufanyika kumtafuta, bado hawakufanikiwa na ndipo timu ya uokozi ilipopewa taarifa kutoka Dar es laam ili kufika hapo na kutoa msaada zaidi.


Wakati wa mapambazuko ndipo meli ipopiga honi kuashiria inafika ukomo wa safari baada ya kuzunguka baharini usiku mzima.



Nani tena kajitosa baharini? Ni vedi? Na kwanini sasa ajitose majini na kuacha ugali ukiliwa Duniani?


Kumjua aliejitosa, ungana nami hapa hapa




Watu wote walitoka na kuelekea nje ya ukumbi na kutazama kule ambako ilisemekana amejirusha, mabaharia kadhaa walikuwa wameshajitosa majini ili kuangalia uwezekano wa kumuona huyo aliejitupa majini.


Licha ya jitihada nyingi kufanyika kumtafuta, bado hawakufanikiwa na ndipo timu ya uokozi ilipopewa taarifa kutoka Dar es laam ili kufika hapo na kutoa msaada zaidi.


Wakati wa mapambazuko ndipo meli ipopiga honi kuashiria inafika ukomo wa safari baada ya kuzunguka baharini usiku mzima.


***


Vedi alishuka kwenye meli na kupita moja kwa moja hadi nje ya eneo la abiria, huko alichukua usafiri na kurudi nyumbani kwake alikokuwa amepanga.

Alipofika akaingia ndani na kujitupa kwenye sofa iliokuwa sebuleni kwake kisha akapumua kwa nguvu na kutupa viatu vyake virefu bila kujali vitakapoangukia.


Vedi alipumua kwa nguvu na kutazama juu kwa tafakuri.


Akakurupuka!


Akauendea mkoba wake mdogo uliokuwa na vitu vyake baadhi na alikuwa nao ndani ya meli.


Akaufungua na kupangua vitu kadhaa vya kujirembea pamoja na taulo ya kike ambayo aliiweka kwa dharura.


Hatimae macho yake yalipata kile alichokitaka.


Kilikuwa ni kile Kitabu kidogo cha kumbukumbu alichokichukua ndani ya kikontena wakati alipokuwa ndani ya meli.


Akakifunua!


Alikutana na mambo machache katika ukurasa wa kwanza na alipoyasoma hakuona kama ndicho alichokihitaji katika kitabu kile.


Kwanza alihitaji kujua kama kitabu kile kimeandikwa kwa matumizi sahihi ya kitabu chenyewe, yani kimeandikwa mambo muhimu ya mmiliki wake. Pia alihitaji kujua kama atafanikiwa kujua kama mmiliki aliandika jina lake na watu wake wa muhimu ikiwemo na mawasiliano yao..


Katika ukurasa uliofuata alikuta jina na tarehe.


“Banzi Kela….tarehe 06/4/2017”


Akafunua tena kurasa nyingine na alifanya hivyo ili kujiridhisha na mawazo yake.


Baada ya kusoma maelezo ya ukurasa ule akarudi tena kwenye ukurasa ambao ulikuwa na jina na tarehe na hapo ndipo alijiridhisha na fikira zake ya kuwa kitabu kile kilianza kutumika tarehe ile na yawezekana lile neno Banzi Kela ni jina na ni la mmiliki wake.


Kichwani mwake akapitisha jina hilo na umiliki wa kitabu kile.


Aliendelea kufungua kurasa moja na nyingine na kusoma yaliondikwa hatimae alifika kwenye ukurasa uliokuwa umeandikwa ujumbe maalumu kwa ajili ya mtu ambae aliamini ni mpenzi wa Banzi.


“Kwako Mamu!

Ni ukweli nakupenda sana kuliko sana yenyewe. Mamu najua unanipenda pia, ila kwa tulipofikia inabidi niwe mbali na wewe. Sio kama umenikosea la hasha ni kwa kuwa tu nataka uishi kwa amani zaidi ukiwa mbali na mimi. Hivi sasa mimi si Banzi tena ila ni marehemu mtarajiwa Banzi. Usiniulize kwanini ila kabla ya kuuliza nenda Hard Rock kwa Jezebeli anaujumbe wa matumaini yangu.” Ulisomeka hivyo ujumbe ule.


Vedi aliganda kwa sekunde kadhaa baada ya kuusoma.


Ni kawaida kwa wapenzi kuandikiana jumbe nyingi, ila ni mara chache kuandikiana jumbe za kutisha na kusononesha namna ile.


Banzi alikuwa na mpenzi anaitwa Mamu na anamtahadharisha juu ya mauti yanayotembea nae.


Mh!!


Vedi akaguna huku akijiweka sawa kwenye sofa yake.


Kwanini sasa Banzi ajitabilie kifo? Na je ujumbe ule ulimfikia Mamu mwenyewe?


Hakuwa na majibu wala wa kumjibu.


Haraka haraka akaanza kupitia kurasa moja na nyingine,alikuwa anatafuta lau mawasiliano ya huyo Mamu na aliamini kabisa mawasiliano yatakuwemo mule.


Hadi anamaliza kukipitia bado hakuwa amebahatika kuona namba yoyote ile ya simu.


Akarudia tena kupitia kwa mara nyingine, bado hali ilikuwa ile ile.


Mh!!.


Akaguna peke yake na kurudi pale kwenye ukurasa wa ujumbe wa Mamu.


Kuna kitu alikiona..


Katika ukurasa ule mwishoni kabisa kulikuwa kuna namba imeandikwa na ilikuwa ni sifuri..


Alifunua tena ukurasa mwingine na hakuona namba ila uliofuata aliona tena namba ikiwa imeandikwa na ilikuwa ni namba Saba.


Akaendelea kupitia na kuzinakili namba zile kwenye simu yake na zilikuwa ni namba kumi kwa ujumla wake.


Aisee!!

.

Vedi alishangaa akili nyingi za Banzi. Banzi alikuwa anasababu gani kuficha namba zile katika aina ile?.


Vedi alijiaminisha kabisa ya kuwa kuna kitu kilikuwa kinaendelea kwa Banzi si bure.


Akajaribu kuzipiga zile namba.


Simu haikutoka!!..


Vedi akarudia tena na hali ilikuwa ile ile.


Akatazama ntandao katika simu yake na alikuta upo chini hausomi.


Ebo!!

.

Na laini iliandika “emergency”


Aisee!!


Tatizo nini?


Hakupata wa kumjibu.


Alibaki akiwa amefadhaika.


Akajinyanyua kwenye sofa na kuelekea ndani kwake ambako alichukua ndoo ya maji na kumimina kwenye ndoo nyingine maalumu ya kuogea kisha akatoka nje na kwenda kuoga ili kuondoa uchovu wa usiku uliopita.

.


Dakika kadhaa badae alitoka na kukuta wapangaji wenzie wakiwa wamekaa vibalazani mwao, akawasabahi na kuelekea ndani kwake.


Akaanza kujiremba harakaharaka ili awahi kituo cha kusajilia laini apate utatuzi wa laini yake kisha amtafute mmiliki wa namba alioikuta kwenye kitabu cha Banzi.


Wakati anaendelea kujipara akachukua kitenzambali(rimoti) na kuwasha runinga.


Alikutana na habari ambayo ilikuwa inamalizikia ila alisikia jina lake likitajwa na kisha zikafuatia picha ambazo zilipigwa wakati mabaharia wakijitahidi kuokoa mtu aliesemekana kujitosa baharini.


Roho ilianza kwenda mbio na kushindwa kuelewa dhumuni la jina lake na picha za uokozi.


Habari iliishia na hakuambua japo maana ya kile alichokiona mwishoni.


Akarukia simu yake kwa pupa, mara akanywea kama maji katikati ya vumbi baada ya kukumbuka simu yake haisomi mtandao.


Akavaa haraka haraka na kutoka nje.

.

Ebwana eeh!


Alishangaa wadada wawili wakirukia ndani kwao kama walioona jini katikati ya kiza kinene huku wakipiga ukunga wa kuogopa.


Alisita kutoka mlangoni kwake akabaki akitizama milango ya wadada wale.


Mhh kuna nini tena?


Alijiuliza peke yake huku hisia mbaya zikianza kumwandama kichwani mwake.



“ooh no! Isiwe kweli basi” Alijisemea huku machozi yakianza kumlenga.


Kuna hisia mbaya ilipita ubongoni mwake kuhusu habari alioona inamalizikia.


Alihisi anahusanishwa katika kifo kile cha mtu kujitupa ndani ya maji.


“Au ile maiti imetupwa majini na uchunguzi umeangukia kwangu baada ya kuacha kadi ile…” Alijikuta akitoa chozi huku akianza kupiga hatua ndefu kutoka pale alipokuwa amesimama.


Haraka yake ilikuwa ni kufika kwa kijana anaesajili laini za simu aliekuwa jirani na hapo alipokuwa akiishi.


Aliihitaji laini ili awasiliane na wazazi wake na kisha amtafute mmiliki wa namba alioipata kwenye kitabu cha kumbukumbu alichokitoa ndani ya meli.


Alitembea kwa hatua za haraka haraka na kuvuka barabara kisha akapita vichochoro viwili na kutokea sehemu iliokuwa imechangamka kidogo.


Akaangaza kidogo na kumuona kijana aliemhitaji ambae wakati huo alikuwa amezungukwa na mabinti wengine wawili waliionekana kuhudumiwa.


“Mambo!” Vedi alimsabahi kijana yule huku akimshika bega kwa nyuma na kijana yule akageuka.


Loh!


Kijana akaruka juu kama shoga lililotekenywa na mtoto.


Hakuishia kuruka tu, akapiga kelele kwa sauti huku akirusha mikono yake kama mtu anaeshambuliwa na nyuki na kitendo kile kilifanya wale mabinti waliokuwa wakihudumiwa nao waanze kutimua mbio huku wakipiga kelele bila kujua wanapiga kwa sababu gani.


Vedi alivutwaika.


Macho yake hayakubanduka kwa yule kijana ambae alikuwa amefika mbali kidogo na kugeuka huku akiwaeleza jambo watu waliokuwa wameanza kujaa kumshangaa.


Vedi alishindwa kuelewa.


Macho ya Vedi yalitua kwenye meza ya kazi ya yule kijana,aliona simu janja ya kijana yule na ilikuwa bado inaonesha mwanga kuashiria ilikuwa kwenye matumizi dakika chache zilizopita.


Akavutiwa na kile alichokiona.


Akaichukua simu ile na kuanza kusoma.


Ebana eeh!


Vedi aliishiwa akili ya kufikiri na kujikuta machozi ya kimtoka huku nafsini mwake kukiwa na sauti kubwa ya kupingana na jambo lile.


Alirudi tena kusoma na hakikuwa kimebadilika kitu.


Alikuwa anasoma katika tovuti moja ya kuwa mtu aliejurusha ndani ya maji amaekolewa na kufahamika kwa jina la Vedi Mashimo mkazi wa kisutu Dar es laam.


Kisutu ndio aliishi na hilo jina ni lake na sio jina tu hata picha zilikuwapo za kwake kuonesha yeye ndie alijitosa baharini na kupoteza maisha.


Akairejesha ile simu na kupiga hatua kuelekea nyumbani kwake; Baadhi ya watu waliomfahamu wakajiweka mbali nae.


Vedi alifadhaika kwa kitendo kile,machozi yalimtoka na mwili ulimwia uzito na kujikuta akipiga hatua za kinyonga.


Akajitahidi na kurejea nyumbani kwake, ila wakati anaingia tena, majirani zake wakaanza kupiga kelele za woga huku wakiita jini jini.


Hakuwajali akaingia ndani kwake ambako wakati anatoka hakufunga mlango.


Ebana eeh!


Ndani napo hakukuta mabegi yake ya nguo na viatu na baadhi ya picha pia zilichukuliwa huku akiachiwa mkoba tu ambao alikuwa ameuangusha uvunguni mwa meza.


Akachanganyikiwa!


Haraka akatoka nje na kuelekea upande wa pili ambako aliamini waliochukua vitu vyake ni lazima waliacha usafiri huko.


Hakuamini macho yake, aliona gari la baba yake mzazi likiwa linaingia barabara kubwa likiwa linatokea pale kwake.


“aah ina maana nyumbani nao wanajua nimekufa hadi wafuate nguo zangu?” Alijiuliza huku akiwa ameweka mikono kichwani.


Vedi hakujua afanye nini katika dakika zile ili kuondoa uongo ule ambao ulikuwa unasambaa kwa kasi kama moto wa kifuu.


Nb: Maoni yako ni muhimu Sana katika kazi hii.

Karibu kwa maoni yako juu ya hiki kitu




Hakuamini macho yake, aliona gari la baba yake mzazi likiwa linaingia barabara kubwa likiwa linatokea pale kwake.


“aah ina maana nyumbani nao wanajua nimekufa hadi wafuate nguo zangu?” Alijiuliza huku akiwa ameweka mikono kichwani.


Vedi hakujua afanye nini katika dakika zile ili kuondoa uongo ule ambao ulikuwa unasambaa kwa kasi kama moto wa kifuu.


****

Vedi aliona kama utani,ila ndivyo ilikuwa; vyombo vyote vya habari vililiripoti tukio lile kwa marefu na mapana huku sababu ya binti kujiua ikihusanishwa na wivu wa kimapenzi.


Habari zingine zilisema Vedi alijiua kwa kuwa hakupenda kuona rafiki yake akiolewa na bilionea kijana kabisa alieitwa Boneka.


Vedi habari zote alizipata akiwa kwenye kituo cha internet ya kulipia.


Alijifuta machozi kisha akachukua mkoba wake na kwenda kupanda gari kuelekea kwa dada yake aliekuwa akiishi Tabata bima. Alihitaji kujua kinachoendelea kabla hajafika nyumbani kwao ambako aliamini kabisa watakuwa wanaomboleza kifo chake.


Licha ya jambo hilo kumpata ila hakutaka kulihusanisha na tukio aliloshuhudia usiku ndani ya meli. Aliamini pengine walichanganya taarifa tu na alijua kabisa ataliweka sawa akifika nyumbani kwa dada yake.


Vedi akamfikiria Mama yake.


Hakujua ni vipi Mama yake atakuwa amepagawa na taarifa za kifo chake bandia.


Wakati akifikiria hayo kuna kitu kilimjia kichwani pake.


Kwanini ndugu zake wamefanikiwa kuamini uvumi haraka kiasi kile kiasi wakaharakisha kufuata nguo zake kwake?.


Akajifuta chozi lililoanza kumwanguka.


Akarudia tena kuwaza kitu kile.


Akaguna!!


Inamaana kama wamefanikiwa kupata taarifa za kifo chake basi wataitwa hospitali kuutambua mwili ule na je baada ya kutambua ndio wakaamua kufuata mizigo yake kule kwake?.


Hata! .


Kuna namna ipo.

Haiwezekani iwe rahisi kiasi hicho.


Wakati akiwaza yote hayo alikuwa mbali na kuikumbuka simu yake ambayo iligoma kufanya kazi kabisa hadi wakati huo ambao alikuwa ndani ya gari kuelekea tabata kumuona dada yake.


Hatimae safari yake ilikomea kituo cha bima kisha akachepuka upande wa pili na kuelekea mashariki ambako aliishia kwenye vichochoro kadhaa kisha akakunja tena na kwenda hadi kwenye nyumba iliokuwa na geti jekundu.


Kikawaida Vedi amezoea kufika kwa dada yake na kusukuma kigeti kidogo na kuingia bila kugonga hodi,alijua mazoea ya dada yake ya kuacha geti lile wazi huku akisema hapendi kusumbuliwa na hodi nyingi.



Aliona geri la dada yake likiwa limeegeshwa nje huku mlangoni kukionekana viatu vyeusi alivyopenda kuvivaa dada yake.


Mara nyingi Vedi alipenda kujikaribisha mwenyewe kwa dada yake. Hata siku hii pia aliingia na kukaa kwenye sofa huku akimsikia dada yake akivuta kamasi chumbani kwake.


Hakujua kama analia ama anafanya kitu gani, yeye aliendelea kukaa.


Dakika kadhaa badae alisikia mtu akilia huku anaukaribia mlango wa kutokea chumbani.


Mara dada yake akatokeza akiwa amejifunga ushungi huku machozi yakimtiririka.


Ebana ee!


Tofauti na matarajio ya Vedi; dada yake aliruka kwa woga na kupamia mlango wa chumbani kwake huku akitoa kilio cha woga na licha ya kupamia mlango ila bado hakufanikiwa kuingia ndani hivyo akabaki akisota kwa matako chini na kizuizi kilibaki ni mlango.

.

Macho ya dada ake Vedi yalimtoka mithili ya mtu aliepigwa ngeta.


Vedi alishindwa hata kuongea, akasimama.


“Tafadhali usiniue… .usiniue!!”


Eeh!


Vedi alishangaa,akageuka kutazama nyuma yake pengine ataona mtu anaeambiwa maneno hayo.


Hakuona mtu, na hivyo iliashiria maneno yale yalimlenga yeye.


Ajabu hii!!.


“Dada unakichaa kwani!” Vedi aliuliza kwa mshangao.


Bado dada yake aliendelea kutoa macho huku akiomba asiuliwe n mara hii alizidi kutetemeka..


“Dada mi ni Vedi”


“No! Mdogo wangu kafariki na nimemuona mwenyewe hospitali,wewe sio Vedi” Dada wa Vedi aliongea huku akiwa amefumba macho kama alieona jini mbele yake.


Vedi akazidi kupagawa kwa tukio lile.


“Dada mi ni mzima kabisa nipo hapa” Alijitetea Vedi.


Bado Dada yake aliendelea kulia kama bwege pale chini alipodondokea.


Vedi akapiga hatua ili amfikie dada yake amshike.


Ohoo!


Dada yake akasota kwa nguvu na kuusukuma mlango kisha akaingia ndani kwake na kufunga haraka.


Vedi alijikuta akishindwa kuamua, ama alie ama acheke kwa tukio lile.


“Jamani mi nimekufa?” Alijiuliza bila kupata jibu na hapo akakumbuka kauli ya dada ake ya kuwa amemuona akiwa amekufa hospitalini na hapo ndipo alijua kwa nini walifuata nguo zake nyumbani kwake.


Haiwezekani bwana!


Alijisemea Vedi huku akipiga hatua kuelekea kwenye mlango ili atoke nje.


Mara akasita gafla!


Kuna wazo lilipita kichawani mwake.


“au kweli nimekufa, mana wanasemaga roho huwa zinahagaika kabla ya maziko” Alijisemea huku akijifinya kwa kucha zake ili asikie maumivu.


Maumivu aliyapata!


“Sijafa bwana!” Alisema huku akipiga hatua ndefu kuuendea mlango akiwa na lengo la kuelekea nyumbani kwao.


Alivuka kichochoro cha kwanza na kabla hajafikia kichochoro kingine alikutana na mtu mmoja aliekuwa amevaa koti mtelezo jeusi.


Mtu yule alikuwa amejikunja kuwasha sigara yake.


Vedi alimpita.


Mtu yule nae aligeuka na kuanza kumfuata Vedi.


Vedi hakujali kufuatwa mana Dar kila mtu mambo yake.


Aliendelea kusonga hadi alipofika barabarani na kungojea daladala.


Akiwa amesimama na mtu yule nae alisimama mbali na kituo huku akindelea kuvuta sigara yake.


Gari ilifika na Vedi akapanda huku mtu yule nae akigeuka na kutoka pale alipokuwa amesimama.


Kwao Vedi ilikuwa ni mabibo na alielekea huko.


****


Baada ya foleni za hapa na pale, hatimae alishushwa kwenye kituo alichohitaji na baada ya hapo akaanza kutembea hatua za kivivu kuelekea nyumbani kwao.


Akiwa amebakiza mita chache ili afike kwao; Vedi aliona umati wa watu ukiwa nje ya nyumba yao huku magari nayo yakiweka jamu kwenye barabara na baadhi ya majumba ya jirani na pale kwao.


Mwili ulimsisimka kuona amewekewa msiba ilihali yeye ni mzima wa afya.


Akaona kupita lango kuu la kuingilia kwao ni kuzua taharuki isio na sababu ni bora atumie geti la dharura ili aingie ndani na azungumze na ndugu zake na waweke sawa lile jambo.


Akachepuka kwa tahadhari ili watu wasimuone na akapita kichochoro kimoja na kujikuta akiwa nyuma ya nyumba yao.


Akasikia sauti za wamama zikitokea upande ule na alipotizama aliona moshi ukipepea angani kuashiria mapishi yalikuwa yakiendelea upande ule.


Akajitazama mavazi aliovaa.


Hayakuweza kumsitiri vyema asifahamike, yeye alivaa suruali na T-shirt ya zambalau na mkononi alibeba mkoba ambao haukuwa na mtandio isipokuwa ulikuwa na vipodozi vichache na taulo za kike kwa ajili ya dharura na pia kulikuwa kuna kitabu cha kumbukumbu alichokitoa ndani ya meli.



Akapiga moyo konde na kuusogelea mlango ule wa dharura.



Ilikuwa ni bahati mbaya kwake,kwani wakati anataka kusukuma geti ili aingie ni wakati huo ambao geti lilifunguliwa na mwanamke alietaka kumwaga maji machafu nje.


Yule mwanamke alipiga mweleka wa nguvu baada ya kukutana na Vedi kisha akarudi mbio huku akipiga kelele za woga na kitendo hicho kilifanya wamama wengine nao watake kujua kulikoni huko getini.


Aah!


Hawakuamini wanachokiona.


Walishuhudia Vedi akiwa amesimama getini kama sanamu la kariakoo.


Nani abaki sasa!


Kukaibuka kitimutimu cha ajabu ambapo kila mtu alikuwa anaokoa roho yake kwa kuona mzimu wa Vedi ambae wamethibitisha amefariki na taratibu za mazishi zinaendelea vije tena mtu aonekane mzima getini.


Wamama walipiga kelele na kukumbilia mbele kulikokuwa na watu wengine wakiwa wamekaa.


Wababa nao hawakuwa nyuma kuungana na wamama kutimka kutoka nje ya geti huku wale wanene wakilaani dhahama ile wasioijua, kelele za jini jini, zilisikika kila kona huku vilio vya woga vikitamalaki eneo zima la nyumba ya Mzee Mashimo.


Wanaume baadhi walisalia na kutaka kuona kilichotokea na wakaungana japo kiuoga kuelekea kule walikotokea wale wamama.


Wakaelekea huko na hakuna walichoshuhudia.


Walirejea na jibu moja ya kuwa hakuna jini wala zimwi waliloliona huko nyuma ya nyumba.


Akaitwa yule mama alieanzisha sekeseke lile.


Nae kwa uhakika kabisa alisema amemuona Vedi akiwa amesimama getini,hoja yake ikaungwa mkono na wamama wengine waliokuwa katika upishi kule nyuma, nao wakaeleza wazi ya kuwa walimshuhudia Vedi akiwa amesimama getini akiwatizama.


Watu wa imani wakaita mchungaji wa kanisa alilosali Vedi;akaombea pepo baya linaloanza kundama nyumba ile.


Ndugu wa karibu walioguswa na msiba ule baada ya tukio lile wakaanza kulia upya ni kama walitoneshwa vidonda vyao ambavyo havikupona.


Wengi walilia ila kuna mtu mmoja ambae hakuwa akilia kabisa na alikuwa kimya jambo ambalo lilifanya kuzuke minong’ono miongoni mwa waombolezaji waliokuwa wamekusanyika ndani ya nyumba kufariji wafiwa.


Alikuwa ni mama Msangu;Mama wa Vedi na Msangu binti yake mkubwa ambae alimkimbia Vedi kule Tabata alikokuwa akiishi.


Msangu alifika nyumbani kwao na kuelekea alipokuwa amekaa mama ake.


Kama wengine nae alianza kulia huku akimsimulia namna alivyotokewa na muzimu wa Vedi.


Mama yake akamtazama kwa machungu sana kisha akamwambia

“Sina hakika kama mwanangu kafariki, sijauona mwili wake ila nafsi yangu inakataa kabisa kukubaliana na suala hili”


Msangu alikaa kitako huku akifuta machozi na kumtazama mama yake na asielewe kabisa.


“Mama nimeitwa kuhakikisha maiti ile na pasi na shaka ni Vedi yule, namjua mdogo wangu” Alisema Msangu kwa sauti ndogo ili wengine wasisikie maongezi yao.


“Mwanangu wewe hujazaa, ila ukizaa utajua kwanini nayasema haya, yani mwanao hata akifinywa uko nae mbali mwili wako utakupa taarifa ya maumivu yake sembuse kifo?” Alisema mama Msangu.


“Yani hata nikijilazimisha kulia bado machozi hayatoki kabisa mwanangu hajafa” Alizidi kusisitiza mwanamke yule.


Punde akaingia mzee Mashimo na kumuita mkewe chumbani.


“Mke wangu umesikia yalitokea huko nje?” Alihoji Mzee Mashimo.


“Kwa hiyo na wewe unaafiki ya kuwa watu wameona muzimu?” Alihoji Mama msangu bila kujibu alichoulizwa.


“Unamaana gani kusema hivyo Mke wangu”


“Vedi hajafa, mwanangu yupo hai kabisa na hajafa eti”


Aya!!


Mzee Mashimo alikodoa macho kwa kutoamini anachosikia kutoka kwa mkewe.


“Mke wangu unaanza kuchanganyikiwa kwa kifo hiki ngoja niite mchungaji ak..”


“Nipo mzima kabisa wala sijaugua na naomba tusitishe msiba huu Baba Msangu”


“Mama Msangu unakufuru sasa!” Mzee Mashimo aliwaka kwa hasira na kisha akatoka ndani na kuelekea nje bila kutia neno zaidi na aliona kama mkewe ameanza kuchanganyikiwa na msiba ule.


Maongezi yao yalikuwa yanasikiwa vyema na mdada aliekuwa amamekaa karibu kabisa na chumba walichokuwamo wazee wale alikuwa ameshika simu janja yake akionekana kuperuzi ila alikuwa anatuma ujumbe mahali na ujumbe ule uliibua jambo lingine tena katika familia ile ya mzee Mashimo.


Jambo ambalo kamwe hawatakaa walisahau katika maisha yao yote.


****



Nb; Maoni yako ni muhimu kwa kila sehemu unayosoma ili kuboresha sehemu inayofuata.

Soma na shusha utabiri wako kwa kitakachofuata, kosoa sifia ili uandishi uwe mzuri zaidi.





Mzee Mashimo alikodoa macho kwa kutoamini anachosikia kutoka kwa mkewe.


“Mke wangu unaanza kuchanganyikiwa kwa kifo hiki ngoja niite mchungaji ak..”


“Nipo mzima kabisa wala sijaugua na naomba tusitishe msiba huu Baba Msangu”


“Mama Msangu unakufuru sasa!” Mzee Mashimo aliwaka kwa hasira na kisha akatoka ndani na kuelekea nje bila kutia neno zaidi na aliona kama mkewe ameanza kuchanganyikiwa na msiba ule.


Maongezi yao yalikuwa yanasikiwa vyema na mdada aliekuwa amamekaa karibu kabisa na chumba walichokuwamo wazee wale alikuwa ameshika simu janja yake akionekana kuperuzi ila alikuwa anatuma ujumbe mahali na ujumbe ule uliibua jambo lingine tena katika familia ile ya mzee Mashimo.


Jambo ambalo kamwe hawatakaa walisahau katika maisha yao yote.


****


Wakati hayo yakiendelea nyumbani kwa kina Vedi; Vedi yeye alikuwa ndani ya daladala akielekea hospitali ya mwananyamala kulikokuwa kumehifadhiwa mwili wa mtu aliesemekana ni yeye.


Nae alitaka kujihakikishia mwenyewe mtu huyo ambae dada yake alithibitisha ni yeye hadi kupelekea kuwekwa msiba nyumbani kwao.


Mwanzo hakuwa ameona uzito wa jambo lile,ila muda ulivyozidi kusogea aliona ni jambo ambalo halijatokea bahati mbaya ni kama kuna mipango hivi inayoendelea juu yake.


Mipango ndio; lakini ni nani hasa yupo nyuma yake na kwanini?. Je ni kile kitabu cha marehemu Banzi au ni maiti ya Banzi ama shida ni nini hasa!.


Hakukuwa na wa kumjibu swali lake hilo,na wala hakuona kama ni jambo linaloweza kupelelekea taarifa za kifo chake ingali yu hai.


Safari iliendelea huku mawazo lukuki yakikipitia kichwa chake na kumbukumbu ya jinsi alivyoshuhudia watu wakipamiana baada ya kumuona wakihisi ni mzimu wa Vedi na si Vedi mwenyewe.


“Inamaana hata mama nae anajua nimekufa?” Alijiuliza huku taswira la ya mama yake ikijirudia kichwani, aliona upendo wa mama yake kwake tangu yu ngali mdogo hadi ukubwa wake huo.


Alijifuta machozi kwa mgongo wa kiganja chake.


“Hata baba?” Alijiuliza tena na hapo akamkumbuka dada yake Msangu.


“Ooh shiit! Dada nae anahakikisha kaniona mochwari? I can’t believe this…” Alijiwazia kwa uchungu Vedi.


Kamasi na machozi yalitoka kwa pamoja na akatumia tena mgongo wa kiganja chake kujifuta.


Konda nae akatangaza kituo cha Mwananyamala hospitali na gari likasimama.


Wakashuka watu akiwemo na Vedi.


Vedi akavuka barabara na watu wengine waliokuwa wanaingia langoni mwa hospitali ile kwa shida mbali mbali.


Vedi akaingia na kuanza kupiga hatua kuelekea upande uliokuwa umeonyeshwa ni maalumu kwa wagonjwa mahututi.


Akavuka majengo kadhaa na kutafuta kibao kilichokuwa kimeandikwa “Mochwari”


Akakiona!


Ila wakati anapiga hatua ili akifuate na kufuata uelekeo kulipooneshwa;aliona mtu akiwa na watu wengine wawili na jumla akawa ameona watu watatu.


Wawili walikuwa wamevaa fulana nyeupe zenye rangi ya kufanana na suruali za jinzi zenye rangi tofauti.


Walionekana kuwa ni watu wenye mazoezi kwa jinsi miili yao ilivyoonekana imara.


Wawili wale hakuwafahamu kabisa na ndo mara ya kwanza kuwaona,ila mmoja kati yao alikuwa anamfahamu na alikuwa amevaa mavazi yale yale aliomuona nayo siku ya kwanza.


Koti jeusi na kichwani alivaa kofia ya pama na miwani usoni, viatu vyeusi vya buti na suruali ya Jinzi na mikononi aliziba viganja vyake kwa glavu nyeusi.


Alikuwa ni yule yule jamaa aliemuona ndani ya meli usiku wa ndoa ya rafiki yake kipenzi Nyamizi.


Ni yule yule bwana ambae alimuona akiingia na kutoka ndani ya kikontena kilichokuwa kwenye chumba cha ufundi ndani ya meli, alikuwa ni yule jamaa ambae walikutana mlangoni na kisha akamuona akiwa ukumbini akitafuta kitu ambacho yeye hakukijua.


Alikuwa ni yule mtu anaevaa miwani hata wakati wa giza nene.


Vedi alijikuta akihisi kama maji yanamwagika tumboni mwake kisha mwili ukaingiwa na ubaridi wa woga.


Hakujua ni kwa nini hali ile ilimkuta punde tu baada ya kumuona mtu yule.


Akajichanganya na watu wachache ambao walikuwa wanapishana huku na huko, ila macho yake bado yalikuwa kwa wale watu watatu ambao walikuwa wakijadili jambo huku wakiwa wameegemea nguzo ilioshika bati.


Vedi alijikuta anashawishika kutaka kujua watu wale walikuwa pale kwa dhumuni gani.


Akaangaza kidogo na kuona gari moja ikiwa imepaki sehemu ambayo yeye aliona itamfaa kujibanza na kushuhudia nyendo za watu wale.


Akajibanza!


Watu wale waliendelea kuongea na punde akatokea kijana mmoja aliekuwa amevaa mavazi ya kitabibu;koti jeupe na alizungusha shingoni kifaa cha kupima mienendo ya mapigo ya moyo.


Kijana yule akawasabahi watu wale na kisha akapeana nao mkono kila mmoja.


Walifahamiana bila shaka.


Walizungumza kidogo kisha tabibu yule akaanza kuondoka na wale watu nao walimfuata.


Vedi nae akafuata!


Walitembea kidogo na kuingia kwenye ofisi ambayo tofauti na ofisi zingine yenyewe iliandikwa jina la mwenye ofisi ile.

“Dr.Willy Masimba”.


Kwanini iliandikwa vile wakati ofisi zingine zote ziliandikwa majina ya vitengo wanavyohudumu matabibu wanaokuwa ndani yake?



Hilo hakujua.


Vedi akakumbuka kitu, akaingiza mkono kwenye mkoba wake na kutoa kalamu na kile kitabu alichokuwa amechukua ndani ya kontena na baadae aligundua kinamilikiwa na mtu alieitwa Banzi.


Akaandika jina la ofisi ile na pembeni yake akaandik pia jina lake ili yeyote atakaekuja kukutana na kitabu kile kitabu, basi aelewe kilitumiwa na watu wawili tofauti.


Akamalizia kwa kuandika tarehe ya siku hiyo.


Akasubiri kwa dakika ishirini zaidi ili aone watu wale kama watatoka, ila bado hakuwaona na wala hakuona dalili za kutoka kwao.


Akaelekea kule alikotaka kwenda mwanzo.


Akafuata uelekeo huo na hatimae alijikuta akiingia kwenye ofisi za wahifadhi maiti.


Akajitambulisha kwa jina bandia kisha akaomba kuutambua mwili wa rafiki yake alieitwa Vedi Mashimo.


Wahusika walimpa mtu wa kumpeleka kwenye hivyo vyumba vya kuhifadhia maiti.


Akapelekwa hadi kwenye jokofu lililokuwa limehifadhi maiti ya Vedi kulingana na maelezo yaliokuwa yamewekwa kwenye kitabu cha kumbukumbu.


Mlinzi akavuta.


Na hapo mlinzi akamkazia macho Vedi na kisha akarudisha macho kwenye jokofu, mara akaruka nyuma kwa nguvu huku akiachia ukelele wa woga.


Vedi nae akachungulia.


Lauhaula!!!


Alijiona yeye mwenyewe akiwa ametulia tuli ndani ya jokofu. Hata mavazi aliokuwa amevaa usiku wa sherehe ile, hadi mtindo wa nywele ulikuwa ni ule ule aliokuwa ameuweka siku ile.


Vedi akaruka nyuma huku vidole vyake vikiwa vimekimbilia kuziba mdomo ili asipige kelele.


Alijiona yeye mwenyewe akiwa ndani ya jokofu la kuhifadhia maiti.


Mlinzi nae alikuwa hoi akitetemeka.


Mara mlango ukasukumwa na wakaingia wale watu watatu aliowaona Vedi wakiwa wameongozana na Dr. Masimba.


Vedi akagwaya!!.




Vedi nae akachungulia.


Lauhaula!!!


Alijiona yeye mwenyewe akiwa ametulia tuli ndani ya jokofu. Hata mavazi aliokuwa amevaa usiku wa sherehe ile, hadi mtindo wa nywele ulikuwa ni ule ule aliokuwa ameuweka siku ile.


Vedi akaruka nyuma huku vidole vyake vikiwa vimekimbilia kuziba mdomo ili asipige kelele.


Alijiona yeye mwenyewe akiwa ndani ya jokofu la kuhifadhia maiti.


Mlinzi nae alikuwa hoi akitetemeka.


Mara mlango ukasukumwa na wakaingia wale watu watatu aliowaona Vedi wakiwa wameongozana na Dr. Masimba.


Vedi akagwaya!!.


Lilikuwa ni tukio ambalo liliwastua Vedi na mlinzi aliempeleka mule.


Vedi alibaki akiwa ameganda kama sanamu asijue cha kufanya.


Yule mtu ambae awali alimuona ndani ya meli;hakuhangaika kutazama aliowakuta mle ndani badala yake moja kwa moja alielekea kwenye jokofu lililokuwa wazi ambalo lilibeba maiti ya mtu aliefanana sawa na Vedi. Wale jamaa wengine nao ambao walikuwa sambamba na mtu yule, walielekea jokofu lile.


Dr. Masimba alitoa taarifa bila kuwazatazama aliowakuta mle na wengine pia hawakutazama na ni kama walifanya makusudi kabisa kufanya vile.


Vedi hakutaka kusubiri, haraka akajitosa mlangoni na kutoka kwa kasi na alipofika nje, haraka akaondoka eneo lile bila hata kutazama nyuma.


Wakati anatoka kabisa nje ya lango kuu la hospitali ile ya mwananyamala,kuna kitu kiliingia kichwani mwake.


“Kwanini nieondoke bila kuwafahamu watu hawa?” alijiuliza na kusimama kwenye eneo ambalo watu walikuwa wanaingia na kutoka kwa wingi.


Akatulia tu kama ambae hana kazi ya kufanya aendako.


Dakika ishirini badae, aliona wale watu wakitoka na lile gari lao walilokuwa wameegemea karibu na ofisi za Dr Masimba.


Lakini gari lile halikuwa gari la kawaida, bali lilikuwa ni gari ambalo lilikuwa maalumu kwa ajili ya kubebea maiti.


Na jeneza lilionekana, huku kukiwa kuna wanawake wawili wakiwa nyuma ya lile gari.


Walikotoka, hakuna aliejua.


Vedi alishindwa kuelewa kama ni maiti ya yule wanaefanana ama ni maiti ya nani iliochukuliwa.


Alihisi ni yake sababu walienda pale lilipokuwa jokofu lililobeba maiti yenye ufanano nae.


Na kama ni ile maiti; wao wanaipeleka wapi.


Mambo yale yalimchanganya Vedi; akaamua kutoka kwenye kundi la watu na kuongoza njia.


Kuna mahali alitaka kufika na kujisitiri kwa siku hiyo.


Alihitaji walau kuoga na kutoa uchovu, lakini pia alihitaji kupata mawazo kwa mtu aliemwamini na alihitaji mtu wa kumliwaza na wajue kitu wanachokifanya kwa majanga yale.


Akiwa anatembea kwa wasiwasi mwingi, akatoa simu yake baada ya kuona sehemu ya kusajili kadi za simu.


Alijongea pale na kusema shida yake kisha akatoa kitambulisho chake cha kupigia kura na walianza utaratibu wa kukamilisha usajili.


Haikuchukua dakika nyingi, tayari usajili ukawa umekamilika.


Akanunua vocha na kuondoka pale bila kuweka wala kuangalia kama simu yake imesoma usajili wake.


Akatembea taratibu hadi kona ya mwananyamala A kisha akasimamisha gari zilizokuwa zinaelekea mbagala.


Akapanda na hakukawia kupata nafasi ya kukaa.


Alipokwisha kukaa akaona ndio muda muafaka wa kuweka kadi kwenye simu yake na kisha aweke vocha na kupiga anakotaka kwenda ili ajue kama anaemhitaji yupo na kama hayupo basi afike nyumbani haraka mana yeye ndo anaelekea huko.


Ajabu tena!


Simu haikusoma na mtandao uliandika “emergency”.


Haiwezekani bwana!


Alijisemea kivivu, kisha akatoa kadi zote na kisha akazirejesha.


Hali ikawa ile ile.


Simu hazikusoma.


Akili yake ikamwambia, yawezekana tatizo sio la kadi za simu ila ni simu yenyewe.


Lakini simu ile haikuonekana kuwa ni bandia hadi ifungwe na mamlaka husika.


Hakuwa mgeni wa simu na alipoigusa gusa aliona kabisa itakuwa imefungwa.


“IPhone5 tangu lini zikawa na toleo bandia?” Vedi alijiuliza huku akirejesha simu ndani ya mkoba.


Alichoka hakika.

****

Gari ilifika kwenye kituo anachoshukia.


Akashuka na kuelekea mtaa alioukusuidia.


Tambo za miguu yake zilimfikisha kwenye nyumba ya uswahilini kidogo ila ilikuwa ni nyumba ya kisasa na ilikuwa na pande mbili.


Upande mmoja ulikuwa na milango mingi na kila mlango kulisikika sauti za muziki mkubwa huku nyimbo nyingi zikiwa ni za taarabu ya kuchambana.


Wanawake wa dar hao.


Alijisemea huku akipita na kuelekea upande wa pili ambako kulikuwa kuna nyumba iliojitegemea ikiwa na vyumba viwili na sebule.


Nyumba hii aliizoea na kila mara alifika pale.


Aliutazama mlango,alitabasamu baada ya kuona ukiwa wazi.


Akasukuma na kuingia.


Sebuleni hakukuwa na mtu ila alisikia muziki kwenye chumba alichokizoea kuliko hata sebule aliokuwapo wakati huo.


Akagonga mlango wa chumbani mara tatu kwa mtindo ambao alijua kabisa aliekuwamo angejua mgongaji ni nani.


Mlango ukafunguliwa taratibu na uso wa mtu ukatokea.


Vedi alitabasamu kwa unyonge.


Tabasamu halikujibiwa.


Ikaanza kumtia wasiwasi Vedi.


Mtu yule akaufungua mlango wote na kuingia na kumruhusu Vedi aingie ndani.


Vedi akaingia, kisha akaenda kukaa kitandani na kubaki akimtizama mwenyeji wake akiwa anavaa tai shingoni na kupamba mwili wake uliositiriwa na shati jeupe na suruali nyeusi na viatu vizuri vyeusi.


Vedi alibaki akimtizama bwana yule kwa mambo mawili.


Mosi alishangaa vile mtu yule alivyompokea bila kuonesha furaha yoyote usoni mwake, lakini pili alishangaa ni kwanini bwana yule hajastuka kwa ujio wake, au hajasikia kuhusu kifo chake? Au hajasikia kuhusu maiti inayofanana na yeye?


Sasa kama yote hajasikia;kwanini anamnunia tofauti na siku zote!


“Vedi naenda msibani” Hatimae bwana yule aliongea na kuvunja ukimya uliokuwa umeanza kutanda ndani ya chumba kile.


Vedi alistuka kidogo.


“Msiba wa nani tena” Alihoji.


Bwana yule akatabasamu kidogo kisha akamgeukia Vedi huku akifunga mkanda wa saa kwenye mkono wake wa kushoto.


“Ni kweli kwamba hujui kama umekufa na saa chache zijazo utazikwa?” Alizungumza yule bwana.


Heee!!


Vedi alishangaa.


Ilikuwa ni ngumu kumeza, mtu anazungumza kama vile ni jambo la kawaida kusema Vedi amekufa na wanazika na anaeambiwa maneno hayo ni Vedi mwenyewe.


Ajabu hii!!


Vedi alihisi hali ya ajabu ikiukumba mwili wake na wala hakuamini maneno yale makavu yanatoka kinywani mwa mchumba wake waliependana sana na walitarajia kufunga ndoa hivi karibuni.


“Juma; kwa hiyo na wewe unaamini nimekufa?” Alihoji Vedi huku akilengwa na machozi.


“Ndio,najua umekufa na umekufa na umeshakufa moyoni mwangu pia” Juma alijibu huku akitungua koti kwenye enga.


Vedi aliona ua likiwa kwenye mfuko wa kushoto wa koti lile, ilimanisha kweli Juma alikuwa anaenda kuzika na zile ni nguo za maombolezo.


“Jay, kwa hiyo hapa unaongea na nani; mzimu wa Vedi au picha ya Vedi?” Alihoji Vedi huku akisimama kumfuata Juma au Jay alivyopenda kumwita.


“Vedi; tangu juzi usiku nilikuua katika moyo wangu, hivyo hata wakati naambiwa umekufa, bado sikustuka japo roho yangu ilikataa kukubaliana na ukweli na hatimae umefika kama nilivyotarajia, lakini Vedi kwanini umeamua kuyafanya haya?” Jay aliuliza kwa sauti ya uchungu huku akijitahidi kuzuia machozi yasimtoke.


Vedi aliganda kama sanamu, ni kama hakumwelewa vizuri mahabuba wake. Maneno aliyoyazungumza yalimchanganya.


“Nimefanya nini tena mimi hadi unilaumu hivyo?” Vedi alihoji kwa upole.


“Usijifanye hujui Vedi; yani Vedi unaamua kutengeneza kifo chako ili uende kuishi ulaya na mwanaume mwingine? Haya kwa nini usingevunja uchumba wetu kisha umtambulishe huyo bwana kuliko kuigiza kifo ili mtokomee?” Jay alizungumza kwa hisia.


Ebanee!


Vedi aligwaya hakika,na hakujua ajieleze vipi katika jambo jipya kama lile,hakujua ni nani alievumisha tena habari hizo mbaya.


“Mbona sikuelewi wewe!” Vedi alifoka.


“Hunielewi sio!” Jay alisema huku akichukua simu yake kwenye meza ya kitanda na kutoa nywila kisha akapekua kidogo na kumwonesha Vedi.


Asalalee!!


Vedi alitoa macho kama komba mlevi,hakuamini anachokiona kabisa.


Kwenye simu aliona picha akiwa amepiga picha mtu.


Zilikuwa picha za kimahaba kwenye bustani nzuri ya kupendeza.


Lakini mtu aliepiga nae picha zile ndie aliezua utata katika akili ya Vedi.


Alikuwa ni yule mtu anaevaa miwani usiku na mchana; mtu ambae alionesha ukatili wa kutisha licha ya kuachia tabasamu lake la kukopa.

Mtu yule alikuwa ni yule bwana aliemuona kule melini na kisha hospitali ya mwananyamala.


Tofauti ilikuwa ni moja tu, ya kuwa wakati wanapiga picha zile mtu yule alikuwa amevaa suti maridhawa ila haikumoendeza kabisa na pia hakuwa amevaa miwani na kupelekea jicho lake moja kuonekana likiwa tofauti na jicho lingine.


Bila kificho jicho moja lilikuwa la bandia; jicho la kondoo.


“Aah!! Sio mimi bwana” Vedi alilalamika akiwa haamini anachokiona.


Yani aliona mtu sawa na yeye akiwa amepiga picha za kimahaba na yule bwana ambae alikuwa na ukatili ulioonekana wazi wazi usoni mwake.


“Sasa kama sio wewe ni nani aliepiga picha hizi” Alifoka Jay.


“Jay sio mimi eti”

Vedi alijitetea.


“Hizi nguo hukuvaa wewe wakati unapita kuniaga unaenda harusini?” Jay alifoka tena.


“Ni hizo ila zimefanana na wala huyo mtu simjui kabisa Jay” Vedi alizidi kujitetea.


“Na kweli humfahamu” Alisema Jay huku akipekua simu yake na akatoka tena picha nyingine ilioonesha maongezi kwa njia ya ujumbe mfupi kwa mtandao maarufu wa whatsapp.


Vedi akausoma tena ujumbe ule.


Ulikuwa ni ujumbe wa makubaliano baina yake yeye na mtu mwingine ambae alimwandika kwa jina la “Kingbae” na namba ilikuwa ni ya kwake.


Doh!!


Vedi alichanganyikiwa kwa kushindwa kuelewa yalivyo mambo yale.


Kweli namba ni yake na hata picha iliokuwa “profile” ni yake.


Aligwaya mwanamke yule ambae taratibu uzito wa mwili wake ulianza kupungua.


“Nadhani umeona mlichokubaliana na huyo bae wako, sina mwanamke anaeitwa Vedi ila nina mwanamke anaeitwa marehemu Vedi. Si ndivyo ulitaka?” Alimaliza kwa kuhoji bwana Juma.


“Tafadhali Jay naomba unisikilize mpenzi wangu” Alisema Vedi kwa kusihi.


“Huna cha kunambia, nawahi msibani nikamzike mpenzi wangu” Jay alisema na kuendea mlango.


“Nooo!! Ja….” Hakumalizia kauli yake alijikuta peke yake ndani ya chumba huku akisikia mlango ukifungwa kwa nguvu na kutoa kelele za malalamiko huku mfungaji akiufunga kwa hasira.


Vedi alijikuta peke yake chumbani na badala ya kujadili kilichomleta na kusaidiwa mawazo ila amejikuta akikutana na jambo jipya kabisa.


Hakujua habari zile za uongo ni nani aliempa mchumba wake na aliempa alilenga nini.


Hakika ulikuwa ni mtihani usiojibika.


***


Karibu kwa maoni yako tafadhali





Aligwaya mwanamke yule ambae taratibu uzito wa mwili wake ulianza kupungua.


“Nadhani umeona mlichokubaliana na huyo bae wako, sina mwanamke anaeitwa Vedi ila nina mwanamke anaeitwa marehemu Vedi. Si ndivyo ulitaka?” Alimaliza kwa kuhoji bwana Juma.


“Tafadhali Jay naomba unisikilize mpenzi wangu” Alisema Vedi kwa kusihi.


“Huna cha kunambia, nawahi msibani nikamzike mpenzi wangu” Jay alisema na kuendea mlango.


“Nooo!! Ja….” Hakumalizia kauli yake alijikuta peke yake ndani ya chumba huku akisikia mlango ukifungwa kwa nguvu na kutoa kelele za malalamiko huku mfungaji akiufunga kwa hasira.


Vedi alijikuta peke yake chumbani na badala ya kujadili kilichomleta na kusaidiwa mawazo ila amejikuta akikutana na jambo jipya kabisa.


Hakujua habari zile za uongo ni nani aliempa mchumba wake na aliempa alilenga nini.


Hakika ulikuwa ni mtihani usiojibika.


***


Vedi alitumia zaidi ya nusu saa akiwa amekaa chini huku akilia na alishindwa kabisa kuelewa ni kitu gani hasa kilikuwa kinaendelea katika siku mbili zile.


Alichoka kulia na alinyanyuka chini kisha akachukua maji ya kuoga na kuelekea bafuni kuoga na alipomaliza alibadili nguo na kuvaa nguo zake ambazo huwa anaziacha nyumbani kwa mchumba wake kama dharura tu.


Alivaa gauni refu na kwa ndani aliamua kuvaa suruali na kisha akajifunga mtandio na aliporidhika akataka kutoka na hapo akakumbuka kitu, akaamua kufungua droo ya kitanda na kutoa simu ndogo.


Alijua simu ile huwa inakuwa pale siku zote na ni baada ya kukosa matumizi kwa wahusika wake.


Akatoa laini mpya aliokuwa ameisajili na kuiweka, kisha akawasha simu na ikafanya kazi, akaweka vocha na kupiga namba alizochukua kwenye kitabu cha Banzi.


Alipiga simu na simu ikabaki ikiita bila kupokelewa na hatimae ikakata.


Akapiga tena!


Ikaita muda mrefu na hatimae ilipokelewa na mpokeaji alikaa kimya.


Vedi nae akakaa kimya kwanza.


Kutegeana kwao kuongea, hatimae aliepigiwa akauliza.


“Nani!?”


Vedi akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akajibu.


“Naitwa binti Mashimo”


“Ndio nikusaidie nini” Alihoji mpokeaji.


“Bila shaka naongea na Mamu?” Alihoji Vedi.


Upande wa pili ukaguna kisha kwa jaziba akasema.


“Wewe ni askari; mgambo ama bado mnanifuatilia?”


Zilikuwa ni sentesi mbili zenye maana mbili tofauti.


Aliuliza kama ni askari aliepiga, lakini pia aliuliza kama ni wanaomfuatilia.


Kina nani?


Vedi alikosa jibu katika maswali aliojiuliza.


“Mimi si yeyote kati yao Dada” Alijibu Vedi.


“Ila ni nani na wataka nini!?” Alifoka tena.


“Samahani dada naomba kukuona tafadhali!” Vedi alisema kwa kusihi.


Upande wa pili ukakaa kimya kwa sekunde kadhaa kisha ukasikika.


“Shida gani hadi tuonane na unahisi ni lazima kuonana?”


“Ni kuhusu Banzi Kela!” Vedi aliamua kutupa jiwe gizani na kweli lilimpata mtu.


Vedi alisikia mtu yule akipandisha na kushusha pumzi kwa haraka yani ni kama mtu alietoka usingizini na kubanwa na kichomi cha gafla.


“Unasema nini wewe!” Alihoji Mamu.


“Simu si salama dada naomba tuonane tafadhali” Alisihi Vedi.


Mamu aliongea kama ambae hataki watu wengine wasikie anachomwambia binti Mashimo.


“Sasa sikia, jitahidi ufike Hard Rock Café saa moja jioni, ukichelewa hautonikuta” Alisema Mamu na kukata simu.


Vedi akabaki akiiangalia ile simu kama vile haamini kama ni simu au ni mdoli.


Hard Rock Café!

Akalitamka tena lile jina.

Kama aliegutushwa na kitu akaudaka mkoba wake na kutoa kitabu cha kumbukumbu alichokichukua ndani ya meli.


Akakifunua kurasa kadhaa na hatimae akapata kile alichokitaka.


Ulikuwa ni ukurasa uliokuwa na jina lile la Hard Rock Café lakini pia kulikuwa kuna jina la mtu au jina la kitu chenye uhai; Jezebeli.


Vedi hajawahi kukutana na jina hilo la Jezebeli wala hakuwahi kusikia mtu akiitwa hilo jina na halikufanania kuwa la mtu, ila litakuwa linatumika kwa kiumbe kilichohai au kumaanisha jambo.


Jambo gani; Vedi hakujua kabisa bali akaamua kupitisha tu ya kuwa linatumika kwa kiumbe hai.


Sasa kwa nini limeandikwa kwenye kitabu hiki na lina husishwa na mgahawa ule maarufu ndani ya jiji la Dar?


Hakukuwa na wa kumjibu.


Vedi akatazama saa ukutani.


“Ooh my God!!” Vedi alilalama.


Ilikuwa ni saa tisa na nusu mchana na alijua ni huo muda ambao kulikuwa kuna mazishi ya mtu kama yeye.


“Inamaana kweli watu wote wanaamini nimekufa kweli? Lakini mbona…mh…


Vedi alimalizia kwa kuguna, kuna kitu kilipita kichwani mwake.


Alipoenda kwa dada yake Msangu alikutana na taharuki na mwishowe dada yake akamkimbia na halikadhalika alipofika nyumbani kwao watu walimkimbia, lakini kwa nini Juma yeye hakustuka wala kushangaa alipoingia ndani.


Inaweza kuwa ni kwa zile jumbe na picha? Hapana kuna kitu mimeona machoni mwa Jay; Jay namjua vyema kuna kitu…aah..kitu gani sasa?


Vedi alijiuliza bila kupata majibu.


Vedi aliwaza tena kwenda nyumbani kwao, ila aliogopa kuzua mtafaruku mkubwa zaidi, akachukua tena simu yake na kupiga simu ya baba yake baada ya kunakili namba alizokariri.


Simu iliita bila kupokelewa.


Akanakili namba za Mama yake; nazo alipiga hazikupokelewa.


Akaweka simu kwenye mkoba wake na kujilaza kitandani huku akikadiria muda wa kuamka ili asichelewe miadi yake na Mamu.


****


Juma ama Jay kama alivyoitwa na mchumba wake Vedi; baada ya kutoka ndani na kupigiza mlango, alielekea barabarani moja kwa moja kwa lengo la kupanda daladala awahi mazishini. Alikuwa akitembea huku akilia kiume, alilia bila kutoa machozi.


Kuna kitu kilikuwa kinamsumbua rohoni mwake na kitu kile kilizidi hasa baada ya kumuona Vedi.


Alisimama njiani huku akijishauri ni kama arudi nyumbani kwake azungumze na Vedi ama aende msibani atoe taarifa za kuwepo Vedi ama afanye nini!


Alikumbuka sauti ya Dr Masimba.


Alitamani siku zirudi nyuma na aone kama ni ndoto tu ya mambo yale mabaya anayoyashiriki bila ridhaa yake.


Akajiuliza ni kwanini alienda kupima kwenye hospitali binafsi ya Dr Masimba ilioko hapo mbagala?


Jay alilaani kitendo alichofanyiwa ndani ya hospitali ile.


Usiku wa ndoa ya rafiki yao Nyamizi yeye hakuhudhuria sababu alikuwa anajihisi ni mgonjwa na aliona bora aende Vedi peke yake,na kulipokuchwa akaamkia kwenye hospitali binafsi ya Dr Masimba iliokuwa Mbagala rangi tatu karibu na kituo cha mabasi; hospitali ambayo ilikuwa ni maarufu sana kwa huduma zake za uhakika na kujali wateja.


Akapanda bodaboda na ilimfikisha hadi hapo hospitali na baada ya taratibu zote kukamilika alielelekea chumba cha maabara ili akachukuliwe vipimo.


Akiwa kule maabara, taratibu zote zilifuatwa na akachukuliwa vipimo na kijana mmoja ambae baada ya kumchukua kiasi kidogo cha damu alielekea chumba maalumu kwa ajili ya upimaji wa sampo ile ya damu.


Kijana yule hakukawia sana, akarejea na kumuomba Jay aelekee chumba namba kumi kilichokua kushoto mwa maabara ile.


Alijua anaenda kupata majibu yake ila alienda kikutana na zaidi ya majibu ambayo yanamwendesha katika maisha yake! Majibu ambayo yalibadili maisha yake kabisa.


Akiwa hana wasiwasi aliingia hadi kwenye chumba kile na alikutana na Dr Masimba mwenyewe na akiwa na watu wengine watatu ambao nyuso zao hazikuonekana kuwa na usalama.


Alipoingia mmoja wa watu wale akaruka na kuukomea mlango kwa ndani.


Jambo lile lilimpa wasiwasi Jay; akataka kufungua ili atoke, ila kasi yake haikuwa sawa na kasi ya mtu yule aliekuwa ameufunga mlango.


Akawa kumzuia!


“Vipi bwana mdogo, haujitaji majibu ya vipimo vyako?” Alihoji mtu mwingine ambae alikuwa amevaa miwani na kofia ya Pama huku akiwa amevaa na koti licha ya hali ya hewa kuonekana ni joto na jua kali.


“Sasa majibu ya vipimo ndo hutolewa hivi?” Alihoji Jay.


“Relax bwana mdogo, taratibu kwanza!!” Alisema Dr Masimba ambae Jay alimfahamu kwa kuwa alikuwa akifika pale mara kwa mara kuangalia afya yake.


“Majibu yaonenesha unaumwa maralia kali sana” Alisema Dr.


Jay baada ya kusikia vile akasimama na kuaga.


“Mbona unaharaka sana komredi, hatujamaliza bado” Alisema yule mtu ambae alikuwa amevaa kofia na miwani usoni.


“Mbali na majibu yako, ila na sisi tuna letu jambo” Alisema jamaa alievaa miwani na kofia ya pama kisha akaendelea.


“Mkeo Vedi; ametuibia, ila kabla hatujamfikia inabidi uwe daraja kwanza”


“Kawaibia nini na mmejuaje mi ndo mumewe?” Aliuliza Jay huku akitetemeka.


“Kwa sasa hatutakwambia alichotuibia, ila unachotakiwa kufanya ni kuwa upande wetu tu, endapo alivhokiiba kikiwa na madhara kwetu” Alisema yule bwana.


“Sasa nitakubali vipi kuwa nanyi ikiwa sijui kimemtokea nini na nyinyi ni kina nani?” Alisema Jay.


Na hapo yule mtu alicheka kidogo huku wengine wakiwa kimya muda wote kama hawamo mle ndani.


“Kwa sasa hupaswi kujua ila hadi tujiridhishe upo upande wetu, na ili uwe upande watu inabidi tukuongezee ugonjwa mwingine” Alisema yule bwana.


Baada ya kusema vile Jay alishangaa akishikwa kwa nguvu na zile njemba mbili ziliokuwa mle chumbani kisha yule aliekuwa amevaa miwani alimfunga na karatasi yenye gundi mdomoni ili asipige kelele,kisha Dr Masimba alisimama na kuchukua sindano iliokuwa kenywe mkebe na ilikuwa na dawa kwenye bomba lake.


Akamfuata Jay ambae alikuwa ameshikwa vyema licha ya kujitikisa kwa uoga bila mafanikio.


Sindano ilizama kwenye nyama na kisha ikasukumwa dawa yote iliokuwa mle na Jay alibaki akiona kizunguzungu huku macho yake yakishindwa kuona vyema, alitamani kuongea ila alishindwa, alitamani kulia napo alishindwa, akajibweteka kwenye kiti baada ya kuachiwa






Baada ya kusema vile Jay alishangaa akishikwa kwa nguvu na zile njemba mbili ziliokuwa mle chumbani kisha yule aliekuwa amevaa miwani alimfunga na karatasi yenye gundi mdomoni ili asipige kelele,kisha Dr Masimba alisimama na kuchukua sindano iliokuwa kenywe mkebe na ilikuwa na dawa kwenye bomba lake.


Akamfuata Jay ambae alikuwa ameshikwa vyema licha ya kujitikisa kwa uoga bila mafanikio.


Sindano ilizama kwenye nyama na kisha ikasukumwa dawa yote iliokuwa mle na Jay alibaki akiona kizunguzungu huku macho yake yakishindwa kuona vyema, alitamani kuongea ila alishindwa, alitamani kulia napo alishindwa, akajibweteka kwenye kiti baada ya kuachiwa.


Alihisi kichwa kikiwa kizito na mwili mzima ukipitiwa na ubaridi wa ajabu huku maungio ya mifupa yake ikizizima kwa ubaridi ule, ni kama akili yake iliganda mana hakusikia kitu wala kuona kitu,alikaa kama sanamu la ibada.


Hakujua amekaa koma muda gani, ila alikuja kupata fahamu na kujikuta akiwa amelala kwenye kitanda cha wagonjwa na mwili wake ukiwa imara ni kama hakujatokea kitu muda mfupi uliopita.


Akainuka kitandani na kukutana na sura za watu wawili wakiwa wamemsimamia.


Walikuwa ni wale wawili wenye kuvaa nguo za kufanana na Dr Masimba pamoja na yule bwana anaevaa miwani hawakuwemo.


Akabaki akiwatizama.


“Umeamka na unajisikia vizuri bila shaka” Alihoji jamaa mmoja.


Jay hakujibu.


“Sasa sikiliza,sindano uliochomwa imekuondolea maralia yako ila imekupa ugonjwa wa kansa ya mifupa” Alisema bwana mwingine tena.


Jay alisimama kwa jaziba na kumvaa jamaa yule, ila alitulizwa chini kwa jebu moja na akabaki akilia kwa uchungu na kujibweteka kitandani kama zoba.


“Aliekuponza ni Vedi; ila usijali, kuna tiba yake na tutakupatia hadi ukifanikisha yale tunayoyataka na kikubwa zaidi uoneshe kufunga mdomo na ukijaribu kusema lolote, tumekuwekea kifaa kitakachokuwa kinatupa taarifa ya mazungumzo yako popote” Alisema jamaa mwingine aliempiga jebu Juma.


Jay aliiunua uso na kuwatazama watu wale na alipojaribu kusema kitu,alijikuta anashindwa kusema na kubaki akilia kwa uchungu.


“Umepandikwa kirusi Flora na kinakula chembe hai nyekundu na ndani ya siku kumi usipopata tiba unakufa, hivyo ni muhimu ufanye tunachokuagiza ili uokoe maisha yako” Alisema tena yule jamaa.


Wakiwa bado wanazungumza mara akaingia yule mtu anaependa kuvaa koti na miwani wakati wote.


“Nadhani mwacheni aende, na maelekezo tutampa kwenye simu” Yule bwana alizungumza na kisha akamgeukia Jay.


“Bwana mdogo;ili usaidike inahitajika utimize tunayoyahitaji na hivi sasa maisha yako yapo kwetu, usiripoti kituo chochote cha polisi na usifanye ujinga wowote ule, nenda kapumzike ujumbe wako utaukuta kwenye simu na endapo Vedi akitokea fanya kile tutakachoakuagiza” Alisema tena bwana yule na punde akaingia mtu mwingine na kumwamuru Jay asimame waondoke pale ndani.


Jay hakuwa mbishi baada ya kugundua yupo kwenye mikono isio salama.


Lakini alijiuliza swali moja!


Kwanini wamtumie yeye kwenye matatizo yao na Vedi?; Vedi kachukua nini muhimu kwa watu hawa?.

Hakupata jibu hata kidogo na alitoka akiwa hana amani ya mwili wake na alihitaji kukaa na kutafakari kuhusu jambo lile.


Hakika alipagawa.


Baada ya kutoka kwenye kile chumba, walibaki watu watatu, ambao ni yule bwana mvaa kofia; koti na miwani pamoja na wale vijana ambao walipenda kuvaa nguo za kufanana wakati wote.


“Sasa Cholo unaamini hii itasaidia?” Alihoji kijana mmoja huku akimtizama yule jamaa anaependa kuvaa kofia na miwani ambae ndie Cholo.


“Panga; tukisema tumuue yule binti hivi sasa kiukwelii, itatupa shida, hatujui hadi hapo kawasiliana na nani baada yakuiona ile maiti, kikubwa ni kufunga mianya yote kisha tutajua cha kumfanya tukiwa na uhakika wa zilipo taarifa za yale alioyaona,kama isingekuwa kadi ya harusi aliodondosha mule na kisha kuchukua kile kitabu nilichokisahau pale, tusingejua lolote kuhusu mtu alieona ile maiti ya Baharia” Cholo alimweleza Panga.


Panga alitikisa mabega na kumwangalia mwenzie.


“Gomba unaonaje hizi mbinu”Cholo alimhoji Muki ambae alikuwa amekaa kimya muda wote.


“Tutazame mienendo yake, akileta utata ile mbinu yetu ya siku zote itamfaa bila shaka” Gomba alijibu na wote wakatabasamu mule ndani na kutoka nje wakikiacha chumba kikiwa kipweke kabisa.


**


Jay alijipiga kichwani baada mawazo yale kumpitia kwa kasi na kubaki akiwa amesimama barabarani bila kujua ametumia muda gani kuwaza yaliompata hadi kupelekea kumkana mpenzi wake wakati huu aliohitaji msaada wake.


Akajitazama na kuona alivyopendeza.


“Eti naenda kumzika Vedi niliemwacha ndani kwangu” Alijiwazia kwa uchungu huku akipiga hatua na kuelekea barabara kuu ili apate uber.


Lakini wale jamaa ni kina nani hasa na Vedi kawafanya nini?


Alijuliza tena huku akishindwa kuyazuia machozi yalioanza kumtoka.


Hakufika barabarani, mara mbele yake ikasimama gari nyeusi na vioo vikashushwa.


Walikuwa ni Gomba aliekuwa dereva na Panga aliekuwa nyuma amekaa.


“Bila shaka unahitaji msaada wa usafiri kwenda msibani!” Alisema Panga.


Jay alibaki akitetemeka baada ya kuwaona wale jamaa ambao ndani ya siku mbili waligeuka kuwa waongoza maisha yake.


“Njoo twende na tafadhali kuwa mtu wa majonzi, wewe ni mfiwa ujue” Alisema Gomba.


Jay hakuwa na namna akafungua mlango na kuingia, na hapo akagundua kulikuwa kuna mtu wa tatu na alikuwa ni Cholo.


“Tunaenda msibani; ila jitahidi sana usioneshe tofauti kama unavyofanya hivi hapo njiani bwana mdogo” Cholo aliasa.


“Lakini kwa nini mnatufanyia yote haya?” Alihoji Jay.


“Kwa sasa wewe bado mdogo ila ukikuwa utajua ndevu za wazee hazichezewi na nzi” Alisema Cholo kwa fumbo ambalo linahitaji akili kulifumbua.


Safari yao ilikuwa ni ya kimya kingi kuliko maneno na baada ya foleni za hapa na pale, hatimae walifika.


“Gomba utaongozana na huyu bwana mdogo” Aliagiza Cholo.


“Kwanini msiniache peke yangu aisee” Jay alisema huku akianza kushuka.


Cholo alicheka kidogo.


“Hadi hapo tushakuona una roho ndogo, hivyo hatuwezi kukuamini hata kidogo.” Cholo alisema huku akijiweka sawa bila kuonesha dalili ya kushuka.


Gomba alishuka na waliongozana na Jay kuelekea kwenye nyumba ya Mzee Mashimo.


“Hakikisha mimi na wewe tunakuwa marafiki na mtu asijue tofauti zetu” Gomba alimuonya Jay huku wakidi kusonga.


Walifika hadi getini kulipokuwa na watu wawili kwa ajili ya kuongoza wageni wanaofika na mmoja kati yao alimfahamu Jay na hivyo alimsindikiza hadi ndani na kisha yeye kurudi.


“Kwa hiyo hadi ndani unataka kuingia?” Jay alimgeukia Gomba.


“Ulipo nipo bwana mdogo na usisahau mimi ni rafiki yako” Gomba alijibu huku akitabasamu kama kwamba ni jambo la kawaida tu analozungumzia.


Waliingia ndani na kuona jeneza likiwa limewekwa sebuleni huku wamama wakiwa wamelizunguka na nyuso za majonzi.


Msangu ambae ni dada yake Vedi alisimama baada ya kumuona shemeji yake akiwa ameongozana na mtu mwingine ambae hakumfahamu kabisa.


Msangu aliangusha chozi baada ya kumuona shemeji yake.


Jay nae aliangusha chozi, ila chozi lake lilikuwa lina mengi ndani yake.


Gomba alikuwa akiangaza na alimuona mwanamke mmoja akiwa amekaa sambamba na waombolezaji, mwanamke yule alimpa ishara fulani na Gomba alielewa mambo hayako sawa pale.


Msangu alimshika mkono Jay na akamwongoza kuelekea chumbani kwa wazazi wake na Gomba nae akafuata.


“Tafadhali, kuna muda inabidi utumie akili kuliko nguvu” Jay alimkoromea Gomba kwa sauti ya chini ila iliojaa jaziba. Gomba akasimama na kutafuta sehemu na kukaa pamoja na waombolezaji wengine.


Jay aliingizwa kule chumbani na kumkuta mama yake Vedi akiwa mkavu usoni huku akiwa hana hata chembe ya chozi.


Mama msangu alisimama baada ya kumuona Jay.


“Na wewe unaamini mkeo kafa kweli?” Mama msangu alihoji na Jay alishindwa cha kujibu.


Mama Msangu alianza kuongea kwa sauti huku akionekana dhahiri kutokukubaliana na suala lile la kifo cha Vedi hata pale ambapo Jay alitaka kutetea hoja ya kifo kile Mama yule alikataa kata kata na hatimae alimshika mkono Jay.


“Mwanangu twende nikuoneshe kitu; Mkeo hakuwa na mwanya kabisa licha ya kujitahidi kufanana ila nimemgusa midomo yake japo watu wamenizuia” Alisema Mama msangu huku akimshika akitembea kuelekea sebuleni.


Na walipotoka watu wakawatazama, Mama yule hakujali na akaelekea lilipo jeneza.


Gomba aliona kitendo kile na tayari alishaambiwa na yule mwanamke aliekuwa pale msibani kinachoendelea, haraka akasimama na kushika mfukoni na akapiga hatua ndefu hadi akawafikia na kwa kuwa Mama msangu alikuwa ameshika mfuniko wa jeneza;wamama wengine nao wakaanza kusogea kumkataza mana alishavuruga huko nyuma na hawakutaka kabisa aliguse jeneza lile,lakini kasi ya Gomba ilikuwa ni kubwa na kwa wepesi akamshika mkono Mama Msangu na Mama Msangu hakutaka kuzuiwa hivyo akautoa mkono ule na kutaka kuufuangua mfuniko wa jeneza.


Mara akasita na kujishika kichwa na kuanguka chini.


Haikupita dakika moja akainuka, ila aliinuka kwa mtindo wa ajabu, aliinuka kwa kujikuna huku akicheka na kuunguruma kama simba na kuongea maneno yasiyoeleweka.


Watu walijawa na taharuki na vilio vilianza upya.


Jay aliona tukio lile ila hakujua Gomba kwa nini alimshika mkono mama yake huyo.


“Wewe bwege umemfanya nini huyu mama?” Jay alifoka kwa jaziba licha ya kujizuia sauti isitoke.


Gomba akainua mabega kukataa.


Jay akamshika ukosi wa shati.


Ukaanza mvutano na mparanganyiko ndani ya nyumba ya mzee mashimo.


Mama Msangu anajikuna na kuunguruma hovyo huku Jay akiwa anavutana na rafiki yake wa bandia,watu nao wamebaha kwa yanayoendelea.


Jay alikuwa amegeuka mbogo alijua kabisa kuna kitu kimefanywa na Gomba kwa Mama msangu.


Yule mwanamke aliekuwa miongoni mwa waombolezaji akasogea hadi nyuma ya Jay na kama anaetaka kujifunia kanga aliojitanda akampiga pigo moja la kisogo bila mtu kugundua kilichotokea na akajitandua kanga na kujitanda tena.


Jay akalegea na kwenda chini kama gunia la chawa wa jaani.


Gomba akapaza sauti ya hamaniko huku akiwa amemshika Jay na watu walizidi kuchanganyikiwa zaidi.


Gomba akaomba kupiga simu ya dharura ili watu wale wawahishwe hospitali; Wazo lake liliungwa na wengi waliokuwapo pale ndani na akapiga simu.


***


Dakika thelathini zilipita na gari la wagonjwa lilifika pale na haraka haraka wauguzi wa huduma ya kwanza walishuka na kuwabeba Jay na Mama Msangu na Msangu na Baba yake walikataliwa kuingia ndani ya gari lile kwa kisingizio ni dogo halitoshi msindikizaji.


Mazishi yaliingiliwa na taharuki, ratiba ikabadiliswa hadi ijulikane mstakabali wa afya za walengwa wa marehemu.


Ajabu nyingine ni kuwa; taharuki ilibeba mawazo ya watu kiasi hakuna aliekumbuka kufuatilia gari lile linaelekea hospitali gani.


Watu waliendelea na malumbano yasioyo na tija.


Lakini wangejua yanayoenda kuwapata ndugu zao, hakika wasingebishania ratiba ya mazishi ya maiti bandia.


**


Weka komenti yako ili iwafikie watu wengi zaidi.






Mazishi yaliingiliwa na taharuki, ratiba ikabadiliswa hadi ijulikane mstakabali wa afya za walengwa wa marehemu.


Ajabu nyingine ni kuwa; taharuki ilibeba mawazo ya watu kiasi hakuna aliekumbuka kufuatilia gari lile linaelekea hospitali gani.


Watu waliendelea na malumbano yasioyo na tija.


Lakini wangejua yanayoenda kuwapata ndugu zao, hakika wasingebishania ratiba ya mazishi ya maiti bandia.


***


Gari ile ya wagonjwa iliishia kwenye nyumba ya kifahari na kisha wakashuka watu wawili waliojifanya kuwa ni wauguzi na baada ya kushuka mmoja akaelekea ndani na punde akarudi akiwa na jamaa wengine wawili waliokuwa wameshiba miili yao na maumbo makubwa yalionasibisha wingi wa mlo wao.


Watu wale wakawashusha na kuwaingiza ndani kisha wakawekwa kwenye chumba cha pamoja na punde mtu mmoja akachukua sindano na kumchoma Jay na kisha alimchoma na Mama Msangu.


Hazikupita dakika tano wote wawili walizinduka na kushangaa wakiwa kwenye chumba kimoja na wamesimamiwa na watu wengine watano ambao walikuwa kimya muda wote.


“Juma mwanangu kwani imekuwaje tena!?” Mama Msangu alihoji kwa woga baada ya kuonekana hayaelewi mazingira waliopo.


Juma akavuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akamjibu.


“Sina la kusema ila nadhani tupo kwenye mikono mibaya”.


Akivyokwisha kusema hivyo haikuchukua hata sekunde akajikuta akinyayuliwa kwa nguvu na kupigwa kichwa matata na kisha akaonywa asirudie kusema hovyo kabla hajaruhusiwa.


Akiwa bado anaugulia maumivu akabebwa kwa nguvu na kutolewa kwenye chumba kile na hata Mama Msangu alipojaribu kutetea aliishia kupigwa makofi mazito yaliomwacha akiwa hajui cha kufanya.


Baada ya kutolewa kwenye kile chumba; Jay alipelekwa kwenye gari ambalo lilikuwa nje ya uzio wa nyumba ile waliokuwamo.


Alikutana na Gomba akiwa na mwanamke ndani ya gari.


“Panda tukurejeshe nyumbani kwako!!” Gomba alisema huku akimtizama Jay.


Jay alipanda na gari ikaondolewa.


“Yani sikuwahi kudhani kama kuna mtu mjinga kama wewe aisee!!” Gomba alifoka huku akiwa makini na usukani wa gari.


Jay alikaa kimya.


“Huna kifua kabisa bwana mdogo na utakuwa tatizo badae” Gomba alizidi kufoka.


Wakati Gomba akiendelea kufoka kwenye gari; ni wakati huo ambao Mama Msangu alikuwa ameshikwa kwa nguvu na hakujua wale vijana waliokuwa wamemzunguka walitaka kumfanya nini.


Walimbana vizuri na hakuweza kufurukuta kabisa na ndipo kijana mmoja alichukua kamera na kuiwasha kisha mmoja wa vijana wale akavua nguo zake zote na kusalia na mtupu, kijana mwingine nae alivua nguo zake zote na kisha wakaenda kumvamia Mama Msangu na kumvua nguo zake zote nae akabaki mtupu kama alivyozaliwa.


Mama Msangu alijionea aibu kuwa vile mbele ya vijana wadogo rika sawa na wanae, alilia kwa uchungu mana akili yake ilimwambia ni kitu gani hasa kilikuwa kinafuata kwake wakati huo.


Kwa uchungu na mapigo ya moyo yakaenda mbio kuliko kawaida na taratibu akalegea na kupoteza fahamu.


“Ooh shit!! Hatuwezi kupiga picha akiwa hivi labda tungoje azinduke” Alisema kijana aliekuwa na kamera na wale vijana waliokuwa wamevua nguo wakavaa nguo zao na kisha mwenye kamera alianza kupiga picha mwili wa Mama Msangu uliolala chini bila fahamu.


Aliporidhika akaomba avalishwe nguo zake na kisha wakamchoma sindano nyingine tena kisha wakakubaliana apelekwe Muhimbili kwenye wodi za watu wenye matatizo ya akili, mana waliamini kabisa akiamka hataweza kuwa kwenye utimamu wake tena kulingana na dawa aliochomwa.


Alikuwa ni kichaa mtarajiwa huku picha zake za uchi alizopigwa akiwa amelala zikihifadhiwa kwa kazi waliojua vijana wale.



Vedi alifika hadi kwenye mkahawa wa Hard Rock na kutafuta sehemu nzuri na kukaa kisha akaagiza maji ya baridi na kunywa huku akingojea dakika chache ili kufika saa moja ya usiku, muda ambao walikubaliana na Mamu kukutana hapo.


Akiwa ametulia mara simu yake ikaita.


Namba zilikuwa ni za Mamu.


Akapokea.


“Upo wapi wewe” Mamu aliuliza kwa mashaka kidogo.


“Nipo mashariki mwa mgahawa huu” Vedi alijibu.


Simu ikakatwa.


Akiwa bado anashangaa kukatwa kwa simu, mara mbele yake alisimama mwanamke mzuri wa sura na umbo la kuvutia, ila hakuonekana kuwa na furaha na kila mara alikuwa akiangaza huku na huko kama anaehofia jambo.


“Wewe ndie binti Mashimo?” Mamu alihoji huku akimakinika kumtazama Vedi.


Vedi alitikisa kichwa kukubali.


Mamu alikaa kwenye kiti kilichokuwa kwenye meza aliokuwa anatumia Vedi.


“Wewe ulipata wapi namba yangu” Mamu alihoji huku akimtizama Vedi usoni.


“Samahani kama nitakuwa nimekukwaza ila nimeipata sehemu ambayo ilinishawishi nikupigie” Vedi alijibu huku akikwepa kujibu mahali alikoipata hiyo namba.


“Sawa! Na ulijuaje inanihusu mimi na Banzi” Aliuliza Mamu kwa sauti ya chini kidogo.


“Niliipata kwenye vitu vya Banzi na pale nilikuwa nabahatisha tu baada ya kuona kuna ujumbe unakuhusu” Vedi alijibu.


“Vitu gani! Begi lake ama simu zake?” Mamu alihoji kwa papara.


“Hapana,sio vyote hivyo” Alijibu Vedi.


“Sasa vitu gani labda!?”


“Kitabu!!” Vedi alijibu.


“Ooh shit!! Hilo ni kosa litakalokugarimu binti” Mamu alisema kwa wasi wasi huku akitizama pande zote kwa makini.


Vedi alitumbua macho kwa kutokuelewa ni vipi hicho kitabu kiwe kina matatizo upande wake.


“Hicho kitabu kidogo kimepeleka wengi kuzimu na yawezekana hata mume wangu nae ameshafariki kwa sababu ya hicho kitu!” Mamu alisema kwa huzuni huku dhahiri akionekana chozi linamtoka.


Eh makubwa,inamaana hajui kama mume wake ameshafariki? Na hicho kitabu kina shida gani hadi kichukue uhai wa watu kiasi hicho hadi Mamu aogope na Mamu anajua nini kuhusu mkasa wa mumewe?


Yalikuwa ni maswali yaliopita kwa kasi ndani ya kichwa cha Vedi.


“Kwani kuna nini katika mambo haya? Alihoji Vedi.


“Trust me kama wanajua una hiko kitabu, watakuhangaisha sana watu wale na kama uliwahi kuonana na Banzi; basi wewe ni sawa na maiti inayotembea.”


Vedi alitumbua macho kwa maneno yale.


“Banzi nilimuonya hakusikia, ona sasa…..anyway hakikisha unaubeba msalaba wa roho zote zilizotoka kwa ajili ya mambo yaliomo humo na pia pigana kwa ajili yetu sote na aamini utavuka majaribu yaliotushinda sisi” Mamu alisema na kusimama ili aondoke; Vedi alimshika mkono.


“Dada unaniachia mafumbo bila utatuzi na peke yangu siwezi, pigana juu ya mumeo tafadhali. Mumeo ameuwawa” Vedi alisema kwa hisia.


Mamu akigeuka na kujibweteka kwenye kiti kama mgonjwa, ilikuwa ni ngumu kukubaliana na hiyo hali ya kusikia kifo cha mumewe kwenye masikio yake, alifuta machozi yalioanza kumtiririka kwa fujo.


“Hapa si pahali salama na wamejaa Jezebeli wenye masikio ya popo,tafadhali fanya niliokwambia, nilipambana kuokoa uhai wake ila nimeshindwa, nawe tumia njia zako kutafuta uhuru wako” Mamu alisema huku akijifuta machozi.


Vedi kuna kitu alikitilia maanani kwenye maelezo ya Mamu.


Neno Jezebeli!


Akajiuliza; Jezebeli ni nini na kama ni watu ni kina nani na kwenye kile kitabu cha kumbukumbu alichonacho Jezebeli alitajwa na alitajwa kupatikana kwenye hilo eneo la Hard Rock Café.


“Jezebeli ni kina nani au ni nani?” Vedi alihoji.


Mamu aliangaza tu kisha akaelekeza macho yake upande wa pili kulikokuwa na wahudumu wa mgahawa ule; Vedi nae alitazama kule ila aliishia kuona wahudumu wakipishana huku na huko.


Hakujua iliashiria nini na zaidi alichogundua ni kuwa miongoni mwa wahudumu wale baadhi hawakuwa wanaume wa kawaida kwa kuwaona tu, walikuwa ni wanaume waliozidiwa na homoni nyingi za kike na kujikuta wakifanya matendo kama ya wanawake.


Wanaume jina tu.


Vedi akarudisha macho kwa Mamu.


“Sijaelewa lolote!!” Vedi alisisitiza


Mamu hakumjibu, akasimama na kuchukua mkoba wake na kuondoka na kumwacha Vedi akiwa aezubaa na chupa ya maji mkononi.


“Hapa kuna kitu sio bure” Vedi alijisemea huku nae akisimama na kutoka ndani ya mgahawa ule.


Alihitaji kurejea nyumbani kwa Jay ili apumzike na asubiri siku ya kesho itakavyokuwa.



Jay alifikishwa nyumbani na Gomba kisha Gomba yeye akapanda gari na kuondoka bila kusema jambo lingine lolote.


Jay alipiga hatua chache na kufikia lango la nyumba yake, akafungua na kuingia ndani.


Nyumba nzima ilikuwa ni kiza kizito na hakuhofia mana alijua ni yeye anaepaswa kuwasha taa ili nuru ipate kutamalaki ndani.


Akavua viatu vyake kuvitupia karibu na sofa kisha akaenda ukutani na kuwasha taa.


Nusura apige mweleka kwa alichokiona.


Kwenye sofa walikuwa wamekaa watu wawili bila wasiwasi; Jay akatazama mlango na kuhakikisha ni yeye alieufungua na si mwingine. Imekuwaje watu hawa wapo ndani tena?


Hakukuwa na wa kumjibu.


Walikuwa ni Panga na Cholo.


“Aisee ninyi mmeingiaje humu?” Jay alihoji kwa wasiwasi.


“Kwa hiyo unahisi sisi ni majini au?” Panga aliuliza kwa kebehi.


“Inabidi mniheshimu hata kama mnaniongoza tafadhali, hapa sio pa kuingia kila mnapotaka aisee!!” Jay alifoka akiwa bado amesimama kwa wasiwasi.


“Shida yetu alikuwa ni mkeo ila kwa kuwa umetangulia wewe, basi haina shida mana hata wewe tunashida na wewe” Cholo alijibu huku akijipapasa kwenye paji la uso bila wasiwasi.


“Unajua dogo leo umetuudhi sana kwa kile ulichoonesha pale msibani, yani kama si ujanja ungeharibu kila kitu aisee!” Panga alilalama.


“Sasa mimi nimefanya nini labda.” Jay alihoji.


“Hujui?” Cholo alishangaa kisha akajichekesha kidogo.


“Kwa hiyo ulivyomkwida Gomba si kuharibu mambo kule? Au unadhani kungekuwa na askari kanzu si angefuatilia kujua kinachoendelea?” Cholo alihoji huku dhahiri sauti yake ikiwa imetawaliwa na jaziba kubwa.


“Lakini alipaswa kunishirikisha kabla hajafanya lolote jamani, akili yangu haipo sawa kabisa mjue!” Jay alilalama.


“mh! Eti akili haipo sawa” Panga alisema huku akimgeukia Cholo.


“Si unaona? Nilikwambia huyu sio njia ya kutufikisha tunakokutaka, ila ni janga hili, sasa akikutana na mwela(polisi) itakuwaje? Panga aliendelea kufoka huku akimlaumu Cholo.


“Sasa tumfanyeje labda,kumuua sasa ni tatizo jipya na kubwa zaidi” Cholo alisema kama vile wanaemeongelea hayupo pale.


Jay aliyasikiliza vyema maongezi yao na hapo aliona kabisa kinachofuata kwake ni kifo bila huruma. Hakutaka hilo limtokeaa.


Haraka akaundea mlango ili atoke nje na awakimbie wale jamaa, ila wakati anafungua mlango alikutana na sura ambayo hakuitarajia kuikuta pale mlangoni na ni kama walijua atafanya hicho kitendo.


Wakati anafungua, alikutana na Gomba akiwa amesimama na kisu mkononi bila wasiwasi.


Jay alistuka kwa sababu aliachana na Gomba akigeuza gari na yule mwanamke ambae hakuwa muongeaji kabisa, sasa vije tena yupo mlangoni kwake? Jay alipagawa na jasho likamtoka mfululizo.


“Dogo; Hivi unadhani unaakili kutuzidi?” Cholo alisema huku akisimama kumfuata Jay ambae alikuwa ameganda kama sanamu asijue cha kufanya.


“Yaani bwana mdogo, tumekuzidi kila kitu, Pesa; mademu; umri; akili na hata dhambi tumekuzidi aisee!” Cholo aliendelea kusisitiza kwa hasira.


Jay aligonganisha viganja vyake ishara ya kuomba radhi kwa wale jamaa watatu ambao aliamini kabisa sio watu wazuri kabisa katika maisha yake wakati huo. Alijiuta kumfahamu Vedi ambae ni dhahiri ndie aliemuingiza kwenye mauzauza yale. Jay aliangusha chozi la uchungu kwa kuona uhai wake unaenda kupotea hivi hivi; Jay hakutegemea kusamehewa na baradhuli wale.


Jay alipiga magoti na kusihi aachiwe huku kimoyo moyo akiomba Mungu wake amuokoe na dhahama inayomfuata.




Mamu aliangaza tu kisha akaelekeza macho yake upande wa pili kulikokuwa na wahudumu wa mgahawa ule; Vedi nae alitazama kule ila aliishia kuona wahudumu wakipishana huku na huko.


Hakujua iliashiria nini na zaidi alichogundua ni kuwa miongoni mwa wahudumu wale baadhi hawakuwa wanaume wa kawaida kwa kuwaona tu, walikuwa ni wanaume waliozidiwa na homoni nyingi za kike na kujikuta wakifanya matendo kama ya wanawake.


Wanaume jina tu.


Vedi akarudisha macho kwa Mamu.


“Sijaelewa lolote!!” Vedi alisisitiza


Mamu hakumjibu, akasimama na kuchukua mkoba wake na kuondoka na kumwacha Vedi akiwa aezubaa na chupa ya maji mkononi.


“Hapa kuna kitu sio bure” Vedi alijisemea huku nae akisimama na kutoka ndani ya mgahawa ule.


Alihitaji kurejea nyumbani kwa Jay ili apumzike na asubiri siku ya kesho itakavyokuwa.



Jay alifikishwa nyumbani na Gomba kisha Gomba yeye akapanda gari na kuondoka bila kusema jambo lingine lolote.


Jay alipiga hatua chache na kufikia lango la nyumba yake, akafungua na kuingia ndani.


Nyumba nzima ilikuwa ni kiza kizito na hakuhofia mana alijua ni yeye anaepaswa kuwasha taa ili nuru ipate kutamalaki ndani.


Akavua viatu vyake kuvitupia karibu na sofa kisha akaenda ukutani na kuwasha taa.


Nusura apige mweleka kwa alichokiona.


Kwenye sofa walikuwa wamekaa watu wawili bila wasiwasi; Jay akatazama mlango na kuhakikisha ni yeye alieufungua na si mwingine. Imekuwaje watu hawa wapo ndani tena?


Hakukuwa na wa kumjibu.


Walikuwa ni Panga na Cholo.


“Aisee ninyi mmeingiaje humu?” Jay alihoji kwa wasiwasi.


“Kwa hiyo unahisi sisi ni majini au?” Panga aliuliza kwa kebehi.


“Inabidi mniheshimu hata kama mnaniongoza tafadhali, hapa sio pa kuingia kila mnapotaka aisee!!” Jay alifoka akiwa bado amesimama kwa wasiwasi.


“Shida yetu alikuwa ni mkeo ila kwa kuwa umetangulia wewe, basi haina shida mana hata wewe tunashida na wewe” Cholo alijibu huku akijipapasa kwenye paji la uso bila wasiwasi.


“Unajua dogo leo umetuudhi sana kwa kile ulichoonesha pale msibani, yani kama si ujanja ungeharibu kila kitu aisee!” Panga alilalama.


“Sasa mimi nimefanya nini labda.” Jay alihoji.


“Hujui?” Cholo alishangaa kisha akajichekesha kidogo.


“Kwa hiyo ulivyomkwida Gomba si kuharibu mambo kule? Au unadhani kungekuwa na askari kanzu si angefuatilia kujua kinachoendelea?” Cholo alihoji huku dhahiri sauti yake ikiwa imetawaliwa na jaziba kubwa.


“Lakini alipaswa kunishirikisha kabla hajafanya lolote jamani, akili yangu haipo sawa kabisa mjue!” Jay alilalama.


“mh! Eti akili haipo sawa” Panga alisema huku akimgeukia Cholo.


“Si unaona? Nilikwambia huyu sio njia ya kutufikisha tunakokutaka, ila ni janga hili, sasa akikutana na mwela(polisi) itakuwaje? Panga aliendelea kufoka huku akimlaumu Cholo.


“Sasa tumfanyeje labda,kumuua sasa ni tatizo jipya na kubwa zaidi” Cholo alisema kama vile wanaemeongelea hayupo pale.


Jay aliyasikiliza vyema maongezi yao na hapo aliona kabisa kinachofuata kwake ni kifo bila huruma. Hakutaka hilo limtokeaa.


Haraka akaundea mlango ili atoke nje na awakimbie wale jamaa, ila wakati anafungua mlango alikutana na sura ambayo hakuitarajia kuikuta pale mlangoni na ni kama walijua atafanya hicho kitendo.


Wakati anafungua, alikutana na Gomba akiwa amesimama na kisu mkononi bila wasiwasi.


Jay alistuka kwa sababu aliachana na Gomba akigeuza gari na yule mwanamke ambae hakuwa muongeaji kabisa, sasa vije tena yupo mlangoni kwake? Jay alipagawa na jasho likamtoka mfululizo.


“Dogo; Hivi unadhani unaakili kutuzidi?” Cholo alisema huku akisimama kumfuata Jay ambae alikuwa ameganda kama sanamu asijue cha kufanya.


“Yaani bwana mdogo, tumekuzidi kila kitu, Pesa; mademu; umri; akili na hata dhambi tumekuzidi aisee!” Cholo aliendelea kusisitiza kwa hasira.


Jay aligonganisha viganja vyake ishara ya kuomba radhi kwa wale jamaa watatu ambao aliamini kabisa sio watu wazuri kabisa katika maisha yake wakati huo. Alijiuta kumfahamu Vedi ambae ni dhahiri ndie aliemuingiza kwenye mauzauza yale. Jay aliangusha chozi la uchungu kwa kuona uhai wake unaenda kupotea hivi hivi; Jay hakutegemea kusamehewa na baradhuli wale.


Jay alipiga magoti na kusihi aachiwe huku kimoyo moyo akiomba Mungu wake amuokoe na dhahama inayomfuata.


“Tunamfanya nini huyu pimbi!” Panga alihoji huku akisimama pale alipokuwa amekaa mwanzo.


“Plan b nadhani inaweza kutuweka salama zaidi kuliko hii plan A.” Gomba alisema huku akichezea kisu chake kwa vidole vyake na akimtizama Jay kwa macho fulani yenye ujumbe usio tafsirika.


Jay aliona akakufa kizembe akiendelea kuzubaa ni lazima afanye jambo litakaloweza kumsaidia aponyoke kwenye mikono ya watu wale wabaya.


Akiwa amepiga magoti chini, aliona namna ambavyo Panga na Cholo walivyokuwa wanamfuata kwa hatua za taratibu huku wakibwabwaja.


Pale alipokuwa aliona pembe ya zulia ipo karibu na magoti yake,akaona huo ndio mwanya wa kufanya kile alichofikiria ili ajinasue kwenye janga linalomkabili.


Akafanya kitendo ambacho hakuna ambae alikitegemea.


Akaishika pembe ya zulia kisha akalinyanyua juu kwa kasi na kusababisha liteleze kwenye marumaru na kisha akalivutia kwake kwa kasi na kufanya Cholo na Panga wapige mweleka mkubwa chini bila kutarajia huku kila mmoja akianguka kwa namna yake na kilio cha hamaniko.


Jay hakutaka kuzubaa, haraka akataka kuruka na kuuendea mlango, ila hesabu zake zilikuwa nyuma ya muda na hii ni kwa sababu hakuwa mzoefu wa mapigano la sivyo hesabu zake angemjumlisha na Gomba.


Kushindwa kupiga hesabu vyema kukapelekea kujutia kosa lake.


Akakutana na ngumi nzito iliomrudisha nyuma bila kupenda,akampatazama tena Gomba ambae alikuwa amesimama bila wasiwasi wowote.


Akajaribu tena bahati yake na akajifyatua mzima mzima ili amkumbe Gomba ila napo hakujua Gomba ni mtu wa aina gani, akajikuta akidakwa kama mchezo hivi na kusukumwa chini kwa nguvu na alipotaka kusimama alikutana na teke zito kutoka kwa Panga ambae alikuwa ameshasimama na gadhabu kubwa.


Jay akataka kujinyanyua tena ila aliishia mikononi mwa Panga na kujikuta akichezea makonde mengi ya uso na kuanza kuvuja damu.


“Punguza jaziba bwana Panga” Cholo alimshika mkono Panga huku akimsihi.


“Pimbi wewe, yani unataka kuweka mchapo na sisi!! Yani wa kutuotea sisi kweli! Ebo!” Panga aling’aka kwa gadhabu huku akijishika makalio ambayo dhahiri yalionekana kupata shuruba wakati anayaangukia.


“Mchezo wa kuotea ni mbaya sana bwana mdogo” Gomba alisema huku akimwinamia.


Jay alijitahidi kusema ila haikuwezekana, kipigo kilimkolea.


“Tunaweka usiku mjue” Panga alizungumza huku bado akionekana kuwa na gadhabu iliopitiliza kwa kitendo walichofanyiwa.


“Sasa tunakupa dozi bwana mdogo na ili uipate ni lazima ututafute na ukumbuke pia unaumwa Kansa ya mifupa na ili upone lazima ututafute,sasa rudia ujinga wako ufe na auche Cholo akimuoa mkeo, si uliona picha zake wakiwa wote lakini eeh!” Gomba alizungumza akiwa bado amemshika kwa kumwinamia Jay ambae alikuwa nusu amelala na nusu ameinuka. Alikuwa kifudifudi.


Ile kusikia neno mkeo, kukawa kama amesikia kitu cha ajabu kikipita mwilini mwake na kumwachia mamumivu moyoni.


Aliona kama ambae amemkosea sana Vedi kwa kutomsikiliza wakati alipomfikia siku hiyo lakini pia nafsi nyingine ilijuta kukutana na Vedi katika maisha yake japo yajayo hawakuwahi kuyajua kama watafikia hapo.


“Hii inaitwa dope na inaliwa na matajiri tu sasa ni bahati kwako kidampa kuipata eti” Gomba alimwambia Jay huku akisogeza ncha ya kidole kisu kwenye pua za Jay. Jay aliona kwa mbali kitu kama poda kikiwa juu ya ncha ya kisu na akalirudia neno “Dope”…


“Noo;msinifanye hivyo…” Jay alijitahidi kusema bila mafanikio na alipojaribu kujitikisa alijikuta akiwa amedhibitiwa vyema na miguu ya Gomba ambae alikuwa amemyanyua na kumbana usawa wa mbavu na miguu yake huku mkono mmoja ukipita kwenye usawa wa mabega yake na kumfanya ainuke kwa kutazama juu.


Bado aliona kile kisu kikimsogelea taratibu, akataka kuvuta pumzi nyingi ili azihifadhi wakati akipambana asivutishwe ule unga.


Alikuwa amechelewa tena hesabu zake.


Wakati akitaka kuvuta ni wakati huo ncha ya kisu ilikuwa sambamba na tundu moja ya pua hivyo akajikuta akivuta sambamba na unga ule.


Akalia kwa uchungu kwa tukio lile.


Gomba alimwachia na kusimama huku akitabasamu kwa kitendo kile kisicho cha kiuugwana.


Jay alianza kuhisi hali ya tofauti ikimjia kwa kasi, alijihisi ni mwepesi na furaha ya ajabu ikimjia, hata yale maumivu ya kipigo hakuyasikia tena na zaidi aliendelea kuhisi amani ikimtawala na yale mawazo mabaya yakiondoka kwake.


Jay alijichekelesha kama bwege.


“Tayari yupo stoned huyu!” Gomba alisema.


“Muda wa high ukifika ndo atajua utamu wa dope na akikolea basi utumwa utamhusu.” Panga aliongeza.


Jay aliendelea aliendelea kushindana na raha ya ajabu iliomkumba,alijitahidi kupishana nayo ila ilikuwa ni kazi bure na alijikuta akiitamani tena ile raha iendelee kuwa nae.


Akajivuta kutoka chini na kuegemea miguu ya Gomba kisha awa hisia.


“Please I need more dope please”


Nafsi yake ilimuwia uzito kukubali kutendo kile cha kuomba ila alijikuta mwili unamsaliti; mwili ulihitaji tena kupata ile raha ya ajabu.


Cholo alisogea na kumwinamia.


“Sikia bwana mdogo,hii kitu tunakupa kwa garama ndogo tu, nayo ni siri kuhusu yanayoendelea, lakini pia tunataka uhakikishe demu wako hakutani na askari yeyote bila sisi kujua na pia hakikisha kila akitoka hapa unajua anakoenda na sisi kila jioni tutakuletea hii kitu” Cholo alimwambia Jay huku akipunga fundo dogo la karatasi hewani.


“Hiyo uliopata inatosha kwa sasa, ukizidisha tutakupeleka mochwari” Cholo alisema tena huku akisimama na kisha akawapa ishara wenzie na wakaanza kutoka ndani ya ile nyumba na kumwacha Jay akianguka chini kwa mauzauza yanayoukumba mwili wake.


Chozi lilitoka kwa uchungu, ila hakuwa na la kufanya zaidi ya kutulia chini na kuacha mwili usisimke kwa furaha ya kununua.


Jay rasimi alikuwa ameingia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya bila kupenda.


Lakini kwa nini hawa jamaa wanayafanya haya yote?


Hakuna aliejua chanzo cha yote ni nini, je ni baharia au ni kitabu cha baharia?


Bado hakuna aliejua na Baharia aliona nini; alijua nini hadi kifo kikamkuta? Bado lilikuwa ni swali bila jibu.


Bado Cholo;Panga na Gomba walikuwa washindi kwenye mchezo ule usio na jina la kueleweka, walitumia nguvu nyingi bila sababu ya msingi kueleweka.



Lakini siku zote waswahili wanasema; “Mwenda kombo kwa hisani, hurudi kwa aibu ya huzuni” mchezo uliingiliwa na wababe wa fitina wakiongozwa na Zedi Wimba.




“Sikia bwana mdogo,hii kitu tunakupa kwa garama ndogo tu, nayo ni siri kuhusu yanayoendelea, lakini pia tunataka uhakikishe demu wako hakutani na askari yeyote bila sisi kujua na pia hakikisha kila akitoka hapa unajua anakoenda na sisi kila jioni tutakuletea hii kitu” Cholo alimwambia Jay huku akipunga fundo dogo la karatasi hewani.


“Hiyo uliopata inatosha kwa sasa, ukizidisha tutakupeleka mochwari” Cholo alisema tena huku akisimama na kisha akawapa ishara wenzie na wakaanza kutoka ndani ya ile nyumba na kumwacha Jay akianguka chini kwa mauzauza yanayoukumba mwili wake.


Chozi lilitoka kwa uchungu, ila hakuwa na la kufanya zaidi ya kutulia chini na kuacha mwili usisimke kwa furaha ya kununua.


Jay rasimi alikuwa ameingia kwenye uraibu wa madawa ya kulevya bila kupenda.


Lakini kwa nini hawa jamaa wanayafanya haya yote?


Hakuna aliejua chanzo cha yote ni nini, je ni baharia au ni kitabu cha baharia?


Bado hakuna aliejua na Baharia aliona nini; alijua nini hadi kifo kikamkuta? Bado lilikuwa ni swali bila jibu.


Bado Cholo;Panga na Gomba walikuwa washindi kwenye mchezo ule usio na jina la kueleweka, walitumia nguvu nyingi bila sababu ya msingi kueleweka.


Lakini siku zote waswahili wanasema; “Mwenda kombo kwa hisani, hurudi kwa aibu ya huzuni” mchezo uliingiliwa na wababe wa fitina wakiongozwa na Zedi Wimba.



Vedi alifika nyumbani kwa Jay na kukuta nyumba ikiwa kimya licha ya taa za ndani kuwaka.


Alisukuma mlango na kuingia kwa tahadhari.


Macho yake yaliona mwili wa Jay ukiwa umelala chini, haraka akakimbia na kwenda kumuinua huku akimuita.


Jay alipofumbua macho alikutana na sura ya Vedi ikiwa inamtazama huku mwili wake ukiwa umepakatwa na Vedi.


Jay alijitahidi kusema kitu ila alishindwa na kuishia kukohoa na kutoa udenda kama teja aliezidisha dozi.


Vedi aligundua mpenzi wake anataka kusema kitu; akainama na kumsikiliza na kwa mbali alipata kusikia alichokisema Jay.


“Tafadhali ondoka hapa kwangu!” Jay alisema kwa tabu kubwa.


Vedi alitikisa kichwa kukataa huku akilia; alilia kwa sababu asingeweza kutoka na kumwacha akiwa katika hali ile.


Uso ulimvimba na alionekana kuwa ni dhoofu wa mwili.


Vedi alisimama na kumkokota Jay hadi kwenye sofa na kumkaliza.


Alihitaji kumpa msaada lau wa kumkanda na maji ya moto baada ya kuona namna alivyoumizwa na uso kumvimba.


Muda wote huo bado Jay alionesha ishara ya kumtaka Vedi atoke.


Vedi hakukubali kirahisi, aliendelea kushugulika na jiko ili yapatikane maji ya moto kwa ajili ya huduma ya kwanza kwa Jay.


Licha ya maswali mengi kichwani mwake kuhusu yaliompata Jay hadi kufikia vile; ila hakuwa na uwezo wa kumuuliza mana alionekana yupo kwenye hali mbaya sana, hivyo alihitaji kupata huduma ya kwanza kisha aone uwezekano wa kumuuliza yaliompata na pia alikuwa na shauku ya kujua msibani kumeendelea nini na kisha amwambie yale yanayoendelea katika maisha yake kwa sasa.


Maji hayakuchukua dakika nyingi kuchemka, akayachukua na kutafuta kitambaa safi kisha akaelekea sebuleni kumpa huduma mchumba wake aliempenda kuliko kitu chochote.


Jay hakuwa na namna zaidi ya kubaki akimtizama tu Vedi.


Vedi alimkanda na kumsafisha hapa na pale kisha akataka kumvua shati na hapo ndipo Vedi alikumbuka kitu.


Wakati anapitisha kitambaa usawa wa pua za Jay ni kama aliona ungaunga mweupe ukiwa umesalia kwenye tundu za pua.


Vedi alimtizama Jay machoni; Jay akakwepesha macho yake na kutazama pembeni.


Vedi kuna hisia fulani zilimpitia, ila akazipuza na badala yake akaendelea kumvua shati Jay.


Alipomaliza alimtaka waelekee bafuni kuoga; Jay alikataa na alisema.


“Naomba uniache tu msaada wako umetosha kwa hapa tafadhali” Jay alikataa na kumfukuza Vedi.


Vedi alitazama pembeni kwa muda kisha akamuuliza.


“Jay ulikuwa na mimi kwa sababu gani labda!”.

Jay alizubaa kwa swali lile mana hakutegemea kulipata kwa muda ule.


“Nilikuwa na wewe kwa sababu nilikupenda sana” Jay alijibu.


“Kwa hiyo sasa hivi hunipendi sio!” Vedi alihoji.


“Kwa ulioyafanya, hakika sikupendi tena na ni bora ukaniacha na maisha yangu tu” Jay alisema huku akitazama pembeni.


Vedi alimtazama kwa muda wa dakika moja nzima bila kusema kitu.


“Kwa hiyo uminizika?” hatimae Vedi alipata kauli.


Jay alistuka kwa swali lile na hapo akakumbuka yaliotokea kwa Mama msangu; Mama yake Vedi na hakujua hadi muda huo ni wapi atakuwa alipelekwa mwanamke yule.


Kitu kama kaa la moto likapita moyoni mwa Jay.


Alitamani kusema kitu ila akajikuta nafsi inakataa, aliwakumbuka Gomba na wenzake hapo nafsi ikajaa woga.


“Nimekwambia sitaki kukusikia mana Vedi ameshafariki na wewe ni kama kivuli chake tu,tafadhali nisingependa uendelee kuwepo hapa” Jay ilibidi afoke huku akikwepa kujibu swali la Vedi.


“Ok! Na nini kilichokukuta hapa ndani hadi kuwe hivi, nimekukuta upo hoi na dhahiri umepigwa na pia unaoekana hapa ndani kumefanyika rabsha za hapa na pale.” Vedi aliuliza huku akiwa amemkazia macho.


Lilikuwa ni swali lingine gumu kujibika kirahisi na hata akijibu Atajibu kwa aina gani ya ushawishi ili aeleweke?


Ikawa ni ngumu kwa Jay.


“Nadhani hupaswi kuniuliza lolote wakati huu, zaidi ningekuona wa maana kama ungeondoka hapa ndani Vedi” Jay alikwepa kujibu swali kwa mara nyingine.


Vedi alisimama kisha akamsogelea Jay.


“Nitazame machoni Jay kisha unambie hutaki kuniona hapa kwako!” Vedi alisema huku akimtizama Jay usoni.


Jay alishindwa kusema lolote.


“afu kuna kitu unakificha mpenzi wangu, na yawezekana una matatizo zaidi yangu” Vedi alimwambia Jay huku akianza kuondoka pale sebuleni.


Jay alikumbuka kitu.


Ili asalimike kwenye mikono ya wale wababe ni lazima awe karibu na Vedi,hivyo kumfukuza ni kumweka mbali nae na pia atakosa tiba ya ugonjwa alioambukizwa.


Mwili wake alihisi unaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida, hivyo akataka kusimama ili aelekee chumbani ila wakati akitaka kusimama ni wakati huo ambao Vedi alifika pale akiwa na kikombe cha chai.


“Nadhani unapaswa kunywa hii ili upashe tumbo joto, hapa sitoki na ukiona nakukera nifukuze kwa kunivuta hapo nitaamini hutaki uwepo wangu hapa.” Vedi alimwambia Jay huku akikaa karibu yake na kikombe cha chai.


Jay alipata kusikia ya kuwa; mtu yeyote ambae anatumia madawa ya kulevya chai kwake ni sumu na endapo akiitumia muda mchache baada ya kuvuta, basi athari kubwa zaidi atakayoipata ni kifo.


Jay aliogopa na hakutaka kuinywa ile chai.


Akaipokea na kisha akamtazama Vedi na akaamua kukwepa kisomi.


“naomba unipikie ugali tafadhali” Jay alisema kiyonge na muda huohuo alimuona Vedi akisimama na kuelekea upande kulipokuwa na jiko na yeye akasimama na kuelekea nje na akiwa na kikombe cha chai mkononi.


Huko nje wala hakunywa chai ile, isipokuwa aliishia kuimwaga tu kisha akabaki na kikombe mkononi huku mambo mengi yakipita kichwani mwake.


Mara akagutuka, alimuona Vedi akiwa ameshika simu na aliambiwa ajitahidi kujua mienendo ya Vedi.


Akatoa simu yake mfukoni na kutafuta namba zilizokuwa zimehifadhiwa kwa jina la “Mtesi” akaandika ujumbe mfupi na alipohakikisha umeenda akaianama na kufuta chozi kwa uchungu.


Nafsi yake ilikataa kabisa kukubaliana na kile alichokuwa anakifanya.


Roho ilimuuma ila hakuwa na la kufanya kuepuka hali ile.


Alikaa nje hadi wakati alipoitwa kula.


Muda mwingi kulitawala ukimya wa kutisha baina yao na hakuna aliemsemesha mwenzie.


Walipomaliza kula; Vedi aliSimu yake na kujaribu kupiga namba za Nyamizi rafiki yake, japo aliamini si rahisi kupatikana kwa sababu fungate walipanga lifanyikie Nairobi baada ya ndoa yao.


Vedi alijikuta akiwaza tu na kupiga.


Muda wote Jay alikuwa akimtizama bila kusema kitu.


Ajabu simu iliita.


Vedi alishangaa, kisha akahesabu siku za ndoa na kugundua zilipita siku nne tu tangu walipokuwa kwenye sherehe za ndoa sasa vije tena simu iwe hewani wakati ilitakiwa wawe Nairobi.

Lakini hata yeye alijishangaa, kwanini alipiga wakati anajua kabisa wapo Nairobi?”

.

Simu ikapokelewa.


“Hallow!!” ikaitika upande wa pili.


Vedi alijua ni sauti ya Nyamizi.


“Vedi hapa naongea!” .


Vedi akasikia upande wa pili ukipumua kwa nguvu.


“Vedi yupi anaeongea?” Nyamizi alihoji.


“Usitake kusema hata sauti yangu hujaijua shoga angu” Vedi alilalama.


“Sauti yako haiwezi nipotea hata nikiwa katikati ya koma, ila imetokea nini tena nasikia sauti yako wakati tumeambiwa umekufa?” Nyamizi alihoji.


Vedi aliguna.


“Wewe upo wapi kwani” Vedi alihoji.


“Huwezi amini nimetokea msibani, nilichanganyikiwa kusikia ni wewe uliejitupa kwenye maji, raha ya fungate ilikata, tafadhali nambie kumetokea nini mpenzi” Nyamizi aliongea kwa hisia.


“Ngoja kukuchwe nadhani tutaonana” Vedi alisema.


“No! Nadhani tuonane hata sasa ili nijiridhishe ni wewe mpenzi” Nyamizi aliongea.


Vedi na Nyamizi walikubaliana kuonana usiku ule na ilikuwa ni mishale ya saa tano za usiku.

Vedi akatoka na kama kawaida.



Jay nae akaandika ujumbe kwenda kwa watesi wake kuwajulisha Vedi anakoelekea.


***




Muda wote Jay alikuwa akimtizama bila kusema kitu.


Ajabu simu iliita.


Vedi alishangaa, kisha akahesabu siku za ndoa na kugundua zilipita siku nne tu tangu walipokuwa kwenye sherehe za ndoa sasa vije tena simu iwe hewani wakati ilitakiwa wawe Nairobi.

Lakini hata yeye alijishangaa, kwanini alipiga wakati anajua kabisa wapo Nairobi?”

.

Simu ikapokelewa.


“Hallow!!” ikaitika upande wa pili.


Vedi alijua ni sauti ya Nyamizi.


“Vedi hapa naongea!” .


Vedi akasikia upande wa pili ukipumua kwa nguvu.


“Vedi yupi anaeongea?” Nyamizi alihoji.


“Usitake kusema hata sauti yangu hujaijua shoga angu” Vedi alilalama.


“Sauti yako haiwezi nipotea hata nikiwa katikati ya koma, ila imetokea nini tena nasikia sauti yako wakati tumeambiwa umekufa?” Nyamizi alihoji.


Vedi aliguna.


“Wewe upo wapi kwani” Vedi alihoji.


“Huwezi amini nimetokea msibani, nilichanganyikiwa kusikia ni wewe uliejitupa kwenye maji, raha ya fungate ilikata, tafadhali nambie kumetokea nini mpenzi” Nyamizi aliongea kwa hisia.


“Ngoja kukuchwe nadhani tutaonana” Vedi alisema.


“No! Nadhani tuonane hata sasa ili nijiridhishe ni wewe mpenzi” Nyamizi aliongea.


Vedi na Nyamizi walikubaliana kuonana usiku ule na ilikuwa ni mishale ya saa tano za usiku.

Vedi akatoka na kama kawaida.



Jay nae akaandika ujumbe kwenda kwa watesi wake kuwajulisha Vedi anakoelekea.


-------------


Mwendo wa nusu saa ulitosha kuwakutanisha Nyamizi na Vedi. Walikutana sehemu walioona ni sahihi kwao kukutana.


Jambo la kwanza walilofanya marafiki wale ni kukumbatiana kwa hisia huku kila mmoja akilia kwa hisia.


Moyo wa Vedi ulifarijika kuona lau sasa amefanikiwa kupata mtu anaeweza kusimama nae wakati mgumu kama huu wakati ambao hata ndugu yake wa damu alimkataa na kumuita jini, wakati ambao watu wamemkimbia na kumwacha akipitia kipindi ambacho hakujua mwanzo wake wala mwisho wake ila alijikuta tu akiingia kwenye kipindi kama hicho, kipindi cha mateso ya akili na hisia bila watesaji kujitokeza mbele yake.


Walikaa sehemu iliokuwa inautulivu katika mgahawa mmoja ambao waliona unafaa.


“Mbona uko peke yako shemeji yuko wapi?” Vedi aliuliza.


“Ndie kanisindikiza hapa ila amepaki kule na kabaki ndani ya gari” Nyamizi alisema huku akielekeza kidole upande wa pili wa mgahawa ule. Vedi aligeuka na kuona gari zuri la kisasa likiwa limepaki.


“Kwanza nambie imekuwaje huko msibani?” Vedi alihoji kwa shauku kubwa.


Nyamizi aliguna kidogo.


“Mchana kuna tukio lilitokea ambalo lilizuia kila kitu na hapa navyokwambia maiti imerudishwa mochwari kwa uchunguzi zaidi” Nyamizi alimwambia Vedi na Vedi alikaa vizuri kwenye kiti.


“Wakati tunasubiri taratibu za mazishi; Jay alikuja ndani akiwa na mtu mwingine na alipofika dada ako akampeleka ndani alikokuwa mama na punde wakarejea huku mama akionekana dhahiri kuna kitu alitaka kumwonesha kwenye ule mwili pale mara tukashangaa Mama anapiga kelele kama mwehu na kujikuna hovyo na kabla hatujafanya lolote Jay nae akaanguka na kuzimia, hazikuzidi hata dakika kumi gari la wagonjwa likafika na kuwapeleka muhimbili”


Vedi alijifuta machozi kwa uchungu.


“Ulifanikiwa kujua kilichoendelea huko Muhimbili lakini shoga angu?” Vedi aliuliza.


“ Shemeji yako alifuatilia na badae akaja na taarifa ambazo hazikumpendeza kila mtu, alisema mumeo hakuonekana hospitali ila Mama amewekwa wodi ya uangalizi wa matatizo ya akili, mana kawa kama kichaa kiukweli” Nyamizi aliongea huku machozi yakimlenga.


“Ahsante sana kwa upendo huo mnaoonesha kwangu, hakika u rafiki mwema sana Nyamizi; kwanza mlikatisha fungate lenu ili mje kuhudhuria msiba wangu na sasa upo hapa na mimi wakati watu wote wakiniona wananikimbia kwa sababu ya kuhofia mimi ni jini” Vedi alijifuta machozi kwa mgongo wa kiganja chake.


“Tuko pamoja mpenzi; kwani Jay anasemaje au umefanikiwa kuonana nae?”


Vedi alibabaika kidogo kwa swali lile.


“Kiukweli Jay nimeonana nae ila amekuwa sio Jay unaemfahamu, amekuwa ni mtu wa ajabu sana hivi karibuni, haeleweki na hapa nimetoka kwake ila hajanambia hata kuhusu mama angu……masikini Mama jamani!” Vedi alianza kulia kwa sauti ya chini.


“basi hupaswi kulia sasa, kikubwa labda unishirikishe kimetokea nini hadi kutangazwa umekufa?” Nyamizi alihoji na alionekana kuwa na uchu wa kujua hilo jambo.


Vedi alivuta pumzi nyingi na kuzishusha, hakuwa na sababu ya kuficha kwa rafiki makini kama yule.


Akamweleza yaliomkuta ndani ya meli na hadi kufikia hapo alipo.



Wakati Nyamizi na Vedi wakisimuliana; Boneka mume wa Nyamizi alikuwa ametulia ndani ya gari huku mawazo yakimpita kwa kasi. Mbali ya ubilionea aliokuwa nao ambao alilirithi kwa wazazi wake ila hakuna mtu ambae alijua ni nini kinaendelea nyuma yake.


Boneka alikuwa ni ofisa wa kitengo maalumu na kazi maalumu na aliwekwa kwenye kitengo kile na Kamishina wa jeshi la polisi Zenge wa Zenge. Kamishina Zenge wa Zenge aliamini akili ya Boneka tangu akiwa kiongozi wake ndani ya jeshi la polisi na walifanya kazi Dodoma na kufanikiwa kuzima mtandao wa mbwa mwitu katika kisa kilichoandikwa vyema na mwandishi Bahati Mwamba na kukipa jina la “DAKIKA ZA MWISHO with Wolf rules” na Boneka alifanya makubwa licha ya kuja kusaidiwa na Zedi Wimba jasusi hatari.

Na sasa Boneka ni mfanyabiashara mkubwa ila bado anatumikia taifa akiwa kwenye kitengo cha “Special operations” kilicho chini ya Kamishina Zenge wa Zenge. Kitengo hiki kimesheheni watu makini akiwemo Zedi Wimba; Honda Makubi; Haji Makame; Elias Ziga na Mwinyi Kisoda. Watu hawa wote wametokea jeshini ila Boneka pekee ndie ametoka jeshi la polisi pamoja na Kamishina mwenyewe. Mbali na Kamishina ambae alikuwa kazini siku zote ila vijana wake wote walikuwa nje ya kazi na kila mtu anafanya kazi zake na hukutana wakati wa kazi maalumu tu na wakimaliza kila mmoja huchukua hamsini zake.


Boneka tangu mwanzo aliposikia kuhusu kifo cha Vedi akili yake haikukubali mapema, mana hata wakati watu wanakimbia ndani ya meli kwenda kuona mtu aliejitupa ndani ya maji, yeye alitoka pia na kwa mbali alimuona Vedi akiwa miongoni mwa watu waliotaka kushuhuidia tukio lile.


Walipofika Nairobi ndipo walipokea taarifa za kifo cha Vedi na hima wakarejea na kazi kubwa alioifanya ni kumtuliza mkewe Nyamizi ambae alikuwa analia wakati wote na hapo wakawasiliana na mwenyekiti wa kamati ya mapokezi ambae alitakiwa kuhakikisha watu wanaingia na kutoka salama na mwenyekiti akatoa majina ya watu wote waliosaini kitabu cha watu waliotoka salama ndani ya meli.


Jina la Vedi aliliona na alimuonesha mkewe sahihi ya Vedi na Nyamizi akakubali ya kuwa ule ni mwandiko wa Vedi.


Kuna nini hapa nyuma? Alijiuliza akiwa peke yake na alichukua kitabu kile akapitia tena majina ya watu walioingia na kutoka.


Jina moja liliingia ila halikutoka.


Lilikuwa ni jina la Masumula Hussein.


Ni nani huyu binti?


Akamuuliza mkewe na jibu lilikuwa ni mtoto wa shangazi yake na Nyamizi na yeye ndie alimpa kadi.


Ikabidi wapige simu nyumbani kwa kina Masumula na jibu lilikuwa ni tangu aage kwenda harusini, hakurejea tena nyumbani.


Boneka akajenga picha ya kuhusanisha mambo yale.


Na akajiuliza kwanini Vedi sasa ndie awe muhanga wa shida ile badala ya Masumula? Na Masumula kwa nini auwawe au Vedi aliona mauaji yake? Na wauaji walitaka kumziba mdomo?


Ikabidi waelekee msibani na hata wakati yale yanatokea msibani; Boneka aliyashuhudia ila alikuwa na mashaka na mwonekano wa Jay mana alimfahamu lakini pia alikuwa na mashaka na rafiki alieongozana na Jay; Macho yake ya kijasusi yalimwambia yule hakuwa mtu mwema kabisa.


Wakati Boneka akiwaza hayo ndani ya gari kuna kitu aliona.


Aliona mtu ambae alikuwa makini na nyendo za mkewe na shemeji yake Vedi ambao walikuwa wamekaa ndani ya mgahawa wakihabarishana mambo yao ambayo hakutaka kuyaingilia.


Alipomtazama vizuri mtu yule alimtambua.


Alikuwa ni yule aliekuwa ameongozana na Jay msibani.


Alimuona Gomba.





Ndio! Alimuona Gomba akiwa makini na nyendo za Nyamizi na Vedi.


Boneka mwenyewe hakujua ni kwa nini hata yeye alijikuta akimhisi vibaya yule jamaa.


Usiku huu anafanya nini hapa, na kwanini anamwangalia sana mke wangu na rafiki yake? Na kweli anaweza kuwa na urafiki na Jay hadi awe na kazi ya kumfuatilia Vedi?


Boneka aliendelea kuuliza maswali bila kupata jibu.


"mh" aliguna peke yake kisha akajiuliza tena "inawezekana kweli huyu Jay akawa anahusika kwenye hili sakata?"


Boneka akiwa bado anajiuliza hayo, mara akaona Gomba akianza kuondoka pale alipokuwa amesimama. Hakujua ni kwa nini aliamua kuondoka.


Boneka nae alishuka na kuanza kumfuata taratibu bila wasiwasi wowote.


Gomba alikuwa anaongea na simu huku akijisaidia haja ndogo kwenye kigiza mbali na mwanga wa taa.


Alikuwa anaongea kwa sauti ya chini sana kiasi kwamba haikuwa rahisi mtu wa mbali kidogo walau kusikia walichozungumza.


Boneka alihitaji kujua kitu kutoka kwa Gomba.


Alikuwa na maswali mawili tu kwake.


Alihitaji kujua pale alikuwa anamchunguza nani kati ya Nyamizi na Vedi na pia alihitaji kujua ni kwanini gari la wagonjwa aliloliita halikufika muhimbili na Jay na badala yake lilimwacha kusikojulikana?


Ni hayo tu!


Wakati Gomba anafunga zipu ni wakati huo aliposikia akiguswa bega lake la kushoto.


Taratibu aligeuka bila papara yoyote huku akikata simu yake.


Alikutana na sura ya kijana mtanashati ambae kimwonekano tu alitangaza ukwasi aliokuwa nao.


Gomba aliweka sura ya kazi bila kusema lolote. Ila ajabu mgeni wake wala hakujali zaidi ya kutabasamu tu na hapo ndipo alipoona kijana mwenye sura ya kike na tabasamu la kiume.


Alikuwa anatazamana na Boneka.


"Nikusaidie nini!" Gomba alihoji.


"Ninahitaji kuongea na wewe kidogo" Boneka alijibu huku akiwa ameweka mikono mfukoni.


Gomba alimtazama juu hadi chini na wala hakuhisi kama kijana yule anaweza kuwa na ubaya wowote ule..


"kwa wema au ubaya!" Gomba alihoji.


"Inategemeana na vile utakavyochukulia ila vyovyote sawa tu" Boneka alijibu.


Ebo!!!


Gomba alishangaa,kijana mdogo ambae amekaa kike kike anakuwaje na mikwara tena.


Gomba alicheka.


"Yani wewe wa kunikatia mkwara mimi! You can't be serious young boy" Gomba alichanganya na kimombo kidogo.


Boneka hakustuka alikaa kimya akimtizama Gomba.


"Haya unasemaje.!" Gomba alihoji kwa kebehi.


"Nikikuuliza hapa umefuata nini unaweza kunijibu?" Boneka alihoji.


"Sasa utaanzaje kuniuliza mtoto mrembo kama wewe au na wewe ni Jezabeli nini?" Gomba aliendelea kudhihaki.


"Mwanzo nilikwambia vyovyote utakavyopenda kuulizwa iwe kwa wema au ubaya, naona sasa unataka tena nikuthibitishie ubaya ninao maanisha" Boneka alimwambia Gomba huku akiwa kwenye kiwango cha juu cha hasira.


Gomba hakutaka kuweka maelezo zaidi. Akanyanyua mkono wake ili amsukume Boneka na aendelee na mambo yake.


Kwa wepesi wa ajabu alijikuta akivutwa kwa kasi na kusukumiwa ngumi nzito kifuani na kabla hajaanguka akadakwa tena na kisha akapigwa kichwa maridadi kwenye paji la uso na akahisi dunia ikizunguka na yeye mwenyewe alipoachiwa alijikuta akiyumba huku na huko kama mlevi huku akili yake ikikataa kukubali ya kuwa yule kijana mpole aliesimama imara ndie aliemwadabisha kwa mipigo miwili tu na kumweka hoi namna ile.


Gomba alitikisa kichwa kuweka sawa akili yake ili asisumbuliwe na mawenge.



Akajipanga ili amkabili Boneka.


Kwa pupa akamwendea Boneka huku akiunguruma kama Simba jike aliekosa bwana.


Boneka akahepa kidogo na kufanya ngumi ya Gomba ipite patupu na kisha akamshindilia teke madhubuti mgongoni.


Gomba alienda kuanguka kifudi fudi huku akilia kama msimbe.


Boneka alibaki akiwa amesimama bila papara yoyote.


Wakati akimsubiri asimame, mara akashangaa gari ikimjia kwa kasi nae akaruka na kujiweka pembeni,gari ile ikaenda kusimama karibu na alipoanguakia Gomba; Gomba hakutaka kuuweka, haraka akafungua mlango na kujitosa ndani na kwa kasi gari ikaondoka pale huku Boneka akiuma meno kwa hasira.



***


Ndani ya gari; Gomba na Panga hawakusemeshana. Panga alikuwa bize na usukani huku Gomba akijibinya paji la uso.


"Yule bwege kaniotea sana aisee!" Gomba alilalama.



"Tangu mwanzo niliona umemdharau yule mtoto na ndio mana umekunwa upele jombaa" Panga alimkebehi Gomba.



"Dah! Miaka mingi sana sijawahi kuotewa namna hii aisee." Gomba alisema tena.



"Ndo inatakiwa ujue hata panya akikatisha uwanja wa vita lazima alambwe njiti" Panga alisema.



"Lakini yule bwege ni nani?" Gomba alihoji.


"Kwa kweli sijamjua vizuri ila tuwe makini sana, tunaweza ona tupo salama na tukajikuta tunaokotwa kama vifaranga ujue!" Panga aliatahadharisha.


"Lakini Taiga angeshatupa taarifa kama kuna watu wapo nyayoni mwetu, kukaa kwake kimya kunaashiria hamna jipya na kama kuna askari anatufuata ingejulikana pia" Gomba alipinga mashaka ya Panga.


Panga alikaa kimya na safari iliendelea.



----------------------



Wakati Boneka anarejea kwenye gari ni wakati ambao mkewe Nyamizi alikuwa anamalizia mazungumzo na kuagana na Vedi.



Nyamizi alihakikisha Vedi amepata usafiri wa kumrejesha ndipo na yeye alienda kupanda gari la mumewe.


"Ulikuwa sahihi mume wangu; Vedi anatatizo kubwa tu linalomsumbua" Nyamizi alisema punde tu alipokaa na kufunga mlango.



"Kakudokeza lolote?" Boneka alihoji.


"Hapana hajafunga lolote ila amenambia kuna tatizo lipo kwenye ile meli ya Serengeti Marine na ndio chanzo cha matatizo yake haya" Nyamizi alisema huku akiegemea kwenye kiti.


"Sasa kwanini hajakushirikisha?" Boneka alihoji huku akiwa makini sana kusikiliza kila neno litakalo semwa na mkewe.


"Alichonambia ni kuwa ili niwe salama ni lazima nisijue kwa sasa na hataki niingie kwenye shida wakati huu"



"Sasa kwanini hajaenda polisi hadi sasa?"



"Kasema amejikuta anasita kufanya hivyo na hajui wa kumwamini na pia anaamini watu walioko nyuma ya jambo lile ni watu wenye mitego mingi hivyo anaweza kuishia kubaya na ikizingatia watu wanajua keshafariki"



Boneka alivuta pumzi nyingi na kuzishusha kisha akasema

"Nadhani nahitaji kuongea nae na kama ataniamini basi nitampa askari makini asaidiane nae, nina marafiki wengi ni watu wa usalama watamsaidia" Boneka alisema na Nyamizi hakujibu kitu.


Nyamizi tangu afahamiane na Boneka hajawahi kujua lolote kuhusu Boneka kufanya kazi idara ya usalama, zaidi alijua mumewe ni mfanyabiashara na bilionea kijana.



Boneka akiwa kimya kabisa alimtazama mkewe ambae alikuwa amejilaza pembeni yake huku akiwa amepitiwa na usingizi.


Boneka alisimamisha gari na kwenda kufungua geti la nyumba yake na kisha akarejea na kuingiza gari ndani kisha akamwamsha mkewe.


Nyamizi aliingia ndani na kumwacha Boneka akijishugulisha kufanya hiki na kile kwenye gari.


Boneka alipohakikisha mkewe ameingia ndani alichukua simu yake na kwenda upande wa ujumbe kimtandao yani barua pepe na kufungua.


Alikutana na jumbe ambayo ilitoka kwa mtu ambae alitumia akiwa ofisini kwao.


"Upo bongo, kesho unakazi? Au kimekurudisha?" Ujumbe ule ulisomeka hivyo.


Alijua kabisa mtu yule alijua uwepo wake hapa Tanzania badala ya Nairobi kwenye fungate lake na ndio mana aliuliza "kimekurudisha?" yani nini kimekurudisha na pia aliuliza kama kesho atakuwa na nafasi, hiyo inamaanisha anahitajika ofisini.


Aliujibu!!



"Msitari mwekundu unaelea kwenye kina kirefu" kisha akautuma na ajabu aliona mpokeaji yupo hewani.


Mpokeaji nae alisoma na alielewa ya kuwa "Mstari mwekundu" ni hatari inayoonekana na "Kina cha bahari" ilimaanisha siri kubwa ya wenye nguvu, hivyo mpokeaji nae akatuma tena ujumbe mwingine


"Basi itakuwa ni Tarasi, Tandara kwenye nyuzi moja"


Boneka alipokea na kuusoma akelewa.


"Tarasi" inamaana katika lugha ya kijasusi ni moja na "Tandara" ni mbili na "Nyuzi" ni kazi.



Hivyo alijua mtumaji amemaanisha hiyo hatari alioona ni moja na hatari ya pili ipo ofisini na wanatakiwa wazifanyie kazi zote, hivyo ni kumaanisha kazini kwake pia kulikuwa kuna kazi inaendelea na ikiongezeka ya kwake basi itakuwa ni kazi moja itakayogawanywa..


Ujumbe mfupi wenye mana kubwa.



Boneka akaingia ndani kwake huku akijua ahsubuhi anatakiwa kwenda ofisini kwake.



Ahsubuh hiyo ndio kikawa chanzo cha jambo lingine jipya kwa pande zote.


***


-----------


Ahsubuhi ilimkuta Boneka akijiandaa kwa ajili ya kutoka kwenda ofisini kwake,licha ya mkewe kumzuia hapa na pale ila mwishoni alitoa sababu ambazo ingekuwa si rahisi Nyamizi kumkatalia.


Alipomaliza kufunga tai yake akainama na kumbusu mkewe ambae alikuwa amelala chali akimtizama.


"Relax my love" Boneka alimwambia mkewe kisha akachukua mkoba wake na kutoka.


Safari yake ilimfikisha hadi karibu na viwanja vya Gymkana, akashuka kwenye gari na kushika kichwa mara mbili kisha akatokea kijana mmoja na bila kuuliza akapanda kwenye gari aliofika nayo Boneka na kuondoka nayo. Boneka akaanza kutembea kwa miguu na wala hakupiga hatua nyingi ikatokea gari yenye vioo vyeusi na kusimama, alipanda na safari ikaanza.


Ndani ya gari hakukuwa na mtu mwingine zaidi ya dereva na kawaida huwa dereva hasalimiani ni abiria wake na wakisalimiana basi kutakuwa kuna tatizo na linahitaji ufumbuzi wa haraka.


Safari yao ilikuwa ni ya kimywa hadi walipofika kwenye karakana moja ya magari mabovu; gari ikaingia na kisha Boneka akashuka na gari iliomfikisha pale ikaondoka.


Pale akaingia sehemu maalumu akabadilisha nguo na kuvaa fulana nyeusi na suaruali ya jinzi kisha akapanda pikipiki kubwa na kuondoka hadi posta,akapaki na kuelekea kwenye ofisi za chuo cha fedha, hakupanda kuelekea ofisini badala yake alipita upande mwingine na kutokea kwenye nyumba nyingine nzuri na ya kifahari huku kwa mbele kukiwa kuna milango ya biashara.


Ilikuwa ni ngumu kujua ile ni ofisi ya kitengo muhimu na si nyumba ya bilionea yeyote hapo mjini na hata wapangaji wa milango hiyo hawakuwahi kumuona mmiliki zaidi ya kuelekezwa akaunti ya kulipia pango kila muda unapofika.


Na kila mfanyakazi aliehusika na ofisi hiyo ili afike hapo ni lazima apitie njia kadhaa ambazo ni lazima akutane na vijana wa ofisi ile ambao ni maalumu kwa kufuatilia nyendo ili kuwa na uhakika wa safari yake bila kufuatiliwa lengo likiwa ni kulinda usiri wa ofisi ile nyeti.


****


Boneka alijikuta ni yeye peke yake aliekuwa amechelewa kuwasili.


Vijana wote waliotakiwa kuwapo ahsubuhi ile walikuwapo, akiwemo Ziga; Zedi na Haji Makame huku Mwinyi Kisoda na Kobelo wakiwa wapo mbali na nchi hii kwa kazi maalumu pia. Honda alikuwa bado anaugulia hospitali na hali yake iliridhisha.



"Ndoa tamu, yani siku mbili tu umenona shavu aisee" Haji alimtania Boneka na wote walijikuta wakicheka kwa furaha huku wakipeana mikono.


Baada ya utani wa hapa na pale Zedi ambae alikuwa kiongozi wa timu ile aliwaomba waende chumba cha majadiliano.


Na walienda wote waliokuwa pale.


Faili kadhaa zilisukumwa upande aliokuwa amekaa Boneka na Boneka alizipitia kwa haraka haraka na aliona picha kadhaa za mabaki ya kitu kilichoungua, huku kukiwa kuna maelezo pia.


Alipomaliza kusoma aliinua macho na kuwatazama wenzie.



"Miezi kama mitano hivi nyuma,kulitokea ajali ya ndege ya shirika letu, ambayo ilikuwa ikitoka Dar kwenda Mwanza." Zedi aliweka kituo na kuwatazama wenzie kisha akaendelea..


"Na katika ndege ile kulikuwa kuna madaktari bingwa wa tiba za magonjwa ya akili na walikuwa wamepata dawa ya kutibu vichaa ambao huwa hawatibiki na walienda huko kwa ajili ya uzinduzi wa dawa hiyo; lakini bahati mbaya ndege yao ilipotea kwenye rada dakika chache tu baada ya kupaa na baada ya siku mbili ilipatikana ikiwa imeanguka kwenye pori la la akiba la Inara huko Njombe" Zedi akameza kidogo mate na kuwatazama wenzie na aliporidhika na usikivu wao akaendelea.


"Mwanzo tulihisi ni ajali ya kawaida ila kuna mambo yaliofanya hadi jambo hili lilifika mezani kwetu badala ya vyombo husika. Ndege hii ilipasuka vipande na watalamu wanasema ilipasuka kwa bomu dogo lililokuwa ndani ya ndege, lakini pia kibokisi cheusi (black box) cha kufuatilia mwenendo wa ndege na kurekodi kilipotea na hakikuonekana, lakini kubwa zaidi ni kuwa ulipatikana mwili mmoja tu wa rubani na miili ya matabibu watatu haikuonekana ilipo hadi leo, hii inamaanisha hawakuwemo ndani ya ndege" Zedi alisema na kuwatazama wenzie ambao bado walikuwa wanamtazama kama hawamjui.


"Guys;swali la kujiuliza hapa ni kuwa watu hao wapo wapi? Bomu lilitegwa saa ngapi na kwa nini mawasiliano yalikatika?" Zedi alihoji.


Watu wote walikaa kimya kila mmoja akitafakari lake.


Boneka akainua macho!


"Afu hii ni ndege binafsi na kama ingeruka kutoka Dar basi ili ifike mwanza bila kituo ingepita anga la Dodoma sio?" Boneka alihoji na hapo wote wakamtazama, aliongea kitu muhimu sana ambacho mwanzo hakikutiliwa maanani..


"Sasa anga la songea ilifuata nini? Na tena karibu na Nyasa huko kama ukilifuata hilo pori bila kwenda songea!" Boneka aliongeza tena.


"Inashangaza kidogo hii" Ziga alidakia huku akiandika kwenye karatasi.


"Hapo napo kuna ukakasi mkubwa si mchezo" Haji aliongeza huku akiweka mikono kichwani.



"Hili linachanganya na ninaomba tuliweke pembeni kidogo na tusikie jambo jipya kutoka kwa bwana harusi mana nae jana usiku alinidokeza kitu" Zedi alisema na wote wakamgeukia Boneka.


"wiki hii kila mtu anajua tukio gani lilikuwa linatikisa jiji; Boneka alikuwa anaoa. Lakini wakati wa kurudi kuna watu walipiga kelele kuhusu kujirusha kwa mtu ndani ya maji na taratibu za uokozi zilipofanyika alionekana ni binti ambae namfahamu mana ni rafiki wa kufa na kuzikana wa Mke wangu anaitwa Vedi." Boneka aliguna kidogo kurekebisha koo kisha akaendelea.


"Taarifa zile zilisambaa sana kama moto wa kifuu na picha zilisambazwa kila pahali na msiba ukawekwa kwao na mimi na mke wangu tukarejea nchini...jamani mwenzenu sikufaidi siku saba" Wote wakacheka kwa utani ule wa Boneka kisha utulivu ukarejea na Boneka akaendelea.


"Tulipofika nchini moja kwa moja tulienda msibani na nikaonana na wafiwa, ila mama mwenye mtoto alinambia kuwa hana imani kama mwanae kafariki, aliongea kwa hisia,nami nikaona siwezi kupuuza nikampigia mwenyekiti kamati ya mapokezi, akanipa orodha ya watu wote waliongia na kutoka, ajabu jina la Vedi lilisaini kuingia na kutoka na mwandiko ulithibitishwa na mke wangu ila jina moja liliingia tu na halikutoka nalo ni jina la binamu wa mke wangu na tulipofuatilia tuligundua kweli hajarejea nyumbani tangu alipoaga anakuja harusini kwetu. Ajabu sasa jioni ya jana Vedi alipiga simu na alionana na mke wangu na mimi nilionana na kibaraka mmoja anaefutilia nyendo za yule binti na bahati mbaya alinitoroka na kwa taarifa za awali inaonekana kuna jambo linaendelea ndani ya ile kampuni ya meli" Boneka alihitimisha.


"Kwa hiyo huyo Vedi kasema nini hadi sasa!" Zedi alihoji.


"Alikataa kumwambia lolote mke wangu kwa kuhofia kumwingiza matatizoni." Boneka alijibu.


Walijikuna vichwa.


Upele ulipata mkunaji, ila wakunaji nao walijikuna vichwa.


Kesi ngumu mezani kwao.


Kitu ambacho hawakujua ni kuwa adui wa kesi zote hizo ni mmoja.


Ni nani sasa?





Tatizo linakuja ni nini sasa kinaendelea kwenye ile meli na je tangu wahusika wagundue kuna mtu kaona siri yao bado wataendelea kufanya makosa?" Haji aliwauliza wenzie.


Hakuna aliemjibu.


"Nadhani unapaswa kuzungumza na shemeji yako vizuri ili tujue nini kinaendelea" Zedi alimwambia Boneka na Boneka alitikisa kichwa kukubali.



"Turudi sasa kwenye hili suala la hii ndege iliodondoka na tujue ni kitu gani hasa kilifanyika hapa na wako wapi hawa madaktari bingwa na tegemezi kwa familia zao" Ziga aliwakumbusha wenzie.


"Jamani tangu Chief aliponipa hii kazi, kabla sijawafikishieni, tayari nilikuwa nimepita huku na kule na tayari kuna mambo machache nilikuwa nimeyabaini" Zedi alichukua kitabu chake kidogo cha kumbukumbu na kukifunua kurasa kadhaa kisha akakipitia kidogo na kusema

"Nilifika hadi uwanja wa ndege na kutaka kujua safari ile ni nani alikuwa rubani, nikapewa jina la rubani Mbondya na nilijaribu kumfuatilia na kugundua anaishi Ilala na nilifika hadi kwake, ajabu nilikuta familia yake na niliambiwa yupo ila ametoka muda si mrefu!,sikutaka kumsubiri nikaondoka na nilikutana pia na baadhi ya wanafamilia wa matabibu wale ila familia moja ilikuwa na majibu ya mashaka kuhusu hali ya muonekano wa ndugu yao siku za karibuni." Zedi aliwatizama vijana wake tena na kuona usikivu wa hali ya juu.


"Mke wake alinambia siku za karibuni mumewe hakuwa katika hali ya kawaida, alikuwa ni mwenye mashaka mengi na hakuwahi kumwambia lolote isipokuwa alimwambia endapo polisi wakifika kwake siku moja basi awambie hali yake ya mashaka siku za karibuni." Zedi alimaliza kuwambia wenzake na kila mmoja alijisawazisha kwa namna yake alioiweza ili kuipa akili yake utulivu wa maamuzi.


"Hapa inabidi apatikane huyu rubani Mbondya ili tujue kilitokea nini hadi hakurusha ndege wakati yeye ndie alieandikwa kama mrushaji wa ndege ile" Ziga alisema na hapo kila mmoja alikubaliana na mwenzake kuhusu suala hilo la kumtafuta Mbondya.



"Okay! Hapa inabidi zifanyike kazi mbili, hiyo ya kwanza ya iwe hii na nitaifanya mwenyewe" Alisema Zedi huku akikusanya faili zilizokuwa zimetapanywa mezani.


"Na hiyo kazi ya kifamilia inabidi ifanywe na Boneka na Wewe Haji unajua unachopaswa kufanya hapa ofisini na wewe Ziga utaendelea kushugulika na hali ya Honda hospitalini ila pia utakuwapo kwa ajili ya msaada wa dharura ukihitajika,ngoja mimi na bilionea kijana tuingie mzigoni ili chief roho yake itulie." Zedi alitoa maagizo kisha wenzie wote wakakubaliana na kusambaratika kila mmoja akienda kwenye jukumu lake alilostahili kulishugulikia.



****


Boneka baada ya kutoka kwenye ile ofisi alielekea kwenye maegesho ya kulipia posta na kwa mbali aliona gari lake likiwa limepaki pale nae akaenda kulichukua huku akijua kila kitu kipo na garama za maegesho zimeshalipwa. Alipanda kwenye gari na kabla hajawasha alimpigia simu baba yake na Vedi na alihitaji kujua hali ya mkewe na alipoambiwa bado ni mbaya aliamua kuuliza utaratibu wa mazishi na wapi ilipo maiti ile.


Alipata jibu la kushangaza kidogo.



"Mwanangu kuna mambo yanazidi kumchanganya hapa" Alisema mzee Mashimo.



"Kivipi tena mzee!" Boneka alihoji.


"Hapa jana wale polisi waliochukua mwili wa mwanangu walisema wanaupeleka Muhimbili lakini ajabu ni kuwa leo naambiwa umepelekwa Mwananyamala na bila maelezo muhimu, kule ni mbali mwanangu na sijui kwa nini haukuachwa muhimbili" Mzee Mashimo alilalama.



"Ok! Yawezekana askari wenyewe wanajua sababu zao! Ila nakuomba kwa sasa sitisha zoezi la msiba na usubiri nitakuelekeza jambo badae na nitagarimikia mimi mambo yote, kikubwa Mama apate ahueni na aje kumzika mwanae," Boneka alimwambia Mzee Mashimo kisha wakazungumza mambo mawili matatu na Boneka alikata simu na bila kusubiri alipiga tena sehemu nyingine.


"Koplo imekuwaje tena" Boneka alimuuliza koplo Maganga ambae aliongoza wenzake kuuchukua mwili wa mtu aliefanana na Vedi na kuupeleka muhimbili.



"Ebana ee mi sijui kilitokea nini ila baada ya wewe kupiga simu na mimi kuja pale kuichukua maiti wala hatukufika hata hiyo muhimbili yenyewe tulikutana na gari la maaskari pale Tazara na tukaamuliwa kuwapa wale askari tulipkutana nao na tulipouliza tuliambiwa ni maagizo kutoka juu" Koplo Maganga alimwambia Boneka.


Boneka akashusha pumzi na kusema

"poa koplo fanya kazi yako nikikuhitaji nitakutafuta kwa maelekezo zaidi" Kisha akakata simu.


"Hili sasa ni tatizo kama lina maagizo kutoka juu, juu kwa nani sasa!" Boneka alijihoji mwenyewe huku akitoka kwenye maegesho...



Alipanga kuelekea Mwananyamala alihitaji kufanya uchunguzi kwa njia alizozijua ili apate kujua ilikuwaje yule mtu afanane na Vedi kiasi kile na kwa nini asipelekwe sehemu nyingine zaidi ya kwa Mzee Mashimo.



Safari yake hiyo iliibua tena jambo jingine ambalo hakulitarajia.



****



Vedi aliamka ahsubuhi na mapema ili afanye usafi na kisha aelekee sehemu ile ya Hard Rock Cafe kumtafuta Jezebeli mana aliamini kabisa Jezebeli ni mtu na atakuwa yupo pale mgahawani.


Ila hakujua ni kwanini mke wa marehemu Banzi alitazama kaunta kwa woga baada ya kutamkiwa neno Jezebeli. Je hapo ndipo ilipo hiyo Jezebeli? au huyo Jezebeli ni kitu gani au ni nani hadi Banzi amtaje kwenye kitabu chake?



Bado alimuona Jay hayupo sawa na hakutaka kuongea nae chochote ili kumpa muda zaidi pengine nae angesema kinachomsibu hadi kukutana na dhoruba ya kipigo namna ile.


Simu yake ilikuwa ikiita mara kwa mara na aliekuwa anapiga ni Nyamizi ili kujua anaendeleaje.


Tatizo Vedi hakujua ni kuwa kila alipopigiwa na Nyamizi; Jay nae alikuwa anaandika ujumbe kwenda kwa Gomba.


Na Gomba alipopokea ujumbe aliuliza Nyamizi ni nani na aliambiwa ni mke wa billionea kijana Boneka.



Gomba na Panga wakataka kujua kilichonyuma ya urafiki wao, wakaanza kutafuta taarifa muhimu kuhusu Nyamizi na kwa bahati mbaya hakuna walichokipata zaidi ya kuambiwa ni mhitimu wa chuo kikuu Dar.


Ila kazi yao haikuwa bure, walipata picha za mume wake..


Gomba alibaha baada ya kuzitambua.


"Ayaa huyu bwege ndo aliniotea jana usiku ujue" Gomba alihamaki.


"Sasa na urembo wote wa huyu jamaa alikuoteaje!" Panga alikebehi.


"Aisee yule jamaa ni mjuzi wala sio muoteaji, ni mwepesi na ngumi zake zinaujazo wa kimazoezi sio mrembo kabisa!" Gomba aliongea kwa upole huku akitafakari.


"Sasa kwa nini akuvamie? Alijua lolote au ni kwa kuwa aliona unamtazama mkewe?" Panga alihoji.


"Sina hakika kama alinivamia kwa wivu, yule jamaa alikuwa anajiamini sana na alikuwa anataka kitu zaidi kuliko kunililia wivu wa kumfuata mkewe" Gomba aliendelea kutafakari huku akimhabarisha Panga mawazo yake.


"Kwa hiyo anaweza kuwa ni mtu wa sisitimu?" Panga nae alizidi kuhoji huku mzaha ukiwa pembeni.



"Sina hakika ila kitendo cha kumuona Vedi wakati nyumbani anajua kuna maiti ya Vedi ni lazima kutampa maswali na kwa pesa yake anaweza kuleta watu wakatuadabisha..lakini yule jamaa ni zaidi ya bilionea aisee!" Bado Gomba alizidi kupambana na hisia zake.



"Kwa hiyo unasemaje?" Aliuliza Panga.


"Tumshirikishe Cholo afu nadhani inabidi Vedi auwawe kiukweli sio tena maigizo" Gomba alisema.


"Na vipi kuhusu huyu mchumba bilionea mwenye sura ya kike!" Panga alihoji.



"Tujue kwanza nyendo zake kisha tutampeleka akasilimie wafu kwanza" Gomba alijibu huku akisoma ujumbe kutoka kwa Jay.


Wanapanga kuua ila hawajui moto wa mtu wanaetaka akasalimie wafu umeshaunguza mifupa mingi hata isiotafunika. ..



Wataweza?





Gomba aliendelea kusoma ujumbe wa Jay na tena akamgeukia Panga.


"Hivi huyu dogo bado anatufaa kweli!" Gomba alihoji.


"Bado kidogo, acha tujue nyendo za yule mtoto wa kahaba afu nae tutampa zawadi yake, hatuzoeleki sisi" Panga alisema huku akipokea simu iliokuwa na ujumbe wa Jay.



----------


Vedi aliendelea na kushika hiki na kila na alipomaliza akamuita Jay mezani kwa ajili ya kupata stafutahi na kisha kila mtu aendelee na mambo yake.


Wakiwa wanaendelea kula mara simu ya Vedi ikaita na alipoangalia mpigaji ilikuwa ni namba ngeni ila aliifahamu, ilikuwa ni namba ya shemeji yake Boneka.


Walisalimiana na kujualiana hali kisha Boneka akasema...


"Shemeji badae nitakuwa na mazungumzo na wewe ila naomba tukutane hapo hapo nyumbani kwenu na pia jitahidi usitoke kwa usalama wako"



"Kuna sehemu nilitarajia kwenda ila nitajitahidi kuwahi na utanikuta " Vedi alijibu..



"Ulitarajia kwenda wapi kwani!" Boneka alihoji kwa umakini sana.


"Kuna mtu wa muhimu nilitaka kwenda kumuona hapo Hard Rock Cafe ila nitawahi" Vedi alijibu.



Walizungumza kidogo kisha wakaagana.


Jay ambae muda wote alikuwa kimya aliinua macho na kumtazama Vedi.


"Vedi hivi ukisikia nimekufa leo au kesho utafanya nini?" Jay alihoji kinyonge huku nafsi yake ikiwa na mabishano makali kuhusu mustakabali wa maisha yao.



"Nadhani ulipaswa kujiuliza ni kwanini ulinifukuza na kunipa tuhuma ila bado nipo hapa kwako najizungusha lakini pia ungejiuliza ni kwanini hujarudia tena kunifukuza baada ya kukomaa kukaa hapa kwako hivyo ukipata majibu basi huna haja ya kuniuliza hilo swali" Vedi alisema kwa hisia jambo ambalo lilimchoma Jay na hakuwa na cha kufanya. Watesi wake walimshika kubaya, alihitaji tiba ya kansa ya kuambukizwa. Likini bado Jay alijiuliza atakaa nalo moyoni hadi lini na ataendelea kumsaliti mchumba wake hadi lini. Hakupata jibu. Akatazama ukutani akaona masaa yanazidi kusogea na alianza kuhofu kuhusu dawa za kulevya alizopewa usiku uliopita ni vipi kama zitahitajika, atazipata wapi ili kujinusuru na vipi Gomba na wenzake watarejea kumpa dawa na vipi kama wakimkuta Vedi watamfanya nini?



Jay alidondosha chozi bila kujijua.


"Mpenzi najua unapitia magumu kuliko hata mimi, lakini unapaswa kunishirikisha na mimi nikushirikishe ili tujue tunaokoka vipi...Jana nilikuta umepigwa na udhoofu wa mwili na juzi nilipofika ulinifokea kama mtoto bila sababu huku ukinisingizia mambo yasioyo kuwepo, ni kipi hasa kinaendelea?" Vedi bado aliongea kwa hisia kubwa.


Jay aliyapokea maneno yale kwa uchungu mkubwa huku akishindwa kujua aanzie wapi kusema neno lolote.


Nafsini mwake alikuwa anajiuliza ni kipi afanye, alinde siri ama aanike kwa mkewe mtarajiwa watatue?


Mara akakumbuka mkwara aliopigwa na Panga kuhusu lolote atakaloliongea basi wao watalisikia popote walipo.


"Watch your back" alijionya.


"bado muda upo tutazungumza ngoja kadhia yako ipite kwanza" Jay alisema huku akinyanyuka na kuelekea chumbani.


Vedi alibaki akimtizama tu bila kusema lolote lile.



----------


Boneka aliegesha gari sehemu ya kuegesha magari nje kidogo ya majengo ya hospitali ya Mwananyamala.


Aliangaza kushoto na kulia ili kujipa uhakika wa mazingira kisha akashuka kwenye gari na kuelekea sehemu ya kusaini kwa wageni wanaoingia na akaandika alikotaka kuelekea.


Alipomaliza alielekea yalipo majengo ya kuhifadhia maiti.


Hakutumia dakika nyingi akawa amefika kwenye ofisi husika.


Akaeleza shida yake na akaomba kuona mwili wa mtu alieitwa Vedi Mashimo.


Walinzi wakaangaliana kisha mmoja akamjibu..


"Tumezuiwa kuutoa huo mwili au kuonesha ni hadi kwa kibali maalumu kutoka ngazi za juu"


Boneka alielewa nini mana ya kauli ile akakubali na kuanza kuondoka..


Lakini wakati anatoka nyuma yake alisikia kuna harakati zinaendelea, akageuka kutazama


Aliona majeneza mawili yakitolewa na kisha akaona yakipakizwa kwenye gari moja.


"ina maana waliokufa wanaenda kuzikwa pamoja au!" ajabu nyingine aliona wamama wawili tu na jamaa mmoja ndio walolioonekana kuwa wafiwa au watu wa karibu na marehemu wale.


Jamaa yule alikuwa amevaa kofia ya pama na miwani huku akipigilia na koti na suruali ya jinzi na viatu vya buti.


Zilifanyika harakati chache kisha safari ya magari matatu ikaanza huku gari la mbele likiwasha taa kuashiria kuna tatizo katika msafara ule.


Boneka akatembea haraka kuwahi gari lake huku lengo lake likiwa ni kuwahi msafara ule na hata yeye alijishangaa ni kwanini aliamua kuutilia shaka msafara ule.


Ukiachilia mafunzo ya kijasusi kutumia milango mitano ya fahamu; yeye aliamua kutumia na kuheshimu mlango wa sita wa fahamu ambao ni "machale".


Katika kozi ya utambuzi wa viashiria vya hatari basi mlango huo wa sita ulikuwa ni muhimu sana na hakupaswa kupuza.



Akawasha gari lake na kuanza kufuata nyuma.


Msafara ule ulielekea barabara ya Makumbusho.


Kabla hawajafika kona ya kuingia kituo cha magari ya abiria; Boneka aligundua kuna gari lipo nyuma yake na yawezekana alifuatwa yeye au lilikuwa ni gari ambalo lilihakikisha usalama wa ule msafara.


Akachukua simu yake na kutafuta jina fulani kisha kwa kutumia mkono mmoja aliandika ujumbe mfupi na kisha akaendelea na safari.


Walitokea barabara ya kawe na aliona msafara ule unaelekea kulia kama waenda kawe, yeye akaelekea Mwenge na kwa kutumia vioo vya kuangalia nyuma aliona lile gari lililokuwa nyuma yake ni kama limeshindwa pa kuelekea.


Boneka akatabamu.


"Hawa hawajui usuvailensi nimeufanya kabla sijafakia hiki kitengo, ngoja sasa mabingwa wa kazi wawafuatilie hadi mwisho tuone" Alijisemea huku akimalizia kuandika ujumbe kwenye simu kuelekeza njia ulikoelekea ule msafara.



"Kwa nini wamezuia ule mwili kutazamwa? Na kwa nini hakuna hao maaskari?" Boneka alijihoji.


Akiwa bado yupo kwenye foleni mara ujumbe ukaingia na alipotazama aliona moja wa kijana aliemtuma kufuatilia msafara ule ameandika ujumbe mfupi tu



"Hard Rock Cafe!" ilimaanisha ulielekea hapo na pia alikumbuka Vedi alimwambia nae anaelekea hapo.


E bwana ee!..



Boneka alichemkwa na damu huku akili ikimtembea kwa kasi, alihitaji kufanya kitu, ila mbele foleni kubwa ya magari na nyuma pia kuna mshono wa magari, atachomokaje na hakuona pa kupaki ili atumie usafiri wa boda boda.


Mh!!!!




Akiwa bado ana mazonge mazonge kuhusu kile alichokisoma;mara ujumbe mwingine tena ukaingia na ulitoka kwa kweli kijana wake ambae alimpa kazi ya kufuatilia mienendo yote ya msafara ule.



"Hapa haujakaa sana....loading" hiyo ilimaanisha msafara ule haukukaa sana pale na sasa kuna sehemu unaelekea.


Boneka alishusha pumzi kwa afueni huku akipanga kufanya kitu ili ajue linaloendelea hapo Hard Rock Cafe.

.


Akatazama muda na kuonesha ilisalia saa moja muda wa kuonana na Vedi ufike.


Akatulia kwenye kiti kusubiri foleni isogee..



*****



Zedi baada ya kutoka ofisini kwao,nae hakutaka kulala na kusubiri kujua undani wa ajali ya ndege ilipotea na matabibu na wagunduzi wa tiba ya magonjwa ya akili.


Lengo kubwa walihitaji kujua kilipo kibokisi cheusi ambacho hurekodi mwenendo wa safari ya ndege. Kilikuwa hakionekani kilipo na haikujulikana kama kilipotea makusudi ama bahati mbaya na watafutaji hawakuwa makini wakati wanakitafuta.


Bado alihitaji kujua ni kwanini rubani alietakiwa kuinyanyua ndege awepo na aliekuwa kwenye ndege awe mwingine. Hilo lilikuwa linahitaji ufafanuzi na hakuna wa kufafanua zaidi ya Mbondya mwenyewe.


Alipiga moto pikipiki yake kubwa na kutumia njia zisizo rasimi na hatimae alijijuta tena amerejea nyumbani kwa rubani Mbondya jirani na shule ya msingi Ilala.


Akashuka kwenye pikipiki na kuiacha kwenye maegesho ya jengo la Nssf mafao, kisha akatembea kwa miguu hadi shuleni na akasimama kutazama upande ambao nyumba ile ilikuwa.


Akavuta hatua na kulifikia geti, kisha akabonyeza kitufe cha kengele na kusubiri.


Punde geti likafunguliwa na akakaribishwa ndani na Mama mtu mzima.


Ilikuwa ni nyumba kubwa ambayo ilistahili kuitwa ya kisasa.


Mama akataka kumpeleka ndani ila alikataa na kuomba wakae kwenye korido ya kupumzika na kulikuwa kuna sofa mbili ambazo zilianza kuchakaa.


Zedi alikaa baada ya mwenyeji wake kukaa.


"Karibu baba!" Mama alivunja ukimya.



"Bila shaka hapa ndio kwao na Mbondya!" Zedi alihoji.



"Ndio baba!"


"Mbondya ameoa?" Zedi alihoji huku akimwonesha kitambulisho bandia yule mama na kitambulisho kile kilimtambulisha kama ni mfanyakazi wa uwanja wa ndege.



"Kwani hajawahi kukwambia!" alihoji Mama..



"aah wapi mama jamaa ni msiri wa mambo yake hatari ni ngumu kujua kama kaoa au la!"



"Bado hajaoa licha ya kumshinikiza sana afanye hivyo, si waona umri wangu hivi sasa nahitaji nipate mjukuu tu." yule mama alianza kujibu kwa kumzoea Zedi na Zedi alitambua yule Mama ni mtu wa kusini kulingana na lafudhi yake.



Zedi akaona akiuliza maswali mengi yule Mama atahoji kulikoni, hivyo akaamua kutumia akili ya kijasusi kupata kile alichokitaka.


Akaingiza mkono mfukoni na kutoa bahasha ndogo na kumpa yule Mama.



"Akija mpe kadi yangu ya harusi na yeye akisoma atajua tu!" Mama akaipokea na kutabasamu..


"Yani vijana mnazidi kuoa tu huku mwenzenu yeye ni kuponda raha tu, hongera mwanangu" Yule Mama alisema huku akiipokea ile bahasha.



"Kwani anapenda sana kujirusha kweli mbona kama hatujawahi kuona hayo mambo kwake hata tukiwa na safarini?" Zedi alijikosha kwa lengo la kupata kile alichohitaji kutoka kwa Mama yule.



"Unajua yule mtoto nimemlea na kumsomesha kwa shida na wakati wote huo hajawahi kuonesha tabia mbovu hadi wakati huu ambao ameanza kupata pesa, amekuwa hanisikilizi kabisa na amekuwa akiambatana na marafiki wa ajabu tu, na kila mara amekuwa na safari ambazo hazina mpango tofauti na zamani anbapo safari zake zilikuwa kwenye ratiba wakati wote, ila siku za hivi karibuni amekuwa mlevi sana..... Mh!" Yule Mama alimalizia kwa kuguna kwa masikitiko huku akionekana dhahiri kuumia kwa tabia ile ya mwanae kipenzi.



"Ooh pole sana Mama, kwani kwake ni wapi au anaishi hapa?" Zedi alihoji kijanja lengo likiwa ni kujua hasa ni wapi atampata Mbondya.



"Hapa siku hizi ni mara chache sana kuja, japo ni lazima aje, ila kwake sio mbali na hapa ni hapo nyuma tu, yani ukitoka kwenye hilo jengo refu yeye anaishi kwenye nyumba inayofuata karibu na barabara.


Zedi alimpigisha soga za hapa na pale kisha akaaga na kuondoka na huku akiwa amejua makazi rasimi ya yule jamaa na safari yake ilikuwa ni kuelekea huko.



Hakuhangaika kutumia usafiri, bali alitembea kwa miguu tu kisha akapita jengo la Nssf na kwa mbele aliona nyumba alioelekezwa ikiwa imezungukwa na miti michache tu mirefu ambayo haikuleta kero barabarani na majirani wake.


Akavuta hatua na kuachana na milango ya biashara, hadi kwenye geti lililoonekana ndilo linalotumika kuingilia.


Akalisukuma baada ya kugundua lipo wazi.


Akaingia na aliona haikuwa nyumba kubwa ni ya kawaida tu iliopaswa kuishi kijana mwenye umri sawa na wake..

.

Kulikuwa kuna gari moja nyeusi iliokuwa imeegeshwa karibu na mlango wa kuingilia ndani.


Sauti kubwa ya muziki ilisikika na hiyo iliashiria wenyeji watakuwepo.



Akapiga hatua za kujiamini na kugonga mlango mara kadhaa bila kuitikiwa na aliendelea kusikia kelele za muziki.


Akasukuma mlango na kuingia huku akiwa makini sana.


Macho yake yakatua kwenye sofa na kuona binti akiwa amelala na kanga moja tu sofani.



Yule binti aligeuza shingo kivivu na kuona kuna ugeni ambao hakuutarajia..


Akanyanyuka kihasara hasara bila kujali kama kanga yake inaanguka ama la..



Macho ya Zedi yalitembea kwa kasi ya kimbunga na kwa haraka aliona picha za Mbondya akiwa amevaa mavazi ya kikazi na tabasamu murua usoni.


Macho yake akayarejesha kwa yule binti, na hapo akagundua vile yule dada alivyokuwa akimtizama kwa kiulizo.



Lakini sura ya yule dada ilisadifu hali fulani isio ya kawaida, uso wa yule binti ulianza kupoteza nuru ya uzuri wa asili na tayari kulianza kuonekana athari za utumiaji wa vilevi kupitiliza au uraibu wa dawa za kulevya au pombe kali.



Zedi alikaa taratibu huku yule dada akiwa hajahangaika hata kupunguza sauti ya radio iliokuwa juu kupitiliza na ilikera kusikiliza.


Mezani aliona kitenzambali(rimoti) akachukua na kupunguza sauti ya radio kisha akauliza.


"Mbondya nimemkuta?"



Yule binti alitikisa kichwa kukataa..



"Yupo wapi kwani!"

Zedi alihoji tena.



"Kwani umeenda Hard Rock Casino umemkosa?" yule binti alijibu kwa swali huku akipinda midomo kuashiaria alikereka na swali hilo.



"Kwani ndo anakopatikana siku zote!" Zedi alihoji.




"kwani wewe wa wapi hadi uusijue bwana Mapesa yupo huko muda huu, wewe mgeni hapa mjini bila shaka!" yule binti aliongea kwa kushushua.


Zedi alielewa yule dada ni kahaba wa mjini ambae hana nidhamu wakati wa kuongea.


Lakini alijiuliza tangu lini rubani hugeuka kuwa bwana mapesa?


Alimtizama yule binti kwa tuo kisha akawaza kufanya jambo pale ndani.


Akasimama na kutoa pesa mfukoni kiasi cha laki moja hivi na kumpa yule dada.


"Nimekutamani, naomba unichetue kidogo niondoke basi!" Zedi alisema huku akisogeza zile pesa.


Yule dada akasimama huku akiacha kanga yake ikianguka bila kujali na kubaki mtupu huku akijichekesha kibwege.


"Au bwana Mapesa kakutuma unijaribu wewe" yule binti aliongea huku akizipokea zile pesa.


Zedi akamsogelea na kuwa kama anataka kukumbatia hivi,ila kwa kasi akampiga kwa kutumia upande wa kiganja karibu na sikio na yule binti alilegea na kupoteza fahamu.



Zedi akamlaza kwenye sofa kisha akamfunika na kanga na kisha akazima radio na kisha akaanza kupekua hapa na pale.


Aligusa kila mahali ndani ya sebule ile bila kupapata chochote.


Akaamua kuelekea chumbani huku tahadhari ikiwa mbele kama tai.


Akasukuma mlango na kuingia.


Alikutana na chumba safi chenye samani za kisasa hasa kitanda na kabati.


Alitizama hapa na pale na akaona suruali ya kike ikiwa imetupwa chini, bila shaka ilikuwa ni ya yule binti.


Akaikota na kuikagua mifukoni.


Alitoka na vitu viwili ambavyo havikumpa shida kuvifahamu.


Kimoja kilikuwa ni kete ya unga wa dawa za kulevya, lakini kingine ilikuwa ni kadi ya kuingilia casino na pia kulikuwa kuna jina la kasino ile.


"Hard Rock Casino"


Akavirudisha kwenye suruali na kuiacha chini.


Alikagua hapa na pale na hatimae aligota kwenye droo ya kitanda.


Ikamgomea!


Akaichunguza vyema kisha akatoa funguo moja kwenye mfuko wake, funguo ile haijawahi kushindwa kufungua kitasa chochote kile.


Akaipachika na kitasa kikaachia.


Macho yake yalikutana na kadi nyingine tena..

Akaisoma na kadi ile ilikuwa na majina mawili.


"Hard Rock Cafe na Hard Rock Casino" ilimaanisha mgahawa na kasino vyote ili uingie ni lazima utoe kadi.


Zedi aliguna baada ya kumaliza kusoma kadi ile na macho yake kuyarejesha kwenye droo ile.


Noti nyingi za dola ya kimarekani zilikuwa zimepangwa vyema kwenye ile droo.


Lakini pia aliona kitu kingine cha ziada...


Aliona visa ya kusafiria ikiwa imeambatanishwa na pesa zile.


Akaivuta kutoka nayo, akaisoma na kuona nchi kadhaa ambazo mbondya alitarajia kuzifikia ama visa ile ilimruhusu kuzifikia. Lakini alipondelea kukagua aligundua Mbondya alipanga kusafiri siku chache mbili zijazo kwa kutumia ndege ya abiria na tayari alikata tiketi iloonesha anaelekea falme za kiarabu..


"Kaacha kazi?" Zedi alijihoji bila majibu.

.


Zedi hakutaka kwenda kwenye kampuni aliofanyia kazi Mbondya ili kujua kinachoendelea ili kuepuka kuharibu harakati zake.


Alichukua ile hati ya kusafiria kisha akaiweka mfukoni na akarudisha vitu kama alivyovikuta na kufunga kisha akatoka. Lengo likiwa ni kumharibia safari..


Hawezi kusafiri bila hati ile.


Zedi akatoka sebuleni na kukuta bado yule binti hana fahamu, akachukua pesa yake na kuondoka.


*****




***


Zedi alipitia kwenye maegesho akachukua piki piki yake na kuondoka huku kitu pekee alichokuwa anakiwaza ni Hard Rock Cafe na Hard Rock Casino.


Alihitaji kujua mengi kuhusu hizo sehemu lakini pia alihitaji kukutana na Mbondya p.a.k bwana Mapesa.


Kazi anayoifanya ni kazi ambayo ina pesa nyingi ila haiwezi kuwa kazi ya kumpa vibunda vile vya dolali na pia kazi anayoifanya msingi mkuu ni kutokuwa mlevi wa kila muda, hiyo ni kwa usalama wake na abiria anaowabeba pale anapohitajika, sasa ni ajabu kusikia Mbondya ni mlevi wa kupindukia hadi Mama yake analalama.


Lakini pia alijiuliza kuhusu aina ya mtu aliemkuta nyumbani kwa Mbondya.


Mtumiaji wa dawa za kulevya, lakini pia alikuwa na kete kwenye nguo zake na kikubwa yule ni kahaba.


Je Mbondya hakujua hilo au nae ni mtumiaji? Lakini kwanini safari iliomhusu hakwenda na kwanini bado hajaripoti kazini tangu kuanguka kwa ile ndege? na inaonekana muda wote hakusafiri, kwanini asafiri hivi karibuni sasa!


Yalikuwa ni maswali bila majibu.


Pikipiki iliendelea kuburuza barabarani.


Alijikuta anamhitaji sana Mbondya kuliko hata kumhitaji mtu alienyuma ya mchezo ule,mana kumpata Mbondya ni hatua kubwa ya kumfikia mtu alie nyuma yake.



****


Boneka alikuwa bado yupo kwenye foleni huku muda wa kuonana na Vedi ukiwa unakaribia..


Akasikia ujumbe ukiingia kwenye simu.


Akaufungua!

.


Ulitoka kwa Vedi na alimjulisha tayari anamsubiri.



Vedi nae baada ya kutuma ujumbe alienda chumbani kwa lengo la kujilaza kidogo ili walau apate kupunguza kidogo mawazo yake kwa kijiusingizi kitakachomchukua.


Mara Jay akaingia.



"Nilisikia una mgeni badae kidogo sio!" Jay alihoji.


"Ndio na anakuja muda sio murefu" Vedi alijibu.



"Ok sawa!" Jay alisema huku akitoka chumbani na kwenda sebuleni.



Jay alipokea ujumbe ambao ulimwelekeza ya kuwa ajitahidi Vedi asionane na Boneka na hiyo ni baada ya Jay kutoa taarifa ya Vedi kutembelewa na Boneka pale kwake.


Na alipokea ujumbe huo uliosisitiza ajitahidi wasikutane.



Atafanya nini, hilo ndilo alilohitaji kufanya na kujiuliza.



Aliona akimtaka watoke itakuwa ngumu sana kwake July alias akizingatia ya kuwa siku za karibuni wamekuwa hawana maelewano mazuri kabisa.



Akazidi kuwazua bila jibu.


Mara ujumbe ukaingia kwenye simu yake.


"Muda wa kupata dozi unakaribia, hivyo mwambie aje hapa nyuma ataona gari jeusi alifuate na atakuletea. Ila baada ya kuhakikisha huyo bwana katoka hapo" Ulikuwa ni ujumbe wa Panga.



Akimtuma kwa kawaida sio rahisi Vedi kwenda na atakuwa na kiulizo, jambo ambalo litasababisha Boneka amkute hapo.


Jay akaanza kujinyonga akiwa amekaa kwenye sofa, alijinyonga mithili ya mtu anaepitia mateso makali ya maumivu ya tumbo.



Alipoona juhudi zake hazimvutii Vedi; ikabidi atoe miguno ya maumivu na hila zake zilifanikiwa.



Vedi alisikia ile miguno, akatoka haraka ili kujua kulikoni.


Alikuta Jay anaugulia maumivu huku akiwa ameshika tumbo na kutumbua macho kama mgonjwa anaekaribia kukata roho.



"Shida nini tena jamani!!" Vedi aliuliza kwa mashaka huku akihangaika kumshika hapa na pale.


"Tumbo linaniuma sana na kitu kimebana kifuani" Jay alizungumza kwa tabu kidogo.


Vedi akakurupuka ili kuwahi kuchukua dawa za tumbo ambazo huwa wanaweka ndani kwa dharura.


"Tafadhali naomba nisikilize kwanza" Jay alimwambia Vedi baada ya kuona anataka kutoka na kumwacha.


Vedi akarejea kumsikiliza.



"Kuna jamaa zangu hapo nyuma wana gari jeusi, tafadhali nenda wambie waje mnipeleke hospitali"



Vedi hakutaka kusubiri, akatoka ndani mbio na kuelekea nje kuelekea usawa alioelekezwa.



Alipotoka tu, ni wakati huo ambao Jay alinyanyuka na kwenda chumbani kuchukua simu yake na kuwasiliana na Panga.


"Naombeni msifanye kitu kibaya huyo binti jama!" Jay aliwandikia huo ujumbe.


"Sasa kagua vitu vyake, kuna kitabu kidogo cha kumbukumbu, tunaomba ukichukue na utoke nacho nje" Panga alimwandikia Jay.



Jay akahaha kukitafuta hicho kitabu huku roho yake ikiwa inahangaika na kichwa chake kikipita kwenye tanuru la fikira kujua kitu gani wale jamaa watakifanya kwa Vedi.


Roho ilimsuta ila hakuwa na la kufanya, alihitaji kufanya linalowezekana ili Vedi asiingie matatizoni.



Atafanya nini wakati ameshamtuma kwa wabaya wake.


"ooh shiit!" Alijisemea huku chozi la usaliti likimdondoka,hakika alipitia hali ngumu.



Mikono yake inayotetemeka iliendelea kuhangaika kupekua mikoba ya Vedi.


Hatimae alikipata kitabu kile kikiwa kina kalamu iliobanwa pamoja nacho.

.


Akaanza kutoka ili akipeleke kama alivyoelekezwa.


Lakini alisita kidogo alipofika kwenye mlango wa chumba chake.

.


"Kama hiki nikiwapa ndo watatuua itakuwaje?".Jay alijiuliza bila kupata majibu..


Akajikuta akiwa na maswali mengi kuliko majibu,huku akiwa amekishikilia.

.


Akaamua kutoka ili apeleke!...



Kitu ambacho haukujua ni kuwa kikifika mikononi mwa Panga; wao watakuwa hawana thamani tena.


Hilo hakujua kamwe!

..


*****






****


Wakati anafungua mlango na kutoka sebuleni;alikuwa na haraka isioelezeka, alipita sebuleni kama hakujui.



Wakati anafungua mlango ili atoke nje, wala hakupiga hata hatua moja; uso wake ulikutana na mtu ambae licha kujua ujio wake ila si kwa uharaka namna ile.


Alikutana na Boneka!


Kwa kuwa alikuwa na haraka nyingi na pia alikuwa ana kazi ya kuhakikisha anamchelewesha akifika; alijikuta anapata mshituko mkubwa kiasi hadi kitabu alichokuwa ameshika kikidondoka chini.


"Aah karibu komredi" Jay alisema kwa kubabaika baada ya kumuona Boneka.



"Vipi komredi kwema lakini!" Boneka alihoji huku akiinama kukiokota kile kitabu.



"aaah ni kwema... Aah karibu.. Afu hiki kitabu.." Jay aliongea kwa kurukia maneno bila kujua alitaka kuongea nini wakati huo.


"Hebu tuingie ndani komredi, inaonekana haupo sawa kabisa" Boneka alimwambia huku akimshika mkono Jay ili waingie ndani.



"Hapana komredi, wewe ingia afu nisubiri nakuja!" Jay aliongea huku akijinasua mikononi mwa Boneka na kwa kasi aliondoka.


Boneka alibaki akishangaa mambo yale.

Na Jay alikuwa anawahi kuona wale jamaa zake watamfanya nini Vedi na kwa haraka zake akajikuta anasahau kuchukua kile kitabu cha kumbukumbu mikononi mwa Boneka..



Boneka alibaki akikitazama kile kitabu, kisha akaingia ndani na kuona kama Vedi atakuwepo ama la.



Aliita mara kadhaa bila kuitikiwa, akachukua simu yake ili apige.



Simu ikaita kidogo ikapokelewa na Vedi.



Boneka hakusikia mtu akiongea, ila alisikia kama sauti ya mtu anahema na kukimbia kwa kasi.


Alijitahidi kuita bila mafanikio ya kuitikiwa.


Aliendelea kusikia hekaheka za mbio na mara simu ikakata.



Boneka alishindwa kuelewa yanayoendelea.

Alishindwa kujua kama mbio za Jay zilikuwa ni kumuwahi Vedi au vipi na je wamegombana hadi kufikia kutimuana namna ile?


Hata!


Nae akatoka kasi huku akiwa na kile kitabu na alielekea njia aliohisi Jay alipitia..



Mbio zake zilimfikisha barabarani, lakini hakuona mtu wala dalili ya mtu au watu kushangaa jambo fulani.


Alishindwa aulize nini kwa wapita njia.


Akachukua simu yake tena na kupiga, ila wakati huu simu iliita bila kupokelewa.


Boneka alishindwa aamue lipi hasa.


Akarejea alipoiacha gari yake na haraka akapanda na kutaka kuondoka, ila alijikuta anasita baada ya kutupia jicho kitabu alichokuwa amekishika.


Alitaka kukipekuwa ili aone kama ni sahihi kutembea na kitabu cha kumbukumbu za mtu wakati hajui kina umuhimu gani kwa mtu mwenyewe.


Aliamua kukipitia ili aone kama anastahili kukirejesha ama la.


Kitu kimoja kilichomsaidia ni kuwa yeye ni mpelelezi na katika kozi za ujasusi alichofunzwa ni kutokupuuzia hisia zake hasa wakati wa mambo ya kuchanganya.


Alifunua kurasa ya kwanza, alikutana na jina la Banzi Kela na hakukuwa na maelezo mengine zaidi.


Aliendelea kufunua na kukutana na ujumbe ambao ulimpa hisia za ajabu kichwani.


Ujumbe ule ni ambao Vedi aliukuta na ilikuwa ni ujumbe unaomhusu Mamu; lakini katika ujumbe ule kulikuwa kuna kuasa jambo fulani la hatari.



Ujumbe ule ulimtaka Mamu akae mbali na watu wabaya endapo yeye akifa bila kuonana nae...


Boneka aliona kabisa ujumbe ule ulimlenga Mamu na ulitoka kwa Banzi; sasa iweje kitabu kile kiwe mikononi mwa Jay?..



Aliendelea kukifunua na hapo alikutana na kitu alichokitilia shaka.


Kila baada ya kurasa kadhaa aliona kuna namba imeandikwa chini.


Alichukua simu yake na kuzipiga zile namba.


Ajabu ziliita!



"Samahani ndugu!" Boneka aliongea baada ya upande wa pili kukaa kimya.



"Nani!" Iliunguruma sauti kavu ya kike.



"Samahani! Nimepata hizi namba kwenye kitabu fulani cha kumbukumbu!" Boneka alisema huku akiaacha sentensi ikielea hewani.



"Diary? Ya nani!" Sauti upande wa pili iliuliza.


"Banzi Kela!" Boneka alijibu kiufupi.


Alisikia upande wa pili ukipumua kwa kasi kama mtu alieona nyoka mkubwa.



"Najua unataka kuonana na mimi na hicho kitabu kama kimefika kwako basi ukionana na mimi ni kujitia matatizo tu, ila naomba uniletee tafadhali" Mamu alisema bila kujua mpiga simu atapokeaje hiyo taarifa.



"Uko wapi?" Boneka alihoji.



"Tukutane Hard Rock Cafe!" Mamu alijibu huku akikata simu.



Boneka alishangaa ni mara ya tatu anasikia neno Hard Rock Cafe katika mazingira tofauti.


Mara ya kwanza aliambiwa na Vedi ya kuwa anaenda hapo; mara ya pili aliambiwa na kijana wake ya kuwa msafara alioona unatoka hospitali uliingia pale na kutoka n mara ya tatu anaalikwa kuonana hapo na mtu ambae alihisi ndie Mamu.


"Kuna nini hapo Hard Rock Cafe?" lilikuwa ni swali bila jibu.


Aliendelea kugeukia kurasa zingine na hapo alikutana na kurasa moja ambayo ilimfanya atokwe jasho.


Kurasa ilikuwa na maelezo yenye maneno na namba bila ufafanuzi wake.


"Hizi code zimeandikwa kwa ugumu hasa!" Boneka alijisemea huku akijitahidi kuzifungua bila mafanikio.


Alirudia kusoma code moja wapo.


"N1820H=DR KUSEKWA" hapo alijaribu kuzungusha kichwa bila majibu.



Aliishia kuambulia jina la Dr Kusekwa.


Mara ujumbe ukaingia kwenye simu yake akafungua,ulitoka kwa Mamu.



Mamu alikuwa amemwandikia ujumbe kumwelekeza muda ambao walistahili kukutana.


Ilisalia nusu saa tu ili ufike muda huo.


Boneka aliweka pembeni kitabu kisha akawasha gari na kutoka kwa kasi kuwahi huko alikotakiwa kuwapo ndani ya muda huo.


*****


Safari yake ilikuwa ni ya kupita njia zisizo rasimi na baada ya dakika arobaini alifanikiwa kufika pale Hard Rock Cafe akiwa yupo nyuma kwa dakika kumi.


Haraka akaegesha gari lake na kuingia ndani ya mgahawa huku akitumia ujanja mwingi kuzugusha macho yake bila kumstua mtu ambae angelikuwa anamfuatilia.


Kwenye meza moja kulikuwa kuna mwanamke alievaa suruali ya bluu na shati jeupe na mkoba aliuweka juu ya meza huku akiendelea kuperuzi na simu janja yake.


Kwa kubahatisha; Boneka nae alienda kukaa pale pale.


Akajaribu kuita jina alilohisi ndo la mtu aliempeleka pale.


"Mamu!!"


Yule mwanamke alitikisa kichwa kukubali.



Boneka alipumua kwa afueni.



"Niite Boneka!"



"Kitabu kipo wapi, nakiomba tafadhali" Mamu alisema huku akijaribu kuzuia sauti isifike meza za jirani.



Mhudumu nae hakuwa mbali, alifika na kupokea oda kisha akaondoka.


"Nadhani tuna mengi ya kuzungumza afu nitakupa hicho kitabu" Boneka alisema.



"Nakwambia haya kwa kuwa sitaki kukujua na ninaona u mtu mwema tu bila hata kukuuliza" Mamu alisema huku akimtizama usoni.



"Kila ambae huwa anaonana na mimi kuzungumzia hiko kitabu, maisha yake ni mafupi, sijui kilichomo ila nimekisikia mara kadhaa na kila aliekipata ni lazima anipigie, hivyo sasa ni vizuri nikiwa nacho mwenyewe pengine nitaokoa wengi" Mamu alisema huku dhahiri akionekana kuwa mbali kihisia.



"Kwa nini unahisi kinakuhusu hicho kitu!" Boneka alihoji.


"Banzi Kela; huyo ni mchumba wangu japo naweza kusema ni alikuwa mchumba wangu!"



"Kwanini unasema alikuwa, kwani sasa sio mchumba wako?"


"Mtu wa mwisho kuwa na hiki kitabu alinambia Banzi si mtu tena ila ni maiti tayari na hapo kwenye maiti ndipo alipokipata hiko kitabu!"


Boneka alimakinika kidogo.



"Alikwambia amemuona wapi na kina nani waliomuua?" Boneka alihoji.


"Wewe ni askari?" Mamu nae alihoji.



Boneka alibabaika kidogo huku akijiuliza kama ni sahihi yeye kumwambia kazi yake..


Boneka alikumbuka moja ya sheria za mpelelezi ni kuwa wazi panapobidi ili ili kupima uzito wa jambo lililombele yake.



"Ndio mimi ni askari" Alijibu.



"Umepataje hiko kitabu"


"Kuna binti ni ndugu yangu na tulikubaliana tu...." Boneka hakumalizia kauli yake alikatishwa na Mamu.



"Usiniambie binti Mashimo nae kauwawa" Mamu alihamanika kidogo.



"No! Sina hakika kama ameuwawa ila kwa asilimia zote naamini yupo hai ila ni bahati mbaya tu mi nilikutana na hiki kitabu, japo sijamkuta hapo"



Mamu alishusha pumzi kwa afueni.


"Ok! Banzi alikuwa ni mpenzi wangu na karibuni tungefunga ndoa, ila wiki kadhaa kabla ya ndoa alibadilika huku kila mara akinambia anahisi yupo hatarini kwa mambo fulani ambayo aliyaona" Mamu alinyamaza baada ya mhudumu kufika.



"Alikwambia anaogopa nini?"



"Hapana! Ila alinambia kama akifa, basi Diary yake ina majibu yote.....na bahati mbaya amekufa hiyo diary haipo kwangu na maiti yake sijaiona hadi sasa!" Mamu alifuta chozi kwa mgongo wa kiganja chake.


"Banzi alikuwa na kazi gani kwani!?"



"Banzi alikuwa ni Baharia!; alikuwa mpishi kwenye meli ya Serengeti Marine na ndiko maiti yake ilikoonekana!" Mamu alijibu kinyonge huku akijitahidi kuzuia chozi lisidondoke.



"Kwa hiyo unahisi ndiko alikoona hayo yaliomuua?" Boneka alihoji..



"Wakati fulani aliwahi kunambia tuje kwenye mgahawa huu, na tulipo fika alinambia mashaka yake yanaanzia hapa na hapa ndipo kifo chake kilipo!" Mamu alisema kwa uchungu mkubwa.



"Kwanini hapa!" Boneka alihoji.


"Hata mimi nilimuliza kama wewe ila alinambia neno ambalo sikulielewa hadi leo"Mamu alisema.



"Neno gani!?" Boneka alihoji huku akiwa makini na anachotarajia kusikia.



"Jezebeli!" Mamu alijibu.



"Ndo nini sasa!" Boneka alihoji.


"Hata mimi sijui na wewe ni askari nadhani unastahili kujua sasa" Mamu alisema huku macho yake yakiwa upande wa kaunta ya pale mgahawani.



"Nadhani hiko kitabu kipo pahali sahihi, hivyo nitakihitaji ukimaliza shida zako. Mume wangu amekufa na kafia Serengeti Marine" Mamu alisema huku akichukua mkoba wake na kuanza kuondoka.

.

Boneka alibaki akimtizama tu namna alivyoondoka.


Boneka aligeukia kahawa aliokuwa ameagiza.


Akasonya baada ya kugundua imepoa..

.

Akasimama na kuacha pesa mezani kisha akaanza kuondoka, mara akasikia kelele upande wa barabara.


Akapiga hatua kubwa kuwahi, akaona umati unasogea katikati ya barabara.


Nae akawahi kuona kilichotokea.


"ooh my God" Boneka alijisemea baada ya kuona mwili wa mwanamke ukiwa umelala chini huku damu ikisambaa.


Alikuwa ni Mamu!


Watu walikuwa wanalaani gari iliomgonga Mamu.


"Kagongwa makusudi huyu binti " Boneka alijisemea huku akijitahidi kupangua watu na akamfikia Mamu.


Aliinama na kumgusa; Mamu alikuwa anahema kwa mbali sana.


Boneka akaomba msaada wa wasamaria wanuwahishe hospitali.


Mamu alitulia kimya katikati ya dimbwi la damu.



Waliamua kumnyamazisha, na Boneka alikubali kwamba; tatizo linaanzia Hard Rock Cafe.


Jezebeli! Ni nani au ni nini?"



******


MWISHO



1 comment:

Blog