Search This Blog

Sunday, July 24, 2022

MSAKO WA MANGE KIMAMBI

  

MTUNZI: ZULFA HUSSEIN



“Uko wapi?”

“Magomeni.”

“Unafanya nini?”

“Niko ndani ya gari…kwenye foleni.”

“Mambo yameharibika huku.”

“Kivipi?”

“Kirusi kimekwishaingilia mafaili.”

“Sijakuelewa.”

“Ingia Instagram kwa Mange Kimambi” sauti ya mwanamke upande wa pili alisema kisha akakata simu. Alikuwa ni mke wa waziri. Scora Mtinika.

Stanley Massawe, mwanaume mfupi, mweusi, mwenye kitambi kilichotokana na ulaji wa kuku wa kienyeji, sanjari na bia mbili tatu za afya, alikuwa amekamata simu ile, kama vile ndio mara ya kwanza kukitia mkononi kifaa kile cha mawasiliano.

Alikuwa amebung’aa huku akihisi mapigo ya moyo yakimwenda kasi kuliko kawaida, ingawa ndani ya gari lake dogo, alikuwa amefungulia kiyoyozi, (Air Condition) jasho lilimchuruzika maungoni mwake kwa kasi kiasi cha kulowanisha shati lake la kijani alilokuwa amevaa na kuacha baka kubwa eneo la kwapani.

Sauti ya mtu aliyezungumza naye kwenye simu ilikuwa ikijirudia kichwani mwake.

“Kirusi kimekwisha ingilia mafaili….. Ingia instagram kwa Mange Kimambi” alikumbuka maneno yale.

Moyo ukawa unampwita kwa nguvu. Alimfahamu vema mwanamke yule, mwanaharakati anayetumia akaunti yake ya ‘Instagram’ kuibua mambo mazito ya wanasiasa, wafanya biashara, wasaniii, na watu mbalimbali mashuuri.

“Kaandika nini huyu kahaba” alinong’ona taratibu huku akiingia mtandaoni kuona kile kilichoandikwa na Mange Kimambi.

“Piii..piiii…piii..” sauti za honi za magari zilisikika nyuma ya gari lake.

Kabla hajanza kuperuzi alistushwa na honi zile. Askari aliyekuwa akiongoza magari alikuwa ameita magari ya upande wake.

Akasitisha kwa muda zoezi la kuangalia kile kilichokuwa kimeandikwa na mwanamke yule aishiye nchini Marekani.

Aliliondoa gari kwa kasi, akavuka mataa ya Magomeni, akaanyooka na njia ya Kinondoni, alipofika pale Magomeni Kanisani, alikata kushoto akashika barabara ya Tandale Uzuri.

Mita kama miamoja akaingia kwenye kinjia kilichochepuka, upande wa kulia ambapo kuna makaburi ambayo yapo mkabala na gereji bubu ya magari.

Akapaki gari lile aina ya Toyota Harrier ukingoni mwa ukuta wa makabauri. Akatizama mbele na nyuma kupitia kioo cha nyuma akaona hayupo katika njia ambayo angeweza kusababisha lapsha za hapa na pale.

Alinyakua simu ile aliyokuwa ameitelekeza kwenye dashboard, kisha akabofyabofya, punde akawa anaupitia ukurasa wa Mange Kimambi.

Hazikuzidi sekunde tatu kabla ya kuona habari. ambayo sio tu ilimstua lakini pia, ilimwogopesha.

“Mungu wangu!!!” alihamaki.

Macho yalimtoka kama mtu aliyefumaniwa akizini na mke wa mtu chumbani kwa mume. Alikuwa hapumui sawasawa kutokana na uzito wa habari ile ambayo ilipostiwa na mwanamke yule.

Akarudia tena kutizama habari ile, akaona kwa siku hiyo stori hiyo ilikuwa imepata ‘views’ ‘like’ na ‘Coments’ nyingi kuliko habari yoyote.

Habari iliyopostiwa na Mange ilimwonyesha yeye akiwa na mwanamke mmoja aitwaye Scora. Mke wa Waziri Hussein Mtinika. Wakiwa kama walivyozaliwa, ndani ya chumba cha Hotel moja ya kisasa huko Pemba visiwani Zanzibar.

Picha ile ya video iliwaonyesha wakiwa wametoka kuvunja amri ya sita, huku wakiwa katika mahaba mazito na mwanamke huyo wa Kigogo.

Katika video hiyo, Mange Kimambi alikuwa akimsifia kwa kejeli Stanley kwa kutembea na mke wa Waziri yule ambaye kwakwe, alikuwa ni kiongozi asiye na huruma na maisha ya watu.

“Hakika wewe ni mwanaume wa shoka, umeweza kumsuuza mke wa Waziri Hussein Mtinika….sema pamoja na yote, umeniangusha..unakibamia!! sidhani kama ulimsuuza vizuri!!” ujumbe ule ulisomeka hivyo.

“Nimekwisha!!...nasema nimekwisha mimi!!” Stanley alipayuka huku machozi yakimchurika.

Jambo lile lilikuwa ni zito mno maishani mwake. Kamasi lilimtoka, jasho jingi zaidi ya lile la awali lilimchuruzika. Wasiwasi ulikuwa umtenda moyoni mwake.

Kamwe hakutegemea kama tukio lile alilolifanya miaka saba iliyopita, ambalo alimini siri ile kamwe isingejulikana kwakuwa hapakuwa na yeyote aliyekuwa akifahamu uhusiano wake na mke yule wa waziri zaidi ya wao wawili.

“Sasa nani amevujisha siri hii kwa hiki kirusi cha Instagram??” Stanley alinon’gona.

Akiwa bado katika taharuki, simu yake iliiita, alipoangalia kwenye kioo cha simu ile akaona mpigaji ni Scora Mtinika, mke wa waziri.



Akasita kuipokea simu ile akawa akaitizama kama vile ndani ya kifaa kile kulitegeshwa bomu, simu iliendeleakuita kiganjani mwake.

Akakata shauri akabofya kitufe cha kupokelea nakuweka simu sikioni.

“Hallow” sauti nyembamba ilisikika

“Nakusikia”

“Umeona ?” scola, mke wa waziri mtinika alimuuliza.

“Nani ametufanyia huu unyama?”

“Sijui” scola alijibu.

Stanley akapiga kimya huku simu ikiwa bado ipo sikioni. Kisha akauliza kwa kwa sauti ya unyonge.

“Tunaweza kuonana?”

“Nini!!” Scola akahamaka kwa mshangao

“Tunaweza kuonana?” Stanley akauliza tena.

“Ili?”

“Tulizungumze hili”

“Hapana stanley, naogopa”

“Maji yamekwisha mwagika hatuna budi kuyaoga, Unapoendelea kuishi katika hofu ndivyo unayoikaribisha zaidi hatari maishani mwako” Alisema Stanley.

ukimya mwingine ukapita, kisha scola akazungumza simuni kwa sauti ya unyonge.

“Hatuwezi kuzungumzia kwenye simu?”

“Lakini kwanini hutaki tuonane?”

“Hebu kuwa mwelewa Stanley, kila kona sasa hivi wanazungumza jambo hili, kitendo cha kuonekana tukiandamana pamoja mtaani ni kuzidi kudhihirisha kile kinacho sambaa mtandaoni.

“Hufikirii ni hatua gani atachukua mume wangu dhidi yetu? Huna hofu kabisa na jambo hili Stanley, usisahau kabisa kwamba mimi ni mke wa waziri, na usijifanye hujui kwamba jambo hili limemdhalilisha mume wangu kwa kiwango kikubwa sana, na usidhani kwamba atalipuuza tu kama mwendawazimu, mimi na wewe kuanzia wakati huu hakuna ambaye yupo salama”

Scola alisema, Stanley alishusha pumzi ndefu, kwa mara nyingine alihisi tumbo likipata joto, hofu kubwa ikamvaa, alitamani ardhi ipasuke atumbukie ndani yake. Maneno ya Scola yalimwingia sawia mvulana yule chakalamu.

“Sasa naomba unisikilize kwa makini” Stanley alimwambia.

“Nakusikiliza” Scola akajibu.

“Waandishi wa habari wamekwisha kupigia kukuliza juu ya jambo hili.?” Stanley akamuuliza.

“Wamenipigia sana, lakini hadi sasa sijapokea simu yoyote, na sijaongea na mtu yeyote”

‘Vizuri sana, sasa unachotakiwa kufanya ni kulikanusha jambo hili kwa nguvu zote, likanushe kwa waandishi wa habari na kwenye akaunti zako mbalimbali za miotandaoni” Stanley alisema.

“Nitasema nini sasa wakati video iko wazi ikinionyesha mimi na wewe tukifanya uchafu ule”

“Unatakiwa useme picha hizo za video zimetengenezwa, shikilia msimamo huo,” stanley alisisitiza.

Ukimya mwingine ukapita baina yao, hatimaye scola akatikia kwa sauti ya taratibu:

“Sawa, nitafanya hivyo”

“Vizuri, hata mimi huo ndio utakuwa msimamo wangu, nitakukana popote pale niendapo”

Wakakubaliana hivyo.

Masaa machache badaye tukio la kuvuja kwa video ya Scola mke wa waziri na Stanley wakiwa katika mahaba motomoto ilikuwa gumzo nchi nzima.

Kila kona mada kuu ilikuwa ni kitendo hicho, vituo vya redio na runinga viliripoti jambo lile kadiri walivyoweza.

Mke wa waziri Mtinika, Scola mtinika alipopigiwa simu kutoa ufafanuzi juu ya ile sintofahamu alikana Kwa nguvu zote huku akiliweka tukio hilo katika muktadha wa kisiasa.


“Hizi ni hila anazofanyiwa mume wangu na maadui zake wa kisiasa kwa kunitumia mimi, kwakweli siwezi kukubali jambo hili linichafue kwa kiwango hiki, nimekwisha ongea na mwansheria wangu kwa ajili ya kupeleka jambo hili mahakamani. Na nina wahakikishia mange kimambi nitamtia adabu” Scola alijitetea mbele ya waandishi wa habari.

“lakini video inaonesha ni wewe, ukweli wa jambo hili ukoje?” mwandishi mmoja akauliza.

“Niwajibu mara ngapi kwamba hii ni hila ya mange kimambi, video hiyo ni ya kutengeneza, mtu ninaye husishwa naye simjui, na ifahamike mimi ni mke wa kiongozi mkubwa, kamwe siwezi kufanya uchafu wa kiwango hiki.” mwanake yule alizidi kujitetea.

Kwa upande wa waziri mtinika ambaye alikuwa ziarani nchini Marekani, alipotafutwa na waandishi wa habari kwa njia ya simu ajabu simu yake ilikuwa haipatikani, hata Scola, mke wa waziri huyo naye alipojaribu kumtafuta mumewe ili amweleweshe juu ya bomu lililolipuliwa na Mange Kimambi, hakumpata simuni.

“Mungu wangu nini kimempata mume wangu, kwanini hapatikani na siyo kawaida?” Scola alijiuliza kimoyomoyo.

Ndani ya muda huohuo mara simu yake ya mkonoi ilianza kuita, alipocheki kwenye kio cha simu akaona namba ya Stanely, moyo wake ukamdunda maana walikwisha kubaliana kutotafutana.

Simu iliita hadi ikakatika, mpigaji akapiga tena, mwisho alikata shauri akaona acha apokee:

“Hellow” alisema baada ya kupokea simu

“umeona kitu kingine alichoposti hiki kirusi”

“Kirusi gani?”

“Si Mange Kimambi”

“Kaposta nini tena?”

“ingia uangalie, alichoposti safari hii ni kibaya kuliko alichopost awali”

“Mungu wangu!!” Scola aliogopa.



Alikata simu, upesi akaingia katika mtandao wa Instagram, moja kwa moja akafungua katika akaunti ya Mange Kimambi.

Alichokiona alijikuta akipiga kelele kama mwendawazimu.

“Khaaa! Nini hiki!!” alibweka mithili ya jibwa koko lilonusurika kumezwa na chatu, jambo aliloliona lilikuwa zito mno.

Kwenye ukurasa ule wa Mange Kimambi , mwanamke yule aishiye Malekani kwa mara nyingine alikuwa ameweka ‘post’ inayomwonyesha yeye, akiwa na Stanley chumbani, huku wakizungumza juu ya mimba aliyopewa na mwanaume huyo namna anavyotakiwa kuficha siri hiyo na mtoto huyo kumbambikia Mheshimiwa Waziri Hassan Mtinika.

Post ile ilisomeka hivi:

“Jomon leo nataka niweke kila kitu wazi kuhusu huyu waziri mpuuzi, ambaye kazi yake ni kuwaonea wanyonge na kujiona yeye ndiye Mungu mtu hapa duniani, unaambiwa jamaa kabambikiwa watoto. Yanii hili jinga kama zoba vile.

“Cheki hii ni vedeo inayoonyesha jamaa aliyepiga mimba mkewe wakiwa hotelini na mchepuko wake, wakipanga namna ya kulibambikia mimba hili kubwa jinga”

Post ilimalizika kusomeka hivyo huku ikiwa imeambatana na picha za video na sauti ambazo zilikuwa zimepigwa kwa siri.

“Nimekwisha!!!” Scola Mtinika alibwata, alikuwa amechanganyikiwa vibaya sana.

Siri aliyoitunza kwa miaka kumi iliyopita, kwanza kuchepuka na mwanaume mwingine pili, siri ya kuzaa na mchepuko kisha akabebeshwa mimba na mtoto kumbambikia mumewe, sasa jambo lile ilikuwa wazi.

Alitamani ardhi ipasuke utumbukie ndani yake, alihisi kama anaelea angani akiwa hana pa kujishikiza, akili ilimzunguka, kizunguzungu kilikuwa kikimnyemelea kwa kasi kubwa.

“Mange kwanini unanitendea haya, nimekukosea nini Mange eeh!!” alisema peke yake, machozi yakimtoka.

Alimfikiria mtoto wake Rolland ambaye alizaa na hawara yake wa miaka mingi Stanley kabla ya kumbambikia mimba mumewe, alishia kusikitika, alijiona yupo uchi katikati ya halaiki kubwa ya watu.

Aliujua fika ukatili wa mumewe, alifikiria endapo mumewe ataamua kwenda kupima DNA na mtoto yule ambaye alimbambikia, kisha akabaini kuwa kiumbe yule si wake, aliona siku zake za kuishi yeye na mtoto wake zilikuwa zikihesabika.

“ Nifanye nini!” aliwaza, maji yalikuwa yamekwisha mfikia shingoni.

Alitumia dakika 5 tu kuwaza, kisha akawa amepata jibu. kitu pekee alichoona ni nusura kwake ni kuikimbia yeye na mwanaye.

Tatizo likawa ni moja tu. Wapi akimbilie? ambapo mkono wa mumewe hautaweza kumfikia. Alifkiria kwa kina mwisho akabaini sehemu pekee ambayo anaweza kuwa salama ni kukimbilia nchini kongo.

Alifikiria nchi ya Kongo kwa kuwa aliamini mumewe asingeweza kufikiria kuwa alikimbilia katika taifa hilo ambalo kwa wakati huo ilikuwa katika vita kali ya serikali na waandamanaji wanaotaka rais wan chi hiyo kung’atuka madarakani.


Alichofanya ni kuchukua kila akitu alichoona kitamsadia mbele ya safari, akaelekea katika shule ambayo mtoto wake Rolland alikuwa akisoma na kuishi bweni.

Baada ya kufika, alimwombea ruhusa kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo, haikuwa tatizo kupata ruhusa, muda mfupi uliofuata Scola na mwanaye Rolland walikuwa ndani ya gari la kifahari la mwanamke yule wakiliacha jiji la Dar es salam.

“Mama tunakwenda wapi?” Rolland aliuliza.

“Tunakwenda kwa bibi Kigoma” Scola alimdanganya, asingeweza kumwambia mtoto yule mdogo mambo yaliyokuwa yamemsimbu.

“Kufanya nini?” mtoto akaendelea kuuliza.

“Tukifika utajua, usiulize maswali mengi Rolland”

“Lakini huu sio wakati wa likizo mama?”

Hata hivyo Scola hakumjali, aliendelea kukanyaga mafuta na kuliacha kabisa jiji la Dar.

“Nkrii! Nkrii! Nkrii!!!” simu ya Scola iliita kwa nguvu.

Alipungaza spidi ya gari akaitizama simu simu iliyokuwa kando, macho yake yalipotua kwenye kioo cha simu ile hakuamini macho yake..

Mtu aliyekuwa akimpigia alikuwa ni Stanley Massawe, tumbo lilimkata, kila alipoona simu ya mwanaume yule kulikuwa na bomu jingine lililolipuka.


Akafikiria kama anatakiwa kupokea simu ile mwisho akaona kwakuwa amekwisha chukua maamuzi ni kheri kutotizama nyuma. Akaacha kupokea simu ile.

Hata hivyo, hazikupita dakika nyingi baada ya simu ile kukatika, mara simu nyiingine ikaingia, alipoangalia, akaona mpigaji ni mumewe!! Mheshimiwa waziri, Hassan Mtinika.

TOBA!!



“Nkrii! Nkrii! Nkrii!!!” simu ya Scola iliita kwa nguvu.

Alipungaza spidi ya gari akaitizama simu simu iliyokuwa kando, macho yake yalipotua kwenye kioo cha simu ile hakuamini macho yake..

Mtu aliyekuwa akimpigia alikuwa ni Stanley Massawe, tumbo lilimkata, kila alipoona simu ya mwanaume yule kulikuwa na bomu jingine lililolipuka.

Akafikiria kama anatakiwa kupokea simu ile mwisho akaona kwakuwa amekwisha chukua maamuzi ni kheri kutotizama nyuma. Akaacha kupokea simu ile.

Hata hivyo, hazikupita dakika nyingi baada ya simu ile kukatika, mara simu nyiingine ikaingia, alipoangalia, akaona mpigaji ni mumewe!! Mheshimiwa waziri, Hassan Mtinika.

TOBA!!


Endelea nayo…


Scola akawa njia panda, hakujua achukue maamuzi gani, apokee simu ya mumewe, ama achane nayo. Kadhalika akaendelea kuijiuliza, kwa nini tangu kuibuka kwa lile songombingo mume alikuwa hapatikani? Wakati huu ambapo anatorka ndipo mwanaume huyo anapompigia simu?

Swali kuu likawa, je mumewe amekwisha baini kila kitu juu ya kuwa alikuwa akitoroka na Rolland, ama laa?

Simu iliendelea kuita kwa nguvu hadi ikakatika, pamoja na kwamba gari lile lilikuwa limefunguliwa mashine za kupoza joto, lakini mwili wa Scola ulindelea kutokwa na jasho kiasi cha kulowanisha shati na kuacha baka kubwa.

Haukupita muda mwingi mara simu ile ilianza kuita tena, mpigaji akiwa ni mumewe, baada a kutafakari kwa kina mwisho akaamua kuipokea ile simu.

“He…llow” alisema kwa kitetemeshi

“Uko wapi?” sauti nzito iliyojaa kisirani ilisikika upande wa pili, alikuwa ni Muheshimiwa waziri, Hassani Mtinika.

“Sa..sa…Sasa…. Hivi?” Scola naye akamuuliza kwa kitetemeshi.

“Uko wapi?” sauti ya amri ikasika tena, safari hii sauti ile ikiwa ya kutisha zaidi ya awali.

“Nakwenda,…nakwenda.., nipo Kariakoo” mwanamke yule alitoa majibu ya uongo huku akiwa mwingi wa hofu.

“Unafanya nini?’

“Nimekuja tu mara moja”

“Una uhakika?”

“Ndio”

“Rolland mpo naye?” waziri yule aliendelea kumuuliza maswali ya mtego mwanamke yule.

“Ndio”

“Kwanini umekwenda kumchukua shule wakati si muda wa likizo?” swali lile likamfanya Scola ajawe na mate mepesi mdomoni.

Akajikuta anaikata simu ile na kuizima. Mambo yalikuwa yamekwisha haribika, alikwisha tambua mumewe alikwishatambua kila kitu juu ya nyendo zake.

Aliikumbuka ile namba mabayo mume alimpigia akabainiilikuwa ni namba ya Tanzania.

“Inamaana maana kisha rujea nchini” alinong’oa.


Hata hivyo ndani ya muda umfupi uliofuatia aliliona Gari jeusi aina ya Nissan likija kwa kasi ya kimbunga nyuma yake.

Gari lile lilimpita kwa kasi kisha likaenda kama mita 200 na kusimama katikati ya barabara.

Watu wawili wenye bastola walishuka ndani ya gari lile na kulipungia mkono gari la Scola kumtaka asimame.

Lilikuwa ni shambulio baya mno kwa Scola, alitambua fika mambo yamekwisha haribika, na alikuwa kwenye vita kubwa kati yake na mumewe.

Aliogopa sana, hakutaka kabisa kupingia mikononi mwa wale watu wawili waliomsimamisha mbele yake, alipofikira suala la kutotii kusimama, aliona dalili za kifo aidha yeye ama mwanaye kutoka kwa wale wavamazi zipo waziwazi.

Alikanyaga breki na kusimamisha gari, wale wavamizi wakalizunguka gari na kuwataka wateremke yeye na mwanaye.

Rolland alianza kulia, hakuna alichojua kwa wakati huo, kila kitu kwakwe ilikuwa ni ‘suprize’

“shukeni wote kabla hatujamwaga damu ya mtu” jamaa alisema kwa ukali.

“Fanya haraka we Malaya” mtu wa pili alifoka alipoona Scola anababaika kushuka.

“Kuna nini jamani mbona hivyo?” Scola aliuliza

“usituulize maswali ya kipuuzi, utakwenda kujua tukifika Dar”

Scola hakuwa na la kufanya, watekaji wale, walichofanya ni kumfunga kamba mwanamke yule, pamoja na mwanaye, kisha wakawaweka katika siti za nyuma za gari lilelile, jamaa mmoja akaketi kwa dereva huku mwingine akiweka ulinzi upande wa Scola na mwanaye Rolland.

Hapo Scola akatambua watu wale hawakuwa wawili tu, bali zaidi ya wawili, maana pindi walipoanza safari ya kurudi Dar, ile Nissan waliyokuja nayo wale jamaa nayo iliunga tela kwa nyuma, hilo likamfanya atambue kuwa wavamizi wale walikuwa na wenzao walikuwa wamebakia kwenye lile gari dogo.

Safari ya Dar ilipoanza, Scola aliona ule ndio ulikuwa mwisho wa maisha yake, aliamini pasina shaka kwamba mambo yale yalikuwa yakiratibiwa na mumewe. Lakini pia hakutaka kabisa kujidanganya kwamba mambo yale hayakuwa ni matokeo ya post za Mange Kimambi kufumua siri zake za maisha ya nyuma.

Alianza kusali sala zake za mwisho, kwani alitambua kivyovyote mumewe asingeweza kumwacha hai endapo angethibistha ukweli wa mambo yote yaliyosewa dhidi yake.

Kumsaliti na kumbambikia mtoto ilikuwa jambo baya ambalo linachukiwa na wanaume kwa kiwango cha mwisho.


Mange kwa nini umenipa dhabu hii, kwa nini huku post watu wenye wenye matatizo ya umeme hadi ufumue siri hii” Scola alilalama kimoyomoyo.

Alianza kusali sala zake za mwisho, hakuamini kabisa kama wale watekaji, watu wasiojulikana wanaweza kumwacha salama.

“Mange Kimambi umenikomesha” aliongea peke yake kama mwendawazimu




Safari yao ilishia katika nyumba moja pweke maeneo ya Mbezi beach, magari yale mawili yaliingia ndani ya ngome ya nyumba ile kisha geti likafungwa.

Scola na mwanaye walishushwa na kuingizwa kwenye moja ya vyumba vilivyokuwa ndani ya jumba lile. Wakati wote Rolland alikuwa akilia, kutokana na umri wake mdogo hakujua kwa nini mambo yale yanamtokea maishani.

Scola alijisikia vibaya sana kila alipoona kilio cha mwanaye, hakupenda kabisa kuona mtoto huyo anakufa, kama makosa alikuwa ameyafanya yeye, aliona mtoto wake kuunganishwa katika dhambi alizotenda yeye ilikuwa ni jambo lisilokubalika nafsini mwake.

“Ulikuwa unakwenda wapi ?” mtu mmoja alimuuliza kwa ukali.

“Nyie ni akina nani na kwa nini mnaniuliza maswali hayo?” Scola alijibu kwa ukali huku machozi yakimtoka na kutengeneza mifereji mashavuni mwake.

“Unajitia ujeuri we kahaba?”mtu yule alimwambia, akamsogelea na kuanza kumshushia kipigo cha nguvu.

Dakika moja badaye mwili wa Scola ulikuwa umechafuka kwa damu, majeraha ya kipigo yalitapakaa mwilini mwake.

Scola alitambua mambo yote yale yalifanywa kwa maagizo kutoka kwa mumewe, Mange Kimambi alikuwa ameleta balaa kubwa maishani mwake.

*****

Wakati mambo hayo yakiendelea kwa Scola mtinika, mke wa mheshimiwa waziri, upande wa pili, Stanley Ngonizi, mwanaume wa kisasa, ambaye mavazi na mwonekano wake ungeweza kudhani ni moja ya wasanii mashuhuri, kwa upande wake alikuwa ameamua kuchukua maamuzi ya kukabaliana na songombingo lile kwa staili ya aina yake.

Hakuwahi kutegemea kama siku moja angeingia kwenye 18 za Mange kimambi na siri zake nzito kuanikwa hadharani, siri ambayo siku zote aliamini kama ingekuwa hadhani, basi ingeweza kuharibu kabisa maisha yake.

Kitendo cha kutembea na mke wa kigogo wa serikalini na kumpa mimba kisha mtoto yule akabambikiwa yule kigogo ilikuwa ni jambo ambalo lilikuwa limeyaweka maisha yake kitanzini.

Kutokana na unyeti wa siri ya kuwa na ahusiano wa kimapenzi na mke wa waziri, hakutegemea kabisa jambo lile kufumuliwa kirahisi. Alihisi huenda kulikuwa na mambo ya kishirikina yaliyokuwa yakitokea, akili yake ilikuwa haikubaliani kwamba palikuwa na mtu wa tatu aliyekuwa akitambua siri ile zaidi ya Scola.

Na hakuamini kabisa kama Scola angeweza kutoboa siri ile kwa mtu mwingine kutokana na hatari ya jambo lenyewe.

Nafsi yake iliendelea kukiri wazi kwamba Mange Kimambi alikuwa akijihusisha na nguvu za giza. Uchawi.

Licha ya kuwahi kuwa shabiki wa mwanamke yule, ambaye anaungwa mkono na mamilioni ya Watanzania yeye akiwa miongoni mwao. Kwa wakati huu alikuwa akionja shubiri ya mwanaharakati yule.

“Kivyovyote huyu Mange ni mwanga, lazima atakuwa mchawi huyu…” alinong’ona

“Kajuaje jambo hili? Nani kamwambia kama sio uchawi tu!” mawazo ya kihayawani yaliendelea kujengeka kichwani mwake.

“ Sasa nitamfunindisha adabu, analeta uchawi kwangu, hajui kama na mimi sijaribiwi kwenye anga hizi” Stanley aliongea peke yake ndani ya gari.

Alikuwa akiendesha kuelekea Bagamoyo kwa mganga wa kienyeji, alidhamiria kupambana na Mange Kimambi kwa nguvu zake zote.

“Ama zake, ama zangu” akawa ananong’ona kwa morali kubwa.

“Mzee Omary Muhaji, kazi hii ataiweza vizuri tu, kama anatumia uchawi kwangu amegonga mwamba” aliendelea kuwaza, uso wake ulikuwa umemzodoka vibaya sana.

Alipowasili Bagamoyo, alielekea mtaa uitwao Nasa, ambapo kulikuwa na nyumba nyingi za kizamani, hapo ndipo yalipokuwa makazi ya mganga Kiboko aliyesifika sana katika wilaya ile ya kitalii. Bagamoyo.

Baada ya kuwasili kwa mzee huyo mwembamba mwenye mvi nyingi kichwani, alimsimulia kila kitu kilichotokea.

“Pole sana” mganga Muhaji alimpa pole.

“Nishapoa babu”

“Huyo mange kimambi nimepata kesi zake nyingi sana”

“Kweli ndio?”

“Ndio. Watu wengi wamekwisha fika kwangu kutaka nimkomeshe”

“Sasa kwa nini hujamkomesha hadi sasa?”

“Wote waliofika hapa, Mange hawagusi tena,”

“Mimi nataka umtie kichaa, ikiwezekana umue kabisa”

“Kuua siwezi, labda kumtia kichaa”

“Mtie kichaa yeye na mtu aliyempa siri zangu” Stanley akashadadia.


“Ngoja tuangalie tuone nani aliyempa siri huyo mwanamke” Mganga yule aliongeza.

“Yanii nataka umtie adabu huyu Mange Kimambi, yanii ikiwezekana mbali ya kumtia wazimu awe kipofu kabisa namchukia sana”

“Ngoja kwanza tuangalie usipate tabu” mzee Muhaji alisisitiza.

“Sawa” Stanley akaitikia.

Mganga yule alitayarisha vifaa vyake vya kiganga kisha akaanza kupiga ramri.

“Tayari nimekwishamtambua mtu aliyetoa siri zenu kwa Mange Kimambi” mzee yule mganga alisema baada ya kumaliza kupiga ramri.

“Ni nani?” Stanley aliuliza kwa kiherehere.




Mganga yule wa kienyeji aitwaye mzee Omary Muhaji, alitia mbwebwe za kiganga, kisha akamwambia:

“Ni mume wa Mange Kimambi ndiye anayempa siri zako”

“Mume wa Mange!!!!!.....” Stanley alimaka. Macho yalimtoka pima.

“Ndio”

“Mume wa Mange ni nani?”

“Ni jini”

“Unasema!!!!” Stanley akauliza kama vile hakusikia vizuri kile alichoambiwa.

“Mume wa Mange siyo binadamu ni Jini” aitwaye Dnganjilo.”

“Mungu wangu!! Kumbe yule Kigagula mwanga eeh”


“Ndio. Mange Kimambi analo jini liitwalo Dnganjilo, ambalo anaishi nalo kama mume, jini huyu ndiye amekuwa akimtumia kupata siri mbalimbali.”

“Acha wewe!! kweli?” Stanley alizidi kuchanganyikiwa jambo alilokuwa akiambiwa lilimpa taharuki kubwa.


“Huniamini?” Mganga naye akamuuliza kwa pozi na mbwembe za kiganga.

“Sina maana hiyo. Ila inawezekanaje hilo babu?”

“Iko hivi”mganga akaanza kumweleza.

“Majini ni viumbe ambao wameumbwa kwa moto na walikuwa wakiishi duniani kabla ya binadamu miaka Milioni nyingi iliyopita. Viumbe hawa wana tabia kubwa mbili;

Yaani ya kibinadamu kwa maana wanakuwa wanafanya mapenzi, wanazaa na wanakufa.

Tabia nyingine ni ya Kimalaika ambayo ni kwamba wana uwezo wa kujigeuza katika umbo lolote wanalotaka na vilevile wanaruka na kwenda wanakotaka au kupita wanakotaka bila kutumia chombo chochote.


“Pamoja na mambo mengi wanayoyafanya, hujihusisha na binadamu, hufanya kazi za Malaika hasa zile za mambo ya kupeleka habari na kuwalinda binadamu, mambo ya doria za Angani. Kazi hizi siyo zao lakini kwa vile wanapenda kuiga mambo, basi huiga. na mara nyingi hushiriki kwenye mambo mabaya kama ambavyo huyu Jini wa mange anavyotumika”


“Mungu wangu. Mbona makubwa”

“Tena huyu jini wa Mange Kimambi ni ni kiumbe hatari sana”

“Kweli Mange nyok* (akamtukania mama yake)

“Sana” mganga akashadadia.

“Kwa hiyo tunafanyaje babu?”

“Nitapambana naye, unayo picha yake”

“Ndio, picha yake ninayo” Stanley alijibu, akatoa simu na ‘kudownload picha ya Mange mtandaoni.

“Hii hapa”

“Sitaki picha ya simuni, nataka ikiwa kwenye kalatasi”

“Basi itabidi nikaisafishe studio?”

“Kasafishe, halafu kama utaweza kupata kipande cha nguo yake kazi itakuwa rahisi sana kummaliza” Muhaji alimwambia.

“Babu uongo mbaya kupata nguo ya Mange ni mtihani”

“Basi uacha kiasi cha fedha ambacho tutalazimika kutafuta mbuzi kutoka upareni, ambako huko ndiko chimbuko la msichana huyo. Tutamtumia mbuzi huyo kuiteketeza nafsi ya Mange”

Stanley alikubaliana na wazo la mganga. alichofanya ni kutoa burungutu la fedha na kumkabidhi mganga yule ili kazi ya kumroga Mange Kimambi ianza

“Shubamit, Mange kwisha habari yako,” Stanley alinong’ona kwa kuona anakaribia kutimiza kile alichodhamiria kufanya.

*****

LOS ANGELS MAREKANI.


MANGE Kimambi alikuwa mbele ya computer kubwa aina ya Mark, ndani ya nyumba moja ya kisasa, nyumba iliyosheheni fenicha ghari, alikuwa akikazana kupitia habari mbalimbali za nchini Tanzania.

Kwa siku hiyo, vyombo vyote vya habari, ikiwemo mitandao ya kijamii habari kubwa ilikuwa ni juu ya video ya ngono ya mke wa mheshimiwa waziri Mtinika Hassan, Scola na hawala yake Stanley . Kuchepuka na mwanaume mwingine Kisha kumbambikia mtoto waziri huyo wa mambo ya ndani. Ilikuwa ni fedheha kubwa.

Watu mbalimbali mashuuri, wakiwemo viongozi wa serikalini, wabunge wa chama tawala, na wale wa upinzani, mawaziri nk kila mmoja alikuwa ametoa maoni vile utashi wake ulivyoliona jambo hilo.

Mange akiwa kiumbe mwenye jeraha baya nafsini mwake dhidi ya serikali iliyokuwa madarakani, alikuwa tayari kumuadabisha kiongozi yeyote kutoka serikalini, kwa kumwaga siri zao mbaya hadharani kama tu angeingiliwa kwenye vita ile.

Pamoja na kwamba wasaa ule alikuwa akiperuzi mitandao ya Tanzania, hata hivyo alikuwa mwenye wahaka mkubwa kila alipoona ujumbe ukiingia kwenye simu yake.


Taarifa alizokuwa akizisubiri kwa hamu, kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali juu ya kile kinachoendelea kwa Scola Mtinika ilikuwa kwa siku hiyo hakuwa amembulia chochote.


Tangu alipopenyezewa taarifa madai ya kupotea kwa mwanamke yule, aliamini muda wowote lazima angekuwa wa kwanza kupata taarifa juu ya mahali alipo mwanamke huyo kama ilivyokuwa ada. Ajabu hapakuwa na taarifa yoyote.

“Nkrii, nkrii” ujumbe katika account ya whatsapp ulingia.

Alinyakua simu yake na kufungua harakaharaka.

Ajabu alichokiona sicho alichotegemea, alikutana na kitu kingine, picha za Stanley akiwa wilayani Bagamoyo, huku mbele yake akionekana kuwepo mtu aliyeonekana kama mganga wa kienyeji ilimchanganya.

Mtumaji wa ujumbe ule aliadika neno moja tu”

“Unarongwa”

Toba!!.


MWISHO




0 comments:

Post a Comment

Blog