Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

MY DREAM

  


MTUNZI: LATIFA




Ni jumamosi tulivu nikiwa najiandaa kwa safari yakurudi nyumbani kwetu Tanzania baada ya miaka minne niliyokuwa naishi nje ya nchi kikazi Dubai.

Nilijawa furaha sana kwasababu nilikuwa naenda kuonana na familia yangu zaidi mamayangu kipenzi nilimkumbuka sana.

Hatimae muda ulifika nikiongozana na boss wangu ambae alinisindikiza adi Airport tuliagana kwa huzuni sababu alinizoea lakini hakukuwa na jinsi ni lazima nirudi nyumbani

"Latifa bye byee but i will miss you"

Aliniaga kwa majonzi sana nilimuonea huruma uyu mama wa kizungu akutaka niondoke alinizoea sana niliishi nae kwa furaha na amani uku akinichukulia mimi kama binti yake.

"And me mom iwill miss you so much"

"Please come back latifa i want you"

nilimuonea huruma sana nakumsogelea tukakumbatiana sana akutaka kuniachia haraka adi machozi yalimtoka ikabidi nichukue kazi ya ziada kumbembeleza mwisho aliniacha namimi nikaondoka nakuingia ndani nikaguliwe mizigo yangu.

Nikiwa sehemu ya ukaguzi nikamuona kaka mmoja ananiangalia sana lakini sikumfatilia niliona kawaida tu baada ya kumaliza nilikaa sehemu yakusubiri muda ufike ili nipande kwa ndege nianze safari yakurudi nyumbani kwetu.

"Haloo mama ndo nipo Airport apa naisi kesho saa sita mchana sijui nitakuwa uko jaman uje na wadogo zangu wote mnipokee"

Nilimpigia simu mama nakumueleza ayo moyo wangu ulikuwa na raha sana.

Baada ya muda mfupi nikasikia tangazo tunahitajika kupanda kwenye ndege niliinuka fasta nikabeba mizigo yangu nakuwahi kwenda bahati nzuri nilikatiwa tiketi siti ya dirishani nilifurah kwailo nikafika nakukaa uku nikichat Facebook na whatsapp kuwataarifu marafiki zangu narudi Tanzania ilikuwa siku ya pekee sana kwangu furaha yake haielezeki.

Mara gafla akaja yule mkaka nilimuona akinitazama sana wakati nakaguliwa

"Habari yako?"

Alinisalimia nikamtizama vizuri alionekana ni mtanzania pia nikamjibu

"Nzuri za kwako?"

"Salama tu mzima wewe"

"Mzima sijui wewe?"

Tulimalizana apo kusalimiana kila mtu akafanya lake mimi nilikuwa bize na simu ila yeye alikuwa anacheck movie kwa Television ndogo inayokuwepo kwenye siti apo tulipokaa.

Mara tangazo likatajwa tufunge mikanda ndege inaanza kuruka bahati mbaya mimi kufunga sijui sikuona aibu nilimueleza uyo kaka akanigeukia nakuchukua mkanda kunifunga alishika tumbo langu niliruka kidogo mwili ulisisimka sana sababu miaka yote iyo sikuwahi kuguswa na mwanaume

"Pole mamy"

Alisema kwa sauti yake ya upole

"Samahani mimi naitwa Kassim nawewe je"

"Mi...miii....Laaa...tii...faa"

Nilishikwa na kigugumizi gafla sikujua kimetokea wapi nilijikuta navutiwa sana na uyu kaka sikujua kwanini ila nilipenda sana anaongea vizuri kwa upole sauti yake ilivyo sikutamani anyamaze moyo wangu ukavutiwa nae nilijishangaa sana

"Sorry kassim ivi umeoa?

Nilimuuliza

"Ndio nina mke"

Jibu alilonipa lilinivunja nguvu bila kutegemea machozi yalinitoka ata yeye mwenyewe alinishangaa nalia kwanini.





Nilishindwa kujizuia machozi yasinitoke Kassim akaniuliza nalia nini alishangaa Ghafla tu

"Latifa mamaangu nini unalia jamani nimekukosea kitu gani nambie?"

Aliniuliza kwa sauti yake nzuri ya upole kama ananibembeleza aliniongezea maumivu zaidi

Kama alipigilia mwiba moyoni mwangu nikajikuta naangua kilio zaidi aliwahi kuniziba mdomo sauti isitoke akanisogeza kifuani kwake nakunilaza apo kwikwi ilinishika ya kilio sikujua kwanini ilikuwa ivyo nilishangaa sana

"Imekuwaje Latifa mimi nina nini kwani lakini?"

Nilijiuliza mwenyewe nakukosa jibu.

Muda huo ndege bado ipo angani inapasua mawingu tu safari inaendelea,

"Latifa nikwambie kitu"

Alisema yani sauti yake ndo ilinimaliza kabisa.

"Nambie"

Nilimjibu kwa sauti ndogo sana alishusha pumzi kidogo kisha akasema

"Latifa unamacho mazuri sana upaswi kuyatoa machozi huyatendei haki nakuomba usirudie tena kulia sawa mama?"

Jaman uyu mwanaume adi nilimuonea wivu mkewake japo simjui.

Nikajikuta natabasamu mwenyewe lakin sikutoka kifuani kwake bado

"Naomba uniangalie"

Alisema nakuniinua tukaanza kutazamana bila kusema lolote ni kama mioyo yetu ilikuwa inazungumza kuhusu upendo ila hakuna alieweza kumtamkia mwenzie anampenda.

Tuliangaliana sana kama tuligandishwa vile

Alietushtua ni muhudumu wa ndege sijui anaitwaje alituletea chakula

"Excuse me"

Alisema nakunifanya nijisikie aibu kumuangalia alitupatia chakula kisha akasonga kwa wengine kuwagawia.

Bila kuongea lolote tulianza kula ukimya ulitawala juu yetu adi tulipomaliza nilishtuka na mlio wa mesejii kwenye simu yangu nilichukua nikakutana na meseji nyingi za watu wakinitakia safari njema nilifurahi sana.

Nikaanza kuchat sasa Facebook nilikuwa bize ata mawazo kwa Kassim yalitoka nilichat sana nikaisi kichwa kinauma niliacha.

Kugeuka pembeni namuona kassim pia yupo bize anachat kwenye Laptop yake wivu ukanishika nilijua tu anachat na mke wake moyo uliniuma sana.

"Kwanini naumia sana kwa uyu kaka mbona nilishaapa sitopenda tena kwani hana nini huyu au kaniroga? Mmmh hapana kaka wa watu handsome anajuaje kuroga jaman lakini Ghafla tu najikuta naumia juu yake kwanini"

Maswali mengi nilijiuliza jibu nilikosa nikabaki naumia moyoni.

Alichat sana nayeye mwisho akafunga laptop yake nakunigeukia akitabasamu

"Latifa uko poa?"

Aliniuliza

"Aaahh...mmm..ndi.oo..."

Sijui kigugumizi kilitoka wapi.

"Pole naisi umechoka jaman"

Alizidi kunimaliza nguvu maana iyo sauti tu mie hoi

"Asante kassim"

"Sorry ivi unaishi wapi kwa Tanzania?"

Alizidi maswali japo mimi mvivu sana kuongea ila kwa sauti yake nilijikuta naongea tu sikutamani anyamaze nilipenda aongee muda wote tu

"Kwetu ni ubungo"

"Wow ni karibu mimi nyumbani ni mbezi beach"

"Ooh sawa"

Basi tuliongea mengi tukafahamiana zaidi.

Bado tupo angani yote hayo yakitokea hatujafika Tanzania tulizoeana kwa muda mfupi tu kassim alikuwa mcheshi alipenda kutabasamu muda wote

Usiku uliingia nilichoka kuchat nikajiegamiza kichwa changu kwenye siti niliyokalia nikapitiwa usingizi bila kujijua

Nilishtuka na sauti ya Kassim alikuwa anaongea na mtu nikafumbua macho kuangalia ni nani kumbe ni simu basi nilikaa tuli bila kumsemesha

"Morning Latifa"

Alinisalimia nikamuitikia ila nilijisikia kwenda toilet nikamuomba anipishe alisimama nakunipisha nipite basi nilitoka nakuelekea maliwatoni kujisafisha kidogo kisha nikarudi nilimuona Kassim akiniangalia sana adi nilijisikia aibu

Alisimama tena kunipisha nikae

"Mmmh Latifa Mashaallah unaumbo zuri sana japo umevaa baibui lakini linaonekana hongera napenda sana mwanamke anaejistiri"

Aliongea uku akitabasamu sikujua nimjibu nini nilikaa kimya tu.

"Sorry Latifa unae boyfriend?"

"Hapana sina"

"Yani kwa urembo wote huo huna kweli siamini"

"Kassim sitamani kuwa na mwanaume nimeumizwa sana kila nikipenda natendwa tu"

"Jaman pole sana ila usikate tamaa omba mungu atakupatia mwanaume mkweli ambae hatokuumiza kamwe"

Nilimshukuru kwa mawazo yake basi tukaongea mengi zaidi nilijawa na furaha kujuana na kassim sikujuta kukaa nae nilifariijika kwa mengi

"Samahani ivi uku unatoka wapi kwa nani yani nilikuona umesimama na mwanamke wa kizungu ivi mkiagana ?"

Aliniuliza

"Yule ni boss wangu uku nilikuwa kikazi ndio narudi nyumbani"

"Ooh sawa ila alikuwa na huzuni sana yule mama inaonyesha amekuzoea kweli"

"Ha haha haa ni kweli miaka minne nimeishi nae nikimfanyia kazi kanizoea sana"

Nilisema alishtuka

"Haaaaa miaka minne latifaaaa! Na ujawahi kurudi Tanzania?"

"Ndio kassim"

"Mmmh naisi wazazi na ndugu zako wamekumiss sana kukuona"

"Ni kweli lakini leo wataniona"

Niimjibu nikitabasamu na yeye pia alitabasamu macho yetu yakakutana tena tukaanza kuangaliana niliwahi kukwepesha macho yangu nilijisikia aibu kiasi

Basi tulikaa kidogo hatimae ndege ilitua anga nakukanyaga Ardhi ya Tanzania nilifurahi sana kufika kwenye nchi yangu baada ya muda mrefu kutokuwepo furaha ilitawala moyoni mwangu ndege iliposimama tu kila mtu alitoka kivyake nilikuwa na hamu kuonana na ndugu zangu niliwahi sehemu ya ukaguzi nilipomaliza tu nilitoka nje nakulakiwa na wadogo zangu watatu Zulfa, Salim na Yasin

"Waooooo dadaaa...dadaaa...dada"

Walipiga kelele waliponiona tulikumbatiana sana uku wakuniambia wamenikumbuka Ghafla akili inakijia kuhusu kassim niligeuka nyuma kuangalia mlango wakutokea labda nitamuona lakin mara nikaona amesimama na mwanamke mtu mzima niliisi ni mamayake ila alikuwepo msichana mwengine wakiwa wamekumbatiana moyo wangu ulikufa ganzi nilijua ni mkewake Ghafla wakaachiana nakupanda kwenye gari wakaondoka nilibaki nimeganda naangalia lile gari uku machozi yakinitoka kibaya zaidi sikuwa ata na namba yake ya simu nilimpoteza Kassim moyo wangu uliuma sana niliisi Dunia nzima imenielemea machozi yalinitoka kama maji nililia sana uku nikijilaumu kutokupata mawasiliano nae mama akashangaa nina tatizo gani yeye ndie alinishtua na sauti yake

"Wewe Latifa unatatizo gani?"


Mama ndie alinishtua na sauti yake

"Wewe Latifa unatatizo gani?"

Nilijifuta machozi fasta sikutaka wajue lolote kuhusu kassim

"Furaha tu mama siamini kama nimerudi salama nakuwaona tena"

"Jaman ndo adi ulie?"

"Machozi ya furaha jaman tena mngejua nilikuwa naogopa kwenye ndege natetemeka mwenzenu yani naisi kama inaanguka nakufa"

"Hahahhaa dada bwana wakati mimi natamani kupanda iyo ndege"

Basi maongezi yaliendelea nakunifanya nimsahau kidogo kassim hali yangu ikawa sawa tulipanda kwenye tax na safari yakurudi nyumbani ikaanza.

Tulifika salama nikasaidiwa kuingiza mizigo yangu ndani

"Zulfa washa jiko bandika maji ya ugali"

Mama alimwambia mdogo wangu wakike

"Hee mama umejuaje yani ninahamu nao huo ugali sana tena na matembele pikeni"

Niliwaambia basi walitoka kuandaa chakula mimi nilikuwa chumbani kwangu naweka nguo zangu sawa.

Baada ya muda mfupi nilikuja kuitwa chakula tayari nilitoka nikajumuika nao pamoja tulikula nilifurahi sana kukaa na familia yangu.

Siku iyo ilipita hatimae wiki moja ikaisha bila kuwasiliana na Kassim sikuweza kumsahau kila mara nilimkumbuka sana niliumia kumkosa najua anamke lakini ata salamu yake tu ilitosha kuliko kumkosa kabisa niliumia sana.

Baada ya mwezi mmoja kupita siku moja nipo ndani chumbani mama na wadogo zangu walitoka nilibaki mwenyewe tu

Nikiwa napekuapekua kwenye handbag langu lile nililokuja nalo wakati wa safari nikashangaa naona ni business card nilishtuka jina kassim

Niliruka kwa furaha fasta nikaichukua namba nakuweka kwenye simu yangu nikaipiga iliita sana adi nilikata tamaa baada ya nusu saa Ivi ikapokelewa na mwanamke

"Hallow"

Nguvu zote ziliniisha ile furaha niliyokuwa nayo ilitoweka machozi yalinitoka kama maji moyo uliniuma sana

"Kassim najua unamke lakini kwanini umpe simu apokee kwanini unaniumiza mimi nilisema bila kujua simu bado ipo on nikashtuka labda wamesikia nilikata simu nakubaki mnyonge nilikosa amani kabisa.

Sikumpigia tena nikajua labda atanitafuta ilikuwa tofauti wiki nzima sikuiona simu yake nikajaribu kumpigia siku moja nilimpata yeye mwenyewe lakini alijifanya hanijui aliniongezea maumivu

"Kassim mimi Latifa tulikutana kwenye ndege tulikaa wote siti moja"

"Mmmh nina kazi kidogo subiri tutaongea baadae"

Alikata simu nilikuwa mjinga sana kuumia kwa mtu asiejali hisia zangu kutoka ndani ya moyo wangu nilimpenda kwa dhati lakini ningeanzaje kumwambia nampenda atanichukuliaje mimi malaya au nilikosa ujasiri

"Acha niumie tu sina jinsi"

Nilijisemea mwenyewe usiku sikuweza kulala nilikuwa nalia tu nakosa raha moyo unaumia sana

"Si bure uyu kaka kaniroga kweli kabisa kwanini naumia sana juu yake ivi yeye hajui kama nampenda mimi jaman kwanini ananitesa"

Nilikuwa nawaza mengi sana bila majibu.

Siku moja alinipigia simu kassim

"Halo mambo mamy"

"Safi za kwako"

"Njema tu! Natamani nikuone"

Nilishtuka aliposema ivyo

"Nani mimi au?"

"Latifaaa ni wewe ndio jaman nimekumiss sana"

"Mmmh sawa unione wapi?

"Guest nataka"

"Kassim gesti kufanyajeee?"

Moyo ulienda mbio nilishtuka sana

"Jaman si kuongea tu"

"Mmmh apana sipo tayari bora ata Restaurant ivi"

"Sina pesa Latifa siwezi kukaa sehemu iyo"

Alisema nakunifanya nimshangae

"Kwaiyo wanaokaa Restaurant ni watu wenye pesa tu?"

"Ndio sasa ukiwepo pale ukaagiza mapiza mabaga majuice makubwa dah si hasara iyo mimi pesa natoa wapi?"

"Hhhhahhaha kassim usinichekeshe mi ungejua sipendi ivyo vitu usingesema"

"Wewe muongo unaonekana mtoto wakishua ivyo ndo vyakula vyenu nyie"

"Kassim sema utaki kuonana namimi tu".

"No mamy tukutane gesti jaman"

Ukweli nilimpenda sana kassim lakini sikuwa tayari kukutana nae sehemu anayotaka kwanza nilijua anaemke mimi kuwa hawara sikutaka yani anichezee kisha aniache kama kweli atanipenda ni bora niwe mkewake wa pili ila sio kuwa mchepuko akinichoka aniache sikutaka ilo litokee nilitamani awe mume kabisa nilimgomea kukutana nae alichukia sana

"Sawa mama hutaki najua utanikumbuka sana"

Alisema nakukata simu nilijikuta najilaumu sana ningekubali kuonana nae lakini nikasema potelea pote siwezi kujiraisisha kwake ata kama nampenda.

Maumivu hayakunitoka kukosana na kassim iliniuma sana ila sikuwa na jinsi

Tangu siku iyo namba yake haikupatikana tena nilizidi kuumia nilitamani japo nisikie sauti yake lakini haikuwezekana.

Miezi sita sasa imepita sina mawasiliano nae nilisumbuliwa kimapenzi na wanaume wengi lakini sikumuona anaeweza kunifanya nimpende kama kassim niliwapotezea wote nakubaki pekeyangu tu.

Siku moja nilitoka nakuelekea beach kuinjoy nikiwa na wadogo zangu nikajipiga picha nyingi nakutuma Facebook

"Jaman marafiki zangu anaetaka kuniona aje coco beach"

Niliandika uku wengi wakinitania kwenye comment nilijisikia furaha sana kujiachia maeneo hayo

"Dada Dada nataka maji ya kunywa"

Uyo ni mdogo wangu akisema nikawa natoa pesa

"Wee kaka wee majiiii njooo"

Uyo ni Zulfa akimuita muuza maji

Alikuja karibu yetu akatoa maji makubwa mawili nakumpa mdogo wangu mimi nilikuwa sijamuona uyo mkaka niliinama kutoa pesa kwenye pochi yangu ile nainua macho juu kumuona uyo anaeuza maji nilipatwa na mshtuko sana

"KASSIM"

Niliita nisiamini nimuonae mbele yangu.





"KASSIM"

Niliita nisiamini nimuonae mbele yangu

"Haaa Latifa! Mambo mzima wewe?"

Nayeye pia alishangaa kuniona lakini akushtuka kwa lolote

"Jaman kassim ndo nini umenisusa mda mrefu kimya?"

Nilimuuliza wala sikujali muonekano wake alivyo nakuuza maji nilishtuka kumuona sikutegemea nilishakata tamaa yakuonana nae.

"Mambo mengi mamy wewe acha tu"

Alisema akisikitika nikaisi kuna tatizo alafu wadogo zangu nao walinishangaa najuana vipi na huyu muuza maji

"Dada uyo ndo shemeji"

Aliuliza Yasini wenzie wakacheka niliwatizama sikupata lakuwajibu nikainuka pale nilipokaa nakusimama kisha nikashika mkono wa kassim

"Twende uku"

Nilimwambia tukatoka walipo wadogo zangu ambao walikuwa wanatucheka

"Shemeji nipe shilingi mia basi"

"Hahhhaha dada amepata shemejii oyooo tucheze hainaga ushemeji tunakulagaa"

Wakaanza kuimba singeri sijui uku wakicheza Salim na Yasin watukutu sana hawa watoto uku Zulfa yeye anacheka tu.

Basi niliwapotezea nakuondoka na kassim adi sehemu moja tukakaa apo chini.

"Aya nambie sasa tupo pekeyetu hakuna fujo uku"

"Latifa ni story ndefu kwanza mama mgonjwa anaumwa sana miguu inamsumbua pia mkewangu ni mjamzito mwezi huu anajifungua yani nina matatizo mengi biashara yenyewe ndo hii naitegemea mwenzio simu niliuza ile nipate pesa ya kumnunulia vifaa vya kujifungua mkewangu ndo maana ukaona kimya"

Alisema kwa huzuni sana kassim nilimuonea huruma ata mavazi yaliyovaa yalijulisha tu yupo na matatizo mengi.

"Pole sana kassim pole jaman mungu atakusaidia kwa yote"

"Nashukuru sana Latifa! Naomba nikuache basi niendelee na biashara yangu tutaongea siku nyingine"

"Jaman natamani nizidi kukaa nawewe! Siku nyingine nitakuona wapi mimi?"

"Latifaaa leo mbona tumeonana jaman ata siku nyingine tutaonana pia"

"Mmmh basi chukua namba yangu unitafute"

"Ooh sawa nipe"

Nilitoa business card yangu nikampa kassim kisha nikachomoa elfu kumi nakumpatia lakini aliikataa

"Latifa nashukuru sana iyo pesa wanunulie ata juice watoto usijali bye"

Alisema akainuka nakuondoka.

Nilibaki nimeganda namuangalia adi alipopotea machoni mwangu maswali mengi sana yalipita kichwani nilikosa jibu.

"Uyu kassim imekuaje yupo hapa na kule kwenye ndege alikuwa anatoka wapi? Kumbe maisha yake magumu ivi maskini dah mungu amsaidie ila sitoacha kumpenda moyo wangu umefarijika kumuona"

Nilisema nikitabasamu nikaamua kurudi kwa wadogo zangu tukajiandaa nakuondoka kurudi nyumbani.

Zilipita wiki mbili bila mawasiliano yoyote kassim akunitafuta tena niliumia sana nilitegemea angenipigia ila ilikuwa kimya nilitamani japo nisikie sauti yake tu moyo wangu uridhike lakini ilishindikana.

Baada ya mwezi mmoja kassim akanipigia simu

"Haloo mambo mimi kassim nipigie"

Alisema ivyo akakata simu fasta niliipiga ile namba lakini haikupatikana

"Kassim kwann unanitesa jaman?"

Niliongea pekeyangu nikilia.

Niliipiga zaidi kila muda haikupatikana adi jioni kama bahati nilipiga ikaita

"Latifa nisamehe simu ilizima chaji"

"Sawa usijal, uko poa lakini?"

"Ndio niko poa sijui wewe?"

Basi tulisalimiana tukaongea kidogo lakin kamwe sikutaka kumweleza lolote juu ya upendo wangu kwake wala kiasi gani naumia ilikuwa siri ya moyo wangu tu.

Baada ya siku chache kassim alinipigia simu nakusema mamayake anaumwa hana mtu wakumuangalia akaniomba mimi nikakae nae nilikubali zaidi nilifurah nitakua karibu na kassim niliona kama bahati.

Siku ilifika akanielekeza niende pugu kajiungeni wala sikusita nikajiandaa nakwenda adi maeneo hayo nikamkuta yupo stand ananisubiria tulisalimiana kisha tukaongozana adi kwa mamayake.

Nyumba ilikuwa imechakaa inaonyesha yazamani sana uku maji machafu yakiwa yamejaa nje kilikuwa kipindi cha mvua nilipoingia ndani nilikuta godoro lipo chini uku kukiwa na beseni dogo la vyombo apo kwenye godoro alikuwa amelala mwanamke mtu mzima nilimsogelea nakumsalimia

"Mama shikamoo"

"Mmmh marahabaa"

Alinijibu kwa nyodo uku akinitazama nakunishusha

"Mama uyu rafik yangu anaitwa Latifa utakuwa nae apa akikusaidia kazi"

"Wewe kassim usiniletee wezi ndani kwangu sitaki msaada mimi"

"Mama wewe mgonjwa na mkewangu unajua anakaribia kujifungua jaman ebu mkubali latifa uishi nae apa"

"Mmmh sawa nimekuelewa"

Alisema uyo mama mimi nilikuwa kimya nawasikiliza tu

"Latifa nakuomba mvumilie mamayangu ashakuwa mtu mzima huyu chochote vumilia mkewangu akijifungua tu mimi nakuja kumchukua mama nikaishi nae kwangu kwasasa siwezi kuwaweka pamoja hakuna wakumsaidia mwenzie"

Alisema kassim nikamuonea huruma kwa vile ninampenda nilikubali.

Basi alikaa adi jioni akaondoka uku akisema kesho yake atakuja

Wiki mbili zilipita kassim hakurudi kibaya zaidi simu alikuwa hana sikujua nimtafute wapi nyumba inawaka moto uyu mama alikuwa mkorofi sana nilishinda nalia tu muda wote kassim ni mweupe mamayake pia ni mweupe sana

"Wewe mtu mweusi nasikia njaa mimi nataka kula"

Alinidharau sana kibaya zaidi ndani hakuna kitu chochote bahat nzuri nilikuwa na pesa kidogo tigopesa nilitoa nakununua unga nikasonga ugali nakumpelekea ale ajabu alichukua maji akauweka ule ugali nakugoma kula

"Uwezi kunilisha ugali mimi mshenzi wewe nataka wali na kuku"

"Mama jaman sina pesa mimi kassim hayupo nitafanyaje"

"Mimi hainihusu iyo utajijua mwenyewe"

Dunia nzima niliona chungu machozi hayakukauka machoni mwangu mama alikuwa hawezi kufanya lolote kulala tu muda mwengine mikojo inamtoka mimi nafua nguo zake kwenda chooni hawezi lakini namsaidia kumuinua nampeleka uku nakula matusi moyo wangu ulikuwa unauma sana nitafanyaje kumuacha pekeyake nilishindwa kassim atanichukuliaje mimi wakati kanikabizi mamayake naanzaje kumuacha alafu niondoke.

Pesa iliniishia mama hakunielewa alikuwa ananisema ananidharau matusi makubwa makubwa natukanwa sikujua nimemkosea kitu gani alinichukia sana nilijuta kumjua uyu mama ila nilivumilia yote kamwe sikuwahi kumjibu vibaya kumtukana wala kumuacha pekeyake nilikuwa radhi nikakope dukani nipike ale ashibe japo alinichukia mimi nilimpenda sana mamayangu mzazi nilimueleza nipo kwa

Rafik yangu namsaidia kumuuguza mamayake ila sikumwambia yanayonikuta kwa uyu mama ilikuwa siri yangu mwenyewe.

Siku moja alinambia nimpeleke chooni ila alipofika kabla ajavua nguo kujisaidia akajikuta anajiharishia kibaya zaidi akaanza kunitukana mimi nimesababisha moyo uliniuma sana lakini sikuwa nalakufanya nilichukua nguo zake nakwenda kufua uku ninalia sana

"Kassim utanisamehe mamayako kanishinda naondoka mimi"

Nilisema nikizidi kulia ila kuna sauti ilisikika moyoni mwangu ikisema

"Mvumilivu hula mbivu usichoke kuvumilia"

Sikujua inatoka wapi iyo sauti lakini nikajipa moyo wakuzidi kukaa na uyo mama vitimbwi vilizidi kilasiku lakini sikuchoka naliaaa nanyamaza naendelea kumsaidia.

Miezi miwili ilipita bila kumuona kassim hatimae siku moja alikuja nakusema mkewake yupo hospital ameshajifungua tatizo anadaiwa pesa kama laki moja ivi aliongea uku akilia hana izo pesa nilimuhurumia

"Kassim muangalie mama kidogo ngoja niende nyumbani ninazo pesa nije nikupatie"

Nilimwambia alikubali basi niliondoka fasta nakwenda adi nyumbani kufika nikachukua laki mbili nikaingia shopping kununua zawadi za mtoto alisema wa kike kisha nikatoka nakupanda gari adi pugu ilikuwa usiku tayari lakini nilishangaa nyumba imefungwa hayupo mama wala kassim Gafla simu yangu iliita

"Hallow njoo mbezi beach sasa ivi"

"Kassim! Kuna nini uko mama yupo wapii unamsumbua anaumwa jaman?"

"Latifaa ebu njoo uku bwana utajua ukifika"

"Tizama saa moja hii nitafika saa ngapi uko?

"Wewe panda ata ungo ila mladi ufike uku"

Alisema akakata simu sikuwa na jinsi nilianza kusumbuka na magari foreni barabarani adi saa nne usiku nikafika sehemu aliyoniagiza nilikuwa nimechoka sana jasho linanitoka vumbi tupu miguuni dera nililovaa lilikuwa limeloana jasho nilikuwa kama kinyago.

"Wow nafurahi kukuona Latifa karibu"

Alinipokea kassim kitu nilichokiona mbele yangu nilishtuka sana.



"Wow nafurahi kukuona Latifa karibu"

Alinipokea kassim kitu nilichokiona mbele yangu nilishtuka sana kwanza kassim alikuwa amependeza sana nilimshangaa amevaa suti nzuri ya Gharama nilishangaa alinishika mkono akanivuta tukaingia ndani kwenye jumba kubwa kukiwa na uwazi kumepambwa vizuri kama kuna sherehe ivi nilijua labda anafanya sherehe ya mtoto wake uyo aliezaliwa moyo wangu ulikosa raha niliisi kuumia.

Mziki laini ulikuwa unasikika uku watu wengi wamekaa wanapata vinywaji walikuwa wamependeza sana nikajisikia aibu mimi nilivyo kama kinyago vumbi tupu dera limeloa jasho nimechoka mwili huo uso hauelewi.

Kassim alinichukua moja kwa moja adi mbele kabisa tukasimama apo

Gafla bila kutegemea nilimuona mama yake kassim akija nilishtuka sikutegemea alikuwa amependeza sana alivaa gauni kubwa la bluu lefu adi chini linaburuzika juu alifunga lemba kama mnigeria alipendeza sana na vile ilikuwa usiku lilikuwa likiwakawaka

"Latifa mamaangu nisamehe sana"

Alisema uyo mama akinisogelea nakutaka kunikumbatia lakini nilikwepa nilimuogopa alikuwa mkorofi mkali sana sikutaka aniguse

"Latifa usiniogope nakuomba nielewe na unisamehe kwa yote ayo Kassim naomba ongea nae Latifa mwelezee kilakitu"

Alisema uyo mama nikabaki nashangaa tu sielewi kitu gani kinaendelea

"Kassim mkeo na mtoto wapo wapi kuna nini kwani mbona sielewi jamani na huyu mama si mgonjwa uku amekujaje wakati hawezi kutembea?"

Nilimuuliza Kassim sababu ni kweli nilikuwa sielewi kiachoendelea.

"Latifa punguza presha mama sawa leo nataka nikueleze ukweli ujue ila naomba usimchukie mamayangu"

Alisema Kassim nakuchukua kipaza sauti akaanza kusema

"Mabibi na mabwana habari zenu jaman?

Yule mtu alietufanya leo tuwe hapa ameshafika ni huyu apa anaitwa Latifa ni mwanamke jasiri sana anastaili tunzo ameweza kuvumilia mengi juu yangu"

Alisema kisha akanigeukia nakunitizama kidogo kisha akaendelea

"Latifa unakumbuka siku ya kwanza mimi kukutana nawewe Dubai pale Airport nilikuwa nakutizama sana kipindi unaagana na yule mwanamke wa kizungu nilivutiwa Gafla nawewe nilikupenda sana nilifurahi nilipokuja kwenye siti nakukaa pamoja nawe nilifarijika sana pale tuliokuwa tukiongea, niligundua ata wewe unanipenda lakini sikutaka kukupa nafasi mapema nikakudanganya nina mke ili nikuone utakuwaje lakini nilijua uliumia sana.

Latifa ulipoinuka kwenda chooni niliweka business card yangu kwenye handbag lako sababu nilijua huwezi kuniomba namba ya simu.

Latifa siku ile ulipiga simu akapokea mwanamke ni dadayangu si mkewangu kama ulivyozania.

Latifa niliwahi kukwambia tukutane guest nilikupima tu nikuone utasemaje

Latifa miezi mitatu sikuwa online nilifanya makusudi lakini Facebook nilikuwepo nikawa nakufatilia kilakitu chako adi siku ile nikajua upo coco beach nikaamua kuja lakini nilijifanya nauza maji yote nikujionyesha mimi maskini.

Latifa nilipanga na mama ajigeuze mgonjwa ili ukaishi nae tuone utaweza kuvumilia au utashindwa miezi miwili mingi sana alikutukana alikunyanyasa najua maumivu gani ulipata lakini wewe ni shujaa kuweza kustahamili yote hayo nimeamini kweli unanipenda kwa dhati

Latifa familia yangu inauwezo mkubwa sana mimi pia nina mali nyingi lakini nilikosa penzi la kweli wasichana wa siku izi waongo sana wanapenda pesa hawana upendo wa kwel niliamua kwako nijaribu labda utakuwa mkweli kwangu nashukuru Mungu nimekupata mwanamke wa ndoto zangu

YOU MY DREAM

LATIFA I WANT MARRY YOU.

alimaliza kusema Kassim ukumbi mzima ulikuwa kimya ukishangaa maneno aliyokuwa akiongea mimi nilikuwa siamini kabisa anachosema nilijua ni ndoto sikuweza kuona vizuri uso mzima ulijaa machozi macho hayaoni vizuri nililia sana sikuamini.

Ghafla akaja msichana mzuri akiwa ameshika kiboksi ivi akampatia Kassim ambae alikifungua nakutoa pete iliyonakshiwa na Almas akanisogelea

"Latifa nakupenda naomba kubali uwe mke wangu"

Alisema akanishika mkono wangu nakuanza kunivalisha iyo pete nilitetemeka sana kwikwi ya kilio ilinishika nikaisi giza mbele yangu

NILIPOTEZA FAHAMU.



"Latifa nakupenda naomba kubali uwe mkewangu"

Alisema akanishika mkono wangu nakuanza kunivalisha pete.

Kwikwi ya kilio ilinishika nikahisi giza mbele yangu nilipoteza fahamu.

Sikujua kilichoendelea adi baada ya muda mfupi nilizinduka nikajikuta nipo kitandani nimelala nilianza kupepesa macho chumba kilikuwa kizuri sana nilistaajabu nipo wapi! Ghafla akaingia Kassim humo ndani akitabasamu

"Wow umeamka mkewangu nimefurahi sana mmmwaaaah"

Alinisogelea nakunikiss kwenye paji la uso

"Kassim jaman nini kinaendelea naisi nipo ndotoni siamini mimi"

Nilianza tena kulia akanisogelea karibu nakunikumbatia

"Latifa nakupenda sana kuliko unavyonipenda wewe nakuhitaji uwe mkewangu sitaki nikukose kabisa naomba nielewe"

"Kassim lakini....

Nilisema akanikatisha

"Shhiiii inuka unasubiriwa uko nje ila tambua mamayangu anakupenda sana hana roho mbaya kama unavyoisi ni yeye ndio alienambia nikupeleke kwake ukaishi nae miezi miwili akupime unafaa kuwa mke kwa mtoto wake au hufai msamehe kwayote yaliyotokea nakuomba"

Alisema kassim nilimkubalia kwa kichwa ata sauti haikutoka

"Ilove you my lovely wife mmmwaah plz don't cry mom"

Sauti yake ndo ilikuwa ikinimaliza kabisa ata sikuamini kama kwel nipo na mwanaume ninaempenda sana.

Basi alinishika mkono nikainuka tukasimama kwenye kioo kikubwa humo ndani alikuwa nyuma yangu kanishika kiuno

"Umependeza sana malkia wangu nafurahi kuwa na mke mzuri najivunia kuwa nawewe"

Alisema nakuzidi kunisifia akanichumu shingoni nilisisimka sana

"Baby come on"

Alinivuta kwake nakuanza kunipa romance niliisi kupagawa mwili ulilegea nguvu ziliisha Ghafla, alininyonya kidogo tu akaniachia alafu akaanza kucheka vile nilivyokuwa

"Unamacho mazuri mkewangu jaman yani nitafaidi mengi"

"Kassim lakin mbona unanitesa?"

Niliongea kwa sauti yangu yakudeka

"No baby sikutesi bwana ebu twende uku kwanza tunasubiriwa sisi ujue"

Basi ikabidi nijikaze tukatoka nikiwa nimependeza sana sijui nilitengenezwa muda gani nilirembwa usoni uku nimevalishwa gauni lefu la bluu kama la mamamkwe nilipendeza sana.

Tulipofika apo ukumbini watu walishangilia walipotuona Kassim ni mrefu kwangu tuliendana sana.

Basi siku iyo nilitamburishwa kwa ndugu zake tukafahamiana watu walikula wakanywa sherehe ilikuwa nzuri uku umbo langu likiwa kivutio kwa wengi nakuomba wapige picha na mimi sikuwa na hiyana niliwakubalia.

Ni siku ya pekee sana maishan mwangu kiukwel Kassim alinitesa sana siamini adi sasa nipo nae nilifarijika sana.

Saa saba sherehe iliisha uku mamamkwe akiwa na furaha sana nilichogundua apo ni nyumbani kwao na Kassim walishi yeye na mamayake na mdogo wake wa kike Nasra alikuwa binti mrembo anasoma bado.

Siku iyo ikabidi nilale apo sikwenda nyumbani adi siku ya pili yake kabla sijaondoka tukawekwa kikao na mamamkwe

"Latifa naomba utuelekeze kwenu tulete posa Kassim akuoe nataka uwe mkwe wangu kihalali sawa mama?"

Aliongea kiupole huyu mama adi nilishangaa

"Sawa mama hamna shida"

Nilimjibu

"Nakuomba usiniogope mimi ni mama mwema kwako sina ubaya nawe yaliyopita tuyasahau sawa eeh"

"Sawa mamaangu nimekuelewa"

Basi nilisema nikamsogelea nakumkumbatia uyu mama alifurahi sana tangu siku iyo sikumuogopa tena.

Baada ya maongezi Kassim akanichukua adi kwenye gari lake nakunirudisha nyumbani

"Lakin Kassim mimi naogopa nyinyi matajiri mtanitesa mimi maskini"

Nilisema uku nimeinamisha kichwa chini najishika vidole vya mikono ikambidi Kassim asimamishe gari apo tushatoka mbezi tupo ubungo

"Latifa wallah nakuapia sitokuumiza kamwe nakupenda sana tena kizuri mimi najua dini sio muhuni ata utajiri wetu ni halali mungu ndie tegemeo letu nakuomba ondoa hofu juu yangu"

Alisema akaniinua uso wangu nakunikiss

"Nakupenda Kassim usiniumize"

"Usijal mama siwezi kufanya ivyo"

Basi alinifikisha nyumban akaniacha apo nakuondoka.

Nilimuelezea mama yote kuhusu Kassim alishangaa sana nakunipa pole kwa yaliyonikuta

Siku iyo iliisha hatimae kesho ikafika wakaja washenga kuleta barua nyumbani majibu yakarudishwa siku hiyo hiyo mahari yangu nilipoulizwa nikawaambia

MSAHAFU

Hakuna alieamini kila mtu alishangaa basi wakaondoka na baada ya wiki moja Ndoa ilifungwa sikuamini siku ninayoolewa na Kassim mwanaume alienifanya niumie moyo wangu leo hii anakuwa mumewangu sikuamini kabisa.

Ndoa ilifungwa salama bila tatizo usiku ikafanyia sherehe ya nguvu tulipata zawadi nyingi sana rafik yake mmoja akajitolea honey moon yetu tukafanye kwenye hotel yake Zanzibar basi Kesho yake tulienda uko na boti binafsi.

Sasa nipo chumbani kitandani na yule mwanaume ninaempenda adi sielewi




Hatimae leo ni siku ambayo nipo chumbani na yule mwanaume wa ndoto zangu ninaempenda sana sikuamini yani kilakitu nilikuwa naona ni ndoto tu.

"Jaman mkewangu mbona unamawazo! Unaniogopa au?"

Aliniuliza Kassim

"Mmmh...aahh...hapana"

Sijui kigugumizi kilitoka wapi

"Haya mama twende tukaoge basi"

Aliposema ivyo moyo ulipiga Paa nilishtuka sana

"Tukaoge pamoja? Tangulia ukimaliza namimi naenda"

"Latifaaa jaman mimi si mumewako unachoogopa nini au hunipendi"

"Sio ivyo Kassim bwana"

"Alafu sipendi uniite Kassim mimi mumeo ebu inuka tukaoge tupumzike"

Nilikuwa natetemeka yani kama sijiamini ivi moyo unaenda mbio tu.

Sikuwa na jinsi nilikubali tukaingia bafuni

Hotel ya hadhi yake ndo mara ya kwanza kuingia yani uko chooni sijui bafuni unaweza kulala kabisa kuzuri loh ushamba mbaya jamani nilizoea kuona kwenye Television tu hatimae leo namimi naenda kuoga kwenye bafu la matajiri sio kwetu choo cha makuti hakina bati juu ndoo moja ya maji na kopo unajimwagia tu lakini uku sasa unafungua maji yanamwagika yenyewe kuna sink pia lakuogea ukipenda unaingia humo yani unasahau ata kufa ndo maana matajiri wengi wanakufuru kutokana na maisha wanayoishi wanajisahau sana.

"Mke wangu naomba ingia humu nataka nikuogeshe"

"Haaa Kassim mi siwezi nitaoga mwenyewe"

"Latifa sipendi upinge ninalokwambia utaumiza moyo wangu nakuomba nikubalie"

"Mmmh"

"Baby please"

Aliongea kwa kubembeleza na ile sauti yake nilijikuta mwili unasisimka kabla sijaguswa ikanibidi nikubali tu kuingia uku nina nguo ya ndani tu mwilini

Basi maji yasabuni yalijazwa humo Kassim alikaa kwa nje nakuanza kuniogesha jaman uyu mwanaume mtundu sana sijui alisomea kuogesha mwanamke au vipi sielewi alinisugua kuanzia unyanyo vidole vyote miguu nakupanda juu zaidi adi alipomaliza mimi sijiwezi kutembea nilishindwa ikabidi anibebe nakunipeleka chumbani akanilaza apo akaenda kujimwagia maji fasta nakuja mi nilikuwa nimeanza kupitiwa usingizi Kassim alipokuja akuniamsha nilijiisi kama nyoka ananitembea mwilini ivi nikashtuka nakumkuta ni yeye akiulamba mwili wangu alijua kutumia ulimi wake mikono yake adi miguu yani zaidi ya fundi iyo ndo mara ya kwanza kujua mapenzi yanafanywaje alikuwa tofauti na wanaume wengine niliowahi kuwa nao Kassim alikuwa zaidi ya fundi hakuna sehemu asiyonigusa nilipagawa sana kibaya zaidi nilikuwa na muda mrefu sijakutana na mwanaume hamu ilijaa sana hisia zilipanda sauti ilikauka nililia nakuongea maneno mengi ata siyajui mengine lakini akuniachia alizidisha utundu wake yote tisa! Kumi aliponiingilia akuwa na papara alienda taratibu kama hataki vile raha niliyosikia haina mfano kumbe alikuwa na haki anitese maana Mapenzi aliyajua haswa

"Kaaaa....siiiiiiiii...mmmmmmmmmm

Basiiiiiiiii....ooooopsssss.

Nililalamika aniachie lakin sauti yangu ilikuwa kama inamwambia azidishe adi nafika kileleni sikujiweza sijui nilizimia kwa raha au vipi nilikuja kushtuka kesho yake asubuhi.

****

Yani hayo ndo Mapenzi sasa sio wengine wamekutana club sijui kwenye daladala uko washabebana adi gesti ya vichochoroni wameingia ndani hamna kuoga wala kunyonyana au kuandaana kila mtu anavua nguo kivyake mwanaume kavua uko boksa inanuka panya kaidaka kakimbia nayo washaparamiana wameruka kitandani chaga mbovu zimevunjika wanaamua kuweka godoro chini kunguni kibao wanawan'gata sasa hayo mapenzi au mauzauza jaman?

Alafu wanasemaga watu kunyonyana kuna madhara si kweli mtu ukiwa msafi unajitunza huna ugonjwa ayo madhara atapataje anaekunyonya lakin we mchafu nywele zimejaa nguo ya ndani wiki ujabadirisha utakosa ugonjwa kweli lazima anaekunyonya apate maradhi unakutana na msichana chupi chafuu iyo hamu yakumnyonya itakuwepo kweli au mdomo unanuka ata mswaki haujui unaanzaje sasa apo kunyonya mdomo wake?.

Raha ya mapenzi wote muwe wasafi zaidi muandaane sio kukurupuka tu ndo mana wasichana wengi hawajawahi kufika kileleni hii kwasababu ya wanaume hawajui kuandaa wapenzi wao wakiingia chumbani mwanaume anajua kupiga mihuri basi akikojoa yeye imetoka hajali kama mwanamke pia anatakiwa aridhike.

***

Basi nilishtuka asubuhi mwili hauna nguvu nimechoka nakujiona mwepesi sana

"Umeamkaje mkewangu mzuri"

Nilikutana na tabasamu zuri la mumewangu

"Kassim sina nguvu Nimechoka"

"Pole mkewangu twende nikuogeshe basi"

"Aaah sitak mi siogi"

"Joto bwana twende ukaoge"

"Sawa naoga pekeyangu sitak uniogeshe"

"Haya mama inuka basi"

Nilijaribu nikashindwa

"Kassim umenifanyaje lakini ona"

Niliongea kwa sauti ndogo yakudeka Kassim alicheka akanisogelea nakunikiss alafu akaniinua

"Mmmh mkewangu umejaaliwa jaman alafu we mtamu nafaidije mimi"

"Muone toka apa"

"Ha hahaha"

Basi alinipeleka bafuni akaniacha nayeye kufanya mpango wa breakfast aliagiza nilioga nilipomaliza nikatoka nakujumuika nae tupate kifungua kinywa tulipomaliza ukawa muda wa mahaba nilifurahia sana kuwa na mwanaume ninaempenda zaidi anaenipenda nilishukuru mungu kwailo.

Wiki mbili tulika hapo hotel uku tukiinjoy Mapenzi yetu hatimae siku ilifika tukaondoka nakurudi nyumban kwake kassim sio kwa mama tukanza maisha yetu upendo uliongezeka kilasiku tulipendana sana hakika sikujuta kumpenda Kassim mwanaume niliekuwa namuota kilasiku leo hii nipo nae nilishukuru sana.

Zile siku tulizokaa hotel hazikuenda bure Kassim alikuwa kidume haswa baada ya mwezi mmoja hali yangu ilibadirika kichefuchefu mara homa za ajabu nilikuwa nachoka sana ikabidi nipelekwe hospital kupimwa nikajulikana nina mimba iyo furaha yake haikuwa na mfano mama alipopata taarifa alifurahi sana

Mumewangu akazidisha upendo kwangu nilijiisi kama malkia mbele ya Mfalme hakuna nilichokosa kwake mwanaume watofauti sana huyu anaupendo wa ajabu nilijisikia faraja kuwa nayeye sijui kama wapo wanaume kama kassim wanaopenda kwa dhati maana mapenzi ya siku izi majanga tu baada ya miezi tisa kupita nikajifungua mtoto mzuri wa kiume nakuongeza furaha kwenye ndoa yetu.


MWISHO.






0 comments:

Post a Comment

Blog