Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

SHAMBULIO LA DAMU

  

MTUNZI: NYEMO CHILONGANI 



Dunia nzima ilikuwa kimya kwa muda, hakukuwa na mtu aliyeamini kile kilichokuwa kimetokea. Waliokuwa mbali na televisheni, wakazisogelea, waliokuwa na simu zilizokuwa na uwezo wa kuingia kwenye huduma za internet, walifanya hivyo na kuangalia taarifa iliyoonekana kuingia muda huo.

Taarifa iliyokuwa ikionekana ndiyo ambayo iliwavuta watu wengi na kutamani kujua ni kitu gani hasa kilichokuwa kikiendelea. Kulikuwa na taarifa kubwa juu ya upotevu wa ndege kubwa ya Shirika la Ndege la Orange Airlines, Airbus A350-900 walibaki wakiuliza ni kitu gani kilitokea.

Watu hawakuamini, taarifa zilianzia mbali kwamba ndege hiyo ya sita kwa ukubwa duniani iliyokuwa ikifanya safari yake kutokea nchini Marekani kuelekea Uholanzi na Dubai kwa kupitia viwanja kadhaa vya ndege barani Ulaya ilikuwa imepotea katika mazingira ya kutatanisha.

Kila mtu alichanganyikiwa, tukio la kupotea kwa ndege hiyo likawarudisha watu nyuma na kuikumbuka ndege ya Shirika la Ndege ya Malaysia, Airlines Flight 370 ilivyokuwa imepotea mwaka 2014.

Kila mtu aliogopa, waandishi wa habari walipopata taarifa kuhusu ndege hiyo hawakutaka kupoteza muda, haraka sana wakawasiliana na mamlaka husika ili kujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea.

Hakukuwa na mtu aliyelizungumzia tukio hilo kwa undani kwani mpaka muda huo watu wengi walihisi ilikuwa ni tetesi kwa lengo la kuwatisha watu fulani. Watu wa mamlaka husika walichokisema kilikuwa ni kimoja tu kwamba wangehakikisha wanawasiliana na marubani wa ndege hiyo na kuzungumza nao ili kuona kama kulikuwa na ukweli wowote ule.

Tetesi hizo ziliendelea kuvuma, kila mtu aliyesikia alihitaji kujua ukweli kwa kile kilichokuwa kimetokea. Waliokuwa na ndugu zao humo hawakutulia, tetesi zile ziliwaumiza na kuhisi kwamba zilikuwa kweli kabisa.

Ndege hiyo ambayo iliondoka nchini Marekani ndani ya Jiji la New York katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JFK ilitarajiwa kuingia nchini Uingereza baada ya saa tano ambapo ingetumia saa mbili juu ya Bahari ya Atlantiki lakini kitu cha ajabu kuanzia muda ambayo iliachia ardhi ya Marekani, hawakuweza kuwasiliana nao kitu kilichomfanya kila mmoja kuogopa.

Watu wakajazana katika uwanja wa ndege wa JFK, walihitaji kujua kilichokuwa kikiendelea, walichokisema ni kwamba mara ya mwisho waliwasiliana na wenzao walipokuwa angani lakini baada ya dakika chache hawakuweza kuwapata kitu kilichoonyesha kwamba kulikuwa na tatizo mahali fulani.

Hiyo haikuishia nchini Marekani tu, bali hata nchini Uingereza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Heathrow uliokuwa jijini London kulikuwa na watu wengi waliotaka kufahamu kuhusu ndege hiyo, kwa kifupi, hakukuwa na mtu aliyekubali kama ndege hiyo ilipotea.

Viongozi wa Kampuni ya Orange Inc ambayo ilikuwa ikisimamia ndege hiyo wakakutana katika kikao cha dharura kwa ajili ya kuzungumza kile kilichotokea.

Kwenye kikao hicho kila mmoja alitoa maoni yake, hapo kabla waliwasiliana na watu wa rada na kuzungumza nao na kuwaomba kuwapa taarifa juu ya ndege hiyo lakini kitu cha ajabu kabisa hakukuwa na taarifa nzuri waliyopewa kwani hata watu wa rada hiyo nao walishangaa kuona mawasiliano yanakatika pasipo kujua sababu iliyofanya kitu hicho.

Baada ya saa moja na nusu, taarifa hizo hazikuwa tetesi tena, zilithibitishwa kwamba ndege hiyo ilipotea hivyo watu walitakiwa kuripoti na kuwaambia watu wengine.

Kila mtu alizungumza lake, wapo waliosema kwamba Marekani alihusika kupotea kwa ndege hiyo, wapo waliosema Kundi la Kigaidi la Mujahdeen liliilipua ndege hiyo kama ishara ya kuitisha dunia kwamba walikuwa na nguvu ya kufanya kitu chochote kile.

Kila mmoja alichanganyikiwa, waliongea mambo mengi lakini hakukuwa na mtu ambaye alikuwa na taarifa kamili kuhusu ndege hiyo iliyopotea.

Kwa kutumia jeshi la anga, Marekani ikatuma ndege zake na kwenda kuitafuta, walizunguka sehemu kubwa kwa ndege hizo za kasi, walitumia mpaka satalaiti zao lakini kitu cha ajabu kabisa, hawakuweza kufanikiwa kuipata.

“Labda itakuwa imekwama kwenye milima mirefu!” alisema mwanaume mmoja.

“Kwa hiyo?”

“Tuzitume ndege zikaangalie huko,” alisema mwanaume mwingine.

Hilo ndilo lililofanyika, haraka sana ndege zikatumwa na kuelekea katika milima mikubwa kama Evarest, Himalaya na mingine kwenda kuangalia ili kuona kama ndege hiyo ilikuwa imekwama huko.

Baada ya saa kadhaa tangu watu hao waondoke, simu ikapigwa na kuambiwa kwamba ndege hiyo haikuonekana huko, haikuwepo kitu kilichomaanisha kwamba walitakiwa kwenda kuangalia sehemu nyingine.

Hiyo iilikuwa ni siku ya kwanza kupotea kwa ndege hiyo, dakika zilikatika, saa zilikimbia, siku ya pili ikaingia lakini hakukuwa na taarifa zilizosema mahali ambapo ndege hiyo ilipokuwa.

“Hebu wasilianeni na CIA tuone watatuambiaje,” alisema mwanaume mmoja na hivyo simu kupigwa huko.

Wao ndiyo waliokuwa na nguvu ya kupiga simu katika kampuni ya Kimarekani ya CPS Engeneering iliyokuwa jijini Washington DC ambao walikuwa watu pekee waliokuwa na jukumu la kutengeneza injini za ndege kubwa za Boeing na kuwauliza kuhusu ndege hiyo.

Bosi wa kampuni hiyo, haraka sana akawasiliana na vijana wake wa IT na kuzungumza nao. Kwa kawaida, kwenye kila injini ya ndege kubwa waliyokuwa wakiitengeneza, kwa ndani waliweka GPS kwa ajili ya kuifuatilia kila mahali ilipokuwa ikienda.

Hilo lilikuwa suala la siri sana ambalo halikuwa likijulikana zaidi ya vijana hao wa IT, bosi wa kampuni hiyo na baadhi ya viongozi wa Kijasusi kutoka hapo CIA.

Vijana hao walipoambiwa kuhusu kupotea kwa ndege hiyo, wakaingia kwenye kompyuta zao na kuanza kuitafuta huku wakiliandika jina la ndege hiyo, namba ya injini yake, ikaja na kuanza kuzunguka kila kona wakiitafuta.

Kazi ilikuwa kubwa, kabla ya saa moja asubuhi, ilikuwa ikionekana, GPS ilisema kwamba ilikuwa usawa wa Bahari ya Atlantiki ikielekea katika Bara la Ulaya lakini baada ya muda fulani, hata GPS yenyewe haikuweza kusoma kitu kilichowashangaza hata wao wenyewe.

“Hii ndege itakuwa imeanguka kwenye maji,” alisema kijana mmoja.

“Kipi kinachokufanya kufikiria hivyo?”

“Ni kwa sababu kifaa cha GPS kimeacha kusoma ndege ikiwa usawa wa bahari, inawezekana kabisa iliangukia baharini na hivyo kifaa kuingia maji na kuzima,” alisema kijana huyo.

Taarifa hiyo ikapelekwa mpaka makao makuu ya CIA, hakukuwa na sababu ya kubaki ofisini tu bila kufanya juhudi za kuwatuma watu kwenda huko. Simu ikapigwa na wanajeshi wa majini wakaanza kuelekea huko wakiitafuta ndege hiyo.

Ilikuwa kazi kubwa ambayo hawakuwahi kukutana nayo kabla, walizunguka kila kona, walitumia vifaa vikubwa kuingia ndani ya bahari, huko walikutana na meli zilizozama, ndege nyingine ambazo ziliwahi kuanguka lakini hawakuweza kukutana na ndege hiyo kubwa.

Wakati wao wakiendelea na utafutaji, dunia nzima ilikuwa ni kilio tu, watu walihuzunika, zaidi ya abiria 550 hawakujulikana walipokuwa.

Lilikuwa jambo baya na gumu kuvumilika, wengi waliendelea kuilaumu serikali ya Marekani kwani waliamini kabisa kwamba walikuwa watu ambao waliipoteza ndege hiyo kwa malengo yao binafsi na ndiyo maana hawakutaka kulizungumzia sana suala hilo.

Rais wa Marekani kipindi hicho, Bwana Powell Ludovick akaingiwa doa, kwake, kitendo cha kupotea kwa ndege hiyo na wakati alikuwa na nguvu katika taifa kubwa kama Marekani ilionekana ni kama dharau, hakutaka kuona kila mtu akiizungumzia Marekani kwa ubaya hivyo kuwaagiza watu wake wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha ndege hiyo inapatikana haraka sana.

“Tunajitahidi mkuu!” alisema Mkurugenzi wa CIA, Bwana Matt.

“Fanya kila liwezekanalo, tuna muda mfupi,” alisema Powell.

Siku ya tatu ikaingia, ya nne nayo ikaja, mpaka wiki inakatika bado hapakuwa na taarifa rasmi ya kuzungumzia mahali ndege hiyo ilipokuwa.

Hilo lilikuwa jambo lililoshangaza, ndege nyingi zilizokuwa zimepotea zilionekana isipokuwa ndege hiyo tu ambayo watu wengi walihisi inawezekana ilitoka nje ya dunia na kwenda katika sayari nyingine.

Wakati mwingine hata jambo hilo lilionekana kuwa gumu kukubalika kwani kwa jinsi habari hiyo ilivyokuwa gumzo duniani, jinsi ilivyokuwa ikisumbua vichwa vya watu wengi basi NASA (National Aeronautics and Space Administration) ambayo ilihusika na masuala ya anga isingebaki kimya, ni lazima wangesema mahali ndege hiyo ilipokuwa kama tu ingekuwa imetokea nje ya dunia hii.

Watu waliokuwa na ndugu zao ambao walikuwa ndani ya ndege hiyo wakaanza kuzika nguo za watu hao kwa kuamini hapakuwa na dalili zozote za kuwapata watu hao na inawezekana kabisa huo ndiyo ungekuwa mwisho wao.

Ilikuwa ni huruma, makaburi ya pamoja yalijengwa haraka na watu kuzika nguo na vifaa vingine vya ndugu zao waliokuwa kwenye ndege hiyo.

Kama kulalamika, walifanya hivyo sana, walilia mno lakini hakukuwa na kilichobadilika, kila mmoja alikuwa na uhakika kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wa ndugu zao, yaani ndege ile iliwezekana ilikuwa mahali fulani, huko, ililipuliwa na volkano au ilianguka katika Bara la Antaktika ambako hakukuwa na mtu yeyote aliyekuwa akiishi huko kutokana na baridi kali.

Japokuwa watu walikuwa wakilia na kuomboleza, hapakuwa na mtu ambaye alijua kilichokuwa nyuma ya ndege hiyo kubwa.

Kati ya watu 550 waliokuwa ndani ya ndege hiyo, pia ndani yake iliwabeba watu watano, wasiojuana ambapo kila mmoja nyuma yake alikuwa na stori nzito ya maisha yake.

Ili kwa baadhi ya watu sehemu nyingine wawe na amani, furaha ilikuwa ni lazima watu hao wafe, wapotee katika mazingira ya kutatanisha ambayo kusingekuwa na mtu yeyote atakayejua kama walikuwa wameuawa.

Humo ndani ya ndege watu hao watano hawakujuana lakini walikuwa na mambo makubwa maishani mwao. Kama watu hao wangefika salama huko walipokuwa wakienda ilikuwa ni lazima dunia ichafuke, ili dunia iendelee kuwa sehemu salama, ilikuwa ni lazima kifanyike kile kilichofanyika.

Ni stori za watu watano tu ambao leo hii walisababisha zaidi ya abiria 550 kutokujulikana mahali walipokuwa. Ni hao watu watano ndiyo waliosababisha kipindi hicho dunia nzima ilie na kuomboleza kwa kuamini kwamba kweli ndege hiyo ilipotea na kwenda kulipuka sehemu fulani.


Kwa sababu simulizi ya Biashara ya Kifo inakaribia mwishoni, nimeanza na hii simulizi mpya huku tukiendelea kusubiri ile iishe.


HISTORIA YA MTU WA KWANZA KATI YA WALE WATANO ILIYOMFANYA KUWA NDANI YA NDEGE HIYO.


Mtu wa kwanza ndani ya ndege


“Natalie! Tell me, what the is going on?” (Natalie, niambie, ni kitu gani kinaendelea?) aliuliza mwanaume mmoja aliyevalia suti ambaye alisimama mbele ya msichana mmoja mrembo wa sura, mwenye umbo namba nane ambaye alikuwa na sura ya kitoto, vishimo mashavuni mwake vilivyomfanya kupendeza zaidi.

“Nothing Gabriel,” (hakuna kitu) alijibu Natalia huku akimwangalia mwanaume huyo aliyeitwa Gabriel aliyekuwa akimwangalia katikati ya macho yake.

Bado Gabriel alihisi kabisa kulikuwa na tatizo mahali fulani, alimfahamu Natalia, alikuwa ndugu yake, alimzoea, kila alipokuwa na tatizo alijua kabisa kwamba kulikuwa na kitu kinaendelea.

Kwa jinsi alivyoonekana siku hiyo alijua kabisa kulikuwa na kitu kikubwa kilichokuwa kikimtatiza. Natalie alikuwa dada yake wa damu, walikua pamoja na walifanya mambo mengi wakiwa pamoja. Siku hiyo msichana huyo alionekana kuwa tofauti. Akamsogelea na kuanza kuzungumza naye kwa karibu zaidi.

Natalia alikuwa mtawa ambaye alimaliza masomo yake katika kanisa lililokuwa Stockholm nchini Sweden. Alisoma huko kwa miaka mitatu na hatimaye kumaliza na kuwa mtawa aliyekamilika ambaye katika maisha yake yote alijiahidi kwamba angemtumia Mungu mpaka siku atakapoingia kaburini.

“Kuna nini? Natalia, kuna jambo unanificha,” alisema Gabriel huku akimwangalia ndugu yake huyo.

“Ninaumia moyoni mwangu! Hivi Mungu anaujua huu uchafu unaofanyika humu kwa baadhi ya watu waliokosa hofu yake?” aliuliza Natalie huku akimwangalia Gabriel.

“Uchafu gani?”

“Hapana! Nitakwambia siku nyingine!” alisema Natalia.

Hilo ndilo jambo lililomuumiza kichwa Gabriel, hakutaka kumuona ndugu yake huyo akiwa kwenye hali hiyo, alichanganyikiwa, moyo wake ulimuuma kupita kawaida.

Akakosa amani, furaha, kila alipomwangalia moyo wake ulimwambia kwamba kulikuwa na jambo hatari lililokuwa likiendelea nyuma ya maisha ya msichana huyo mrembo.

Alichokifanya ni kuanza kumfuatilia. Kila siku asubuhi alikuwa mtu wa kwanza kwenda katika mlango wa chumba cha msichana huyo na kuanza kusikiliza kwa siri.

Alifanya hivyo kwa kuwa alihitaji kujua kilichokuwa kikiendelea huko, hakusikia kama Natalie alikuwa akiwasiliana kwa simu kwani muda wote alikuwa mtu wa kusali huku maneno yake yakisikika kama yakimlalamikia Mungu kwa kile kilichokuwa kikiendelea kutokea kila siku.

Haikuwa nyakati za asubuhi tu, hata alipokuwa akienda mlangoni hapo usiku na kusikiliza, sala yake ilikuwa ileile kwamba kulikuwa na jambo kubwa lililokuwa likiendelea, kwa nini Mungu hakuingilia kati?

“Kuna jambo gani hapa?” aliuliza Gabriel huku akionekana kuchanganyikiwa.

Upelelezi wake kwa ndugu yake huyo haukuisha, kila siku alihakikisha anamfuatilia taratibu, kila alipotoka nyumbani na kwenda kanisani, alikuwa nyuma yake, hakupenda kumuona akiwa kwenye hali hiyo, alitamani kumuona akiwa na furaha kila siku katika maisha yake, hivyo ilikuwa ni lazima kuhakikisha anafanya kila liwezekanalo ili msichana huyo anakuwa na tabasamu muda wote.

Hakuwa akimfuatilia kanisani tu, hata alipokuwa akitoka kwenda kwenye mizunguko yake alikuwa akimfuatilia kwa nyuma.

Alimuona Natalie akienda kwenye mgahawa na kukutana na wasichana wengine wawili ambao nao walikuwa watawa kama alivyokuwa na kuanza kuongea nao.

Alikaa kwa mbali na kuwaangalia kwa darubini, kwa jinsi walivyoonekana, mazungumzo yao waliyokuwa wakiongea hayakuwa ya kawaida hata kidogo, nyuso zao zilionyesha kabisa kulikuwa na kitu kikubwa kilichokuwa kikiendelea katika maisha yao, kitu ambacho walikifanya kuwa siri kubwa mno.

Gabriel hakuwa na uwezo wa kuwafuata na kusikiliza mazungumzo yao ila aliona kabisa kwamba alikuwa na uwezo wa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anayapata mazungumzo yao yote.

Alichokifanya ni kuanza kutafuta kinasa sauti madukani ambacho ndicho angekitumia kunasa mazungumzo hayo. Alihangaika kwenye maduka na hatimaye kukipata kimoja hivyo kujipanga kukiweka katika mkoba wa Natalie ili siku akienda kuonana na wale marafiki zake asikie kile kilichokuwa kikizungumziwa.

Siku zikaendelea kukatika, kila siku ilikuwa ni lazima kwa Natalie kwenda kuonana na marafiki zake hao kwenye mgahawa ule na kuanza kuzungumza.

Kitendo cha kufika mahali hapo mara kwa mara kikawafanya hata wahudumu wa hapo kuwazoea na kuanza kuwaita majina kila walipokuwa wakihudumia.

Gabriel aliacha kufanya mambo yake, alitamani sana kujua kilichokuwa kikiendelea. Alimkumbuka Natalie jinsi alivyokuwa akisumbua kila siku nyumbani kwamba alitamani kuwa mtawa siku moja, ilikuwa ndoto yake ambayo ilikua na kukua na hatimaye kuitimiza na kwenda kusoma huko nchini Sweden.

Japokuwa alisoma na kuhitimu lakini msichana huyo hakukuwa na furaha hata kidogo, alionekana kuwa na maisha fulani ambayo yalikuwa ni ya siri sana yaliyomtisha mno Gabriel.

“Natalie, nakumbuka siku ambayo ulituambia nyumbani kwamba ulitamani sana siku moja uwe mtawa, unakumbuka?” aliuliza Gabriel huku akimwangalia msichana huyo.

“Nakumbuka!”

“Kila mmoja alikuwa akikuombea kwamba ukamilishe ndoto yako, sijui unakumbuka?”

“Nakumbuka sana.”

“Kuna siku baba alituamsha usiku na kusema anahitaji kusali nasi kwani alihisi kabisa hakuwa na siku nyingi za kuishi. Nakumbuka kabisa tulipiga magoti na kutuombea tutimize ndoto zetu, unakumbuka na hilo pia?” aliendelea kuuliza Gabriel.

“Ndiyo!”

“Hatimaye leo hii umetimiza ndoto yako na kuwa mtawa.”

“Namshukuru Mungu kwa hilo.”

“Sasa kwa nini huna furaha sasa?” aliuliza Gabriel.

Natalie akanyamaza, akauinamisha uso wake chini na kuanza kulengwa na machozi na ndani ya sekunde kadhaa yakaanza kudondoka moja kwa moja mpaka sakafuni.

Gabriel alijua kabisa kulikuwa na jambo moja katika kutimiza ndoto hiyo na ndiyo maana kila alipokuwa akimuuliza kuhusu jambo hilo msichana huyo alikuwa akilia.

Gabriel hakutaka kukubali, ilikuwa ni lazima ajue kile kilichokuwa kikiendelea. Alimlazimisha sana Natalie kumwambia kila kitu ambacho kilisababisha machozi yake kutoka kila siku lakini msichana huyo hakutaka kukubali.

“Kwa nini hutaki?”

“Nikikwambia! Kesho tu utauawa!” alijibu Natalie jibu ambalo lilimshtua Gabriel.

“Yaani nitauawa?”

“Ndiyo! Utauawa.”

“Na nani?”

“Kuna siri kubwa sana Gabby! Usione kwamba sitaki kukwambia ukweli, ninaona kabisa utauawa kama tu utajua ukweli,” alisema Natalie.

“Sawa. Tufanye kwamba mimi mwenyewe nataka kufa, kwa nini usiniambie?”

“Nitakwambia siku nyingine.”

“Natalie...”

“Nitakwambia siku nyingine,” alisema Natalie, hapohapo akachukua simu yake na kupiga sehemu, baada ya sekunde kadhaa akawa anazungumza na msichana mmoja ambaye alimwambia kwamba waonane kama ilivyokuwa siku nyingine.

Wakati msichana huyo akiwa bafuni anaoga, haraka sana Gabriel akaenda chumbani kwa Natalie na kukiweka kile kinasa sauti kwenye mkoba wake ili kama ingetokea angetoka nao basi aweze kunasa mazungumzo ambayo yangekwenda kuzungumziwa siku hiyo.

Akarudi sebuleni, alibaki akimuomba Mungu kwamba msichana huyo achukue mkoba wake na kuondoka nao ili ajue ni kitu gani kilikuwa kikikiendelea.

Baada ya dakika kadhaa, Natalie akatoka huku akiwa amevalia vazi lake la kitawa,shingoni akiwa na rozali kubwa na kuondoka nyumbani hapo huku akiwa na mkoba wake kitu kilichomfanya Gabriel kumshukuru Mungu.

Haraka sana akachukua kompyuta yake, akaweka headphone na kutaka kusikiliza kile kilichokuwa kikizungumziwa kila wasichana hao walipokuwa wakikutana katika mgahawa huo.

Natalie alipofika na kukaa tu, Gabriel akaanza kusikiliza mazungumzo yao waliyokuwa wamepanga kuongea siku hiyo. Hakwenda kuwaona, kusikia sauti tu kwake ilitosha kabisa kujua kile kilichokuwa kikiendelea huko.

“Umewasiliana nao?” aliuliza Natalie.

“Ndiyo! Walisema kwamba watakuja niwape ushahidi wa picha ili waupeleke makao makuu lakini hawakuwasiliana nami tena na kuna taarifa nilizipata kwamba wameuawa,” alisikika msichana mmoja.

“Mh! Mbona jambo hili linanitisha sana?” aliuliza Natalie.

“Yaani wewe acha. Kama itatokea na mimi nikauawa, nina picha zote za ushahidi, nimezificha nyumbani kule chini kwenye shimo, humo, kuna kisanduku ambacho kipo nyuma ya picha ya Yesu, ukiitoa hiyo picha, utakutana na hicho kisanduku ambacho kinafunguliwa kwa namba ya siri ambazo ni 2728,” alisema Mary.

“Mary! Hautokufa, hautouawa mpaka tufanikiwe katika hili!” alisema Natalie.

“Nani atatusaidia kama watu tunaotaka watusaidie wanauawa kila siku?” aliuliza msichana mwingine.

“Anna! Nadhani tunatakiwa kulifikiria hili kwanza, ila ni lazima hizi habari zifike makao makuu! Nilitamani sana kuwa mtawa, sikuamini kama walewale maaskofu wangu ndiyo ambao wangenibaka na kuniuza kwa matajiri ili wafanye na mimi mapenzi kwa sababu ya kupata pesa za kuendesha maisha yao! Siwezi kukubali,” alisema Natalie huku akisikika akianza kulia kwa kilio cha kwikwi.

“Ni lazima tufanye kila liwezekanalo kuhakikisha dunia nzima inajua huu unyama. Natalie, picha zako siku ulipokuwa unafanyiwa matukio hayo zipo?” aliuliza Anna.

“Ninazo! Na kama itatokea nikauawa, picha zangu zipo chumbani kwangu, nimeziweka chini ya kapeti, kuna sehemu ina kishimo ambacho humo ndipo picha zilipo,” alisema Natalie.

Huku nyuma ambapo Gabriel alikuwa akisikiliza kwenye kompyuta yake, aliposikia kwamba picha hizo zilikuwa chumbani kwa Natalie, akaenda, akaufungua mlango kwa ufunguo wa akiba na kuingia ndani.

Mwili wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira, hakuamini maneno yale aliyoyasikia, machozi yalimtoka, kitendo alichofanyiwa ndugu yake kiliugusa moyo wake.

Aliamini alikwenda kusomea utawa, alijichunga dhidi ya wanaume mpaka alipokwenda huko kukamilisha ndoto yake lakini kitu kilichotokea ni kwamba alianza kutumikishwa kingono na watu walioitwa maaskofu.

Alipofika chumbani, akaenda mpaka sehemu aliposikia, akafungua kapeti na kuona hiyo sehemu ambayo akaifungua na kukutana na bahasha ambayo akaichukua na kuangalia ndani.

Alikutana na picha, alipoziangalia, uchungu mkubwa, hasira zikaushika moyo wake, akajikuta akikaa chini na kuanza kulia.

Picha zile zilimuonyesha tajiri mmoja akimbaka dada yake, tajiri huyo alionekana kuwa na furaha, alikuwa akijipiga picha ambazo inawezekana Natalie baadaye aliziiba.

Haikuishia hapo tu, pia aliziona picha nyingine zikimuonyesha dada yake na wasichana wengine wakibakwa na watu wengine ambao aliwafahamu kabisa, walikuwa mabilionea ambao kwa maneno waliyokuwa wakizungumza walisema kwamba waliuzwa kwa mabilionea na kwenda kufanya nao mapenzi kisiri, tena walilazimishwa huku bastola zikiwa pembeni.

Haraka sana Gabriel akazichukua zile picha na kwenda kuziprinti kwenye kompyuta chumbani kwake na kubaki na kopi kama ushahidi na kuzirudisha zile orijino palepale alipozichukua, akatoka na kwenda chumbani kwake kuendelea kusikiliza mazungumzo yao.


Je, nini kitaendelea?




Wasichana hao watatu walifanyiwa mambo ya kinyama, hawakuwa na mahali pa kusemea kwa kuwa waliogopa kuuawa kama walivyouawa wengine, ilikuwa ni lazima watafute mtu ambaye angeyapeleka malalamiko yao katika uongozi wa Kanisa la Living Christ lililokuwa maarufu duniani na kuzungumza kile walichokuwa wakifanyiwa huko chuoni.

Hawakujua ni nani ambaye alistahili kuambiwa maneno hayo na kumpa picha hizo kwa sababu kila mtu ambaye walijaribu kufanya mawasiliano naye, aliuawa hata kabla hajawafikia na kuwapa picha zile za kuzipeleka makao makuu yaliyokuwa nchini Ubelgiji kwa ajili ya maaskofu hao kuchukuliwa hatua.

Baada ya kuziangalia picha zile, Gabriel akarudi kwenye kompyuta yake na kuendelea kusikiliza, alijua mahali picha za wasichana wawili zilipokuwa lakini hakujua mahali picha nyingine za Anna alipozificha na ilikuwa ni lazima kujua mahali zilipokuwa ili siku ambayo angezihitaji basi angekwenda kuzichukua.

Wakati akiwa hapo tayari kwa kuwasikiliza, alisikia kelele za treni na kugundua kwamba walimaliza kuzungumza na hivyo kila mtu kutawanyika.

Gabriel alibaki chumbani kwake akilia kwa maumivu makali, hakuamini kama kile kilichokuwa kimetokea, watu ambao walikuwa wakiaminika, waliokuwa wakiendesha ibada kila siku ndiyo ambao waliwafanyia wasichana hao matendo ya ngono kwa kuwachukua na kuwapeleka katika makasri ya matajiri na kuwafanyisha ngono.

Hilo lilimuuma kupita kawaida na kujiapiza kwamba ni lazima dunia ijue kile kilichotokea, ni lazima picha hizo zifikishwe makao makuu ya kanisa hilo na kuwaonyeshea uovu uliokuwa ukifanywa na maaskofu ambao kila Jumapili walikuwa wakisimama mbele ya kanisa na kuwaambia watu kwamba waache uovu.

“Ni lazima nitapeleka ushahidi wa picha zote, hata kama itatokea nitauawa, basi niuawe nikiwa nimekwishafika nchini Ubelgiji,” alisema Gabriel huku akijiapiza kwamba ni lazima afanye jambo kuwaokoa wasichana wengine waliokuwa wakienda kusomea utawa katika vyuo vya kanisa hilo.

***

Kanisa la Living Christ lilikuwa miongoni mwa madhehebu makubwa kabisa duniani ambalo lilikuwa na wafuasi zaidi ya milioni mia mbili na themanini duniani kote.

Mbali na dhehebu la Kiroma ambalo lilikuwa na wafuasi wengi duniani, kanisa hilo lilikuwa likishika nafasi ya pili kwa kuwa na watu wengi duniani nyuma ya Waroma.

Kila nchi makanisa makubwa yalijengwa huku yakiongozwa na watu waliokuwa na vyeo vya maaskofu, tofauti na Waroma ambao waliongozwa na mapadri.

Living Christ nao walikuwa na watawa ambao walitakiwa kusomea masomo maalumu kwa ajili ya kulitumikia kanisa hilo maisha yao yote.

Kila msichana ambaye alitakiwa kujiunga na kozi ya utawa, sharti la kwanza kabisa lilikuwa ni kuchunguzwa kama alikuwa bikira.

Hiyo ilikuwa ni kazi maalumu iliyofanywa na askofu mmoja aliyeitwa kwa jina la David Ishmael ambaye yeye ndiye alikuwa akithibitisha kwamba huyu alitakiwa kwenda au kuachwa.

Askofu huyo alikuwa nchini Ubelgiji yalipokuwa makao makuu ya kanisa hilo. Kila siku alikuwa akipokea wasichana wadogo ambao walikuwa na ndoto za kuwa watawa ili wamtumikie Mungu maisha yao yote.

Kila aliyekuwa akiingia ndani ya ofisi yake na kutaka kujiunga na chuo cha kanisa hilo ilikuwa ni lazima amwangalie kama alikuwa bikira au la, na kama alikuwa na sifa ya kuwa bikira, ilikuwa ni lazima aitoe, msichana ambaye angekataa basi asingeweza kujiunga na chuo hicho.

Msichana Natalie alifika hapo, ndani ya chumba hicho akiwa na furaha tele. Alisafiri kutoka nchini Marekani kwa ajili ya kwenda kuchukua masomo ya utawa na kumtumikia Mungu maisha yake yote.

Alijitunza, hakumruhusu mwanaume yeyote yule auguse mwili wake, alimuwekea ahadi Mungu wake kwamba katika maisha yake yote angekuwa bikira na ndiyo maana aliamua kuwa mtawa huku akiacha kufanya mambo mengine maovu.

“Hii imekuwa ndoto yangu kwa kipindi kirefu, hakika ninakwenda kuitimiza, nitamtumikia Mungu maisha yangu yote,” alisema Natalie huku akiwa katika viti nje ya ofisi ya Askofu David akisubiri kuingia ndani..

Baada ya dakika chache zamu yake ambaye ndiye alikuwa mtu wa mwisho akaingia ndani ya ofisi ya Askofu David na kuanza kufanyiwa usaili.

Hiyo ndiyo ilikuwa nafasi yake ya mwisho, askofu huyo ndiye alikuwa mtu wa mwisho kudhihirisha kwamba msichana fulani alikuwa bikira au la.

Kwenye nafasi hiyo hawakutaka kumuweka mwanamke, kwenye dhehebu lao hawakuwaamini wanawake, walitaka kila kitu kifanywe na mwanaume na ndiyo maana hakukuwa na askofu wa kike kwa kuwa tu hata enzi za Mfalme Daudi hakukuwa na mwanamke yeyote aliyepewa madaraka ndani ya kanisa.

“Unaitwa nani?” aliuliza Askofu David huku akimwangalia Natalie aliyeonekana kuwa na furaha ya ajabu.

“Natalie Andrew.”

“Unahisi una vigezo vya kuwa mtawa katika kanisa letu?” aliuliza Askofu David huku tayari tamaa ya mwili ikiwa imeanza kumkamata.

“Ndiyo baba askofu!” alijibu msichana huyo, Askofu David akaangalia mitihani aliyoifanya, alifaulu vizuri ila alitaka kuhakikisha kitu kimoja tu, kama alikuwa bikira au la.

“Hebu panda hapo juu ya meza, vua nguo zako,” alisema Askofu David maneno yaliyoonekana kumshtua Natalie.

“Unasema?”

“Nataka nione kama wewe ni bikira kweli,” alisema askofu huyo.

Natalia akawa na moyo mzito kufanya kile alichoambiwa, maishani mwake mwote alijiapiza asingefanya mapenzi na mwanaume yeyote yule, na si hivyo tu bali hata kuuona utupu wake.

Kulikuwa na wanaume wengi waliomfuata kwa ahadi mbalimbali lakini aliwakatalia, kitendo cha askofu kumwambia apande juu ya meza na kuvua nguo zake ili ahakikishe kama alikuwa bikira ulikuwa mtihani mzito mno.

Huku akiwa anafikiria ni kitu gani alitakiwa kufanya, akamuona askofu huyo akianza kuvua nguo zake na kubaki mtupu kama alivyozaliwa.

“Panda juu ya meza nikuchunguze,” alisema askofu huyo huku akichezea sehemu zake za siri.

Natalie alibaki akishangaa, hakuamini kile alichokuwa akikiangalia, hakuamini kama ile ndiyo staili ambayo Askofu David alikuwa akiifanya ili kuona kama mtu fulani alikuwa bikira au la.

Alitamani kutimiza ndoto aliyokuwanayo tangu utotoni lakini kile alichotaka kufanyiwa kilionekana kuwa kama unyama fulani.

“Hii ndiyo nafasi yako ya mwisho! Kama ni bikira, basi umepita, ila kama si bikira, utarudi kwenu, na kama utakwenda kumuhadithia mtu yeyote kile kilichotokea humu, kanisa litatumia nguvu zake kukumaliza kama lilivyowamaliza wengine,” alisema askofu huyo maneno yaliyomtisha msichana huyo.

Hakuwa na la kufanya, hakukubali kuona akikosa nafsi ya kuwa mtawa, kitu ambacho alikitamani tangu alipokuwa mdogo.

Yeye mwenyewe akapanda juu ya meza, macho yake yakaanza kuwa mekundu, akawa analia lakini askofu David hakutaka kujali, akaanza kumvua nguo moja baada ya nyingine mpaka kumuacha mtupu kabisa.

Natalie hakuamini kama bikira yake alikuwa akienda kuipoteza ndani ya ofisi hiyo, kila alipomwangalia askofu David ambaye alikuwa mzee sawa na umri wa baba yake alibaki akilia tu.

Mwanaume huyo akamlalia kwa juu na kuanza kumbaka juu ya meza hiyo. Alisikia maumivu makali chini ya kitovu, damu zikaanza kumtoka mfululizo, alilia lakini askofu huyo hakutaka kujali, ndiyo kwanza alikuwa akienda juu na chini kuhakikisha bikira ya Natalie inatoka ndani ya ofisi hiyo.

Hiyo ndiyo ilikuwa siku ya kuumiza maishani mwake kuliko siku nyingine. Alilia sana lakini askofu huyo hakujali, alifanya naye kwa dakika kumi ndipo akamwambia kwamba amepita, ni kweli alikuwa bikira hivyo angepelekwa nchini Sweden kwenda kusoma.

Hiyo ndiyo ilikuwa kazi yake aliyokuwa akiifanya miaka yote, hakukuwa na kiongozi wa kanisa aliyejua, ilikuwa ni siri ya wasichana waliokuwa wakifanyiwa usaili mahali hapo, mbaya zaidi hapakuwa na yeyote aliyediriki kusema kilichokuwa kikitokea huko kwa kuogopa kufukuzwa.

Siku hiyo alikaa na kulia sana, hakuwa peke yake, kulikuwa na wasichana wengine wawili, Anna na Mary ambao nao walifanyiwa vilevile kama alivyofanyiwa yeye na wote walikuwa wakilia tu.

Walibembelezana na siku iliyofuata wakaondoka na kuelekea chuoni huko Sweden ambapo huko wakaanza masomo yao katika chuo cha kanisa hilo.

Hakukuwa na mtu aliyekuwa na furaha tena, si wao tu bali hata wasichana wengine waliokuwa chuoni hapo walionekana kuwa kama wao.

Walijua kabisa kwamba na hao pia walifanyia mambo ya kinyama kama walivyofanyiwa wao. Walisoma huku kila mmoja akiahidi kwamba kitendo cha kufanya mapenzi na Askofu David angekuwa mtu wa mwisho na wasingeweza kufanya tena mpaka siku watakazoingia kaburini.

Wakati wakiendelea na masomo chuoni hapo huku kila siku wakisali na kumuabudu Mungu, wakaanza kuona mambo yasiyokuwa ya kawaida yakiendelea chuoni hapo.

Kila siku ya Jumapili wasichana watatu walikuwa wakichukuliwa na kuondoka kuelekea nje ya chuo hicho na kurudi usiku wa manane. Kila walipouliza, waliambiwa walipelekwa katika ibada maalumu na viongozi wengine kwa ajili ya kuyaombea mataifa yaliyokuwa na vita.

Hilo likawatia hofu, hawakuamini kama kile walichoambiwa ndicho kilikuwa ukweli. Walikaa chuoni hapo kwa hofu kubwa mpaka wakati mwingine wakajutia ndoto zao za kutamani kuwa watawa kama walivyokuwa.

Baada ya miezi mitatu, wakaambiwa nao walihitajika na kiongozi wa chuo hicho kwani kulikuwa na jambo muhimu walilotakiwa kuambiwa.

Kwanza wakashtuka, mara nyingi watu waliokuwa wakiitwa katika ofisi ya mkuu wa chuo ilikuwa ni kwa wale wasichana waliotakiwa kwenda kuhubiri neno la Mungu nje ya chuo hicho kama walivyofanya wale wengine.

“Kuna nini?” aliuliza Natalie huku akionekana kuwa na hofu.

“Mh! Sijui! Ila ninachohisi na sisi tunatakiwa kutoka usiku kwenda kufanya maombi na viongozi,” alisema Anna huku akionekana kuwa na hofu.

“Kutoka nje ya chuo?”

“Ndiyo! Nimesikia hivyo! Mungu wangu, hivi kwa nini nilitaka kuwa mtawa?” alisema Anna huku akianza kulia huku akiilaani siku ambayo alipata ndoto ya kuwa mtawa.

“Hebu twendeni, labda kuna jingine,” alisema Mary.

Wakaanza kwenda huko.





Nathalie, Anna na Mary hawakutaka kwenda kule walipoambiwa watakwenda lakini hawakuwa na jinsi, ni uongozi wa chuo ndiyo uliowaambia kwamba waende kwa sababu kulikuwa na ibada maalumu ambayo huwakutanisha wasichana mbalimbali na maaskofu kutoka nchi nyingine duniani na kufanya maombi ya pamoja.

Walipoambiwa hivyo kidogo wakawa na amani mioyoni mwao na kuhisi kwamba inawezekana kweli kule walipokuwa wakipelekwa kulikuwa na ibada maalumu na kukutana na watu wengine kwa ajili ya kusali pamoja.

Ilipofika majira ya saa tatu usiku, wakaingia ndani ya gari na kuondoka huku wakitangulizana na wazee wawili waliokuwa kwenye uongozi wa juu katika chuo hicho cha utawa.

Walikuwa kimya garini, hawakutakiwa kuzungumza kitu chochote kile. Safari iliendelea kwa zaidi ya saa mbili, gari likatoka ndani ya mji na kuelekea huko mbali kabisa. Ilikuwa ni safari ndefu ambayo hata wao wenyewe walishangaa.

Walitamani kuongea na kuulizana kuhusu safari hiyo lakini hawakuruhusiwa, walinyamaza mpaka gari lile lilipoanza kuingia ndani ya jumba moja kubwa na la kifahari.

Walishangaa, walichokitegemea ni kwamba wangeingia ndani ya kanisa kubwa ambalo ndilo waliambiwa kulikuwa na ibada iliyokuwa ikiendelea na maaskofu wengine.

Kwa jinsi walivyoliangalia jumba lile, walijua kabisa sehemu hiyo haikuwa salama hata kidogo, hivyo wakasubiri kuona ni kitu gani ambacho kingetokea.

Wanaume watatu waliokuwa na bunduki wakalisogelea gari lile na kuufungua mlango kisha kuwataka kuteremka.

Walishtuka, kitendo cha kuona watu hao wakiwa na bunduki kikawapa uhakika kabisa kwamba sehemu hiyo haikuwa salama kwani kama ni kanisani, kulikuwa na ibada kusingekuwa na watu waliokuwa na bunduki kama walivyokuwa.

Wakaingizwa ndani ya jumba hilo, lilikuwa la kifahari, walikaa kwenye masofa makubwa huku wakionekana kuwa na hofu kupita kawaida.

Kwenye kuta za jumba hilo hapo sebuleni kulikuwa na picha kadhaa za wanawake waliokuwa uchi wa mnyama, wengine walikuwa wakifanya mapenzi na wanaume mbalimbali, kwa jinsi ilivyoonekana tu, hawakuwa na maswali zaidi, walijua kile ambacho kilikuwa kikienda kutokea ndani ya jumba hiyo.

Wakati wakiwa wametulia, wanaume watatu wakafika sebuleni hapo, walikuwa ni wazee wa umri kuanzia miaka hamsini, walivalia mataulo huku wakiwa na vitambi vya saizi ya kati.

Wakawaangalia wasichana hao, nyuso zao zikaonyesha tabasamu pana na kufurahia uwepo wao ndani ya nyumba hiyo.

“I want that one,” (namtaka huyo) alisema mzee mmoja huku akimuonyeshea kidole Nathalie.

Wanaume hao walijichagulia wasichana hao kama walikuwa sokoni, Nathalie na wenzake walibaki wakishangaa, hawakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, ilikuwaje wapelekwe sehemu hiyo na wakati waliambiwa walikuwa wakienda kuungana na maaskofu kwa ajili ya kufanya ibada?

Wale viongozi waliowapeleka wakaanza kuwaambia maneno ya vitisho kwamba kila kitu ambacho kingetokea mahali hapo kilitakiwa kuwa siri kubwa na kama kungekuwa na mtu yeyote angethubutu kuitoa siri hiyo basi ilikuwa ni lazima auawe kama wengine.

Hawakuishia hapo, waliendelea kuwaambia hiyo ndiyo ilikuwa siri ya kanisa hilo kubwa kujiendeleza. Lilikuwa na pesa nyingi kwa sababu walikuwa na wafadhili wengi ambao wengine walikuwa wazee hao, mabilionea waliokuwa wakilipa kiasi kikubwa cha pesa.

“Kumbukeni, kwa yeyote atakayetoa siri hii, kichwa chake kitakutwa sokoni, lakini pia kila mtakapokuwa mkifanya mapenzi mtakuwa mkipigwa picha na kurekodiwa. Siku ukitoa siri, picha zinawekwa kwenye mitandao ya ngono kabla ya kuuawa,” alisema kiongozi wao ambaye alionekana kutokuwa na hofu kwa kile kilichokuwa kikienda kutokea.

Hilo ndilo lilikuwa kanisa la Living Christ ambalo lilijiendelea kwa kuwauza wasichana waliokuwa wakisomea utawa katika vyuo mbalimbali.

Biashara hiyo ilikuwa ni ya siri kabisa, watu walipata pesa kwa njia za hatari na hawakutaka dunia ijue wala viongozi wao wa juu kabisa wajue kilichokuwa kikiendelea.

Siku hiyo ilikuwa ni nyingine iliyokuwa na maumivu makali mioyoni mwao, ilikuwa ni siku ambayo iliibadilisha mioyo yao na kuichukia dini ya Kikristo kwa kuamini kwamba madhehebu yote yalikuwa yakifanya kama hivyo.

Walifanya mapenzi huku wakipigwa video, iliwauma, walilia lakini wazee hao hawakutaka kuwaacha, ilikuwa ni kama walikuwa wakiigiza mkanda wa ngono na waigizaji maarufu kama Mandingo, Johnny Sin na wengineo.

Baada ya saa tatu, wakamaliza na hivyo kupandishwa ndani ya gari na safari ya kurudi chuo kuanza. Njiani walikuwa wakilia, hawakuamini kile kilichotokea, waliliamini dhehebu lao, waliwaamini viongozi wao lakini kumbe mwisho wa siku walikuwa wakifanyishwa matendo ya kikatili kama yale.

Bado waliendelea kupigwa mikwara mingi kwamba hawakutakiwa kumwambia mtu yeyote yule kwani vinginevyo wangeuawa kikatili na maiti zao kufichwa sehemu au kwenda kuchomwa moto. Hilo likawaogopesha na hivyo kunyamaza kimya.

***

Mabilionea waliendelea kufanya mapenzi na wasichana wabichi kwa malipo ya dola laki tano ambazo zilikuwa ni zaidi ya shilingi bilioni moja kwa kila baada ya miaka mitatu.

Hawakuwa na muda wa kwenda mitaani na kununua machangudoa, kitu walichokifanya kilikuwa ni kuwasiliana na viongozi wa vyuo vya watawa na kuamua kuwalipa malipo makubwa lakini kwa makubaliano ya kupelekewa wasichana warembo kila Jumapili.

Ilikuwa ni biashara kubwa na ya siri sana ambayo hakukuwa na watu wengine waliokuwa wakifahamu kama mabilionea hao walikuwa na tabia hiyo ya kuwachukua wasichana wadogo na kwenda kufanya nao ngono kila Jumapili.

Kule chuoni, kila mmoja alikuwa kimya, kile kilichotokea kilitakiwa kuwa siri kubwa, hawakutakiwa kuzungumza kwa mtu yeyote yule, waliambiwa wanyamaze mpaka siku ambayo wangeingia kaburini.

Huo ndiyo ukawa mchezo, kila siku za Jumapili wasichana walikuwa wakichukuliwa na kupelekwa kwa mabilionea hao na kutumikishwa kingono huku pesa wakipewa viongozi wa chuo hicho.

Siku ziliendelea kukatika, siri ikawa mioyoni mwao, si kwamba wao pekee ndiyo waliokuwa wakifanyiwa michezo hiyo bali nusu ya wanachuo chuoni hapo walikuwa wakifanyiwa michezo hiyo hatari.

Baada ya miezi miwili ya kutumikishwa kingono, Nathalie akafahamiana na msichana mwingine aliyekuwa hapo chuoni, msichana huyo aliitwa Magdalena Khan.

Alikuwa mzuri wa sura, alitokea nchini Ujerumani. Kama alivyokuwa yeye hata msichana huyo naye alikuwa na ndoto za kuwa mtawa siku moja.

Alijitunza kwa miaka mingi huku akimuahidi Mungu kwamba angekufa akiwa bikira lakini baada ya kukutana na Askofu David kwenye usaili, ndoto zake zikafia hapo na kuendelea kutumikishwa kingono hata alipokuwa chuoni.

Magdalena alikuwa na hasira kali, hakutaka kuendelea kuona akinyanyaswa kingono katika miaka mitatu yote ambayo angekuwa chuoni hapo, ilikuwa ni lazima apambane, ni lazima atoroke ndani ya chuo hicho na kwenda nje ambapo huko angesimulia kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Alilia sana, alihuzunika, hakuwa na siri moyoni mwake, baada ya kuzoeana kidogo na Nathalie, akaanza kumuhadithia kile kilichokuwa kikiendelea kila alipokuwa akitolewa chuoni na wenzake kupelekwa sehemu.

Alijua hiyo ilikuwa kwao tu kumbe nusu ya wanachuo walikuwa wakitumikishwa kingono kama wengine. Kwa jinsi alivyokuwa akimuhadithia Nathalie, mpaka msichana huyo akaanza kulia, japokuwa yeye aliumizwa lakini kila alipomwangalia Magdalena, Magdalena alionekana kuumizwa zaidi yake.

“Nathalie! Nina mimba,” alisema Magdalena maneno yaliyomfanya Nathalie kushtuka.

“Una mimba?”

“Ndiyo! Ni siri, ninakwambia wewe tu. Nilipopelekwa kule kutumikishwa kingono, niliambiwa na yule mzee tusitumie kinga,” alisema Magdalena huku akilia.

“Umeuambia uongozi?”

“Ndiyo nafikiria kufanya hivyo!” alisema.

Magdalena hakutaka kuwa kimya, alichokifanya ni kumfuata kiongozi ambaye alikuwa akiratibu biashara hiyo na kumwambia kwamba alikuwa na mimba.

Kiongozi huyo aliyeitwa Fonce Thomas akashtuka, hakutegemea kuambiwa kitu kama hicho kwa kuwa aliamini wasichana wenyewe walikuwa wakijitunza kwa kujua siku zao za hatari.

Akamwangalia sana Magdalena, akajua kabisa kwamba kama wangeruhusu msichana huyo aendelee kuwa na mimba hiyo basi ingekuwa hatari kwao na inawezekana kabisa kila kitu kingejulikana.

Akawashirikisha wenzake na kuwaambia kilichotokea, kama alivyoshtuka yeye, hata nao wakashtuka na hivyo kutakiwa kufanya jambo kuficha hilo.

“Mimba itolewe,” alisema Fonce.

“Hapana! Bado ni tatizo! Nimefikiria kitu kimoja,” alisema mwanaume aliyeitwa kwa jina la Michael.

“Kipi?”

“Huyu msichana auawe! Tunatakiwa tutengeneze ugonjwa ambao utamuua ndani ya mwezi mmoja tu, ufanane na kansa, nitazungumza na daktari mmoja na ninaamini atanipa sumu ya kumuua ndani ya mwezi mmoja,” alisema Michael.

Haraka sana Michael akawasiliana na daktari mmoja na kumwambia kilichotokea kwamba kuna msichana mmoja alitakiwa kuchomwa sindano iliyokuwa na virusi vya Vabyrosis ambavyo vilikuwa na nguvu ya kuufanya moyo wa binadamu kuanza kuchakaa na mwisho wa siku kufa huku akionekana kuwa na kansa ya ndani katika moyo wake na mapafu.

Hilo halikuwa tatizo, daktari huyo akakubaliana naye na hivyo uongozi kumchukua Magdalena na kuondoka naye kuelekea huko hospitalini.

Alichoambiwa ni kwamba uongozi haukuwa ukiamini kama kweli alikuwa na mimba hivyo walikuwa na jukumu na kumchukua na kwenda kumpiga ili kujua ukweli.

Walipofika, hawakuuchukua mkojo wake, wakachukua sindano iliyokuwa na virusi vile na kumchoma, baadaye ndipo wakajifanya kuchukua mkojo wake.

“Ni kweli ana mimba,” alisema daktari.

“Basi sawa!”

Akapewa majibu, alilia sana, hakutarajia katika maisha yake kupata ujauzito kwa kuwa alijiahidi angekufa akiwa bikira.

Wakaondoka hospitalini hapo huku akilia. Hakunyamaza, mpaka anaingia bwenini bado alikuwa akilia sana lakini hakumwambia mtu mwingine kilichotokea zaidi ya Nathalie, aliogopa sana kwa kuwa alipewa vitisho kwamba kama angediriki kumwambia mtu yeyote yule basi wangemchinja.

“Imekuwaje?” aliuliza Nathalie, aliamua kumfuata kisiri usiku.

“Nimekutwa nayo! Moyo umeniuma sana,” alijibu Magdalena.

“Kwa hiyo walikupima tu?”

“Ndiyo! Walinichoma na sindano!”

“Ya nini?”

“Sijajua! Daktari alisema anichome sindano tu!”

“Ila mimba si wanapima kwa mkojo! Sasa kwa nini uchomwe sindano?”

“Sijajua! Ila walinichoma sindano! Unahisi kwamba wanataka kuniua?” aliuliza Magdalena huku akilia, alionekana kuogopa kupita kiasi.

“Hawawezi kukuua!”

“Sasa ile sindano ya nini?”

“Sijajua! Ila hawawezi kuua,” alisema Nathalie huku akimtia moyo.

Kitendo cha kuambiwa alichomwa sindano kikaanza kumtia hofu Nathalie, hakujua hasa dhumuni la msichana huyo kuchomwa sindano hiyo.

Akahisi kulikuwa na kitu nyuma ya pazia, hakutaka kumwambia mtu yeyote yule mpaka aone kile ambacho kingeendelea baada ya hapo.

Lilikuwa jambo lisilowezekana kwa msichana kama huyo kupata mimba halafu uongozi usifanye kitu chochote kile, yaani apate mimba, wamuulize tu, akubali, apimwe, ionekane halafu wakae tu, kwake halikuwezekana.

Akawa na hofu, alitamani kuwashirikisha wenzake lakini akasita, alitaka kuona mwisho wa jambo hilo lingekuwa nini, alihitaji kuona kama Magdalena angekufa au la kwani moyo wake ulimwambia hivi; kama kweli msichana huyo alichomwa sindano ambayo hakuijua, basi kuna jambo lingeweza kutokea, hasa mimba kutoka.

Japokuwa Nathalie alitamani sana jambo hilo likae moyoni mwake na asimwambie mtu yeyote, akashindwa hivyo akawashirikisha wenzake kila kitu kilichotokea kwa msichana huyo kwamba aligundulika ana mimba na alipowaambia viongozi walimpeleka hospitalini ambapo huko akachomwa sindano.

Hiyo sindano ndiyo walishindwa kujua ilikuwa na nini, wakaanza kufuatilia huku wakionekana kuogopa kupita kiasi kwani walikwishagundua kabisa mahali hapo hakukuwa salama tena na kama ingetokea kwa mtu yeyote kupata mimba basi kilichokuwa kikifuata ni kuchomwa sindano ile.

Siku ziliendelea kukatika, baada ya mwezi mmoja hali ya Magdalena ikaanza kubadilika, akaanza kuhisi baridi kali huku mwili wake ukianza kuwasha sana, hakujua kilichokuwa kikiendelea, alikuwa mtu wa kukesha usiku akilia kwani hakujua kitu kilichokuwa kikimsibu mpaka kuwa kwenye hali hiyo.

Viongozi walewale wakamchukua na kumpeleka hospitali ambapo huko iligundulika moyo wake haukuwa ukifanya kazi vizuri na alikuwa na muda mfupi wa kuishi hivyo alitakiwa kujiandaa kufa.

Hilo lilimuumiza sana, alichogundua ni kwamba mimba haikuwa ikimpenda, hakukumbuka kuhusu ile sindano aliyochomwa, alichokikumbuka ni kuhusu mimba tu.

Akarudishwa chuoni huku akilia, wanafunzi wakatangaziwa tatizo alilokuwanalo msichana huyo na kwa sababu alikuwa na ugonjwa huo basi walitakiwa kuungana naye kwenye maombi na kuanza kumuombea.

Nathalie na wenzake walilia sana, waligundua kwamba sindano ile ndiyo iliyokuwa imebadilisha kila kitu na wala haikuwa ile mimba. Walikusanyika kanisani na kumuombea Magdalena lakini walijua kabisa kwamba walikuwa wakifanya kitu ambacho kilikuwa ni bure kabisa.

Hali ya afya yake ilizidi kuwa mbaya. Akaanza kukohoa madonge ya damu, ngozi ikaanza kusinyaa huku rangi yake nyeupe ikibadilika na kuanza kufifia na kwa mbali kuanza kupata unjano fulani.

Haikuishia hapo, alianza kukonda na kuwashwa mwili mzima. Magdalena alikuwa kwenye mateso makali, aliteseka, alilia peke yake chumbani kwake na baada ya siku kadhaa, akafariki dunia huku akiwa kitandani hapo.

Ilikuwa ni huzuni kwa kila mtu, wanafunzi wengi walilia, waliyaona yale aliyokuwa ameyapitia, ilikuwa ni picha yenye kuumiza kwamba msichana yule mrembo ambaye alikuwa na ndoto ya kuwa mtawa mwisho wa siku alikufa kwenye kifo kibaya na kilichokuwa na maumivu kama kile.

Moyo wa Nathalie ukawa na hasira kali, aliumia, alimuomba Mungu, alimlaumu kwa kuruhusu jambo lile. Yeye na wenzake wakaanza kukaa kwa hofu huku wakimuomba Mungu katika miaka yote mitatu ambayo walitakiwa kukaa mahali hapo na kusoma basi awasaidie wasipate mimba na kuwatokea yale yaliyomtokea Magdalena.

Kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma ndivyo ilivyokuwa ikiendelea, bado waliendelea kutumikishwa kingono kila wikiendi huku wakipigwa video za picha zilizokuwa zikionyesha kila kitu kilichokuwa kikifanyika.

“Ni lazima nifanye kitu nipate hizi picha,” alisema Nathalie.

Hicho ndicho alichokuwa akikihitaji, alijua kabisa kwamba picha zile walizokuwa wakipigwa zilihifadhiwa, hawakujua lengo lakini ilikuwa ni lazima afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anazipata picha hizo.

Kwa kuwa alikuwa msichana mjanja na mrembo, kwa yule mwanaume aliyekuwa akifanya naye mara kwa mara akajifanya kumzoea huku akimuonyesha mapenzi matamu kana kwamba alikuwa mume wake wa ndoa.

Alimfanya kujisikia raha, huru na muda mwingi alimwambia kwamba kwa kuwa walizoeana basi ingekuwa vizuri zaidi kama wangekuwa wanafanya kwa uhuru kama mke na mume.

Hilo likamfanya bilionea huyo kumwamini Nathalie na kila alipofika, kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kumuuliza msichana huyo, alimchukua na kuelekea naye chumbani.

Wanaume walikuwa wakibadilishana lakini kwa mzee Kurtson ilikuwa ni tofauti kabisa, yeye alimuhitaji mtu wake ambaye aliamini kwamba aliletwa katika dunia hii kwa ajili ya kuwa naye tu.

Kipindi cha kwanza hakuwa mzoefu sana lakini kwa kuwa mara nyingi alikuwa akifanya mchezo huo, akapata uzoefu, akajua kuzilegeza nyonga zake, akajua kuutumia mdomo yake kikamilifu kitu kilichomchanganya mzee huyo.

Alichowaambia watu wake ni kwamba walitakiwa kuwa wapole kwa Nathalie kwani ndiye alikuwa msichana aliyebadilisha maisha yake na kumuonyeshea ni kwa jinsi gani mapenzi yalitakiwa kufanywa.

“Hii nyumba yangu ni nyumba yako pia,” alisema mzee Kurtson huku akimwangalia Nathalie aliyekuwa pembeni yake akimchezea kifua chake.

“Kweli bebi?”

“Ndiyo! Yaani wewe jisikie huru kabisa,” alisema.

“Na hao wanaume wengine kwenye vyumba vingine?” aliuliza.

“Hao huwa wanakuja kulala na kuondoka, ila mwenye nyumba ni mimi,” alitamba mzee huyo.

“Nashukuru kulifahamu hilo bebi!” alisema Nathalie, hapohapo akamnyonya mdomo na kuanza kubadilishana mate.

Hayo yote alikuwa akiyafanya kwa kulazimishwa, alihitaji kuzipata picha zilizokuwa zikipigwa, hakujua ni kwa jinsi gani angezipata lakini aliamini kwa sababu alianza kuzoeana na mwanaume huyo basi ingekuwa rahisi kwake kuzipata picha zote.

“Ila nataka ufanye kitu kimoja!” alisema Nathalie kwa sauti nyembamba.

“Chochote utakacho!”

“Nikiwaga chuo huwa ninakukumbuka sana, hivi huwezi kuniruhusu hata siku za masomo niletwe peke yangu bebi nije kulala na wewe mpaka asubuhi?” aliuliza.

“Hilo si tatizo! Ngoja nizungumze na viongozi wako,” alisema.

“Au wewe hutaki?”

“Nataka sana bebi! Yaani nilitamani mno kitu hicho kitokee,” alisema mzee huyo.

Siku hiyo hiyo akazungumza na viongozi wa chuo hicho cha watawa na kuwaambia kuhusu kile alichoambiwa na Nathalie, hilo halikuwa tatizo kwa sababu aliahidi kutoa malipo makubwa zaidi.

Wakakubaliana naye hivyo Nathalie kuchukuliwa siku za kawaida peke yake na kupelekwa huko. Hakukuwa na mtu aliyejua kilichokuwa kikiendelea, kwenye hilo, hakutaka kuwaambia hata marafiki zake, alihitaji kulifanya hilo yeye peke yake.

Kila alipokuwa akiingia katika nyumba hiyo, ndani alikuwa yeye na mzee huyo, wafanyakazi wawili na walinzi ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kulinda nyumba hiyo.

Kila kona kulikuwa na kamera, alihitaji kuzipata picha zilizokuwa zikipigwa kwa kamera hizo na ndiyo maana aliona ili kuzipata kwa urahisi ilikuwa ni lazima aende huko na kujifanya kama alikuwa akihitaji kuwekwa ndani kabisa.

Kila alipofika kitu cha kwanza kilikuwa ni kwenda jikoni na kupika chakula, alikuwa akifanya kila kitu kana kwamba alikuwa ameolewa.

Mzee Kurtson ambaye alikuwa kazini, kila aliporudi alikuta kila kitu kikiwa tayari na hivyo kufikia kula na baada ya hapo ilikuwa ni kwenda kuzikonga nyoyo zao kitandani.

Hilo liliendelea kwa mwezi mzima, kazi yake ilikuwa kila Jumamosi, Jumanne na Alhamisi ni kwenda kwa mzee huyo kumbe kazi kubwa ilikuwa ni kuhangaika kuzipata picha zile.

Huko, akazoeana na kijana aliyeitwa Armando ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kushughulika na mambo yote ya zile kamera na kuzihifadhi picha zilizokuwa zikipigwa kila siku.

Alipogundua hilo, hakutaka kuchelewa, akaanza kuweka urafiki naye kwa karibu. Kijana huyo aliogopa, alijua kabisa kwamba mzee Kurtson alikuwa mtu hatari kama tu angegundua kwamba alikuwa karibu na msichana huyo.

Alijaribu kumkwepa lakini Nathalie hakukwepeka, kila alipofanya hili na lile, msichana huyo alikuwa karibu naye.

“Armando...” alimuita Nathalie kwa sauti ndogo.

“Nini?”

“Ninakupenda sana mpenzi!” alimwambia.

“Unanipenda mimi? Naogopa, bosi atajua!” alisema.

“Kwani utamwambia?”

“Hapana!”

“Sasa atajuaje?” aliuliza Nathalie.

Hakujibu swali hilo kwani alishtukia kinywa cha Nathalie kilikwenda kinywani mwake na kuanza kubadilishana mate huku akianza kuchezewa sehemu ya zipu.

Kijana huyo akachanganyikiwa, Nathalie alijua jinsi ya kumdatisha mwanaume, alimfanyia matendo ya hatari ambayo yalimfanya kijana huyo kulalamika kimahaba kupita kawaida.

Siku ya kwanza walifanya kwa siri, walipomaliza, akavaa nguo zake na kuelekea kitandani kwa mzee Kurtson na kulala hapo mpaka mzee huyo aliporudi na kupokelewa kwa mahaba tele.

Huo ndiyo ulikuwa mchezo wao, muda wote Nathalie alikuwa makini kutaka kugundua mahali memori kadi zilipokuwa zikikaa, alipogundua tu, kazi ikawa kwake kumpagawisha mwanaume huyo mpaka apate nafasi ya kuichukua.

Hilo halikuwa jambo gumu kama alivyofikiria kwani ilimchukua wiki moja tu, akafanikiwa kuichukua na kuiweka kwenye kitambaa cha nywele zake na kuifunga vilivyo kisha kurudi chumbani huku akiziacha kamera zile zikiwa hazina memori kadi ambayo ilikuwa ikitumika kurekodi kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Aliporudi chuo siku hiyo akawaita marafiki zake na kuwaambia kila kitu kilichokuwa kimeendelea kwamba alifanya kila liwezekanalo kuhakikisha akipata memori kadi na alifanikiwa hivyo baada ya kuondoka hapo Sweden, kazi ilikuwa ni kwenda kuziprinti na kumtafuta mwanaume ambaye angewasaidia kuzipeleka picha hizo makao makuu.

***

“Memori kadi ipo wapi?”

“Nimeihifadhi ndani, ina picha na video zote.”

“Kweli?”

“Ndiyo!” alijibu Nathalie kitu kilichomfanya kila mtu kuwa na furaha.

Japokuwa alipata alichokuwa akikihitaji lakini hakutaka kuacha kwenda nyumbani kwa mzee Kurtson, ilikuwa ni lazima afanye hivyo kwa sababu alihisi kwamba kama angekatisha kwenda basi inawezekana angegunduliwa kila alichokuwa amekifanya.

Aliendelea kwenda huko huku akimuomba Mungu asipate mimba kwani alijua kabisa kwamba kama kitu hicho kingetokea basi ilikuwa ni lazima na yeye auawe kama alivyokuwa kwa Magdalena.

“Mungu nisaidie katika hili,” alisema huku akiwa ameishika rozali yake.



Sehemu ya Tano.


Miezi ilizidi kusonga mbele, miaka ikakatika na baada ya miaka mitatu, watatu hao na wanafunzi wengine wakamaliza chuo na hivyo kutakiwa kuondoka kurudi nchini mwao ambapo waliunganishwa na makanisa ya huko kwa ajili ya kwenda kumtumikia Mungu.

Tiketi za ndege zikakatwa lakini kabla ya kuondoka, wanafunzi wote wakaitwa kwenye chumba maalumu na kuanza kupewa maneno ya mwisho juu ya kila kitu kilichotokea.

Kubwa zaidi ilikuwa ni kutunza siri, hayo yalikuwa ni maagizo ya kanisa hilo na kila mtu ambaye alionekana kuwa mtawa kwenye kanisa hilo, alipita kulekule walipokuwa wamepita hivyo hakukutakiwa kwa mtu yeyote kwenda kusema siri hiyo sehemu yoyote ile kwa usalama wa kanisa.

“Kama tutakugundua, tutakuua kama tulivyowaua wengine ambao walifanya kinyume na kile tulichowaambia,” alisema mkuu wa chuo hicho aliyeitwa Askofu Andrew Markov.

Baada ya kuambiwa maneno mengi ya vitisho, wakaletewa simu na kuambiwa wazichukue kwa ajili ya mawasiliano mara baada ya kuondoka katika chuo hicho.

Waliambiwa kwa kawaida chuo hicho kiliingia ubia na kampuni ya kutengeneza simu za Mercury ya nchini Ujerumani kwa ajili ya kuwawezesha watu wao kuwasiliana na hata kutumia internet kwa kasi kubwa.

Wakapewa simu hizo, zilikuwa nzuri, walizipenda na siku iliyofuata wakaingia ndani ya ndege na kuondoka.

Nathalie alikuwa akielekea nchini Marekani huku Mary na Anna wakielekea nchini Canada. Katika kipindi cha nyuma walichokuwa wakienda nchini Sweden kwa ajili ya kukamilisha ndoto zao za kuwa watawa, walikuwa na furaha tele, waliona kabisa maisha yao yalikuwa yakienda kubadilika lakini kile walichokutana nacho huko kiliwafanya kulia mno kiasi kwamba hata safari hiyo ilionekana kuwa mbaya kwa maisha yao.

Ndege ilichukua saa kadhaa, ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Toronto Pearson uliokuwa katika Jiji la Toronto ambapo wawili hao wakateremka na kumuacha Nathalie akielekea nyumbani kwao nchini Marekani.

Ndege ilichukua saa kadhaa ikafika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JKF ambapo akateremka na kukutana na kaka yake, Gabriel aliyeonekana kushtushwa na hali aliyokuwanayo kwani hakuwa na furaha kama alivyoondoka, pamoja na kukamilisha ndoto yake ya kuwa mtawa lakini alionekana kuwa na maumivu makali mno.

Gabriel hakumuuliza kitu, wakaingia, wakaondoka mahali hapo. Njiani walikuwa kimya, Nathalie alikuwa na mawazo tele, kile kilichokuwa kimetokea nchini Sweden kilimuumiza kupita kawaida.

Baada ya dakika kadhaa wakafika nyumbani ambapo Gabriel akateremka, akafungua buti la gari na kutoa begi na mizigo mingine ya ndugu yake na kisha kuelekea ndani.

Siku nzima hiyo ilikuwa ni ya mateso kwa Nathalie, alibaki akilia, kumbukumbu ya kile kilichokuwa kimetokea nchini Sweden kilimuumiza mno. Alilia sana lakini hakuweza kubadilisha kitu chochote kile.

Alikuwa na memori kadi yake, baada ya siku mbili akawapigia simu wenzake na kuwaambia kwamba ilikuwa ni lazima waonane nchini Marekani kwa ajili ya kuzungumza ili wajue ni kitu gani kilitakiwa kufanyika na nani ambaye walitakiwa kumwamini kipindi hicho.

“Kuna mtu anaitwa Zion, anaishi nchini Ujerumani, nimezoeana naye, nadhani huyo ni mtu sahihi sana kama tutakutana naye na kuzungumza,” alisema Anna.

“Unahisi ataweza kuzifikisha hizi picha makao makuu ili kuwaokoa wasichana wengine ambao watakwenda kusomea utawa?”

“Nadhani! Nina uhakika ataweza kusaidia,” alisema Anna, wakati huo walikuwa wameunganisha simu kwa watu watatu na hivyo kulijadili suala hilo.

Nathalie akawaambia kwamba ilikuwa ni lazima kuhakikisha kila mmoja anakuwa na picha hizo kama ushahidi ambao ungetumika katika kanisa hilo na hata mahakamani ili watu wote watiwe nguvuni na kuhukumiwa kwa kile walichokuwa wamewafanyia.

“Haina shida.”

“Ila kwanza tuonane,” alisema Nathalie.

Wakaonana nchini Marekani na kuanza kulizungumzia suala hilo, ilikuwa ni lazima wajadili kwa pamoja na kujua ni kitu gani ambacho walitakiwa kufanya ili kuhakikisha watu wote waliokuwa wamehusika katika mchezo huo wanafungwa gerezani na hata washirika wengine wa kanisa hilo waachane nalo kwani halikuwa kanisa la kumtumikia Mungu kama walivyokuwa wakiaminishwa.

“Basi wasiliana naye!”

“Haina shida! Hilo ondoeni shaka. Natumaini tutarekebisha, atakuja hapa na tutampa hizi picha,” alisema Anna. Picha zile zikaprintiwa na kila mtu kukabidhiwa zake na kuondoka.

***

Viongozi wa kanisa la Living Christ walikuwa makini kwa kila kitu, hawakutaka kumwamini mtu yeyote yule, waliwajua wanawake, walikuwa watu wenye mioyo mepesi ambao hawakuwa na uwezo wa kutunza siri kwa kipindi kirefu na ndiyo maana hata walipokuwa wakiondoka mahali hapo ilikuwa ni lazima kuwafuatilia.

Ufuatiliaji wao ulikuwa ni wa kisasa kabisa, hawakutaka kutuma mtu bali kwa zile simu ambazo waliwakabidhi siku ya mwisho kabla ya kuondoka chuoni hapo ndizo ambazo zilikuwa zikitumika kunasa mawasiliano yao.

Ilikuwa ni kazi nyepesi kujua walikuwa wakiwasiliana na nani, hakukuwa na ugumu wa kufahamu ni mahali gani watu hao walipokuwa.

Walifuatilia kila kitu na hata wasichana hao watatu walipokuwa wakiongea na kupanga mipango yao, waliwafuatilia kwa karibu kabisa.

Waligundua kwamba walifanya mpango wa kuonana nchini Marekani, mbali na kifaa cha GPS walichokuwa wameweka ndani ya kila simu pia kulikuwa na kimaiki kidogo ambacho kilinasa mazungumzo, kiliyarekodi na kuyatuma kule chuoni ambapo viongozi walikuwa wakiyasikia.

Waliposikia kwamba wasichana hao walikuwa na picha juu ya kilichokuwa kimetokea huko Sweden, walichanganyikiwa, hawakulitegemea hilo kwani waliamini kwamba kila kitu kilikuwa siri kubwa na hakukuwa na mtu yeyote ambaye aliruhusiwa kwenda na simu, sasa ilikuwaje mpaka watu hao wapate picha hizo?

Wakajua kulikuwa na kitu kilichokuwa kimetokea, haraka sana wakafuatilia maisha ya wasichana hao chuoni hapo, wakagundua Nathalie ndiye aliyekuwa na nafasi ya kwenda nje ya chuo hicho kuonana na bilionea Kurtson na inawezekana kabisa mtu huyo ndiye aliyeruhusu picha za kila kitu kilichokuwa kimetokea kuibwa.

Haraka sana wakampigia simu na kuanza kuzungumza naye, waliongea kwa hasira, kwao waliona kama walikuwa wakigeukiwa kwani hawakutegemea kama kungetokea kitu kama hicho.

Mzee huyo alipoambiwa kuhusu picha hizo, akashtuka, hakutegemea kuambiwa kitu kama hicho na hivyo kuuliza zaidi huku akitaka kupewa ufafanuzi kwamba ni kwa namna gani msichana Nathalie alichukua picha hizo na wakati zilikuwa zikirekodiwa na kamera za CCTV.

“Hatujui! Kwanza kuna memori kadi?” aliuliza kiongozi mmoja.

“Ndiyo!”

“Ndiyo umekwenda kuangalia au?”

“Subiri!”

Mzee huyo akaondoka na kwenda kwenye chumba cha kuhifadhia video na picha ambapo akamkuta kijana wake Armando akiendelea kufanya kazi yake.

Kitu cha kwanza kabisa ni kumuuliza kuhusu memori kadi. Kijana huyo hakuwa na hofu, alichojua ni kwamba memori kadi ilikuwepo na ilikuwa ikirekodi kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Akakifuata kifaa ambacho kilikuwa kikihusika na kutunza kumbukumbu kutoka kwenye memori kadi, alipokifungua na kuangalia ndani, memori kadi haikuwepo.

Alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alichokijua ni kwamba kila siku memori kadi hiyo ilikuwa humo, sasa iweje isionekane? Iweje leo ionekane kwamba hakukuwa na kitu chochote kilichokuwa kikirekodiwa?

“Vipi?” aliuliza mzee Kurtson.

“Memori kadi haipo,” alijibu Armando.

Mzee huyo alichanganyikiwa, hakujua ni kitu gani alitakiwa kuwaambia wanaume hao ambao nao walionekana kama kuchanganyikiwa kama yeye. Kabla ya kuwapigia simu kwanza akakaa chumbani kwake, hakujua ni kitu gani alitakiwa kuwaambia.

Kama kweli aliruhusu mpaka memori kadi ile kuchukuliwa, inamaana huo ndiyo ungekuwa mwisho wa yeye kupelekewa wasichana kwa kuwa tu iligundulika hakuwa makini na kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Alikaa kwenye hali hiyo kwa dakika kadhaa, akachukua simu yake na kuwapigia kisha kuwaambia kilichotokea. Kwanza akakaripiwa kama mtoto mdogo lakini uamuzi wa mwisho uliotolewa ni kwamba hakutakiwa kupelekewa wasichana kama ilivyokuwa.

“Nahitaji mnisamehe! Nitaishi vipi bila kuwapata wasichana hao?” aliuliza mzee huyo, alikuwa akilia kama mtoto, kufanya mapenzi na wasichana wadogo ndiyo ilikuwa tabia yake, alizoea tangu alipokuwa na miaka ishirini, mpaka miaka hiyo ya hamsini na tano, starehe yake ilikuwa ni kufanya mapenzi na wasichana wabichi.

Viongozi hao walikuwa wakijadili ni kitu gani kilitakiwa kufanywa ilimradi wawanyamazishe wasichana hao kwa nguvu kubwa.

Hawakujali kuhusu pesa, kitu pekee walichokihitaji ni kuona ile siri waliyokuwanayo inaendelea kufichwa kwa nguvu kubwa.

Wakati wakiendelea kuwafuatilia ndipo wakagundua kwamba walitaka kuonana na mwanaume aliyeitwa kwa jina la Zion aliyekuwa nchini Ujerumani ambaye ndiye angepewa picha hizo na kuzipeleka makao makuu.

Hawakutaka kukubali, haraka sana wakaanza kumfuatilia mwanaume huyo kupitia namba yake ya simu. Waliweza kumpata na ilionyesha kwamba alikuwa katika Jiji la Berlin, ilikuwa ni lazima kutafutwa hukohuko.

Kwa kupitia namba ileile, wakaangalia usajili wake, nyumba aliyokuwa akiishi, na kipindi hicho Zion alikuwa akisoma katika Chuo Kikuu cha Berlin masomo ya Utabibu.

“Ni lazima auawe haraka sana!” alisema mwanaume mmoja kwenye chumba hicho.

Mawasiliano yakafanyika harakaharaka baina yao na vijana wao waliokuwa nchini Ujerumani na kuwapa kazi moja ya kumuua mwanaume huyo.

Kwa kupitia simu yake wakafanikiwa kupata mpaka picha yake na kuwatumia ambapo baada ya kuipata tu, wakafanikiwa kwenda chuoni, walipomkosa wakaelekea nyumbani kwake.

Huko wakamkuta, wakajitambulisha kwamba walikuwa ni polisi kutoka makao makuu ya polisi hapo Berlin na walifika mahali hapo kwa kuwa walitakiwa kumchukua na kwenda naye kituoni.

“Kuna nini?” aliuliza Zion.

Walimwambia walifuatilia mawasiliano yake kwa njia ya simu na kugundua aliwasiliana na magaidi kutoka katika kundi la kigaidi la Al Qaida lililokuwa na makazi yake huko Mashariki ya Kati.

Zion akashtuka, katika maisha yake hakuwahi kuwasiliana na watu kutoka huko Uarabuni lakini hata kabla hajakubaliana kufuatana na watu hao, akahitaji vitambulisho vyao, wakamuonyeshea, akaridhika na kukubali kuondoka nao.

Njiani, hakuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alijaribu kuvuta kumbukumbu zake, hakuwahi kufanya mawasiliano na Waarabu, sasa iweje watu hao wamwambie aliwahi kufanya mawasiliano hayo?

Hakujua nyuma ya pazia mpango uliokuwa umefanywa, hakujua kama alitakiwa kuuawa haraka iwezekanavyo.

Alikuwa kimya ndani ya gari, huku wakiwa wamefika katika makutano ya Barabara iliyokuwa ikielekea mjini Koln, akashtukiwa akiguswa na kitu cha baridi ubavuni, alipoangalia, macho yake yakatua kwenye bastola ndogo aina ya Revolver 90.

“Hutakiwi kutingishika, la sivyo utumbo wako utamwagika humuhumu,” alisema mwanaume aliyekaa upande wake wa kushoto, kijasho chembamba kikamtoka, akajua kabisa siku hiyo ndiyo ilikuwa ya mwisho kuvuta pumzi ya dunia hii.





Nathalie na wenzake walikuwa na uhakika kwamba Zion angefika nchini Marekani kuchukua hizo picha na kuzipeleka nchini Ubelgiji katika makao makuu ya Kanisa la Living Christ.

Kwa muda huo hawakutaka kumwamini mtu yeyote zaidi ya mwanaume huyo, si kwa njia ya barua pepe na wala DHL, kwa zile picha walizokuwanazo zilibeba siri kubwa mno ambayo haikutakiwa kugundulika na mtu yeyote zaidi ya viongozi wa juu wa kanisa hilo.

Walichokifanya ni kumsubiri, Zion aliwaambia ndani ya siku mbili angekuwa nchini Marekani lakini kitu cha ajabu kabisa, baada ya siku ya pili kuingia tu hakuwa akipatikana kwenye simu, na mbaya zaidi hakuwa amekwenda nchini Marekani.

Hilo liliwashangaza mno, hawakujua ni kitu gani kilitokea, walichokitegemea ni kwamba mwanaume huyo angefika huko lakini cha ajabu kabisa hakutokea jambo ambalo wakati mwingine liliwafanya kuhisi alitaka kuwauza.

Waliumia mioyoni mwao, Zion akawaonyeshea kwamba hawakutakiwa kumwamini mtu mwingine yeyote hivyo kama kweli walihitaji kuzipeleka picha hizo huko makao makuu, walitakiwa kwenda wao na si kumwambia mtu mwingine.

“Nani aende?” aliuliza Nathalie.

“Nitakwenda mimi!” alijibu Anna huku akiwaangalia wenzake.

“Una uhakika utafika salama?”

“Kwa hilo msijali!” alisema msichana huyo huku akionekana kujiamini kupita kawaida.

Haukuwa uamuzi mbaya, waliona kabisa kwamba kama kweli Anna alitaka kuzipeleka picha hakukuwa na tatizo lolote lile hivyo wakakubaliana naye kuelekea huko.

Siku iliyofuata, Anna akajiandaa tayari kwa kuanza safari hiyo. Saa mbili kabla ya kuanza safari hiyo, waliwasiliana na mkuu wa kanisa hilo, Askofu Richard Poff aliyekuwa nchini Ubelgiji na kuzungumza naye kwa dakika kadhaa huku wakimwambia kulikuwa na kitu cha siri sana na kama wasingechukua hatua kama kanisa basi wangeweza kuliona likianguka kutokana na aibu ambayo ingelikumbuka.

Askofu Poff alishtuka, hakuamini kusikia maneno kama hayo, hakujua ni kitu gani kilizungumziwa, hakujua kulikuwa na nini ambacho wasichana hao walikuwanacho hivyo kukubaliana nao kwamba mmoja aende nchini Ubelgiji na kumpa kitu hicho.

Baada ya muda wa safari kufika huku akiwa na tiketi yake ya Shirika la Ndege la American Airlines, Anna akaagana na wenzake na kuingia kwenye ndege huku akiwa na begi lake ambalo kwa ndani kulikuwa na picha hizo.

Ndani ya ndege hakuzungumza na mtu yeyote yule, alikuwa kimya kabisa, aliogopa, alihisi kabisa kwamba kama kungekuwa na mtu ambaye alifahamu kile kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni lazima kumchezea mchezo hivyo kupoteza kila kitu alichokuwanacho.

Kwenye kiti cha watu wawili alichokuwepo alikaa na mwanaume mmoja wa Kizungu kama yeye ambaye kwa kumwangalia tu alionekana kuwa mchangamfu ambaye muda mwingi alitamani kuzungumza na Anna ambaye alivalia vazi la kitawa huku akionekana kuitilia umakini mkubwa safari yake.

Mwanaume huyo hakutulia, pale alipokaa alikuwa akibabaika huku muda mwingi akijaribu kuweka ukaribu na Anna lakini msichana huyo hakumpa nafasi hiyo.

“Where to sister?” (unakwenda wapi mtawa?) alimuuliza huku akimwangalia kwa uso uliokuwa na tabasamu pana.

“Belgium!” (Ubelgiji) alijibu kwa kifupi.

“Ooh! To preach the Word of Living God?” (Ooh! Kulihubiri Neno la Mungu aliye hai?) aliuliza.

“Yes!” (ndiyo)

Majibu yake yalikuwa ni kwa kifupi sana, hakuhitaji kuzoeana na mtu yeyote yule, alihitaji kuwa mkimya huku akiwa peke yake, kwenye safari hiyo ambapo alibeba siri kubwa alitakiwa kuwa makini, hakukutakiwa kuzoeana na mtu yeyote yule kwa kuogopa kufanyiwa mchezo mbaya.

Baada ya ndege kukaa angani kwa saa ishirini na sita ndipo ikaanza kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Brussels uliokuwa jijini humo nchiniUbelgiji, akateremka na abiria wenzake na kuanza kuelekea kwenye jengo la uwanja huo kwa ajili ya upekuzi kisha kuondoka.

Hakuwa na mizigo mingi zaidi ya hilo begi alilolibeba, moja kwa moja alipoonekana hakuwa na tatizo lolote lile, akaanza kuelekea nje ya uwanja huo mahali kulipokuwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa wakiwasubiria wageni wao, hapo akamuona msichana mmoja akiwa ameshika bango lililoandikwa jina lake huku akiwa amevalia vazi la kitawa.

Alipoyakutanisha macho yake na msichana huyo, akaachia tabasamu pana na kuanza kumsogelea. Alipomkaribia, wakasalimiana Kikristo na kisha kumchukua na kuelekea naye ndani ya gari.

“Huyu ni Askofu Martin ambaye tumetumwa kuja kukupokea mtumishi wa Mungu,” alisema msichana huyo aliyejitambilisha kwa jina la Lucy ambaye kwa kumwangalia tu ilikuwa ni rahisi kugundua alikuwa mtumishi wa Mungu mzuri tu.

“Nimefurahi kukufahamu,” alisema Anna huku akimpa mkono Martin.

Watatu hao wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea makao makuu kuanza. Lucy ndiye aliyekuwa akiendesha gari huku pembeni yake akiwemo Martin, walikuwa wakipiga stori za kidini tu, muda wote walizungumza matendo makuu ambayo Mungu aliendelea kuwatendea katika maisha yao kiasi kwamba hata Anna aliamini kwamba watu hao walikuwa upande wake.

Baada ya dakika kadhaa, huku stori zikiwa zimenoga, gari likasimama kwenye mataa, hata kabla hawajafanya kitu chochote kile, wanaume wawili waliokuwa na miili mikubwa wakaingia ndani ya gari hilo kwa nyuma, mmoja aliingilia mlango wa kushoto na mwingine mlango wa kulia.

Anna akashtuka, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea. Huku hata kabla hajauliza swali lolote lile, wanaume hao wakatoa bastola zao na kuzishika huku wakimtaka msichana huyo atulie kwani kama angefanya kitu chochote kile au hata kupiga kelele basi wangeweza kumuua humohumo na kusingekuwa na mtu yeyote ambaye angejua.

“Tulia hivyohivyo kama unataka kupigwa picha. Ukitingishika tu au hata kupiga kelele, kitakachotokea ni roho yako kuacha mwili,” alisema jamaa aliyekuwa upande wa kulia.

Anna alibaki akitetemeka, kijasho chembamba kikaanza kumtoka, hakujua kilichokuwa kikiendelea. Martin na Lucy ni kama hawakuona vile, bado walikuwa wakiendelea na stori zao za kumsifu Mungu kama kawaida yake kana kwamba walikuwa gari tofauti.

Baada ya dakika moja, mataa yakaruhusu na kuondoka mahali hapo. Anna alibaki akitetemeka, mapigo ya moyo yalikuwa yakidunda kwa kasi, hakuwajua watu hao walikuwa akina nani, hakujua walitaka nini mpaka kuingia ndani ya gari hilo.

***

Simu zilipigwa katika vyuo mbalimbali vya utawa vilivyokuwa vikihusika na michezo hiyo ya ajabu. Kila mtu aliyesikia kile kilichokuwa kikiendelea, aliogopa na kuona kama wasingefanya kitu fulani basi ingekuwa hatari zaidi kwao.

Walichokipanga ni kufuatilia mawasiliano ya wasichana hao na hata zile stori walizokuwa wakipiga kuhusu kile kilichoendelea.

Walichokigundua ni kwamba mtu aliyewasiliana naye alikuwa Zion, watu wakatumwa na kwenda kumuua kisha mwili wake kuuchoma moto katika jumba moja la Bilionea Mitchel ambaye naye alikuwa akihusika kununua watawa waliokuwa katika chuo kimoja kilichokuwa huko Berlin.

Kwenye mazungumzo ya wasichana hao ndipo wakagundua mmojawao aliamua kusafiri yeye mwenyewe kwenda nchini Ubelgiji kukabidhi picha zile kwa Askofu Poff kitu.

Msichana huyo alitakiwa kunyamazishwa haraka sana hivyo baada ya kujua ni muda gani alikuwa akisafiri, wakajipanga kumpokea huku wakijifanya kutoka kwa askofu huyo ambaye bado aliendelea kujiuliza maswali mengi kuhusu kile walichokuwanacho wasichana hao ambao walisema ilikuwa ni hatari tupu na kanisa lingekwenda kuchafuka.

Hawakutaka kuona msichana huyo akifika kwa Askofu Poff, ilikuwa ni lazima kumnyamazisha hata kabla ya kusimama mbele ya mwanaume huyo.

Ili kumpata kwa urahisi, aamini kwamba walitumwa na askofu huyo, wakaamua kumtafuta msichana ambaye alitakiwa kuvalia kitawa na kwenda huko ilimradi asimtilie shaka kwa lolote lile.

Walipompata msichana huyo wakamjaza maneno na kumlipa kiasi kizuri cha pesa na kumwambia aende uwanja wa ndege akitangulizana na mwanaume mmoja.

Walipofika, walimpokea Anna na kuondoka naye kuelekea mahali walipoambiwa wampeleke.Waliambiwa kila kitu kwamba mara baada ya kufika katika makutano ya barabara nne, kungekuwa na foleni hivyo hapo dereva alitakiwa kutoa loki za milango na wanaume wawili wangeingia ndani.

Hilo likafanyika na wanaume hao kuingia ndani ya gari hilo na kuanza kuondoka. Safari hiyo iliishia ndani ya jumba moja, Anna akateremshwa na kupelekwa ndani huku akitetemeka kupita kawaida.

Kitu cha kwanza akapokonywa picha alizokuwanazo na kufungiwa ndani ya chumba kimoja na kuanza kupewa adhabu kwa kile alichotaka kukifanya.

Aliteswa sana, alichapwa mijeredi, alipigwa shoti ya umeme na kupewa mateso mengine makali. Aliumia, mwili ulikosa nguvu mpaka kufikia hatua ya kuomba Mungu aichukue roho yake lakini si kuona akiendelea kuteseka kama ilivyokuwa.

“Kill me! I don’t deserve to live, just kill me now,” (niueni! Sistahili kuishi, niueni tu) alisema Anna kwa sauti ya chini ambayo ilikuwa ni rahisi kugundua ni kwa kiasi gani alikuwa akisikia maumivu makali mwilini mwake.

Haraka sana simu ikapigwa mpaka kwa viongozi hao na kuwapa taarifa kwamba msichana huyo alikuwa amepatikana na walikuwa naye.

Viongozi hao walitoa amri moja tu kwamba kama Anna alikuwa mikononi mwao ilikuwa ni lazima wamuue na kuzipeleka picha hizo kwa mmoja wa viongozi wa chuo cha watawa kilichokuwa hapo Ubelgiji kwani naye pia alikuwa akihusika kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

“Muueni tu! Nyama yake mtawapa mbwa wale, si vizuri wanyama kuwanyima chakula,” alisema kiongozi aliyekuwa upande wa pili.

Hawakutaka kusubiri au kusikia amri nyingine. Mwanaume mmoja akaelekea katika chumba alichokuwa Anna, alipofika humo akachukua bastola yake na kumuwekea kichwani.

“Unakufa! Utamwambia Mungu kwamba umbeya wako ndiyo uliokumaliza,” alisema mwanaume huyo na mlio wa risasi kusikika.

“Paaaaa...”

Risasi hiyo ikatoka na kumpata Anna kichwani mwake, damu zikaruka, ubongo ukafumuka na kuanguka chini huku damu nyingi zikimtoka kichwani. Ulikuwa ni unyama wa aina yake, viogozi hao walikuwa wakifanya kila liwezekanalo kuwazima watu wote ambao walitaka kwenda kupeleka taarifa juu ya kile kilichokuwa kikiendelea katika vyuo mbalimbali vya watawa.

Walipoona Anna amekufa, wakambeba, wakamvua nguo zote na kumpeleka kwenye banda lililokuwa na mbwa zaidi ya watano waliokuwa na njaa kisha kumtupa humo ambapo mbwa hao wakaanza kumgombea na kumla mpaka walipobakiza mifupa tu.




Nathalie na Maria walikuwa wakiendelea kusubiri. Anna alipofika jijini Brussels, tena akiwa pale uwanja wa ndege aliwasiliana nao na kuwaambia aliingia salama na hivyo alijiandaa kuelekea nje ambapo angechukua teksi mpaka makao makuu ya kanisa hilo.

Wakapumua na kuona wangefanikiwa kwa kile walichokitaka lakini kwa bahati mbaya baada ya hapo hawakuweza kuwasiliana naye tena. Walimpigia simu, ilikuwa ikiita, haikuwa ikipokelewa na baada ya saa moja, kila walipokuwa wakipiga haikuwa ikipatikana kabisa.

Walichanganyikiwa, hawakujua ni kitu gani kiliendelea. Walikubaliana kuwasiliana naye kila hatua aliyokuwa akipitia lakini jambo la ajabu kabisa, hakuwasiliana nao tena kitu kilichowapa presha na kuhisi inawezekana kulikuwa na jambo baya lilitokea huko.

Walijipa moyo kila kitu kingekuwa salama kabisa, walivumilia na kusubiri kwa kuhisi Anna angewapigia simu lakini haikuwa hivyo. Hiyo ilikuwa siku ya kwanza tu, ya pili ikaingia, ya tatu mpaka wiki nzima inakatika hawakupata simu kutoka kwa msichana huyo, wakahisi kulikuwa na tatizo sehemu na inawezekana alipata ajali na kufa baada ya kufika nchini Ubelgiji.

Wakabaki wawili, ilikuwa ni lazima kuhakikisha picha hizo zinafika makao makuu. Hawakutaka kumwamini mtu, kama ni kufa walikuwa tayari kufa lakini si kuona wakishindwa kabisa kuzipeleka zile picha mahali ambapo zilitakiwa kufika haraka iwezekanavyo.

Muda wote huo, wakati wakifanya mipango Gabriel alikuwa akiwafuatilia, moyo wake ulimuuma mno, kitendo cha dada yake kufanyiwa vitendo vichafu alipokuwa akisomea utawa nchini Sweden kulimpa hasira na kutamani kuonana na watu hao ambao walimfanyia ndugu yake huyo vitendo hivyo.

Alisikiliza mazungumzo yao yote, rafiki yao alikwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kupeleka picha hizo lakini hawakupata mawasiliano kutoka kwake. Hilo likamfanya kuwa na wasiwasi kwamba inawezekana msichana huyo alikuwa ameuawa na watu hao.

Akahisi kwamba watu hao walikuwa na mtandao mkubwa, kama waliweza kufanya jambo kubwa kama hilo ilikuwa ni lazima kujilinda hivyo alikuwa na uhakika kwamba wasichana hao walikuwa wakifuatiliwa na ndiyo maana hata baada ya Anna kufika huko hakuweza kupatikana.

Hakujua ni kwa jinsi gani angemwambia Nathalie kile kilichokuwa kikiendelea, alitamani kuwapa mbinu lakini swali kubwa ambalo alihisi kabisa angeulizwa ni kuhusu mahali alipozipata taarifa hiyo. Akaacha huku akiendelea kufuatilia kimyakimya ili kuona ni kitu gani kingeendelea.

Kila siku Nathalie alionekana kuwa mnyonge, asiyekuwa na furaha hata kidogo. Hilo lilimuumiza kaka yake lakini hakutaka kuonyesha tofauti yoyote ile, kama alivyokuwa akiishi kipindi cha nyuma, aliendelea kuwa vilevile.

Wakaacha kufuatilia ishu ya Anna, wakahisi kabisa msichana huyo alikuwa ameuawa huko alipokuwa hivyo kuendelea na maisha yao kama kawaida. Wakati mwingine Nathalie alitamani kumwambia Gabriel ili ampe ushauri juu ya nini walitakiwa kufanya lakini alihofia.

Hakutaka kaka yake ajue kwamba hakuwa bikira, wakati mwingine pia alihisi kama angelaumiwa kwa kuwa yeye ndiye aliyetaka kuwa mtawa na mwisho wa siku kufanyiwa matendo ambayo hawakuwa mazuri kusimulika.

Mwezi mmoja ulipokatika tangu Anna aondoke kuelekea nchini Ubelgiji, wakapokea kadi ya mualiko kutoka makao makuu ya Kanisa la Living Christ ambapo watawa wote waliokuwa wamesoma katika vyuo vyao walikaribishwa huko kwa ajili ya kumshukuru Mungu lakini pia kupewa vyeti vyao vya kumaliza kozi hiyo ya miaka mitatu.

Hiyo ikaonekana ndiyo nafasi yao ya kufanya kile walichokitaka, walikuwa na picha zote na kwa kuwa walikuwa wakialikwa kuelekea huko ilikuwa ni lazima kuondoka na picha hizo mpaka nchini Ubelgiji ambapo wangezikabidhi kwa Askofu Poff ili aone kile kilichokuwa kikiendelea huko vyuoni.

“Hii ndiyo nafasi yetu,” alisema Nathalie.

“Kweli kabisa. Ni lazima twende na kukabidhi hizi picha!” alisema Maria.

Siku zikakatika, Maria hakutaka kurudi nchini Canada, alidhamiria kubaki nchini Marekani kwenye apatimenti aliyopanga mpaka siku ambayo angeona kile alichokuwa amepanga na wenzake kinatimia.

Wakati zikiwa zimebaki siku tatu kabla ya kuondoka kuelekea nchini Ubelgiji wakaanza kukutana kwenye mbuga ndogo ya wanyama iliyokuwa jijini New York ambapo huko waliamua kuanza kupanga mipango yao.

Ilikuwa ni lazima wacheze mchezo mmoja hatari, yaani kusiwe na mtu yeyote ambaye angewadaka kirahisi kama tu mpango mzima ulikuwa ni kuwakamata na kuwaua.

Kitu cha kwanza walitakiwa kuchukua ndege tofauti, zilizokuwa zikienda nchini Ubelgiji lakini zilitakiwa kutua kwenye viwanja tofauti.

Nathalie alitakiwa kuchukua ndege ambayo ingekwenda kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Brussels lakini Maria alitakiwa kuchukua ndege ambayo ingetua hapo Brussels lakini angeunganisha na kwenda kushuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Antwerp.

Walipanga mipango yao hiyo kwa sababu walihisi kabisa kulikuwa na watu waliokuwa wakiwatafuta, ilikuwa ni lazima wahakikishe watu hao wanawakwepa, kama mmojawao angeuawa basi mwingine aweze kufanikiwa.

Wakakubaliana hivyo na kupanga kwamba siku inayofuata ndiyo ilikuwa mwisho wa kuonana kwenye mbuga hiyo na keshokutwa walitakiwa kuanza safari ya kuelekea nchini Ubelgiji.

Nathalie akarudi nyumbani. Kama kawaida alionekana kuwa na huzuni, furaha iliondoka maishani mwake na hakujua kama ingetokea siku yoyote ile angekuja kuwa kwenye hali ya kawaida kama zamani.

Nyumbani, bado kila kitu kiliendelea kuwa siri, hakutaka kumwambia Gabriel zaidi ya kumuaga na kumwambia kuhusu mualiko ule kwamba alitakiwa kuondoka kwenda nchini Ubelgiji kwa ajili ya kuhudhuria sherehe ya kukabidhiwa cheti.

“Unahisi utakuwa salama?” aliuliza Gabriel huku akimwangalia Nathalie.

“Natumaini hilo!”

“Hutopotea kama alivyopotea Anna?” alimuuliza.

Nathalie akashtuka kusikia hivyo, akamwangalia kaka yake ambaye alipiga hatua na kumsogelea kwenye kochi alilokuwa, akapiga magoti na kuishika mikono yake na kumwambia kuhusu kile kilichokuwa moyoni mwake.

Alishindwa kuyaficha maumivu yake, machozi yakaanza kumlenga na hatimaye kuanza kutiririka mashavuni mwake. Alimwambia jinsi alivyoumia kwa kipindi kirefu tangu alipogundua kulikuwa na kitu ambacho Nathalie alimficha.

“Ulitakiwa kuniambia ukweli Nathalie,” alisema Gabriel huku akimwangalia ndugu yake.

“Ukweli kuhusu nini?”

“Picha! Hili suala hamuwezi kulifanya peke yenu, hamtoweza kwa sababu mnapambana na watu hatari, wenye nguvu,” alisema Gabriel maneno yaliyomfanya Nathalie kugundua kwamba hilo halikuwa siri ya watu watatu kama ilivyokuwa, kulikuwa na mtu wa nne aliyejitokeza.

Gabriel alimwambia kila kitu kwamba kama wangeendelea kulichukulia jambo hilo wawili kama ilivyokuwa basi hali ingekuwa ngumu zaidi na kuna uwezekano wote wawili wakauawa kama alivyouawa Anna.

“Tufanye nini?” aliuliza Nathalie huku akilia.

“Nipeni hizo picha nizipeleke mimi mwenyewe,” alisema Gabriel.

“Hapana! Watakuua!”

“Nitapambana nao. Ni kazi rahisi kupambana nao kuliko nyie, hamuwezi kupambana na watu hawa,” alisema Gabriel.

Alimbembeleza sana Nathalie na hatimaye akakubaliana naye kwamba azichukue picha hizo na kuzipeleka nchini Ubelgiji kwa Askofu Poff ambaye huyo angejua kile kilichokuwa kikiendelea na kuwachukulia hatua watu hao.

Kwake, halikuwa tatizo hivyo ikambidi afanye mawasiliana na Maria na kumwambia kuhusu Gabriel. Akachukua simu yake na kumpigia.

Simu ikaanza kuita, iliita na kuita lakini haikupokelewa. Hiyo haikuwa kawaida, ni mara nyingi alipokuwa akimpigia simu msichana huyo, haikuwa ikiita sana ilipokelewa kwa kuwa kipindi hicho simu ilikuwa kitu kilichotumika sana kuliko vitu vingine.

Hakukata tamaa, aliendelea kupiga lakini bado majibu yalikuwa yaleyale. Hilo likaanza kumtia hofu na kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichotokea.

Hakutaka kufanya siri tena, akamwambia Gabriel ambapo baada ya kuambiwa hivyo tu, akabadilika, akamwangalia Nathalie na kumwambia tayari walimuua msichana huyo.

“Wamemuua!” alisema Gabriel.

“Unasemaje?”

“Watakuwa wamemuua! Twende anapoishi!” alisema Gabriel.

Hawakutaka kubaki mahali hapo, haraka sana wakaondoka na kuelekea kwenye apatimenti aliyokuwa akiishi Maria.

Njiani kila mtu alionekana kuwa na mawazo tele, hawakuamini kile kilichokuwa kikiendelea. Walihisi kabisa msichana huyo aliuawa kwani kwa mambo yote yaliyokuwa yakiendelea, yaliwatia hofu sana.

Hawakuchukua dakika nyingi wakafika huko, wakateremka na kuanza kuelekea katika apatimenti hiyo.

Walipokishika kitasa, kikafunguka na kuingia ndani. Sebule, chumba, pote huko palikuwa peupe na msichana Maria hakuonekana jambo liliwatia hofu kupita kawaida.

“Yupo wapi?” aliuliza Nathalie huku akianza kutokwa na machozi.

Waliangalia kila kona, walimuita lakini hakuonekana, hawakutaka kubaki, wakaondoka na kurudi nyumbani, bado walihisi kulikuwa na jambo kubwa lililokuwa limetokea.

Walipofika nyumbani, wakaelekea sebuleni na kukaa kwenye kochi. Kila mmoja kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, Nathalie hakutaka kukubali, bado aliendelea kumpigia simu Maria lakini muda huo haikuwa ikipatikana, ilionyesha kwamba mtu aliyekuwa nayo aliamua kuizima kabisa.

“Ngriiii....ngriiii....ngriiii...” ulisikika mlio wa simu ya mezani.

Kila mmoja akashtuka, wakaangaliana. Japokuwa walizoea kuisikia simu hiyo ikiita lakini siku hiyo ilionekana kuwa tofauti kabisa.

Kwa jinsi walivyoangalia ni kama walikuwa wakisakiziana kwamba ni nani alitakiwa kwenda kupokea simu hiyo.

Gabriel akasimama na kuifuata, alipoifikia, akaunyanyua mkonga wa simu na kuupeleka sikioni huku Nathalie akimsogelea mpaka pale alipokuwa na kuanza kusikiliza.

“Who is talking?” (nani anaongea) aliuliza.

“You have twenty four hours to live,” (mna saa ishirini na nne za kuishi) alisema mwanaume huyo ambaye hakutaka hata kujitambulisha.

“Who the hell are you?” (wewe nani?) aliuliza Gabriel, mwanaume huyo hakujibu swali hilo, akakata simu.





Viongozi wa vyuo mbalimbali vya utawa kutoka katika Kanisa la Living Christ waliwasiliana na kukubaliana kwamba ni lazima wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha wanawamaliza wasichana wale ambao kiu yao kubwa ilikuwa ni kwenda kuzungumza na maaskofu kuwaambia uovu uliokuwa ukifanyika vyuoni.

Hawakutaka hilo litokee na ndiyo maana wakapanga mikakati ya kuwamaliza wote wawili. Wakaanza kumfuatilia Maria, walihitaji kufahamu mahali alipokuwa akiishi, ilikuwa ni lazima wamuue msichana huyo kwa sababu alikuwa mmoja wa watu hatari sana, yaani kumuacha hai lingekuwa kosa kubwa.

Vijana wao waliokuwa nchini Marekani ndiyo walikuwa kila kitu, waliwaambia jinsi mchezo ulivyotakiwa kuchezwa mpaka kuhakikisha Maria anaanza kufa na baadaye kufuata Nathalie.

Wakati wawili hao wakiagana katika mgahawa na kuondoka, vijana wawili ambao walikuwa na bastola zao wakaanza kufuatilia Maria ambaye aliondoka, akapanda treni na kuelekea huko kulipokuwa na apatimenti yake.

Ndani ya treni kichwa chake kilikuwa na mawazo tele, alijua kabisa kile walichokuwa wakienda kukifanya kilikuwa hatari na ilikuwa ni lazima wajipange mno na pia hawakutakiwa kumwamini mtu yeyote yule.

Hakujua katika treni aliyopanda kulikuwa na watu wawili waliotamani sana kuona akifa. Walikuwa humo, hawakuonyesha ishara zozote zile za kumfuatilia msichana huyo zaidi ya kujifanya nao abiria ambao walikuwa wakienda nyumbani kwao.

Maria alipofika katika kituo chake, akateremka na kuelekea nyumbani kwa kutembea. Vijana wale walikuwa nyuma yake, walitembea kwa mwendo wa taratibu huku wakijifanya kupiga stori na hawakuwa na muda naye.

Baada ya dakika kadhaa wakamuona akiingia ndani ya nyumba moja ambayo ilikuwa ni apatimenti, akaanza kupanda ngazi, nao wakaanza kupanda kwa nyuma yake mpaka kufika katika chumba alichokuwa akiishi ambapo walisikia tu mlango ukifungwa na kugundua kilikuwa ni chumba hicho.

Wakausogelea na kuanza kugonga kama watu waliokuwa na uhitaji fulani. Maria aliyekuwa ndani hata kabla ya kubadilisha nguo zake, akasikia hodi hiyo ambapo moja kwa moja akaelekea mlangoni na kuufungua.

Macho yake yakatua nyusoni mwa watu wawili, kwa kuwaangalia harakaharaka ilikuwa ni rahisi kugundua kama walikuwa watu wema, nyuso zao zilitawaliwa na tabasamu pana hali iliyoonyesha hakukuwa na tatizo lolote lile.

Ili kuwafanya wajisikie vizuri, naye Maria akaanza kutoa tabasamu lakini ghafla nyuso za watu hao zikabadilika na kuonekana katika hali nyingine kabisa na kutoa bastola zao.

Wakamsukumia Maria kwa ndani, akaanguka na kuumiza, akafutwa pale alipokuwa na kuchukuliwa, akafungwa kitambaa machoni na na kupelekwa nje huku akitakiwa kuwa kimya.

Hakujua watu hao walikuwa akina nani na walihitaji nini kutoka kwake. Moyo wake ulikuwa na hofu, alikuwa akilia huku akiomba msamaha kama kulikuwa na jambo baya alilifanya lakini watu hao hawakuongea kitu chochote kile.

Wakamchukua na kumpeleka ndani ya gari lao, wakaondoka mahali hapo huku Maria akiendelea kulia mfululizo. Wakiwa humo, mwanaume mmoja akachukua simu yake na kupiga sehemu, baada ya sekunde kadhaa, ikapokelewa na sauti ya mwanaume mmoja kusikika kutoka upande wa pili.

“Imekuwaje?” ilisikika sauti hiyo ikiuliza.

“Tunaye ndani ya gari! Kwa hiyo?”

“Kammalizeni halafu fanyeni kazi ya kumpa mwingine wa mwisho,” alisikika mwanaume huyo.

“Sawa.”

Kwa jinsi watu hao walivyokuwa wameongea kwenye simu ilionyesha kabisa hakukuwa na uhakika wa Maria kupona. Aliendelea kulia huku akiomba msamaha lakini hakukuwa na mtu aliyemsikiliza.

Wao walichotaka kufanya ni kile walichoambiwa na mwanaume mmoja kwenye simu kwamba wamuue na wafanye kila liwezekanalo kumpata msichana mwingine.

Gari likaondoka mpaka sehemu fulani ambapo kulikuwa na jumba kubwa. Huko ndipo ambapo walitakiwa kufanya mauaji yao na ndiyo sehemu ambayo waliamua kuichukua kwa ajili ya kazi hiyo tu.

Walipofika, gari likaingizwa ndani na Maria kuteremshwa. Hakunyamaza, bado alikuwa akilia mfululizo, hakujua ni mahali gani alipokuwa kwani bado kitambaa kilikuwa machoni mwake.

Akaingizwa ndani ya jumba hilo na kupelekwa katika chumba kimoja kilichokuwa na michirizi ya damu.

Wakawapigia simu wakubwa wao na kuwaambia tayari walifika katika jumba la mauaji hivyo walikuwa wakitaka kusikia neno kutoka kwao.

“Huyo bakini naye kwanza, tutawaambia ni nini cha kufanya,” alisikika mwanaume kutoka upande wa pili.

“Sawa bosi!”

“Tutawasiliana nanyi, bado mmoja amebakia,” alisema mwanaume aliyesikika kutoka upande wa pili.

Viongozi hao waliokuwa nchi mbalimbali barani Ulaya wakapigiana simu na kupeana taarifa kwamba tayari Maria alikuwa ametekwa na kulikuwa na msichana mmoja, Nathalie ndiye ambaye alibaki na kwa namna yoyote ile ilikuwa ni lazima naye atekwe na kuuawa pamoja.

Bado waliendelea kudukua mawasiliano yake, walimsikia alivyokuwa akiongea na Gabriel na kumwambia mambo mengi kuhusu yale yaliyokuwa yametokea.

Walisikia mengi mpaka mpango wa kwenda nchini Ubelgiji kwenye sherehe ya utoaji wa vyeti kwa wanafunzi wote ambao walisoma katika vyuo mbalimbali vya Kanisa la Living Christ.

Walijua kabisa kwamba kama wangempata Nathalie na kumuua bado isingesaidia sana kwa sababu tayari kulikuwa na mtu mwingine ambaye naye alijua kile kilichokuwa kimetokea.

Wakati wakipanga mikakati ya kumteka Nathalie na kumuua ilikuwa ni lazima wajipange kwa ajili ya kumuua Gabriel ambaye naye pia aliambiwa kila kitu jambo ambalo lingeweza kuwa tatizo kubwa kama tu wangethubutu kumuacha mwanaume huyo.

Haraka sana mwanaume mmoja akachukua simu na kupiga nyumbani kwa akina Nathalie, simu iliita kwa sekunde chache, ilipopokelewa, sauti ya Gabriel ilikuwa ikisikika.

Alichokisema mwanaume huyo aliyepiga simu ni kwamba watu hao walikuwa na saa ishirini na nne tu za kuishi kwani ndani ya saa hizo ilikuwa ni lazima wauawe kama walivyouawa wengine.

“Nimewaambia,” alisema mwanaume huyo huku akiwaangalia wenzake.

Hawakutaka kuishia hapo, kwa kuwa walijua anuani ya mahali watu hao walipokuwa wakiishi, wakawapigia simu vijana wao na kuwapa amri ya kuwaua watu hao kama walivyowaua wengine.

“Tupeni saa mbili tu, tutaifanya kazi hiyo,” alisema mwanaume kutoka upande wa pili.

“Tena fanyeni haraka sana!”alisema na kukata simu.

Upande wa pili mara baada ya Gabriel kupokea simu hiyo na kusikiliza maneno aliyoambiwa na kukatwa, akabaki akimwangalia ndugu yake, moyo wake ulikuwa kwenye hofu nzito, aligundua kwamba kuwa watu ambao walikuwa nyuma ya kila kitu walikuwa hatari ambao wangeweza kuwamaliza muda wowote ule.

Ilikuwa ni lazima picha hizo zipelekwe nchini Ubelgiji lakini kitu ambacho mpaka muda huo kiliwapa maswali mengi ni juu ya namna watu hao walivyojua kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Walijitahidi kufanya mambo yao kwa siri sana lakini watu hao walifahamu kila kitu, hilo liliwapa hofu na kuhisi walikuwa wakifuatiliwa na watu hao pasipo kujua.

“Wamejuaje mambo haya yote? Mliwaambia?” aliuliza Gabriel.

“Hapana!”

“Sasa wamejuaje?” aliuliza Gabriel.

Wakati wali hilo likiwa halijajibiwa, mawazo yake yakakumbuka kuhusu filamu mbalimbali jinsi watu walivyokuwa wakidukua mawasiliano ya simu na kusikiliza kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Gabriel akaichukua simu ya Nathalie, akaanza kuiangalia kwa makini, alihisi kwamba watu hao walifanya hayo yote kwa kupitia simu hiyo.

“Hii simu uliinunua wapi?” alimuuliza Nathalie.

“Tulipewa vyuoni!”

“Wote watatu?”

“Ndiyo!” alijibu Nathalie.

Gabriel hakutaka kuchelewa, haraka sana akaondoka na kuelekea chooni ambapo huko akaitumbukiza na kuflashi. Nathalie alishtuka, hakujua sababu iliyomfanya ndugu yake huyo kufanya jambo kama hilo, akaanza kulalamika.

“Nathalie! Mawasiliano yenu yalidukuliwa, inawezekana walikuwa wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea kupitia simu zenu,” alisema Gabriel.

“Hapana! Haiwezekani!”

“Sasa unahisi ilikuwaje mpaka watu hao wakafahamu kilichokuwa kikiendelea? Wenzako waliuawa, walijuaje kama Anna alikwenda nchini Ubelgiji? Mlimtuma mtu aje, mbona hakuja? Inawezekana naye wakawa wamemuua, walijuaje hayo yote? Uuh?” aliuliza Gabriel maswali ambayo yaliingia kichwani mwa Nathalie na kutengeneza maana kubwa.

“Kwa hiyo tulikuwa tukifuatiliwa?” aliuliza Nathalie!

“Hiyo ndiyo maana yangu!”

Nathalie alichoka, naye akaamini watu hao hawakuwa wa mchezo mchezo, walitakiwa wafanye kila liwezekanalo kujificha na mwisho wa siku kutoroka mahali hapo kwenda kujificha sehemu fulani.

“Nathalie! Ni lazima tuondoke mahali hapa,” alisema Gabriel.

“Sawa!”

Wakakubaliana, wakatoka na kuondoka mahali hapo huku wakiwa na picha zile zilizopigwa walipokuwa chuoni huku picha nyingine wakizificha ndani ya nyumba hiyo.

Lengo lao lilikuwa ni kwenda katika Mtaa wa Livingstone alipokuwa akiishi baba yao. Walitumia dakika ishirini njiani ndipo wakafika na kukaribishwa nyumbani huko.

Walikaa huko kwa dakika kadhaa ndipo baadaye simu ya Gabriel ikaanza kuita, haraka sana akaichukua na kuangalia kioo, ni namba ngeni ndiyo iliyokuwa ikionekana, akaipokea.

“Halo!” aliita.

“Halo! Gabriel, upo wapi? Nimekuja hapa nyumbani siwaoni, mmekwenda wapi?” aliuliza msichana aliyekuwa akiongea upande wa nyuma.

“Wewe nani?” aliuliza Gabriel.

“Maria!”

“Maria?” aliuliza Gabriel huku akionekana kushtuka, si yeye tu bali hata Nathalie aliyekuwa pembeni akashtuka.

“Ndiyo! Mbona umeshtuka?”

“Hakuna kitu!”

“Mpo wapi?”

“Tulitoka...” alijibu Gabriel na hapohapo Nathalie akampokonya simu ile.

“Maria! Upo wapi?” aliuliza Nathalie huku akionekana kuwa na hofu.

“Nipo kwenu! Kuna watu walikuwa wakinifuatilia na gari, nimekimbia! Walikuja nyumbani kwangu na kutaka kuniteka. Nathalie, naomba uniokoe...niokoeee...” alisema Maria huku akilia, hapohapo akakata simu.

Nathalie alichanganyikiwa, sauti aliyokuwa ameisikia alijua kabisa alikuwa Maria, hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kumuokoa msichana huyo, alisema kwamba alikuwa nyumbani kwao, kama ni hivyo ilikuwa ni lazima aondoke kwenda huko.

Akamwambia Gabriel kwamba walitakiwa kwenda nyumbani kumchukua Maria, Gabriel hakukubali, alimwambia inawezekana hiyo ilikuwa mbinu ya watu hao kutaka kuwateka hivyo hawakutakiwa kwenda huko.

Nathalie hakukubali, Maria alikuwa rafiki yake mkubwa, alihitaji msaada kwa sababu kulikuwa na watu waliokuwa wakimfuatilia, alijua kabisa kwamba kama angemuacha huko basi watu hao wangeweza kumuua kama ilivyokuwa kwa Anna.

Akataka kwenda peke yake, Gabriel akamzuia. Huo haukuwa muda wa kuzuiliwa, akaporonyoka katika mkono wa Gabriel na kuondoka zake.

Mwanaume huyo akamuita, Nathalie hakutaka kurudi nyuma, katika kile kilichokuwa kikiendelea, ilikuwa ni lazima kuhakikisha wanakuwa pamoja ili kuongeza nguvu.

Alichukua gari la kaka yake, akamuacha mahali hapo na kuondoka kwa kasi kubwa. Njiani alikuwa akilia, hakuamini kama alikuwa akienda kuonana na Maria ambaye alikuwa akimuhitaji sana kipindi hicho.

Ni ndani ya dakika kumi tu akafika nyumbani kwao, haraka sana akateremka na kuelekea ndani ya nyumba hiyo ambapo aliamini kwamba tayari Maria alikuwa ndani kwani alijua mpaka mahali funguo zilipokuwa zikikaa.

“Maria....Maria...” aliita huku akifungua mlango wa sebuleni.

Nathalie akafika sebuleni na kuangalia huku na kule, hakuona mtu, kulikuwa na ukimya mkubwa kiasi kwamba akaanza kuogopa kwani hakuwahi kuiona nyumba hiyo ikiwa na ukimya kama ilivyokuwa kipindi hicho.

Hakuacha kuita, bado moyo wake ulimwambia kwamba Maria alifika nyumbani hapo hivyo kuendelea kumuita zaidi. Hakuitikia mtu yeyote lakini wakati amekwenda chumbani na kurudi tena sebuleni akakutana na watu ambao kwa kuwaangalia tu, hakuwatambua.

Hata kabla hajauliza swali walikuwa akina nani na walifika hapo kufanya nini, wakatoa bastola zao na kumnyooshea, akaogopa na kuhisi kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake.

Akaamuriwa apige magoti na kunyoosha mikono juu, hakubisha, akafanya hivyo, mwanaume mmoja akamsogelea na kumfunga kamba mikononi mwake na kutoka naye ndani kuelekea nje.

Nathalie hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mahali hapo, alikuwa na hofu tele na muda wote ule alihisi kabisa angeuawa kwani kwa jinsi alivyowaangalia wanaume wale, walionekana kuwa na hasira naye kupita kawaida.

Walipofika nje, wakaingia naye ndani ya gari na kuondoka mahali hapo. Kila kitu kilichokuwa kikitokea nje, Gabriel alikuwa akikifuatilia kwa ukaribu.

Katika kipindi ambacho ndugu yake huyo aliondoka kule kwa ndugu yao na kuelekea nyumbani, aliamua kumfuatilia kwa nyuma, hakutaka kugundulika lakini alihakikisha dada yake huyo anakuwa salama kabisa.

Mpaka alipoingia ndani, alikuwa akifuatilia na ghafla akawaona watu wakiingia humo na walipotoka walikuwa na msichana huyo, wakaingia ndani ya gari na kuondoka zao.

Alisikitika, aliumia lakini hilo halikuwa suluhisho la kuzuia picha zile kufika nchini Ubelgiji, ilikuwa ni lazima awahi katika sherehe hiyo na kuwakabidhi maaskofu na kuwaonyeshea kile kilichokuwa kikiendelea.

Tumaini kubwa lilikuwa kwake, yeye ndiye ambaye alitakiwa kuamua kufuatilia suala hilo mpaka mwisho kwa sababu wale ambao walitakiwa kufanya hivyo, walitekwa na kuuawa na mbaya zaidi mpaka dada yake alitekwa mbele ya macho yake.

Moyo wake ulimuuma, alijua kabisa kitu ambacho kingefuata ni msichana huyo kuuawa, hakuwa na nguvu ya kwenda kushtaki polisi kwani aliamini hata kama angefanya hivyo ilikuwa ni lazima watu wale wamuue kwa sababu alikuwa amechelewa sana.

Haraka sana akakata tiketi, kitu pekee ambacho kingeonekana kuwa kama malipo kwa ndugu yake huyo na wasichana wengine wawili ilikuwa ni kuzifikisha picha zile sehemu husika na kuwaonyeshea unyama wote ambao wasichana wadogo walikuwa wakifanyiwa na viongozi wa makanisa ambao walipewa majukumu ya kusimamia vituo vilivyokuwa vikifundisha utawa.

Gabriel hakutaka kuchelewa, siku hiyohiyo akakata tiketi katika Shirika Ndege la Orange na hivyo kutakiwa kusafiri siku hiyohiyo na moja ya ndege kubwa ya shirika hilo iitwayo Airbus A350-900 iliyokuwa ya sita kwa ukubwa duniani.

***

Vijana ambao waliondoka na Nathalie nyumbani kwao wakaelekea katika jumba moja chakavu lililokuwa hapohapo New York tayari kwa kufanya mauaji ya mwanamke huyo.

Huko, wakamuunganisha na Maria ambaye alikuwa humo tayari, wawili hao walipoonana, wakaitana, wakakumbatiana na kuanza kulia pamoja.

Walijua kile ambacho kingetokea, walijua fika kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wao kwani watu wale hawakuonekana kuwa na masihara hata kidogo.

Pamoja na hayo yote hawakuacha kumuomba Mungu. Walimkumbusha jinsi walivyokuwa wamejitolea maisha yao yote kumtumikia, jinsi walivyohangaika kuhakikisha wanakuwa watawa na kumtumia maisha yao mpaka vifo vyao.

Walilia mno lakini hakukuwa na mtu aliyewasikiliza, ndiyo kwanza waliwaambia walitakiwa kubaki kimya kwani kelele zao zilikuwa chukizo mno masikioni mwao.

“Maria! Nimefurahi kukuona, hata kama tutauawa, tuuawe huku tukiwa tunamtumikia Mungu,” alisema Nathalie huku akimwangalia rafiki yake huyo ambaye alionekana kufarijika sana kumuona mwenzake mahali hapo.

“Mungu atutangulie, hata akina Yohana walikufa kwa kupata mateso makali, kama ni matendo makuu ya Mungu kwa kutaka kulibadilisha hili kanisa, ninaamini kwamba kuna siku ukweli utajulikana,” alisema Maria huku akimwangalia mwenzake.

“Ninaamini hilo.”

“Zile picha zipo wapi?”

“Anazo Gabriel! Najua atazifikisha tu, hata kama sisi tutauawa, ninaamini picha hizo zitafika katika mikono salama,” alisema Nathalie huku akimwangalia rafiki yake huyo.

Hawakuacha kulia, hawakuacha kumuomba Mungu kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Walishikilia rozali zao huku muda wote wakimshukuru Mungu kwa kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo.

Baada ya dakika kadhaa wanaume wawili wakaingia huku wakiwa na mikanda ya suruali, walichokuwa wameambiwa ni kwamba walitakiwa kuwatesa wasichana hao, wawapige na mwisho wa siku wawaue kwa sababu waliwasumbua sana mpaka kutumia kiasi kikubwa cha pesa kuhakikisha wanakufa.

Hicho ndicho kilichofanyika, siku hiyo ilikuwa ni ya mateso makali, walichapwa mikanda, walivimba mpaka kutoka damu lakini hakukuwa na mtu yeyote yule aliyeonekana kujali.

Ni ndani ya nusu saa tu wasichana wote wawili walikuwa hoi, damu zilikuwa zikiwatoka, walivimba kila sehemu na hata kuongea hawakuwa wakiweza kabisa kutokana na mateso waliyokuwa wamepewa kuwa makubwa kupita kawaida.

Hakukuwa na muda wa kupoteza, baada ya kuhakikisha wamewatesa vya kutosha, wakawasiliana na viongozi wao na kuwaambia kilichotokea hivyo kusikilizia ni kitu gani ambacho kilitakiwa kufanywa.

“Wamalizeni!” alisema mwanaume ambaye alipigiwa simu.

“Sawa.”

Hicho ndicho kilichofanyika, baada ya kuambiwa hivyo, hawakutaka kusubiri sana, wakawachukua na kuwapeleka katika chumba kingine, huko, kilichofanyika ni kupigwa risasi za vichwa na miili yao kufungwa kwenye makabati maalumu na kuchomwa moto humo.

Huo ndiyo ulikuwa mwisho wao, watekaji hao wakaondoka mahali hapo lakini wakapigiwa simu na kuambiwa kwamba kulikuwa na mtu mwingine ambaye naye alitakiwa kuuawa haraka iwezekanavyo.

Mwanaume huyo alikuwa Gabriel, ni kwamba taarifa zilisema alikata tiketi tayari kuanza safari ya kuelekea nchini Ubelgiji lakini wakawa na hofu inawezekana kabisa mwanaume huyo alikuwa na picha hizo hivyo ilikuwa ni lazima auawe haraka iwezekanavyo.

Wakati wakipiga simu na kuwaambia kuhusu hilo, walikuwa wamechelewa kwani hata walipokwenda uwanja wa ndege, waliambiwa kwamba tayari abiria walikuwa tayari ndani ya ndege.

Walitaka kukata tiketi na kuingia humo lakini ilishindikana, ndege ilijaa lakini pia isingewezekana kupata tiketi kwa haraka sana hasa kwa ndege ambayo ilikuwa ikiondoka muda huo.

Wakawapigia simu mabosi zao na kuwaambia kuhusu suala hilo, wao wakawaambia waachane nao kwani kungekuwa na mpango mwingine ambao wangeupanga kama mabosi kuhakikisha Gabriel anauawa hata kabla ndege haikutua nchini Ubelgiji.

Haraka sana kikao cha dharura kikaitishwa nchini Ubelgiji, ilikuwa ni lazima kuhakikisha mwanaume huyo anakufa haraka iwezekanavyo hata kabla ya kufika nchini humo.

Wale ambao walikuwa katika nchi nyingine wakashirikishwa kwa njia ya simu na kuendelea na kikao hicho huku mada kubwa ikihusu kummaliza Gabriel ndani ya ndege hiyo vinginevyo kila kitu walichokipigania kingefeli na kuonekana kufanya kazi ya bure kipindi chote hicho.

“Kama vipi ndege ipotezwe kwa ajili yake,” alisema mwanaume mmoja.

“Ipotezwe? Kivipi?”

“Yaani ipotee kama ile ya Malaysia!” alijibu mwanaume huyo ambaye alitoa wazo la kupotezwa kwa ndege hiyo.

Hilo lilikuwa wazo zuri ambalo lilitakiwa kufanyiwa kazi haraka sana. Wakakubaliana na hatimaye kupanga mipango ni kwa namna gani ndege hiyo ingepotezwa.

Wakawasiliana na Kundi la Yamong Tsu lililokuwa nchini Thailand na kuwaambia kile kilichotokea kwamba ndege hiyo kubwa ya abiria ilitakiwa kupotezwa.

Wakati mipango hiyo ikiwa imepangwa, upande wa pili tayari abiria katika ndege hiyo walikuwa wamekaa katika viti vyao na tayari safari ya kuelekea barani Ulaya na Asia kabla ya kuingia Afrika ikaanza.

Kila mmoja alikuwa kimya! Walifunga mikanda yao na ndege kuondoka katika ardhi ya Marekani. Gabriel alikuwa humo, naye alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wakiondoka nchini humo.

Kwenye begi lake la mgongoni ambalo lilikuwa kwa juu aliweka picha zile zilizokuwa zikionyesha michezo michafu ambayo ilikuwa ikichezwa na watu waliopewa jukumu la kusimamia vyuo vya wasichana waliokuwa wakisomea utawa katika Kanisa la Living Christ.

Wakati safari hiyo ikianza, hakujua kama upande wa pili kulikuwa na watu waliokuwa na mpango wa kuipoteza ndege hiyo ili picha zile alizokuwanazo zisiweze kuonekana.





HISTORIA YA MTU WA PILI KATI YA WALE WATANO ILIYOMFANYA KUWA NDANI YA NDEGE HIYO.


Mtu wa Pili Ndani ya Ndege.

“Guys, tell me what the hell is going on,” (jamani niambieni kitu gani kinaendelea) alisikika mwanaume mmoja aliyeitwa Sam Scott kutoka katika ofisi ya ndani kabisa katika jengo la makao makuu ya Shirika la Kijasusi nchini Marekani, CIA (Central Intelligence Agency) yaliyokuwa Langley, Virginia, McLean, Virginia nchini Marekani.

“The president calls the press,” (rais amewaita waandishi wa habari) alisema mwanaume mwingine kwenye simu.

“I want to get the feedback as soon as possible,” (nataka kupata kinachoendelea haraka iwezekanavyo) alisema Scott na kukata simu.

Dunia nzima ilikuwa bize kusikilizia kile kilichokuwa kikiendelea nchini Iraq. Watu walitega masikio yao, walihitaji kujua sababu ya rais wa nchi hiyo, Sharif Hamis kuwaita waandishi wa habari na kutaka kuzungumza nao.

Kila mmoja alimfahamu rais huyo, alikuwa miongoni mwa marais viburi waliowahi kutokea hapa duniani. Alikuwa mtu aliyependa fujo ambaye alitawala kibabe nchini mwake.

Watu hawakumpenda kwa sababu alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa ambaye alikuwa na uwezo wa kufanya kitu chochote kile, wakati wowote pasipo kuogopa chochote.

Marekani walijitahidi kumuwekea vikwazo rais huyo, hakujali, kitu alichokijua ni kwamba alikusanya pesa nyingi kutokana na visima vya mafuta vilivyokuwa nchini mwake.

Nchi iliingiza pesa nyingi kupitia mafuta, ilijiendesha kama ilivyotakiwa kuwa kwa sababu tu biashara hiyo ilikuwa na pesa, aliziunganisha nchi nyingi na kuziuzia mafuta hayo ambayo yalimfanya kupata pesa nyingi.

Hakujali kuhusu Marekani, walimwambia wangeweza kuilipua nchi yake lakini hakutaka kujali, kwake, kelele zao zilikuwa ni sawa na muziki uliopigwa mbele ya mbuzi ili acheze lakini hakufanya hivyo.

Siku zikaendelea, baada ya Urusi kuona kulikuwa na maslahi makubwa nchini Iraq, rais wa nchi hiyo, Bwana Petrov Ludovick akampigia simu Rais Hamis na kumwambia kwamba hakutakiwa kuogopa kwa sababu alikuwa upande wake, kama kungekuwa na mtu yeyote ambaye angembabaisha basi angemsaidia kupambana na adui huyo.

Kwa Hamis akakenua, hakuamini kama angepata msaada kutoka kwa nchi kubwa kama Urusi, kitendo cha Rais Ludovick kusema angemtetea kwenye kila hatua, kwake ikaonekana kuwa ushindi mkubwa, akaongeza kiburi zaidi.

Alichokuwa akikiangalia Ludovick si kumlinda tu mwanaume huyo bali alihitaji kuingia kwenye biashara ya mafuta na nchi hiyo, aliamini kwamba Marekani alihitaji sana kupata mafuta kutoka nchini humo kibabe, yeye hakutaka kufanya hivyo na ndiyo maana kitu cha kwanza kabisa ambacho alihitaji kukipata ni kuchukua nafasi ya kufanya biashara na Iraq kwa kutengeneza urafiki.

Urafiki huo haukuwa siri, Marekani wakajua kwamba Urusi aliingilia kati, kulikuwa na mipango mingi ambayo nchi hiyo ilipanga, waligundua kwamba rais Ludovick aliahidi kumlinda Hamis, hata kama kungekuwa na wabaya walihitaji kupambana naye, mtu wa kwanza kabisa ambaye angejitokeza angekuwa Urusi.

Hilo liliwaumiza vichwa Wamarekani, walishindwa kujua nini cha kufanya. Urusi ilikuwa nchi kubwa na yenye silaha kubwa za kijeshi lakini kubwa zaidi ni kwamba walikuwa karibu na Marekani.

Kama ambavyo Marekani alivyokuwa mbabe, hata Urusi alikuwa hivyohivyo, hawakuwahi kupatana na kila siku walikuwa wakiangaliana kama maadui, yaani ni kama kila mmoja alikuwa akimsubiri mwenzake amchokoze.

Baada ya siku nyingi kupita hatimaye Rais Hamis akawaita waandishi wa habari na kutaka kuzungumza nao kitu, kila mtu alihitaji kusikia ni kitu gani kingezungumzwa mahali hapo mbele ya waandishi wa habari.

Waandishi hao walifika ikulu, waliweka kamera zao, waliujua ubabe wake, walijua kabisa kama siku hiyo mwanaume huyo alihitaji kuzungumza kitu cha kuigusa dunia kwa sababu tu hakuwa akipatana na mataifa mengi nje ya himaya ya Waarabu.

Baada ya dakika kadhaa, rais huyo akafika mbele ya waandishi wa habari. Alivalia kanzu nyeupe, iliyong’ara huku akiwa na kilemba kichwani mwake, kwa kumwangalia harakaharaka ilikuwa ni rahisi kusema mtu huyo alikuwa mtakatifu, mwenye moyo mzuri na wa kujishusha kama Mtume Muhammad kumbe haikuwa hivyo, alikuwa mwanaume aliyeishi katika dunia yake ya kibabe aliyependa kila mtu duniani amuogope.

Akakaa kwenye kiti chake, kabla ya kuzungumza kitu chochote kile, akaachia tabasamu pana, akachukua maji na kuanza kunywa, alihitaji kuzungumza kitu ambacho alijua kabisa dunia ingeshtuka na kuona hakukuwa na amani tena.

Hakutaka kupoteza muda wa waaandishi wa habari, akaanza kuzungumza kile kitu kilichomfanya kuwaita waandishi wa habari, aliwaambia kwamba alikuwa na mabomu ya nyuklia saba ambayo yalitengenezwa na watu wake, alikuwa na silaha nzito ambazo kila mtu alitakiwa kumuogopa.

Kila mtu aliyesikia hivyo, akashtuka, hapakuwa na mtu aliyeamini kama kweli mwanaume huyo alikuwa na mabomu ya nyuklia, Marekani wenyewe kwenye stoo ya mabomu yao kipindi hicho walikuwa na mabomu matatu tu ambayo walikuwa wakiringia nayo, cha ajabu Rais Hamis alikuwa na mabomu saba, alionekana kuwa mtu tishio.

Haraka sana Rais Ludovick wa Marekani akaitisha kikao ikulu na kutaka kuzungumza na viongozi wa juu wa CIA. Alihitaji kuwaambia kile kilichokuwa kimetokea, walitakiwa kujipanga na kuhakikisha wanashinda kila kitu kilichokuwa mbele yao.

Simu ikapigwa na ndani ya nusu saa watu hao walikuwa ikulu na kufanya kikao hicho kidogo. Walizungumza mambo mengi ikiwemo lile la kuwamaliza watu waliokuwa wametengeneza mabomu hayo lakini kitu kikubwa zaidi kilikuwa ni kuhakikisha wanapata formula ambayo wataalamu wa Rais Hamis waliitumia kutengeneza mabomu hayo.

“Tuhakikisheni tunafanikiwa katika hilo, sawa?” alisema Rais Ludovick.

“Sawa.”

Wakaondoka, aliwaachia kazi ya kuhakikisha hilo linafanyika haraka pasipo kugundulika. Ili hilo lifanikiwe ilikuwa ni lazima kumtuma mtu kwenda nchini Iraq ambapo huko angefanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanafanikiwa katika hilo.

Hawakutakiwa kumtuma jasusi wa Kizungu kwa kuwa walijua ingekuwa ni rahisi kugundulika, mtu ambaye alitakiwa kwenda huko ni jasusi mweusi ambaye angejifanya kama mfanyabiashara kutoka barani Afrika, ila baada ya kufika huko angefanya kila liwezekanalo kuhakikisha anagundua kila kitu kilichokuwa kikiendelea pamoja na kupata formula hiyo.

Walichokifanya ni kumchukua jasusi aliyeitwa kwa jina la Kennedy Edward ila kwenye kazi hiyo alitakiwa atumie jina la Ibrahim Munir ambaye angejifanya kuwa mfanyabiashara wa mafuta aliyekuwa na kampuni yake nchini Kenya.

Kabla ya yote, kitu cha kwanza walichokifanya ni kumtengenezea hati za kusafiria ambazo zilionyesha alikuwa akitokea nchini Kenya, hawakuishia hapo bali wakatengeneza tovuti yake binafsi ambayo ilionyesha shughuli mbalimbali za kijamii alizokuwa akizifanya nchini Kenya huku kukiwa na picha za kutengenezwa.

Kwa kuwa walikuwa na uhitaji wa kukamilisha kazi yao ilikuwa ni lazima Kennedy asafirishwe kuelekea nchini Kenya ambapo huko angetembelea vituo vya watoto yatima.

Hilo halikuwa tatizo kabisa lakini pia alitakiwa kubadilisha muonekano wake, haraka sana sura ya bandia ikaletwa na kuvalishwa, kila kitu ambacho kilikuwa kikienda kufanyika katika nchi za Kiarabu kilitakiwa kuwa siri kubwa, hakutakiwa mtu yeyote kufahamu kama alitumwa kwenda nchini humo kwa kazi maalumu.

Ilikuwa ni lazima kazi ifanyike, picha zipigwe huko Kenya na hatimaye kuingizwa kwenye tovuti hiyo na kwa sababu walikuwa siriazi na kazi hiyo, wakamtengenezea ukurasa wake wikipedia ambapo humo kulikuwa na stori yake ya uongo kuhusu maisha yake na mpaka alipoanza kufanya biashara ya mafuta huku akiwa ametokea katika familia ya kimasikini.

Mbali na yote hayo, pia walimtaka kupiga picha nyingi akiwa na kanzu, ilikuwa ni lazima aonekane kama alikuwa Muislamu hivyo alitakiwa kuuvaa uhusika na kupelekewa ustadhi ambaye alikuwa na kazi ya kumfundisha kuswali na kufanya mambo mengine katika dini hiyo.

Alikuwa makini kwa kila kitu, kichwa chake kilikuwa na uwezo mkubwa wa kukariri kila kitu alichokuwa akifundishwa, baada ya mwezi mmoja na kuonekana alikuwa tayari kwa kila kitu, akasafirishwa mpaka Dubai huku hati zake zote za kusafiria zikionekana kama alikuwa raia wa Kenya na kuanza kuelekea nchini Iraq.

Kabla ya kufika huko, tayari Wamarekani waliwasiliana na watu wao juu ya mtu huyo, waliwaambia watangaze kwamba mfanyabiashara mkubwa kutoka nchini Kenya alikuwa akienda nchini Iraq kufanya utalii wa kuzunguka sehemu mbalimbali ambazo mitume ya zamani ilikuwa imepitia.

Watu walitakiwa kujua ujio wake, si hilo tu bali pia watu walitakiwa kufahamu kwamba mtu ambaye alikuwa akija alikuwa bilionea mkubwa ambapo akaunti yake ilisoma kuwa na kiasi cha dola bilioni thelathini ambazo zilikuwa ni zaidi ya trilioni sitini, pesa hizo zote zilikuwa hewa lakini hilo hakukuwa na mtu aliyekuwa akilifahamu zaidi yake na watu waliokuwa wamemtuma.

Matangazo yakaanza kutolewa sehemu mbalimbali, kitendo cha bilionea kutoka Kenya kutangazwa kwamba alikuwa akienda nchini humo kutembelea sehemu mbalimbali za makumbusho na hata kutoa misaada, kila mmoja alichanganyikiwa, alikuwa Mwafrika lakini Waarabu hawakutaka kujali kuhusu ngozi, walichokuwa wakikijali ni kuona nchi yao ikinufaika na ujio wa mwanaume huyo.

Kila kona kulikuwa na stori kuhusu yeye, hakuwa amefika nchini humo lakini wale watu ambao walitumiwa kufikisha habari nchini humo walifanya kazi kwa uaminifu mkubwa mno kiasi kwamba ndani ya siku mbili tu, tayari alikuwa mwanaume maarufu sana.

Wale ambao hawakuwa wakimfahamu walikwenda kwenye tovuti mbalimbali na kulitafuta jina lake. Hawakupata tabu kumpata, ni ndani ya dakika chache tu walimuona akiwa sehemu mbalimbali Afrika huku akionekana kuwasaidia watu wengi waliokuwa kwenye matatizo.

Kwa jinsi alivyokuwa akijitoa, kila mmoja alifurahia, alionekana kuwa mwanaume mwenye roho nzuri ambaye alitamani kuona kila mtu akipata kile kidogo alichokuwanacho.

Uso wake ulikuwa wa huruma sana, alionekana kama malaika ambaye alitumwa duniani kwa ajili ya kuwasaidia watu waliokuwa wakiteseka kwa njaa kila siku.

Katika nakala zake alizobeba, aliandikiwa kwamba alitakiwa kufikia katika Hoteli ya Sultani Alwaqidr iliyokuwa pembezoni na Mji wa Baghdad.

Katika hoteli hiyo kulikuwa na msichana aliyeitwa kwa jina la Nurat ambaye alitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha msichana huyo anakuwa na ukaribu naye kwa sababu baba wa msichana huyo aliyeitwa Shabir Kuwad alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa matunda ndani ya jiji hilo.

“Sijaelewa, lengo hapa ni nini?” aliuliza Kennedy ambaye alijulikana kwa jina la Ibrahim Munir.

“Tunahitaji utengeneze ukaribu naye, umpende, umjali lakini mwisho wa siku tunataka uende mpaka nyumbani kwao, huko, tengeneza ukaribu na baba yake ambaye ni muhimu sana kwetu,” alisema mwanaume kwenye simu.

“Halafu?”

“Kwanza fanya hivyo, tutakwambia kazi kubwa ya baba yake. Hakikisha kwanza unaanza kumteka kimapenzi Nurat, halafu baada ya hapo tutakwambia ni kitu gani unatakiwa kufanya. Nakutumia picha ya Nurat ili isiwe vigumu kumpata,” alisema mwanaume huyo na kumtumia picha ya msichana huyo.

“Sawa. Nimemuona, nitakamilisha kila kitu na formula tutaipata tu,” alisema Kennedy na kisha kuzima simu ambayo ilikuwa ikitumia huduma ya wireless ndani ya ndege ile.





Hapakuwa hata na mtu aliyehisi kama ujio wa mwanaume huyo ndani ya nchi hiyo ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuhakikisha anapata formula iliyotumika kutengeneza mabomu ya nyuklia nchini humo.

Kila mmoja alijua mwanaume huyo alikuwa rafiki mkubwa ambaye alikuja kutoa misaada kwa watu wasiojiweza, kufanya biashara ya mafuta lakini pia kutembelea sehemu mbalimbali ambazo mitume ilikuwa imepita.

Watu walimsubiri kwa mbwembwe, wale ambao walikusanyika katika uwanja wa ndege walikuwa wakiimba kwa shangwe kana kwamba kulikuwa na mtu mkubwa kutoka serikalini alikuwa akifika. Shamrashamra zote hizo ziliandaliwa na msikiti wa Al-Rahman ambao ulikuwa mkubwa katika Jiji la Baghdad.

Baada ya dakika kadhaa, ndege ya Shirika la Ndege la Qatar ikaanza kutua ndani ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Baghdad. Miongoni mwa abiria mia mbili na ishirini waliokuwa ndani ya ndege hiyo alikuwemo Kennedy.

Macho yake yalikuwa yakiangalia nje, jinsi Jiji la Baghdad lilivyojengwa, kila alivyokuwa akiliangalia, moyo wake ulimwambia kwamba hapo ndipo alipotakiwa kufanya kazi ya hatari ambayo kama tu angegundulika basi ilikuwa ni lazima auawe.

Katika maisha yake yaliyokuwa katika tovuti feki ilionyesha aliishi maisha ya kawaida sana na ndiyo maana hata usafiri wa ndege aliokuwa akiutumia ulikuwa ni wa jumuiya na hakutaka kabisa kununua ndege ambayo angeitumia yeye peke yake.

Alimuomba Mungu mpaka pale ambapo ndege ilisimama na kuanza kuteremka. Alipofika chini na abiria wenzake wakaanza kuelekea katika jengo la uwanja huo, walipokaguliwa, akaondoka na kutoka ndani.

Alishangaa kukuta watu wengi wakimsubiri kwa shangwe, moyo wake ulisikia furaha mno, hakuamini alichokuwa akikiona, kila mtu alimkaribisha huku akionekana kuufurahia ujio wake mahali pale.

Watu wakaanza kumpiga picha na kumuingiza ndani ya gari na kuondoka mahali hapo. Njiani, mashehe ambao walipanda naye garini wakaanza kuzungumza naye mambo mengi kuhusu maisha yake, alipotoka na hata kuhusu ushirika wake katika suala zima la dini.

Kwa jinsi alivyokuwa akijibu, ilionyesha kabisa mwanaume huyo aliishika dini na alijua mambo mengi kuhusu Uislamu kumbe hakuwa hivyo, ni mafunzo maalumu ambayo alipewa ndani ya wiki moja tu na kuyashika vilivyo.

Alionekana kuwa na furaha mno, hakutakiwa kuwaonyeshea watu hao kama alikuwa na kitu kingine moyoni mwake, ilikuwa ni lazima aonyeshe tabasamu pana ambalo lingemfanya kila mmoja aamini alikuwa mtu mwema kwa ajili ya maisha yao.

Hoteli iliandaliwa na Wamarekani lakini kwa kupitia jina lake. Akapelekwa huko na kutulia chumbani huku watu wale ambao walimpokea wakisema kwamba wangerudi siku inayofuata kwa ajili ya kumchukua na kumtembeza sehemu kadhaa kuangalia mazingira.

Ujio wake uliendelea kuwa gumzo nchi nzima, televisheni zilionyesha jinsi alivyopokelewa uwanja wa ndege, alionekana kama mtu fulani maarufu ambaye alifika nchini humo.

Maofisa wa CIA walipokuwa wakiangalia kwenye televisheni, walifurahia kwani waliona walifaulu kwa kile walichokuwa wamekifanya, walichotakiwa kusubiri ni utekelezaji tu.

Alitulia chumbani ndani ya Hoteli ya Sultani Alwaqidr, kazi yake ilikuwa ni kuwasiliana na wenzake na kuwaambia tayari alikuwa ameingia nchini humo na kitu pekee kilichobaki kilikuwa ni utekelezaji tu.

“Umekwishakutana na Nurat?” aliuliza mwanaume kutoka upande wa pili.

“Hapana! Ila nimekutana na wasichana wengi warembo, nahisi mmojawapo anaweza kuwa Nurat,” alisema na kuanza kucheka kwa kicheko cha chini.

“Sawa. Ila usikosee hesabu, hakikisha unakutana na huyo Nurat na kufanya tulichokwambia. Kuna pesa zimeingizwa katika akaunti yako, tumia unavyojua ila kumbuka kwamba ni lazima ufanikishe kujua formula iliyotumika kutengenezea mabomu hayo,” alisikika mwanaume huyo.

“Hakuna shida.”

Akakata simu na kuanza kupanga mikakati. Ilikuwa ni usiku wa saa tatu, alichoka kukaa chumbani hivyo akatoka na kuelekea kwenye mgahawa uliokuwa hotelini hapo kwa chini.

Hakutaka kugundulika kwani kila mmoja alijua kwamba alikuwa bilionea mkubwa, aliyejiamini kulindwa na Allah kwani hata walinzi hakuwa nao hata kidogo.

Alipofika chini huku akiwa na kilemba chake kiasi cha kutoweza kugundulika kwa urahisi, akaelekea kwenye mgahawa huo na kuagiza kahawa, akaletewa na kuanza kunywa.

Kule alipokaa kulikuwa na giza, ilikuwa ni vigumu kugundulika kwa kuangaliwa. Macho yake hayakutulia, yalikuwa yakiangalia huku na kule kana kwamba alikuwa akitafuta kitu fulani.

Kwanza alihitaji kuonana na huyo Nurat, azungumze naye, amchangamkie na mwisho wa picha kabisa wawe wapenzi na kuambiwa ni kitu gani kilitakiwa kufuata baada ya hapo.

Hakutaka kuvumilia, alichokifanya ni kumuita kijana mmoja na kumuuliza kuhusu huyo Nurat, kwanza kijana huyo alishtuka, haikuwa ikiruhusiwa kwa mteja yeyote kwenda kwenye mgahawa na kumuulizia mhudumu fulani.

Hiyo ndiyo ilikuwa sheria ya Uarabuni, si Iraq tu bali kila kona huko. Kijana yule akahisi kabisa kwamba mtu aliyekuwa akizungumza naye alikuwa mgeni, hakufahamu kama kile alichokuwa alikifanya kilikuwa kosa kubwa.

“Who are you brother?” (wewe nani kaka?) aliuliza mhudumu huyo kwa lafudhi ya Kiarabu.

“A customer!” (mteja)

“Do you know the rules?” (unazijua sheria?)

“What rules?” (sheria zipi?)

Kijana yule akaanza kumwambia kuhusu kile kilichokuwa kikiendelea, Kennedy hakujua lolote lile, alimshukuru kijana yule lakini alimwambia kwamba alitamani sana kumuona msichana huyo kwa kuwa alikuwa na shida naye.

Aligundua kwamba kijana huyo alikuwa mgumu hivyo alichokifanya ni kuingiza mkono mfukoni na kutoa dola mia tatu na kumuwekea mezani kisiri ili watu wengine wasione.

“Nahitaji kumuona, nimemkumbuka sana. Kweli hutaki kunisaidia?” alisema Kennedy na kuuliza swali huku akizisogeza zile pesa upande wa kijana yule aliyekuwa amesimama mbele ya meza yake.

“Hakuna tatizo,” alisema kijana yule huku akizichukua.

“Nashukuru!”

“Ila sasa!”

“Kuna nini?”

“Amekwisharudi nyumbani! Kesho akija nitamwambia kwamba unamtafuta. Unaitwa nani?” aliuliza kijana yule.

“Ibrahim Munir.”

Kijana yule aliposikia jina hilo akashtuka, hakuamini kama mwanaume ambaye alikuwa mbele yake alikuwa Ibrahim. Alimfahamu mwanaume huyo, alikuwa bilionea mkubwa ambaye alikwenda kutembelea nchi hiyo huku akiahidi kutoa misaada mbalimbali.

Alimwangalia vizuri, Kennedy alikuwa kwenye mwanga hafifu hivyo kumgundua ilikuwa ni lazima umsogelee. Kitendo cha kumuona kijana huyo akiwa na ngozi nyeusi, aliamini moja kwa moja kwamba alikuwa mwanaume huyohuyo ambaye aliambiwa alifika nchini humo siku hiyo.

“Ibrahim!” alisema kijana huyo kwa kushtuka.

“Ndiyo! Naomba unisaidie!” alisema Kennedy huku akionekana kuomba sana.

“Hakuna shida. Nitakusaidia kwa gharama yoyote ile,” alisema huku akionekana kuwa na furaha mno.

“Nitashukuru!”

***

Siku iliyofuata asubuhi na mapema Nurat akaenda kazini kwake, alipofika tu, kitu cha kwanza kilikuwa ni kufuatwa na kijana yule aliyeonana na Kennedy usiku uliopita na kuanza kuzungumza naye.

Kwanza kabisa akaanza kumpongeza kwa mbwembwe, Nurat hakujua sababu za kupongezwa huko, alibaki akimwangalia mwanaume huyo kwa macho ya mshangao.

Alihitaji kujua sababu za pongezi zile, kwake, kilionekana kuwa kitu cha ajabu kupongezwa huku akiambiwa kwamba alikuwa na bahati kubwa mno.

Alihisi inawezekana alipandishwa cheo hapo kazini lakini hilo likapotea kichwani mwake kwa sababu kitu cha kwanza kabisa ambacho kingetakiwa kufanywa ni kupewa barua ya kupandishwa hicho cheo.

Akamuuliza kijana yule, hapo ndipo alipoanza kufunguka kuhusu bilionea ambaye alikutana naye usiku uliopita na kuanza kumuulizia huku akionekana kuwa na uhitaji wa kuonana naye. Nurat alibaki kimya, ni kama alipigwa na mshangao, kile alichoambiwa hakukiamini hata kidogo.

Ilikuwaje mwanaume atoke huko barani Afrika halafu afike nchini Iraq na kumuulizia yeye? Alimjuaje na kulikuwa na kitu gani alichokihitaji kutoka kwake? Hiyo haikumuingia akilini lakini wakati mwingine alijiona kama alikuwa na bahati kubwa, kuuliziwa na mtu mwenye jina kubwa kama Ibrahim haikuwa kawaida, ni lazima kungekuwa na kitu.

“Wewe umehisi nini?” aliuliza Nurat huku akimwangalia kijana yule.

“Anataka akuoe!” alijibu.

“Anioe mimi?”

“Ndiyo! Kwani wewe siyo mzuri?”

“Sidhani! Labda kama kuna kitu kingine alikwambia halafu unanificha,” alisema msichana huyo.

Wakazungumza kwa dakika chache na kisha kuondoka. Kichwa cha Nurat hakikutulia, muda mwingi alifikiria kuhusu yale maneno aliyoambiwa, yalimchanganya kichwani mwake, alitoka kwenye familia ya kawaida sana ambayo haikuwa na uwezo mkubwa kipesa, baba yake alikuwa muuzaji wa matunda katika kambi ya jeshi, hakuona kama kulikuwa na sababu zilizomfanya mwanaume huyo kufika nchini humo na kumuulizia huku akitamani sana kuonana naye.

Hakutaka kujiuliza maswali mengi sana, kwa kuwa alisema alihitaji kumuona basi akasubiri, hata kama angemaliza kazi zake, alikuwa radhi kumsubiri na kuanza kuzungumza naye.

Wakati huo Kennedy alikuwa amekwishafuatwa na kupelekwa katika sehemu mbalimbali hapo Iraq. Alionyeshewa msikiti mkubwa wa Al-Rahman na sehemu nyingine nyingi.

Kila mtu aliyekuwa akimwangalia alimfurahia, kwa muonekano wake wa nje tu alionekana kuwa ustadhi mkubwa aliyeijua sana dini ya Kiislamu kumbe hakuwa huko kabisa, alikuwa Mkristo mzuri ambaye kila Jumapili alikuwa akienda kanisani kusali.

Siku hiyo ilikuwa ni ya kuzunguka huku na kule, waandishi wa habari walialikwa na hivyo kufuatilia na kupiga picha kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Wote walifurahia, uwepo wa mwanaume huyo ulionekana kuwa kama baraka kutoka kwa Mungu kumbe ukweli wa mambo walimkaribisha mwanaume hatari kuliko wote waliowahi kufika nchini humo.

Wakati hayo yakiendelea, walichokifanya Wamarekani ni kumtuma mwanaume mwingine mweusi aliyeitwa kwa jina la Backnon kwenda huko Iraq kwa ajili ya kufanya kazi nyingine ambayo waliamini ingewasaidia sana.

Walihitaji aelekee huko na kwenda kupanga nyumba fulani kubwa, walijua kabisa kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima kutumika kama kweli walihitaji kuijua formula ya Waarabu ambayo waliitumia kutengeneza hayo mabomu ya nyuklia.

Backnon akaenda huko, naye alijifanya kuwa Muislamu mzuri kabisa, hakutakiwa kujulikana, kitu ambacho alitakiwa kufanya ni kuonyesha kwamba alikuwa na uhitaji wa kupanga nyumba kwa ajili ya matumizi yake binafsi.

Hilo halikuwa tatizo, akapewa nyumba moja iliyokuwa pembeni kabisa na Jiji la Baghdad ambapo kulikuwa na jangwa na kwa jinsi ilivyoonekana ilikuwa kama sehemu iliyotengwa kwani hakukuwa na watu wengine.

Baada ya kukabidhiwa nyumba hiyo, akaambiwa asubiri kitu chochote ambacho kingetokea kwani kwenye suala hilo, wao kama Wamarekani walikuwa wamejipanga kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kinavyotakiwa.

Kennedy alitumia saa kadhaa, ilipofika majira ya saa saba, akaenda msikitini kusali kisha kurudi hotelini kupumzika. Hakuhitaji mlinzi yeyote yule, aliwaambia Waarabu kwamba katika maisha yake yote alimwamini Mungu, unapokuwa na ulinzi wa Mungu hautakiwi kuhofia maisha yako kwa sababu huwa ni mkubwa kuliko hata ulinzi wa wanadamu.

Maneno hayo yakawafanya wampende zaidi pasipo kugundua kwamba mwenzao hakutaka kufuatiliwa, alihitaji kufanya mambo yake kimyakimya pasipo mtu yeyote yule kufahamu jambo lolote lililokuwa likiendelea.

Alipoingia hotelini, Nurat alikuwa akimwangalia tu, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu, hakuamini kama mwanaume huyo, bilionea alihitaji kuonana naye. Alitamani amuite na kumwambia alichotaka kumwambia lakini Kennedy alionekana kuwa bize mno, hivyo akaacha kwanza akapumzike.

“Ila mbona anaonekana hanijui?” aliuliza Nurat.

“Umejuaje?”

“Nimepishana naye, kama angekuwa ananijua basi angenisalimia,” alisema.

“Hapana! Unajua hawa mabilionea huwa wanakuwa na akili sana, ameamua tu kukupotezea ili usichanganyikiwe mtoto wa watu,” alisema kijana yuleyule aliyempa Nurat taarifa za kuuliziwa.

“Mmh!”

“Ndiyo hivyo! Ngoja giza liingie, nitakushtulia!”

“Sawa.”

Kazi hazikufanyika kama siku nyingine, kitu pekee kilichokuwa kichwani mwa Nurat ni mwanaume huyo tu. Alitokea kumpenda kwa sababu alikuwa bilionea, kwake, hakujali kuhusu ngozi yake, hakujali kitu chochote kile, alitamani sana amchukue, amuoe na kuondoka naye.

Ilipofika majira ya saa moja usiku, kama kawaida Kennedy akatoka chumbani kwake na kwenda kwenye ule mgahawa na kukaa palepale alipokuwa amekaa na kumuita yule kijana.

“Yupo wapi?” alimuuliza.

“Ngoja nikakuitie,” alisema na kuondoka.

Kennedy alisubiri mahali hapo, kichwa chake kilikuwa kikifikiria mambo mengi, alihitaji kuzungumza na msichana huyo kidogo, wazoeane na kuendelea na mambo mengine.

Baada ya dakika chache, kijana yule akarudi na Nurat kisha kukaa kwenye kiti na yeye kuondoka. Msichana huyo alimaliza kazi zake, alivalia nguo za nyumbani hivyo hakukuwa na tatizo lolote lile, kama alitaka kuongea naye, basi afanye hivyo kwa muda wowote aliohitaji.

“Nimesikia kwamba uliniulizia,” alisema Nurat huku akimwangalia Kennedy.

“Ndiyo! Nilihitaji sana kuzungumza na wewe,” alisema Kennedy.

“Kuhusu nini?”

“Mambo ya kawaida kuhusu maisha. Ila kubwa zaidi ni kujenga mazoea na urafiki,” alisema Kennedy huku akitabasamu.

Huo ndiyo ulikuwa ukweli wa mambo, hakuhitaji awe mpenzi wake kwa sababu tageti yake haikuwa msichana huyo. Alitakiwa kujenga naye urafiki lakini lengo lake kubwa ni kuonana na baba yake Nurat na kuanza kupanga naye mikakati.

Njia nzuri ya kumuingia mzee huyo ilikuwa ni kupitia kwa binti yake, alitakiwa kujifanya kuwa marafiki wakubwa lakini mwisho wa siku apate kile alichokuwa akikihitaji.

Hilo halikuwa tatizo, hapo alipokuwa akaanza kuzungumza na Nurat, alimwambia alikuwa msichana mwenye akili sana ambaye muda mwingi alifikiria kumsaidia kwa kuwa uwezo wa akili yake ulikuwa mkubwa mno.

Maneno hayo yaliingia kichwani mwa Nurat, kwa kuwa Kennedy alionekana kuwa bilionea, akakubaliana naye na hivyo kuendelea kuzungumza kama kawaida.

Walicheka pamoja, walifurahi na ilikuwa ni vigumu kwa watu kugundua kama watu hao siku hiyo ndiyo ilikuwa ni ya kwanza kuonana na kuzungumza.

“Ni biashara gani kubwa unaweza kuifanya hapa?” aliuliza Kennedy aliyejulikana kwa jina la Ibrahim.

“Kuna biashara nyingi sana, tatizo mtaji tu!”

“Hilo si tatizo tena!”

“Basi sawa, ila zipo nyingi! Nitakwambia kama tutaendelea kuonana,” alisema Nurat.

“Usijali! Ninahitaji upanue mawazo yako, uniambie mchakato wake, faida na hata hasara zake, nitakusaidia, hakika wewe ni msichana wa mfano sana,” alisema Kennedy huku akimwangalia msichana huyo.

Hiyo ilikuwa siku ya kwanza tu, wakaagana na Nurat kuondoka. Japokuwa alionekana kuwa msichana mgumu lakini kwa Kennedy hakuwa lolote lile. Mwanaume huyo alijua kuongea, kumzoea mtu kwa haraka na hata kujenga uaminifu mkubwa kwake.

Kichwa cha Nurat kilikuwa kikifikiria mapenzi tu, kwa jinsi alivyozungumza na Kennedy kwa nusu saa tu aligundua wanaume wenye pesa walikuwa na mawazo tofauti, stori zao walizokuwa wakipiga walionekana kuwa tofauti na wao.

Alifurahia mno, alihisi kabisa maisha yake yalikuwa yakienda kubadilika na kuwa mtu mwenye pesa nyingi kwa kuwa hata mbinu alizopewa na mwanaume huyo namna ya kutafuta pesa zilikuwa kiboko na aliamini kabisa kwamba kama angezifanyia kazi, basi siku moja angekuwa na pesa nyingi kama alizokuwanazo mwanaume huyo.

“Nauona utajiri mbele yangu! Kama atanisaidia, au atataka kunioa, nipo tayari kwa lolote lile,” alijisemea Nurat huku akionekana kuwa na furaha tele, hakujua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia.



Urafiki wao ulitakiwa kuwa siri kubwa, hakukuwa na mtu yeyote ambaye alitakiwa kufahamu kile kilichokuwa kikiendelea kati ya watu hao wawili. Kila siku walikuwa wakionana hotelini hapo katika sehemu iliyokuwa na mwanga hafifu na kuanza kuzungumza.

Kennedy ambaye alijulikana kwa jina la Ibrahim alijifanya kuwa rafiki mkubwa, muda mwingi alimchangamkia msichana huyo kana kwamba walifahamiana kipindi kirefu kilichopita. Nurat akajisahau, kuchangamkiwa kule huku Kennedy akijifanya kuwa rafiki yake wa karibu ambaye baada ya hapo alitarajiwa kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi, ukamchanganya zaidi na kuona kwamba tayari alikuwa mke wa mwanaume huyo.

Siku zikaendelea kukatika, kila kitu kiliendelea kuwa siri kubwa, baada ya wiki mbili za mazoea makubwa hatimaye Kennedy akamwambia msichana huyo kwamba alitamani sana kama angepata nafasi ya kuonana na familia yake kwa kuwa tu alikuwa na mipango mingi juu yake.

Nurat akafurahi, kwake, hiyo ilionekana kuwa nafasi kubwa, ukweli kutoka moyoni mwake alimpenda sana Kennedy, hakuona kama kulikuwa na mwanaume mwingine aliyestahili kuutoa usichana wake zaidi ya mwanaume huyo ambaye kwa kuongea tu ilikuwa ni rahisi kugundua alikuwa na akili nyingi.

Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, Nurat akakubaliana naye na hatimaye siku hiyo kumchukua na kuanza kuelekea naye nyumbani kwao. Walitembea huku Kennedy akijitahidi kujificha kwani hakutaka kugundulika kama alikuwa yeye, endapo tu angegundulika basi aliamini kila kitu kingekufa muda huo.

Baada ya dakika kadhaa wakafika nyumbani. Aliingia kikawaida sana lakini baada ya familia yake kumuona, kila mmoja alichanganyikiwa, hawakuamini kumuona mwanaume huyo mahali hapo. Alikuwa maarufu na tajiri mkubwa lakini mbali na hayo mawili, alipenda dini sana na kuswali

“Karibuni sana,” alisema mzee Shabir Kuwad huku akimwangalia Kennedy.

Bado aliona kama ndoto, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, kwake, Kennedy alikuwa mtu wa tofauti sana, maarufu ambaye alijizoelea sifa nyingi hapo Iraq. Aliheshimiwa kila kona alipopita kiasi kwamba watu wengi walikuwa wakimuhusudu kuonana naye lakini hakuwapa nafasi.

Mzee huyo aliona ni bahati ya kipekee kuonana na mtu huyo, alitafutwa kila kona, mpaka kufika nyumbani kwake ilimaanisha alizivuka nyumba nyingi, alitembea umbali mrefu mpaka kuthubutu kuingia humo ndani, hayo yote yakamfanya kuhisi kama alimkaribisha mtume nyumbani kwake.

Wakaanza kuzungumza, kila mmoja kwenye familia hiyo alionekana kuwa na furaha, waliongea mambo mengi, kwa kirefu na mwanaume huyo aliwaambia kuhusu mpango wake. Alihitaji kumsaidia sana Nurat lakini pia alihitaji kumsaidia mzee Shabir katika biashara zake alizokuwa akizifanya.

“Ninasambaza matunda serikalini,” alisema mzee huyo.

“Na ina faida?”

“Kiasi chake! Tatizo ni moja tu, usafiri, natumaini kama ningepata usafiri, ningefurahi zaidi,” alisema mzee huyo.

“Hilo si tatizo hata kidogo!”

Kennedy aliongea kwa kujiamini kupita kawaida. Kununua gari kwa ajili ya mzee huyo halikuwa tatizo lolote, alichohitaji ni kufanikiwa kwa kile kilichokuwa kimepangwa na hatimaye nchi ya Marekani kuwa na sifa kubwa kwa kila kitu kuhusu Rais Hamis ambaye mpaka kipindi hicho alijiona kuwa mjanja kuliko mtu yeyote yule.

Walizungumza mambo mengi na siku iliyofuatia, gari mpya aina ya Double Cabin likaingia nyumbani kwake na kuambiwa ilikuwa mali yake alinunuliwa na mtu mmoja kutoka nchini humo.

Mzee huyo hakuamini macho yake, akachukua kadi ya gari na kuangalia jina, liliandikwa jina lake, kulikuwa na vibali vyote na vililipiwa, hakutaka kujiuliza, aligundua kwamba alikuwa ni Kennedy ambaye alizungumza naye na kumwambia angemsaidia.

Hakutaka kuchelewa, haraka sana akachukua simu yake na kumpigia binti yake, Nurat na kumwambia kilichotokea. Msichana huyo hakuamini, alihitaji kuliona gari hilo hivyo siku hiyo haraka sana akarudi nyumbani, alipofika, akalikuta limepaki, huku machozi yakianza kumtoka, akamsogelea baba yake na kumkumbatia.

Familia nzima ilikuwa na furaha, wakampigia simu Kennedy na kumwambia siku hiyo walitakiwa kula wote chakula cha usiku, hilo halikuwa tatizo, akakubaliana nao na usiku huohuo kwenda nyumbani hapo.

Walipomuona, walimsogelea na kumkumbatia kwa furaha. Walimshukuru, mwanaume huyo alionekana kuwa na umuhimu mkubwa kuliko mtu yeyote yule katika dunia hii kwenye familia hiyo. Walizungumza naye mambo mengi, walimsifia pasipo kugundua kama mwanaume huyo alikuwa na mipango yake, gari halikuwa tatizo, walichokuwa wakihitaji ilikuwa ni lazima kifanyike.

“Tunashukuru sana, yaani sana,” alisema mzee Shabir huku akiikutanisha mikono yake.

“Hakuna shida. Allah amenigusa kufanya hivi,” alisema Kennedy huku akionekana kumaanisha alichokisema.

Wakaendelea na mazungumzo mengi, hapo ndipo Kennedy akatumia nafasi hiyo kumwambia mzee huyo kwamba alihitaji kuona sehemu aliyokuwa akipeleka matunda, kulikuwaje na kulikuwa na akina nani ambao kila siku ilikuwa ni lazima awapelekee matunda hayo.

Kwa kuwa alipewa gari, alikuwa na furaha kubwa hakusita kumwambia mambo mengi. Alisema kwamba matunda hayo alikuwa akiyapeleka jeshini kila siku usiku kwani kulikuwa na watu muhimu ambao walitakiwa kula matunda kwa kuwa kazi waliyokuwa wakiifanya ilikuwa kubwa na ya siri sana.

“Kazi gani?” aliuliza Kennedy, hakutaka kulitilia mkazo katika swali hilo, hivyo alikuwa akiuliza kama masihara kumbe alihitaji mzee huyo afunguke.

“Si wale wanaotengeneza nyuklia!” alisema mzee huyo.

“Nyuklia? Hivi kuna mtu anatengeneza nyuklia zaidi ya nchi za Magharibi?” alijifanya kuuliza, alihitaji kufahamu ukweli.

“Hujafuatilia habari?”

“Hapana! Huwa siangalii televisheni, muda mwingi nasoma Koran na kumuabudu Allah!” alijibu.

“Unapitwa,” alisema mzee Shabir na kuanza kumwambia Kennedy kila kitu kilichokuwa kikiendelea.

Hakutaka kumficha, utajiri wa uongo aliokuwanao ukamfanya mwanaume huyo kumwambia kila kitu, jinsi alivyokuwa akienda huko na kukutana na watu hao na kuwauzia matunda.

Walifichwa, walikuwa katika chumba cha siri na hakukutakiwa kuingia watu wengine wengi, ni yeye, viongozi wa serikali na wale ndugu wa karibu tu, tena wa damu.

“Daah! Kumbe napitwa, sasa na mimi naweza kuwaona? Nataka nijifunze mengi kuhusu wao,” aliuliza Kennedy.

“Kuwaona?”

“Ndiyo!”

“Sijajua!”

“Ila wewe si huwa unaingia?”

“Ndiyo!”

“Sasa kwa nini usinifanye mimi kama mfanyakazi wako halafu niingie na wewe?” aliuliza Kennedy.

Ilikuwa ni vigumu kukubaliana naye lakini kwa sababu alikuwa na ushawishi mkubwa kipesa na maneno matamu, mzee huyo akakubaliana naye na hivyo kupanga mipango ya kwenda huko.

Kwanza alitakiwa kubadilisha muonekano wake, hakutaka kuwa kama alivyokuwa, alitakiwa kutokugundulika na angekwenda naye huko kwa siku tatu tu kwani vinginevyo serikali ingegundua kilichokuwa kimetokea na hivyo kuingia kwenye matatizo na hata kupoteza kazi.

Kwa Kennedy halikuwa tatizo hata kidogo, alikubaliana naye na hivyo kuondoka kurudi hotelini huku wakiwa wamekubaliana kwamba siku hiyo wangekwenda katika nyumba hiyo huku akiwa na muonekano wa kimasikini na kuwaona watu hao.

Akarudi hotelini kwake. Kitu cha kwanza kilikuwa ni kuwasiliana na wenzake nchini Marekani na kuwaambia kila kitu kilichotokea, wao wakamwambia awasiliane na Backnon ambaye alikuwa mahali huko na kumwambia kile alichotakiwa kufanya.

“Nipeni mbinu, niwateke au niwamalize?” aliuliza Kennedy.

“Hapana! Wateke, tunahitaji kujua hizo formula ambazo wanazitumia kutengenezea mabomu hayo,” alijibu mwanaume kutoka upande wa pili.

“Ooh! Sawa haina shida! Basi nitahitaji dawa yenye nguvu ambayo inaweza kuwafanya watu kulala ndani ya dakika chache,” alisema.

“Haina shida. Backnon atakupa,” alisema mwanaume huyo na kukata simu.

Haraka sana Kennedy akawasiliana na Backnon na kumwambia kilichokuwa kimejadiliwa, kwa kuwa mwanaume huyo alikuwa hapohapo Baghdad, wakaonana hotelini na kuanza kuzungumza.

Alimwambia kwamba angempa dawa moja kali ya usingizi ambayo ilikaa katika chupa fulani na kama angeifungua, ingeanza kutoka na kusambaa chumbani na hatimaye watu wote hao kulala usingizi mzito na hivyo kufanya kile alichotaka kufanya.

“Mh! Na mimi si nitalala manake nitakuwa humo chumbani?” aliuliza Kennedy.

“Usijali! Hutoweza kulala! Yaani kuna dawa nitakupa ambayo itakuzuia wewe kulala kama wengine,” alisema Backnon.

Hicho ndicho alichomwambia, wakayapanga huko huku akimpa kamera iliyokuwa na muonekano wa kalamu ili kuitumia kuchukulia picha na kurusha moja kwa moja mpaka nchini Marekani na Backnon kuondoka hotelini hapo huku akimuacha Kennedy akiendelea kufanya mambo yake kama kawaida.

Kwa kuwa hakutaka kugundulika, aliendelea kuwasiliana na Nurat na kumwambia ni kwa jinsi gani alikuwa muhimu kwake, hakutaka kumtongoza lakini kitu alichokifanya ni kumtumia kiasi kikubwa cha pesa. Hakumtumia yeye tu bali hata mzee Shabir ambaye baada ya kuzipokea, alijikuta akichanganyikiwa na kumpenda Kennedy maradufu.

Siku iliyofuata usiku akaonana na mzee huyo na hatimaye kuanza kuelekea katika nyumba hiyo kubwa kwa ajili ya kupeleka matunda kwa kutumia gari yake mpya. Alipofika huko, kila mtu alishangaa, hawakuamini kama mwanaume huyo alikuwa na usafiri huo wa kifahari, kila mtu aliyekuwa akimuuliza, alimwambia alipewa zawadi na Mungu kwa kuwa alisaidia sana watu wenye matatizo mbalimbali.

“Na huyu nani?” aliuliza mlinzi.

“Huyu ni mfanyakazi wangu, nimenunua usafiri, sasa kwa nini nisiajiri mtu wa kunisaidia kazi zangu?” aliuliza mzee huyo huku akitoa tabasamu lililopokelewa kwa tabasamu pia kutoka kwa walinzi wa eneo hilo.

Walimwamini mzee huyo, alijiheshimu na hivyo kuliingiza gari hilo ndani huku akiwa na Kennedy ambaye alijifunga kilemba na ilikuwa vigumu kugundulika kwa sababu ilikuwa ni usiku sana.

Akaliingiza gari lake mpaka ndani. Kwenye uwanja wa nyumba hiyo kubwa hakukuwa na watu, walikuwa wachache sana ambao walikuwa wakilala humo. Wakateremka na kuondoka kuelekea ndani huku wakibeba makapu makubwa na kuingia mpaka kwenye chumba kile walichokuwa watu hao.

Macho ya Kennedy yakatua kwa watu hao waliokuwa mahali hapo. Walionekana kuwa na afya njema, walikuwa sehemu salama ambayo ilikuwa na ulinzi wa kutosha kwani mbali na wao, pia kulikuwa na askari waliokuwa wakilinda humohumo ndani huku wakiwa na bunduki zao, yaani watu hao walikuwa wakilindwa kupita kawaida na kila siku usiku ilikuwa ni lazima Rais Hamis kupiga simu na kujua maendeleo yao kama walikuwa chakula cha kutosha na matunda au la.

Walipoingia mule, macho ya Kennedy yalikuwa yakiangalia huku na kule, hiyo siku ya kwanza ilikuwa ni ya kuusoma mchezo, kulikuwa na nini na nini, watu gani walikuwa mahali gani.

Waliwaangalia watu hao, walikuwa watatu ambao walionekana kuwa wataalamu sana kwani muonekano wao tu ilikuwa ni vigumu kutokugundua kama walikuwa na akili kubwa.

Wakaanza kuwagawia matunda. Watu hao hawakuwa wakitoka, muda mwingi walitumia kuwa ndani ya nyumba hiyo na hawakutakiwa kupata taarifa yoyote kutoka nje na ndiyo maana hata huyo Kennedy alipoingia hawakugundua kama alikuwa Ibrahim kwa kuwa hata yeye mwenyewe hawakumjua.

Kamera ile ilikuwa ikiendelea kupiga picha kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali pale. Hakukuwa na mtu yeyote aliyegundua hilo, nchini Marekani walikuwa wakipata kila kitu, waliwaangalia wataalamu hao, hivyo wakajipanga kumwambia Kennedy kwamba siku nyingine ambayo wangeingia humo ilikuwa ni lazima ahakikishe kwamba anawateka watu hao na kuondoka nao.






Kila picha ambayo ilipigwa kwa kutumiwa kamera ndogo aliyokuwanayo Kennedy ikapelekwa mpaka nchini Marekani ambapo huko wakampongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya na hivyo kumsisitizia kwamba ni lazima ashirikiane na Backnon kuhakikisha wanawateka watu hao na kuondoka nao.

Kilichokuwa kimepangwa kutumiwa ndani ya nyumba hiyo na kuwapata kilikuwa ni dawa ya usingizi lakini baada ya kufikiria sana wakagundua kitu kizuri ambacho kilitakiwa kutumika ni kuwawekea sumu kwenye matunda ambapo baada ya kula tu, walewe na kulala na kisha Kennedy awachukue na kuondoka nao.

Hilo lilionekana kuwa wazo zuri, akakubaliana nao na hivyo kuendelea na maisha ya huko nchini Iraq kama kawaida. Hakuacha kuonyesha mapenzi kwa Nurat, alijua kabisa kulikuwa na kazi ngumu, ilikuwa ni lazima akubalike kabla ya kufanya lile alilotaka kulifanya.

Hakuacha kufanya mambo na serikali ya nchi hiyo, alihakikisha anawafanyia kila kitu walichokuwa wakitaka, alifanya mambo mengi, alikutana na mawaziri mpaka Rais Hamis ambaye alimsifu kwa kuwa alifanya mambo mengi kwa ajili ya nchi yake.

Kwenye mazungumzo yao mengi na rais huyo alimwambia wazi kwamba katika maisha yake alikuwa akiichukua Marekani na nchi za Ulaya kwa sababu zilimtenganisha na familia yake.

Kwa stori yake ya uongo alimwambia kwamba familia yake iliuawa na Wamarekani baada ya kugundulika kwamba baba yake alikuwa akishirikiana na Waarabu katika mambo nyeti kabisa hivyo ili kumaliza ishu hiyo ilikuwa ni lazima waiteketeze familia yake pia.

“Wewe uliponaje?” aliuliza Rais Hamis huku akimwangalia Kennedy.

“Kipindi hicho nilikuwa nikisoma Urusi. Baba pia alikuwa na uhusiano mzuri na Warusi hivyo alizungumza na rais wa huko kwamba nilitakiwa kulindwa kwa kuwa ningeuawa muda wowote ule kwa sababu tayari kulikuwa na taarifa taifa la Marekani lilitaka kuimaliza familia yetu,” alisema Kennedy kwa huzuni kabisa, kwa jinsi alivyoonekana, ilikuwa ni rahisi kusema kile alichozungumza mahali hapo kilikuwa kweli kabisa.

Walizungumza mambo mengi na Rais Hamis pasipo kugundua kwamba mazungumzo yake yalikuwa yakinaswa na Wamarekani ambao walikuwa maadui zake wakubwa.

Walifurahia na kula pamoja huku wakipiga stori mbalimbali mahali hapo. Baada ya kumaliza, akaondoka zake kurudi hotelini.

Kesho, magazeti ya nchi hiyo yote yalikuwa na habari kuhusu Kennedy aliyekuwa akijulikana kwa jina la Ibrahim. Aliheshimika kila kona, alipendwa na wengi kuona kwamba alikuwa mtu muhimu sana ambaye Mungu alimtuma ndani ya nchi hiyo kwa ajili ya kuleta neema humo.

Hakukuwa na mtu yeyote aliyegundua kama mwanaume huyo alikuwa adui namba moja. Maofisa wa usalama wa taifa kutoka nchini humo walifuatilia kuujua undani wa mwanaume huyo lakini hawakugundua kitu zaidi ya kuonyesha alikuwa bilionea mkubwa nchini Kenya ambaye alifika humo kwa ajili ya kutembelea sehemu zilizokuwa na makumbusho ya mitume na kufanya mambo mengine ya biashara ya mafuta.

Hakutaka kuwaonyeshea kama alikuwa mtu hatari, aliwaambia nchini humo kulikuwa na mtu ambaye alikuwa rafiki yake, alikutana naye kupitia binti yake aliyeitwa Nurat.

Alimtambulisha mzee Shabir kwamba ndiye aliyekuwa mwenyeji wake, walizungumza mambo mengi na hivyo kila mmoja kumkubalia kwamba alikuwa mtu mzuri.

Hapo Baghdad akawasiliana na Backnon na kumwambia kwamba walitakiwa kutafuta dawa ambayo ingewekwa kwenye sindano na kuchomwa kwenye matunda ambayo watu hao walitakiwa kula.

Hilo halikuwa tatizo, dawa hiyo ikatafutwa na kupewa, akaambiwa kwamba ni lazima ayachome matunda hayo ambayo yangepelekwa huko na watu hao kulishwa.

Akapanga na Backnon kwamba siku hiyo achukue gari lake na kwenda kulipaki mbali kidogo na sehemu ambayo kulikuwa na nyumba hiyo kwa sababu wakati ambao angetoka na watu hao kwa kutumia gari la mzee Shabir basi aondoke nao na kuwaingiza ndani ya gari hilo na kwenda kwenye nyumba ambayo alikuwa akiishi.

Siku ambayo alipanga kufanya tukio hilo, kwanza yeye ndiye aliyehusika katika kuyanunua matunda hayo, aliagiza ya kutosha na yalipopelekwa kwa mzee Shabir, alihakikisha anachukua sindano yake na kuanza kuyachoma huku akijifanya kuendelea kufanya kazi nyingine.

Ilikuwa ni vigumu kugundua, kanzu ambayo aliivaa ilificha kila kitu, ilikuwa ni kwa siri kubwa, hakukuwa na yeyote ambaye aligundua na sehemu ambayo matunda hayo yalikuwa yakihifadhiwa ilikuwa ni kwenye kibanda kimoja.

Matunda hayo yakiwemo maembe, ndizi, matango, machungwa na mengine yalichomwa na hivyo usiku kuyachukua na kuanza kuelekea katika nyumba ile waliyokuwa wakiishi wale wataalamu wa kutengeneza mabomu ya nyuklia.

Njiani walikuwa wakizungumza mambo mengi, siku hiyo Kennedy alionekana kuwa mchangamfu mno, alizungumza mfululizo huku akimwambia mzee huyo ni kwa jinsi gani alitakiwa kufanya biashara zake na kufanikiwa. Aliaminika kwa sababu tu maisha yake yenyewe yalikuwa ni ya kifahari sana.

“Hutakiwi kudharau biashara ndogo,” alisema Kennedy huku akimwangalia mzee huyo aliyekuwa akiendesha gari.

“Kwani utajiri wako ulianzia huko?”

“Ndiyo! Nilianza kwa kuuza vitambaa vya suti, nakumbuka enzi hizo Waafrika hawakuwa wakivaa suti kabisa,” alisema.

“Sasa ilikuwaje mpaka kufanikiwa?”

“Ilikuwa ni vigumu mara ya kwanza lakini baada ya televisheni kuingia na watu kuona Wazungu wakivaa suti, wakapenda na hivyo kuja kununua kwangu,” alisema Kennedy.

“Oh! Kweli hatari! Ulivumilia sana!”

“Ndiyo! Kwenye biashara ni lazima uvumilie, kuna wakati unakutana na watu ambao wanajaribu kukukatisha tamaa kwa kusema kwamba huwezi, ukikubaliana nao, umepotea,” alisema Kennedy.

“Aisee kweli kabisa.”

Walizungumza kuhusu mafanikio, hayo yote alihitaji kuaminika na mzee huyo, hakutaka kumuonyesha kama kulikuwa na jambo lolote lililokuwa likiendelea.

Safari ilikuwa ikiendelea na baada ya dakika kadhaa wakafika katika nyumba hiyo na kuanza kuyashusha matunda hayo. Wakayaingiza ndani na kuwawekea watu hao, hilo halikuonekana kuwa jambo zuri kwa sababu Kennedy alitaka watu hao wale matunda hayo na kufanya mambo yake, akaanza kuwagawia.

Hilo lilikuwa jambo geni kwa mzee Shabir, si kwake tu bali hata kwa watu wale. Walimuona kuwa mtu wa ajabu, kwa Uarabuni kufanya tukio kama hilo ilikuwa ni nadra sana, ilionyesha ni kwa kiasi gani alikuwa na mnyenyekevu.

Walifurahia, wakayapokea na kuanza kula. Hakuishia hapo, aliwafuata walinzi na kuwapa matunda yale. Wote waliona kwamba alikuwa mtu mkarimu, hawakujua kama upande wa pili mwanaume huyo alikuwa na mipango yake.

Mzee Shabir akafurahi sana, kwake, kile alichokiona kikifanywa na mtu aliyekuwa na pesa kama Ibrahim ilikuwa ni kama muujiza. Alimwangalia mwanaume huyo, siku hiyo alidhihirisha hakuwa mtu wa majivuno, alikuwa mtu mpole na mkarimu ambaye kila mtu alitakiwa kuiga mfano kwake.

“Mbona wananishangaa?” aliuliza Kennedy huku akimwangalia mzee Shabir.

“Unavyowagawia matunda!” alijibu mzee huyo.

“Kwani kuna tatizo?”

“Ni heshima kubwa sana. Hilo wanatakiwa kufanya wanawake kwa wanaume, ila mwanaume kwa wanaume, unaonekana una heshima na mkarimu sana,” alisema mzee Shabir.

“Oh! Kumbe! Basi na wewe karibu,” alisema Kennedy huku akimpa ndizi mzee huyo.

Hakutaka kula lakini kwa sababu bilionea huyo alimuonyeshea heshima na ukaribu wa hali ya juu, naye akachukua na kuanza kula. Mpaka kufikia hapo tayari Kennedy aliona alifanikiwa kwani kila mtu aliyekuwa akimwangalia humo, alikuwa bize kula matunda.

Nchini Marekani walikuwa wakifuatilia kila kitu kupitia ile kamera aliyokuwanayo Kennedy, hawakuamini kama kazi ingekuwa nyepesi namna ile, kila mmoja akafurahi na kuona kwamba walifanikiwa kuwapata watu hao.

Ni ndani ya dakika kumi tu, kila mmoja akawa hoi, macho yakawa mazito, wakakaa chini na kulala, walinzi waliokuwa na bunduki zao, zikawaanguka na wao kulala, ile dawa ya usingizi iliyowekwa kwenye matunda yake ikaanza kufanya kazi kwa kasi.

“Mbona wanalala?” aliuliza Kennedy, alikuwa akimuuliza mzee Shabir ambaye naye macho yake yalianza kuwa mazito.

“Sijajua kwa nini! Hata mimi macho yangu yashaanza kuwa mazito, hebu subiri nikae hapa kwanza,” alisema mzee huyo, akakaa pembeni na kulala.

Yote yaliyokuwa yakitokea, Kennedy alikuwa akiangalia tu, kazi yake ilikuwa ni kuhesabu ni watu wangapi walikuwa wakiendelea kulala.

Humo kulikuwa na watu zaidi ya ishini, wote wakalala, hakutaka kuwa na presha, akachukua simu yake na kumpigia Backnon na kumwambia asogeze gari kwani tayari alifanikiwa kwa kila kitu.

Gari hilo likasogezwa na kuwachukua watalaamu hao, wakawapakiza ndani ya gari na kuondoka nao kuelekea kule alipokuwa amepanga Backnon kwani ilikuwa ni lazima sehemu hiyo itumiwe kwa ajili ya kuhakikisha wanapata formula hiyo.

Hawakuchukua muda mrefu, wakafika humo na kuwaingiza ndani, kila kitu kilikuwa kimeandaliwa, kulikuwa na watalaamu wanne, viti vyao vilikuwa tayari, wakakalishwa kisha kuvumiliwa nguo zote, wakawekewa nyaya za umeme mbavuni na sehemu za siri huku wakiwa usingizini.

Wakawafunga mikono na miguu, midomoni mwao wakawafunga gundi nzito ambayo isingekuwa rahisi kwao kufumbua midomo na kusema neno lolote lile.

Baada ya kila kitu kukamilika, wakapokea simu kutoka nchini Marekani ambapo huko walikuwa wakifuatilia kila kitu, wakawaambia kwamba walitakiwa kufanya lolote liwezekanalo kuhakikisha wanatoa siri zote vinginevyo basi wawamalize kwani hawakuwa na muda mrefu wa kukaa nchini humo.

“Hilo usijali! Ngoja wapate fahamu, watatuambia kila kitu, kwenye kazi zetu hamtakiwi kuwa na hofu hata kidogo,” alisema Kennedy, katika maisha yake yote hakuamini kama kungekuwa na mtu ambaye angejifanya kuwa mgumu kwake, alijiamini na kwa jinsi alivyowaangalia watalaamu wale, ilikuwa ni lazima wamwambie kile alichokuwa akikihitaji.





“Did you find his name?” (umelipata jina lake?)

“Yes sir!” (ndiyo mkuu)

“Who is he?” (ni nani?)

“Kennedy Edward!”

“Very nice. I want to know where he lives, his family too, just give me everything I want, right?” (safi sana! Ninahitaji kujua anapoishi, familia yake pia, nipe kila kitu ninachohitaji, sawa?)

“Yes sir,” (ndiyo mkuu)

Hayo yalikuwa ni mazungumzo baina ya Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa nchini Uingereza, MI6 aliyeitwa Pegg Burn ambaye alikuwa akizungumza na kijana wake, mtaalamu katika masuala ya kompyuta aliyeitwa Baines Cole.

Walipewa taarifa za chini kabisa kwamba wapinzani wao wakubwa, Marekani walikuwa wamepeleka mtu nchini Iraq kwa ajili ya kuhakikisha wanapata formula iliyotumika kutengeneza mabomu ya nyuklia ambayo alikuwa akijivunia Rais Hamis.

Japokuwa alikuwa ameaminiwa sana lakini Backnon ndiye ambaye alitoa taarifa hiyo kwa watu hao na kuwaambia kuhusu Kennedy. Ulikuwa usaliti mkubwa kufanywa na mtu kama yeye lakini hakuonekana kujali, kwake, kitu alichokuwa akikiangalia ni pesa tu kutoka kwa Waingereza ambao walikuwa wakimlipa vizuri sana mtu ambaye aliwapa siri kuhusu Marekani waliokuwa wakipambana nao kisiri.

Hizo zilikuwa taarifa zilizowaumiza sana, walilifahamu taifa hilo, halikuwahi kushindwa kitu, walikuwa na watalaamu, wajanja ambao kama kweli walikuwa wakihitaji kitu chochote kile ilikuwa ni lazima wakipate hata kama wangechukua muda gani.

Backnon aliwapa taarifa aliwaeleza kwa kifupi sana na kuwataka wao wafuatilie ili wapate zaidi kile walichotakiwa kukipata. Hilo halikuwa tatizo, haraka sana Cole akaanza kutumiwa na hatimaye kumpata mwanaume huyo aliyeitwa kwa jina la Kennedy Edward.

Ilikuwa ni lazima waipate formula hiyo, walijua kabisa kwamba kama wangezungumza naye na kumuomba lingekuwa jambo gumu sana hivyo walitakiwa kufanya kitu fulani ambacho kingemfanya mwanaume huyo afanye kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba anawapelekea formula hiyo.

Kitu ambacho walifikiria ni kuiteka familia yake. Waliamini kwamba alikuwa na mke na watoto ama mtoto hivyo ilikuwa ni lazima wafanye juu chini mpaka kuhakikisha wanaipata familia yake.

Hawakujua alipokuwa akiishi nchini Marekani lakini baada ya kufuatilia katika kompyuta zao, wakagundua mpaka mahali alipokuwa akiishi na familia yake, yaani mkewe na mtoto wake aliyeitwa Nicole.

“Ana mke na mtoto mmoja,” alisema Cole.

“Safi! Anaishi wapi?”

“Jijini New York kwenye mtaa wa Shakespeare W56 nyumba namba 1709 karibu na Barabara ya St. Victoria,” alijibu Cole.

“Nahitaji kujua kuhusu familia yake!”

“Mtoto wake anasoma katika shule ya Prince Richard ambayo si mbali sana na mahali wanapoishi,” alijibu.

“Sawa. Naihitaji familia yake, watume vijana waende huko haraka sana,” alisema Burn.

Siku hiyo ilikuwa ni kivumbi, kila kona ndani ya makao makuu ya MI6 ilikuwa balaa, kila mmoja alikuwa bize kuhakikisha familia ya Kennedy inatekwa haraka iwezekanavyo.

Kulikuwa na mpango mzito ambao ulikuwepo katika kuhakikisha wanaipata formula hiyo, wao kama wao walijaribu kwa nguvu zote kuingia nchini Iraq lakini ilishindikana hivyo kama Marekani walifanikiwa basi ilikuwa ni lazima wahakikishe wanaipata hata kama hawakifanyia kazi hata kidogo.

Vijana waliokuwa nchini Marekani wakapigiwa simu na kuambiwa kilichokuwa kikiendelea, wao, walitakiwa kufanya kila liwezekanalo mpaka familia hiyo itekwe na kupelekwa mahali fulani kufichwa.

Hilo halikuwa tatizo, vijana hao wakaondoka na kuelekea katika Mtaa wa Shakespears ambapo huko wakaelekea karibu na nyumba hiyo na kutulia. Siku hiyo, kwa kuwa waliwahi asubuhi na mapema, wakamuwahi mke wa Kennedy, Eve ambaye alikuwa akimtoa mtoto wake na kumpeleka shule.

Walimwangalia, hawakutaka kwenda kumteka, siku hiyo ilikuwa ni maalumu ya kuangalia ni kitu gani alikuwa akikifanya, yaani akitoka shuleni anakwenda wapi mpaka kukamilisha mizunguko yake.

Baadaye aliondoka na kuelekea kazini ambapo jioni akamfuata mtoto wake na kurudi nyumbani. Mpaka hapo wakajua kwamba alikuwa na sehemu tatu za kwenda, yaani shuleni, kazini na nyumbani hivyo kama kweli walitaka kumteka walitakiwa kufanya hivyo wakati akirudi kutoka shuleni.

Wakawasiliana na wenzao kutoka nchini Uingereza na kuwaambia kuhusu kile kilichotokea, haraka sana wakawaambia kwamba walitakiwa kufanya utekaji jioni kwa sababu kusingekuwa na magari mengi kama asubuhi.

Hilo halikuwa tatizo hata kidogo, siku iliyofuata wakafuatilia na mwisho wa siku, majira ya jioni wakati Eve akitoka shuleni na mtoto wake kurudi nyumbani ndiyo wakatumia nafasi hiyohiyo kwenda kulisimamisha gari lao mbele ya gari la mwanamke huyo wakati akiwa kwenye barabara ya mtaani kwao kwenda nyumbani kwake, wanaume hao wakateremka na kumfuata kisha kuwatoa wote wawili ndani ya gari.

“Twende huku,” alisema mwanaume mmoja, usoni mwake alikuwa na kinyago, mkononi alishika bastola, yaani alikuwa na muonekano wa mtu hatari.

Wakawachukua, wakawaingiza ndani ya gari na kuondoka zao. Hakukuwa na mtu aliyeliona tukio hilo, katika mtaa waliokuwa wakiishi hakukuwa na watu nje, kila nyumba ilikuwa na geti lake, watu waliokuwa wakiishi huko wengi walikuwa wafanyakazi wa serikali ambao walijengewa nyumba hizo na serikali.

Ndani ya gari Eve alikuwa akitetemeka, alikuwa na hofu, kwa jinsi alivyowaangalia watu hao, kwa jinsi walivyoonekana ilionyesha walikuwa watu hatari ambao wangeweza kuwafanya jambo lolote baya kama tu wangeleta ubishi ndani ya gari hilo.

“Don’t kill us, pleaseee....” (tafadhali msituue...) alisema Eve huku akionekana kuwa na hofu.

Wanaume wale walimwangalia, hawakujibu kitu zaidi ya kumtaka kunyamaza kwani kama angeendelea kuomba kutokuuliwa, basi wangemuua.

***

Wataalamu wanne wa kutengeneza mabomu ya nyuklia walirudiwa katika hali yao ya kawaida na kushangaa kujiona ndani ya nyumba moja huku wakiwa wamefungwa kamba na kuwekwa kwenye viti.

Hawakuwa na nguo zozote zile, miilini mwao kulikuwa na nyaya za umeme ambazo zilipitishwa kwenye swichi zilizokuwa humo ndani.

Hawakujua walikuwa mahali gani, walishangazwa kwani walichokumbuka ni kwamba walikuwa ndani ya nyumba yao ambayo ndiyo walikuwa wakiitumia kwa ajili ya kufanyia mambo yao mengine, kwenye nyumba waliyokuwa kipindi hicho, haikuonekana kuwa sehemu salama hata kidogo.

Wakabaki wakiangalia, ghafla mlango ukafunguliwa na wanaume wawili kuingia ndani. Walishangaa, mmoja walimfahamu, alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakipeleka matunda ndani ya nyumba yao ile.

Walishangaa! Kwa nini walikuwa mahali hapo? Walifanya nini? Kila walichojiuliza walikosa majibu. Walitamani kuzungumza kitu lakini midomo yao iliwekwa gundi, haikufumbuka, hivyo walitakiwa kubaki kama walivyokuwa.

“Karibuni sana! Tunasikitika kwa sababu mmechukua muda mrefu mpaka kurudiwa na fahamu, ila msijali, natumaini kila kitu kitakwenda kama kinavyotakiwa,” alisema Kennedy huku akiwaangalia, wanaume hao walibaki kimya tu.

“Tuna dakika chache sana!” alisema Backnon.

“Usijali! Ngoja tuanze kazi yetu,” alisema Kennedy na kuanza kuwafafanulia kuhusu zile nyaya alizokuwa amewawekea.

Aliwaambia kwamba zilikuwa ni nyaya ambazo zingewapa mateso makubwa mno, zilikuwa na nguvu za kupitisha umeme kwa kiwango cha 150W ambacho kilikuwa kikubwa mno na kingeifanya miili yao kubadilika na kuwa kama mkaa ndani ya kipindi kifupi kabisa.

Yote hayo wangewafanyia kama tu wasingeonyesha ushirikiano wa kile walichokuwa wakikihitaji mahali hapo.

Wataalamu hao walikuwa wakimsikiliza tu, maneno aliyowaambia yaliwatisha na kuona kabisa kulikuwa na hatari kubwa mbele yao.

“Tunahitaji kitu kimoja kutoka kwenu. Nyie ndiyo mliotengeneza formula ya mabomu ya nyuklia, kwa hiyo tunahitaji hiyo formula. Ooh! Samahani kumbe sijatoa gundi, atakayepiga kelele, tutamlipua,” alisema Kennedy huku akiwaangalia.

Akawapa karatasi, alihitaji kujua formula ambayo ilitumika kutengeneza mabomu yale. Kuitoa formula hiyo ilikuwa kazi kubwa, ni siri ambayo kama wangemwambia mtu yeyote yule basi kungekuwa na uwezekano mkubwa wa kumdhoofisha Rais Hamis kitu ambacho hawakutaka kabisa kuona kikitokea.

Walifunguliwa mikono ya kulia na kuambiwa kuandika lakini kila mmoja alionekana kusita kufanya hivyo. Hivyo alichokifanya Backnon ni kuzichukua karatasi zile, akachukua ndoo ya maji na kuwamwagia.

Hawakupenda kabisa ubishi, kwao, kitu walichohitaji kilikuwa ni kufanya kile walichowaambia, hilo lilikuwa kosa, hawakutaka kushindwa hivyo baada ya kuwamwagia maji wakawasha umeme ambao ulikwenda kwenye chombo kilichokuwa na nguvu ya kupunguza na kuongeza halafu kwenda moja kwa moja kwenye miili yao.

Walipigwa shoti, walitetemeka, nywele ziliwasimama. Ulikuwa umeme mwingi hivyo ukapunguzwa kidogo lakini maumivu hayakupungua, kwa jinsi shoti ilivyokuwa ikiwapiga, hata kupiga kelele walishindwa kabisa. Baada ya sekunde thelathini tu, wakazima umeme.

“Huwa ninawapenda wanaume jeuri kama nyie, yaani mnaifanya siku yangu kuwa nzuri kabisa,” alisema Kennedy huku akionyesha tabasamu, yaani kama alifurahia kuona wale watu wakikataa kufanya kile alichotaka wakifanye.

Wataalamu hao wakawa hoi, walijua kabisa walikuwa katika mikono ya watu hatari ambao wangeweza kuwamaliza kama tu wasingefanya kile walichokuwa wakikihitaji mahali hapo.

Walishindwa kuvumilia, umri wao ulikuwa mkubwa, hawakuwa imara kwenda sawa na maumivu yale hivyo wakakubali kuwaambia juu ya hiyo formula waliyokuwa wakiitaka.

Wakaandika kwenye karatasi, zilikuwa ndefu mno, kila mtu na yake kisha kuzichukua karatasi zote nne na kuangalia kama zilikuwa zinafanana, kweli zilikuwa sawa. Wakaridhika kwani kitendo cha kuwapa hizo formula tu ilionyesha wangefanikiwa kwa kile walichohitaji kipindi hicho.

Walipomaliza, wakawaambia hawakuwa na muda, ilikuwa ni lazima waondoke mahali hapo na kuwahakikishia kwamba wangewasiliana na watu ambao wangekuja mahali hapo na kuwafungua.

Wakaondoka! Walipokaribia nje, Kennedy akaitoa sura ya bandia aliyokuwa ameivaa na kuitupa humo kisha yeye kuondoka na Backnon.

“Hakikisha hizo karatasi unazishika wewe,” alisema mwanaume kutoka upande wa pili kutoka Marekani, hawakuwa wakimwamini sana Backnon.

“Sawa. Haina shida!” alisema.




Scott na maofisa wengine wa CIA walikuwa wakifuatilia kila kitu kilichokuwa kikiendelea, kwa Kennedy, mwanaume huyo alionekana kuwa muhimu kupita kawaida. Ilikuwa ni lazima wahakikishe kwamba anaingia nchini Marekani salana kabisa.

Muda ulizidi kwenda, siku ambayo waliwasiliana naye na kumwambia kwamba alikuwa njiani kwenda huko ndipo wakagundua kwamba kulikuwa na simu ambayo alipigiwa Kennedy kutoka nchini Uingereza. Hawakujua walizungumza nini lakini baada ya kuifuatilia sana kwagundua kwamba ilitoka katika Shirika la Kijasusi la MI6.

Mpaka kufikia hapo wakajua kabisa kulikuwa na mchezo. Kitu cha kwanza kabisa ambacho walijiuliza ni namna ambavyo MI6 walipata namba ya simu ya Kennedy, kwenye hilo hawakutaka kujiuliza sana kwani tayari waligundua kwamba Backnon alikuwa akifanya mawasiliano na watu hao hivyo kulikuwa na uhakika kwamba yeye ndiye aliyewapa watu hao namba hiyo.

Scott akaagiza watu hao wafuatiliwe kwani tayari alihisi kulikuwa na jambo kubwa ambalo lilitakiwa kutokea mahali hapo ambalo yeye kama yeye hakutaka kabisa kuona likitokea kwa sababu Kennedy alikuwa na karatasi ambazo zilikuwa muhimu mno.

Baada ya dakika kadhaa akaona akipigiwa simu na Kennedy na mwanaume huyo kuuliza kuhusu familia yake, alihitaji kujua kama ilikuwa salama au la. Hapo akapata kitu kwamba inawezekana kabisa kulikuwa na jambo kubwa lililokuwa likiendelea nyuma ya pazia.

Akawaagiza maofisa waende nyumbani kwake kuiangalia familia hiyo na walipofika huko, kitu ambacho waligundua ni kwamba familia hiyo haikuwepo. Wakampigia simu Scott na kumwambia kile kilichotokea, mwanaume huyo alichanganyikiwa, akahisi labda inawezekana mke wa Kennedy alimchukua mtoto wake na kuelekea kazini, akatuma watu huko, jibu walilolipata ni kwamba mwanamke huyo aliondoka muda mrefu sana.

Hilo likawachanganya kupita kawaida, hapo wakapata jibu kwamba inawezekana kabisa familia ya Kenney ilikuwa kwenye matatizo na ndiyo maana kitu cha kwanza kabisa ambacho mwanaume huyo alihitaji kufahamu ni kuhusu familia yake.

Hapo wakapata jibu kwamba inawezekana kabisa familia ya Kennedy ilitekwa na Waingereza na kumwambia kwamba alitakiwa kuhakikisha anapeleka karatasi hizo nchini humo. Ili kumuaminisha kwamba familia yake haikuwa imetekwa, Scott akazungumza naye na kumwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile, familia yake ilikuwa salama kabisa.

Alijua kulikuwa na kosa kumwambia hivyo lakini hakuwa na jinsi, karatasi zile alizokuwanazo zilikuwa muhimu kwao kuliko kitu chochote kile. Wakati akiwa amemwambia hivyo, aliwaambia maofisa wake wahakikishe familia ya Kennedy inapatikana haraka iwezekanavyo kwani bila hivyo kusingekuwa na uhakika wa kuzipata karatasi hizo.

Maofisa hao wakaondoka kwa lengo la kufanya kazi hiyo lakini pia alimtumia ujumbe Kennedy kwamba alitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anamuua Backnon kwani tayari alionekana kuwa adui wao ambaye hakutakiwa kuishi kabisa.

Kennedy aliwaambia ugumu wa kufanya hivyo ila walitakiwa kumtumia mtu mwingine kabisa kwa ajili ya kufanya kazi hiyo. Kwa Scott hakukuwa na tatizo, Wamarekani walijipanga, kwenye kila ndege ambayo ilikuwa ikikanyaga ardhi ya Marekani ilikuwa na mhudumu ambaye aliwekwa na CIA, hiyo ilitokana na shambulio la kigaidi ambalo lilitokea Septemba 11/2001.

Kennedy akawaambia kabisa kwamba kwa mazingira yaliyokuwepo ndani ya ndege lingekuwa suala gumu kufanya hivyo, walitakiwa kumtuma mtu ambaye alikuwa ndani ya ndege hiyo kama mhudumu kwa ajili ya kumuua mwanaume huyo.

Wakati akiwasiliana na Scott, Backnon alijifanya amelala lakini muda mwingi alikuwa akimfuatilia Kennedy kwa kujaribu kuangalia simu yake lakini alishindwa kabisa kuyaona mazungumzo yao. Alijua kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea na ilikuwa ni lazima afanye kitu chochote kile, wakitua Marekani tu akimbie zake na kutokomea kusipojulikana.

Huo ndiyo ulikuwa mpango wake lakini kwa upande wa Kennedy, tayari alikuwa na wasiwasi kwamba familia yake haikuwa salama kama alivyokuwa ameambiwa. Alihisi kabisa kulikuwa na tatizo mahali fulani na bosi wake, Scott hakutaka kumwambia ukweli.

Kilichomjia kichwani mwake ni kuondoka na kuelekea nchini Uingereza kama tu angegundua kwamba familia yake haikuwa salama kama alivyokuwa ameambiwa. Haraka sana akakata tiketi kwenye mtandao wakati ndege ikiwa imetulia angani ikiendelea na safari zake, katika anga ambayo waliruhusiwa kutumia huduma ya internet ndani ya ndege hiyo.

Akapata tiketi ya ndege ambayo ilikuwa ikiondoka ndani ya dakika saa moja na nusu baada ya ndege hiyo kutua nchini Marekani. Akawa nayo kwenye barua pepe yake na kitu pekee alichokuwa akikisikilizia ni kwa ndege hiyo kutua nchini Marekani na kuondoka zake kurudi nchini Uingereza.

Baada ya nusu saa, mhudumu mmoja wa kike akawasogelea pale walipokuwa huku akiwa na vinywaji kwenye chombo chake na kumuuliza Kennedy alikuwa akitumia kinywaji gani. Akasema hatumii chochote kile, akamuuliza Backnon ambaye alikuwa wa kwanza kabisa kwenye kiti kile cha watu wawili na yeye kusema kwamba hatumii chochote.

“Sawa,” alisema msichana huyo na kuanza kuondoka, alipoona amesimama pembeni ya Backnon kwa nyuma, akachukua sindano aliyokuwa nayo na kwa haraka sana kumchoma mwanaume huyo shingoni kwa nyuma.

Backnon akashindwa hata kupiga kelele, alishtuka tu na hapohapo usingizi mzito kumpata. Kennedy hakushtuka, alijua kilichokuwa kikiendelea, hivyo akatulia lakini akiwa makini kabisa kuhakikisha kwamba mchezo kama ule hauchezwi kwake hata kidogo.

Ndege iliendelea na safari, aliona kabisa kwamba kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kuhusu familia yake hivyo ilikuwa ni lazima afanye kila liwezekanalo kuhakikisha anaiokoa familia hiyo popote pale ilipokuwa.

Wakati safari hiyo ikiendelea ndipo akakumbuka kwamba ni lazima afanye kitu kimoja kwa ajili ya kuondoka salama katika ndege hiyo kwani kwa jinsi hali ilivyokuwa, alihisi kabisa uwanja wa ndege kungekuwa na maofisa wa CIA ambao walikuwa wakimsubiri, wamchukue na kuelekea naye ofisini kwa ajili ya kuwakabidhi karatasi zilizokuwa na formula hiyo.

“Ni lazima nifanye kitu,” alisema Kennedy.

Hicho ndicho alichokifikiria, hakutaka kuona akishikiliwa na kupelekwa makao makuu na kukabidhi formula ile na wakati hakujua kuhusu familia yake.

Haraka sana akafungua begi lake dogo na kuchukua koti kubwa na kulivaa ambalo lilikwenda mpaka karibu na magoti yake, akaondoka na kuelekea chooni, huko ilikuwa ni lazima apange mipango mipya kuhakikisha hakuna mtu anayemshtukia kwa lolote lile. Kule chooni, akaufungua mlango kidogo na kuangalia upande mwingine, aliuona mlango ambao uliandikwa ‘Staff’ akajua tu humo kulikuwa na nini.

Akatoka chooni huku akiangalia huku na kule, akaufungua mlango huo na kuangalia ndani. Akakutana na nguo nyingi za wahudumu pamoja na za marubani. Kwa pembeni kabisa kulikuwa na sehemu ambayo ilitengwa kwa ajili ya mizigo ya abiria.

Haraka sana akaanza kuzifuata nguo za marubani, alipokaribia mahali zilipo, akamuona msichana mmoja akiendelea kupanga nguo nyingine, kwa kuwa hakuwa ameonekana na msichana yule alimpa mgongo, akamsogelea, alipomfikia, akamkaba kwa nyuma, si kwa lengo la kumuua bali kumzimisha kwa muda.

Ni ndani ya sekunde chache tu msichana huyo akatulia na kumuweka chini. Akachukua vazi moja la rubani, akalivaa, kwa juu akavaa na koti lake kama kulificha na kisha kutoka ndani ya chumba kile huku akiwa ameishika kofia yake kwa kificho.

Alifanikiwa, hakuonekana, alitulia kwenye kiti na wakati huo ndege iliondoka nchini Canada na kuelekea Marekani baada ya kumaliza kuvuka katika Bahari ya Atlantiki.

Baada ya nusu saa, wakaambiwa wafunge mikanda, haraka sana akafanya hivyo na ndege kuanza kutua. Iliposimama, abiria wakaanza kuteremka, hakutaka kuwa na presha, akatoka na kurudi chooni, humo alisubiri kwa dakika kadhaa, alipohakikisha kwamba abiria wote wametoka, akavua koti lake, akabaki na mavazi ya rubani, akavaa kofia na kuanza kuteremka.

Kwa kumwangalia ilikuwa ni vigumu kugundua kama hakuwa rubani, alifanana vya kutosha, alikuwa akitembea kwa mwendo wa kawaida na kwenda kwenye mlango maalumu na kupita.

Maofisa kadhaa wa CIA walikuwa hapo, walimwangalia kila abiria aliyekuwa akiteremka, ilikuwa ni lazima wamchukue Kennedy na kuondoka naye mahali hapo lakini kitu cha ajabu kabisa mpaka abiria wanamalizika, mwanaume huyo hakuonekana.

“Vipi?” aliuliza Scott kwenye simu, alikuwa akimuuliza Kennedy.

“Hayupo!”

“Hayupo? Unamaanisha nini kusema hayupo?” aliuliza huku akiwa amechanganyikiwa.

“Yaani hatujamuona!”

“Hamjamuona? Kivipi?”

Kila swali alilouliza na kupewa jibu, aliibuka na swali jingine. Kile alichoambiwa hakukiamini kabisa, alichojua ni kwamba Kennedy alitoka Dubai akiwa amepanda ndege hiyo baada ya kubadilishwa, sasa ilikuwaje mwanaume huyo asiwepo.

Akahitaji kupata taarifa kutoka ndani ya ndege. Akaambiwa kwamba kulikuwa na tatizo, kuna mwanaume ambaye alichukuliwa na kukabidhiwa kwao, alikuwa Backnon lakini pia kulikuwa na jingine.

“Lipi?”

“Kuna mtu alivamia kwenye chumba cha nguo na kumzimisha mhudumu kwa muda,” alisema mwanaume huyo.

“Huyo ni Kennedy,” alisema Scott huku akishusha pumzi ndefu.

Wakafuatilia na kugundua kwamba kulikuwa na nguo za rubani zilikosekana humo, ilipotea katika mazingira ya kutatanisha lakini wakajua kabisa kwamba ni Kennedy ndiye ambaye alihusika kuzichukua nguo hizo.

Wakaondoka hapo na kuelekea katika chumba kimoja kwa lengo la kuangalia kwenye kamera ndogo za CCTV ili kuona kilichotokea. Huko, wakamuona Kennedy akitoka kwa kupitia mlango wa marubani, hakuonekana kuwa na hofu, alijiamini na alitembea kwa kujiamini kana kwamba alikuwa rubani kweli.

Mpaka kufikia hapo wakakubaliana kwamba walimkosa hivyo ilikuwa ni lazima wafanye kila liwezekanalo kuhakikisha anapatikana kwa sababu mtu huyo alikuwa muhimu mno.

Tayari maofisa wengine wa CIA walikuwa nyumbani kwake, waliizunguka kwa mbali kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kuonekana. Walikuwa wakimsubiria Kennedy ambaye waliamini ni lazima afike humo kwa lengo la kuangalia kama kulikuwa na familia yake ndani ya nyumba.

“Tuvamie?” aliuliza mwanaume mmoja.

“Hapana! Subirini mpaka atakapokuja,” alisikika Scott kutoka upande wa pili.

“Sawa. Tunasubiri! Tutakupa taarifa!” alisema mwanaume huyo huku kila mmoja akiwa na uhakika kwamba ni lazima Kennedy angefika nyumbani hapo kwa lengo la kuhakikisha kama familia yake ilikuwa humo kwani kila alipokuwa akimpigia simu mke wake, hakuwa akipatikana.




TAMATI




0 comments:

Post a Comment

Blog